The Radar Scandal: Investigation & Progress

The Radar Scandal: Investigation & Progress

Wanabodi,
Hizo siasa tuachane nazo.. mimi bado Mtanzania hata kama sina pasi ya Bongo!. Mnitambue msinitambue mimi mbongo na nitakufa mbongo!... pasi ni kitambulisho cha kusafiria tu!.kwa sababu siwezi kusafiri na birth certificate mkononi!
Hata hivyo, mnamfahamu huyu Kijana?...
 
Wanabodi,
Hizo siasa tuachane nazo.. mimi bado Mtanzania hata kama sina pasi ya Bongo!. Mnitambue msinitambue mimi mbongo na nitakufa mbongo!... pasi ni kitambulisho cha kusafiria tu!.kwa sababu siwezi kusafiri na birth certificate mkononi!
Hata hivyo, mnamfahamu huyu Kijana?...
Huu ndiyo undani NA NDIYO MAANA HATA HIZI NCHI ZINAZOWAPA WATU URAIA WAO BADO LAZIMA WAONGEZE NA UASILI WA HUYO MTU.
 
Mkandara, ilinichukua siku moja tu kuonesha kuwa alichosema Muungwana si kweli. Labda kwa vile wameandika "Uhuru" watatilia maanani. Ila sitashangaa akienda mahali pengine na akarudia maneno hayo hayo walisema "sikio la kufa..."

Mzee Mwanakijiji,

Nilinukuhu thread yako - na nika relay msg kwa vichwa vya watu visivyotaka kuelewa! Walitaka kunipiga - hawakuamini kwamba BAE Systems si kampuni ya Serikali ya UK!!
 
Hivyo ndivyo watu walivyolala na wanafikiri hizi pesa ambazo Lunyungu analalamikia kwa nini ziitwe za JK. Kwa mana hiyo kazi ni kubwa.
 
Waziri akiri rushwa ilimwagwa ununuzi wa rada
*Ataja hadharani mawakala wanaotumika

JINAMIZI linaendelea kuikaba kampuni ya silaha ya Uingereza, BAE Systems, ambayo iliiuzia Tanzania rada ya gharama ya mabilioni baada ya siri muhimu kuendelea kuibuka juu ya vitendo vya maofisa wake kutumia rushwa kupata mikataba.

Katika sakata hilo, safari hii waziri mwandamizi nchini Jamhuri ya Cheki, amekiri hadharani kuwepo kwa vitendo vya rushwa iliyokithiri vinavyofanywa na kampuni hiyo.

Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Cheki, moja ya nchi ambako BAE tayari inachunguzwa kwa madai ya kutoa rushwa kupitia mawakala, amekuwa ofisa wa kwanza wa ngazi za juu kukiri BAE kutumia rushwa.

Kwa mujibu wa gazeti la The Guardian la Uingereza toleo la jana, Bw. Jan Kavan, aliyekuwa waziri hadi mwaka 2002, amesema katika mahojiano ya waandishi wa habari kuwa 'fedha zilibadilisha kila kitu' wakati BAE ikiingia mikataba nchini humo.

The Guardian lilinukuu kuwa Bw. Jan licha ya kuthibitisha kuwepo rushwa, amewataja maofisa waandamizi wa kampuni hiyo ya Uingereza kuwa ndio hasa waliokuwa wakimwaga pesa kupitia mawakala mbalimbali.

Kati ya maofisa waliotajwa na waziri huyo yumo, Bw. Julian Scopes, ofisa wa zamani katika Wizara ya Ulinzi ya Uingereza ambaye baadaye aliajiriwa na BAE kama Mhamasishaji Mkuu wa Biashara.

Pia ametajwa Bw. Alan Clark, ambaye ni Mwakilishi wa BAE mjini Prague, ambaye tayari amekwishatajwa kwenye orodha ya watoa rushwa.

Kutokana na mahojiano aliyoyafanya waziri huyo na baadaye yakarushwa kwenye televisheni ya Taifa ya Uswidi, Taasisi ya Kuchunguza Makosa ya Ulaghai (SFO) ya Uingereza, imeanza kulifanyia uchunguzi suala hilo.

