Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua Nyumbani

UMUGHAKA

JF-Expert Member
Sep 1, 2021
2,217
10,989
Nisikuchoshe na usinichoshe, tusichoshane!

Kwenye haya maisha kuna wakati huwa ninakaa chini na kusema "Kama sikufa kipindi kile,basi siwezi kufa mpaka Mungu atakaporuhusu"

Nadhani wengi mtakumbuka ni siku chache tu zimepita nimeandika kisa cha maisha ambayo nilikutana nayo wakati nikiwa nimekwenda kumsalimia baba yangu mdogo akiwa ni Headmaster huko Tabora Tulichomfanya yule mchawi hatakuja kusahau kamwe maisha yale yalikuwa ya kawaida ila washirikina walifanya tukakosa amani.Sasa baada ya hapo nilifaulu vizuri tu kuelekea shule ya upili(advance)na nikapangiwa huko Tanga kwa mchepuo wa Sayansi wenye combination PCB.

Hali yangu ya maisha ya shule kiukweli ilikuwa mbaya sana mpaka nikajuta kwanini nilichukua hiyo combination, siyo kwamba sikuwa na akili, la hasha!, akili ilikuwepo ya kutosha kwasababu nilifaulu kwenda advance kwa divisheni 2, ni combination iliyohitaji kupiga msuli kana kwamba umetumwa na kijiji, haikutaka mchezo wala kujisahau hata kidogo,sasa mimi nilipofika huko nikajikuta naungana na makundi na kujanjaruka kuwashinda hata niliyowakuta!.

Mkurya mimi kutoka wilayani Tarime kijiji cha Mogabiri nikajikuta nazamia kwenye dimbwi la mapenzi ya mtoto wa kitanga ambaye alifanya hata kusoma nikaacha nikawa namuwaza yeye na utamu wa papuchi yake!.

(Shamima popote ulipo ulaaniwe mbwa wewe kwa kuniharibia maisha). All in all ni kwamba napambana na maisha yanasonga japo ni kibishi!. Sasa haya ya kwanini nilifeli nadhani kwa leo si mahala pake,nitawaeleza tu kilichofuata baada ya mimi kufeli shule!.

Kiasili mimi ni mkurya kutokea wilaya ya Tarime huko kijijini Mogabiri,ingawa hatukuishi sana hapo kijijini lakini ndipo chimbuko letu lilipo hapo, kwa pale Tarime mjini nyumbani kwetu ni Rebu.Pia tunao ndugu wengi tu waliotapakaa karibu kila kona ya hii nchi!, hapa Dar es salaam wamejaa ila wanajifanya kama hawanioni vile! (Maisha ya sikuhizi yamekuwa yakipumbavu sana).Kwakuwa wanajifanya kukausha na mimi pia napiga mikausho ya hatari!,sitaki kumgasi mtu!.

Basi bana, nakumbuka ile nimemaliza skonga nikawa nashangaa shangaa pale nyumbani kusubiri tokeo la kuelekea chuo, sasa nilifahamu kabisa siwezi kufaulu kwa kile nilichokifanya kule skonga, Mzee yeye aliamini toto lake limemaliza shule na anajivunia kwasababu nilikuwa nina akili,hakuelewa kabisa kwamba baada ya kufika shule nilijanjaruka kuwazidi hata niliowakuta!. Baada ya matokeo kutoka na ikaonekana nimepata divesheni zero, mimi kwa upande wangu sikushituka ila Mzee alihamaki sana na kushangaa nilipatwa na nini hadi nifeli!.

Tangu nimeanza darasa la kwanza hadi darasa la saba, sikuwahi kuvuka namba 5,ingawaje sikuwahi kuwa namba 1 lakini nilikuwa nacheza kwenye namba 2-4. Nilipofika form 1 hadi form 4 wembe ukawa uleule! nashika namba 3 -5,sasa hadi nafaulu kuingia advance Mzee wangu hakushangaa maana alifahamu kabisa toto lake nilikuwa nina akili!

Mzee wangu kiukweli alikuwa mkali mno na ilikuwa ikitokea nimefanya kosa akanikamata, kiukweli nilikuwaga naimba Haleluya!.Yeye alikuwaga achapi kwa fimbo za miti ya kawaida,bali alikuwa anachapa kwa nyaya ya umeme! Aisee usiombe kukutwa!

Kuna muda nilikuwa nikifahamu nimefanya kosa siku hiyo najiwahisha kuoga na kuingia kulala na kujifanya naumwa! Sasa akija akikushika shingoni kama anakupima joto akakuta huna joto,aisee utaomba ardhi ipasuke ikumeze ili ikuepushe na kipigo kisichokuua ila chenye kukufanya ukajuta kwanini ulizaliwa!.

Kutokana na kutokuridhika kwa mzee na yale matokeo, kuna siku kadhaa sikumuona pale nyumbani nikajua uenda atakuwa kwenye mambo yake, sasa kumbe mzee amesafiri hadi Tanga kwenda kuonana na Headmaster kufahamu mwanae ni kwanini nimefeli kiasi kile na wenzangu kufaulu!

Alichoamini mzee ni kwamba sikustahili kufeli na nilipaswa nifaulu!. Ule mpango wa yeye kwenda Tanga kumbe hadi Maza nae alikuwa akifahamu ila aliamua kula buyu ili ukweli ufahamike! Mama yangu alikuwa rafiki yangu mkubwa sana na yeye peke yake ndiye shida zangu zote nilikuwaga nikimwambia!.Ila safari hii na yeye aliukaza uso wake na hakutaka kabisa kucheka na kima!

Mwanaume niliendelea kujinafasi na kujimwayamwaya kwa kipindi kile kifupi ambacho mzee hakuwepo nikiamini atakuwa ameenda kwenye shughuli zake, akili yangu iliamini kwasababu mzee wangu alikuwa akinimini basi angenipatia mtaji ili nianze biashara!.

Baada ya kama siku 5 mzee alirejea, sasa tukiwa tunapata chakula usiku alikuwa akiniangalia kwa jazba sana, sikuwa na tatizo nae kwasababu niliamini yeye kuwaga na hasira za karibu ndiyo ilikuwa kawaida yake!. Sasa ile naendelea kula sijui ili wala lile,nilishitukia amenipiga kofi ambalo lilifanya kuanza kuona maluweluwe!.

Mama "Tatigha omwana araghere!"(Muache mtoto ale)

Mzee "Amos hebu niletee waya hapo chumbani"

Sasa mdogo wangu aitwaye Amos akaagizwa waya akachukue waya ili viboko vichukue nafasi!.

Mzee "Leo nakuua mbwa wewe"

Kiukweli siku hiyo nilijua kabisa nakufa maana mzee wangu alikuwaga hana masikhara kabisa na maneno yake! Basi mama alikuwa akijaribu kumtuliza mzee lakini bado ikashindikana, kwa wakati huo sikuelewa kabisa ni kitu gani kilimsibu mzee wangu ambaye alikuwa amerejea kutoka huko alikokuwa ameenda!

Mzee alinyanyuka akatoka akaenda ndani ambako sikufahamu alikwenda kufanya nini,wakati huo kiukweli hata chakula sikuwa na hamu nacho tena kwasababu mabanzi na makwenzi niliyokuwa nimechezea yaliniharibia mudi kabisa!.Baada ya mzee kutoka chumbani alikuja na kamba ya katani akanisogelea akanifunga na kunibana miguu kana kwamba anataka kuchinja kuku.

Sasa akauchukua ule waya uliyoletwa na dogo nikaanza kuchezea stiki! kiukweli nilipigika sana!. Baada ya kuona ameniadhibu vya kutosha alinilaza kifudi fudi wakati huo kanifunga mikono kwa nyuma kama vile jambazi au mwizi amepigwa pingu.

Mzee "Leo nakuua, sali sala yako ya mwisho!"

Aliendelea "Siwezi kuharibu pesa yangu halafu wewe uende shule kuwa mtoro!"

Baada ya kusikia ile kauli basi nikajiongeza kiakili na nikafahamu kabisa atakuwa alikwenda shuleni kuutafuta ukweli wa mimi kufeli!.Kiukweli nilikiona kifo kiko karibu yangu!.

Mzee "Yaani nakulipia karo wewe unaenda kuvuta bangi shule?"

Aliendelea "Hizo bangi ulianza kuvuta lini?"

Sasa nikaanza kushangaa ni nani alimwambia nilikuwa navuta bangi? Kiukweli kitu ambacho sikuwahi kukifanya kwenye maisha yangu ni huo uvutaji wa bangi alionieleza!.

Mimi "Hapana baba sivuti bangi!"

Mzee "Leo utanitambua mshenzi wewe"

Kiukweli kujitetea ilikuwa ngumu sana maana kila nilipojaribu kujitetea nilionekana muongo na kuishia kukandamizwa viboko visivyokuwa na idadi!

Sasa kumbe alipokwenda kule shuleni, walimu walimwambia ya kwamba mimi nilijiingiza kwenye kundi la waliokuwa wameshindikana na kuanza kujihusisha na uvutaji wa bangi!walimu pia hawakufahamu hicho hakikuwa chanzo cha mimi kufeli bali ilibidi wamwambie mzee kwasababu ya kuniona mimi kukaa na watu ambao pale shuleni walikuwa wameshindikana!

Na kwa kipindi kile walimu walikuwaga hawaangaiki na mtoto wa mtu,wao walikuwa wakituambia mwisho wa mambo yote ni pepa(mtihani)ndiyo utakaochuja nafaka halisi na magugu!.

Basi bana, baada ya kupigika sana na mzee kunishikia panga, ilibidi maza aingilie kati kwa kujifunga kibwebwe na kumkoromea mzee!.

Mama "Hivi baba Sarah unataka kumuua mtoto kisa kufeli shule!"

Aliendelea "Kama humtaki mtoto muache akatange tange huko!"

Basi baada ya mama kuingilia kati, mzee aliniacha na akanitaka nipotee pale nyumbani na nisije kumtambua kama baba yangu. Mama alinisogelea na kunifungua zile kamba mkononi na miguuni!. Kiukweli nilipigika sana.

Nilitoweka pale sebuleni nikaelekea chumbani kulala huku nikiendelea kulia kwa kwikwi, mwili wangu wakati huo ulikuwa umejaa alama ya nyaya za umeme zilizosababishwa na kile kipigo!

Usiku huo kiukweli sikupata usingizi kabisa kutokana na maumivu ya viboko!-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-SEHEMU YA 2
Kwakuwa mzee alikuwa amesema nisionekane pale nyumbani na nisije kumtambua kama baba yangu,kulipokucha asubuhi alirudia hayo maneno mbele ya mama na akamwambia endapo akirudi akinikuta,basi mimi na mama tutaondoka wote!,kibaya zaidi hakutaka kabisa nikanyage kwa ndugu zake wa hapo Tarime,yaani baba zangu wadogo na mashangazi.Hakukuwa na namna ilibidi nifungashe virago vyangu na kuondoka!.

