TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

Fyafyafya

Member
Nov 30, 2017
53
150
Hii ni wiki ya pili hapa nchini umeme ukisua sua. Maeneo mengi nchini umeme unakatika hasubuhi saa 2 na kurudi jioni saa kumi na mbili. Hali kadharika maeneo mengine hushinda kutwa nzima ukiwepo na jioni saa kimi na mbili au saa moja hukatika. Hii ikimaanisha kuwa inakuwa zamu ya wale waloshinda bila umeme.

Hapa mjini Moshi Jana tulishinda nao na jioni saa moja ukakatika. Ulirudi usiku na saa mbili hasubuhi ya leo wameukata. mpaka sasa hatuna umeme.

Pengine na wewe msomaji unaweza luwa shahidi kwa ninayo yasema. Je kwenu mgao upo?

Huu unaweza kuwa mgao wa kimya kimya!!!

Watanzania bado hatujawa huru kiivo. Ado hatujajua kutafuta haki zetu. Maana mambo mengi tunaibiwa na kunyanyaswa. Kwa nini nasema haya?

Hembu fikiria watanzania wengi tunatumia ving'amuzi vya Television; na tunalipia gharama za kuangalia. Kuna wanaolipia kwa siku moja hadi siku saba yaani wiki; wengine hulipia kwa wili 2 ama tatu na wwngine hulipia kwa mwezi. Swali linakuja hivi; kama umeme unakuwa wa mgao kwa namna hii na watu wanaukosa kutwa nzima ama usiku mzima hata hawaanalii tarifa ya habari Je Kampuni za ving'amuzi huwaongezea muda au siku kwa maana kuna kutwa umeme haukuwepo na wateja wao hawajatumia?

Je sisi wateja tukatoe malalamiko kwenye hizo kampuni za ving'amuzi ili watufidie siku ambazo umeme haukuwepo?

Je tukaishitaki TANESCO kwa makampuni hayo ya Ving'amuzi?

My Take:

Kwa style hii ya ukisefu wa uwazi wa matumizi ya nishati ya umeme utaadhiri dhamira ya Mh. Rais ya kuwa na nchi ya Viwanda!
 

Black jew

Member
Sep 4, 2017
50
125
Wanasingizia vifaa vimealibika ila mvua Ilikuwa chache mwaka jana ikasababisha akiba ya maji katka mabwawa ikawa chache ndo mana wazir kasema kuwa marekebisho ya vifaa yatakamilika mwez december tareh 20 ukweli ni kuwa ,kwana wanategemea muda huo nyanda za juu kusin mvua huwa inakuwa imechangNya na maji kina kitakuwa kimeongezeka ,
Stand to be corrected.
 

Mbao za Mawe

JF-Expert Member
May 11, 2015
22,968
2,000
Sasa hivi wapole hata hawaongei sasa itokee kuna watu wamelimbikiza madeni ya umeme weee wanaongea kama askari wa gwaride.
 

mitale na midimu

JF-Expert Member
Aug 26, 2015
10,209
2,000
ni kweli tanesco haina magari ya kupeleka wakaguzi wenu kwenye site za wateja wa line mpya au ni mbinu za rushwa za wafanyakazi wenu?
 

Zee la kitaa

JF-Expert Member
Oct 25, 2017
403
250
Khabarini wadau muda huu naandika uzi huu kama nusu iliyopita mpaka sasa umeme umekatika.Nachojiuliza ni kuwa mgao wa umeme umerudi nchini ama nini ? na kama umerudi si wautangazie umma wa watanzania waelewe kinachoendelea.
Hii wanafanya kama siri kwa manufaa ya nani kwa sababu sisi wananchi ndio tumewaweka madarakani ila kwa nyendo za hapa karibuni hili suala la umeme imekuwa kero kwa wananchi mbalimbali. Hivi hivyo viwanda mnavyohimiza vijengwe vitaendeshwa kwa kutumia nini kama hali ya umeme ndio hii . Wanasiasa kuweni wa kweli kwenye mambo ya maana mnakaa kimya ila kwenye upuuzi ndo mnatoaga matamko yenu ya kipuuzi puuzi.
Kama kazi imewashinda mrudisheni Prof. Muhongo maana kwa kipindi chake tatizo la kukatika ovyo kwa umeme halikuwepo na tulianza kusahau suala la kukatika ovyo kwa umeme.
Nawasilisha
Kwa hiyo Muhongo ndio anakata umeme. Tanesco walitoa taarifa kunahitilafu wanafanyia kazi. Hitalfu ni jambo la kawaida; tunakaa na kulaumu as if sisi ni technicians. Waacheni wenye proffession zao watatue tatizo.
 

kivyako

JF-Expert Member
Feb 2, 2012
14,282
2,000
Old forest mbona umeme bwerere tu
Utakuwa ni waziri mwenye dhamana, ndo majibu yenu kuficha tumbo la kuhara, mwisho kijiharishia, hapa dar mitaa kibao haina umeme kwa kila siku, sasa hivi hapa nilipo haupo na jana na juzi mida hii haukuwepo! Kwa nini mnaleta siasa katika mambo ya msingi?
 

kizeze

JF-Expert Member
Sep 25, 2012
288
500
Dah...huku Kigogo Luhanga wamekata tena yaani hawa TANESCO wanaboa ni heri kungekuwa na kampuni mbadala ya umeme kwani wanaringa sana na wanazingua sana
 

Arien

JF-Expert Member
Aug 29, 2017
11,027
2,000
Mshatugeuza vikaragosi!


Mmekata saa 3 asubuhi mkaurudisha saa 5 hii...mkaona mmekosea mkakata tena! Au kisa nyinyi mmebomolewa jengo lenu ndo mnataka kutuunguzia nyumba zetu?!
 

Camp 05

JF-Expert Member
Apr 27, 2013
1,151
1,500
asante tumelipokea na tutalifanyia kazi
Hii taasisi inayumba siku zote,washaurini wanasiasa waache unafiki muingie kwenye other sources of electric generetion,Solar power could be a vital soution at a moment otherwise mrudiaeni Lugemalila na Singasinga.
 

bhachu

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
6,703
2,000
Utakuwa ni waziri mwenye dhamana, ndo majibu yenu kuficha tumbo la kuhara, mwisho kijiharishia, hapa dar mitaa kibao haina umeme kwa kila siku, sasa hivi hapa nilipo haupo na jana na juzi mida hii haukuwepo! Kwa nini mnaleta siasa katika mambo ya msingi?
Tuliza munkari mkuu, Old forest haipo gridi ya taifA.
 

SWEET GIRL

JF-Expert Member
Dec 29, 2011
499
500
Ni vigumu sana kufuta LEGACY ya Prof. Muhongo kwenye utendaji wa Wizara iliyoitwa ya NISHATI NA MADINI. Katika uongozi wake figisu za mgao wa umeme ziliisha na kasi ya kusambaza huo umeme vijijini ilikuwa SUPER.
Kabisa aisee prof muhongo alikua mtu sahihi kwenye hii wizara.umeme ulifika mpaka vijijini.ni kweli alikua na mapungufu yake but maadamu tulipata umeme haina shida.wamrudishe tu hamna namna
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom