Je, una Maoni/Ushauri kuhusu Jambo au Utaratibu unaotamani ubadilike katika kuboresha Sekta ya Afya Nchini?

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Aug 7, 2018
625
938
IMG_20230709_013114_587.jpg


SEKTA YA AFYA: Je, una Maoni/Ushauri kuhusu Jambo au Utaratibu unaotamani ubadilike katika kuboresha Sekta ya Afya Nchini?

Usikose kujiunga nasi katika Mjadala wa Mapendekezo kwa Wizara ya Afya siku ya Alhamisi Julai 13, 2023, kuanzia Saa 12 Jioni hadi Saa 2 Usiku, kupitia Twitter Space ya JamiiForums

Wizara itakuwepo kusikiliza na kuchukua maoni ya wadau wote ili iyafanyie kazi au kuyatolea maoni (itakapobidi)

Pia unaweza kuandika maoni yako kwenye uzi huu yatasomwa siku ya mjadala.

Karibu

Kujiunga na mjadala gusa hapa

====
Bosco, Mtaalam wa afya ya akili
Wizara ya afya iboreshe upande wa afya ya akili hasa taarifa zinazowahusu wagonjwa. Wagonjwa wengi taarifa zao hazijahifadhiwa vizuri.

Kila kada ya afya iwe na leseni.

Dr. Derick Nyasebwa
Huduma za afya haziwezi kutolewa bure. Kisiasa linaweza kusemwa, ila practically haiwezekani. Afya ni huduma ya pili kwa kutumia fedha duniani. Huduma za afya ni gharama kubwa sana.

Zinalipiwa sababu ya sustainability ya kila wakati, pia ili ziwe na ubora. Mfano, MRI mashine inanunuliwa karibu bilioni 3 hadi kuifunga kituoni. Pia, inatakiwa iwake saa 24 kwa uhai wake wote bila kuzima.

Fikiria kuhusu umeme na vimiminika vinavyotumika kuiendesha, inaweza hadi kula lita 60 kwa saa.

Lazima huduma za afya zilipiwe. Huu ni mfano mmoja tu kati ya mifano mingi.

David Joseph
Matibabu yanaweza yasiwe bure, lakini gharama zake zinaweza kupunguzwa ili hadi yule mwananchi wa chini kabisa aweze kumudu gharama.

Kuendesha sekta ya afya ni gharama kubwa sana, lakini walau gharama zipunguzwe.

Maeneo kama yale ya mama na mtoto hayana vifaa vya kutosha, huko nako Serikali ikuangalie. Pia gharama zipunguzwe.

Hatukatai kuchangia, bali gharama zipunguzwe.

Anodi Kaihula
Tukubali kuwa dunia ya sasa hakuna kitu cha bure, tunaposema bure maana yake kuna mtu analipa.

Naungana na wadau wanaosema huduma za matibabu zinazidi kupanda, sio kwa kuwa serikali inapenda, huduma haziwezi kuwa bure na kama taifa lazima tukubali.

Tunaweza kuona namna ya kufanya kila mtu anapata huduma hata bibi wa kijijini aweze kugharamia.

Hii notion ya bure pia ina changamoto zake kwenye ubora wa huduma na uhuru wa kuhoji, ni kama chakula cha hotelini unaweza kuhoji ila chakula cha msibani (cha bure) hauwezi kuhoji wala kulalamika.

Lazima tuwe na sera shirikishi itakayomfanya kila mtu achangie na awe na nguvu na uhuru wa kuhoji.

Kachapa Chwade
Kila mwananchi analipa kodi iwe moja kwa moja au kupitia TRA, Serikali inajua wananchi ni maskini na wananchi wanachangia pato kupitia kodi.

Serikali ione namna ya kusaidia hawa watu, na walipa kodi wakubwa wapewe motivation ili waendelee kulipa kodi.

Abdy Mrisho
Serikali inaweza kutoa matibabu bure, kama imeweza kutoa elimu bure basi na afya inawezekana.

Huduma nyingi za afya ni ghali, hata bima sio rahisi kuipata kwa mtanzania wa kawaida.

Pia bei za dawa ni kubwa, vipimo pia ni ghali sana kwa mtanzania anayetegemea kilimo.

Kama imewezekana kwenye elimu, Serikali inaweza kutengeneza namna ya kuwezesha pia matibabu yawe bure.

Dr. Kimweri
Kiukweli kutoa huduma ya afya kwa wananchi wote bure ni ngumu kwa hizi nchi zetu zinazoendelea, maana hata budget zinategemea misaada ya nje.

Kitu ambacho mimi nafikiri kinaweza kufanyika ni serikali kukamilisha mchakato wa bima ya afya kwa wote itasaidia.

Labda pia serikali inaweza kuondoa kodi kwenye dawa za kawaida zinazotumika sana kwa watu wetu, maana yake hata gharama za matibabu zitashuka.

Kimmoto
Yeyote anayedhani tunaweza kupata huduma za afya bure anapaswa kusahau hili wazo, huduma za afya ni ghali.

Tunaweza kulazimisha iwe bure, lakini tujiandae unaweza kwensa ukakuta tu mkeka.

Mifumo ya serikali itengenezwe kidigitali, mtu anaweza kuchukuliwa kipimo (mfano cha ultrasound) akiwa Morogoro kisha ikasomeka kote atakapoenda kwa rufaa.