Mama "Sasa utaenda wapi baba"

Mimi "Nitajua huko huko mbele ya safari"

Kiukweli nilichafukwa sana wakati huo na nilimuona mzee wangu ni mkatili sana kuniadhibu mbele ya dogo!.Nilifahamu kabisa ya kwamba nilitenda kosa na kama ni adhabu nilikuwa tayari nishapewa lakini suala la mzee kunitimua nyumbani niliona kabisa alipofika ilikuwa ni hatua mbaya sana.
Mzee wangu alikuwa mfanyabiashara wa nyumba za kupanga pamoja na nyumba za kulala wageni(Guest houses)za kutosha pale Tarime mjini,ingawaje leo amebaki kukodoa macho tu kama kabanwa na mlango asijue la kufanya baada ya kujiingiza kwenye siasa na kujikuta ana madeni ya kufa mtu na kuanza kuuza moja baada ya nyingine!.Kibaya zaidi siasa zenyewe bora angekuwa chama tawala wangemlinda,yeye aliamua kuwa upande wa pili!.

Mama "Uende kwa mama yako mkubwa"

Aliendelea "Hebu shika hii"

Basi mama akanipatia shilingi elfu 5 ya kitanzania na kunitaka niifanye kama nauli ya kunitoa hapo Tarime mjini kuelekea kijiji cha Gamasara alipokuwa akikaa mama yangu mkubwa!.Niliipokea ile hela nikaikunja na kuitumbukiza kwenye mfuko wa suruali.Kwakuwa nilikuwa sina pa kwenda,ilibidi niondoke tu hivyo hivyo kishingo upande kuelekea kwa mama yangu mkubwa.

Baada ya kufika stendi nilikamata hiace iliyokuwa ikipakia abiria wa Musoma na nikampa konda shilingi 1500 nikamwambia nashukia kijiji cha Gamasara.Mama aliniambia nikifika kwa dada yake nisiwaambie kilichotokea,aliniambia endapo mama yangu mkubwa akiniuliza basi nimwambie tu nilienda kuwasalimu kwa muda wakati huo yeye huku nyumbani akiendelea kumshawishi mzee ili nirudi kuishi nyumbani na ikiwezekana anipatie pesa ya mtaji niweze kufanya biashara.

Basi ile Hiace baada ya kujaza abiria kadhaa ikawa kama inaondoka huku konda akiendelea kuita abiria,sasa ilipokuwa ikifika umbali kadhaa inageuka tena inarudi stendi taratibu huku konda akiendelea kupiga kelele akiita abiria!.Kile kitendo kilikuwa kinawachukiza abiria wengi kwasababu ilionekana kama usumbufu na upotevu wa Muda.Yaani ilikuwa inatoka na kutembea hata umbali wa Km 1 halafu inageuka tena,sasa kile kitendo kilifanyika mpaka abiria walipolijaza lile gari.Abiria wengi walichukia lakini hakukuwa na lakufanya!.

Baada ya mwendo mrefu kidogo,hatimaye ile gari ikasimama pale senta kando ya barabara ya kijiji cha Gamasara na mwanaume nikashuka.Sikutaka kushangaa na kupoteza muda,nikaondoka mdogo mdogo kuelekea kwa mama yangu mkubwa.

Ma'mkubwa "Eeenh mwanangu umekuwa mkubwa!"

Mama mkubwa baada ya kuniona alifurahi sana,alichukua begi langu akawa ameliingiza ndani.Mama yangu mkubwa kwa wakati huo alikuwa na mabinti wawili na kijana wake mmoja ambao alikuwa akiishi nao hapo,mabinti zake wawili wakubwa walikuwa na miji yao tayari,mmoja alikuwa ameolewa Mwanza na mwingine alikuwa hapo hapo Tarime mjini.

Basi baada ya kukaa kwenye kiti nililetewa Togwa na viazi nikaanza kupooza njaa.Kiukweli ulikuwa ukiniangalia ni lazima ungejua kulikuwa kuna shida,nilijikaza na kutabasamu kishingo upande lakini moyo wangu ulikuwa ukiniuma sana!.

Ma'mkubwa "Mama yako mzima mwanangu"

Mimi "Yeye mzima,anawasalimia tu"

Ma'mkubwa "Hata hivyo ni siku nyingi sijaenda"

Aliendelea "Ulishamaliza shule?"

Mimi "Nilimaliza mbona muda tu mama,ila matokeo hayakuwa mazuri"

Ma'mkubwa "Kwahiyo utaenda chuo?"

Mimi "Hapana mama labda nirudie shule"

Ma'mkubwa "Bora umwambie baba yako akupe hela ufanye biashara ya kukodisha punda"

Mimi "Kukodisha punda tena!"

Ma'mkubwa "Eeeh mbona mwenzio Matiko amefanya na tayari amenunua gari yake"

Mimi "Matiko?,Matiko yupi?"

Ma'mkubwa "Ina maana humfahamu Matiko wa mjomba wako Wegesa?"

Mimi "Mimi watoto wa mjomba Wegesa ninao wafahamu ni wawili tu,huyo Matiko sijawahi kumuona"

Ma'mkubwa "Eeee ni kweli mwanangu,hata hivyo nyie mlikuwa bado wadogo"

Sasa mama yangu huyu alikuwa ni mtu wa stori nyingi mno,yaani atakupigisha stori za watu ndani ya ukoo ambao hata wengine sikuwahi kuwaona wala kuwafahamu,sasa kwenye maelezo yake alitaka mzee anipatie hela ninunue punda niwe nawakodisha kwa watu kwa ajili ya kubeba mizigo pamoja na kulimia,aliniambia ile biashara ilikuwa ikilipa sana kwa wakati huo.Sikutaka kumkatisha maongezi yake ikaonekana nina dharau,hiyo biashara ya punda kiukweli haikuniingia akilini kabisa,kwakuwa alikuwa ni mama niliamua kumsikiliza tu.Mpaka wakati huo hakufahamu kabisa ya kwamba kule nyumbani nilikuwa nimetimuliwa na baba yangu!.

Maisha ya pale kijijini Gamasara yalichukua nafasi na nilianza kuyazoea ingawaje hayakuwa maisha bora kama ilivyokuwa kwa nyumbani kwetu.Mama yangu huyo mkubwa alikuwa na vimbuzi na vikondoo kadhaa ambavyo kila siku niliamka kuwasaidia kuchunga,yule dogo ambaye ni mtoto wa mama yangu mkubwa yeye alikuwa bado akisoma,sasa mara moja moja wikiendi ndiyo tulikuwa tukichunga nae.Niliendelea kuwajibika pale nyumbani ili nionekane mtoto mwema.

Sasa kuna siku nikiwa nawatoa wale mbuzi na kondoo hapo nyumbani ili niwavushe barabara ya lami niwaingize upande wa pili kwa ajili ya malisho,kuna Hiace ilikuwa imesimama ikimshusha abiria na mzigo wake hapo kando ya barabara,sasa nikaona konda akishuka kwa haraka akaelekea nyuma ya ile gari ambako ile buti ya gari ilikuwa imefungwa kwa kukazwa na kamba,wakati jamaa anafungua na kushusha ule mzigo ndipo nikammaki vizuri alikuwa jamaa yangu mmoja ambaye tulikuwa tukiishi nae kule mtaani Rebu.

Mimi "Mtatiro mambo vipi mwanangu!"

Mtatiro "Ahaa mwanangu Umughaka,mambo vipi wewe!"

Mimi "Poa mwanangu za siku"

Mtatiro "Na huku unafanya nini?"

Mimi "Nipo kwa maza mkubwa nimekuja kuwasalimia"

Mtatiro "Nina haraka,naingia MS(Musoma) mara moja,ila nageuka"

Mimi "Haina noma mwanangu"

Basi kwakuwa jamaa alikuwa na haraka,alifunga ile buti na kuikaza tena kwa kamba na kuondoka!.Yule jamaa ni mtu fulani ambae alikuwaga hachagui kazi kabisa,kuna muda unamkuta anaosha magari,kuna muda unaweza kumkuta anapiga debe.Nilitamani kuongea nae sana lakini sikuweza kwakuwa alikuwa na haraka sana.

Basi kuna siku pia ile jioni nikiwa pale senta na yule dogo wa mama yangu mkubwa ile gari aliyokuwa akifanyia kazi Mtatiro ilipita ikiwa inatokeo Musoma na jamaa akawa ameniona na kunipungua mkono huku akianiambia kwa nguvu tungeonana kesho,kwakuwa nilielewa ilikuwa ni lazima ile Hiace ipite pale barabarani mida ya asubuhi kuelekea Musoma na kugeuka mida ya jioni,nilianza kuwa muhudhuriaji mzuri pale barabarani kila inapofika jioni ili nionane na Mtatiro niweze kumuomba na mimi aniunganishie kazi kama yake niweze kupata angalau tupesa twa kuzugia mtaani!.Nilikuwa nimeamua kabisa nitafanya kazi yoyote ili nijipatie kipato halali.

Sasa kuna siku jamaa alipita hiyo mida ya asubuhi akawa amenifanyia ishara ya kidole kwamba anageuza muda si mrefu,sikutaka kabisa kucheza mbali,dogo alipotoka shule alikuwa na kawaida ya kunifata mahali nilipokuwa nikiwaangalia wale mbuzi ili tuweze kupiga stori za hapa na pale,sasa alipokuja hiyo mida ya saa 10 alasiri nilimwambia awaangalie wale mbuzi mara moja.Nilitoka nikaelekea kule barabarani maana nilielewa kabisa ile gari ilikuwa ikipita mida ya saa 11 kuelekea saa 12 kurudi Tarime,basi mida hiyo nikawa yale maeneo.Kweli!,mida hiyo ile gari nikawa naiona inakuja na iliponipita kwa mbele ikasimama na ilikuwa ikichukua abiria.

Mtatiro "Twenzetu mwanangu tutageuka kesho"

Basi sikutaka kabisa kupoteza muda nikaikimbilia nikazama ndani!.Hakukuwa na Abiria wengi,siti nyingi zilikuwa tupu!.

Mtatiro "Mwanangu sikuhizi sikuoni kabisa mtaani,kumbe umezamia Gamasara"

Mimi "Nilikuja kumuona Maza mkubwa"

Mtatiro "Mwanangu mshauri mzee wako anunue chuma akukabidhi,siunaona watu wanavyopiga pesa"

Aliendelea "Sema dingi yako ni bahili mno,yule mkurya sijui wa wapi!,aloo!"

Jamaa alikuwa akiongea maneno mengine ambayo niliona kabisa yako serious ingawaje yalikuwa na utani ndani yake,alikuwa akinimbia nimwambie mzee wangu anunue Hiace iingiie barabarani ipige kazi.Wakati huo hakufahamu kabisa mzee wangu alikuwa amenitimua nyumbani!.Basi tulipofika Tarime mjini,ile gari ilipelekwa Car wash kuoshwa,na yeye Mtatiro ndiye aliyekuwa akiendesha baada ya dereva kumkabidhi.Sikutaka kumficha kitu ikabidi nimueleze kila kitu Mtatiro ambacho kilikuwa kinaendelea kati yangu na mzee wangu!.

Mtatiro "Sema mwanangu dingi yako ni mkuda mno!"

Aliendelea "Ila hapa mjini mbona wajanja wengi,wewe ngoja kesho mimi nitakuunga kwa mwanangu mmoja uwe unapiga deiwaka angalau upate hela zako"-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-SEHEMU YA 3


Baada ya ile gari kumalizika kuoshwa tuliondoka kuipeleka nyumbani kwa yule tajiri wa ile gari aliyekuwa akikaa mitaa ya Magamaga.Baada ya kuondoka pale kwa tajiri,Mtatiro akaniambia tuingie gengeni tukapate msosi halafu anipeleke gheto nikapige mbonji na yeye aelekee kulala kwa demu wake.

