Hongera TBC kwa uboreshaji wa vipindi vyenu

Mausingizii

Member
Jul 14, 2022
82
67
Ni ukweli usiopingika kuwa tukivizungumzia vyombo vikubwa vya habari nchini, hatutasita kulitaja shirika la habari Tanzania.

Hii ni kutokana na ukongwe na jina lililojijengea kutoka radio Tanzania hadi TBC na hata uwezo wa kuwafikia wanachi Tanzania nzima.

Ni wazi kuwa mfumo uliokuwepo awali ulipelekea TBC kuonekana kama Televisheni ya wazee na vigogo walioko serikalini, hii ni kutokana na maudhui na namna ya uwasilishaji wa taarifa zake.

Taarifa za TBC kwa kiasi kikubwa zilitofautiana na Taarifa kutoka Chanel nyingine, kwani zilionesha kuegemea upande mmoja, ukasuku na taarifa zisizo na (human interest).

Uwasilishaji wa hoja bado ulikuwa wa kizamani, wazee hawataki kubadirika na kwenda na usasa, wameng'an'gania script na si kujikita katika ubunifu kama vyombo vikubwa vya habari ambavyo vinamvuta mtazamaji mwanzo hadi mwisho wa stori au habari, tena kwa njia ya muingiliano wakiwa wamerelax.

Vifaa havikuakisi hadhi ya televisheni ya taifa, muonekano haukua bayana, inakwama hali inayopoteza ladha na umakini kwa watazamaji.

Kwasasa naona kasi kubwa ya mabadiliko kuanzia muonekano wa picha mjongeo, mgawanyo wa majukumu ambao umewezesha kuwapa fursa vijana wengi ninaowaona kwenye runinga, mfano katika vipindi vya burudani, elimu na hata sasa mmejiongeza na kuwa na waandishi vijana wanaotangaza kwa lugha ya kiingereza, hongereni sanaaa.

Lakini licha ya hayo bado mnasafari ndefu ya kutuhabarisha, bado mna mengi ya kutujuza wasikilizaji wenu ,lazima mboreshe baadhi ya mambo kama televisheni ya Taifa ya kuwasemea wananchi.

Rekebisheni ubinafsi miongoni mwa watumishi, ushirikiano baina yenu na wanaofanya field na intern ni mtu.

Mna ubinafsi hasa nyie wakongwe kwa kuhisi kuwa mtazidiwa kete na wageni.

Hamtoi ushirikino na mnaishia kuwabeza, hali inayopelekea kukesana kwa changamoto mpya katika sekta hii. Angalau aliyekua mkuu kitengo cha habari alihamishwa naona ushirikishwaji wa wageni umeleta tija na mabadiliko.

Jambo la pili ni kuhusu habari zimejikita katika kuisifu serikali na kupelekea chombo hicho kuwa kama PR wa serikali, maana ya televisheni ya taiga ni kutusemea, tupelekeeni changamoto zetu kwa serikali na si kutoa masifa kutokana na utawala huu kwenda huu na maslogani kibao.

Kipindi cha Magufuli ooho tujifukize, kipindi cha Samia ooh tuchanje, mnakuwa kama chawa sasa.

Mbali na hilo habari za so..said so ndo nyingi.

Eeh waziri kasema, oooh watumishi wamesema watawajibika, tunataka habari tamu zenye uzito, hoja nzuri hats km ni machawa chaweni kwa hoja, igeni kipindi cha Dk 45 cha ITV, hoja nzito za kuleweka.

Siyo kuwapaka mafuta na kujifanya tumefanyaa tumefanyaaa, tumetekelezaaaa tumetekeleza.

Na ambayo hayajatekelezwa aseme lini atatekeleza.
Mwisho niwatakie utekelezaji mwema wa maukumu yenu.
Chao.
 
We vipi? Hujui kuwa tbc ni mdomo wa serikali? Unalinganisha na independent television, ni bora ungelinganisha na kbc, ubc, mbc na zbc maana hao wanafanana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom