Uchaguzi 2020 Sokoine, Mbeya: Magufuli asema Tulia amemsumbua sana kwa ajili ya maendeleo ya Mbeya, amuomba Joseph "Sugu" Mbilinyi kura

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
35,073
2,000
Leo Dkt. Magufuli anaendelea na kampeni katika mkoa wa Mbeya

Uwanja umefurika wananchi wa itikadi mbalimbali na bendera zao hakika siasa siyo Uadui.

Viongozi mbalimbali wanaendelea kuwasili hapa uwanjani.

=========

C4E731B4-5B63-49E2-8941-BA2DA835D110.jpeg

MAGUFULI: Mwaka 2015 tulipita hapa kuwaomba kura wana-Mbeya, mlitusikiliza na natambua nilipata kura nyingi sana Mbeya lakini kwa mbunge aliyekuwa wa CCM mkasema hapana, mkanichagulia pia baadhi ya madiwani lakini mkanichagulia wabunge katika maeneo ya Mbeya, Mkanichagulia Kyela, Chunya na maeneo mengine.

Hapa mjini mkasema hapana, niseme kwa dhati, nilisikitika lakini sikuwachukia na nikaja nikaambiwa kwamba, kushindwa kwa CCM katika jiji hili la Mbeya ilitokana na ugomvi wa wana-CCM wenyewe.

Nilichofanya ndugu zangu na nataka niwaeleze hapa leo, kutaka kuhakikisha kwamba Mbeya haipotei kwenye ramani, nilimtafuta mwanamama mmoja msomi aliyekuwa akiitwa Dr. Tulia nikamteua kuwa mbunge kwamba yale yatakayokuwa kuwa yanajitokeza kwa ajili ya Mbeya angalau yawe na msemaji.

Nilipomteua Dr. Tulia kuwa mbunge na ndiye mbunge mmoja wa kwanza niliyemteua, alipoingia bungeni akateuliwa pia kwa nyota aliyokuwa nayo, akateuliwa kuwa naibu spika wa bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Amefanya kazi zote zilizotakiwa kufanywa na mbunge wa Mbeya, napenda leo kusema kwa hadhara hii Tulia nikushukuru sana kwa sababu ulinisumbua sana kwa ajili ya maendeleo ya Mbeya na kwa sababu leo umekuja mwenyewe na kwa vile sitakuteua tena kwa viti maalum, nimekuleta kwa wazazi wako, dada zako, kaka zako, wazee wako wakusulubu wewe kwa ajili ya kazi zako nzuri.

Nina matumaini makubwa kwa hadhara hii, tofauti zilizopo miongoni mwa wana-Mbeya mtaniletea Dr. Tulia Ackson awe mbunge wa hapa.

Ninayasema haya kwa sababu pamonja na kwamba hakutuchagua hapa Mbeya mjini tuliendelea kufanya kazi kwa manufaa ya wana-Mbeya wote kwa sababu ninafahamu maendeleo hayana chama.

===
MBEYA: MAGUFULI AMUOMBA KURA SUGU

Mgombea Urais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM amewaomba kura watu wote, akiwemo Joseph Mbilinyi, mbunge wa Mbeya mjini aliyemaliza muda wake maarufu kama Sugu

Ameyasema hayo alipokuwa Mbeya kwenye mkutano wa kampeni anazoziendeleza kuelekea uchhaguzi mkuu Oktoba 2020

Amesema maendeleo hakuna vyama, dhamira yake ni kuibadilisha Mbeya kabla muda wake haujaisha, ili liwe jiji la mfano kitaifa na kimataifa
 

Sizinga

JF-Expert Member
Oct 30, 2007
8,468
2,000
Debate fanyeni na akina Shibuda.

Dr Magufuli kazi zake zinaonekana bwashee!
Hii inanikumbusha enzi za shule, kipanga namba 1 class hashiriki debate zozote kwani matokeo ya darasani yanajulikana.... Ingawa kwenye zile detabe za shule wakishiriki walikuwa wanapigwa na average students
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom