TBC
1. Boresheni ubora wa mwonekano wa picha na sauti
2. Vipindi vingi vilenge kuinadi Tanzania na sio siasa za chama tawala (kama italazimu kunadi vyama kuwe na balance ya chama tawala na upinzani kama kipindi cha uongozi wa Tido Mhando nilijishangaa wakati wa taarifa ya habari nahama channel kwenda TBC maana habari zilikuwa na mvuto mkubwa sana...na kwa mwendo ule nilikuwa nadhani vyombo vingine vingefifia....KUSEMA UKWELI TIDO MHANDO ALIIFUFUA TBC kutoka ilivyokuwa TVT)
3. Kuwepo na subchannels za miziki ya zamani (zilipendwa) pamoja na ya kizazi kipya (NB: zichaguliwe nyimbo za kuelimisha na zenye maadili zilizopigwa kwa mtindo wa kizazi kipya badala ya kupiga nyimbo za mapenzi tu na zisizo na maadili....kama chombo cha taifa kiwe "sensitive" kulea kizazi kipya kwenda kwenye mwelekeo sahihi kimaadili).
4. TBC itumike kuitangaza Tanzania kimataifa....uongezwe ubora wa picha/video kuonesha vivutio vya utalii
5. Vipindi vya kuelimisha watoto wajue kuandika, kusoma na kuhesabu ni vizuri viendelezwe
NB
Kwa sababu taifa la Tanzania linawajumuisha wanachama wa CCM, wanachama wa upinzani na wasio na vyama mi ningeshauri TBC iache kabisa kuonesha shughuli za chama chochote bali ijikite zaidi na masuala mapana ya kitaifa yanayogusa makundi yote kwa mfano michezo, elimu, afya, kilimo, muziki, utamaduni, n.k (maendeleo ya taifa kwa ujumla wake na sio maendeleo ya chama....viongozi wa CCM wanapotumia TBC kunadi sera za chama kunasababisha makundi ambayo ni "neutral" na "non-CCM" kukereka na kuichukia TBC....I wish TBC iwe ni kioo cha taifa na sio kioo cha chama.