Kuna mambo ya msingi sana ambayo Kuhani Mkuu ameyahoji ambayo kuna haja ya kuyajibu. Kwa mfano, mosi, Chenge yupo London kutoa ushahidi au kawa arrested? Pili, kulikuwa na haja kweli JK kutoa search warrant yeye mwenye personally, hakuna vyombo vingine vya kufanya hili? Tatu, ok, kama JK alitoa hiyo search warrant, ilikuwa ni lazima kweli aitoe kisirisiri, si Chenge alikuwa waziri wake, aliyemteua yeye mwenyewe bila shinikizo tena kinyume kabisa na maoni ya wananchi walio wengi, au JK alikuwa na anamuogopa Chenge? Sasa kwa nini amuogope? Hapa ndipo nami nakubaliana na Kuhani Mkuu kuwa bado kuna maswali mengi zaidi kuliko majibu.
Simplicity is the enemy of truth!
Mjomba Kitila,
Ukitumia neno search warrant, tutarudi kule kule kwa kudai je JK ana mamlaka gani kusaini search warrant.
Mimi logic yangu kutokana na hii habari ni hivi.
SFO na serikali yao walimtumia ujumbe JK na kumwambia, katika suala la Radar, uchunguzi wetu unaonyesha kuwa Chenge ni mtu muhimu sana, anaweza kuwa shahidi au mtuhumiwa. SSFO wakamwambia JK, tuna ushahidi mkubwa wa kuonyesha kuwa Chenge amehifadhi mshiko mkubwa ambao source yake ni hiyo kampuni ya Red Diamond na Vithlani ambao ndiyo wahusika wengine wa BAE scandal.
Ilikuwa ni jukumu la JK kukubali au kukataa kama Saudia Arabia walivyofanya kwa kukataa Prince Bandar asiendelee kuchunguzwa.
JK kakubali na hata kawapa barua ya Ikulu inayowapa kibali kufanya kazi nchini na hata kumpekua na kumfuatilia Chenge. Yawezekana alimpa amri Manumba au Mwema wasaini sasa hiyo "search warrant" ili kufuata taratibu za sheria. Hivyo Chenge alipofuatwa na kugongewa hodi, SFO walikuwa na "Search Warrant" na barua kutoka Ikulu.
Kwa nini JK kaamua kumtosa Chenge ambaye alikuwa ni waziri wake? Hapa swali ni gumu kwa Kikwete si kwetu. Uswahiba wa Kichama, Kiserikali na kufichiana siri ndio ulimfanya Kikwete ampe Chenge uwaziri alipounda ile timu ya American Footbal January 2006. Je kwa nini alimrudisha Chenge ambaye tayari alikuwa na tuhuma nzito ya IPTL? jiulize IPTL ilipoanza na ilipofanyika, JK alikuwa wapi na nani? Je mikataba ya madini na kuletwa kwa kina Sinclair kulifanywa na nani? Hata tukienda kwenye mambo ya EPA na ushindi wa Tsunami wa Kikwete au wa Chenge kwenye Halmashauri kuu, bado kuna common denominator ambayo zinawaunganisha (speculation)!
Hivyo yawezekana Chenge kufanywa waziri na Kikwete yalikuwa malipo ya fadhila na siri fulani, hata alipomchagua kwa mara ya pili mwezi Februari, ndiyo maana Chenge aliwaambia Watanzania wakamhoji JK kwa nini karudishwa madarakani.
Sasa hapa kuna wengine watasema ohh JK alikuwa anampigia time na kuvuta muda ili ajikaange mwenyewe kwa kuwa SFO walikuwa wameanza uchunguzi na m=kumfuata Kikwete. Wengine watasema, Kikwete ni naive sana kwa kupuuza mambo ambayo ni obvious mabovu. Sasa hapo chagua mwenyewe lipi lina make sense.
Ujeuri na tabia za viongozi wetu ndio umewafikisha waingie kwenye aibu kubwa kama hizi. Yawezekana Chenge alirudi Bariadi kama mtemi bila kujua kuwa sasa kwa kujiuzulu kwake ambako inawezekana ndiko JK alikuwa anasubiri ili SFO wafanye kweli, ndiko kulikukuwa chachu kwa yeye kubadilishwa kutoka kuwa Shahidi na sasa mazingira kuwa ni Mtuhumiwa.
Kwa nini JK yupo kimya na kujikausha kuachia SFO wafanye kazi hii na si Mwema na Manumba au Mwanyika? ni kwa kuwa wote walikuwa chungu kimoja na Chenge na SFO wamewasitiri JK na labda Mkapa kwa kuwa walikuwa maraisi (another logic speculation)!
Tanzania haitafanya uchunguzi dhidi ya Chenge mpaka CCM iondoke madarakani.