Basi bana asubuhi kama kawaida akawa amekuja mida ya saa 12 akanigongea nikaamka.

Mtatiro "Vipi mwanangu nikuache ulale au tusepe zetu?"

Mimi "Ngoja ninawe uso tuondoke mwanangu"

Sikutaka kabisa kulala kwasababu jamaa angeniona mzembe.Baada ya kujipaka mafuta tuliondoka na Mtatiro akawa ameelekea kwa bosi wake kuchukua ile gari ili ampelekee dereva ambaye angemkuta pale stendi.

Mtatiro "Ngoja twende kuna jamaa yangu ana kipanya(Probox)kina piga ruti ya Sirari nikaongee nae tuone kama anaweza kukusaidia"

Aliendelea "Siunaweza kukomaa mwanangu?"

Mimi "Nitakomaa mwanangu wala usijali"

Mtatiro "Dingi yako nilikuwa namuona ni mjanja kumbe ana mambo ya kinoko hivyo!"

Mtatiro yeye alichoamini ni kwamba mzee wangu ndiye mzinguaji bila kufahamu yote hayo msababishaji ni mimi.Sikutaka kabisa kumweleza mambo mengi ya nyumbani,nilichomwambia ni kwamba mzee kanitimua nyumbani niende nikajitegemee!.Baada ya kufika pale stendi akamkabidhi dereva gari kisha akamuomba simu ili ampigie yule jamaa yake mwenye kimchomoko aweze kuzungumza nae.

Walipozungumza na huyo jamaa,jamaa alimwambia niende nitamkuta kwenye njia ya Nyamwaga Road amepaki na akawa amemuelekeza namba za gari.Nilitembea kwa haraka ili nimuwahi jamaa.Nilifanikiwa kumkuta jamaa na tukasalimiana.

Jamaa "Mambo vp?"

Mimi "poa kaka"

Jamaa "Sasa tutaondoka nitakuacha pale sirari,wewe utahakikisha unakuwa unanitafutia abiria wa kuja nao Tarime halafu nitakuwa nakupa posho"

Mimi "sawa kaka"

Jamaa "Lakini si utaweza?,maana hii kazi siyo lele mama"

Mimi "Nitaweza kaka wala usijali"

Jamaa "Ningekuweka hapa Town sema kuna wakuda fulani watakusumbua pale kijiweni"

Sikuwahi kabisa kufanya kazi za kwenye magari lakini sikuwa na namna ilibidi nipambane kama mwanaume ili nipate pesa!,nilitaka na mimi niwe kama Mtatiro aliyekuwa mchangamfu na mcheshi asiyejali kitu!.Yule jamaa alikuwa akimiliki gari aina ya Pro box(Kimchomoko) na alitaka mimi nikawe mpiga debe wa kumtafutia abiria upande wa sirari!.

Jamaa "Ingia twende zetu"

Basi tuliondoka yale maeneo niliyomkuta na kuelekea kwenye stendi za zile gari za kuelekea Sirari,baada ya kufika pale nilitelemka nikakaa pembeni kuangalia wahuni walivyokuwa wakigombania abiria kuwapeleka kwenye magari waliyokuwa wakiyapigia debe!.Baada ya zamu yetu ya kupakia kufika,kuna jamaa wakaanza kuitia abiria mpaka gari ikajaa.Gari ilipojaa jamaa akaniambia niingie nyuma ya buti ambapo pia kulikuwa na abiria wengine wawili ili twende akaniache Sirari niianze kazi yangu ya kupiga debe rasmi!.

Tulipofika pale sirari nikashuka na nikaanza kuchangamka maana nilitelemsha mizigo ya abiria kwenye kile kigari,nilianza kuita abiria kwa kuchangamka lakini nikaja kugundua haikuwa kazi rahisi hata kidogo!.Lile eneo kiukweli niliwakuta baadhi ya wapiga debe ambao kila mtu alikuwa na gari zake alizokuwa akiitia abiria!.

Namshukuru Mungu abiria wakajaa kwenye gari na jamaa akaondoka mimi nikabaki,Sasa kwakuwa mimi na wale jamaa kazi yetu ilikuwa moja,tulianza kupiga stori za hapa na pale.Kuna jamaa mmoja ambaye nilikuwa nasikia wenzie wakimuita pengo na sikufahamu kama ndilo lilikuwa jina lake au ulikuwa ni utani tu!,alikuja tukawa tunazungumza.

Pengo "Mwanangu,hivi Keraryo ni bosi wako?"

Mimi "Keraryo ndiyo nani?"

Pengo "Huyo jamaa uliyemuitia abiria!"

Mimi "Yule ni brother tu"

Pengo "Sikia mwanangu,angalia jamaa asije akakudhurumu posho yako"

Aliendelea "Jamaa wamemkataa watu kibao hapa kijiweni kwasababu hatoi posho!,unamuitia abiria akiondoka ndo imetoka!,na ndiyo maana unaona gari yake ikifika wahuni hawana habari nayo"

Mimi "Hakuna tatizo mwanangu yule ni brother"

Pengo "Sawa mwanangu kama ni brother wako haina noma"

Basi sikutaka maneno mengi sana kwakuwa ndiyo ilikuwa mara yangu ya kwanza kuifanya ile kazi.Ilipofika jioni baada ya kujaza tena ile gari,jamaa alinikabidhi posho ya siku ambayo ilikuwa buku 3,kiukweli nilikata tamaa sana baada ya jamaa kunipatia ile hela lakini sikutaka kumwambia,niliamua kujikaza kisabuni kama mwanaume!.Kumbuka tangia asubuhi nilikuwa sijaweka kitu chochote tumboni.
Baada ya jamaa kunipatia ile posho akaniambia niingie kwenye gari turudi Tarime mjini maana sasa ilikuwa giza,nilipofika mjini nilielekea kwa mama ntilie kupata msosi kisha niliondoka kuelekea kwenye geto la Mtatiro ambaye nilikuta amefunga mlango,nilikaa nje kumsubiri na ilipofika mida ya usiku wa saa 4 jamaa alirudi akiwa na mwanamke!.

Mtatiro "Mwanangu umefika muda mrefu?"

Mimi "nimefika mida ya saa 1"

Mtatiro "Nilienda kwa shemeji yako"

Baada ya kuzungumza,jamaa alifungua gheto akawa ameingia yeye na demu wake,sasa kiukweli niliwaza sana ni wapi nitakwenda kulala maana jamaa alikuwa na demu wake,nadhani baada ya jamaa kuona nina mawazo aliniambia nisiwaze kwani tungelala wote mle ndani.Basi bana,jamaa alitandika chini mifuko ambayo juu yake akaweka nguo akanitaka niegeshe ile kibishi ilimradi kupambazuke tukaendelee na mitikasi ya utafutaji!.

Ule usiku kwakweli kwa upande wangu ulikuwa usiku mbaya sana kwasababu jamaa alianza kutafuna papuchi ya yule demu wake bila huruma,hakujali kabisa na wala hakuona aibu!,kibaya zaidi yule demu wake nae akawa analia kilio kisicho cha machozi huku mwanaume mimi nikiendelea kujigeuza kila sekunde kana kwamba nimepakwa upupu!.Niliapa kabisa ya kwamba,nisingethubutu kabisa kulala kwenye geto la mshikaji kama hizo ndizo zilikuwa habari zenyewe!.

Namshukuru Mungu asubuhi kulikucha na sisi tukaondoka zetu huku demu wa jamaa akiwa bado amelala!.Baada ya kumaliza kazi ile jioni,sikutaka kabisa kurudi Tarime mjini na nilimwambia jamaa kesho angenikuta hapo Sirari nikimsubiri.Usiku ule niliamua kutafuta guest ya bei nafuu iliyokuwa maeneo ya jirani nikalipa elfu 5 nikawa nimelala.

Baada ya kufanya ile kazi ndani ya wiki moja huku nikiendelea kukaa hapo Sirari,nilipata marafiki ambao pia walinifundisha namna ya kufanya kazi zaidi,badala ya kutegemea gari ya brother Keraryo pekee,nikawa naitia abiria na gari za mabosi wengine kisha napata posho,kiukweli nilianza kuchangamka na kuizoea ile kazi,kwa siku nilikuwa sikosi elfu 15 mpaka 20 mfukoni,hiyo ilikuwa ni posho tu!.

Nilipokusanya pesa ya kutosha,ndani ya mwezi huo nilitafuta chumba cha elfu 15000 nikapanga.Sasa kwakuwa sikuwa na hela ya kununua godoro,nilienda kwenye duka nikanunua maboksi ya kutosha kutandika chini niweze kuweka mbavu.-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-


SEHEMU YA 4


Sasa kwakuwa nilikuwa tayari nishapata chumba cha kuishi,nilirudi kule Gamasara kwa mama yangu mkubwa kwenda kuchukua begi langu la nguo.Sikutaka kupoteza muda,nilimuachia mama mkubwa elfu 10 nikamwambia naondoka kurudi nyumbani,yeye aliamini ni kweli narudi nyumbani kumbe mwanaume ndiyo kwanza mapambano yalikuwa yameanza.

Ile kazi ya upiga debe na kutafuta abiria kwenye vile vimchomoko niliifanya kwa takribani miezi 7,ilikuwa ndiyo kazi yangu na kiukweli nilikuwa nimeshaizoea sana!,uhuni na ujuaji wa pale kijiweni nilikuwa naufahamu wote!.Sikuwa tena na wasiwasi kuhusu hela kwasababu nilikuwa sikosi elfu 10 mfukoni kwa wakati huo!.Sasa niliamua kununua simu kwa ajili ya mawasiliano ya marafiki zangu kwasababu karibia vijana wenzangu wote pale kijiweni walikuwa na viswanswadu!.

Mwili wangu ulianza kutakata na kung'aa kwasababu nilikuwa nakula vizuri na kuvaa vizuri!,sikutaka kabisa stress kutoka kwa mtu yeyote!.Ulikuwa ukinitazama kwa kipindi hicho,huwezi kuamini kama nilikuwa mpiga debe na muita abiria maarufu pale Sirari!.

Sasa siku moja nikiwa nipo pale kijiweni,alinipigia simu rafiki yangu Mtatiro na tukazungumza mambo mengi sana ikiwemo utani wa hapa na pale!.

Mtatiro "Mwanangu hatuonani!"

Mimi "Mwanangu siunajua tena kazi zetu hizi,nikiondoka hapa ina maana sipati kitu!".

Mtatiro "Kabisa mwana ni kukomaa tu"

Aliendelea "Sasaa kuna ishu nataka nikwambie mwanangu"

Mimi "Ishu gani mwana?"

Mtatiro "Kuna jamaa yangu mmoja yupo hapo Buhemba kuna dili aliniambia niende tukazungumze lina hela,sasa mimi sipo nimekuja Mwanza mara moja"

Mimi "Mwanza umeenda lini mwanangu?"

