Ridhiwani kaenda Ukerewe?

Ridhiwani kaenda Ukerewe?

Kwa hiyo mnataka kusema kuwa wakerewe toka 1918 wanaiangalia hiyo mali wakati wenyewe masikini?
 
Hawa jamaa si walikuwa na mkutano
attachment.php

You made my day. This is the photo of the week!
 
Kwa hiyo mnataka kusema kuwa wakerewe toka 1918 wanaiangalia hiyo mali wakati wenyewe masikini?

Zakumi,
Waonee huruma Wakerewe ndugu zangu. Sidhani kwamba kama wangekuwa na habari za kuwepo hiyo mali wangeendelea kuzubaa. Nimeshaangalia movie nyingi za treasure hunting unakuta wale hunters ni watu waliopata vidokezo kuwa sehemu fulani kumefichwa kitu. Sasa kama Riz katumia influence ya baba yake kujua kuwa kuna mahali Wajerumani walificha kitu, tusiwalaumu Wakerewe. Lakini kama ni kweli hizo mali zipo, basi zinatakiwa kuwa hazina ya taifa na wa kwanza kufaidika nazo ni Wakerewe. Si Riziwani.
 
Labda kuna MZIGO alitaka kupitisha huko maana siku hizi TRA kwenye vituo vya Namanga, Holili, na Horohoro wamekuwa wakali mno.
 
Mkuu CAMARADERIE, hilo ndilo lile jiwe linaloitwa Nabulebeka?
Hebu tupia na picha ya ule mti ulioangushwa chini kwa misumeno na wapasua mbao, then kesho yake wakaukuta umesimama ilihali matawi yake ya juu yamekatwa na msumeno wao pale mti ulipokuwa chini.
Nasikia pia kuna mti kando ya Ziwa Vicky ambao majani yake yakipukutika yakidondoka na kugusa maji ya Ziwa kila jani linageuka Mamba.
Ukerewe usipime kwa ulozi!
Hilo jiwe linaitwa "Nyabhurebheka" linacheza ndobolo balaa!.
 
Nasikia huko ndiko kunaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya albino.

Hapa ni Ukara penyewe - sehemu ya maombi.

kanisa+la+roma+ukara.JPG




Picha chini ndipo ilipokuwa benki ya watemi wa Ukerewe ambapo walikuwa wanahifadhi mali zao zenye dhamani, vito, fedha, madini na kadhalika

makumbusho+ya+watemi+ukerewe.+(10).JPG


Huu ndio ulikuwa mlango wa kuingilia benki ya watemi. Kama wewe mnene hupiti hapo.

makumbusho+ya+watemi+ukerewe.+(8).JPG


Barazani mwa benki ya watemi

makumbusho+ya+watemi+ukerewe.+(4).JPG


Korido inayotenganisha pango la hifadhi na benki ya watemi

makumbusho+ya+watemi+ukerewe.+(6).JPG



Mzee Mwanakijiji sie tushafika siku nyingi huko na kurudi.

Wakati nyie mnaenda kuunga foleni kwa babu wa Loliondo sie tulikuwa huku.

Mengine naomba nisiyaseme hapa. Tuyaache kama yalivyo.

Wale wanaopenda kutafuniwa kila kitu itakula kwao.
 
Kule Bwana hakuna jengo lolote la Mjerumani, ila kuna sehemu flani hivi kuna muinuko mmoja wa ajabu wakati eneo lote la karibu na hiyo sehemu ni tambarare. Wenyeji wa huko wanasema kuna madini mengi sana chini ya huo mwinuko, hiyo sehemu inaitwa "Kuchala". Labda jamaa yupo katika harakati za upembuzi yakinifu kutaka kujua uhalisi wa hiyo story!.
 
dogo anafanya remix ya ile hot single ya baba yake alokuwa mtalii wa kwanza na mwisho duniani kwenda kuona alama ya unyayo wa mtu wa kale loliondo, lakini alivyotoka huko ndo babu wa loliondo akaibuka, tusubiri hii ya ukerewe itakuwaje.
 
EMT wewe ni chiboko....una picha za mapango yote ya huko, he he he!.

