TBC MPYA: Ushauri, Maoni na Mapendekezo ya ubora wa vipindi (Television Content)

Pili, boresheni ubora wa vipindi pamoja na ubora wa picha.
Yaani jamaa amegusa kwenyewe. Ninategemea kuiona TBC ikiwa na vipindi dizaini ya Hardtalk, Leaders with Laqua, Empire (Al Jazeera), The Heat (CGTN) na dialogues kadhaa zinazoongozwa na watu wenye kuuliza maswali magumu na sio mepesi mepesi. Naamini huwa wanaziona hizi channel lakini mpaka inafika wakati unajiuliza kama wanajifunza chochote kutoka kwa wenzao waliowatangulia kama hawa
 
Ndani ya muda wa nusu saa, unahabarishwa mambo lukuki na yasiyoendana. Mfano; yanaanza matangazo ya biashara,unaingia mziki wa aibu wa kina Diamond, inaingis hotuba fupi ya Mh. Rais, linaingia tangazo la kampeni, inatokea hotuba ya Rais ya kutekeleza ahadi , zinsingia habari za bunge nk.
Katika mchanganyiko kama huo, mtazamaji huchoka akili mapema. Kwa maana nyingine anaona kama makelele fulani hivi.
Rai: Ubunifu na upangaji vipindi uboreshwe.
 
huyu mkurugenzi wao wa sasa bure kabisa wameshindwa kubuni vipindi vya maana kila siku ni hayohayo tu
 
Sina uhakika kwa Dunia hii na Afrika kwa ujumla kama kuna shirika la habari lenye Archive kubwa[Maktaba] kama TBC. kuanzia mziki, hotuba na kadhalika mfano wa sasa kwa miaka 20 baadae ni kama watakavyokuja kumsikilia kwa wakati huo Mwl Kashasha say 2040.
Ifanyeni hii archive ya kibabe iwe hai na sasa pia, na isikilzwe na wengi pia.

Chagueni vijana wachache kwenye Tasnia na kushare nao hii archives japo kwa hotuba madhalani Adam Mchovu kwenye segment yake ambayo pia anagusia siasa, na wengine kwenye michezo pia.
 
Back
Top Bottom