Naomba kujua kijiji ninachoishi kama kipo kwenye mpango wa leya awamu yatatu kijiji kinaitwa londoni wiliyani manyoni mkoan singida kwasasa kuna umeme wabei yajuu sana tena unalipia umeme kwa whats ambapo whats 1unainunua shilingi 1.5 pia hauna uwezo wakuendesha vitu vingine kama mashine za kuchoma na vitu vingine kama hivyo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Swali hili mmeshindwa kulijibu? Au mnachagua maswali ya kujibu
Tunahitaji kujua kiasi alicholipia pamoja na kujua kama kuna nguzo inahitajika au laaa ili kutoa majibu stahiki

TANESCO "Tunayaangaza maisha"
 
Tunahitaji kujua kiasi alicholipia pamoja na kujua kama kuna nguzo inahitajika au laaa ili kutoa majibu stahiki

TANESCO "Tunayaangaza maisha"

Nimelipia 1,284000/= ambazo Ni Mita 4,sihitaji nguzo maana nguzo zipo tiari
 
Nimelipia 1,284000/= ambazo Ni Mita 4,sihitaji nguzo maana nguzo zipo tiari
Asante, kama kazibyako haina nguzo TANESCO tutakujengea umeme ndani ya siku 30 za kazi.


Ndugu mteja kama umelipia mwezi wa saba bado siku 30 za kazi hazijaisha, tutaifuatilia kazi yako

Asante

TANESCO "Tunayaangaza maisha"
 
Tumewapigia simu mnasema mnakuja ila Hadi sasa hamjatokea tunaomba muje muirekrbishe maana mvua ikinyesha madhara yanaweza kutokea
IMG_20170818_125840.jpg
 
Nyumba ninayoishi tuna kawaida ya kununua umeme wa elfu kumi tunapata 26 ambazo ndani ya wiki nne au chini ya hapo zinaisha na matumizi yetu ni tv pamoja na kuwasha na kuzima (taa) usiku lakini kuna wengine ambao wao hununua umeme wa bei hiyo hiyo (elfu kumi) na wanapata units nyingi zaidi

Naomba ufafanuzi juu ya tofauti hizo
 
Nyumba ninayoishi tuna kawaida ya kununua umeme wa elfu kumi tunapata 26 ambazo ndani ya wiki nne au chini ya hapo zinaisha na matumizi yetu ni tv pamoja na kuwasha na kuzima (taa) usiku lakini kuna wengine ambao wao hununua umeme wa bei hiyo hiyo (elfu kumi) na wanapata units nyingi zaidi
Naomba ufafanuzi juu ya tofauti hizo
Tunaomba namba yako ya mita mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uhamasishaji wa mradi wa Umeme REA 3 ukiendelea ktk mkoa wa pwani , vijiji vya disunyara na kilangalanga Kwa kushirikiana na mbunge wa Kibaha vijijini mh Abuu Jumaa . Wananchi wameshaanza kutapeliwa .



TANESCO "Tunayaangaza maisha"
 
Kwanza niwashukuru kwa kujizatiti na kuamua kufungua akaunti ili kurahisisha zaidi huduma na kuwafikia watumiaji.

Mimi ni mkazi wa Temeke kata ya Buza mtaa wa kwa lulenge lakini hapa mtaani kwetu kuna shida kubwa sana ya kukatika umeme pasipo kua na sababu za msingi. Weekend tunakosa umeme siku nzima jumamosi na jumapili ukiuliza vipi kuna mgao?

Majibu ni hakuna. Mpaka hivi sasa tupo njia panda. Kila siku ni lazima umeme ukatike lakini mbaya zaidi ni eneo la mitaa ya kwa lulenge tu lakini maeneo ya jirani huduma wanaendelea kupata kama kawaida. Hili tatizo ni la muda mrefu takribani miezi 4 sasa.

Tunaomba ufafanuzi chanzo cha tatizo ni nn? Alafu pili marekebisho ya kulitatua hili tatizo yatafanyika lini? Na tutegemee yatachukua muda gani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama kweli tanesco wamedhamiria kuondoa kero kwa wateja wao basi kero kubwa inayo sumbua kila kona ya taifa hili ni:

1.KUKATIA UMEME MARA KWA MARA BILA TAARIFA.
hii ni kero inayo ongoza kila eneo, na wala haiitajii kulalamikiwa kwani mnaijua vizuri sana. mkitaka fanyeni utafiti kidogo tu.

kero hii ni sugu!! haiwezi kuondoka na wateja wake kamwe hawawezi kuisahau labda shirika hili libinafsishwe!!?
 
Back
Top Bottom