Nishafika huko na ushuhuda wangu huu hapa. lol.

nyaburebeka.JPG


na Jovither Kaijage, Ukerewe



MKUU wa Mkoa wa Mwanza, Abbas Kandoro, ameshangazwa na kushitushwa na jiwe la ajabu lililopo katika Kijiji cha Nyamanga katika Kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe, linaloimbiwa na kucheza na kuahidi kulitangaza ili liweze kuchangia pato la taifa.
Ahadi hiyo aliitoa juzi baada ya kutembelea jiwe hilo vikiwemo vivutio kadhaa vya utalii vilivyopo katika Wilaya ya Ukerewe ambapo pia aliziagiza halmashauri za wilaya mkoani humo kutambua na kutunza vivutio hivyo kwa faida ya vizazi vijavyo.
Akiwa eneo la jiwe hilo lililo kando ya Ziwa Victoria, Kandoro alishuhudia jiwe hilo linalokadiriwa kuwa na uzito wa tani 2,000 likiimbiwa na kucheza, kitendo ambacho kilishangaza wengi waliofika kushuhudia maajabu hayo. Mmoja wa wana ukoo wa Rwakatimba wanaotunza mila na desturi ya jiwe hilo, mzee Magesa Makolokolo (90), mbali ya kueleza historia yake pia ndiye mwenye jukumu la kuimbia jiwe hilo licheze. Katika taarifa yake pia aliomba serikali imsaidie gharama za uendeshaji na kutunza mila hiyo, kwa kuwa kila mwaka linafanyiwa tambiko linaloghalimu sh 300,000 na wakati mwingine hushindwa kutimiza sharti hilo kwa kukosa fedha.

Mkuu unapoambiwa kuwa hii nchi ni tajiri usidharau.

Tembelea nchi uuone utajiri wake.

makumbusho+ya+watemi+ukerewe.+(1).JPG


Hapa ni pembezoni mwa himaya ya makumbusho ya watemi wa Ukerewe. Eneo zima halina mlinzi yoyote.

Wako katika taifa lenye "rasilimali za kumwagiruru mpaka kusaza".
 
Mkuu sasa hiyo himaya ya Watemi ipo kisiwa gani ili na sisi tukaitembelee?.
 
Zakumi,
Waonee huruma Wakerewe ndugu zangu. Sidhani kwamba kama wangekuwa na habari za kuwepo hiyo mali wangeendelea kuzubaa. Nimeshaangalia movie nyingi za treasure hunting unakuta wale hunters ni watu waliopata vidokezo kuwa sehemu fulani kumefichwa kitu. Sasa kama Riz katumia influence ya baba yake kujua kuwa kuna mahali Wajerumani walificha kitu, tusiwalaumu Wakerewe. Lakini kama ni kweli hizo mali zipo, basi zinatakiwa kuwa hazina ya taifa na wa kwanza kufaidika nazo ni Wakerewe. Si Riziwani.

Sina huruma na watu wanaokalia uchumi na wazembe.
 
Mkuu sasa hiyo himaya ya Watemi ipo kisiwa gani ili na sisi tukaitembelee?.

duh ndugu kuna kaharufu kama na wewe unataka geuka treasure hunter.Naona uanuliza kama vile mwanamume anapojaribu muuliza binti mrembo alivyobakwa,huku akitaka pata details zote huku akioyeshwa kila kitu.

Ukitaka jua kuna kitu waangalie wajerumani wanaokuja, wape escort, anyalyse maswali yao, na jinsi gani wana jiweka mbali na historia yao huku wakijifanya kuwa wanataka juwa african something, angalia vitabu wanavyoungua bila kuwashtua,kwani wakiona kuwa ni mjana san anao watakuwa wakificha reference zao wanapopajua, jaribu wauliza kam wana interest ya kuwekeza maeneo fulani ya sehemu walizo too curious.Then ujue kuna sehemu wameficha mzigo.Ila ukiona tofauti ujue kuwa ni historia tuu.Hawa jamaa wana documentation zote kule kwao, ila kwa sasa wanpata shida kidogo wanapojitahidi update info kwa GPS.Kwa vile maeneo mengi wabongo wameyavuruga sana.

Ukienda kichwkichwa utajikuta unafumua mahandaki ya mabomu, waliyoficha wajerumani kabla ya kuchapwa na muingereza.Dogo aombe mUngu asijikute ktk handaki lililotoswa.
 
Back
Top Bottom