Uchaguzi 2020 Sokoine, Mbeya: Magufuli asema Tulia amemsumbua sana kwa ajili ya maendeleo ya Mbeya, amuomba Joseph "Sugu" Mbilinyi kura

Anza wewe kufanya debate humu na siyo kejeli
Mimi sigombei Urais! Leo USA wamefanya the first debate.... incumbent Trump amepata 28% support... Biden 60%.... Hapa itakuwa 1% or less kwa incumbent.
 
Leo Dkt. Magufuli anaendelea na kampeni katika mkoa wa Mbeya na mkutano huu utarushwa mubashara kupitia TBC, Channel ten, Star tv, ITV na mitandao mbalimbali.
Karibu.

Updates;
Uwanja umefurika wananchi wa itikadi mbalimbali na bendera zao hakika siasa siyo Uadui.

Viongozi mbalimbali wanaendelea kuwasili hapa uwanjani.

=========

MAGUFULI: Mwaka 2015 tulipita hapa kuwaomba kura wana-Mbeya, mlitusikiliza na natambua nilipata kura nyingi sana Mbeya lakini kwa mbunge aliyekuwa wa CCM mkasema hapana, mkanichagulia pia baadhi ya madiwani lakini mkanichagulia wabunge katika maeneo ya Mbeya, Mkanichagulia Kyela, Chunya na maeneo mengine.

Hapa mjini mkasema hapana, niseme kwa dhati, nilisikitika lakini sikiuwachukia na nikaja nikaambiwa kwamba, kushindwa kwa CCM katika jiji hili la Mbeya ilitokana na ugomvi wa wana-CCM wenyewe.

Nilichofanya ndugu zangu na nataka niwaeleze hapa leo, kutaka kuhakikisha kwamba Mbeya haipotei kwenye ramani, nilimtafuta mwanamama mmoja msomi aliyekuwa akiitwa Dr. Tulia nikamteua kuwa mbunge kwamba yale yatakayokuwa kuwa yanajitokeza kwa ajili ya Mbeya angalau yawe na msemaji.

Nilipomteua Dr. Tulia kuwa mbunge na ndiye mbunge mmoja wa kwanza niliyemteua, alipoingia bungeni akateuliwa pia kwa nyota aliyokuwa nayo, akateuliwa kuwa naibu spika wa bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Amefanya kazi zote zilizotakiwa kufanywa na mbunge wa Mbeya, napenda leo kwa hadhara hii Tulia nikushukuru sana kwa sababu ulinisumbua sana kwa ajili ya maendeleo ya Mbeya na kwa sababu leo umekuja mwenyewe na kwa vile sitakuteua tena kwa viti maalum, nimekuleta kwa wazazi wako, dada zako, kaka zako, wazee wako wakusulubu wewe kwa ajili ya kazi zako nzuri.

Nina matumaini makubwa kwa hadhara hii, tofauti zilizopo miongoni mwa wana-Mbeya mtaniletea Dr. Tulia Ackson awe mbunge wa hapa.

Ninayasema haya kwa sababu pamonja na kwamba hakutuchagua hapa Mbeya mjini tuliendelea kufanya kazi kwa manufaa ya wana-Mbeya wote kwa sababu ninafahamu maendeleo hayana chama.

===
MBEYA: MAGUFULI AMUOMBA KURA SUGU

Mgombea Urais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM amewaomba kura watu wote, akiwemo Joseph Mbilinyi, mbunge wa Mbeya mjini aliyemaliza muda wake maarufu kama Sugu

Ameyasema hayo alipokuwa Mbeya kwenye mkutano wa kampeni anazoziendeleza kuelekea uchhaguzi mkuu Oktoba 2020

Amesema maendeleo hakuna vyama, dhamira yake ni kuibadilisha Mbeya kabla muda wake haujaisha, ili liwe jiji la mfano kitaifa na kimataifa
Umejenga bwawa la umeme,SGR, mbona inapiga magoti tena babu?
 
