Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,817
4,566
1693949768689.png

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imetangaza kupanda kwa bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli hapa nchini zitakazotumika kuanzia Jumatano September 06, 2023 saa 6:01 usiku ambapo kwa mwezi September 2023, bei za rejareja za mafuta katika Mkoa wa Dar es Salaam petrol ni Tsh. 3213 kwa lita, dizeli Tsh. 3259 na mafuta ya taa 2943.

EWURA imesema mabadiliko ya bei za mafuta kwa mwezi September 2023 yaliyoonesha kupanda kwa bei yanatokana na kupanda kwa gharama za mafuta katika soko la dunia kwa hadi 21%, gharama za uagizaji wa mafuta hadi 62% ikilinganishwa na mwezi August 2023 na maamuzi ya kisiasa katika nchi zinazozalisha mafuta kwa wingi (OPEC+).

Itakumbukwa bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli hapa nchini kwa mwezi uliopita zilizoanza kutumika kuanzia Jumatano August 02, 2023 saa 6:01, bei za rejareja za mafuta katika Mkoa wa Dar es Salaam petrol ilikuwa ni Tsh. 3199 kwa lita, dizeli Tsh. 2935 na mafuta ya taa 2668.

1693948477706.png

1693948527949.png

1693948583525.png

1693948629916.png

1693948674624.png

1693948742276.png

1693948785314.png
 

Attachments

  • Cap Prices wef 6th September 2023 - Kiswahili 59_230905_230037.pdf
    209.4 KB · Views: 6
This mus stop..

Hakuna haja ya kutesa wananchi bila sababu....
Udalali sio kitu kizuri kwa taifa lolote changa kama la kwetu.
Hiyo sio biashara ni uhuni....

Na kama EWURA wameshindwa waache twende kiholela kuliko kuwa na a buch of people paid by tax payers money doing nothing and or protecting the interests of cartels......

Mnaharibu image ya nchi kwa vitu visivyo na maana..

Kwahiyo hata umeme kukatika mara kwa mara ni short supply ya soko la Dunia?
 
Back
Top Bottom