The Radar Scandal: Investigation & Progress

The Radar Scandal: Investigation & Progress

Wewee mbona umechelewa...... this happened over 4 days ago, jitahidi sometimes ukipata muda uwe unasoma gazeti la huko kwenu la The Gurdian na the Times, achana na tabloids za News of the World na Daily Star!!!

Una maana mkuu huwa anasoma The Sun, tena page three? Kwi kwi kwi!!!!
 
Mtanzania,
Page 3 huwaga na picha nzuri tu ya kisura. Au wamebadilisha siku hizi?
kwi!kwi!kwi!
 
Mkuu Susuviri,

Na the likes, ninasema hivi hizi dataz hazina ubishi wala mikwaruzo, toka jana Media nzima ya bongo inanipigia magoti niwauzie, nimesema siuzii mtu kwa sababu ninaamini katika kuwaelemisha wananchi na pia siku zote kuweka heshima ya hii forum,

Kwa taarifa yako na wenzio, kama alivyosema Lunyungu, sijawahi ku-withdraw dataz na hazijawahi kuwa disputed na ukweli zaidi yake, lakini ni kweli kila ninapozitoa huwa kunakuwa na mashambulizi ya personal against me ambayo hayahusiani na the dataz, sababu huwa ni moja muhimu, nayo ni wivu na uwezo mdogo wa kufikiri kwa wahusika,

Nimesema mara nyingi sana na ninarudia kuwa think kabla hujaandika hapa, kwa mfano in the name of dataz, hapa JF ninawajua ndugu wa karibu na Chenge, angalau wawili ambao so far wametulia, meaning kwamba hata wao nimewasaidia maana walikuwa hawajui kuhusu hii ishu, I do not have to do this lakini ni vyema tukawasaidia wenye akili hapa, nilipoziweka hizi dataz Lunyungu ameenda kuzifuatilia na kuja na zake zaidi na kukubali ukweli wa dataz, mimi mtu yoyote akiweka dataz hapa kazi yangu ni kuzifuatilia na kuthibitisha kama nina-concern, na kumwambia ukweli wa ishu kwa kumuonyesha wapi amekosea na dataz zake, kwa mfano Chenge nimemuona jana yupo Dar, Rostam na Karamagi hawakusaifiri last week, ukweli ni one, two, and three, au kunyamaza kwa sababu kwenye maisha si kweli kwamba kama wewe hujui basi wengine wote hawajui,

Dataz ni dataz, I mean just dataz hatuna njia nyingine yoyote ya kuziweka, they are just dataz, kwa sababu tunapewa na watu ambao huwa wana-risk sana na kazi zao sasa ni wajibu wetu kutumia akili on how tunaziweka hapa, ndio maana nimesema kuwa ninajua hata jina la mahali huko London ambako hizi shughuli zinakofanyika,

na bado ninaendelea kuzikusanya more dataz, and more dataz yaaani ni just dataz tupu, asiyezitaka badili station tu lakini ninajua kuwa ni wengi wanaozitaka kwa sababu toka jana PM yangu imejaa mara mbili, halafu mind you PM yangu inachukua message 1000, sasa zote nimezi-print, mesage karibu 2500, leo nataka nijaribu kuzisoma, kwa wale wenye nia ya kuwa na ile DVD thing, ni kwamba nina vipande vinne, nimeangalaia viwili so far in full, bado vipande viwili vingine, kabla ya kuanza kuziweka zote nne in one master DVD, ili niweze kuzirudisha nilikoazimwa kwa muda, niliongea na Mkulu MMJ on what to do next ili kuiweka hapa, hilo halina ubishi itakuja when the time is right!

A Luta Na More Dataz Soon..........!

