Seanolson Mzungu: Wanawake wa bongo ni omba omba

Seanolson Mzungu: Wanawake wa bongo ni omba omba

Na kama siuzi mwisho wa siku napata nini kwenye hayo mahusiano ili nithaminishe uwepo wangu hapo, assume na mimi nakutaka pia… (umenitongoza na mimi nataka kukubalia)

Wanawake sio wajinga, mbona watu kibao tu wanaendesha mahusiano bure…. ninyi mnaotozwa ushuru lazima mjihoji nia zenu!!!
Kama hauuzi basi utapata kile ambacho nawe unakitoa. Kwa tamaduni zetu waafrika majukumu na wajibu wa kila jinsia kwenye mahusiano/ndoa unajulikana.

Hapo aya ya mwisho umesema kwamba kuna wanaume wanaendesha mahusiano bure?
 
Yoda kwenye hili specifically naomba tukubali kutokubaliana.

Tukiingia kwenye mahusiano kila kundi linabeba risk zake, hizo risk ndizo zinazofanya wanaume mtetee wanaume na wanawake tutetee wanawake.

Inahitaji empathy ya hali ya juu sana kuelewa kundi lingine linasema nini, again, who cares?
Hili suala halipaswi kuwa na utata, hakuna mtu anayemchezea mwenzake katika mahusiano ya dating, pande zote wanaume na wanawake inaweza kutokea wakati wowote mmojawapo akaona hawezi kuwa na future na mwenzake akayamaliza mahusiano.

Ikitokea mwanamke ndiye amemaliza mahusiano huwa haisemwi alikuwa anamchezea mwanaume ila ikitokea mwanaume ndio anaona mahusiano hayawezi kuendelea akayamaliza inasemwa alikuwa anamchezea mwanamke! Hii ni double standard ambayo siwezi kuielewa kirahisi, labda kwa sababu wanawake wengi huwa hawajiendelezi kibinafsi hata katika mahusiano ya dating badala yake huwa wanabaki tegemezi tu kwa mwanaume kama tayari wameolewa vile kwa hiyo mahusiano yakiisha ghafla wanakuwa hawana mueleko wowote.
 
🤣 Kuna mambo hamtuonei, hata sisi tunafahamu kuwa hamtuonei!

Unaona hiyo case yako, ninyi hamkuwa kwenye mahusiano, wewe ulikuwa kwenye mahusiano pekeyako na huyo binti.

Ni muhimu kujua hisia zetu zinapochezewa na mbinu za kujilinda, wanawake wameona mbinu ya kujilinda ni kuomba hela mambo yasiwe mengi!
Ndio ujinga wenyewe alafu manzi kama huyu asipoolewa anakuja mitandaoni kulalamikia wanaume na kushinda kwa mwamposa akiomba ndoa
 
halafu siku hizi mpaka mahohehae na matahira mandazi wanatumia hako kamsemo! saa ingine hana hata cha maana naye mlala hoi tu kama mwenzie, sijui wanataka tulete nini, familia zetu au? wanalazimisha mambo mwishowe wanaletewa watoto wa nje! haya mimi naleta chumvi na nyanya, stupid!
Ni ujinga mtupu. Hata zamani, mwanaume ulikuwa unaenda kuoa ni kuchukua binti toka kwao. Siku ya harusi (anapotoka kwao) mwanaume ulikuwa unampa dada yako sanduku lina hata chupi atakayovaa bibi harusi. Kila kitu anakiacha kwao anakuja kama alivyozaliwa. Akifika kwenu kila kitu anakikuta. Vyako ni vyenu, vyake alivyochuma kabla ya ndoa anaviacha kwao. Huo ndiyo utamaduni wa kiafrika. Hata katika maandiko imeandikwa mwanamke hapendi huwa anapendwa.

Kitu mwanamke anategemewa kutoa ni K yake na nguvu zake tu, siyo material things
 
Mtihani sana, ndo mana Kuna campaign vijana wameanzisha ili utongozwe lazima uwe na kazi inayo tambulika, uwe na pesa, uwe na vitu vya ndani tofauti n hapo unaliwa unaachwa
Nilikua siijui hii kampeni. Nafikiri nahitaji pia na mimi kuipa nguvu. Zama za mwanamke kuingia kwenye mahusiano akiwa masikini asiyeweza hata kumudu mahitaji yake lazima zifike mwisho.

