Zanzibar: Bei ya petroli yashuka huku bei ya dizeli na mafuta ya ndege zikipanda kwa mwezi Septemba

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (ZURA) imetangaza Bei mpya za Mafuta kwa Mwezi wa Septemba 2023 ambazo zitaanza kutumika rasmi Siku ya Jumamosi Tarehe 09/09/2023.

Bei zilizotangazwa kwa Mwezi Septemba ni kama zifuatazo Petroli TZS 2,950, Dizeli TZS 3,012, Mafuta ya Taa TZS 2,921 na Mafuta ya Ndege TZS 2,448 ambapo kwa Mwezi Agosti 2023 Bei za Mafuta zilikua Petroli TZS 2,970, Dizeli TZS 2,843, Mafuta ya Taa TZS 2,921 na Mafuta ya Ndege TZS 2,365.

Bei hizo zimetangazwa Siku ya Ijumaa Tarehe 08/09/2023 katika Ofisi za ZURA zilizopo Maisara na Meneja wa Kitengo cha Uhusiano Ndg. Mbarak Hassan Haji kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu ZURA na kueleza sababu za kuongezeka Bei za Dizeli na Mafuta ya Ndege ni kuongezeka Bei hizo katika soko la Dunia kwa asilimia 21 na gharama za bima na usafirishaji kwa asilimia 62 ikilinganishwa na Mwezi Agosti.

Aidha, Meneja huyo alitaja vigezo vinavyotumika na Mamlaka katika kupanga bei, ambavyo ni Wastani wa mwenendo wa mabadiliko ya bei za mafuta Duniani (Platts Quatations), Gharama za uingizaji Mafuta katika Bandari ya Dar-es-Salaam na Tanga, Thamani ya Shilingi ya Tanzania kwa Dola za Kimarekani, Gharama za Usafiri, Bima na ‘Premium’ hadi Zanzibar, Kodi na Tozo za Serikali na Kiwango cha faida kwa Wauzaji wa Jumla na Reja Reja.

Mamlaka hutangaza Bei za Mafuta Tarehe 8 ya kila Mwezi ambapo hutoa wito kwa Wananchi kununua Mafuta katika Vituo halali vya Mafuta na kudai Risiti za Kielektroniki kila wanaponunua Mafuta.
 
  • Thanks
Reactions: K11
Kinachoongezeka huku kipeleke kule kikafidie ile pungufu ya kule.

Siasa ni sayansi.
 
Back
Top Bottom