Nadhani sasa baada ya Chenge kutiwa nguvuni ni vyema kungojea kuona next move .Wambeya hapa wamenasa .Mimi nimezima sasa simu yangu baada ya kuwa kero .Wanataka kuuua ukweli lakini nimesema kesho nitakuwa ofisini tuonane huko leo napumzika .Ukweli umesimama na hata CCM na Ikulu kawaulize .They are all shocked kwamba habari hizo hazikulala na tunazo .ES
naujua unyonge wako mkuu lakini kwenye data no has disputed your data .Wamekuja hapa wambeya kibao akina GT na majungu lakini kila wasemalo mwisho ni fitina binafsi ama ku twist wakiwa kazini .

naomba tuwe focused sasa .Issue ni kukamatwa kwa Chenge na mali kibao za walafi kukamatwa .Sasa tumpe JK sifa ama hapana .Utaamua wewe .Mimi nampo kidogo kwa kuamua kutoa kibali cha Chenge kukamatwa na kumwambia Rostam na Karamagi kwenda kusema wanayo yajua .

Connection hapa ni kubwa Chenge si Rada pekee .Chenge amekiwa AG mwa kipindi kirefu namuda huo wote madhambi makubwa na mikataba kibao imewekwa .Hili pekee linaleta utata si UK pekee hata TZ kama kweli tuna utawala bora and unfortunately hatuna .

Habari nzima aliyoandika Mkulu ES ni kweli!!,Hamtopata jibu rahisi kwa baadhi ya maswali ya kiutendaji mnayouliza "eti nani alisaini search Warrant",hata Polisi Lance Koplo pale Central Police anaweza kusaini warrant ikiwa tu atapata Go ahead kutoka kwa Wakuu wake....

Ni kweli kwamba Mzee Chenge yupo London,na siku nzima ya Jana (Ijumaa) alikuwa tight kwa masuala ya ushahidi.Kesi hii ni kubwa,na kuna wengi wanahusika,Tutegemee aibu kubwa kwa baadhi ya Viongozi wakuu wa nchi.Kwa mara ya kwanza na Mheshimiwa JK ametajwa,nae alihusika kiaina alipokuwa Foreign Minister,naomba nisiulizwe kivipi,kama upo makini na unafuatilia issue hii utaelewa.Mama Maria kejo nae anaingia humu,(Tumpe pole kuna taarifa kuwa Jumatano amefiwa na kaka yake),nae atakwenda London baada ya shughuli za Msiba.Mzee Mwanyika nae moto upo Mgongoni mwake,kwa mujibu wa datas alitoa kauli za uongo alipoonana na watu wa SFO.

Wakubwa stay tuned mambo makubwa yanakuja mbele!!,Mzee wa vijisenti ataondoka na wengi,na ndio mtakumbuka kwa nini alijibu "Muulizeni Rais" mara baada ya kurudishwa kwenye Cabinet baada ya Cabinet kuvunjwa kutokana na Lowassa kujiuzulu.....Anajua kila uchafu wa hawa wakubwa,na sasa atayaanika yote wazi....Hala hala tu serikali isije ikavunjwa tena !!

Mzee ES waambie vijana,nini kinajiri huko,kwa sababu vyanzo vyako vya habari ni makini....

Unafahamu hapa sasa tumeingiliwa na akina karumekenge's kwa hiyo nyani akomwe kisawasawa . Shukran FMES na Mwawado.

Mwawado

Usipotee sana namna hii haifai. Karibia mkekani. Hapa hatulali mpaka wote washikishwe adabu maana wanafikiri Tanzania ni mali waliyorithishwa na wahenga wanakula hadi kutapika. Thomas's wasubiri Daily news, Habari Leo etc. ndio waamini maana bado matongotongo kuwatoka machoni.
 
Habari nzima aliyoandika Mkulu ES ni kweli!!,Hamtopata jibu rahisi kwa baadhi ya maswali ya kiutendaji mnayouliza "eti nani alisaini search Warrant"

Sidhani habari nzima ni kweli. Polisi wa Uingireza hawezi ku execute search Warrant ya Kitanzania na Rais wa Tanzania hawezi ku sign Search Warrant ya Kiingereza. Tumeambiwa "Dataz" zimesema Kikwete aliandika na ku sign Search Warrant. Stori imepinda!

... hata Polisi Lance Koplo pale Central Police anaweza kusaini warrant ikiwa tu atapata Go ahead kutoka kwa Wakuu wake....

