TBC MPYA: Ushauri, Maoni na Mapendekezo ya ubora wa vipindi (Television Content)

Travic

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
719
1,000
Ndugu WanaJF,

Kumekuwepo na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi na hata hapa JF kuhusiana na changamoto ya vipindi vya Televisheni ya Taifa (TBC1). Malalamiko hayo yameegemea zaidi katika eneo la ubora wa picha na ubunifu wa vipindi.

Kwa bahati nzuri, Mkurugenzi pamoja na Watendaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) ni wadau wakubwa wa JamiiForums na huwa wanafuatilia taarifa na mijadala mbalimbali inayoendelea hapa. Hivyo tukiitumia vyema nafasi hii, tutawasaidia kuboresha maeneo ambayo yanatakiwa kurekebishwa kwa haraka.

Naomba tutumie uzi huu kutoa maoni, ushauri na mapendekezo kuhusu aina ya vipindi na ubunifu ambao ukitumiwa utasaidia kuifanya televisheni hii ya taifa kuvutia kutazamwa na kufurahiwa.

Tumeshalalamika sana. Sasa ni wakati wa kuchukua hatua na kutaja suluhu kwa mifano ili kuimaliza changamoto hii kabisa.

Karibuni sana.
 

boniuso

JF-Expert Member
Mar 13, 2013
298
500
Daaa nyie hatakuwashaur hatujui wapi pa kuanzia......... Labda kwanza mungeibadir iyo T iwe Ccm Broadcasting Television CBT. Kifupi mnatuboa saana mpka kutoa ushaur tunaona uvivu
 

Chumchang Changchum

JF-Expert Member
Nov 1, 2013
4,436
2,000
Mafunzo ya mwezi kivipi? Unaweza fananisha viwango vya elimu vya TBC na chombo chochote nchini? Wao huajiri kujari sana elimu mnaotaka sauti muonekano nendeni TV za mitaani jua hiyo ni ya serikali kamwe haiwezi fanana na binafsi
Kama mtaeshimu michango yetu ili mbadilike nina uwakika mtaboresha TBC. Ikiwa mnajibu kifedhuli kama hivi mjue ilo chombo kitakufa kwa midomo yenu michafu.
Mafunzo ya vitendo kwa vyombo vingine na msione aibu nendeni hata private television mkajifunze kwa kujitolea...
Kusoma sio mpaka muingie darasani..
 

deo paul555

JF-Expert Member
Oct 22, 2018
1,326
1,500
Daaa nyie hatakuwashaur hatujui wapi pa kuanzia......... Labda kwanza mungeibadir iyo T iwe Ccm Broadcasting Television CBT. Kifupi mnatuboa saana mpka kutoa ushaur tunaona uvivu
Haiwezekani ccm wanayo yakwao chanelten,TBC 1 ya serikali toa mapendekezo kipi kifanyike acha kupotosha watu au kupoteza maana ya huu ukurasa
 

ipogolo

JF-Expert Member
Aug 15, 2011
5,966
2,000
Waambieni watangazaji wenu hasa Hawa vijana, wanapotutajia NAMBA za Simu watamke taratibu.
Waige mfano wa Mbazigwa, Swed Mwinyi. Wanataka tarakimu vizuri.
 

FRESHMAN

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
3,852
2,000
kwa kweli TBC inasikitisha sana..

millard ayo ana cover habari nyingi na ana waandishi nchi nzima... hata tukio la mbali bado anafanya coverage .. ila tbc na rasilimali zote na ruzuku zote ila hakuna kitu..

millard ana matangazo na wazamini wengi.. mpaka misri kwenye afcon kapeleka waandishi wake ila tbc.. kimyaa..

hata kuonesha mechi za taifa starz wameshindwa? rais piga chini tbc nzima tuanze upya tu
 

Lord eyes

JF-Expert Member
Aug 2, 2018
7,378
1,995
Itawezekana endapo upinzani ukichukua nchi maana wapo kuhakikisha meko na naibu wake wawe juu kisiasa
 

LOTH HEMA

JF-Expert Member
Dec 6, 2015
5,031
2,000
Ki Ukweli Yule Bosi Wake Kakosa Ubunifu, Tofauti na yule bosi mwingine aliyemtangulia alikuwa anaenda na wakati wa matukio. kumbe wataalamu nao hutofautiana kwenye mission zao. ila huyu jamaa wa sasa anapaswa kupumzishwa kazi au apangiwe kazi nyingine, hakuna mabadiliko makubwa aliyoyafanya tangu awe bosi pale
 

share

JF-Expert Member
Nov 22, 2008
3,955
2,000
Hili dudu TBCCM linaboa sana. Linachojua ni KUUNGA JUHUDI tu kwa mtindo wa kujikomba. Hivyoooo!
 

Haji2017

Member
Dec 30, 2018
13
45
Maoni yangu kwanza muwe na ratiba ya vipindi maana unaweza ukakaa wiki nzima kipindi hiko hiko sasa cjui mna kwama wapi kingine ubora wa picha bado poor kabisa wakati mna vifaa vya kisasa au kama mnashindwa kuvitumia iteni wataalam wawapige msasa mna gari zuri la kurushia matangazo ila hamuonyeshi hata timu yetu ya Taifa ikiwa inacheza hapa uwanja wa nyumbani ila mpo tayari kusafiri masafa mkarushe matangazo ya ccm live hapa nashindwa kuelewa ni TV station ya chama au ya Taifa
 
Top Bottom