The Radar Scandal: Investigation & Progress

Hongera Mkjj, huyo Chenge anajibu kwa kiburi ila haitamsaidia kitu mambo yako hadharani na yatamnyima usingizi kwa sana! Whether anarudi ahera au anarudi Tz sheria ichukue mkondo wake.Pesa za wizi zina kiburi sana huu ni ushahidi tosha!
 

Umesoma biography ya Biko ukiwa na miaka 13? Hongera sana. Nilimsoma Fanon nikiwa na umri huo huo na sikumwelewa hadi nilipomsoma tena nilipokuwa mtu mzima.

MLK= Mandela kabla ya Umkhonto we Sizwe, Malcolm= Steve Biko.

Ndiyo maana nilikuuliza ulimsoma KWELI ukamuelewa?

Najua hii inayofuata iko nje ya mada, lakini nivumilie! With all due respect,ulitaka Madiba afanye nini wakati alipokuwa rais? Kumbuka haikuwa tuu makaburu waliokuwa tumbo moto bali a virtual civil war kati ya ANC na wakina Buthelezi ilikuwa inaendelea kwenye townships! Huyu amabe pamoja na ushindi wa tsunami aliwakaribisha wazulu na wengine kwenye serikali yake? Huyu ambae pamoja na kupendwa (naam bado anapendwa) aliachia ngazi kwa hiari yake?

Ile nchi ina wazungu ambao ni raia kama alivyokuwa yeye. Ulitaka awafukuze ili athibitishe kuwa sisi waafrika tunaweza bila wao? Au ulitaka awagawie mashamba na maghorofa yote wale walioko Alexandria na Soweto? Angekua kama Mugabe ndiyo ungemuona true revolutionary? Potelea mbali watu wanakufa njaa lakini uchumi uko mikononi mwa waafrika weusi wenzetu!

Basi iko kazi! Kwa mtazamo huo, naona kweli utajifunza mengi kutoka kwa Chenge kuliko kwa Madiba!

Kwa vile naona tumeelewana tunatokea wapi, basi mimi nakaa pembeni.
 

Mimi nimekwambia sijacompare MLK na Malcolm X.

The brain behind the leadership even during Mandela's time was Mbeki!! Na Zuma kamshinda Mbeki kwasababu watu watakaomchagua Zuma wanafikiri atatatua matatizo yao, wakati hata Zuma mwenyewe anaelewa waliochemsha ni Mandela, Mbeki and crew! Mandela alikuwepo pale symbolic tu. Aliaachia ngazi kwasababu alikuwa hana nyimbo wala upeo wa kuongoza modern economy. Aliongoza kipindi cha kwanza kwa heshima tu.

Mambo yote uliyoweka thread ya kwanza kuhusu jamaa, nothing special, hata mimi sijasoma form 1. Alikubali atoke jela kwa masharti, ingawa kuna quotation alitoa mtoto wake anasema otherwise......Maaan please.

Kwavile humpendi Chenge, labda nikupe mfano mwingine. Nitajifunza zaidi nikikaa na Attorney General wa South Africa provided kakaa muda mrefu kama Chenge, kuliko nikiongea na Mandela. Mandela namwona kama babu yangu. A wise old man.

People are willing to point at weaknesses of great men like Nyerere, lakini hamtaki Mandela akosolewe? Pleease!

naenda kulala. gnite mate. nothing personal, just difference of opinion.
 
Nzoka,
Chenge alikuwa mwanasheria mkuu wa serikali kwa miaka mingapi?
 
hiiiiiii...kumbe hili liNzoka nalo lisomi la mavitabu!!!!..... lol


Nzoka,
Chenge alikuwa mwanasheria mkuu wa serikali kwa miaka mingapi?
.........shhhhhhhhhhhi...mwache bana, utamkamatisha bure.....
 
Nzoka,
Chenge alikuwa mwanasheria mkuu wa serikali kwa miaka mingapi?

hiiiiiii...kumbe hili liNzoka nalo lisomi la mavitabu!!!!..... lol



.........shhhhhhhhhhhi...mwache bana, utamkamatisha bure.....

hahaaa, hamna adabu nyie.
State Attorney from 70s, first post on thread inasema State Attorney. AG kipindi cha Mkapa. Jinsi usingizi unavyozidi, msinitege.

Message sent!
 

Nimekutolea mfano wa MLK na Malcolm kwa vile uliwafananisha madiba na Steve Biko!

Yaani kweli unaamini kuwa Madiba alikuwa mwanasesere tu! Unadhani the biggest challenge walioi'face' South Afrika wakati ule ilikuwa ni uchumi tu? Kweli hamridhiki.Mnapata kiongozi anayekubali kuongoza wakati ambao ni mgumu na kuachia ngazi wakati bado anapendwa leo mnamgeuka na kusema alikuwa figure head tu! Mnapopata know-all despots kama wakina Mugabe ndiyo mnawaona werevu! Iko kazi, kizazi cha kesho.




Hii sasa inakuwa tedious!

Asiyempenda Chenge nani? I only took offence ulipomlinganisha na Mandela, that's all.


Zaidi ya kusema kuwa Mandela anakuboa haujatoa criticism yeyote dhidi yake bali myths kama alikuwa akitumiwa na wazungu,na hii ya kuwa Mbeki alikuwa anaendesha nchi! Lord have mercy, huyu bwana alimwachia Buthelezi nchi itakuwa Mbeki! Atakuwaje wise wakati unaona hakuna unachoweza kujifunza kutoka kwake?

Madiba ana matatizo yake. Kwa mfano, aliufumbia macho ugonjwa wa Aids wakati wake. Siwezi kukana hilo. lakini aliacha nchi yenye amani ambayo ingeweza kukumbwa na machafuko makubwa! Hili sio dogo hata kidogo hasa katika mazingira yetu ya Afrika.