Right! Unatofautiana na mwenzio, Mkuu mwenye "dataz." Tumeonyesha sheria ya hicho unachokisema hapo (pitia pitia matundiko ya nyuma kidogo). Tatizo la "dataz" ni kwamba zimesema Chenge alileta ubishi akaonyeshwa Search Warrant iliyoandikwa na ku sainiwa na Kikwete (na ni kichekesho kusema mtu anaandika na ku sign warrant yeye mwenyewe - inakuonyesha mtoa "dataz" alivyo pitwa na vitu kidogo - just to put it mildly. Unaanza ku doubt kama anajua anacho kisema. Kwa hiyo, ongea na mtoa "dataz" wako mrekebishane.

Ni kweli kwamba Mzee Chenge yupo London,na siku nzima ya Jana (Ijumaa) alikuwa tight kwa masuala ya ushahidi....

Hatujabisha hilo, ila wengine wakauliza, very trenchantly, nini ni newsy kuhusu Chenge kwenda London? Mkasema, ooooh, kaonekana na Pingu. Wait a minute now, Chenge sio target wa Investigation, how come akamatwe? Ndio ikaonekana maswali haya hayana dataz ila yana logic, na hatuendi na logic hapa JF (yet another kituko)! Kwani sisi ndio tumeleta "dataz" au tunaswalisha veracity ya hizo "dataz" alizo zileta Mkuu kuona kama kuna mantiki?

Kesi hii ni kubwa, na kuna wengi wanahusika,....Kwa mara ya kwanza Mheshimiwa JK ametajwa,....Mama Maria kejo ... Mzee Mwanyika ...Mzee wa vijisenti ataondoka na wengi...kwa sababu vyanzo vyako vya habari ni makini....

"Vijisenti" na Mafisadi wenzake watamalizwa, Tanzania - if at all - sio UK. Huko wao sio target wa wrongdoing. Vyanzo vya habari vyenu hatujavikataa, tumeviswalisha. Vyombo vingine vinasema, sio tu kwamba Chenge sio target, ila pia hajashitakiwa mtu bado, sasa atakamatwaje mtu?

Sasa hapa tunafanya stringent vetting kuliko MwanaHALISI na Tanzania Daima kwa sababu tumewaalika waandishi wa Bongo waje kujifunza Journalism hapa. Tuta maintain viwango vya juu kuliko Nyegezi na UDSM tulipo waomba wa drop out! Hapata geuka MwanaHALISI hapa kama mchangiaji mmoja alivyo onya.

BAE corruption investigation switches to Tanzania


· Focus on £28m radar deal with East African state

* The Guardian, April 12 2008.
* David Leigh and Rob Evans

Following the uproar over its halted Saudi investigation, the Serious Fraud Office is expected to decide whether to bring fresh corruption charges against arms manufacturer BAE within six weeks, over a second arms deal, this time with Tanzania.

A minister from the east African state has denied that more than $1m (£507,500) in his offshore accounts came from BAE.

Investigators involved in a three-year inquiry after the controversial deal to sell Tanzania a £28m radar system identified the money in Jersey accounts controlled by the poverty-striken country's infrastructure minister, Andrew Chenge.

Investigators say Chenge could be a valuable witness. The target of their investigation is not him but BAE. The arms company made the commission payments to a local agent in Tanzania to promote the £28m radar sale, through an elaborate chain of offshore companies and a Swiss bank.

The agent has now left the country and is wanted by Interpol.

...The Guardian subsequently disclosed that £1bn had been paid into accounts controlled by Prince Bandar during the deal. Bandar says the payments were not improper.

The Tanzania deal, although smaller in cash terms than the Saudi deals, is equally controversial: Tanzania is one of the world's poorest countries, and the UK government is paying more than £100m this year to help the heavily-indebted country's budget.

It was Blair again who forced the radar deal through the British cabinet, despite protests from the then international development secretary, Clare Short. She said the sale, for which Tanzania had to borrow yet more from a commercial bank, was corrupt and "stank".

