Kwamuda mrefu nilishaacha kuangalia TBC kutokana na namna ambavyo wanaendesha vipindi ikiwemo taarifa ya habari. Siku mbili zilizopita nililazimika kuangalia TBC hasa taarifa ya habari ili kuona kama kuna jipya nikilinganisha na KBC, kwakweli TBC mjitathmini, haiwezekani taarifa ya habari nzima ni kusifia na kuelezea tu mambo mazuri yanayofanya na watendaji. Huenda wanalazimika kufanya hivyo ila nashauri TBC wajitahidini sana kujiweka kitaifa, inachosha na inaudhi sana kuona taarifa zilezile zenye mwelekeo uleule, kitu ingalau cha kunifanya labda niangalie labda ni michezo ila kwa kweli TBC kwa mtindo huu bado sana mnasafariNdugu WanaJF,
Kumekuwepo na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi na hata hapa JF kuhusiana na changamoto ya vipindi vya Televisheni ya Taifa (TBC1). Malalamiko hayo yameegemea zaidi katika eneo la ubora wa vipindi na ubunifu.
Kwa bahati nzuri, Mkurugenzi pamoja na Watendaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) ni wadau wakubwa wa JamiiForums na huwa wanafuatilia taarifa na mijadala mbalimbali inayoendelea hapa. Hivyo tukiitumia vyema nafasi hii, tutawasaidia kuboresha maeneo ambayo yanatakiwa kurekebishwa kwa haraka.
Naomba tutumie uzi huu kutoa maoni, ushauri na mapendekezo kuhusu aina ya vipindi na ubunifu ambao ukitumiwa utasaidia kuifanya televisheni hii ya taifa kuvutia kutazamwa na kufurahiwa.
Tumeshalalamika sana. Sasa ni wakati wa kuchukua hatua na kutaja suluhu kwa mifano ili kuimaliza changamoto hii kabisa.
Karibuni sana.