Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 15,301
- 9,727
Ndugu zangu Watanzania,
Huo ni ukweli mchungu ambao napenda umfikie Joseph mbilinyi au Sugu, kuwa nafasi aliyoipata siku za nyuma ya kuongoza jimbo la Mbeya mjini kwa miaka kumi haipo tena.
Haiwezi kurudi tena, hawezi kuipata tena na hakuna mwenye hamu wala wazo la kumpigia na kupoteza kura yake kumpa kura ya ndio Sugu.
Kwa kuwa katika miaka kumi jimbo la Mbeya mjini lilikuwa na Mbunge hewa, lilikuwa wazi,lilikosa wa kulisemea na kulipigania Bungeni, lilikosa mtetezi, lilikosa sauti yenye ushawishi, nguvu na kusikika masikioni mwa serikali.
Miaka yote ya Ubunge wake Sugu alifanya kazi ya kuzurula tu, kupigania maslahi yake binafsi na tumbo lake, alifanya kazi ya kutafuna posho na mshahara wa ubunge pasipo kuufanyia kazi.
Wananchi katika miaka yote ya Sugu walikosa mahali pa kukimbilia kupeleka shida, kero na changamoto zao kwa kuwa muda wote Sugu alikuwa bize na biashara zake, mambo yake, bize na Dar tu huku Mbeya akifanya kama kituo cha kugongea muhuri wa kwenda Bungeni kama mbunge.
Aliwafanya wana Mbeya kama wajinga, akajiona yeye ni mtoto pendwa na kwamba yeye ni yeye mwenye hati miliki na jimbo la Mbeya mjini na kwamba hayupo wa kuchukua nafasi hiyo isipokuwa yeye tu aliyemteule wa Mbeya mjini.
Wanambeya walipochoka na dharau zake na ubabaishaji wake pamoja na kushindwa kwake kutimiza majukumu yake ya kibunge, wakaamua kugeukia upande wa pili kulikokuwa na CCM ikiwakilishwa na wakili Nguli na msomi, walimu wa walimu wa sheria, Naibu Mwanasheria Mkuu Mstaafu na Naibu Speaker wa Bunge Dr. Tulia Acksoni Mwansasu kwa kumpa ushindi wa kishindo ulioitetemesha Mbeya nzima.
Dada msomi, msikivu wa hali ya juu, mkalimu, mcheshi, mchapakazi, mnyenyekevu, mpole, mwenye moyo wa huruma na upendo, mzalendo wa kweli na aliyebarikiwa na Mungu kipawa na Karama ya uongozi.
Mwenye kujuwa nini maana ya maisha, mcha Mungu na mwenye hofu ya Mungu na aliyekulia katika maisha ya kawaida na ya chini ya kipato cha kuuza mboga mboga huku akimtumainia na kumtegea Mungu wake katika kila hatua aliyopita.
Wana Mbeya wameshuhudia ndani ya muda mfupi wa Ubunge wa Dr. Tulia namna Mbeya ilivyobadilika, namna inavyochipua kwa miradi ya maendeleo, namna inavyoendelea kupokea mamilioni kwa mamilioni ya fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
Wana mbeya wanaona kwa mara ya kwanza chini ya Ubunge wa Dr. Tulia wanakwenda kupata barabara za lami njia nne kutoka Igawa Mbeya hadi Tunduma, zenye urefu wa KM 237.9 wana shuhudia namna ambavyo shule, vyumba vya madarasa, zahanati, vituo vya afya, barabara za mitaa zimekuwa zikijengwa wakati wote wa Dr. Tulia.
Wana Mbeya wameshuhudia namna wakati huu wa Dr. Tulia ambavyo viongozi wakuu wa serikali wamekuwa wakifika na kuitembelea Mbeya na kuahidi kuleta mamilioni kwa mabilioni ya pesa kwa ajili ya miradi mbalimbali.
Wana Mbeya wanaona namna jiji linavyoendelea kupangwa katika kulifanya liwe na sura halisi na hadhi ya jiji, na siyo kuwa jiji lenye mkusanyiko wa nyumba nyingi tu.
Ujio huo wa maendeleo na miradi ya maendeleo mfululizo ambayo wanambeya wameipata ndani ya muda mfupi imewafanya wajute na walaani sana kumpatia Sugu miaka kumi kuwa Mbunge wa Mbeya mjini.
Imewafanya wajipige vifua vyao na kuapa kuwa katu na kamwe hawatampa kura za ndio tena sugu kuwa mbunge wa Mbeya mjini. Wanasema walifanya makosa ambayo kamwe hawawezi kuyarudia kuyafanya.
Hawawezi kurudia mzaha huo wa kufanya majaribio ya maisha yao kwa kumpa mtu uongozi asiye jitambua wala kutambua thamani na heshima aliyokuwa amepewa.
Kazi iendelee, mama ametufikia na kuwafikia Watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya Watanzania wanyonge wasio na sauti.
Lucas Hebel mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.
0742-676627.