A lengthy SFO investigation in the UK subsequently discovered that 31% of the deal's contract price had been diverted via Switzerland.

BAE transferred the money to a subsidiary, Red Diamond Trading, registered anonymously in the British Virgin Islands.

Red Diamond then moved the cash to a Swiss account in the name of a Panama company, Envers Trading Corporation. This entity had two Panamanian nominee directors. But it was secretly controlled by a Tanzanian middleman, Shailesh Vithlani, according to Dar es Salaam court papers.

Investigators are now checking whether Vithlani arranged to pass any money in turn to Tanzanian politicians and officials.

Sources said the bank in Jersey had promptly frozen transactions and filed a suspicious activity report when the Tanzanian inquiries began.

Vithlani, who is of Indian extraction but holds a British passport, is listed as wanted by Interpol.
 
Kuhani mkuu

Hatujabisha hilo, ila wengine wakauliza, very penchantly, nini ni newsy kuhusu Chenge kwenda London? Mkasema, ooooh, kaonekana na Pingu. Wait a minute now, Chenge sio target wa Investigation, how come akamatwe? Ndio ikaonekana maswali haya hayana dataz ila yana logic, na hatuendi na logic hapa JF (yet another kituko)! Kwani sisi ndio tumeleta "dataz" au tunaswalisha veracity ya hizo "dataz" alizo zileta Mkuu kuona kama kuna mantiki?

Kama yeye sio target kwa nini wame-freeze pesa yake iliyo Jersey? Just asking?
 
Kuhani mkuu



Kama yeye sio target kwa nini wame-freeze pesa yake iliyo Jersey? Just asking?


Ninachojua mimi nchi nyingi zinatumia sheria ya mpokeaji na mtoaji rushwa kama wote waharifu.Hivyo basi soon itakapobainika kwamba "Visenti" Vilivyopo jearsy vimetokea BAE mheshimiwa ana kosa la kujibu.
 
20061101_starbucks_900x600.jpg
 
Ukumbi huu mnanifurahisha. kila mtaalamu wa Sheria leo, lakini siku tukiambiwa tuchanguwe mambo ya muhimu yanapoanza kuharibiwa, kila mtu anasubiri aletewe kifungu cha sheria au katiba.

Inawezekana kabisa FMES kapotosha kwa kutumia neno search warrant/arrest warrant ambayo inatufanya tuanze kuwa Lamwai au Muckaddam, lakini ni obvious kuwa kulikuwa na communication of some sort ambayo inawezekana ilipelekwa Ikulu hata kabla ya Chenge kuachia ngazi ambapo Rais alipewa taarifa na akaafiki watgakachofanya SFO.

Inawezekana hii "search/arrest warrant" ilishaidhinishwa na JK hata kabla ya safari ya China au magazeti kututamkia kuwa Chenge ana vijisenti vyake.

Kumbukeni SFO wangeweza kwenda kwa IGP, lakini kwa kuwa Mwajiri wa Chenge alikuwa ni JK, hivyo protocal ilikuwa ni kumtonya JK kwa faili zima na kumwambia kitakachofanyika.

Sasa inaelekea nasi tumekuwa kama Chenge na kubwatuka hili haliwezekani, sasa ni lazima tuonyeshwe hiyo barua au kibali kilichotoka Ikulu kwenda kwa SFO kuwapa baraka za uchunguzi wao?

We are now trying to play with technicalities, but where were the technicalities when our country was being raped?

What I need to hear is what is GVTZ doing about this. Is it waiting for the British kufanya vitu vyao au GVTZ is in such a shock and embarrasment kuwa vichwa vingi vitapitiwa na upanga?
 
Kuhani mkuu

Kama yeye sio target kwa nini wame-freeze pesa yake iliyo Jersey? Just asking?

Ninachojua mimi nchi nyingi zinatumia sheria ya mpokeaji na mtoaji rushwa kama wote waharifu.Hivyo basi soon itakapobainika kwamba "Visenti" Vilivyopo jearsy vimetokea BAE mheshimiwa ana kosa la kujibu.

