Naomba, msaada wa mawazo ni lipi nifanye;
Nililipia umeme new connection 2 poles, tangu tarehe 20/03/2022 hadi leo no connection.

Nikifuatilia naambiwa nisubiri, nipo jirani na office za TANESCO, (TANESCO kufika kwangu hakuna gharama za usafiri!

Niichukue hatua gani ukizingatia hii ni biashara, pesa yangu shirika linazarisha faida, mimi ninaingia gharama zingine za kununua mafuta ya taaa, kuchaji simu kwa jirani, kuangalia taarifa vyombo vya habari kwenye migahawa, inanikerela sana!
 
Eneo Igumbilo -Iringa majengo mapya bypass, Mwaka 2021 Julai nilipeleka form ya maombi ya kuunganishwa umeme ikiwa imekamilika, mpimaji akaja kupima, akasema kutoka na nguzo zipo mbali na nilipo na nyumba zote za eneo nilipo hazijapatiwa umeme hivyo tusubiri Mradi ambao wangeuleta mwezi septemba 2021, lakini mpaka sasa hii juni2022 wamekuwa kimya kila tukifuatilia majibu yao yanakuwa hayaeleweki. Cha ajabu zaidi hapa ndio tunaona TANESCO Iringa wanatuhujumu mwezi mei2022 tarehe 20 wamekuja wamewaunganishia nyumba mbili umeme SASA SIJUI HUO NDIO MRADI AMBAO WALITUAMBIA WANATUANDALIA AMA VIPI, urasimu umezidi TANESCO Iringa tunahitaji huduma kama kuna namna twambieni nasi tufanye, 0734659840 Kwa maelezo zaidi .
 
TANESCO,shughulikieni changamoto ya mita na nguzo za umeme.ili kutoa huduma kwa wateja 84,000 wanaotaka huduma kwenu.
Aidha wafanyakazi wa TANESCO wanaoidhinisha vifaa kwa ajili ya ujenzi wa service line kwa wateja wapya na Mita waache urasimu.
Kwa kuwa miundo mbinu ya umeme ni mali ya TANESCO na gharama zake ni kubwa,kwa shirika na wateja Ni busara TANESCO na Serikali kwa ujumla ikatafuta njia ya kutoa huduma kwa wateja kwa haraka na bila usumbufu.
Kwa wateja wa mijini wanaohitaji huduma ya umeme, na wanaohitaji nguzo zaidi ya moja kupata umeme (kwa gharama ya shs690,000 na zaidi). Gharama hizi ni kubwa kwa wananchi wa kawaida ambao wamevunja vikoba vyao na kujijengea vijumba vyao.

Ushauri
1). TANESCO ianishe mahitaji yote ya wateja wanaohitaji nguzo mbili na zaidi (ambazo zinaitwa Miradi (WP) au maneja wa Wilaya wawe na kitengo Cha Mipango/Miradi chenye majukumu ya kutembelea Sehemu mbalimbali za makazi mpya,ili kubainisha mahitaji ya huduma ya umeme na kuandikia mahitaji na makadiro ya vifaa na gharama zake
2. Serikali/TANESCO ikope fedha yenye riba nafuu kwa ajili ya kupeleka miundo mbinu ya umeme Karibu na Wananchi,
3). Wateja wawe wanalipia Shs320,960 za service line.
4). wateja wanaohitaji nguzo mbili wapatiwe huduma na watakiwe kulipa kwa instalment nne au sita.na wanaweza kulipa instalment moja au mbili kama commitment kwa wanaotaka huduma kwa mkopo.
5). Serikali ya mtaa inaweza, kuwadhamini wakazi wa mtaani kwao watakao hitaji kulipia huduma ya umeme kwa instalment
 
Hivi nyie watu wa TANESCO, kwa nini suala la mita za umeme kwa wateja wenu linawatesa sana ??! Ni mtaji mdogo wa kununua mita, au ni mradi wa wakubwa fulani?!

Ushauri wa bure; Ruhusuni watu wenye mtaji mkubwa waingize hizo mita nchini na ziuzwe madukani kama bidhaa nyingine ili mtu anayehitaji umeme ajinunulie mita yake na nyie TANESCO, kazi yenu iwe ni kuzithibitisha na kuwafungia wateja.

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
 
NIKONEKT kwanini msitoe matangazo ya kutosha kwa sasa? Pia kwa sasa bado changamoto ni kubwa kwa Wakandarasi na Mafundi walio sajiliwa na EWURA hapa mkoa wa Kagera ni wachache sana wamefanikiwa kujiunga na mfumo mpya na kesho ndiyo tunaanza kuutumia.
 

