JKT yakanusha suala la kunyanyasa vijana

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,817
4,566
Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), limewataka Wazazi na Walezi wa Vijana kupuuza taarifa za uzushi unaolenga kuwatia hofu Vijana waliopangiwa kuhudhuria Mafunzo ya JKT katika makambi mbalimbali kutokwenda kuripoti makambini, kwa kile kinachodaiwa kuwa eti, mafunzo ya JKT ni mateso, yana unyanyasaji na udhalilishai hususani kwa Vijana wa jinsia ya kike.

JKT imesema taarifa hizo ni uzushi kwani mafunzo hayo ni muhimu sana kwa ustawi wa Vijana na Taifa kwa ujumla

“Hivi karibuni JKT ilitoa wito kwa Vijana wote waliohitimu elimu ya sekondari kidato cha sita mwaka 2023, kutoka Shule zote za Tanzania Bara kuhudhuria Mafunzo ya JKT kwa mujibu wa Sheria lakini kumezuka taharuki kubwa katika mitandao ya Kijamii kutoka kwa baadhi ya Watu wenye nia ovu wasilolitakia mema Taifaletu”

“Mafunzo ya JKT kwa mujibu wa sheria na yale ya Kujitolea yamelenga kumjengea kijana wa kitanzania uzalendo, ukakamavu, nidhamu na kuleta umoja wa kitaifa na yanaendeshwa kwa kuzingatia mila, desturi na tamaduni za kitanzania”

“JKT katika kuhakikisha Vijana hao wanakuwa salama wakati wote, Makambi na Vikosi vote vya JKT vina Baba na Mama Mlezi (Patron a Matron) ambao wamewekwa mahususi ili kusimamia ustawi wa Vijana wa kiume na wa kike kwa kipindi chote wanapokuwa makambini”
 
Hakuna mateso huko bhna,..Sisi tuliienjoy Op Magufuli. Ila kuna kupigwa tochi🤣🤣🤣
 
Serikali iweke utaratibu wa kulazimisha watu waende JKT. Kwa mfano ingekuwa hila JKT huwezi kufanya application ya chuo mbona watu wangeenda! Ila kwa vijana wenye matatizo ya kiafya sijui ingekuwaje?
 
Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), limewataka Wazazi na Walezi wa Vijana kupuuza taarifa za uzushi unaolenga kuwatia hofu Vijana waliopangiwa kuhudhuria Mafunzo ya JKT katika makambi mbalimbali kutokwenda kuripoti makambini, kwa kile kinachodaiwa kuwa eti, mafunzo ya JKT ni mateso, yana unyanyasaji na udhalilishai hususani kwa Vijana wa jinsia ya kike.

JKT imesema taarifa hizo ni uzushi kwani mafunzo hayo ni muhimu sana kwa ustawi wa Vijana na Taifa kwa ujumla

“Hivi karibuni JKT ilitoa wito kwa Vijana wote waliohitimu elimu ya sekondari kidato cha sita mwaka 2023, kutoka Shule zote za Tanzania Bara kuhudhuria Mafunzo ya JKT kwa mujibu wa Sheria lakini kumezuka taharuki kubwa katika mitandao ya Kijamii kutoka kwa baadhi ya Watu wenye nia ovu wasilolitakia mema Taifaletu”

“Mafunzo ya JKT kwa mujibu wa sheria na yale ya Kujitolea yamelenga kumjengea kijana wa kitanzania uzalendo, ukakamavu, nidhamu na kuleta umoja wa kitaifa na yanaendeshwa kwa kuzingatia mila, desturi na tamaduni za kitanzania”

“JKT katika kuhakikisha Vijana hao wanakuwa salama wakati wote, Makambi na Vikosi vote vya JKT vina Baba na Mama Mlezi (Patron a Matron) ambao wamewekwa mahususi ili kusimamia ustawi wa Vijana wa kiume na wa kike kwa kipindi chote wanapokuwa makambini”
Uende JKT halafu usipewe kashi kashi hilo litakuwa jeshi au kikundi cha ngoma ya baikoko?
 
Wanaweza kuwa sahihi lakini kuna lingine kijana aliyemaliza Iringa kupelekwa Mara Kwa gharama za mzazi. Kwa uchumi wa wazazi Mtu atoe 300,000 kwenda na kurudi na vifaa vya kujinunulia? Sidhani kama walioteua walizingatia uchumi wa wazazi.
 
Wazazi wengine wana vijana wawili hata watatu..hizo hela za maandalizi na nauli zinatoka wapi?
Ni nini thamani ya vijana kwa nchi yao? Kama vitu vidogo kwa serikali lazima wazazi wagharimie.
 
Videmu vya makamanda siku hizi havipo..?
Hii nchi imekuwa ya ajabu Sana , imefikia mahali wazazi wanaingilia Hadi program za mafumzo ya jkt. JKT ni jeshi sio shule za msingi au sekondari. JKT waambieni ukweli pale ni jeshi na wanapewa mafunzo ya ujasiri na ukakamavu wa kijeshi , kwa tafsiri nyepesi wanaandaliwa kuwa jeshi la akiba. Haya ndo madhara ya kupeleka watt shule za st. vitoto plus wazazi wanafikra za umayaimayai .
 
Ifikie kipindi haya mambo yawe mtu akipenda.. dunia imebadirika sanaa.. Isipokuwa wao JKT wafanye mazingira ya kuwavutia.. yani mtu yupo class avutiwe sana kujiunga na JKT mwenyewe
 
Back
Top Bottom