Mchelea Mwana,

"Vijisenti" hawezi kuwa na kosa la kujibu UK. Hajawatenda UK kosa. Na Uingereza haina nguvu ya kisheria, haina jurisdiction, juu ya Chenge. Wana dili la watu wao BAE kwa sababu ni kampuni iliyo sajiliwa UK, inabanwa na Sheria za UK. Chenge kama raia wa TZ habanwi na Sheria ya UK isipokuwa kama ametia mguu UK, au amewatenda kosa UK.

Na hela za Chenge hazija freeziwa na Wachunguzi. Hela zime freeziwa na Benki ya Jersey baada ya Uchunguzi wa Tanzania kuanza, na sio kufuatia uchunguzi wa UK. Benki huwa zina taratibu za kushirikiana na vyombo ya dola kudhibiti uhalifu ili kujijengea sura, kama sio kwa kwa shuruti ya sheria ya nchi iliyo sajiliwa.

Ile taarifa niliyo post imesema:

Sources said the bank in Jersey had promptly frozen transactions and filed a suspicious activity report when the Tanzanian inquiries began.

Kwa hiyo, Chenge inabidi tummalize sisi wenyewe. Prosecutors wa UK hawataki kutusaidia sisi katika hili. Wanatafuta samaki wakubwa, BAE. Na wasingeweza - hata wangetaka- kutusaidia kwa sababu ya mipaka ya dola na sheria.
 
Kwa kifupi JK alikuwa anajua kuwa mmoja wa mawaziri wake anatakiwa kupekuliwa, whether alisaini au hakutosaini hayo ni mengine...
Niko interested na kujua Chenge alipekuliwa lini, was it before JK hajavunja baraza la mawaziri au baada?
 
Ukumbi huu mnanifurahisha. kila mtaalamu wa Sheria leo, lakini siku tukiambiwa tuchanguwe mambo ya muhimu yanapoanza kuharibiwa, kila mtu anasubiri aletewe kifungu cha sheria au katiba.

Inawezekana kabisa FMES kapotosha kwa kutumia neno search warrant/arrest warrant ambayo inatufanya uanze kuwa Lamwai au Muckaddam, lakini ni obvious kuwa kulikuwa na communication of some sort ambayo inawezekana ilipelekwa Ikulu hata kabla ya Chenge kuachia ngazi ambapo Rais alipewa taarifa na akaafiki watgakachofanya SFO.

Inawezekana hii "search/arrest warrant" ilishaidhinishwa na JK hata kabla ya safari ya China au magazeti kututamkia kuwa Chenge ana vijisenti vyake.

Kumbukeni SFO wangeweza kwenda kwa IGP, lakini kwa kuwa Mwajiri wa Chenge alikuwa ni JK, hivyo protocal ilikuwa ni kumtonya JK kwa faili zima na kumwambia kitakachofanyika.

Sasa inaelekea nasi tumekuwa kama Chenge na kubwatuka hili haliwezekani, sasa ni lazima tuonyeshwe hiyo barua au kibali kilichotoka Ikulu kwenda kwa SFO kuwapa baraka za uchunguzi wao?

We are now trying to play with technicalities, but where were the technicalities when our country was being raped?

What I need to hear is what is GVTZ doing about this. Is it waiting for the British kufanya vitu vyao au GVTZ is in such a shock and embarrasment kuwa vichwa vingi vitapitiwa na upanga?

Ha ha hahaaa aaa Mchungaji, duuh. Sijawahi kukuona umewaka.

Mtu wako, the illustrious, the one and only, great old Field Marshall E(something?) Systems, kuanzia jana kidogo kawekwa kiti moto juu ya kiti umeme hapa!

Usikonde Mkuu. Tunajaribu kuwa na mfumo wa kuthibitisha na kuchambua "dataz," tusije tukalazimika kuomba wakina Aziz na Chenge misamaha hapo baadae. Unajua Bongo hamna true Media, kwa mawazo yangu, kwa hiyo hapa JF tuna raw Press yetu wenyewe (na kwa kweli sitakiwi kukuambia wewe haya; wewe ni vete na mmoja wa Statesman wa JF Nation). Lakini japo Press yetu JF ni rough and raw, tunataka iwe na viwango vinavyo zidi MwanaHALISI na Tanzania Daima. Ni hicho tu.

