Labda useme unataka wanawake wapate nini kwenye mahusiano.
Mimi ninachofahamu kwenye mahusiano ni kumjenga kila mmoja auwe the best version of himself/ herself huku mkiwa na malengo kwamba siku mmoja mtakuwa familia rasmi labda na watoto wenu. Sidhani kama mahusiano ni sehemu ya mwanamke kuchuma pesa za mwanaume, inaweza kutokea mara moja umetolewa lunch, dinner au vacation Zanzibar, umepewa zawadi ya birthday n.k ikabidi mwanaume agharamike basi shukuru lakini sio kuwa entitled au kumganda kijana wa watu akuhuhudimie kama baba yako au kumgeuza ATM.