Kampuni ya Kiswidi iitwayo Saab ndiyo inayotajwa kuwa wakala wa BAE katika kugawa rushwa kwa ajili ya kushinda tenda mbalimbali katika Jamhuri ya Cheki, hivyo Serikali ya Uswidi nayo inafanya uchunguzi.

Akihojiwa bila kujua kuwa alikuwa akirekodiwa kwenye televisheni, Bw. Kavan alisema; " Ukweli kwamba fedha ilitumika kubadili kila kitu unafahamika hata kwa wabunge na karibu kila mtu alikuwa akijua...mimi niliyasikia hayo kutoka kwa marafiki zangu."

Bw. Kavan alikuwa akiongoza kundi la waliokuwa wakipinga Serikali ya Cheki kununua silaha kutoka BAE mwaka 2002.

BAE imeendelea na msisitizo wao wa kila siku kuwa hawahusiki na tuhuma hizo.

Hata hivyo Mike Turner, Ofisa Mtendaji Mkuu wa BAE, kufuatia kuibuka kwa kadhia hiyo, amejitokeza kwa mara ya kwanza hadharani na kuonekana aking'aka kuwa tuhuma zote zinazoelekezwa kwa kampuni yake si za kweli na zinaiharibia jina.

"Tuhuma hizi dhidi ya watumishi na kampuni yetu si za msingi na tunaomba zifikie tamati haraka iwezekanavyo ili zisiendelee kutuharibia jina," alisema.

Wakati huo huo, kumekuwa na tetesi kuwa SFO inayochunguza kwa sasa tuhuma zote za rushwa zinazoikabili BAE Systems, huenda ikavunjwa na kuunganishwa na vitengo vingine.

Kwa mujibu wa gazeti la The Guardian, tayari kuna kamati inafanyia kazi mapendekezo hayo.
Kwa mujibu wa vyanzo vilivyonukuliwa na gazeti hilo, kuna uwezekano SFO ikaunganishwa na Taasisi ya Kupambana na Makosa ya Uhujumu Uchumi (soca) ambayo inafananishwa na FBI ya Marekani na ilizinduliwa rasmi mwaka jana.
Wafanyakazi wengine wa SFO huenda wakatakiwa kujiunga na Idara ya Kuendesha Mashtaka.

Wakizungumza kwa masharti ya kutowekwa bayana majina yao, baadhi ya wafanyakazi wa SFO wameonesha kukatishwa tamaa na vitendo vya Serikali kuingilia kazi za idara hiyo.

" Hapa sasa pamekuwa si mahali pazuri. Upo uwezekano wa kuendelea lakini kuna mambo yanatukwaza," kilisema chanzo hicho kilichokiri pia kufahamu kuwepo kwa mpango wa kuvunjwa taasisi hiyo.

Akijibu taarifa hiyo, Mwanasheria Mkuu wa Uingereza (AG), Bw. Peter Goldsmith, alikanusha kuwepo kwa mpango huo na kusema ameunda kamati kuangalia upya uwezo wa SFO katika kuchunguza na kuendesha kesi lengo likiwa ni kuiimarisha na si kuivunja.

Juzi Mwenyekiti Chama cha Wananchi (CUF),Profesa Ibrahim Lipumba alidai aliitahadharisha Serikali, Bunge na Rais wa awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa kuwa Serikali isinunue rada kwa fedha nyingi lakini alipuuzwa.

Akizungumza wakati akifungua mkutano wa Baraza Kuu la CUF, Dar es Salaam Prof. Lipumba alisema, CUF ilijitahidi kupinga ununuzi wa rada lakini ushauri wake haukuthaminiwa.

Alidai aliandika barua bungeni Desemba 27, mwaka 2001 kupitia kwa aliyekuwa kiongozi wa upinzani bungeni, Dkt. Amani Kaborou kuwashawishi wabunge wasipitishe muswada wa kununua rada hiyo lakini wabunge waliipuza barua hiyo.

Profesa Lipumba alidai aliandika barua nyingine Juni 17, mwaka 2002 kwenda bungeni na nakala yake kumpelekea Rais Mkapa kumtahadharisha kuhusu ununuzi wa rada hiyo kuwa unaambatana na rushwa ya ndani na nje nayo, hakikutiliwa maanani.