Ni hicho tu, mtu wangu.
 
Wakuu tunaendelea na kuzifuatilia dataz za Chenge, leo hakukuwa na any movement, kwa hiyo tunasubiria kesho na kuendelea,

Ninaomba kutoa shukrani zangu nzito sana kwa Lunyungu, Mwawado, na mkuu wangu Halisi kwa kuweza kuzithibitisha hizi dataz kuwa ni za kweli, na kuna za zaidi na zaidi, ambazo pole pole tutaendelea kuziachia hapa,

kwa wale vimbwenelehi hatuna peremende hapa, tulisema mwanzoni kuwa tutaendelea kukoma nyani hapa na kumwaga dataz mchana kweupee, na ninaomba nirudie kuwa huwa dataz zetu hazitoki kwenye ku-paste internent, huwa zinatoka jikoni no competition we just move the crowd,

From Jambo Forums mpaka Jamii Forums mwendo ni ule ule wa mdundo, heshima mbele haitashuka hata siku moja, kwa sababu tumekuwa into this game for too long na hatuna mpango wowote wa kupunguza speed, maana mafisadi tunajua kuwa wanaombea sana hilo, wakiwatumia watu wao hapa, ambao tayari wote tunawajua hata kwa majina yao kamili na tunaweza kuwataja vile vile hapa hapa JF mchana kweupee!

Kwenye hizi dataz Tanzania media yote toka jana iko hapa kula dataz, na tumeipigisha magoti hapa JF, mimi sio journalist wala muandishi wa habari, mimi ni mbongo mwenye uchungu na taifa langu period, and I got the juice anytime 24/7!

I love JF, na Mungu Aibariki Tanzania Yetu!
 
Kwa kifupi JK alikuwa anajua kuwa mmoja wa mawaziri wake anatakiwa kupekuliwa, whether alisaini au hakutosaini hayo ni mengine... Niko interested na kujua Chenge alipekuliwa lini, was it before JK hajavunja baraza la mawaziri au baada?

Icadon, hayo sio mengine, ndio yaliyo letwa hapa, na kuswalishwa. Ukisema hayo hauko interested nayo nakuelewa 100%. Lakini wengi wameshuku, na mimi nimebisha, Waingereza ku execute Warrant ya Kitanzania au Kikwete ku saini Warrant ya Kiingereza. Na kwamba Chenge kakamatwa London wakati mashitaka bado hayajaletwa na wala yeye sio target, na habanwi na Sheria yao.

Ahsante.
 
Icadon, hayo sio mengine, ndio yaliyo letwa hapa, na kuswalishwa. Ukisema hayo hauko interested nayo nakuelewa 100%. Lakini wengi wameshuku, na mimi nimebisha, Waingereza ku execute Warrant ya Kitanzania au Kikwete ku saini Warrant ya Kiingereza. Na kwamba Chenge kakamatwa London wakati mashitaka bado hayajaletwa na wala yeye sio target, na habanwi na Sheria yao.

Ahsante.

I doubt kama ilitolewa warrant ya Kitanzania.....huu ni mtihani mkubwa sana kwa vyombo vyetu vya sheria maana wameshafanyiwa kila kitu imebaki kumeza tuu, sijui watafungua kesi au ndio itakuwa amerudisha asilimia kubwa mwacheni apumzike.
Hivi kwenye upekuzi huu ndio HDD ya Chenge ilikutwa na evidence za kufa mtu au nachanganya madawa??
 
1.
Mtu wako, the illustrious, the one and only, great old Field Marshall E(something?) Systems, kuanzia jana kidogo kawekwa kiti moto juu ya kiti umeme hapa!

