Tena Mbowe hao wahamiaji wakiingia CHADEMA siku hiyo hiyo wanakuwa wajumbe wa kamati kuu na machadema wote wanakaa kimya. Machadema wote waliokipigania chama wanakuwa wanyonge mbele ya Mbowe ni kusifu tu. Ukweli huu hawawezi kuukubali hata kidogo, kwa sababu ya ushabiki na ufuasi iliokubuhu.
Hii ni ujinga gani leo anajiunga na chama kwa sababu tu ya jina kubwa huko alikotoka anapewa ujumbe wa kamati kuu, kikao nyeti cha chama? Anapoondoka kurudi anasema wimbo hauimbiki ugenini! How do you feel? Shame on you! Msipende kujipa maneno ya matumaini ya uongo kumlinda Mbowe.
Hivi huyo mbowe haoni kwamba hao vijana waliokaa magerezani kwa ajili ya kuipigania CHADEMA ndo walifaa kuwa kamati kuu? Kwa nini hao wapambanaji wa kweli anawaacha?
 
Huyo Mbowe kwa nafasi yake anatakiwa aongoze mapambano dhidi ya hiyo mifumo, ambayo ndiyo chanzo cha Covid 19 badala ya kupambana na Covid 19 ambayo ni zao la huo mfumo.
Kweli Mbowe ndio amekiua Chama

Sababu Mbowe aliwapa MaDED mamlaka kusimamia chaguzi...

Mbowe ndio aliwateua MaDC...

Mbowe ndio amiri jeshi mkuu ambaye majeshi yote yanamtii...

View attachment 1769179
 
Huyu mwenyekiti wetu anagenge la watu wasiokuwa na busara. Kazi yao kubwa ni kumtetea kwa kila jambo atakalofanya hata kama halina manufaa kwa chama chetu.

Mathalani alitafuna bil 8 za michango yetu lakini watu wanamtetea.

Alijigawia gari ya chama Ford ranger lakini watu wanamtetea.

Sasa hivi chama kina hali mbaya hakuna mtu anayemhoji wanampigia makofi tu.

Sisi makamanda wenye uchungu na chama tukiongea wanatutukama mitusi hii haifai kabisa.
 
Hua nasema kila siku humu.

Mbowe, Lipumba, Zitto wanadhooficha harakati za demokrasia nchi hii.

Haiwezekani chadema wasitengeneze succession plan ya mtu mwingine mwenye uwezo kumrithi Mbowe halafu wanataka tuwakabidhi nchi yetu, hivi si watabadili katiba watawale milele?

Zitto amejipa cheo cha juu ambacho hakipigiwi kura, eti kiongozi mkuu wa chama na mshauri mkuu wa chama. Hataki uchaguzi, hapo anataka uchaguzi huru kwenye nchi huku yeye hauonyeshi huo uhuru kwenye chama chake.

Wapinzani wa nchi hii ndio wanaua demokrasia. Demokrasia wanaiongea mdomoni lakini mioyoni mwao ni madikteta wakubwa, hawataki upinzani kwenye chama, hawataki uchaguzi kwenye vyama na hata wakifanya uchaguzi ni geresha tu ila wao wako pale pale.

Hivi wao demokrasia ni uchaguzi mkuu wao washinde ila kwenye vyama hakuna demokrasia?

Vyama vya siasa Tanzania ni family party, sio political party. Vinatumika kwa maslahi ya viongozi wake. Zitto anaitumia ACT kwa maslahi yake, Chadema Mbowe anaitumia kwa maslahi yake.

Nchi hii CCM majanga, upinzani vimeo.
 
Back
Top Bottom