(c)Majira.
 
British millionaire linked to BAE commission payments in papers

David Leigh, Rob Evans and Mark Milner **The Guardian {United Kkingdom}

A little-known British millionaire has been named as a confidential agent for BAE, the embattled arms company facing worldwide corruption investigations. Brigadier Tim Landon, one of Britain's richest and most secretive men, provides a conduit for BAE commission payments, according to documents obtained by investigators.
Known as the "White Sultan", Landon has a fortune estimated at £500m. He earned his nickname as the power behind the throne in Oman, a Gulf oil state. He returned to England to purchase a Hampshire estate with village and a string of grouse moors. His lawyers describe him as "intensely private". Czech police investigating BAE's arms deals are alleged to have found secret payments were made through Valurex, an offshore company controlled by Brig Landon. According to the documents, Valurex was used in turn to engage an Austrian count, who promoted controversial BAE fighter sales to the Czech government.

Article continues.....

According to the documents published this week from Czech sources, Brig Landon's company Valurex is also promoting sales by BAE throughout eastern Europe, to Hungary, Bulgaria and Slovakia. More than £4m was allegedly paid to Valurex, starting in 2003. "We are not guilty of corrupt practices," Brig Landon's lawyers said yesterday. It is not alleged that he or his company was involved in any improper payments themselves. Czech police, along with the Serious Fraud Office in Britain, are investigating BAE's use of the Austrian agent, Count Alfons Mensdorff-Pouilly. The deals he was promoting, to lease Anglo-Swedish Gripen fighters to Prague for £400m, have been the subject of bribery allegations. Count Alfons denies he was linked to Valurex, and that he paid any bribes.
A Swedish TV programme this week published documents it said implicated Count Alfons and two other prominent Czech agents in receiving secret payments from BAE. The US government protested to Britain when allegations of bribery were made. But Sir Kevin Tebbit, permanent secretary at the British Ministry of Defence, refused to investigate.

The Czech deal is being scrutinised in three countries: by the Serious Fraud Office, by Czech police, and by the Swedish authorities. Yesterday, Christer van der Kwast, the Swedish chief prosecutor, said he had requested documents from Saab, BAE's partner in the deal, and will decide "in short time" whether to launch a full-scale investigation. He has also obtained documents from SFO investigators after meeting them in London this month.

BAE, which is due to announce its annual results today, has cancelled its traditional press conference because of "time pressures", a spokeswoman said.
 
Huu mzozo wa BAE na ndgege za kivita za Sweden "Gripe" ni kweli umeonyeshwa na TV ya Sweden. Yaelekea BAE imechafua kila kona ya ulimwengu wakati wanauza radar zao au kusaidia patrner wao (SAAB ya Sweden) kuuza ndege za kivita.

Rushwa ni ndio njia kubwa ya BAE ya kuuzia vifaa nyao. Bila ya rushwa hakuna biashara.
Sasa kama wanasiasa wa vyama kadhaa wa Czech walipewa "hongo" ili wanunuwe hizo ndege za kivita basi ni wanasiasa wangapi Tanzania walihongwa ili BAE iuze radar mbovu Tanzania?
 
Moderator/Admin au mtu yeyote
Naomba mnisaidie thread iliyokuwa na habari ya mdogo wake??? na RA aliyepo London? na kwamba ana majumba London? na biashara Iran au Oman??
 
Ustaadh Dr. Khamis

Karibu saaana jamvini JF.
 
Dr. Khamis,

Duuuh huyu muungwana nimetoka naye mbali sana!.. karibu janvi la JF lakuhitaji.
 
'Chenji' ya rada Tanzania kuambulia patupu

*Wanasheria wamshauri Rais Kikwete
*Wasema fedha hiyo ni ngumu kuidai

Hassan Abbas na Grace Michael

TAMKO la Rais Jakaya Kikwete kuwa Serikali yake italazimika kuidai kampuni ya BAE Systems ya Uingereza sehemu ya fedha zilizozidi (chenji), iwapo mkataba wa ununuzi wa rada utabainika kuwa uliongezwa thamani ili kuwanufaisha watu wachache, imeelezwa kuwa inaweza kugonga ukuta na kubaki ya kisiasa kutokana na sababu nzito za kisheria.

