Sasa ni dhahiri Bungeni kuna kundi la Rais Samia na kundi la Hayati Magufuli. Spika Ndugai awataka wabunge wa CCM kuitisha kikao cha usuluhishi

Uko sahihi wanataka waonekane wako wengi na wana nguvu, lkn group bila kiongozi wa kikundi ni kazi bure.
 
Nje ya Muungano Kuna Wapemba na Waunguja.....

Kuna Wanzanzibari na Wanzanzibara.

Wapinzani hawapo bungeni, Sasa Kuna wabunge wa Darasa la Saba C na Wabunge Wasomi.

Kuna Wabunge kundi la Mwendazake Mfalme Jiwe na Kuna Wabunge kundi la Mama Samia suluhu Hassan .

Na Kuna Wabunge wanawananga wapinzani ambao hawapo bungeni kuwa wanakawiza maendeleo.

Kazi ni Kudemka tu
 
Spika wa Bunge Job Ndugai amemuagiza Katibu wa wabunge wa CCM Jasson Rweikiza kuitisha kikao cha kamati ya wabunge wa CCM (party caucus) kwasababu ndio mahali wanaweza kudhibitiana..
Kumbe midemko bado yaendelea?
 
Karma ya kuchezea haki za watu lazima iendelee kuwatafuna. Imeanzia kwa stering itafika mpaka kwa mwenyekiti wa kitongoji. Hakuna atakaye pona. Suluhisho ya hato yote ni kuhitisha uchaguzi uwe huru na haki,hata kama CCM watashinda nafasi zote gattakuwa na tatizo sisi wapenda haki kwa sababu tutaona tumeshindwa kihalali.
 
Asipojirekebisha na kutubu hatà yeye (Ndugai) atakufa kama alivyokufa mwenzake kama suluhu ya matatizo ya nchi hii...
 
His legacy will be forever there, ndio tatizo hapo.
Legacy haina tatizo lolote, tatizo ni waliopo kunufaisha matumbo kwa kisingizio cha legacy.
Kuna mwizi huko saa hii anaimba wimbo wa legacy ili CAG asichunguze wizi wake na kuuweka wazi.
 
1 Nchi yote ilikuwa na lugha moja na usemi mmoja.
Mwanzo 11:1

2 Ikawa watu waliposafiri pande za mashariki waliona nchi tambarare katika nchi ya Shinari; wakakaa huko.
Mwanzo 11:2

3 Wakaambiana, Haya, na tufanye matofali tukayachome moto. Walikuwa na matofali badala ya mawe, na lami badala ya chokaa.
Mwanzo 11:3

4 Wakasema, Haya, na tujijengee mji, na mnara, na kilele chake kifike mbinguni, tujifanyie jina; ili tusipate kutawanyika usoni pa nchi yote.
Mwanzo 11:4

5 Bwana akashuka ili auone mji na mnara waliokuwa wakiujenga wanadamu.
Mwanzo 11:5

6 Bwana akasema, Tazama, watu hawa ni taifa moja, na lugha yao ni moja; na haya ndiyo wanayoanza kuyafanya, wala sasa hawatazuiliwa neno wanalokusudia kulifanya.
Mwanzo 11:6

7 Haya, na tushuke huko, tuwachafulie usemi wao ili wasisikilizane maneno wao kwa wao.
Mwanzo 11:7

8 Basi Bwana akawatawanya kutoka huko waende usoni pa nchi yote; wakaacha kuujenga ule mji.
Mwanzo 11:8
 
Well advanced "UNAFIK" uliopindukia! = "UZANDIK"

"Haya tuangalie wanavyotafunana..." Wenyewe kwa Wenyewe!
 
MHE SPIKA JOB NDUGAI AWATOLEA UVIVU WABUNGE WA CCM.

Na Elius Ndabila
0768239284

Ieleweke kuwa Bunge lililopita minyukani ilikuwa ni ya Wabunge wa CCM vs Wabunge wa Upinzani. Bunge hili halina Wabunge wengi wa Upinzani hivyo kuna dalili Wabunge wa CCM wameanza kunyukana wenyewe kwa wenyewe. Inawezekana ni phase ya pili ya kujivua gamba.

Jana tr 19/04/2021 wakati Wabunge wakijadili bajeti ya Wizara ya TAMISEMI Ofisi ya Rais iliyowasilishwa na Mhe Ummy Mwalimu (Mb) Waziri, Mhe Spika Jobu Yustin Ndugai alizungunza maneno haya:-

Ninanukuu, "Mimi nitoe ushauri tu kwamba Katibu wa Party caucus ya Wabunge wa CCM, muitishe vikao vya mara kwa mara kama kweli mnaamini kuna makundi miongoni mwenu. Basi mahali mnapoweza mkadhibitiana Wabunge kutoka Chama kimoja wapo si humu kwa Spika. Kwa sababu hapa ni vigumu sana kufanya hivyo. Mahali mnapoweza mkazungumza wazi na mkajibiana na mtuhumiwa akapata nafasi ya kujibu kama yupo ni kwenye caucus.

Sasa Mambo ya kwenye Caucus mkiyahamishia hapa mnatupa ugumu tu wanamna ya kuendesha. Maana kusema ukweli Mimi sijui kundi. Na Bunge hili ni jipya sana, na kundi hilo kundi la nini? Makundi ya nini?

Nahitaji hata Mimi kujua. Hebu yapelekeni kwenye caucus tunaweza tukajifunza kule, kwamba kuna nini?

Mbona Mimi ninaona kama kawaida tu? Yaani what is there? What is the objectives? Kama mtu, ana lengo gani? Kuna nini yaani? Sana sana mtu mmoja akisimama ana zoza kivyake. Tunawajua. Sasa mtu mmoja akizoza haiwezi kujulishwa kuwa ni shughuli ya Bunge. Lakini kama yapo, Basi hayo ni ya akina Lwekiza na Shangazi ila ni hivyo vikao.

Siku ya Jpili ita kikao saa tano asubuhi, ndivyo tulivyokuwa tunafanya zamani. Watu wanapigana mpaka saa kumi na mbili jioni. Mnasemana weeeee.....yanaisha. Kesho yake ikiwa Bunge tunafanya kazi ya bunge, makundi makundi unayaacha huko huko huko kwa sababu katika hali ya Siasa makundi si kitu cha ajabu. Ni kitu cha kawaida. Siasa ni makundi. Lakini ilimradi hayaleti sumu inayotufanya tusiende vizuri". Ndugai

Mhe Ndugai aliendelea kusema kwamba, " Na katika mazingira ya sasa Bunge hili ni salama kabisa. Mimi sijaona kama tumefika mahali ambapo tunayumba sana. Lakini kama hiyo Hali ipo wenzangu mnaiona basi kwenye caucus. Mkihamishia hapa Mambo ya caucus tunachanganya madawa. Ahasante sana" Jobu Ndugai Spika wa Bunge.

Haya ndiyo maneno ya Spika ya jana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…