For your information, hata ungemfananisha Chenge na Nyerere, nisingekuelewa. Una over-reach katika kujaribu kumtetea Mheshimiwa. Aliyoyafanya ni makubwa lakini there is no way unaweza kumlinganisha na Madiba. Ulikuwa disrespectful, that's all!

Enough said!
 
...Madiba ana matatizo yake... lakini aliacha nchi yenye amani ambayo ingeweza kukumbwa na machafuko makubwa! Hili sio dogo hata kidogo hasa katika mazingira yetu ya Afrika.

Fundi, heshima mbele.

Mimi huwa natatizwa sana tukimpa mtu sifa kwa jambo ambalo anategemewa alifanye. Tukisema sasa siku hizi kuto kupigana vita ndio mafanikio ya Afrika tunakuwa tumeshusha sana viwango. Kwa hiyo sidhani kama Mandela inabidi asifiwe kwa hilo.

Vinginevyo inabidi tumtuze Mkapa, Mwinyi na Kikwete kwa mafanikio makubwa Tanzania kwa sababu wali iepusha nchi na vita. Ahsante.
 
unajua mtu anazungumza with contempt... the guy is not humble at all.. he is in a fight or flight mode..
 
Hiyo jeuri haitamsaidia kabisa kwenye court of public opinion....(not to say that it matters...but in a way it does)
 
Kwa hapwa JF ile sosi ya habari hii inabidi sasa iane kutiliwa shaka ,au kwa inavyoonekana ulaji umeanza kuwafikia wadau wa habari nyeti hapa jungu kuu yaaani sasa badala ya ukoko wanaleta na matandu.
 

Hapana Mkuu! Hauwezi kulinganisha hata siku moja hali iliyojiri Tanzania na ile iliyokuwa Afrika Kusini. Hatujawahi sisi kuwa na utawala dhalimu kama wa makaburu. Mandela angeweza kuamua kulipiza kisasi na wengi wetu tungemuelewa. Sijui kama unakumba lakini mapigano na mauaji baina ya wafuasi wa ANC na wale wa chama cha Chief Buthelezi yaliishaanza. Watu walikuwa wanuana ovyo kwenye hostels. Si hizi ngonjera zetu za kila siku, kule chuki na fujo viliishaanza. Ni yeye aliyeweza kuzima kwa kumkaribisha Buthelezi na kumfanya makamu wa rais ingawa ANC ilishinda uchaguzi kwa kishindo. Ilifika hata kuna wakati alisafiri na kumuachia Buthelezi nchi! Ni kiongozi gani wa kiafrika angeweza kufanya hivyo? Sisi hapa tunapata kigugumizi kukabili matatizo ya Zanziba ambako wote tunajua CUF wanakubalika na sehemu kubwa ya jamii? Makaburu waliishaanzisha kasehemu kao mpaka hapo Mandela alipowafuata kuongea na mjane wa nadhani Vorster! Hawa waliomfunga kwa miaka 27! Nani katika viongozi wetu angeweza kufanya hivyo? Nchi ilikuwa imegawanyika imewagawanyika katika michezo ( na kuna ushabiki gani unaoshinda wa kwenye michezo, pengine wa dini) akawaunganisha wakati wa mashindano ya dunia ya Rugby. Huyu bwana aliitwa kama shahidi (akiwa rais) mahakamani akaenda na kukubali kuapishwa kama raia mwingine. Huyu ndiye aliyeanzisha the Truth and Reconciliation Commission kujaribu ku'heal' jamii ya watu wake badala ya kukimbila kwenye visasi. Sasa hivi nchi nyingi zinaiga mfano huu. Na zaidi ya yote, baada ya term moja akaamua kuachia ngazi! Ana matatizo yake kama binadamu wengine lakini hatuwezi hata siku moja kumfananisha na hawa wa kwetu. Yeye na huyo mwengine ambaye hawa arm chair revolutionaries wana gall ya kumuita kibaraka, Archbishop Tutu, ni watu ambao mimi kama mwafrika wananihakikishia kuwa SIVYO TULIVYO.

Amandla!
 

Mh! kweli dunia ni mduara, tuliyoyashuhudia miaka ya '84 ya watu kuzikana pesa zao yameanza tena kujitokeza! ama kweli mzimu wa Sokoine bado unafanyakazi. kweli mtu unatuma ujumbe kwenda kumbembeleza mtu iliakubali kutolea maelezo pesa ambazo ziko kwenye akaunti yako!!???.

Naomba Mungu huyu Mjumbe arudi na jibu bovu kuwa jamaa amekataa kuzitolea maelezo, kisha waniite mimi ama wabandike matangazo sehemu mbalimbali kutafuta mtu mwenye sifa ya kuweza kutolea maelezo zile pesa ajitokeze ili ziwe zake!

Naombeni jamani, huyo mjumbe atakaporudi tujulisheni kaja na jibu gani! Kwani unaweza kujikuta unaanza kuimba zile nyimbo zetu za wakati huo;

Shilingi ya Nyerere katikati kuna mwenge!..dolly dolly, dolly Samora!
 

Naona unaweka mkazo kweli kweli kwenye Havard wakati jamaa ameshindwa hata kutengeneza contracts za maana kwa ajili ya mwajiri wake ambaye ni serikali ya TZ?

Mambo yale yale ya kufikiri kwasababu kasoma Havard university basi ana uwezo mkubwa.

Kama ana uwezo mbona hata hizo contracts zimechoka ile mbaya?
 

Hivi kama contract kachemsha hivyo, waTanzania wanasubiri nini kuzibadilisha sasa? All you do is complain and complain, kama uchungu wa nchi upo, nini kinawazuia hayo mabadiliko?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…