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Majira kwa wiki kadhaa kwa kuangalia sheria na rejea ya kesi mbalimbali za Uingereza na za Tanzania katika masuala ya mikataba, kauli hiyo ya Rais Kikwete, aliyoitoa hivi karibuni alipokutana na wahariri wa vyombo vya habari, imebainika, inaweza kuishia kuwa ya kisiasa.

Katika utafiti huo sheria za Kiingereza na hata zile za Tanzania, imebainika, zinakubaliana katika msingi mmoja, ambao ndio kikwazo cha kwanza kwa azma ya Rais Kikwete kwamba mkataba wowote unaposainiwa, kwa pande mbili husika kukubaliana, suala la thamani ya mkataba kama imepunguzwa au imepandishwa halina msingi.

Katika dhana hiyo, wasomi wa taaluma ya sheria wanasema masharti ya msingi ya kusainiwa mkataba yakifikiwa, kama vile wahusika kukubaliana bali shuruti wala ulaghai, na ikabainika kuwa waliohusika wote wananguvu au mamlaka kisheria kuingia kwenye mkataba, inatosha kuufanya mkataba huo kuwa halali.

Msimamo huo unaonekana kuikwaza azma ya Tanzania kudai kile tunachoweza kukiita 'chenji' hata kama itabainika kuwa mkataba wa ununuzi wa rada, uliongezwa thamani katika mazingira ya rushwa.

Katika utafiti huo, Majira limebaini kuwa kudai chenji katika mkataba wa rada iwapo maofisa wa Tanzania walijua kwa dhati suala la bei na aina ya mtambo wanaoununua una thamani na teknolojia ya kiwango gani, ni jambo litakalokosa mantiki kisheria labda ziwepo sababu ambazo wataalam wanaziona zitasaidia.

Katika kufafanua hoja inayofanana na sakata hilo, Mahakama ya Rufani ya Uingereza tayari imeweka bayana mawazo yake kupitia shauri mashuhuri la Chappell & Co. LTD VS Nestle Co. LTD (1959) 2 All ER, 701, ambapo iliamuliwa kuwa hata kama mhusika katika mkataba aliamua mwenyewe kuuza gari lake kwa pauni moja, kisheria mkataba huo utakuwa halali.

Katika uchunguzi huo, Majira limebaini zaidi kuwa ushahidi uliopo mpaka sasa kwenye ripoti rasmi (Hansard) za Bunge la Mamwinyi (House of Lords) la Uingereza unaibana zaidi azma hiyo ya Rais.

Katika 'Hansard' hizo, maafisa kadhaa wa Tanzania wamenukuliwa humo, wakitetea kuwa rada iliyonunuliwa ndiyo ambayo Tanzania ilikuwa ikiihitaji na iliridhika nayo kwa mujibu wa mahitaji yake.

Kauli hiyo na msimamo wa sheria za Uingereza kama ulivyooneshwa katika shauri la Chappell, ni kikwazo ambacho kinaweza kuizima azma ya Tanzania na hata kama Serikali itafungua kesi, yanaweza kujirudia yale ya IPTL, wanashauri baadhi ya wataalam hao.

Baada ya kuangalia msimamo wa sheria za Kiingereza, imebainika kuwa hata sheria za Tanzania hazitofautina sana ambapo kwa mujibu wa Sheria ya Mikataba (The Law of Contract Ordinance [LCO]), thamani iliyokubaliwa na pande mbili zinazoingia mkataba ndicho kitu cha muhimu.

Hata hivyo wataalam mbalimbali wa sheria wanasema, upo mwanya mdogo kwa Serikali ya Tanzania kuweza kufanikiwa katika azma hiyo ambapo itailazimu Serikali kuupitia mchakato mzima wa mkataba wa ununuzi wa rada na waliohusika wahojiwe ili yapatikane masuala matatu ya msingi ambayo yanaweza kuisaidia Tanzania.

Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti, mawakili mbalimbali mashuhuri wa Dar es Salaam, wameyataja mambo hayo kuwa ni Serikali kutakiwa kuthibitisha kwamba wakati wa kusainiwa mkataba kulikuwa na mazingira ya ulaghai, kutokuelewana au upande mmoja kulazimishwa (hata kwa kishawishi cha rushwa) kuingia mkataba huo, ndipo suala la kudai chenji linaweza kueleweka kisheria.

Akizungumza na Majira, Wakili wa kujitegemea Bw. Gaudiosus Ishengoma, alisema kuwa kuhusiana na sheria ya mkataba huwezi ukadai kitu chochote endapo mnunuzi wa kitu hicho aliingia mkataba na muuzaji kisheria bila ya kuwa na msukumo wowote au kulazimishwa kufanya hivyo ili kulinda maslahi fulani ambayo ni kwa faida yao.

" Unaweza ukadai endapo mkataba huo utangundulika ulifanyika kwa njia za ulaghai, kuwepo kutokuelewana au kuwepo msukumo kutoka nje ambao unaweza ukafanywa na watu wengine ili kushinikiza mkataba huo. Hapo ndio sheria inaweza ikachukua mkondo wake na si vinginevyo," alisema Bw. Ishengoma.

Akizungumzia suala la ununuzi wa rada Bw. Ishengoma alisema kuwa Tanzania itaweza kudai fedha hizo endapo tu mkataba huo ulikuwa na makosa hayo.

Naye Wakili Bw. Charles Semgalawe alipohojiwa kuhusiana na masuala ya mikataba kisheria, alisema kuwa inawezekana kudai endapo kulikuwa na chembechembe za udanganyifu, hilo lisipokuwepo inakuwa ni ngumu kudai malipo yoyote.

Kutokana na mazingira hayo kuwa magumu kuyathibitisha kisheria, wengi kati ya wataalam waliozungumza na Majira, waliitahadharisha Serikali isije ikiwaingiza tena Watanzania kwenye hasara kama ya IPTL, ambapo kesi iliongeza gharama za uendeshaji na uzalishaji wa umeme nchini.

Suala la Serikali ya Tanzania kujaribu kupambana na ufisadi katika masuala ya mikataba mingi inayoonekana kusainiwa katika mazingira tete limekuwa tata.

Miaka kadhaa iliyopita Serikali kupitia TANESCO ilijaribu kuuvunja mkataba wake na kampuni ya IPTL kwa kupeleka shauri hilo kwenye Baraza la Usuluhishi wa Migogoro ya Uwezekaji la London, ambapo kimsingi Serikali ilishindwa na kutakiwa kulipa mabilioni zaidi kwa kampuni hiyo na kusababisha gharama za uzalishaji na hata bei za umeme kupanda.

Kwa sasa suala la sakata la rada linaendelea kuchunguzwa na Taasisi za Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKURU) na ile ya Uingereza , SFO.

CHANZO: Gazeti la Majira
 
Mh. Rais alilijua hili kwani hata alivyotoa kauli ya kwamba ikibainika serikali ya uingereza wametudhulumu,tutadai waturudishie kiasi cha zaidi ya bei ya soko kilichozidi,For his best knowledge(moyoni na mawazoni )alikuwa anajua kampuni hiyo si mali ya serikali na ndiyo maana aliweza kutoa kauli tata kama hiyo.
 
Tunachodai wananchi ni kuwajibishwa kwa WATANZANIA wote waliohusika ktk Mkataba huo sio kurudishiwa fedha. Hilo swala la kurudishiwa fedha lilikuwa kifumba macho cha JK ili kubadilisha lugha ya madai ya wananchi.

Watu hawa lazima watolewe ktk uongozi na wale wafanyabiashara hata kama sio raia wapewe masaa kuondoka nchini kwa kosa la kuhujumu uchumi wa nchi. Mali zao kuchukuliwa kama fidia ya chenji yetu!
 
