TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

Acheni siasa fisi maji nyie TANESCO kuna nyumba huku mtaani nimezishuhudia kuanzia msingi hadi inaisha na wamefungiwa umeme sie wengine huu unaenda mwezi wa 7 hatujapata huduma ya kufungiwa na tumeshalipia muda mrefu sana ,na ukiwauliza wa TANESCO ofisi ya Nyakato wanatoa sound za uongo uongo na kuomba rushwa
Ndugu mpendwa Mteja wetu

Tunafurahia kukuhudumia, tafadhali onesha taarifa kamili kwa huduma bora.

Jina

Eneo

Wilaya

Namba ya simu

Tatizo

Toka lini

Namba ya taarifa

Ahsante sana

TANESCO Huduma kwa Wateja

SIMU : 0748550000
 
Jina: Mwananchi Mpita Njia.
Eneo: Mbugani Jirani na Berlin Hotel
Mkoa: Geita
Wilaya: Geita Mjini.
Tatizo: Miti Katika njia ya Umeme mkubwa HT.
Matawi ya Miti yamezidi Katika njia za Umeme , hivyo tunaomba msaada wenu kuyapunguza.

Tokea lini: Endelevu
 
Nimekamilisha taratbu zote za kuletewa umeme toka tarehe 03/11/2021 na nimekuisha lipia lakin mpaka leo hii hakuna dalili za kupata huo umeme shida ni nin Tanesco?maeneo ni busweru jirani na soko la kabwalo
 
Nimekamilisha taratbu zote za kuletewa umeme toka tarehe 03/11/2021 na nimekuisha lipia lakin mpaka leo hii hakuna dalili za kupata huo umeme shida ni nin Tanesco?maeneo ni busweru jirani na soko la kabwalo
Mkuu tupo wengi huku Buswelu tunaosubiri kuunganishiwa ,yani kila siku wanapiga sound tu vifaa vifaaa
 
Kwani shida nini mbona tangu jana tunakatiwa umeme mabibo external kwenye laini hii ya Usangu Treads?? Tumelala giza, saa hiv umerud hata pasi haijapata moto umekatwa tena.
 
Nyie jamaa naona wateja kwenu sio wafalme tena , inawezekanaje mtu analipia umeme tena kwa bei zenu hizi mpya then anakaa miezi miwili hamjamfungia umeme, tena hahitaji nguzo wala nini ni kiwaya tu hata mita kumi hakifiki?

mmechoka kwa kweli na vishoka wanapigia watu simu kuwa maombi yako tayari sijui wapewe hela ya bolt sijui nati nk. Shirika limechoka sana , imagine hapo ni DSM je ingekua huko mikoani
 
TANESCO Nyakato, Ilemela Mwanza naona mnawafungia umeme na kuwapa kipaumbele wale wanaotoa rushwa, mtu kalipa baada yangu lakini Jana kafungiwa umeme na nguzo kaletewa hii ni baada ya kutoa rushwa ,hivi ni haki kweli?? 27000/- tulizolipa hazithaminiki kabisa, mwenye kitita ndio anafungiwa umeme, huu ni mwezi wa 7 unaisha tangu tulipie umeme hakuna huduma ya kufungiwa.

Daah Ili shirika takataka kabisa
 
tuseme inatosha sasa NCHI hii kuchezewa hivi shirika la umma TANESCO KUKAA KIMYA BILA KUTOA taarifa kwa wateja wake ambao ni wananchi hii so sawa
 
86 Reactions
Reply
Back
Top Bottom