Waambieni watangazaji wenu hasa Hawa vijana, wanapotutajia NAMBA za Simu watamke taratibu.
Waige mfano wa Mbazigwa, Swed Mwinyi. Wanataka tarakimu vizuri.
millard ayo ana cover habari nyingi na ana waandishi nchi nzima... hata tukio la mbali bado anafanya coverage .. ila tbc na rasilimali zote na ruzuku zote ila hakuna kitu..
millard ana matangazo na wazamini wengi.. mpaka misri kwenye afcon kapeleka waandishi wake ila tbc.. kimyaa..
hata kuonesha mechi za taifa starz wameshindwa? rais piga chini tbc nzima tuanze upya tu
Ki Ukweli Yule Bosi Wake Kakosa Ubunifu, Tofauti na yule bosi mwingine aliyemtangulia alikuwa anaenda na wakati wa matukio. kumbe wataalamu nao hutofautiana kwenye mission zao. ila huyu jamaa wa sasa anapaswa kupumzishwa kazi au apangiwe kazi nyingine, hakuna mabadiliko makubwa aliyoyafanya tangu awe bosi pale
Maoni yangu kwanza muwe na ratiba ya vipindi maana unaweza ukakaa wiki nzima kipindi hiko hiko sasa cjui mna kwama wapi kingine ubora wa picha bado poor kabisa wakati mna vifaa vya kisasa au kama mnashindwa kuvitumia iteni wataalam wawapige msasa mna gari zuri la kurushia matangazo ila hamuonyeshi hata timu yetu ya Taifa ikiwa inacheza hapa uwanja wa nyumbani ila mpo tayari kusafiri masafa mkarushe matangazo ya ccm live hapa nashindwa kuelewa ni TV station ya chama au ya Taifa
Yaani Morogoro watu zaidi ya 50 wameteketea kwa moto na kadhaa kujeruhiwa, kituo cha taifa kinaonyesha wajasiriamali wadogo!!! TBC are you guys serious?
TBC inahitaji rebranding na kiongozi mbunifu wa kuondoa fikara za kudhani bila ruzuku ya serikali haliwezi kujiendesha wakati kiukweli kwa base iliyonayo tbc ya kutapakaa kila mahali ni mtaji tosha wa kuwa na contents nzuri za kibunifu zinazouzika na kuwavutia wanaohitaji kutangaza na tbc. Sio tu matangazo, bali hata bidhaa mbadala lukuki zinazoambatana masuala ya utangazaji. Hatuyaoni sokoni.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.