Mwanamke masikini akae mbali na mahusiano ajenge maisha yake kwanza, otherwise akubali kutumika kama chombo cha starehe. Tupo kwenye zama za usawa wa kijisnia. Mwanamke kapewa fursa zote akizopewa mwanaume. Hakuna tena excuse ya mwanamke kuingia kwenye mahusiano akiwa masikini

Tunahitaji kuuona kwa vitendo huo u-independent woman wao wanajinasibu nao.
 
Wanaume huwa hawawaachi wanawake kwa sababu wamejipata , Hilo jambo sio kweli kabisa, wanaume wanaweza kuachana na wanawake wao baada ya kukutana na wanawake wanaowapenda zaidi na hii haimaanishi mara zote walikuwa wanampotezea mwanamke muda, tofauti kubwa ni kwamba wanawake wengine pia huachana na wanaume zao katika dating baada ya kukutana na wanaume wanaowapenda zaidi, wenye pesa, mali, umaarafu au wenye malengo ya kuoa kwa haraka, lakini wanaume huwa hawalalamiki wamepotezewa muda.
Mwamba unapigilia Msumari
 
Natamani uelewe hili ni kundi lipi linazungumziwa hapa, vijana wengi wataelewa zaidi, hapa sio mahusiano committed, hapa tayari ni ile hali ya kuviziana, kila mmoja anamuwahi mwenzie atakayechelewa tu inakula kwake, achana na hast generalization kwanza, utaona ni kundi kubwa ndio, lakini halibebi hatma ya kila mwanamake!

kuhusiana na utamaduni wa mahari hata sisi tumeukuta na hatuwezi kuupinga, maana ndio heshima yetu inapotafsiriwa, ni kama swala zima la ndoa wangapi hawaandikishani popote na hawafanyi sherehe lakini wanaishi vizuri tu mpaka mwisho! lakini kwa taratibu zilizowekwa inalazimu wengi wafanye hiyo na wala haina maana yoyote ndani ya ndoa!

swala zima la kuombana pesa linaletelezwa na hali ngumu ya maisha, vilevile tamaa na pressure za mitandao! wanaume wenye pesa wana nafasi kubwa sana ya kupata wanawake wazuri kuliko wasio nazo, hiyo imefanya kwa kiasi kikubwa sana wanawake wengi kutamani wanavyopewa wengine! mtu anaenda chuoni, mwenzie anapaki defender nje, ana biashara mjini hawazi kodi etc.. ukijiangalia wewe unapata ka-bf hakana mwelekeo wowote mnateseka nako na watu wanawacheka! as a human being binti lazima ataangukia hili kundi, wachache sana wanatoboa hapa ni mpaka wawe na ego kama kina sisi! wale masikini jeuri! hii tabia inaanzia mbali inakomaa mpaka kufikia binti kuwa ombaomba haianzi leo, saa nyingine anaona mzazi wake yupo hivyo, au kwenye tamaa anapitia humohumo! wengine haujawahi kuona mama akiombaomba hata kwa bahati mbaya amezoea kukomaa mwenyewe mpaka afikie lengo, tofauti na mabinti wengi anajifungia ndani anafuma mfumo wa kumuingizia pesa kwa style hiyo, akitoka hapo kaiva hana cha kupoteza na hajali wala nini, anaanza kupiga simu kila kona anazozijua! swala la kuomba omba si jepesi kama unavyofikiria ni mfumo unatengezeneka hapo..

kwa upande wangu nimesupport hili jambo, lakini sijabase kwa wauzaji, unasema tusimuweke mwanaume, ila mpaka mwanaume anaombwa pesa inamana amekuja bila adabu! hivi wewe unaniombaje sehemu za siri? hatuna mahusiano tumekutana hata lisaa halijatimia unategemea nitakutreat ipi? lazima tutaishia kukokomoana iwe nataka au sitaki!

Nini kifanyike? tulee ,mabinti zetu katika njia zitakazowafanya waone hili jambo sio la kawaida na inawezekana, ukiwa present father kwa mabinti zako, kuna waepushia mambo mengi ya kuanguka katika shimo hilo huku wakifikiri ndio ujanja au usasa, kumbe ni fedheha kwa jamii zisizokubaliana na hili jambo!
Unaposema wanawake huwa wanaombwa sehemu za siri (sex) ni kwamba wanawake huwa hawatamani kufanya ngono kabisa kabla ya ndoa na wanaweza kuvumilia kirahisi kutofanya ngono mpaka waolewe?? Mimi nafikiri wanawake nao huwa wanatamani kufanya ngono mara nyingi tu ila huwa hawana ujasiri au sijui ndio maadili inakuwa vigumu kuanza kumuambia mwanaume wakafanye ngono kwa sababu wana hamu kwa wanabaki wanategea mwanaume ndio aanze ili waanze kujibaraguza.
 
