Sasa ni dhahiri Bungeni kuna kundi la Rais Samia na kundi la Hayati Magufuli. Spika Ndugai awataka wabunge wa CCM kuitisha kikao cha usuluhishi

Sasa hivi CCM haina kwa kufichia matatizo yao... wabunge wa upinzani walikuwa wanafichia Sana udhaifu wao.

Wangeweza kuwaanzishia zogo wabunge wa upinzani, halafu Spika angemtoa nje Lema ama kumfungia vikao hapohapo upepo ungebadikika.
 
Sasa hivi CCM haina kwa kufichia matatizo yao... wabunge wa upinzani walikuwa wanafichia Sana udhaifu wao.

Wangeweza kuwaanzishia zogo wabunge wa upinzani, halafu Spika angemtoa nje Lema ama kumfungia vikao hapohapo upepo ungebadikika.
nawaangalia nani watamtupia matatizo yao sasa hiv
 
Baba amekufa!
Nyumba na urithi kaachiwa bi mdogo tena kutoka mbali!
Wakimalizana na upinzani watapingana wao kwa wao. Ukiona watu wawili wanapata kwa kila kitu ujue mmoja anafikiri na mwingine amepumzisha akili yake. Hutegemei wabunge wote wafikiri kwa namna moja muda wote. Shida inakuja pale unapopambanisha mwendazake na aliyeachiwa kijiti.
 
Ina maana hao wabunge hawakuelewa jana alivyosema yeye na Magufuli ni kitu kimoja? wana vichwa vizito sana.

Hii inathibitisha Ndugai ni kiongozi dhaifu wa bunge, ameshindwa kurekebisha hali kwasababu nae anaingia kwenye kundi mojawapo kati ya hayo, dawa ni kulivunja hilo bunge tu.

Wazo mjarabu.
Kweli kabisa ni afadhali Mama avunjilie mbali Bunge hili maana LIKO KIMASLAHI ZAIDI na halina tija yoyote kwa Taifa!!
 
Sumu aliyoieneza hayati bado inalitafuna bunge dhaifu yaan mtu kafa lakini masalia ya sumu bado yapo. Chamsingi mama samia kesho avunje bunge kuepuka yeye kupinduliwa na hili bunge dhaifu
 
Nenda kamwage sumu ili wafe wote, roho yako ifurahi zaidi. Maana unakiu ya damu.
Ya nini kujichumia dhambi wakati wanajimaliza wenyewe kiuongozi na kisiasa!

Nina kiu ya kuona taifa limejaa haki,maarifa,hekima na ustawi,sio kuleta utoto bungeni wakati nchi imejaa changamoto nyingi za kuzungumzia.

Sina kiu ya damu.Mimi mtanzania haswa sijazoea mambo unayosema na hapa umetaja damu tu nasisimka maana sijazoea kuona damu na sitaki mazoea nayo kabisa na hata watu wa aina yako wanaopenda kuzungumzia damu..damu.. nawaogopa.Tafadhali usinizoeshe kuzungumzia umwagaji damu..kama umezoea aina hiyo ya mazungumzo basi yaweke mbali na mimi na huu mtandao wetu watanzania hatujazoea aina hiyo ya mazungumzo please!Jinsi nilivyolielezea hili la damu kwa kirefu ikuonyeshe how you irritated me!Acha kuzungumzia damu,na hiyo roho ikutoke kwa jina la Yesu!msss!😡
 
Back
Top Bottom