Mkuu ili uniweke kitimoto, unahitaji kuwa na ukweli tofauiti na dataz zangu, kwa hiyo sidhani kuwa inahitajika kuwa na PHD kujua aliyewekwa kiti moto hapa toka jana ni nani, kati yangu na "wewe na wenzako", na ni very clear kwamba sasa unatafuta njia ya kujisalimisha maana dataz zimekuzidia kwa uzito na ukweli, tatizo lako wewe ni CUF unachojua ni muafaka tu, na mikutano ya kujificha ficha kule basement kwa Mkulu Wangu mmoja DC!

2.
Usikonde Mkuu.

Mimi nikikonda wewe na wenzako mtakuwa kaburini, na haya maneno yako yanadhirisha only one thing, kuwa wewe ni mgeni hapa, maana dataz hatukuzianza leo wala jana, toka mwaka 2004 tupo hapa tunamwaga dataz, tulianzia BCS, TEF, JF, na sasa another JF, mwendo wetu ni ule ule mdundo, hayo yako yalimshinda TTJ, maana mnafanana sana kwa nonesense!


3.
Tunajaribu kuwa na mfumo wa kuthibithisha na kuchambua "dataz," tusije tukalazimika kuomba wakina Aziz na Chenge misamaha hapo baadae.

"Tunajaribu" what a nonesense unajaribu na nani? Kwani hizi ni dataz za kwanza tunamwaga toka tuanze hapa JF? Humu kuna dataz ngapi za Rostam na Chenge? Toka mwaka 2004 tunamwaga dataz za Rostam na Chenge, wameshitaki media nzima ya bongo lakini kwenye hiii wameshindwa siku zote maana huwa ni ukweli mtupu, Rostam amejaribu mpaka kuleta article zake hapa kujaribu kuchafua watu tumezikataa, na hata siku moja huwa hatutegemei article za internet kama ukweli hapana, huwa tunazo dataz, tuna dataz za Rostam toka alipomfunga Rage, miaka ileeeeee! na ahajatisha mtu hapa, sasa kama wewe unatishika na hao mafisadi usituletee hizo tabia hapa, sisi hatuwaogopi!

4.
Unajua Bongo hamna true Media, kwa mawazo yangu, kwa hiyo hapa JF tuna raw Press yetu wenyewe (na kwa kweli sitakiwi kukuambia wewe haya; wewe ni vete na mmoja wa Statesman wa JF Nation). Lakini japo Press yetu ni rough and raw, tunataka iwe na viwango vinavyo zidi MwanaHALISI na Tanzania Daima. Ni hicho tu.

Mkuu again, hapa hakuna anayemlipa mwingine wala aliyemsomesha mwingine ili kuandika anavyotaka yeye, serikali ilipotufungia haikusema tunaandika raw, wala viwango, walilalamika kuwa tuna habari nzito mno against wakuu wa nchi, wewe huna anything cha kuniambia mimi worthy kwa sababu uelewa wako wa siasa za bongo ni finyu sana, ndio maana unawaogopa binadamu wenzio kama Rostam, na unashauri na mimi niwaogope kama wewe, niwe joga kama wewe, nitetemeke kama wewe mbele ya mafisadi, niwe fisi kama wewe mbele ya wezi wa taifa langu, halafu hayo maneno yako ya ufisi na u-chicken unayaita viwango, so much for viwango!

Take viwango vyako na keep them to your self, mimi sivihitaji viwango vya ufisi, na ujuha, hivyo viwango vyako ni nothing but u-idiocy! Either una ukweli zaidi ya niluouweka au kama ulivyothibitisha hapa so far kuwa huna, hivyo viwango vyako peleka CUF uwasaidie na mufaka, as for me mwendo wangu wa kumkoma nyani ni ule ule, na dataz mbele,

