Sasa ni dhahiri Bungeni kuna kundi la Rais Samia na kundi la Hayati Magufuli. Spika Ndugai awataka wabunge wa CCM kuitisha kikao cha usuluhishi

Mbunge wa viti Maalum Lucy Mayenga amedai leo Bungeni kuwa kuna kundi la wabunge wengi ambao wanamepanga kuhujumu legacy ya Magufuli na kutaka kutenganisha Urais wa Samia na urais wa Magufuli

Amedai wabunge hao wanamsifia Samia Suluhu kwa lengo la kuonyesha kuwa Maguuli alikuwa akifanya vibaya na tangu awali wanafahamika kuwa walikuwa wakimpinga Magufuli.
Ameongezea watu hao kuwa wanamchonganisha Samia na watu wa Magufuli ambao alikuwa amewapanga na mikakati yao wanaijua

Zaidi unaweza kumsikiliza hapa

Huyu KADEMKA kwa kinyume chake jamani !!!

Leo nimekutana na kijana mmoja hivi mitaa ya Surrender Bridge ana ubao umendikwa kwa chaki

Inaonekana kuna kundi linalazimisha LEGACY ya marehemu ambayo ni mbaya tu hata iweje haitengenezeki ...

1. WASIOJULIKANA
2. UBAGUZI WA KISIASA
3. UNUNUZI WA WAPINZANI (MADIWANI & WABUNGE KWA FEDHA ZA WALIPA KODI)
4. UKABILA
5. UNUNUZI WA NDEGE KWA CASH
6. UCHUMI WA KATI BILA YA AJIRA
7. UPORAJI WA PESA ZA WATU (BUREAU DE CHANGE)
8. UBAMBIKIAJI KESI
9. UUWAJI (KUPIGWA RISASI LISSU)
10. MIAKA MI'5 BILA YA AJIRA

11 ... to name the less jamani ni mengi jamani LEGACY haitengenezeki tena nimengi mabaya kuliko mazuri
 
Kwa hilo Mkuu utaipenda JF ila nasikitika sana Zitto michango yake mingi humu alitaka ifutwe kwa kuwa hakupenda iendelee kuwa humu na uongozi wa JF ukamkubalia na kufuta michango hiyo.
Mtu akichagua usaliti hatuna cha kumfanya .
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Hizo alama alizoacha ni zipi, keshaenda zake na akili na roho havipo tena.
Ameacha alama ya umaskini, visasi, wivu, ukabila na udini sasa mnataka tuvienzi hivi?
Spika wa Bunge Job Ndugai amemuagiza Katibu wa wabunge wa CCM Jasson Rweikiza kuitisha kikao cha kamati ya wabunge wa CCM (party caucus) kwasababu ndio mahali wanaweza kudhibitiana.

Ndugai ameyasema hayo leo Jumatatu baada ya Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Lucy Mayenga kudai kuwa kuna kundi la wabunge wa chama hicho ambalo linamsifia Rais Samia Suluhu Hassan kwa lengo la kudhoofisha alama zilizoachwa na Hayati Rais John Magufuli.
 
Najiuliza hao group ya Magufuli wanakuwa wanataka nini kwa sasa???? Maana mtu wao sio tu kwamba hayupo serikalini bali ameshafariki sasa wanachotaka nini?

Nachokiona hao wanaojiita Magufuli group itakuwa wanataka kutumia jina kwa manufaa yao maana wamegundua they are about to become irrelevant kabisa sasa the only way to survive ni kujifanya wanatetea mtu ambaye hayupo 🤷🤷🤷🤷
 
Mkuu wewe ulikuwa hujalijua hilo? Mbona thread nyingi tu hapa zinazungumzia hilo jambo?
Upande mmoja kuna msoga gang, kundi linaloongozwa na jk na wafuasi wake (january, nape, riziwani, nk) ambao wanafanya jitihada za nguvu kumtenganisha samia kutoka kwenye awamu ya 5 na hatimaye kuifuta legacy ya Mwendazake.

Hili ni kundi la watu waliokuwa na ulaji kwenye awamu ya 4, iwe kwa vyeo, biashara halali na haramu (vituo vya mafuta, unga, pembe za ndovu, nk) lakini walipigwa chini na mwendazake.

Kundi la pili ni la wale wanaoenda na mass ya watanzania na kusema 'haifutwi legacy ya mtu hapa', wako tayari kuitetea na kuilinda legacy ya awamu ya 5 kwa nguvu zote.

Mipashano imehamia bungeni sasa!
 
Kila kilichokuja kiharamu kitaondoka.Ni suala la muda tu.Sioni mama akifika mbali na hili bunge la ajabu!Na linajimaliza lenyewe,na iwe hivyo haraka iwezekanavyo ili wasitucheleweshe kufanya reforms za msingi kwenye nchi yetu.Hatuna mda wa kukimbizana kidali po na watoto.Waende nje wakamalizie michezo yao kwanza.
Nenda kamwage sumu ili wafe wote, roho yako ifurahi zaidi. Maana unakiu ya damu.
 
Spika wa Bunge Job Ndugai amemuagiza Katibu wa wabunge wa CCM Jasson Rweikiza kuitisha kikao cha kamati ya wabunge wa CCM (party caucus) kwasababu ndio mahali wanaweza kudhibitiana...
Hawa wabunge kweli ni viti maaluma.legacy haitetewi.magufuri pro someni kitabu cha WHO WILL CRY WHEN YOU DIE then muone kwanini kuna Hii sintofahamu bungeni.
 
Back
Top Bottom