Eeeeeeeeeehee life is full of surprise!!!
Haya mambo MMK kwa tabia yetu watanzania yanaonekana ya kipuuzi sana,lakini kwa hao anayoyaona ni ya kipuuzi basi ufahamu wao ni mdogo sana.Yaweza kuwa jambo hili ni tetesi lakin pia tetesi hizo zikawa ndio au hapana.
Binafsi najua hizi simulizi,ambazo binafsi nimeshakutanazo nikiwa na miaka kumin na nne, lakini si ukelewe, ila ninapo unga dot najalibu kuimagine kuwaona gold and treasurer hunters wakimfuata mtoto wa Mkuu wa Nchi nakumlisha maneno matamu,kisha nae katika umri huo ambao yeye binafsi alipaswa kupima kuyatenda ama kuyatenda.Kwa kuwa kwa yeye kuyatenda na ikafahamika kuwa alishiriki kwenye hisia hizo basi hato angaliwa yeye kama Riz bali ataangaliwa yeye kama Mtoto wa Rais aliyeko Madarakani.
Na kwa picha hiyo na kwa tendo hilo,hisia hizo ambazo, upelekwa kwenye tresuary hiyo ni utajiri mkubwa usio na matumizi ya nguvu, bali matumizi ya imani [Spirtul] zaidi, kwa hazina ambayo yasemekana kuwa ipo [Binafsi sikulazimishi mchangiaji kuamini lakini mimi naamini uwepo wa vitu vya aina hiyo kwani si muda mlefu uliopita dunia ililipuka kwa taarifa ya kupatikana kwa New World Tresure kutoka
Spanish Colonial coins hivyo haya mambo yapo].
Binafsi nilifikwa na incident nikiwa mdogo miaka kumi na nne, watu wazima wakatamanishwa habari hizo kuwa ikipatikanika rupia ya zamani, ambayo mimi binafsi sijawai iona,basi watu wazima wale watakuwa matajiri.Basi watu wazima wale ikimuhusisha mama mmoja mkubwa wa familia yangu wakakumbushana kuwa wakiwa wadogo kijijini kwao walipata kuiona fedha ya namna hiyo kwa baba yao aliyepigana vita vya wajerumani. Watu wazima wakathibitishiana kuwa wanajua alipokuwa anaiweka karibu na kiko chake kipendwa kwenye moja ya nyumba aliyokuwa anapenda kuvutia.Kwa wengi wetu mnatambua nyumba nyingi za vijiji vyetu ni za udongo.Babu yangu huyo alikufa mwaka 1974, mimi nimekuja kubebwa kwenda tukio husika kuchukua mzigo nikiwa na mika kumi na nne 14 mwaka 1989.Da uwezi amini waliokuwa wametoka kijijini mwa babu yangu na kuthibitisha kuwa nyumba aliyokuwa anatumia babu yangu huyo kumpumzika na kuvuta kiko chake, walithibitisha kuwa Nyumba hiyo hipo, na wa kuweza kuichukua ni mtu kama mimi.
Basi wakubwa wale wakanibeba mzega mzega ukizingatia utoto unafuata wakubwa wanachokutuma, mimi binafsi nakumbuka raha yangu kubwa ni kusafiri kwamba kuwa naenda rikizo nje ya nyumbani, tena kijijini ambako nina nasaba nako,raha ya utoto kuwa nikiludi nyumbani nina jipya la kuhadithia huko story za matembezi yangu hayo!!.Kwa nilichokishuhudia kwa umri wangu ule wa miaka 14, ile siku tunafika kijinini nakumbuka tuliingia usiku, asubuhi napelekwa eneo la tukio natamalaki kuona wakubwa wanashangaa nyumba yote iko chini na vifaa vyote vilivyokuwemo watu walishasawazisha baada ya mvua kali iliyokuwa imemwagika siku mbili zilizopita kuidodonsha nyumba iliyoacha na babu kama sehemu yake ya kupumzikia toka mwaka 1974 sijazaliwa mpaka natayarishwa kuwa nitasafiri kwenda kijijini Nyumba ilikuwepo, ila kwa siku tatu za kusafiri toka nilikokuwa mpaka kufika kijijini zingatia usafiri wa miaka ile nyumba hiyo ilidondoka na Rupia sikuiona, wala kiko chake,ila kwangu sikuwa na habari zaidi ya kuwaza furaha yangu kuwa niko likizo kijijini.
Kwa watu wazima ilikuwa imekula kwao na ndoto za utajiri zikawa ndio,zimeyeyuka na waliingia hasara ikiwemo wao kusafiri,ila labda ilikuwa wanipeleke mimi kwenda kuona nyumba ya babu yangu, namuita rafiki ambae sikupata kumuona ikidondoka.
MMK nimeadithia haya kwako ili kuunganisha dot,kuwa kama tukio hili ni kweli basi Ritz nae kwa kujua ndiye mtoto ambae kwa sasa Baba yake anazamana ya kusimamia mali ya Watanzania ,hivyo kushirikishwa yeye, ama kwa kujua ukilinganisha na umri wake kuwa mtu mzima, au kwa kutokujua maisha ya kisasa zaidi, basi matamanio ya kuibuka na hazina [Treasure] isiyokuwa na matumizi ya nguvu basi.
Haya mambo mwanakijiji yapo,ila binafsi yanawafikia na kuwatokea wale ambao hawana kabisa kusudio la UTAJIRI kama SIFA, bali wapate hazina hiyo itumike kwa lengo kusudio la MANUFAA YA JAMII.Na ndio maana wale ambao wanazitaka kwa kusudio la SIFA uishi kuaambiwa masharti kibao,ikiwemo yale yenye harufu ya tishio la uhai wa binadamu mwenzie.
Na kwa ujumla mambo hayo bila nafasi za wazee wa Jadi, simaanishi waganga wa kienyeji, nazungumzia wale ambao wanadhamana za kijadi za eneo husika wao ndio kuanzisha mada kwa mujibu wa initution zao ,na si mtu nje ya eneo husika kuja kuanzisha mada kuwa wanataka kitu fulani na kweli wakafanikiwa.Na waha wajerumani kweli waliacha mark nyingi sana za hazina walizokwapua toka kwenye ardhi za mababu na kwa kuwa ardhi za mababu hazikutaka waondoke nazo waliishia kuondoka patupu wakiwa na ramani za Milima , miti mikubwa, mito na vijito, mawe n.k kama ishara ya hazina hizo.
Yawezakuwa alirubuniwa kutumika au la ni rumors za mijini!!! Yapo na yanatokea.