Serikali wekeni ruzuku kwenye Mafuta, hizi bei kwa sasa hazivumiliki tena

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,046
49,730
Sawa bei zimepanda soko la Dunia na mambo kama hayo ila ni muda wa kuweka ruzuku.

Bora kuvuruga Mpango wa miradi 2 au 1 Tupate pesa ya ruzuku kuliko kuua uchumi mzima Kwa kuachia bei ziendelee kuwa Juu kiasi hiki.

Yaani Lita Moja kufikia elfu 4-6 Mikoani huko Vijijini haikubaliki.Mwaka.juzi mliweka ruzuku Kwa nini mwaka huu hamtaki kufanya hivyo?

Wabunge mko wapi kupiga Makelele? Wari Dotto unasairiaje Wananchi? Maana Toka umeingia unatoa matamko tuu yasiyo na impacts.

--
P1.jpg
P2.jpg


--
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), imetangaza bei mpya za mafuta zitakazoanza kutumika leo Jumatano Oktoba 4, 2023 huku bei ya dizeli ikizidi kupaa ikilinganishwa na mwezi Septemba.

Kwa mwezi huu bei za rejareja za mafuta katika
mikoa ya Dar es Salaam, Tanga na Mtwara ni kama ifuatavyo;
Dar es Salaam lita ya petroli ni Sh3,281, dizeli Sh3,448 na mafuta ya taa yakiuzwa Sh2,943. Tanga lita ya petroli ikiuzwa Sh3,327, dizeli Sh3,494 na mafuta taa Sh2,989.

Mkoa wa dizeli imezidi kupaa mara dufu ikiuzwa kwa lita Sh3,520, petrol Sh3,353 na mafuta ya taa Sh3,016.

Ewura imetaja sababu ya mabadiliko ya bei za mafuta kwa mwezi Oktoba 2023 ikiwa ni kupanda kwa gharama za bidhaa hiyo katika soko la dunia kwa hadi kufikia asilimia 4.21 na gharama za uagizaji kufikia asilimia 17 kwa petroli, asilimia 62 kwa dizeli na asilimia 4 kwa mafuta ya taa.

Pia, uamuzi wa wazalishaji wakubwa wa mafuta
duniani (OPEC+) kupunguza uzalishaji na vikwazo vya kiuchumi ambavyo nchi ya Urusi imewekewa na mataifa ya magharibi.

View: https://twitter.com/JamiiForums/status/1709818851582451784?t=jftzZO0aNBzC8MMczQ2kfA&s=19
 
Subiri mama kaingia chimbo na kichwa, akirudi mambo mazuri kabisa.
Waweke ruzuku bwana maana hata mapato ya TRA yameongezeka so uchumi unafanya vizuri unatakiwa kulindwa which means nj kulinda shughuli zetu.

Next month hatutarajii waongeze bei tena
 
Waweke ruzuku bwana maana hata mapato ya TRA yameongezeka so uchumi unafanya vizuri unatakiwa kulindwa which means nj kulinda shughuli zetu.

Next month hatutarajii waongeze bei tena
Wahini fursa, mama anakuja na wawekezaaji kibao wa kilimo.

Mambo ya mafuta yasikupe shida, Mwarubaini wake upo njiani, umeshamsikia Biteko hivi karibuni? Yuko jikoni anakaangiza mambo huko.
 
Wahini fursa, mama anakuja na wawekezaaji kibao wa kilimo.

Mambo ya mafuta yasikupe shida, Mwarubaini wake upo njiani, umeshamsikia Biteko hivi karibuni? Yuko jikoni anakaangiza mambo huko.
Tunazungumzia mafuta , uwekezaji hatufundishwi tuko huko miaka na Miaka na ndio tunaolipa.kodi.
 
Tunazungumzia mafuta , uwekezaji hatufundishwi tuko huko miaka na Miaka na ndio tunaolipa.kodi.
Hujasoma para ya pili, nimeelezea kuhusu mafuta.

Hata uwepo miaka 100, sasa hivi kuna Reforms kwenye kilimo, kuna kitu kinaitwa block farming, kimelenga wawekezaji wakubwa wawawezeshe wawekezaji wa ndani wafanye nao kazi pamoja. Haijawahi kutokea Tanzania.
 
Umekurupuka, rudi juu ukanisome vizuri, la mafuta nimeliongelea post mbili au tatu.

Watanzania mbona mu wavivu sana kusoma?
Mara nyingi unajiona upo 100% na wenzio wapo chini hilo ni tatizo pia wewe usiefanya tafiti wala kusoma vitabu vingi kwa mwaka unajiona ni msomaji sana...
 
Back
Top Bottom