Sio ultrasound tu. Hii inaweza kuwa kwa vipimo vyote. Bado mfumo wetu wa afya una matobo mengi.

Pia gharama za matibabu ziagaliwe, unaweza kukuta bill ya wagonjwa 100 muhimbili ni tsh 10,000,000 lakini hao hao wakienda private unakuta bill ni 100,000,000.

Dr. Derick Nyasebwa
Asilimia 40 hadi 50 tunazotumia kwenye matibabu zipo kwenye dawa.

Hatuna viwanda vya dawa vya kutosha.

Gharama za Kusajili Dawa kwa Tanzania ni karibu Dola 7500 huku usajili ukichukua hadi Mwaka mmoja.

Pia, kuna ishu ya Kodi kwenye Spea za Vifaa Tiba, kuna Spea zinafika hadi Dola 30,000 ukijumlisha na Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) gharama inazidi kuwa kubwa.

Tanzania hadi Miaka 3 iliyopita ilikuwa inahitaji Lita Milioni 30 za Maji ya Drip, kwahiyo hoja kubwa hapa ni kuongeza idadi kubwa ya Viwanda vya Dawa pamoja na Serikali kuwezesha Uwekezaji kwenye Viwanda ili viweze kuzalisha Dawa kwa kiasi kikubwa.

Jackson Ilangali
Kuna njia za kupunguza gharama za Matibabu ikiwemo kuwa na Bima ya Afya, lakini inaweza kufanya kazi kama Mwananchi anaweza kudunduliza kwenye malipo

Njia ya pili ni NHIF kuanzisha Makubaliano na Taasisi za Kifedha ili Wananchi waweze kupata Mikopo ya Kugharamia Afya.

Serikali inaweza kuanzisha Kodi kwa Watengenezaji wa Soda, Bia, Sigara na bidhaa ambazo zinajulikana zinachangia uwepo wa Magonjwa yasiyoambukiza.

Kodi hiyo ingekatwa moja kwa moja kwenye kila bidhaa ili iingie kwenye Mfumo wa Gharama za Afya.
 
Wafundishwe castomer care

Wafanye mtihani kabla hawajaajiliwa

Wodi zifungwe camera za kurekodi matukio

Mwisho waboreshe maslahi na vitendea kazi.
 
Kwa nini? Wazungu na private hospitals wanafanya hivyo kwenye hospital zao
Mkuu, private hospital zipi hizo? Wazungu wapi hao?

Kitu cha kwanza anachofundishwa mtoa huduma wa afya akiwa mafunzoni ni kuhakikisha usiri wa taarifa, huduma na vyote vile atakavyoridhia mgonjwa kufanyiwa.

Haruhusiwi kukufanyia kile wewe hutaki akufanyie.

Kuweka camera wodini ni sawa na kuvujisha taarifa na huduma ulizomwambia kuwa ni siri yake na yako.
 
Mkuu, private hospital zipi hizo? Wazungu wapi hao?

Kitu cha kwanza anachofundishwa mtoa huduma wa afya akiwa mafunzoni ni kuhakikisha usiri wa taarifa, huduma na vyote vile atakavyoridhia mgonjwa kufanyiwa.

Haruhusiwi kukufanyia kile wewe hutaki akufanyie.

Kuweka camera wodini ni sawa na kuvujisha taarifa na huduma ulizomwambia kuwa ni siri yake na yako.
Eg Hospital ya Mt Emaculata Ikonda Njombe
 
Mifumo ya tehama iwepo kuanzia ngazi ya zahanati, inayounganisha ngazi zote za vituo vya huduma za afya nchi nzima, kurahisisha upatikaji wa taarifa za wagonjwa, pia wataalamu wa kuisimamia waajiriwe.
 
Madaktari naona mnatetea upande wenu tu wa biashara. Kweli mko serious kusema serikali inaelemewa kutoa huduma, sijui inajenga hospitali nyingi hivyo tusiibebeshe mzigo mwingine, kwani hamjui anaelipia huduma hizo zote ni sisi wananchi kupitia kodi zetu? Serikali inafanya kusimamia utekelezaji tu ambao ni mbovu kwa sehemu kubwa na ndio maana huduma zinakuwa mbovu.

Tunalipa kodi chungu nzima, kila unachonunua kodi inaenda, tozo, waajiriwa 51% ya mishahara yao inaliwa na kodi, yaani kodi inachukua mgao mkubwa kuliko alichotolea jasho, bado hamjageukia kodi kutoka kwa wafanya biashara nk, lakini zote zinaenda kuishia kwenye matumbo ya watu huku kwenye huduma yanaenda makapi na hapa ndipo zinapokuja huduma mbovu.

Kungekuwa hakuna upigaji kwa viongozi kweli gharama za hospitali zisingekuwa bure? Tena sio hospitali tu huduma zote muhimu zilipaswa kuwa bure. Bilioni 1 kwa serikali ni kitu gani, kama kiongozi mmoja tu anaiba matrilioni ya pesa ndani ya muda mfupi? Ripoti za CAG kila mwaka zinaonesha upigaji wa matrilioni ya pesa halafu mnasema Tanzania haina uwezo wa kufanya huduma hizi kuwa bure, na tena sio huduma bure ni huduma bora za uhakika.

Viongozi acheni wizi, nyinyi ndio mnaotukwamisha Watanzania kupata huduma bora.
 
Back
Top Bottom