...To me, hii kesi ya BAE/SFO inaonyesha wazi hata kama ni tuhuma, kuna ulazima wa Serikali na hasa Bunge kuunda tume/kamati ya Bunge kuchunguza kazi zote alizozifanya kwa niaba ya Serikali.
...washinikize kuundwa kamati ya Bunge kumchunguza Chenge na kazi zote alizofanya kama Mwanasheria Mkuu. Taifa lipewe tathmini ya kina ya yote aliyoyafanya...
Mchungaji, Jina lake lihimidiwe!
Mimi sipendi hizi kamati za Bunge. Ubaya wa kamati, kwanza, hazina nguzu ya kubana watu kisheria. Product yake, at the end of the day, ni mapendekezo tu. Mazao ya kazi ya kamati inategemea mapenzi, discretion, ya Rais kutekeleza mapendekezo. Na Kikwete anajulikana kwa kukalia ripoti. Ilikuwa ni bahati, bahati mno Kikwete kukubali Serikali yake ivunjwe na kamati ya Mwakyembe. Commentators wengi wamesema hii ilitokea kwa sababu Kikwete alikuwa anataka kubadilisha Waziri mkuu to begin with. Kuna kina Sitta mpaka uruke viunzi vyao kabla ripoti haijasomwa, na kina Pinda wako in charge pale Bungeni, watu ambao wamesha foreclose mashitaka ya kina Mkapa kabla hata hayajaletwa. Siku ikija ripoti, wataleta mizengwe tu.
Isitoshe, hizi kamati nazo saa nyingine zinakuwa extrajudicial. Mwakwembe kuna Due Process fulani alizipinda makusudi ili ripoti iwe nzito. Ki ufupi hakumsikiliza Lowassa. Ilikuwa sawa Lowassa kuondoka kwa sababu anajulikana sio msafi, lakini Mwakyembe, kubali usikubali, alimfanyia drive-by.
Tulazimishe vyombo vilivyopo, vyombo vinavyo bana Kisheria na vinavyo banwa na Sheria za Taratibu za Uchunguzi wa Jinai, ili tusitegemee discretion ya Kikwete, na Sitta na Pinda, kuleta mashitaka. Kamati haziwezi kushitaki mtu.
Zaidi ya Tume ya Kulinda na Kutetea wala Rushwa, na Tume mfu ya Maadili, kuna idara nyingine ya kujitegemea chini ya Hazina, Financial Intelligence Unit, ambazo zote zinatakiwa ziwe na nguvu kuzidi hizi kamati za discretion. Na tusisahau, at the end of the day ni kazi za Polisi, na Director of Criminal Investigation, na Director of Public Prosecution kuchunguza huu udhalimu.
Economic Crimes Act of 1984
21.-(1) The investigation of all economic offences reported to the police shall be conducted by police officers, with the assistance of such public officials or category of public officials as may be designated by the Directorof Public Prosecutions after consultation with the Director of Criminal Investigation
Kwa hiyo kazi za hii Mikamati na Mitume na mi Miidara na Wakurugenzi wote ni duplicate tu, na wanapoteza resources na focus.
Hizi Kamati na Tume Msalie Mtume sio za kuzitegemea hizi. Tuimarishe vyombo vya dola.