MpigaKura
JF-Expert Member
- Jan 25, 2007
- 384
- 101
Kwa mujibu wa kumbukumbu za shughuli za Bunge la Mamwinyi la Uingereza, ambako mjadala mzito uliibuka Jumanne wiki hii, Rais Mkapa alitetewa na aliyekuwa Waziri wa Masuala ya Maendeleo wa Uingereza, Bibi Clare Short
Akinukuliwa kwenye taarifa hizo za Bunge, Bibi Short alitoboa siri akisema mkataba wa awali ambao ndio baadaye uliokuja kuifanya Tanzania inunue rada kutoka kampuni ya BAE Systems ya Uingereza, ulisainiwa kabla Bw. Mkapa hajaingia madarakani, hivyo kuifanya Serikali yake kutokuwa na chaguo zaidi ya kuutekeleza
Kwa mujibu wa kumbukumbu hizo za Januari 30 mwaka huu, Bibi Short alikaririwa akisema: "Niliamua kupunguza kiasi cha mkopo tuliokuwa tumeiahidi Tanzania kwa kiasi cha pauni milioni 10 na nikaamua kwenda kuonana na Rais Mkapa, mtu ambaye ninamheshimu sana na aliyeifanyia mambo makubwa nchi yake.
"Akaniambia kwamba mkataba wa awali wa ununuzi wa rada, ulikuwa umeshasainiwa kabla yeye hajaingia madarakani, tayari malipo ya awali yalishatolewa na kulikuwa na kipengele kinachoibana Serikali kwamba ikiamua kujitoa katika mkataba huo, ingewajibika kulipa gharama kubwa," alisema Bibi Short.
Bibi Short aliliambia zaidi Bunge, kuwa baada ya kusikia kauli hiyo ya Rais Mkapa, aliona hakuna jinsi ya kuuzuia mkataba huo, zaidi ya kutumia sheria za Uingereza kuinyima leseni ya usafirishaji kampuni ya BAE.
Akijibu swali la mbunge, Bi. Susan Kramer, aliyeshangaa kusikia kuwa Rais Mkapa alikuwa na mawazo ya kuangalia namna ya kuachana na mkataba huo wa rada, wakati kuna taarifa nyingi kuwa Serikali hiyo ndiyo iliyokuwa ikilazimisha ununuzi huo, Bibi Short alieleza tatizo kuu lililomsibu Rais Mkapa.
Akizungumzia tatizo lililomfanya Rais Mkapa akose nguvu za kisiasa na kiushawishi, na hata kujenga msimamo wa kuepuka rada hiyo, Bibi Short aliliambia Bunge hilo kwamba "Rais Mkapa ni kiongozi maridhawa, Rais safi, lakini hakuwa na nguvu za kisiasa na alijikuta ameurithi mkataba huo.
"Kama Serikali ya Uingereza ingemsaidia kwa kuzuia utoaji wa leseni ya kusafirishwa kwa mtambo huo kwa kutumia kanuni ya 8 (inayozuia mauzo ya vifaa vya gharama kubwa kwa nchi maskini) ni wazi angekuwa mtu mwenye furaha, lakini mkataba ulikuwa na vifungu vya kulipa gharama kama angeuvunja."
Kwa mujibu wa Bibi Short, akimtetea zaidi Rais Mkapa, aliliambia Bunge kuwa kiongozi huyo alipoingia madarakani, mkataba wa awali kuelekea ununuzi wa rada, ulishalipiwa pauni milioni 5.
"Jambo la msingi kufahamu ni kuwa kwa wakati huo, Uingereza ndiyo ilikuwa na nguvu (ya kuweza kusaidia kuuzuia mkataba huo). Niliongea na Waziri Mkuu (Tony Blair), Waziri wa Fedha na pia Waziri wa Mambo ya Nje, Bw. Robin Cook. Mawaziri walikubaliana nami kwamba tuupinge mradi huo.
" Lakini baadaye kikaitishwa kikao cha ghafla cha mawaziri ambapo mawaziri wadogo walishinikizwa kuwa kwa lolote liwalo, waunge mkono uuzaji wa rada...na hapo ndipo tukabaini kuwa kumbe kulikuwa na mazungumzo ya siri ya kulisukuma mbele suala la rada. Wizara ya Ulinzi (ya Uingereza) iliridhia suala hilo."
Bibi Short alisema wakati Serikali ya Uingereza ndiyo iliyokuwa na uamuzi wa mwisho wa kuzisaidia fikra za ndani za Rais Mkapa, yenyewe ikawa ikisaidia kuhakikisha inaweka mazingira ambapo hata suala la leseni kama lisingetolewa, bado mkataba ungefikiwa mwisho kwa rada kupelekwa Tanzania.
"Kwa sababu hiyo, unaweza kusema kirahisi tu kwamba tusingeipa mkopo tena Tanzania kwa sababu kulikuwa na rushwa, lakini nchini humo kuna watu wengi maskini na wenye njaa. Mikopo ni kwa ajili yao. Kuna mtu mwingine aliyeiba pesa, kwa nini tuwaadhibu maskini kama vile wao ndio waliotenda maovu?" alihoji
Katika kikao hicho, Bibi Short akizungumza na kuonesha dhamira ya ndani zaidi ya Rais Mkapa, alithibitisha mbele ya Bunge hilo, kuwa kutokana na mtazamo wake wa ndani juu ya rada, ndiyo maana kiongozi huyo alifikia hatua, baadaye, akapitisha uamuzi wa kuzuia ununuzi wa awamu ya pili wa rada nyingine ambao mkataba wake haukuwa umesainiwa awali.
"Tufanye nini sasa? Hilo ndilo lililotutatiza. Rais Mkapa na mimi tulifikia makubaliano, kwamba kama alikuwa tayari kunihakikishia kwamba hataendelea na awamu ya pili ya ununuzi wa rada nyingine, tungeendelea kuipa misaada nchi yake.
"Nimekutana naye akiwa ameshaondoka madarakani na amenihakikishia kuwa ahadi hiyo inatimizwa. Ingawa alishindwa kuzuia mkataba wa kwanza, lakini angalau sasa fedha zaidi hazitapotezwa," alisema Bibi Short.
Aliliomba Bunge lisaidie jitihada na mtazamo wa Rais Mkapa wa kukataa Serikali ya Tanzania kuuziwa rada nyingine.
Kauli hii ya Bibi Short ni ya kwanza ya mtu aliyeufahamu kwa undani zaidi mtazamo wa Rais Mkapa kuhusu sakata la rada na akaamua kuuweka bayana.
Pia kauli hiyo inaweza kuonesha, kwa mara ya kwanza ni kwa nini Bibi Short na Rais Mkapa, hata baada ya kuonekana hadharani kuwa walitofautina juu ya ununuzi wa rada hiyo, lakini bado walibaki marafiki. Kumbe wote walikuwa wakiamini katika jambo moja adhimu; kwamba rada ilikuwa gharama zaidi kwa Watanzania
JAMANI SASA INAMAANISHA KWAMBA MWINYI NAYE ALISHAMEGA KAMISHENI YA MKATABA WA AWALI?