Mtatiro "Mbona leo ni siku ya tatu nipo huku"

Mimi "Kuna ishu gani mwana?,tupeane madili kaka"

Mtatiro "Aah nilikuja kwa Uncle kuna hela nilimuomba sasa ndo nipo namsikilizia"

Mimi "Siunarudi lakini?"

Mtatiro "Yeah nitarudi"

Aliendelea "Jamaa tangu jana ananisumbua,hebu nenda mwanangu kama ni dili la hela upige kaka mi ni kija tutajua cha kufanya".

Mimi "Sasa jamaa mwenyewe hata simfahamu kaka hilo dili atanipa kweli?"

Mtatiro "Yule ni jamaa yangu huwa kuna vidili vya hapa na pale ananipaga ninapata hela kimtindo,ndiyo maana nataka uende mwanangu kama ni hela usiiache"

Aliendelea "Nitamgeia namba yako atakucheki kama atakuwa na shida ya kufanya kazi"

Mimi "Poa mwanangu"

Basi baada ya yale mazungumzo niliendelea kupambana na kazi yangu hiyo ya upiga debe,sasa baada kama ya siku 3,kuna namba ngeni ilinipigia na mimi sikuwa na hiyana nikapokea ile simu.

Jamaa "Mambo vipi wewe!"

Mimi "Shwari,nani?"

Jamaa "Mimi naitwa Gabi(Gabriel),mshikaji wake na Mtatiro"

Mimi "Oooh ok"

Jamaa "Yeah!,juzi moja nimeongea na mwana akaniambia yupo Mwanza,sasa kuna ishu nilitaka kufanya nae ila akanieleza wewe ni ndugu yake hivyo akitaharibika kitu!"

Aliendelea "Ni kweli wewe ni ndugu yake na Mtatiro?"

Mimi "Yeah!,jamaa ni zaidi ya ndugu kaka"

Jamaa "Uko wapi kwasasa?"

Mimi "Nipo hapa Sirari"

Jamaa "Sawa,nadhani mida ya saa 8 mchana nitakuwa hapo,siutakuwepo?"

Mimi "ndiyo,mimi nipo wewe njoo utanikuta kaka".

Baada ya yale mazungumzo na jamaa ilibidi nimpigie simu Mtatiro nikamjulisha na jamaa akaniambia kwamba,jamaa huyo ni mtu poa sana na hana tatizo,akaniambia Jamaa huyo huwa anaishi Arusha sasa anapokuwa anakujaga hapo Tarime mara nyingi anahitaji kampani za hapa na pale pia kama kuna jambo lake limekwama alikuwa akimtafuta Mtatiro ili kurekebisha kwasababu yeye hakuwa mwenyeji wa Tarime sana japo kiasili alikuwa ni mkurya.

Kweli!,ilipofika mida ya saa 9 alasiri,namba ya yule jamaa ilianza kuita.

Jamaa "Nishafika kaka,uko maeneo gani?"

Mimi "Njoo hapa kwenye hizi gari za kwenda Tarime"

Jamaa "Ok unaiona hii Toyota corolla?"

Mimi "Ndiyo"

Jamaa "Njoo basi hapa"

Nilitembea mpaka kwenye ile corolla jamaa akawa ameniona akanifungulia mlango nikazama ndani!.Tulitoka hapo tukaelekea kwenye bar moja ambayo haikuwa mbali na lile eneo la kijiweni kwangu,tulipofika tukatelemka kwenye gari tukaingia ndani ya ile bar.Jamaa kimuonekano alikuwa ni mtu fulani hivi ambaye hakuwa mkuda(Pongo/ndata) nilichoamini huenda alikuwa akitokea kwenye familia bora.Basi baada ya kufika hapo Bar jamaa akaagiza bia ya safari na mimi nikaagiza soda baridi maana nilikuwa situmii kilevi kabisa!.

Jamaa "Hunywagi bia?"

Mimi "Hapana kaka,hivyo vitu mimi situmii"

Jamaa "Basi agiza nyama tutafune"

Nilienda mpaka nje ambako kulikuwa na jiko la jamaa mmoja anatengeneza nyama choma,nilimwambia atuwekee nyama choma ya buku 3 na kichuri cha kutosha!.Baada ya kutoa hiyo oda nilirejea ndani kumsikiliza jamaa alikuwa na jambo gani!.

Jamaa "Hivi unaitwa nani vile!,maana nishasahau jina lako!"

Mimi "Naitwa Umughaka"

Jamaa "Yeah!,kweli Umughaka"

Aliendelea "Sasa bana Umughaka wewe ni kijana na mpambanaji!"

Jamaa "Hivi umesoma chuo gani kaka?"

Mimi "Chuo sijafika kaka,nimeishia six"

Jamaa "Oooh sawa ndiyo maana upo tofauti kabisa"

Aliendelea "Huo ndiyo umuhimu wa elimu"

Jamaa alikuwa na vimaswali vya hapa na pale ambavyo sikufahamu kwanini alikuwa akizunguka sana,mimi nilitaka moja kwa moja anieleze jambo lililokuwa limemleta kwangu!.

Jamaa "Sasa umughaka kuna kazi nahitaji tufanye na kwa ninavyokuona utaiweza kabisa"

Mimi "Kazi gani hiyo kaka?"

Jamaa "Hupaswi kuwa na hofu ni kazi ya kawaida tu"

Jamaa akaendelea kunywa beer yake na ilipoisha akaongeza nyingine,sasa ile nyama choma ikawa imefika tukaanza kuikung'uta!.Baada ya kumaliza kula jamaa akaniambia tuondoke tuelekee Tarime mitaa hiyo ya Buhemba na angenipatia nauli ya kunirudisha sirari.Mpaka wakati huo jamaa hakuniambia kabisa ni kazi gani ambayo alitaka nimsaidie kuifanya!.

Tulipofika pale Buhemba kuna nyumba moja ambayo ilikuwa na fensi ya michongoma tukawa tumefika hapo,jamaa alishuka akafungua geti la chuma tukazama ndani. Sasa nilipofika ndani nilikuta pia kuna mwanamke aliyekuwa mzuri akiwa amevaa suruali na kimuonekano yule mwanamke hakuwa wa pale Tarime maana wanawake wetu wa kikurya ilikuwa ukimuangalia tu unamtambua!.

Jamaa "Karibu kaka"

Mimi "Ahsante sana"

Jamaa "Huyu ni shemeji yako kaka"

Basi yule demu akanisalimia na ndipo rafudhi ilikuwa ya kichaga,ilitosha kuamini yule mwanamke alikuwa mtu kutokea pande za mikoa ya kaskazini.Baada ya kuhakikisha nyumba imefungwa milango,jamaa alimwambia yule demu alete begi!,sasa yule demu alileta hapo sebuleni begi ambalo kwa namna alivyokuwa amelibeba,ilitosha kuamini ya kwamba lilikuwa zito!.

Alipokifikisha pale akawa anaongea na jamaa lugha za kihuni ambazo niliambulia maneno machache sana na sikujua walikuwa wakiongea nini!.Yule demu kuna muda kama alikuwa anamuuliza jamaa kwamba mimi siyo soro?(Mzinguaji) na jamaa akawa anamtoa hofu,kiukweli niliambulia maneno machache sana maana wao kuna maneno walikuwa wakiongea ya kimtaani zaidi!.

Baada ya muda jamaa akawa amefungua lile begi,kiukweli nilipagawa baada ya kuona pesa,lile begi lilikuwa limejaa noti za elfu 10 halafu zikiwa mpya!.
-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-SEHEMU YA 5


Nilibaki kushangaa zile hela namna zilivyokuwa uimejaa kwenye lile begi!,kiukweli mate ya tamaa yalianza kunitoka ndani ya moyo!.Nilikuwa nipo tayari kusikia maelekezo atakayonipa ndugu Gabi ili niweze kuyafuata ilimradi tu niweze kujipatia zile hela!.Mawazo yangu kiukweli yalihama na kunichukua kuanza kufikiria vitu vya kijinga,nilitaka baada ya kuzipata hizo hela nikanunue mkoko(Gari) ili niende nikamdolishie dingi ajute kunikataa na kuniona sifai!.Kiukweli niliwaza ujinga sana.


Gabi "Sa sikia jamaa yangu"

Aliendelea "Hii ni pesa ya Tanzania lakini si halali"

Mimi "Si halali!,kivipi tena isiwe halali?"

Gabi "Yes!,swali zuri,ndiyo maana nimekutafuta wewe nikiamini unataka hela"

Mimi "Hakuna mtu asiyetaka hela kaka,we niambie nini nifanye"

Gabi "sawa,sasa humu ndani tupo watu watatu,yaani mimi,wewe pamoja na wife".

Aliendelea "Tulipoingia ndani nilimwambia wife afunge mlango ili isije mtu akaingia ghafla kama anaingia chooni"

Gabi "Sidhani kama wewe ni mtoto baada ya hapa ukaanza kupayuka payuka kama mwendawazimu"

Aliendelea "Hizi ni hela bandia na ndiyo maana nimesema si halali"

Gabi "Mimi kukuleta hapa ni kwasababu nina muamini sana Mtatiro na tumeshapiga sana hizi mishe,sasa naomba mwanangu tukubaliane kwanza"

Baada ya jamaa kuniambia zile hela niza bandia,kiukweli nilibaki kushangaa kwasababu ulikuwa ukiziangalia zilikuwa zinaonekana kabisa ni pesa halali kwa matumizi na ilikuwa ni vigumu sana kuzitambua labda mpaka uwe mtaalamu wa hali ya juu.

Gabi "Sababu ya mimi kukwambia ni pesa bandia ni kukulinda wewe na sisi pia"

Aliendelea "Ningeweza kukwambia tu shika mzigo nenda kafanye moja mbili tatu halafu kila mtu akafa na chake,lakini nimeona wewe bado mgeni wa haya mambo na pengine ungedakwa ungewaleta hapa mapongo"

Mimi "Kaka siwezi kabisa kufanya huo upuuzi"

Gabi "Sa sikia Umughaka,kwenye kila elfu 10,wewe yako tano na sisi yetu ni tano"

Aliendelea "Sasa ni juu yako kuhakikisha kila mzigo nitakao kuwa nakupatia unamaliza ili uchukue chako na chetu tukipate!"

Mimi "Sawa kaka,kwahiyo niambie sasa nafanyaje"

Gabi "Mimi kila siku nitakuwa nakupatia shilingi laki moja,wewe ndiyo utahakikisha hiyo laki unaichenji unabaki na yako fyu(50) na sisi ya kwetu fyu".

Basi baada ya jamaa kuniambia vile ikabidi sasa akili ianze kukimbia fasta!,Jamaa alitaka kwenye ile laki moja atakayonipatia kila siku,nihakikishe naingia mtaani kuwashikisha wadau ili pesa yao iwe ni elfu hamsini na yangu pia iwe elfu hamsini,kwakifupi tuwe tunakula pasu kwa pasu!.Baada ya yale mazungumzo jamaa akanitia laki moja nikatia mfukoni akanipatia na nauli ya kunirudisha mpaka Sirari!.

Gabi "Ukiwa unamaliza mzigo utakuwa unanicheki kwenye simu,kama sipo nitakuwa nakujulisha ili ukija utamkuta shemeji yako utamuachia cha kwetu atakupatia mzigo mwingine"

Mimi "Haina noma kaka"

Basi nikaondoka zangu kurudi Sirari!,nikiwa njiani nikamtafuta Mtatiro kwenye simu kutaka kumfahamisha lile dili!.