Na siku hizi wamekuwa wazi haswa utamsikia Mimi nataka mwanaume mwenye hela akiitwa Malaya anakasirika au wanamsemo Mimi siwezi kukupa Bure na akija ghetto lazima atataka umwachie na hela japo kala vizuri na sex kaenjoy kama sio u Malaya ni Nini?
Juzi kati nipo sehemu moja napata kinywaji. Akijisogeza dada mmoja hivi karibu yangu. Tukawa tunapiga story za hapa na pale. Katikati ya story akaniambia "tukiwa kwenye mahusiano unaweza kunipa angalao laki". Kichwani nikajua hapa napiga story na dadapoa wa mchongo
 
Ni ujinga mtupu. Hata zamani, mwanaume ulikuwa unaenda kuoa ni kuchukua binti toka kwao. Siku ya harusi (anapotoka kwao) mwanaume ulikuwa unampa dada yako sanduku lina hata chupi atakayovaa bibi harusi. Kila kitu anakiacha kwao anakuja kama alivyozaliwa. Akifika kwenu kila kitu anakikuta. Vyako ni vyenu, vyake alivyochuma kabla ya ndoa anaviacha kwao. Huo ndiyo utamaduni wa kiafrika. Hata katika maandiko imeandikwa mwanamke hapendi huwa anapendwa.

Kitu mwanamke anategemewa kutoa ni K yake na nguvu zake tu, siyo material things
Kwanza mkishaingia kwenye ndoa ni biashara nyingine kabisa tofauti na huu ujinga wa u-bg na u-gf uchwara! yani tudate miezi 6 unataka nikuletee nini, nikasombe vya baba'angu nikupe? mkiwa ndoani huwezi kuishi na mke kama sanamu lazima kuna mahala atawajibika tu, ukimshirikisha jambo atakuja na wazo hili mnashauriana maisha yanaenda, hivi hawa walalamikaji wanakuaga na ndoa kweli au anaokota tuanafunzi tushenzi huko anakuja kutujazia server tu hum?

Angalia ndoa nyingi ni tofauti na maneno yasemwayo, ukinunua mashamba mke akanasimamia wakulima wewe unaendelea na mishe zako, ukinunua mashine mwanamke atasagisha mahindi auze unga na kutafuta masoko, ukileta chakula atarekebisha ndani vizuri, ukimpa mimba ataza mtalea watoto huku yeye akichukua jukumu la malezi kwa nafasi kubwa zaidi, sasa hapo wanatakaje au ukute mnataka mpewe mimba mkuu ila hamsemi? unaweza kuta unabishana na ijana akili zinawaza pegs tu!
 
Halafu kwa uombaomba wa hivi hata apewe milioni hawezi kufanya kitu cha maana kuanza kujiondoa katika hali hiyo.

Anakuwa ombaomba tegemezi.

Ni kitu kimoja kumsaidia mwanamke anayeweza kujipanga na kusimama mwenyewe.

Huyu hata bila kutaka kumdinya unaweza kumuonea huruma ukamsaidia ayapate maisha hata kama kiroho safi tu umemuona mwananchi mwenzako ana potential ya kufanya vizuri. Labda na wewe ulipitia au kujua matatizo, unajua everybody deserves support. Unaweza kumsaidia hata pale huna nia ya kumdinya. Wanaume huwa tunasaidia hivyo pia. Wengine hatuwezi kutaka kumdinya kila mwanamke tunayekutana naye. Kwanza si kika mwanamke atakuvutia hivyo, wengine wana ukurutu.

Wengine tumewasaidia hata hapa JF bila ya kuwaona tukijua hatutawaona maisha haya wako Africa na mtu kama mimi sijarudi Africa mwaka wa 14 huu na sina mpango wa kurudi mpaka afe mtu wa karibu kabisa. So tumesaidia hata bila ya nia ya ngono, kutoka mbali.

So unamuona mtu analialia njaa huko Africa, unaona pesa anayohitaji ni dola elfu chache tu ambazo kwako unamaliza kwenye anasa ya siku chache, ila yeye inaweza kumuanzishia biashara ya kubadilisha maisha yake, unampa bila hata kufikiria kuwa kuna siku mtaonana, kiroho nzuri tu. Mimi nishafanya hilo. Unajinyima anasa ndogo tu, mtu anapata nafasi ya kubadilisha maisha.

