Sasa ni dhahiri Bungeni kuna kundi la Rais Samia na kundi la Hayati Magufuli. Spika Ndugai awataka wabunge wa CCM kuitisha kikao cha usuluhishi

Johnny Sack

JF-Expert Member
Jan 21, 2017
8,779
18,746
Mbunge wa viti Maalum Lucy Mayenga amedai leo Bungeni kuwa kuna kundi la wabunge wengi ambao wanamepanga kuhujumu legacy ya Magufuli na kutaka kutenganisha Urais wa Samia na Urais wa Magufuli

Amedai wabunge hao wanamsifia Samia Suluhu kwa lengo la kuonyesha kuwa Maguuli alikuwa akifanya vibaya na tangu awali wanafahamika kuwa walikuwa wakimpinga Magufuli.

Ameongezea watu hao kuwa wanamchonganisha Samia na watu wa Magufuli ambao alikuwa amewapanga na mikakati yao wanaijua

Zaidi unaweza kumsikiliza hapa

 
Spika wa Bunge Job Ndugai amemuagiza Katibu wa wabunge wa CCM Jasson Rweikiza kuitisha kikao cha kamati ya wabunge wa CCM (party caucus) kwasababu ndio mahali wanaweza kudhibitiana.

Ndugai ameyasema hayo leo Jumatatu baada ya Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Lucy Mayenga kudai kuwa kuna kundi la wabunge wa chama hicho ambalo linamsifia Rais Samia Suluhu Hassan kwa lengo la kudhoofisha alama zilizoachwa na Hayati Rais John Magufuli.
 
Wache wafu wazikane wenyewe. Ndo hasara ya bunge lenye maccm tupu. Wangekuwepo Upinzani hapo wala wasingegombana maana kazi ya kumbagaza Magufuli ingekuwa ya wapinzani.
 
 
Tuchape kazi ndugu zangu sisi ni matajiri hii nchi imechezewa sana.

images (7).jpeg
 
Back
Top Bottom