Mtatiro "Mwanangu hilo dili lina hela kama ukituliza akili,cha muhimu ni kuwa na siri sana na pia jiamini usije kujishitukia shutikia"

Aliendelea "Mwanangu mi mbona nimefanya sana hiyo kazi na mshikaji,vitu vyangu vyote vya ndani ulivyoviona nimenunua kwa pesa ya mshikaji,ni dili tamu sana sema mshikaji kuna muda nae anapoteaga sana ndo maana nikaamua niingie kwenye hiace angalau niwe napata hela ya kula"

Aliendelea "Mimi nikirudi kama jamaa bado akiwepo tutaungana kaka"

Mimi "Kwahiyo Mtati wewe ulikuwa unafanyaje fanyaje mwanangu,nipe mbinu za kuzibadilisha"

Mtatiro "Jamaa amekwambia atakuwa anakugei kiasi gani?"

Mimi "Ameniambia kwenye kila elfu kumi,yangu tano na yake tano"

Mtatiro "Ni vile vile tu kama kwangu ilivyokuwa,sasa sikiliza wewe uwe unaingia madukani unanunua vocha ya buku,hiyo ni rahisi mno na kwa pale Sirari bado kuna wajinga wengi"

Mimi "Mbona kama buku ni nyingi sana kaka,au niwe nanunua tu ya jero!?"

Mtatiro "Vocha ya jero ni ngumu sana kupewa chenji na nirahisi kushituka ila ukinunua Vocha ya buku kwenye kila teni wewe utakuwa unachukua yako buku nne na jamaa unamlelekea buku tano yake"

Mimi "Sawa kaka nimekuelewa,ngoja niingie kitaa"

Mtatiro "Kwani uko wapi sasa hivi?"

Mimi "Ndiyo natoka kwa mshikaji"

Mtatiro "Sawa mwanangu kapambane,uwe unanikumbuka angalau ka vocha"

Mimi "Haina noma"


Basi niliucahapa mwendo kuelekea barabarani ambapo nilikamata Hiace za kunipeleka mpaka mjini ili nikadandie vimchomoko vya washikaji nirudi Sirari!.Kwa wakati huo baada ya kupata umaarufu na kuwa mwenyeji pale Sirari,nilikuwaga silipi nauli kama nikitaka kwenda Tarime au kurudi Sirari,nilikuwa nadandia tu gari yoyote iliyokuwa ikielekea sehemu husika kwasababu nilikuwa nafahamika!.

Baada ya kufika pale Sirari siku hiyo niliamua kuendelea na kazi yangu ya upiga debe huku nikiendelea kusoma mazingira na namna ya kuifanya hiyo kazi yangu mpya.
Sasa siku iliyofuata nilichukua noti ya elfu kumi kati ya zile hela bandia na kuitazama vizuri,kwakweli ilikuwa ni ngumu sana kuijua kwasababu ilikuwa na kila kitu ambacho kilipatikana kwenye noti halali,utofauti ambao nao ulikuwa kwa mbali labda ilikuwa harufu tu!,zile hela ulikuwa ukizinusa kwa ukaribu sana zilikuwa na hatufu fulani ya karatasi nyuepe(rim paper).

Nilichukua noti 3 ambazo zilikuwa elfu 30 nikaingia zangu pale stendi kupiga debe kama kawa!,sikutaka kabisa kuchenji zile hela kwa wadau wangu wa vimchomoko kwasababu niliona ningewaumiza wadau!.Sasa ilipofika mida ya saa 4 asubuhi nilielekea kwenye duka moja kubwa lilikuwa hapo jirani na mara nyingi tulikuwa tukinunua hapo bidhaa mbalimbali ikiwemo soda,nilipofika nilichomoa noti ya elfu 10 nikamwambia yule maza anipazie Coca baridi,bila tatizo yule Maza aliikamata ile hela akaitia kwenye droo kisha akafungua friji akanipatia soda niliyoiomba!.

Maza "Umughaka utafata chenji bhana sina chenji asubuhi hii"

Mimi "Haina tatizo"

Baada ya kuichukua ile hela nilifurahi kimoyo moyo huku nikijisemea siku zote jamaa alikuwa wapi!.Basi nilihakikisha siku ile zile noti mbili zilizokuwa mfukoni ninahakikisha nazimaliza na ndivyo ilivyokuwa!.

Ile kazi kiukweli niliifanya bila mtu yeyote kushitukia kabisa,sasa kuna muda nilikuwa namkamata mwana yeyote pale kijiweni nampiga liteni namwambia akanunue soda,moja yangu na moja yake,bila kujua unakuta muhuni anafurahi anaenda kununua huku akikimbia!.Uzuri wa pale kijiweni tulikuwa tukiishi kama ndugu,hivyo ukimpatia muhuni hela akanunue eidha soda au fegi anaona unamjali kinoma.

Kiukweli ndani ya mwezi mmoja baada ya kuifanya ile kazi maisha yangu nayo yalianza kubadilika,niliamua kuhama kwenye kile chumba nilichokuwa nina kaa mara ya kwanza ambacho nilikuwa nalipia elfu 15 kwa mwezi,nikaamua kwenda kupanga chumba na sebule,ambavyo nilikuwa nalipia elfu 50 kwa vyote viwili!.

Kazi ile ilikuwa tamu sana na nzuri na ule ukonda kiukweli nilikuwa nazugia tu!.

Ndani kwangu kulianza kubadilika baada ya kununua makochi ya kawaida,nilinunua kapeti nikatandika chini,baadae pia nikanunua subwoofer na TV,nilihakikisha najijenga na kujipanga kama kijana.

Baada ya pesa kunizidi nilianza kujichanganya na wanangu tukawa watu wa viwanja vya starehe pale Sirari,ule mji japo ulikuwa ni mdogo lakini ulikuwa na vistarehe uchwara vilivyokonga nyoyo!.Kipindi hicho ndipo sasa na mimi nikajifunza kunywa pombe huku bia yangu pendwa ikiwa ndovu lager!.Baada kupiga kazi ile ya magumashi kwa miezi 3,jamaa aliniambia mzigo umeisha na ataondoka kwenda Arusha na haitochukua mwezi atakuwa amerudi ili tuendeleze libeneke.
-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-


SEHEMU YA 6.Maisha kwa upande wangu yalikuwa mazuri na hata yale majuto ya mzee wangu kunitimua nyumbani hayakuwepo tena,zaidi ni mimi ndiye niliyetamani nifanikiwe ili nikamringishie ajute kunifukuza nyumbani kwa kunidharirisha!.Nilikuwa nafanya kazi mbili kwa wakati mmoja,kazi yangu ya upiga debe ilikuwa ikinipatia pesa ya kula kila siku,kuhusu kula kwakweli nilikuwa siwazi kabisa!,ile pesa ya kubadili fedha haramu yenyewe ilifanya nikavaa vizuri,nikanunua samani za ndani na kupiga starehe!.

Marafiki na wadau wangu wa pale Sirari wao waliamini mimi ni mjanja mjanja na uenda nilikuwa najiongeza kutokana na elimu yangu kumbe pasipo kufahamu kijana mwenzao nilikuwa nafanya dili haramu.

Niliendelea kumsubiri bwana Gabi(Gabriel) ili atakapo rudi basi tuendelee na kazi yetu ambayo tayari ishanitia uchizi!.Sasa ndani ya mwezi mmoja baada ya kusubiri jamaa alirudi na alipofika tu alikuwa amenipigia simu akinitaka niende nikachukue hela niziingize mtaani ili kila mtu afe na chake!.Kiukweli pesa zilikuwa nyingi sana na sikuwahi kufahamu yeye alikuwa akizitoa wapi!.

Kitu cha kumshukuru Mungu kwa upande wangu tangu nianze kujihusisha na ile biashara haramu,sikuwahi kushitukiwa na mtu yeyote na nilikuwa nimesema endapo siku nikashitukiwa basi mimi ningekufa na mtu yeyote kwa kumsingizia uongo ili nichomoke!.

Sasa nikiwa naifanya kazi ile kwa umakini mkubwa huku nikiendelea kuzuga kwenye kazi yangu ya upiga debe,mpaka muda huo nadhani mtaani nilikuwa nishaingiza si chini ya milioni 10.kuna siku mida ya saa 5 asubuhi mke wa jamaa akawa amenipigia simu huku akihitaji kufahamu niko maeneo gani.Sikuwahi kabisa kuwasiliana na yule mwanamke ijapokuwa namba yangu yeye alikuwa nayo na mimi pia ya kwake nilikuwa nayo,sasa kitendo cha kuniuliza niko wapi sikujua lengo lake ni lipi maana hata mumewe hakuwahi kuniuliza kwamba niko wapi!,nakumbuka ilikuwa ni ile siku ya kwanza tu ndiyo jamaa aliniuliza nipo maeneo gani ili aje tuzungunze!,sasa huyu mkewe lile swali lake la "Uko wapi" na namna alivyouliza ni kama Jamii yetu ya kikurya mwanaume kuambiwa na mkewe kwamba "Nitakupigia".Ikifika hatua hiyo basi unaweza kumkung'uta mwanamke na ukamuua kabisa!.Sasa kitendo cha kuniuliza uko wapi tena bila hata salamu kilinikera na kuniudhi sana lakini niliamua kukausha tu!.

Yeye "Marieta hapa naongea"

Aliendelea "Uko wapi?"

Mimi "Kuna shida?"

Yeye "Wewe niambie uko wapi?"

Mimi "Kwani siku zote huwa napatikana wapi shemu!"

Basi baasa ya kumwambia vile akakata simu,nilifahamu kama kulikuwa na tatizo angenipigia simu yeye,mimi niliendelea na kazi yangu bila presha!.Sasa baada ya kama dakika 10 kupita akawa amenipigia simu.

Yeye "Njoo nyumbani Gabi anakuita"

Mimi "Ok sawa,mwambie nitakuja jioni"

Yeye "Njoo muda huu kama unaweza ni ishu ya haraka!".

Mimi "Shemu kuna shida?"

Yeye "Hapana ni kawaida tu!".

Basi baada ya mazungumzo akawa amekata tena ile simu,sasa yule mwanamke alikuwaga anaongea kwa kisirani sana na kwa mkato,sikufahamu uenda ndivyo walivyokuwa wanawake kutoka huko Arusha au ilikuwa ni tabia yake tu!,kiukweli mimi alikuwa akiudhi sana kama kijana wa kikurya niliyekuwa sipendi dharau na ndiyo maana hata nilikuwa sipandishi nae stori!.

Niliamua kumpigia simu bwana Gabriel mimi mwenyewe kama ni kweli alikuwa akinihitaji wakati ule pale nyumbani ama la!,sasa niliipiga sana ile simu ya jamaa ikawa inaita tu bila kupokelewa,nikaendelea kupiga lakini nikaona holaa!.Sasa akilini mwangu nikaanza kuwaza mambo ya kijinga,nikawa nasema uenda mtoto wa kike anahitaji kupelekewa moto na ile ilikuwa ni Zuga tu kujisemesha naitwa na jamaa ili niende pale nyumbani kwao!,lakini pia kilichonipa ujasiri ni kwamba kama jamaa angekuwa ananihitaji angenipigia simu mwenyewe!,sasa mawazo yakanipeleka mbali sana nikaingia tamaa ya moyo ghafla yule mwanamke akajaa usoni nikaanza kumvutia picha namna alivyo na namna nitakavyo mkung'uta shipa lenye ladha ya kikurya!.Basi nikaamua kumpigia simu ili kujiridhisha tena!.