Hatua za kufuata Ili kuomba umeme​

    • 1

      Chagua huduma ya kuomba umeme​

    • 2

      Chagua Dhumuni, Aina ya ombi, Aina ya muombaji, Aina ya kitambulisho/utambulisho wa mlipa kodi na Namba ya kitambulisho/utambulisho​

    • 3

      Tumia namba ya kitambulisho cha Taifa kwa ombi lililokusudiwa kwa madhumuni ya makazi na fuata muundo huu: 1984081911660000xxx​

    • 4

      Tumia namba ya usajili wa kampuni/TIN kwa Kampuni au Taasisi​

    • 5

      Bonyeza/bofya Anzisha ombi jipya​

    • 6

      Jaza wasifu, mawasiliano mbadala na maelezo ya makazi​

    • 7

      Bonyeza/bofya tuma ombi​

    • 8

      Utapokea ujumbe baada ya kujaza maelezo kwa ukamilifu na kufanikiwa kutuma​

    • 9

      Tafadhali bonyeza/bofya hapa kuona orodha ya wakandarasi wa umeme wanaostahili au tembelea ofisi zao​

    • 10

      Mpatie mkandarasi uliyemchagua namba ya ombi uliyopatiwa kutoka kwenye mfumo na namba ya simu uliyotumia kuombea umeme ili kumuwezesha kujaza maelezo ya mfumo wa mtandao wa nyaya katika jengo/eneo lako kwenye mfumo wa maombi mtandaoni​

    • 11

      Mkandarasi wa umeme atajaza maelezo ya mtandao wa nyaya na tamko lake na kutuma maelezo ya muombaji TANESCO kupitia mfumo wa maombi mtandaoni​

    • 12

      Muombaji utajulishwa kupitia ujumbe mfupi wa maandishi (SMS) moja kwa moja baada ya mkandarasi wa umeme kutuma maelezo yake ya mfumo wa mtandao wa nyaya kwenye jengo/eneo lako TANESCO​

    • 13

      TANESCO itafanya upimaji katika eneo la mteja ili kubaini gharama na mahitaji ya kuunganishiwa umeme baada ya hapo mteja atapatiwa makadirio ya bei na namba ya kulipia ili afanye malipo kupitia ujumbe mfupi wa maandishi(SMS) moja kwa moja au kupitia kupakua kutoka kwenye tovuti ya maombi ya umeme TANESCO​

    • 14

      Mteja atalipia kupitia njia mbalimbali za malipo​

    • 15

      Mteja atajulishwa moja kwa moja kupitia mfumo wa ujumbe mfupi wa maandishi (SMS) baada ya kufanikiwa malipo yake​

    • 16

      TANESCO itaunganisha umeme kuangaza maisha ya mteja​

    • BOFYA LINK HII KUOMBA UMEME

 
Hello Tanesco, nilajaza fomu ili niondolewe kwenye matumizi makubwa taakribani mwaka mmoja ulopita lakini hadi leo ni komya. Naomba majibu tafadhali.
Nakushauri kama ni kubadilishiwa tarriff uende kwenye tawi lao la wilaya mahali ulipo,mie nilifanya ivyo unaandika barua kwa meneja wa wilaya mahali ulipo kisha ukifuatilia unabadilishiwa
 
Acheni siasa fisi maji nyie TANESCO kuna nyumba huku mtaani nimezishuhudia kuanzia msingi hadi inaisha na wamefungiwa umeme sie wengine huu unaenda mwezi wa 7 hatujapata huduma ya kufungiwa na tumeshalipia muda mrefu sana ,na ukiwauliza wa TANESCO ofisi ya Nyakato wanatoa sound za uongo uongo na kuomba rushwa
Hiyo ni kweli kabisa kuna urasimu mkubwa sana kwenye kuunganishiwa umeme ukienda kwa halali kabisa utakaa miezi 10 ila ukitoa rushwa hata siku 7 haziishe
 
Kwa hiyo wale Tuliolipa 27000/- Ndio basi tena!!! Au Rushwa kwanza. Ndio Tulipofikia hapa.Nimelipa umeme Nyumba 2 Tangu mwezi wa 9 mpaka leo kimya mnataka nije kuwasujudia, Wakati majirani mnakuja kuwaunganishia kila siku.

Nawaahidi One Day Yes!!!!
 
Zamani Tshs 10,000 unapata unit 28.1 lakini sasa hiyo point haipo au ukinunua umeme wa 1000 ulikuwa ukipata unit 2.7 lakini sasa hivi unapata chini ya hapo yaani hizo points zimepungua,je tatizo nini na mnadai umeme haujapanda?
 
Zamani Tshs 10,000 unapata unit 28.1 lakini sasa hiyo point haipo au ukinunua umeme wa 1000 ulikuwa ukipata unit 2.7 lakini sasa hivi unapata chini ya hapo yaani hizo points zimepungua,je tatizo nini na mnadai umeme haujapanda?
Msemaji alisema bei ya umeme itakuwa vilevile haito panda
 
Back
Top Bottom