Hili suala halipaswi kuwa na utata, hakuna mtu anayemchezea mwenzake katika mahusiano ya dating, pande zote wanaume na wanawake inaweza kutokea wakati wowote mmojawapo akaona hawezi kuwa na future na mwenzake akayamaliza mahusiano.
Ikitokea mwanamke ndiye amemaliza mahusiano huwa haisemwi alikuwa anamchezea mwanaume ila ikitokea mwanaume ndio anaona mahusiano hayawezi kuendelea akayamaliza inasemwa alikuwa anamchezea mwanamke! Hii Ni double standard ambayo siwezi kuielewa kirahisi, labda kwa sababu wanawake wengi huwa hawajiendelezi kibinafsi hata katika mahusiano ya dating badala yake huwa wanabaki tegemezi tu kwa mwanaume kama tayari wameolewa vile kwa hiyo mahusiano yakiisha ghafla wanakuwa hawana mueleko wowote.
Tutofautiane mitazamo: Kwangu mimi dating ni exploration yenye lengo la kumtafuta unayefit nae. Dating haihitaji any kind of heavy investment from both ends.
1.Tunaweza kuamua kukutana kanisani tuongee
2.coffee shop ambayo bill itakuwa “afu 20” tutashare hiyo bill,
3. naweza kukuletea zawadi ya boxa ukaniletea zawadi ya mswaki,
4.tunaweza kukutana kijiwe cha chips (ofcoz sitakuja)
5.tunaweza kwenda at any poshy restaurant hata bill ije laki 4 tutashare. (Age gape izingatiwe, sababu tell me mtu wa miaka 46 anatafuta nini kwa mtu wa miaka 32, Mtu wa miaka 34 anatafuta nini kwa mtu wa miaka 18?)
it’s dating…. vivyo hivyo haipaswi kuhusisha suala zima la sex…. dating haifanyiki kwenye nyumba ya mhusika yeyote (kwao/kwake/kwetu/kwangu) Tukikubaliana tukafanya commitment ndipo tunayaita mahusiano ambayo yanahusisha mawasiliano ya mara kwa mara, sex na mipango mingine …. Again hizi ni standards zangu ambazo haziamui chochote kwenye jamii.
Dating sio mahusiano ni hatua kuelekea mahusiano, tukiingia sasa kwenye mahusiano ndio mjadala wangu na wewe unakuja, yaani unamaanisha mahusiano hayapaswi kuwa na accountability yoyote, yeyote muda wowote akiamua kuyasitisha anaondoka shwaaa, asisemwe wala asilaumiwe.
Kwenye relationship dynamics, kila gender inabeba risk zake , muda ni risk factor kwa mwanamke kwenye mambo mengi sana, hiyo accountability unayo kwepa hapa Yoda, ndio iliyoiweka jamii kwenye Prostitution era tuliyopo sasa.
Katika habari yako hiyo mbona mnanormalize umalaya, na mnakataa gharama na kwensekwense zake????