Watu hawa lazima watolewe ktk uongozi na wale wafanyabiashara hata kama sio raia wapewe masaa kuondoka nchini kwa kosa la kuhujumu uchumi wa nchi. Mali zao kuchukuliwa kama fidia ya chenji yetu!
.
Mkandara!
Hatutabaki hata na Mh. Rais! Na kwa mantiki hiyo ajiondoe yeye kwanza na sheria imhukumu.Kazi kubwa hiyo!
 
In a light touch...

Tena naona inasemwa chenji yetu ni bilioni 12 za 30%. Kimantiki kama kampuni ilikubali kutoa 30% basi bei halisi pamoja na faida ni 40% tu. Kwa maana lazima 30% irudi kibiashara ama katika ubora wa bidhaa(kwa maana ya kuuziwa kanyaboya) au kitu cha gharama ndogo kuuziwa kubwa zaidi!.

Hivyo chenji yetu ni zaidi ya Bilioni 24.

Sisi tuwashike 'wezi' waliokaribu yetu hao ndio wawataje wengine! Inavyoelekea hivi sasa tunafanya kinyume...tunasubiri kwanza 'wezi wa mbali' ndio waanze kujulikana!

IPTL, RICHMOND na RADA na majaribio ya utawala wa Kikwete.

Tuombe Mungu, Tukishindwa tukate rufaa kwa shetani teh teh teh......
 
Bazee,
Kwani huyo dalali (VS) ambaye kishahojiwa na SFO na kukiri kuwa alivuta 12bn zaidi, kwa nini asiambiwe tu ARUDISHE hiyo PESA? Yeye anajua alimpa nani. Kwa nini iwe kazi ngumu?! Au mi sielewi!
 
Bazee,
Kwani huyo dalali (VS) ambaye kishahojiwa na SFO na kukiri kuwa alivuta 12bn zaidi, kwa nini asiambiwe tu ARUDISHE hiyo PESA? Yeye anajua alimpa nani. Kwa nini iwe kazi ngumu?! Au mi sielewi!
Wa kumwambia na mwenye utashi huo yuko wapi na anatoka wapi?
Labda JF!
 
Wa kumwambia na mwenye utashi huo yuko wapi na anatoka wapi?
Labda JF!


Nyie mmeona wapi anayerudisha hela ni Dalali...!!! Dalali yeye hakulipwa na Tanzania amelipwa na BAE. Tanzania ilikubali kununua radar kwa bei ya juu kutoka BAE, wao BAE wanampa dalali hela yake. Sasa Tanzania itamdai vipi dalali...infact dalali hawezi kudaiwa na mtu yoyote maana yeye kazi yake ameifanya fair and square...amewakutanisha muuzaji na mnunuzi...na kwa kufanya hivyo ujira wake ni 12mil usd.

Wakukabwa koo na masikio ni hao waliokubali kulipa kodi yetu huko BAE...ohha nimekumbuka pengine hawakuwa na UTAALAMU wa kutosha.
 
kisura kesha sema,sisi hatujui kusoma wala kuandika.kwa maana hiyo hapa hakuna mjadala na hayo ndio matunda yake.
 
Nyie mmeona wapi anayerudisha hela ni Dalali...!!! Dalali yeye hakulipwa na Tanzania amelipwa na BAE. Tanzania ilikubali kununua radar kwa bei ya juu kutoka BAE, wao BAE wanampa dalali hela yake. Sasa Tanzania itamdai vipi dalali...infact dalali hawezi kudaiwa na mtu yoyote maana yeye kazi yake ameifanya fair and square...amewakutanisha muuzaji na mnunuzi...na kwa kufanya hivyo ujira wake ni 12mil usd.

Wakukabwa koo na masikio ni hao waliokubali kulipa kodi yetu huko BAE...ohha nimekumbuka pengine hawakuwa na UTAALAMU wa kutosha.

Ndiyo maana nikasema kwa njia ya swali baada ya mmoja wetu kusema ambiwe arudishe kwa kuuliza yuko wapi na anatoka wapi?Nikimaanisha yeye hana mkataba na serikali na hata kama alikuwa na mkataba ni kwamba walishakubaliana kwa terms zilizokuwepo kwenye mkataba na alishatoa huduma husika,sasa haya madai mengine kisheria hayana nguvu.
 
Back
Top Bottom