Yeye "Umefika wapi?"

Mimi "Ndo nadandia usafiri nakuja"

Mimi "Nampigia jamaa simu naona hapokei"

Yeye "Mi sijui bana we njoo"

Basi mwanaume nikadandia mchomoko iliyokuwa ikielekea Tarime mjini nikaondoka!.Baada ya kufika pale Tarime niliingia stendi kule ambako kulikuwa na wanangu wenye magari ya kuelekea Musoma,nikadandia Hiace ikanishusha maeneo ya Buhemba yalipokuwa makazi ya Gabriel na huyo mkewe!.

Basi nilipofika getini nilikuta geti liko wazi nami nikalifungua na kuingia ndani,nilibisha hodi na hatimaye yule mwanamke alikuja kunifungulia mlango,sasa wakati anafungua mlango alionekana ni kama hana amani kabisa tofauti na siku zote!.

Mimi "Shwari?"

Yeye "Shwari,vipi!"

Sasa ile natia tu mguu ndani,kumbe kuna jamaa alikuwa amejificha nyuma ya mlango akawa amenivuta kwa ndani kisha akaufunga ule mlango na funguo akachomoa! .Basi yule jamaa akaniambia kwa ishara niongozane na yule mwanamke kuelekea sebuleni!.

Baada ya kufika sebuleni nikawakuta jamaa 3 na yule aliyefunga mlango walikuwa jumla 4,pia nikamkuta Gabriel amekaa kwenye kochi akiwa hana raha kabisa!.Basi miongoni mwa wale jamaa akaniongelesha kwa ukarimu kabisa!.

Jamaa "Umughaka mambo vipi kaka"

Mimi "Shwari kaka"

Jamaa "Vipi lakini mambo yako!"

Mimi "Mimi niko poa kabisa kaka"

Jamaa "Ooh sawa,sirari wanasemaje kaka"

Mimi "Tupo tu tunapambana"

Jamaa "Hivi pale Sirari huwa unaishi maeneo gani?"

Sasa kabla hata sijajibu,yule jamaa ambaye yeye kwa wakati huo akiwa amekaa na wenzie kusimama kama milingoti,akaniambia nisimame nimsogelee alipokuwa amekaa!.

Jamaa "Hebu tuangalie humu mfukoni umeweka nini bwana Umughaka"

Jamaa moja kwa moja baada ya kumsogelea alizama mfukoni mwangu akatoa simu na hela nilizokuwa nazo!.

Jamaa "Hii simu ya nani?"

Mimi "Ya kwangu"

Jamaa "Na hii hela!"

Mimi "Ni yangu kaka"

Jamaa "Kumbe unaweza kufanya tu kazi zako vizuri na bado ukapata hela nzuri tu bwana Umughaka"

Sasa ile hela niliyokuwa nayo mfukoni muda huo ilikuwa ni elfu 16 na vichenji kadhaa!.

Jamaa "Huyu bwana unamfahamu?"

Mimi "Ndiyo,ni brother angu"

Jamaa "Mtu wa Arusha na mkurya ni ndugu wapi na wapi Umughaka wewe acha hizo bwana!"

Kiukweli yule jamaa alikuwa anaongea kama mtu fulani mnyenyekevu sana lakini kiuhalisia alionekana asiyekuwa na huruma hata chembe!,sasa mpaka wakati huo nilifahamu kabisa mambo yameshaharibika na sikupata tabu kuamini wale walikuwa ni mapongo (Askari).

Jamaa "Mbona jamaa anasema yeye hakujui!"

Sasa wakati jamaa anaongea na mimi alikuwa akiendelea kukipekua kiswanswadu changu.

Jamaa "Wewe unasema jamaa ni brother wako lakini jamaa nimemuuliza anasema hakujui"

Basi nilimtazama Gabriel nikadhani uenda ataniangalia ili anipatie ishara yeyote lakini jamaa akawa ameangalia chini tu huku akichezea vidole!.Baada ya kuona jamaa aniangalii mimi ikabidi nikomae kwamba jamaa ni brother angu!.

Jamaa "Sawa bwana umughaka naona mnateteana Mkurya na muarusha!"

Aliendelea "Jamaa mpaka sasa ameshakupatia shilingi ngapi bwana Umughaka!"

Lile swali kiukweli lilifanya nikakosa pozi nikaanza kujiuma uma hata kujibu nikashindwa!,na kibaya jamaa alikuwa anauliza kama utani lakini alionyesha yuko serious sana!.

Jamaa "Huna haja ya kuficha kaka wewe kuwa mkweli tu ili ukaendelee na shughuli zako".

Mimi "Kiukweli nikihesabu haraka haraka inaweza kufika milioni 1"

Jamaa "Hebu kuwa serious kidogo kaka uache utani,yaani miezi takribani mitano mnafanya kazi awe amekupa milioni 1 tu!"

Aliendelea "Acha hizo mambo bhana,wewe eleza ukweli ili uondoke ukafanye shughuli zako"

Mimi "Kaka hiyo ndiyo nayo ikumbuka"

Jamaa "Haya bhana!"

Aliendelea "Marco hebu nendeni na jamaa mpaka kwake huko nadhani atawaeleza vizuri,pengine hapa anaona aibu"

Basi baada ya jamaa kusema vile,kuna jamaa kati ya wale waliokuwa wamesimama akanishika shingoni akaniambia nisimame tuondoke!,kiukweli nilichanganyikiwa sana siku hiyo na nilifahamu kabisa mambo si mambo,nilijua tu kuna namna Gabriel na mkewe watakuwa waliharibu mahali na mimi sasa ndiyo kujikuta nimo kwenye msafara!.

Tulipotoka nje wale jamaa waliniambia nitembee pasipo kuwa na hofu yeyote na wala nisije kujaribu kukimbia maana wangenipiga mpaka waniue!.Basi tukaanza kutembea kuelekea barabarani kutafuta Hiace ili twende mpaka mjini tukapande mchomoko kuelekea sirari.
Sasa wakati tunatembea,jamaa wao walikaa kushoto na kulia,mimi nikawa katikati yao!.Muda huo tulikuwa tunapiga stori za kwaida kabisa kana kwamba hakuna tatizo huku mimi nikionyesha Kicheko feki kilichojaa majuto ndani yake! .
-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-


SEHEMU YA 7.Sikutaka kabisa marafiki zangu na watu wanaonifahamu pale stendi wahisi kitu,kiukweli japo nilikuwa mikoni mwa wale askari lakini nilijitahidi sana kuonyesha hali ya kawaida na tena tulipofika kwenye hiace ya kuelekea mjini ni mimi ndiye niliyefanya kazi ya kuwaombea lift nikijifanya niwanangu!.Sasa tulipofika pale mjini kukamata mchomoko wa kuelekea Sirari ilibidi askari mmoja atoe hela amlipie yule mwenzie na mimi kudandia bure,wasingeweza kupanda mchomoko bure kwasababu ilikuwa inachukua watu wachache!.
Basi tukaondoka na hatimaye tukafika pale stendi ya mchomoko Sirari,tulipofika pale wanangu walianza kunichangamkia na wengine kuniuliza nilienda wapi,sasa wale askari wakata kunidhibiti lakini niliwaambia kiaina ya kwamba siwezi kukimbia na wasinidharirishe mbele ya wana,bahati nzuri jamaa walikuwa waelewa na wao wakawa wameniacha najifanya kujizungumzisha mbele ya washikaji kana kwamba sina kosa kumbe moyoni naujua ukweli!.

Baada ya mazungumzo pale stendi na wanangu,nilijikuta kitete chote kimetoweka na kisha nikaandamana na wale mapongo hadi nilipokuwa nimepanga!.Nashukuru Mungu hakuna mtu aliyeshitukia mchezo pale stendi.Basi baada ya kufika hapo nyumbani nilifunua kifuta miguu(zulia)pale mlangoni kisha nikatoa funguo nikafungua mlango!.Sasa ile nyumba sikuwa peke yangu,kulikuwa na wapangaji wengine ambao nao kuna wengine walikuwa kwenye shughuli zao na wengine hasa wanawake walikuwa nyumbani,sasa desturi ikawa ni ileile ya kwamba asifahamu mtu yeyote kwamba wale ni askari,nilipofungua mlango niliwakaribisha kwa sauti ya "Karibuni" ili asitokee mtu yeyote akajua kitu.

Baada ya kufika ndani askari mmoja akaniomba funguo akafunga mlango kisha wakanitaka tuanzie kufanya upekuzi chumbani.Upekuzi haukuchukua muda mrefu kwasababu sikuwa nimejaza mle ndani makorokoro,bali kulikuwa na kitanda pamoja na begi kubwa la nguo na vitu vidogo vya kawaida,sebuleni nako kulikuwa na makochi,TV na redio na picha za ukutani zilizopendezesha sebule.Hakukuwa na vyombo vingi kwasababu nilikuwaga sipiki hapo nyumbani bali nilikuwa nakula kwa mama ntilie,nilikuwa na mabeseni mawili pamoja ndoo mbili tatu nilizotumia kwa ajili ya kuwekea maji ya kuoga na kufulia.

Sasa pesa zangu zote nilikuwaga nazihifadhi kwenye mfuko wa suruali kisha naweka hiyo suruali kwenye begi pamoja na nguo nyingine,wale askari walipekua kila mahali bila kuona kitu chochote.Wakati huo nilikuwa nimebaki na zile fedha haramu kiasi cha shilingi elfu 40,pia nilikuwa nina hela halali kiasi cha shilingi laki moja na elfu themanini.

Askari "Nadhani unajua kilichotuleta hapa ni kitu gani,hebu kuwa mkweli pesa umeweka wapi?,au unataka tutumie nguvu?"

Aliendelea "Mpaka tumefika hapa umekuwa mstaarabu,angalia mambo yasije haribikia hapa"

Baada ya jamaa kuniambia vile na akionekana kumaanisha,nilichukua ile suruali iliyokuwa imetupwa chini kutokana na shaghala baghala ya upekuzi nikatoa zile hela nikamkabidhi jamaa!.

Askari "Haya sasa ndiyo mambo,endelea kutafuta najua bado zipo nyingine!"

Mimi "Hapana afande pesa niliyokuwa nayo ndiyo hiyo"

Askari "Kwanini unatupotezea muda?,siutoe pesa mdogo wangu tuondoke!,au unataka tutumie nguvu?"

Mimi "Kweli afande pesa yote niliyokuwa nayo ndiyo hiyo"

Jamaa waliendelea kutafuta kila mahali lakini hawakuona kitu,sasa kwakuwa niliwapa zile hela askari mmoja akawa amesema wanipige pingu kwakuwa tayari kidhibiti nilikuwa nacho.Niliwaangukia miguuni nikawasihi wasinipige pingu na sitowasumbua njiani!,yule askari aliyefunga mlango wakati tunatoka kiukweli akawa akinionea huruma sana kama kijana mwenzie na akamwambia mwenzie asifanye hivyo kwakuwa wakati tunakuja sikuwasumbua,sasa yule mwenzie akawa ameendelea kuweka msisitizo kwamba nipigwe pingu!.

