Jamani hii ni laana ya singa singa senge sechi, kuzima mitamvo ya IPTL yenye MW 200 ni kusababisha mgao mkubwa sana. Sasa ili mgao uishe wawashe iptl au msubiri mpaka mvua zianze mwezi wa tatu
 
Jana umeme umekatika asubuh saa mbili umerudi saa nne usiku. Leo tena saa tatu tu umekatika.
Dar Ubungo
Kama ni mgao si mseme tujipange
 
mgao umeanza hata kabla ya amri ya kubomolewa hilo jengo kutokea
Jamaa wameamua kumjibu!!! Unaboa ofisi wanayopatia Ridhiki !!!! Hawawezi kukuacha hivihivi!!!! Ila tunaoumia ni sisi wananchi!!! Magu hawezi kuwaomba msamaha Kwa kubomoa ofisi yao.
Wito: Magu waombe msamahama tanesco ili wapunguze makali ya mgao!!!
 
Keki zilikuwa kwenye oven ndo hasara tayari hiyo.sasa najiuliza ni Tanzania gani ya viwanda tunayo ihubiri?toka juzi wanakata umeme tena masaa mengi....mhhh mm naona kama mambo sio mazuri huko.na hatujasikia taarifa yoyote toka Tanesco.yaan ndo tumejiajiri kwa hivi vitu vidogo vidogo but umeme sasa imekua issue

acheni kelele chama kimepata ushindi was kishindo kata 42,

pia chama kimeweza kuwapokea wapinzani na bado Wapinzani 200 wanataka kujiunga nasi kwenye mkutano mkuu.

chama chetu kinapendwa sana na wananchi, hata wema na mamayake wako mbioni kurudi chamani.

na bado tuna mkakati was kusaka wanachama mitaani kwa kugawa fedha, vitisho, hata kwamtutu wa bunduki ili tuwe wengi zaidi ya Chadema.

hayo mnayosema sijui uchumi umesinya, sijui umeme hakuna shauri yenu.
 
Tangu jamaa amepewa U waziri kamili ameleta mgao, .. Bado wanavunja jengo pale ubungo?
 
Na anayejua sababu ya umeme kukatika na huu mgao wa kutisha ni ipi?
Huu si mgao bali kuna shida kwenye grid ya taifa,
ambayo kwa leo imezima kama ilivyotokea jana
watu wapo kazini wanaendelea kurekebisha.
Ikumbukwe kuwa grid ikitoka umeme unakatika
karibia nchi nzima namaanisha mikoa yote
iliyounganishwa kwenye gri ya taifa.
 
Pesa zote kachukua bashite ili afanye fiesta yake ya kukaribisha wadogo zetu vyuoni.
 
sikonge tabora umeme ulikatika juz asubuh ulirejea jana saa kumi na mbili jion. Leo saa moja asubuhi tanesco wamechukua umeme wao.

Nakumbuka walisema gesi ikianza kuzalisha umeme uhaba wa umeme utakuwa historia. Lakin mmmmh naona vyuma vimekaza hadi kwenye umeme.
 
Back
Top Bottom