Mchanganuo wa bei za mafuta ya petroli, dizeli na mafuta ya taa Mei 2022

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Jul 7, 2020
6,328
8,243
Kwanza, kuna gharama za mafuta ambayo ni bei ya mafuta katika soko la dunia na gharama ya uagizaji wa mafuta hayo inayojumuisha gharama za usafirishaji, bima na faida ya mletaji wa mafuta (supplier). Katika bei za Mei 2022 gharama hizi zilikuwa ni kama ifuatavyo:

(i) Petroli – bei ya soko la dunia ilikuwa ni Shilingi 1,821 kwa lita na gharama ya uagizaji ilikuwa Shilingi 89 kwa lita na hivyo gharama ya mafuta hayo hadi yanafika katika bandari ya Dar es Salaam ilikuwa ni Shilingi 1,910 kwa lita;

(ii) Dizeli – bei ya soko la dunia ilikuwa ni Shilingi 2,088 kwa lita na gharama ya uagizaji ilikuwa Shilingi 54 kwa lita na hivyo gharama ya mafuta hayo hadi yanafika katika bandari ya Dar es Salaam ilikuwa ni Shilingi 2,142 kwa lita;

(iii) Mafuta ya taa – bei ya soko la dunia ilikuwa ni Shilingi 1,917 kwa lita na gharama ya uagizaji zilikuwa Shilingi 135 kwa lita na hivyo gharama ya mafuta hayo hadi yanafika katika bandari ya Dar es Salaam ilikuwa ni Shilingi 2,052 kwa lita.

Bei inayotumika kushinda zabuni za kuleta mafuta nchini (premium), kwa kawaida inachangia kati ya asilimia 2 na 7 tu ya bei ya mafuta kwenye vituo vya mafuta nchini huku sehemu kubwa ikiwa ni gharama ya bei halisi ya mafuta yenyewe kwenye soko la dunia.

Pili, kuna tozo za Taasisi za Serikali ambazo ni takribani Shilingi 38 kwa lita ikiwa inajumuisha:
(i) Gharama ya matumizi ya bandari inayolipwa TPA ya Shilingi 15 kwa lita;

(ii) Tozo ya huduma (service levy) inayolipwa kwenye halmashauri Shilingi 8 kwa lita;

(iii) Tozo ya Udhibiti inayolipwa EWURA ya kati ya Shilingi 3.20 na Shilingi 5.50 kwa lita;

(iv) Tozo katika biashara ya jumla na rejareja kwa ukaguzi wa miundombinu inayolipwa kwa Wakala wa Vipimo (WMA), Baraza la Mazingira (NEMC), Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) na Kikosi cha Zimamoto (FRF) ya Shilingi 6.47 kwa lita; na

(v) Tozo ya huduma zinazotolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Wakala wa Vipimo (WMA), Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) wakati ya kupokea mafuta ikiwa ni Shilingi 2.81 kwa lita ya petroli, Shilingi 1.02 kwa lita ya dizeli na Shilingi 4.67 ya lita ya mafuta ya taa.

Tatu, ni kodi za Serikali za Shilingi 920.65 kwa lita ya petroli, Shilingi 800.13 kwa lita ya dizeli na Shilingi 745.77 kwa lita ya mafuta ya taa ambayo inajumuisha:
(i)Tozo ya mafuta ya Shilingi 413 kwa lita ambayo inagawanywa kama ifuatavyo:

a) Shilingi 186 kwa miradi ya TANROADS;

b) Shilingi 177 kwa miradi ya TARURA;

c) Shilingi 50 kwa ajili ya kuendeleza miradi ya maji;

(ii)Ada ya mafuta ya Shilingi 100 kwa lita ya petroli na dizeli na Shilingi 250 kwa lita ya mafuta ya taa kwa ajili ya miradi ya kusambaza umeme vijijini;

(iii) Ushuru wa forodha wa Shilingi 379 kwa lita ya petroli, Shilingi 255 kwa lita ya dizeli na Shilingi 465 kwa lita ya mafuta ya taa; na

(iv) Tozo ya maendeleo ya reli ya asilimia 1.5 ya gharama ya mafuta yaliyofikishwa Tanzania. Gharama hii hubadilika kila mwezi kulingana na gharama ya mafuta yanapofikishwa Tanzania. Kwa mwezi Mei 2022, tozo hiyo ni Shilingi 28.65 kwa lita ya petroli, Shilingi 32.13 kwa lita ya dizeli na Shilingi 30.77 kwa lita ya mafuta ya taa.

Nne, ni gharama za uendeshaji wa biashara ya jumla na faida ya wafanyabiashara ambayo kwa ujumla ni Shilingi 161.18 kwa lita ya petroli, Shilingi 160.67 kwa lita ya dizeli na Shilingi 159.36 kwa lita ya mafuta ya taa.

Tano, ni gharama za uendeshaji wa biashara ya rejareja, yaani vituo vya mafuta na faida ya wafanyabiashara hao ambayo kwa ujumla ni Shilingi 118 kwa lita.
 
Itoshe kusema

Tanzania ukiwa mpiga deal regardless ya cheo chako usipotoboa wewe ni mpuuzi, yaani mifumo iko wazi ushindwe wewe upigaji!
 
Back
Top Bottom