Basi baada ya kuwasihi sana huku machozi yakinitoka,wakawa wamekubali na wakanitaka nisije kujaribu kuwakimbia.Sasa wakati tunatoka nikachukua ufunguo nikampelekea dada mmoja aliyekuwa mke wa mpangaji mwenzangu hapo nyumbani,nilimwambia akae na ule ufunguo kuna mahali naenda na nikirudi nitaukuta kwake!.

Tukaondoka na wale askari mpaka stendi tukapanda mchomoko kuelekea Tarime mjini,kwa namna tulivyokuwa tunatembea na wale askari wakiniuliza maswali kadhaa huku nikiendelea kuwajibu nilihakikisha kabisa hakuna mtu anayefahamu jambo lile,mimi sikutaka kabisa kujifanya mjuaji ili kujiepusha na aibu isiyokuwa ya lazima!.

Tulipofika pale Tarime mjini tukitokea Sirari,kuna askari mmoja niliona anaongea na simu na sikufahamu alichokuwa anaongea,sasa baada ya maongezi yale kwenye simu,alimwambia yule askari mwenzake kwamba ahakikishe nakaa chini,basi nilikaa chini huku yule askari mwingine akiondoka kusikojulikana!,wakati nimekaa chini yule askari alikuwa makini sana na mimi na hakutaka kabisa stori na maongezi!.Baada ya dakika 10 niliona difenda imefika lile eneo na kutakiwa kupanda.

Moyo wangu uliuma sana na nilikuwa nawaza napelekwa wapi wakati ilipaswa nirudishwe hadi buhemba nilikokuwa nimetokea!.Sikufahamu hatima ya Gabriel na mkewe iliendelea vipi nilipowaacha!,mimi nilijua huo msalaba tayari ndiyo nishaubeba!.Kilichokuwa kinaniumiza zaidi ni namna wazazi wangu wakija kufahamu ya kwamba mtoto wao nipo polisi au kufungwa gerezani,nilikuwa navuta picha ya Mzee wangu namna atakavyo ongea akisikia nimekamatwa,tena nilijua ndiyo atajihahakishia kabisa kwamba kunizimua pale nyumbani alikuwa sahihi kabisa!.

Basi niliamua kutulia ndani ya difenda na kumuachia Mungu yeye ndiye akawe muamuzi wa lile jambo,kwa hatua niliyokuwa nimefikia sikuwa na msaada wowote zaidi ya kuamini ni Mungu peke yake ndiye anaweza kuniokoa na mkono wa serikali!.

Kuna muda hata kama humjui Mungu na hujawai kukanyaga kabisa kanisani au msikitini,unapofikwa na jambo gumu kiutatuzi ndipo siku hiyo utatamani mahubiri na mihadhara isikike mahali ulipo ili uweze kuamini kuna Mungu na utajaribu kusali sala zote na utatumia lugha zote kumuomba hata kama unayemuomba uliamini hayupo.

Mpaka wakati huo baada ya kujiingiza kwenye upiga debe na vile vistarehe uchwara vya muda mfupi sikuwahi kabisa kukanyaga mlango wa kanisa lakini baada ya kupata hiyo changamoto ya muda mfupi nilikuwa nikimlilia Mungu kimoyo moyo aniokoe na kile kikombe kana kwamba nilikuwa muhudhuriaji mzuri wa ibada!.


Baada ya kupakiwa kwenye ile difenda nilipewa amri ya kukaa chini na kusogea mbele kabisa na miguu kuakalisha chini ikiwa imenyooka,ile difenda iliondoka yale maeneo kuelekea maeneo ya Nyamisangura ambako tulipofika pia huko kuna jamaa kama 6 walipakiwa kwenye ile difenda na kufanya jumla yetu wahalifu kuwa 7.Basi baada ya hapo ikaondoka kwa spidi kali huku askari wengine waliokuwa na bunduki wakidandia na kuondoka!.

Sasa tulipofikishwa pale central,baada ya kushuka tulitakiwa kuelekea ndani kwa kukimbia huku mikono tukiambiwa tuweke kichwani!,baada ya kufika ndani askari mmoja wapo wa wale niliokuwa nao akawa ameniambia nifuatane naye.Ndipo akafungua chumba kimoja ambacho baada ya kuingia ndani nikamkuta Gabriel na mkewe akiwa na yule askari niliyewaacha nae pale nyumbani kwake!.

Askari "Ooh umemleta bwana mdogo"

Aliendelea "Unapofika hapa kwetu bwana mdogo hakuna makaochi hivyo unatakiwa ukae chini!".

Basi baada ya hapo nikaona yule askari anatoa ile hela elfu 40 ambayo haikuwa halali anamkabidhi yule askari ambaye ilionekana alikuwa mkuu wa upepelezi!.Kilichonishangaza ni kutokuona ile laki moja na elfu themanini ambayo ilikuwa halali sikuona anakabidhiwa yule afande na ndipo nikagundua wale askari watakuwa waligawana ile hela!.

Basi baada ya mazungumzo ya muda mrefu hapo ndani huku tukiwa tunahojiwa na yule askari kuandika maelezo yetu,alipomaliza akawa amemwambia yule askari tunapaswa kuwekwa rumande!.Kiukweli nilijuta sana moyoni na sitakaa nisahau ile siku.
Kabla ya kuingizwa rumande nilimuomba yule afande simu yangu ili niwasiliane na ndugu zangu wawe na taarifa,hakuwa na shida kabisa na alinipatia ile simu na akanitaka niongee nikiwa mle mle ndani ya kile chumba.

Basi baada ya kupewa ile simu,nilimpigia mwanangu mmoja tuliyekuwa tumeshibana sana aliyekuwa mpiga debe mwenzangu pale Sirari!.

Mimi "Nyamori mambo vipi?"

Nyamori "Mzee wa kuzugia mbona sikuoni kijiweni wewe!?"

Sasa kwa pale Sirari jina maarufu nilifahamikaga kama mzee wa kuzugia,hii ilikuja baada ya kila sentensi nitakayoongea nilikuwa naweka neno kuzugia au kuzuga na hii kitu nimekuwa nayo hadi leo hii,nadhani ni mazoea tu!.Sasa jamaa baada ya kupokea simu yeye alianza utani wake bila kufahamu kilichokuwa kinaendelea!.

Mimi "Mwanangu nimepata msala!"

Nyamori "Msala gani tena mzee?"

Mimi "Nipo hapa polisi mwanangu,kama vipi mje kunicheki!"

Nyamori "Haina noma mwanangu ngoja niwashitue wana"

Basi baada ya yale mazungumzo nikawa nimekabidhi ile simu tena kwa yule afande.

Kabla ya kuingizwa lupango,tulitakiwa kukabidhi kila tulichokuwa nacho,mimi mpaka muda huo sikuwa na chochote zaidi ya saa ya mononi na waleti ambayo haikuwa na kitu zaidi ya makaratasi na tiketi za gari!.
Basi kwa mara ya kwanza mwanaume nikaingizwa lokapu ambako baada ya kuingia niliona ni heri ukalazwa chooni wiki nzima lakini si mule ndani.-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-


SEHEMU YA 8.
Joto,harufu mbaya,giza na msongamano wa watuhumiwa kwenye ile Selo ilifanya nikajuta kuzaliwa.Ndiyo ilikuwa mara yangu ya kwanza kukanyaga polisi!,sikuwahi kabisa kuamini ya kwamba itatokea siku moja na mimi nitajikuta mikononi mwa mapongo na kuishia lokapu!.
Mazingira ya mle ndani yalikuwa mabaya sana,harufu ya mikojo,vinyesi na majasho ya wahalifu yalinichanganya sana,kibaya zaidi nilikuta kukiwa na mrundikano wa watu huku wengine wakiwa na majeraha katika sehemu tofauti ya miili yao!,wengine nadhani kutokana na kipigo cha raia huko nje walikuwa wanashindwa hata kunyanyuka na kujisogeza!.Kiukweli sitakuja kusahau hiyo siku,ingawa kwasasa nishakuwa mwanaume kamili wa kupambana na changamoto zinazonikabili za kimaisha lakini huwa naepuka sana nisijikute naangukia mikononi mwa vyombo vya dola,ndugu zangu fanyeni mfanyavyo lakini kama hujawahi kukanyaga kule ndani nakushauri tu usithubutu!,lile taizi siyo la mchezo!.

Sasa baada ya kukaa kwa takribani kwa dakika 15 ndipo nikaona lile geti la kile chumba linafunguliwa na kuna mtu akawa ameingizwa,sasa kwakuwa wakati anaingizwa kulikuwa na mwanga wa nje hapo koridoni nilimuona alikuwa ni Gabriel,mle ndani kulikuwa na giza lisilokuwa la kawaida ingawa ilikuwa mchana mida ya saa 9.
Nilimuita Gabriel akawa amesogea eneo nililokuwa nimekaa kwa taabu kwa kukunja na kubana miguu,kuna jamaa alikuwa kando yangu nikamuomba abane kimtindo ili nikae na mshikaji!.

Mimi "Kaka kwani kimetokea nini?"

Gabi "We acha tu,yaani sijui hata nisemeje!"

Gabi aliendelea kusikitika sana akawa anashindwa hata kuongea,mimi ndiyo alizidi kunichanganya kabisa kwasababu nilitegemea kitu kutoka kwake lakini nae akawa kama haelewi ni nini kilotokea!.

Mimi "Sijui tutaachiwa lini kaka!"

Gabi "Nimejaribu kuongea na yule afande kiutu uzima lakini naona kama haelewi"

Mimi "Sasa itakuwaje kaka au ndiyo tunapelekwa gerezani?"

Gabi "Ngoja tuone itakavyokuwa,nimefanya mawasiliano na bosi wangu ameniambia anashughulikia"

Sasa wakati tunazungumza,kuna jamaa mmoja aliyekuwa kando yetu alikuwa kama kachanganyikiwa hivi,kuna muda alikuwa akiongea mwenyewe kama chizi!.Aliposikia Gabi anazungumzia ishu ya kutoka ndani akawa amedakia!.

Jamaa "Humu ndani ukiwa na hela unadhani unakaa?,labda uwe umeua lakini kama hujaua mbona unateleza tu kama nyoka"

Basi sisi hatukutaka kumjibu kitu chochote tulibaki kumsikiliza akiwa anaongea.Kadiri muda ulivyokuwa unayoyoma ndivyo nilizidi kuchanganyikiwa na nilidhani ingekuwa jambo jepesi mimi kutoka kumbe haikuwa kama nilivyofikiria!.

Mimi "Shem wamemweka wapi?"

Gabi "Amepelekwa kwenye selo ya wanawake"

Kiukweli hatukuwa na maneno mengi ya stori mule ndani zaidi ya kila mtu kichwani mwake kuwaza alichokiwaza!.Sasa ilipofika mida ya saa 10 kama na nusu jioni,nilisikia kuna afande anaita kwa sauti!.

Afande "Humu ndani kuna mtu anaitwa mzee wa kuzugia?"

