TBC MPYA: Ushauri, Maoni na Mapendekezo ya ubora wa vipindi (Television Content)


Travic

Travic

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2012
Messages
680
Points
1,000
Travic

Travic

JF-Expert Member
Joined Dec 26, 2012
680 1,000
Ndugu WanaJF,

Kumekuwepo na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi na hata hapa JF kuhusiana na changamoto ya vipindi vya Televisheni ya Taifa (TBC1). Malalamiko hayo yameegemea zaidi katika eneo la ubora wa picha na ubunifu wa vipindi.

Kwa bahati nzuri, Mkurugenzi pamoja na Watendaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) ni wadau wakubwa wa JamiiForums na huwa wanafuatilia taarifa na mijadala mbalimbali inayoendelea hapa. Hivyo tukiitumia vyema nafasi hii, tutawasaidia kuboresha maeneo ambayo yanatakiwa kurekebishwa kwa haraka.

Naomba tutumie uzi huu kutoa maoni, ushauri na mapendekezo kuhusu aina ya vipindi na ubunifu ambao ukitumiwa utasaidia kuifanya televisheni hii ya taifa kuvutia kutazamwa na kufurahiwa.

Tumeshalalamika sana. Sasa ni wakati wa kuchukua hatua na kutaja suluhu kwa mifano ili kuimaliza changamoto hii kabisa.

Karibuni sana.
 
T

Tyupa

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2013
Messages
788
Points
1,000
Age
63
T

Tyupa

JF-Expert Member
Joined Aug 11, 2013
788 1,000
Channel mpya ya Safari Channel ilipoanza ilionekana kama chaneli tishio kwa sababu watu wengi sana wanapenda kuangalia wanyama na matukio ya utamaduni wetu.Watu wengi awali walikuwa waking alia chaneli za wanyama za nje lakini baada ya kufunguliwa hii chaneli ya kwetu watu walihamia nyumbani.Baada ya muda mfupi tayari waandaji wa vipindi vya chaneli hii wameanza kuharibu kwa kasi ya ajabu na tayari watu wameanza kurudi kwenye chaneli zao za nje.Vipindi vingi vya Safari Chaneli vinarudiwa rudiwa mno hadi inakuwa chukuzo.Kuna makabila mengi Tanzania ambayo yote yana utamaduni wao lakini nafasi hayapewi.Mikanda ya wanyama iko mingi na mizuri mno lakini yote haioneshwi kamwe.Waandaji wanashindwa hata kumuenzi mzungu alietengeneza mkanda mashuhuri wa wanyama uliojulikana kwa jina la SERENGETI SHALL NEVER DIE.Huyu mzungu simkumbuki jina lakini katika harakati zake za kupiga picha za wanyama katika mbuga ya Serengeti kwa kutumia helicopter yake binafsi alipata ajali baada ya ndege kugongwa na mapopo na kuanguka na yeye alifarika dunia.Baada ya ndugu zake kufika toka Ulaya waliamua azikwe Tanzania na kujengewa mnara wa kumbukumbu pale pale alipoangukia na ndege yake.Mtoto wake mkubwa katika kutoa neno kwa serikali ya Tanzania alitamka neno la ajabu na la kishujaa mno.Nanukuu alivyosema mtoto huyo, " Baba amekufa lakini Serengeti haitakufa.Alichukua mikoba ya baba
na kumalizia kazi ya kupiga picha wanyama.Filamu yake aliita SERENGETI SHALL NOT DIE!!.Ni picha iliovutia mno watazamaji kipindi kile.Waandaji wa vipindi vya Safari Chaneli sidhani hata kama wanafahamu kumbukumbu hii muhimu na si ajabu hata nakala ya ya picha hawana.Ni aibu kufuta kumbukumbu ya jinsi hii.Nawasihi itafuteni ili vijana wa sasa waweze kujifunza kutoka kwenye mkanda huo wa kusisimua.Kwa sasa watu wamechoka mno navipindi vya kurudia yale yale kila siku.
 
Shine

Shine

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2011
Messages
11,498
Points
1,225
Shine

Shine

JF-Expert Member
Joined Feb 5, 2011
11,498 1,225
Hii TV hata mwaka unaisha sijaangalia chochote maana nadhani ni TV ya chama na hata kama Mimi ni mwanachama wa chama husika haina maana kuwa hitaji langu kubwa ni kuona mambo ya ki chamachama! Kaeni kama kamati fanyieni kazi mawazo ya watizamaji vinginevyo mtakua wa kuwafurahisha vingozi mnaochukua picha zao wakijaribu Ku view waliyofanya huko mtaani kwenye ziara, mna boa mna boa as if kazi hamjasomea kachukuliwa tu na mjomba ' kusoma si unajua tena kiswahili' njoo upige porojo TV na redio zetu zipo, pia cha ajabu kwa miaka hii MTU hawezi kutofautisha R na L unamweka kutangaza TV ya Taifa shame on you, kuahirisha hawezi kutamka unasikia kuhairisha inatia kinyaa cha kutapisha! Mbona zamani hatukusikia uchafu huo!

Sent using Jamii Forums mobile app
Hii ni wengi hatuifuatilii japo baadhi ya ving'amuzi wamejitahidi kuondo local channel ili tuitizame ila bado

Sent using Jamii Forums mobile app
 
S

Salange

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2018
Messages
303
Points
250
S

Salange

JF-Expert Member
Joined Jul 28, 2018
303 250
Nyambona Masamba apewe kazi nyingine sio usomaji wa habari za kimataifa kwa sababu sauti yake inatokea puani na haisikiki vizuri hadi inakuwa kero na mateso matupu kumsikiliza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
N'yadikwa

N'yadikwa

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2014
Messages
3,820
Points
2,000
N'yadikwa

N'yadikwa

JF-Expert Member
Joined Aug 10, 2014
3,820 2,000
Mkuu wa TBC1 tuliambiwa mnakamilisha kufunga mitambo ya nguvu ili picha ziwe angavu yaani HD vipi lini hiyo project inakamilika...maana picha ubora unakwaza wanandugu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
N'yadikwa

N'yadikwa

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2014
Messages
3,820
Points
2,000
N'yadikwa

N'yadikwa

JF-Expert Member
Joined Aug 10, 2014
3,820 2,000
Aidha nashauri mfikirie kufanya uwekezaji mkubwa wa studio sets za TV nikishauri mkajifunze KBC au CITIZEN TV Kenya mpate designer wa studio za kisasa kama za wale wenzetu...studio za sasa zinapwaya sana hasa kwa mtindo wenu wa multiple hosting ya vipindi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
T

Tyupa

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2013
Messages
788
Points
1,000
Age
63
T

Tyupa

JF-Expert Member
Joined Aug 11, 2013
788 1,000
Matangazo ya TBC1ya kipindi cha HADUBINI ya tarehe 13/04/2019 saa 2 usiku hayakuandaliwa vizuri kwa sababu sauti ya mtangazaji ilikuwa mbaya mno na ilikuwa haisikiki vizuri.Pamoja na kwamba kipindi kilikuwa kizuri sana kilichohusu nyumba ya ghorofa mbili iliotelekezwa na mzungu.Watu wengine wote waliokuwa wanazungumza sauti zao zilikuwa zinasikika vizuri.Tatiza la sauti mbaya na kutosikika vizuri liliendelea hadi mwisho wa kipindi kana kwamba fundi mitambo wa TBC 1 hakwepo na hakuona dosara hiyo iliokuwa wazi kabisa.Wahusika pia hawakuomba msamaha kwa Watanzania kutokana na tatizo hilo. Matatizo mengi ya TBC pengine hayafanyiwi maboresho kwa sababu pengine wahusika wanajua wao wanafanyakazi kwa ufanisi mkubwa wakati sio sawa.Kumekwepo na malalamiko mengi sana kuhusu chaneli mpya Tanzania Safari inayoonesha wanyama wetu na utamaduni wa makabila mbali mbali. Malalamiko hayo yanahusu kurudia rudia vipindi vile vile kwa muda mwingi.Yapo makabila mengi na utamaduni wao na iko mikanda mingi ya wanyama lakini TBC wameng'ang'ania ile ile kila siku.Kila siku tunaona wajukuu wa Mkwawa na kabila la Wahzabi na nyumbu. Hivi hakuna hata mtu mmoja wa TBC anaepitia maoni ya wadau mitandaoni ili waweze kuyafanyia maboresho?? Hakika watu wamechoka sana kuangalia marudio ya vipindi.Wahusika tuelezezeni kuna shida gani inawasibu na maandalizi ya vipindi vyenu.Sasa watu wamehamia chaneli zingine za wanyama ambazo nazo nyingi zinatoka mbuga za wanyama wa Tanzania.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Forum statistics

Threads 1,285,027
Members 494,367
Posts 30,847,695
Top