Mimi mara nyingine nakuwa na huruma sana kwa wanawake. Naona shida za Tanzania. Ingawa mimi si tajiri, nafikiria sana kuwa sina shida kama zile. So, I try to give back.

Ila sasa, ukifanya hivyo kumuanzishia biashara asimame mwenyewe, yeye anaona wewe ndiyo danga lake sasa.

Unashindwa kabisa kuelewa hii mentality.

So, ni kitu kimoja kumsaidia mwanamke anayeweza kujiongeza mwenyewe.

Ni kitu tofauti kabisa kumpa pesa mwanamke zombie ambaye hajui kufanya lolote zaidi ya kuomba pesa tu.

Na wanawake wa Tanzania wengi ni wa kundi hili la pili.
Umeongea jambo la msingi sana hata Mimi lilinikuta nilimsaidia Binti mmoja nilikuwa jirani nae akanifungukia shida yake nami ikanigusa nikaamua nimsaidie kiroho safi tangu ni msaidie ikawa kama nifungulia mbwa kila akipata shida lazima aniombe Mimi nimsaidie as if kama vile ni ndugu yake, Baba yake mzazi hama boyfriend wake yaani ndugu yangu inasikitisha kwa kweli
 
Unaposema wanawake huwa wanaombwa sehemu za siri (sex) ni kwamba wanawake huwa hawatamani kufanya ngono kabisa kabla ya ndoa na wanaweza kuvumilia kirahisi kutofanya ngono mpaka waolewe?? Mimi nafikiri wanawake nao huwa wanatamani kufanya ngono mara nyingi tu ila huwa hawana ujasiri au sijui ndio maadili inakuwa vigumu kuanza kumuambia mwanaume wakafanye ngono kwa sababu wana hamu.
Aisee, labda hujajichanganya vizuri, mbona siku hizi wanawake wengi wanaomba tena waziwazi, angalia wanavyojianika uchi huko ndio useme maadili, kuna mmomonyoko mkubwa sana wa maadili mkuu!

Nje ya mada; mbona kama leo umetugeka mkuu imekuwaje mtetezi wetu 🫢
 
Kila kitu kinaanza kwenye mawazo.

Kuna watu wengi wanaangalia mazungumzo haya na kujiongeza kutokana na hoja, amini usiamini kuna wengi wamekaa on the fence wanaangalia hoja, na hoja yako ya hapa JF inaweza kubadili mawazo ya mtu akatae kudanga na kutafuta njia nyingine, au hoja yako inaweza kumfanya mtu akubali kuwa kudanga ndiyo maisha. Hata kama ni polepole tu.

Najua wengi wanapenda kuona mambo ya haraka, ila mabadiliko ya kiutamaduni hayafanyiki kiharaka, hayafanyiki kwa revolution yanafanyika kwa evolution. Mimi napenda revolution, don't get me wrong, lakini naelewa uhalisia unaenda na evolution zaidi.

Kwa hivyo, kwanza tukatae utamaduni wa kudanga sisi wenyewe. Hizi hoja cheap za ku commoditize ngono kama girl power ambazo hata wafeminia wengine wanazo ni za kijinga tu, kwa sababu hata wao wanaona kimsingi this thing is dehumanizing.

Tukatae kudanga, tukatae kutetea kudanga, tulazimishe mabadiliko ya kimsingi katika jamii. Pengine wanawake wanakuwa disadvantaged kibaiolojia wanazaa, wanapoteza muda kwenye career. Kwa hivyo tunaweza ku push mifumo ya kiserikali iwafikirie wanawake kuwa support kwa kuelewa disparity hiyo.

Wanawake ni dada zetu ni mama zetu ni bibi zetu ni binti zetu ni wake zetu, tunawapenda, hatutaki mazungumzo ya haki za wanawake yageuke kuwa ni vita kati ya wanawake na wanaume. Hatutaki wanawake wasio na option katika maisha wanaohitaji kujiuza ili ku survive.

Kwa kubadilisha mifumo hivyo, mwanamke anaweza kufaidika bila kutegemea kudanga.
Sharp!

Yoda Seran Natafuta Ajira Hziyech22 gwapole Labella Ven26
 
Nje ya mada; mbona kama leo umetugeua mkuu imekuwaje mtetezi wetu 🫢
Kuna wakati nilikuwa nafikiri labda ni kesi moja moja tu (isolated cases) za wanawake wachache wa mjini wanaopenda maisha ya kung'aa ila nimekuja kugundua sasa imekuwa mtindo wa maisha kabisa wa wanawake wengi hasa wanawake late 90's na vibinti vya 2000's.
 
Back
Top Bottom