DidYouKnow
JF-Expert Member
- Jul 28, 2019
- 1,094
- 1,691
Kumekuwa na tabia za hivi karibuni, kwamba ili upate nafasi za kazi kwa vyombo vya ulinzi na usalama, mojawapo ya sifa ya waombaji ni kupitia mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa. Huu ni ubaguzi wa wazi kabisa.
Hivi toka lini vijana wote waliohitimu kidato cha sita waliitwa wote kujiunga na jeshi la kujenga Taifa? Ina maana hata wale ambao hawakuchaguliwa kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa, pasipo hiari yao, wameondolewa sifa za kuwa watumishi wa vyombo hivi vya Ulinzi na Usalama.
Kufanya kigezo cha kupitia mafunzo ya JKT kama moja ya sifa ya kupata kazi Polisi, Magereza, Uhamiaji na TAKUKURU ni ubaguzi wa wazi kwa watu ambao hawakuchaguliwa kujiunga na vyombo hivyo na pia ni mwendelezo wa upendeleo kwa watu waliopendelewa kujiunga na kozi hizi za JKT.