Nishati: Petroli yashuka Tsh. 33, Dizeli Tsh. 49 na Mafuta ya Taa Tsh. 670 kwa Dar

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
NISHATI: Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji, (EWURA) imetangaza Bei Kikomo za Bidhaa za Mafuta zinazoanza kutumika leo Januari 7, 2024 ambapo Dar es Salaam Petroli itauzwa Tsh. 3,051, Dizeli Tsh. 3,029 na Mafuta ya Taa Tsh. 2,840 kwa Lita 1.

Tanga Petroli itauzwa Tsh. 3,064, Dizeli Tsh. 3,196, Mafuta ya Taa Tsh. 2,886. Mtwara Petroli Tsh. 3,112, Dizeli Tsh. 3,354 na Mafuta ya Taa Tsh. 2,913 kwa Lita Moja ikiwa ni bie za Rejareja.

EWURA imesema kupungua kwa Bei za Mafuta kunatokana na kushuka kwa Bei za bidhaa hizo katika soko la dunia kwa wastani wa 10.66% kwa Petroli, 11.20% kwa Dizeli, 5.82 kwa Mafuta ya Taa pamoja na kupungua bei za uagizaji Mafuta katika Bandari ya Dar es Salaam.

1707295005050.png
 
Wanapandisha Tsh 534 kwa wakati mmoja ila kushusha wanashusha Cents tu ni kama vile wanapangiwa kiwango cha bei ya mafuta inavyoporomoka huko Soko la Mafuta ni tofauti na hawa Ewura wacha waendelee na sarakasi zao..
 
Back
Top Bottom