Nyamesocho
JF-Expert Member
- May 5, 2023
- 476
- 1,244
Serikali ilianzisha utaratibu wa vijana kujiunga na Jeshi la kujenga Taifa (JKT) pamoja na malengo mengine ilikuwa kuwajengea vijana moyo wa uzalendo na kuipenda nchi yao na kuwa vijana wa kujituma, waadilifu wenye nidhamu na kujitolea kuisaidia jamii.
Lakini ni tofauti sana licha ya watanzania wengi kupitia JKT na kupata mafunzo ya uzalendo kwa nchi yake ndo wizi wa mali za umma umekithiri zaidi na mbaya zaidi wanaohusika ndo walipata mafunzo ya JKT.
Uadilifu na uzalendo wa mtu hutabadilishwa na JKT hata siku moja bali kwenye jamii alipokulia.
Mtanzania hawezi kuwa mzalendo kama alikulia kwenye mazingira yafuatayo;
1. Alipokuwa mtoto alikuwa anadokoa vitu, madaftari ya wanafunzi, nyumbani na mtaani na mbaya zaidi jamii wakimfuatilia wazazi wake humkingia kifua, usitegemee JKT itambadilisha tabia.
2. Kama amekulia mazingira ya umimi, hali ya kutothamini watu wengine haikuwepo usitegemee JKT itambadilisha.
3. Alisoma shule zaidi ya 4 kwa sababu ya nidhamu usitegemee JKT itambadilisha.
4. Kama shule ya msingi na sekondari alikuwa na kiburi na akipewa adhabu wazazi wake wanakuja juu usitegemee JKT itambadilisha.
5. Viboko vitembee kwa wanafunzi visipotembea usifikiri JKT itambadilisha tabia.
Ushauri kwa serikali, inapoajiri iangalie pia historia ya utotoni msingi na sekondari.