Attachments

  • VID-20200929-WA0015.mp4
    901.4 KB
Mimi sigombei Urais! Leo USA wamefanya the first debate.... incumbent Trump amepata 28% support... Biden 60%.... Hapa itakuwa 1% or less kwa incumbent.
Sawa endelea kujilinganisha na USA...
 
Sawa endelea kujilinganisha na USA...
Tuliaminishwa mtu huyu mwaka huu haitaji hata kufanya kampeni, sasa imekuwaje tena?

FB_IMG_1601425432271.jpg
 
Watu wamekuwa wanasombwa kwa mabasi na malori kutoka wilaya xote za mkoa wa Mbeya tangu jana.

Sent using Jamii Forums mobile app
Point yako kuu hapa ni nini? Unataka watu wasiletwe kwenye mikutano kusikiliza sera au tatizo ni nini? Kama chadema hawana uwezo wa kufanya hayo basi wasione kuwa wengine kufanya hivyo ni kosa bali na wao wabuni mbinu nyingine za kuongeza watu kwenye mikutano yao ya kampeni.
 
Magufuli hafanyii mkutano kwenye uwanja wa Sokoine mbona? Anafanyia kwenye Airport ya zamani.
Ethiopia Nchi yenye Ndege zaidi ya 120 kuliko Tanzania, Ethiopia ina Flyovers kuliko Tanzania, Ethiopia ina Tren ya Mwendo kasi kuliko Tanzania, Lakini Leo hii Waethiopia 28 na Wasomali 4, Wamekamatwa Wilayani Pangani, Wakijaribu kutoroka kwenda Kujitafutia Maisha Nchi za Kusin

Halafu maccm yanajisifu bila aibu, fyoko fyoko fyoko ndegeeeeee
 
Hata sugu asiposhinda nna uhakika Magufuli atampa kazi nzuri sana maana huyu baba wa watu anateuaga yoyote

Maendeleo hayana vyama johnthebaptist 😁😁😁😁
 
Leo Dkt. Magufuli anaendelea na kampeni katika mkoa wa Mbeya

Uwanja umefurika wananchi wa itikadi mbalimbali na bendera zao hakika siasa siyo Uadui.

Viongozi mbalimbali wanaendelea kuwasili hapa uwanjani.

=========

View attachment 1585551
MAGUFULI: Mwaka 2015 tulipita hapa kuwaomba kura wana-Mbeya, mlitusikiliza na natambua nilipata kura nyingi sana Mbeya lakini kwa mbunge aliyekuwa wa CCM mkasema hapana, mkanichagulia pia baadhi ya madiwani lakini mkanichagulia wabunge katika maeneo ya Mbeya, Mkanichagulia Kyela, Chunya na maeneo mengine.

Hapa mjini mkasema hapana, niseme kwa dhati, nilisikitika lakini sikuwachukia na nikaja nikaambiwa kwamba, kushindwa kwa CCM katika jiji hili la Mbeya ilitokana na ugomvi wa wana-CCM wenyewe.

Nilichofanya ndugu zangu na nataka niwaeleze hapa leo, kutaka kuhakikisha kwamba Mbeya haipotei kwenye ramani, nilimtafuta mwanamama mmoja msomi aliyekuwa akiitwa Dr. Tulia nikamteua kuwa mbunge kwamba yale yatakayokuwa kuwa yanajitokeza kwa ajili ya Mbeya angalau yawe na msemaji.

Nilipomteua Dr. Tulia kuwa mbunge na ndiye mbunge mmoja wa kwanza niliyemteua, alipoingia bungeni akateuliwa pia kwa nyota aliyokuwa nayo, akateuliwa kuwa naibu spika wa bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Amefanya kazi zote zilizotakiwa kufanywa na mbunge wa Mbeya, napenda leo kusema kwa hadhara hii Tulia nikushukuru sana kwa sababu ulinisumbua sana kwa ajili ya maendeleo ya Mbeya na kwa sababu leo umekuja mwenyewe na kwa vile sitakuteua tena kwa viti maalum, nimekuleta kwa wazazi wako, dada zako, kaka zako, wazee wako wakusulubu wewe kwa ajili ya kazi zako nzuri.

Back
Top Bottom