Luhaga Mpina apiga kura kukataa azimio la Bunge la kufuta kigezo cha JKT kuajiriwa kwenye Majeshi ya Ulinzi na Usalama

Stuka

JF-Expert Member
Jul 19, 2022
214
686
Bunge limepitisha azimio la kuondoa kigezo cha kupitia mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) pamoja na Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU) kwa vijana wanaoomba nafasi za ajira katika vyombo vya ulinzi na usalama huku Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina akipiga kura ya hapana kutounga mkono azimio hilo.

Azimio hilo limekuja kufuatia hoja ya dharura iliyotolewa jana Alhamis Februari 15, 2024 na Mbunge wa Mbozi, George Mwenisongole na kisha Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson kutaka kujiridhisha ikiwa Bunge limeshawahi kutoa maelekezo juu ya jambi hilo.

Hata hivyo baada ya kujiridhisha kuwa hakukuwahi kuwa na maelekezo juu ya jambo hilo alimruhusu Mbunge huyo kutoa hoja ambayo iliungwa mkono na kisha ikajadiliwa na azimio likatoka.

Hata hivyo wakati akitoa hoja ya kuahirisha Bunge Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alilitaja azimio kupitishwa na Bunge kama moja ya maazimio yaliyopitishwa kwenye mkutano huu wa Bunge.

Huyu atahamia Chadema
hawezi kuhamia kwenye chama kutwa kucha kiko kwenye maridhiano huku wananchi wanateseka na matatizo yao ya umeme, sukari, kupanda kwa maisha wao mda wote wako Ikulu kwenye maridhiano ambayo haiwelezwi wanariadhiana nini wanasahau kufanya kazi yao ya upinzani kama Jicho la kuisahihisha serikali wao wanasaka maslahi binafsi...Mpina hawezi kwenda Chadema hawana mfumo wa kitaasisi ataendelea kuwa mwana CCM muumini wa Katiba ya CCM, aZIMIO LA ARUSHA..
 
View: https://youtu.be/5qkvwqBGwEE?si=W9HGqt5i-pC3TTBG

Mmmh...mbona kama hili azimio ni la mchogo wanataka Majeshi nayo watu waanze kuingia kwa memo..? mpina amestukia mapema huu mchongo lakini naamini JWTZ hawatakubali huu ujinga wataendelea na mfumo wao wa namna ya kuwaandaa askari wake... Tulia kama vijana wako wamekosa nafasi waambie waende JKT huwezi kulitumia bunge kufanikisha maslahi binafsi.... Vyombo vya Usalama fuatilieni kwa kina kujua msingi wa azimio hili kama limekidhiri vigezo msiwaruhusu wanasiasa wasiolitakia mema taifa letu wawe waamuzi wa mambo ya ulinzi na usalama wa nchi yetu.
 
hawezi kuhamia kwenye chama kutwa kucha kiko kwenye maridhiano huku wananchi wanateseka na matatizo yao ya umeme, sukari, kupanda kwa maisha wao mda wote wako Ikulu kwenye maridhiano ambayo haiwelezwi wanariadhiana nini wanasahau kufanya kazi yao ya upinzani kama Jicho la kuisahihisha serikali wao wanasaka maslahi binafsi...Mpina hawezi kwenda Chadema hawana mfumo wa kitaasisi ataendelea kuwa mwana CCM muumini wa Katiba ya CCM, aZIMIO LA ARUSHA..

Umeongea utoto gani hapa?
 
Hizi mambo ndio za kuanza nazo iwapo upinzani utachukua hatamu

Haiwezekani kupitishwa azimia ambalo hapo badaye itamhitaji mtu mwenye pesa nyiingi sana za kuhonga (Rushwa) ili kupenya kwenye nafasi hizo, na ama, ccm inajitengenezea mazingira ya kuajiri wanaccm tu hapo tena wale watoto wa vigogo tu, hii ni njia ya kuwakataa watoto wa walala hoi kuingia kwenye ajira hizo
 
Tujiandae kupata JWTZ legelege zaidi ya sasa
Japo sijakubaliana sana na hilo azimio ila kumbuka kuna kitu inaitwa shule ya awali ya mafunzo ya kivita (RTS) kwangu mimi hapo hadi kupavuka wewe ni askari kweli. Kuna wana walipiga NS tena ya volunteer kabisa ila pale kihangaiko walidunda.

Vile vile zipo special intake ambazo watu wanapiga na wanamaliza uzuri wa janx ni kwamba ukifika RTS kuna vitu huwi mgeni navyo milele.
 
Umeona mbali sana kiongozi.
Kigezo cha kupitia jkt kiliwekwa ili kupunguza kubebana ukikiondoa maana yake wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama watakua na power ya kuajiri ndugu zao moja kwa moja hali itakayosababisha wasiokua na ndugu kwenye hizo nafasi wapitie wakati mgumu
 
Tanzania sasa kukosa jeshi la akiba lenye wasomi.

Jeshi la IDF la Israel, South Korea nk wanategemea sana wasomi waliopo ktk jeshi la akiba, maana yake wamepitia kitu na mafunzo yanayofanana na ya JKT.

Maazimio ya bunge letu, ni kumpunguzia amiri jeshi mkuu kuwa na jeshi kubwa la akiba maana sasa kila msomi atakacha kujiunga na jeshi la JKT

Bunge letu linazidi kuonesha kukosa uzalendo kwa nchi yetu, halitizami mbele kuwa pengine taifa litahitaji askari wa akiba waliopitia angalau mafunzo ya JKT ili kukabiliana na adui atakayeleta vita kubwa kama ile ya kihistoria vita ya Kagera tunayosoma na kusimuliwa juu ya mchango mkubwa wa jeshi la akiba kama JKT n.k kwa TPDF / JWTZ.
 
Mmmh...mbona kama hili azimio ni la mchogo wanataka Majeshi nayo watu waanze kuingia kwa memo..? mpina amestukia mapema huu mchongo lakini naamini JWTZ hawatakubali huu ujinga wataendelea na mfumo wao wa namna ya kuwaandaa askari wake... Tulia kama vijana wako wamekosa nafasi waambie waende JKT huwezi kulitumia bunge kufanikisha maslahi binafsi.... Vyombo vya Usalama fuatilieni kwa kina kujua msingi wa azimio hili kama limekidhiri vigezo msiwaruhusu wanasiasa wasiolitakia mema taifa letu wawe waamuzi wa mambo ya ulinzi na usalama wa nchi yetu.
watu wanaumia JKT halafu wakose kazi hii haifai. kumbuka kwenye vyombo vya ulinzi uzalendo ni muhimu JKT ni kisima cha kuchota wazalendo. full stop
 
Kigezo cha kupitia jkt kiliwekwa ili kupunguza kubebana ukikiondoa maana yake wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama watakua na power ya kuajiri ndugu zao moja kwa moja hali itakayosababisha wasiokua na ndugu kwenye hizo nafasi wapitie wakati mgumu
Yawezekana pia wamehisi huu mhimili ni wamuhimu Sana lazima waushike ili kukata kabisa Yale mawazo ya kuachia keki ya taifa Kwa kuhakikisha wanapenyeza vizazi vyao ngazi za juu
 
Back
Top Bottom