Huna dataz, hoja, wala facts ila una logic za CUF, unaambiwa waziri wa nchi yetu masikini ana dola $ 1,000,000 nje ya nchi yetu, wewe unalilia logic ohh kwa nini benki wamesema hela zake hiyo sio sheria, unaambiwa Chenge ana dola millioni 13 kwenye benki za bongo, wewe unalilia logic tu kwa nini benki imesema unajua Chenge na Azizi watatushitaki itabidi tuwaombe msamaha! What a waste! Kazi yote tunayoifanya hapa JF wengine mtaelimika lini? Ni lini mtaamuka? Hivi hawa viongozi wetu wametufanyia uchawi gani? Wewe ni muoga kama fisi hapa JF unataka nini? Kuna watu kama kina MMJ ambao wameipigisha magoti serikali sio mara moja na wametishiwa weee mpaka maisha yao, lakini bado wanaendelea kumkoma nyani, wewe unahubiri tuwe mafisi na kuwaogopa kina Rostam na Chenge?

Kijana mdogo una habari kuwa wakati unamtetea ni majuzi tu ameihamishia Richimonduli/Dowans kwa Manji? Sasa Manji anaendelea kukusanya hela za Tanesco kwa niaba ya Rostam! je unayajua haya kuwa sasa Manji na Rostam, wameamua kuinunua hata Ze Comedy, ili kuipunguza makali ya kuwasema mafisadi kwenye comedy zao? Sasa wakati mafisadi wanafanya haya wewe unafanya nini mwananchi wewe? Eti unawaogopa? Kwa visingizio vya viwango? Sasa unataka wote tuwe hivyo? kama wewe?

Mungu Aibariki Tanzania!
 
Kaondoka Na Charter Nasikia Uwanja Wetu Wa Zamani....mpo????????
Charter To Uk???????babu Kubwa Salute Huyu Mt2
 
Mkuu Es ahsante kwa point nyingi ulizoweka lakini kuna walakini kidogo!!!

Issue ya Chenge kwenda London haina uhusiano wowote na SFO. Narudia, Chenge yuko London kwa mambo binafsi na SFO walishamalizana naye.

SFO hawajaribu kuisaidia TZ in any way or shape, the investigation is against BAE only. The link to TZ ends with Vithlani and it is true Vithlani had some wire transfers to mzee wa Visenti na ndio sababu ya SFO kumkomalia. Now to prove that the said money was BAE money is where Chenge atatupiga goli sababu SFO hawatakuwa na maelezo kuhusu hela za Chenge wao watawabana BAE na corruption.

Now ni aibu kwa sisi watanzania na viongozi wetu kusema eti tunasubiri uchunguzi wa SFO?? This is insane!! SFO hawachunguzi kwa kina ni viongozi gani wa TZ walipewa rushwa, wao wanachunguza kama BAE walimpa rushwa Vithlani na yeye akawapa viongozi wa TZ. Wakiprove hilo, then wanawabana BAE.

Now link ya Vithlani to TZ leaders hilo swala lilitakiwa libebwe na Usalama, DCI, Mwanasheria Mkuu wa Tanzania, DPP na kamati za bunge.

Hapa tunachezewa shere!!

Ni hayo tu wakuu.

Mkuu hata mimi nina habari hiyohiyo.

Kinachonisikitisha kwa sisi wabongo ni uwezo wetu wa kufikiri. Mimi ningekuwa Director wa PCCB au Director wa Investigations ningekuwa nimejiuzulu kwa kuona aibu jinsi watu wa nje ya nchi yangu wanavyofanya kazi yangu vizuri huku mimi nikikomaa na rushwa za mahakama za mwanzo na polisi wa usalama barabarani!

Shame on PCCB na Polisi Tanzania!
 
Ujaona warning kwamba logic is for kids...hapa ni kumwaga matapishi tuu...

Kapinga,

hapo ndio ES anakupiga bao. Mimi source yangu ya habari ilisema yupo Uingereza lakini sio kwa ajili ya SFO, inawezekana ilikosea. Ukiangalia utitiri wa data za ES na Mtanzania alivyosema kuhusu VIZA inaleta maana.

Tatizo lako ni kuwa ukiwa unapingana na mtu mmoja unawajumuisha watu wote wa JF. Si sahihi, JF ni JF wala haipingamani na ES wala wewe. Inabidi ubadilishe jinsi unavyofikiri.

Thanks
 
Back
Top Bottom