Aliendelea "Narudia,humu ndani kuna mtu anaitwa mzee wa kuzugia?"

Mimi "Nipo afande"

Niliitikia kwa sauti kubwa ili aweze kunisikia,nilinyanyuka nikawa nimesogea mpaka pale kwenye lile geti!.

Afande "Jina lako halisi unaitwa nani?

Mimi "Naitwa Umughaka"

Afande "Aisee hebu taja majina yako uliyoandika kwenye kitabu usinipotezee muda"

Nilipomtajia jina langu kamili nadhani alikuwa akiangalia kwenye orodha ya majina ya wahalifu waliokuwa wamefika siku hiyo.Sasa kumbe kuna washikaji zangu wale ambao nilikuwa nafanya nao kazi pale kijiweni wakawa wamefika hapo polisi kuniulizia,kutokana na kwamba hawakujua jina langu halisi nililokuwa nimepewa na wazazi wangu,wao wakawa wamemwambia yule afande aliyekuwa zamu ya kwamba natambulika kwa jina moja la "Mzee wa kuzugia".Basi bana yule afande baada ya kuniuliza maswali kadhaa pale na kujiridhisha akawa amenifungulia ule mlango,kiukweli nilipotoka mle ndani nikakutana na hewa safi ya nje ya kile chumba,nilitamani kabisa nisirudi mle ndani lakini sikuwa na namna!.

Nilipofika pale mapokezi,niliamriwa nikae chini,sasa yule jamaa yangu Nyamori akawa amekuja na wadau wangu wengine wawili huku wakiwa wamebeba mkate na soda ya fanta orange!.Haikutakiwa kabisa nisimame,kama ni kuongea walipaswa kuongea kwa nguvu na mimi niwajibu nikiwa pale chini!.

Nyamori "Mwanangu vipi?"

Mimi "Mwanangu wee acha tu"

Mimi " Hebu wanangu kama mnaweza hakikisheni mnafanya mpango nitoke halafu hayo mengine tutaongea huko nje!"

Nyamori "Usijali kaka haya mambo huwa ni kawaida kwa wanaume,chukua mkate na soda upunguze njaa"

Basi kabla sijapewa ule mkate,yule afande akaamuru ufunguliwe kutoka kwenye mfuko na ukaanza kuchambuliwa kipande baada ya kipande,alipojiridhisha akawaambia kila mmoja aliyekuwa amekuja kuniona achukue kipande kimoja kimoja ale na ile soda kila mmoja apige pafu!,baada ya dakika tano kupita akawa amenikabidhi mkate na ile soda na kutakiwa kula pale pale!.

Nilipomaliza kula tukawa tumeagana na wanangu nikachukuliwa nikarudishwa ndani ambako nilikuwa napaona kama jehanamu!.Japo Nyamori na washikaji zangu waliniletea soda na mkate wa kupunguza njaa lakini kiukweli nilikuwa sihisi njaa na wala sikuwa na hamu ya kula chochote kutokana na yale matatizo!.

Gabi "Alikuwa nani amekuja kukucheki?"

Mimi "Walikuwa washikaji zangu wa kijiweni!"

Gabi "Kwani walifahamu umedakwa?"

Mimi "Kuna muda nilimpigia simu mshikaji wangu kumjulisha"

Gabi "Ooh sawa!".


Ilipofika usiku kiukweli sikuweza hata kupata usingizi wa mang'amu ng'amu kutokana na joto kali lililokuwa likinasibishwa na harufu kali iliyo mbaya pamoja na mbu waliodhani mle ndani kuna sherehe!.Kiukweli nilipata tabu sana na ni moja ya siku ambazo sitokuja kuzisahau kabisa katika maisha yangu!.

Sasa asubuhi mida ya 2 kuna watu walikuja kutolewa mle ndani angalau kukawa na unafuu wa hewa!.Ilipofika mida ya saa 5 asubuhi niliskia jina la Gabi likiitwa na akawa ametika kisha akafunguliwa mlango akatoka.
Nilifahamu kabisa Gabriel uenda akawa amechomoka na mimi kuniacha mle ndani,kiukweli nilijisikia vibaya sana hadi machozi yakaanza kunitiririka!.Kibaya zaidi muda ulizidi kwenda huku nikijifariji labda nitaitwa lakini haikuwa hivyo!.

Sasa baada ya saa 1 kupita nikasikia naitwa jina langu!.-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-SEHEMU YA 9.


Nilifunguliwa lile geti nikawa nimetoka mle ndani.Yule askari aliyenifungulia alinichukia mpaka kwenye kile chumba ambacho jana tulifikishiwa baada ya kufika hapo kituoni!.Sasa nilipofika hapo nilimkuja jamaa mmoja aliyekuwa amevaa suti nyeusi,pembeni yake alikuwa amekaa Gabriel ila shemeji ambaye ni mke wa Gabi sikumuona!.

Afande "Kaa chini bhana hapa huwa hatusimami!"

Afande aliyeniambia nikae chini ndiye yuleyule aliyekuwa akituhoji ile jana na ndiye niliyemkuta kule nyumbani kwa Gabriel!.Basi mle ndani kulikuwa na ukimya wa muda fulani ambapo yule askari yeye alikuwa akiendelea kuandika huku kila mmoja akiwa kimya akimtazama.

Afande "Mkuu nadhani sasa tutawasiliana"

Jamaa "Sawa,haina tatizo!"

Basi baada ya hapo nikaambiwa na yule afande niende pale mapokezi nikachukue vitu vyangu nilivyokuwa nimekabidhi kabla ya kuingizwa Selo!.Baada ya kukabidhiwa vitu vyangu nakutoka nje,ndipo Gabriel akanitaka nipande gari iliyokuwa imepaki kando ya hilo jengo la kituo cha polisi na ilikuwa ni Toyota Prado nyeupe!.Basi nilipoingia ndani ya ile gari nikamkuta na demu wa Gabriel.

Yule jamaa aliyekuwa amevaa suti yeye alikaa mbele kando ya dereva halafu na sisi watatu tukakaa nyuma!.Gari ile iliondoka na tukaelekea nyumbani kwa Gabriel maeneo ya Buhemba!.Tulipofika tulishuka na kuingia ndani ambapo kila mmoja aliingia bafuni kuoga na kubadili nguo,sasa kwakuwa mimi nguo zangu zilikuwa Sirari,Gabriel aliniazima nguo zake nikavaa ingawa aliniambia nisimrudishie amenipatia kama ndugu yake!.

Baada ya hapo yule Bosi wa Gabriel alisema tutoke tutafute sehemu iliyotulia ili tupumzishe akili,sasa wakati tunatoka Gabriel akasema mkewe abaki pale nyumbani,sasa yule bosi wake akasema inabidi twende wote lakini Gabriel akakataa akasema yeye abaki na kama ni chakula angeletewa!.Basi tukawa tumeondoka kuelekea mjini!.

Basi baada ya kufika hotelini ile gari ikapaki na sisi tukashuka kuingia ndani!,baada ya kupata msosi wa nguvu ndipo kila mmoja akaanza kushushia vitu vyake,baada ya kupiga vitu niliona sasa Gabriel akaanza kuchamngamka!.

Gabi "Unajua yule mwanamke ni mpumbavu sana Bosi!"

Bosi "Nani!,Mkeo?"

Gabi "Aah! yule si mke wangu hata hivyo mi napita tu!"

Bosi "Kwanini unasema hivyo!"

Gabi "Kila siku naongea lakini yanapitia huku yanatokea kule"

Aliendelea "Ukiachana na hii ishu lakini nadhani unakumbuka kipindi kile Babati ilivyokuwa kaka!"

Bosi "Yeah!,sasa inabidi uwe makini maana serikali sasa hivi wako makini sana,sema ndiyo hivyo tunabanana na hawa askari,lakini kama sivyo ni hatari sana!"

Sasa mimi sikutaka kabisa kuingilia yale mazungumzo lakini nilichokuja kugundua ni kwamba,yule demu wa Gabi ndiye yawezekana alisababisha yale majanga kwasababu Gabi alikuwa amechukia sana na sikujua alisababishaje maana mimi hakutaka kabisa kuniambia na inaonekana si mara moja,yeye na huyo bosi wake ndiyo walikuwa wakifahamu,mimi kazi yangu niliifanya kwa uaminifu kabisa na sikuwa na longo longo!.

Sasa mpaka tunatoka pale polisi aliyesababisha sisi kutoka ni huyo jamaa ambaye Gabi alikuwa akimuita bosi,sikujua amefanya fanyaje hadi sisi kutoka lakini niliamini ilikuwa ni fedha inaongea maana jamaa alionekana alikuwa na hela hatari,na kitu kingine nilichokuja kukigundua baadae ni kwamba yule jamaa ndiye alikuwa akimpatia Gabi zile fedha!.Hii nchi kuna dili haramu nyingi sana lakini huwezi kukuta watu wanaohusika wanawekwa ndani,siye vinyangarakata tusio na mbele wala nyuma ukizingua kidogo tu,utafia gerezani!.

Bosi "Hivi uliniambia huyu jamaa anaitwa nani!?"

Gabi "Huyu anaitwa umughaka"

Bosi "Ooh sawa!"

Aliendelea "Sawa bana nyie fanyeni kazi kwa umakini,najua kwasasa hakuta kuwa na wanoko maana wale wajinga tushamalizana!".

Sasa wakati nikiwa naendelea kukung'uta vyombo nilikuwa nawaza namna ya kuachana na ile biashara kichaa japo ilinipatia pesa ya kutosha lakini niliona inaweza kuniingiza kwenye matazizo makubwa!.Baada ya kupiga vyombo na kuona vimenitosha niliwaaga wao ili mimi nijikatae kwenda Sirari!.

Gabi "Unawahi wapi wewe,wewe kaa utatindike beer,kwako utaenda tu!"

Basi baada ya kila mtu kuridhika siku hiyo tuliondoka,Gabi alinishawishi sana hatimae sikwenda Sirari nikaamua kwenda kulala kwake ili asubuhi anipatie fungu niondoke nalo kuelekea Sirari!.
Baada ya kutufikisha pale nyumbani yule Bosi na dereva wake wao waliondoka.

Namshukuru asubuhi niliwahi kuamka na ndipo nikaelekea sebuleni kumsubiri Gabi aamke anikabidhi pesa haramu ili mimi niondoke zangu,sasa shemeji ndiye aliyetangulia kuamka na kuja pale sebuleni.

Mimi "Mambo vipi shemu"

Marieta "Safi,za tangu jana

Mimi "poa kabisa"

Mimi "Jamaa bado kalala?"

Marieta "Ngoja nimuamshe"

Basi baada ya dakika 10 jamaa akawa amekuja pale sebuleni.

Mimi "Nataka kuondoka kaka,unaweza kunipatia mzigo?"

Gabi "We nenda tu nitakuletea huko,pia kuna jambo nikija tutazungumza"

Mimi "Poa,basi acha mi niwahi"

Gabi "Mida ya saa 10 jioni nitakupigia simu tuonane mahali"

Mimi "Poa kaka"

Baada ya mazungumzo yale mi nikamuaga jamaa nikaondoka zangu,sikujua ni kwanini jamaa alibadili maamuzi ile asubuhi kwasababu jana yake tulikuwa tumeongea akawa amesema asubuhi angenipatia hela lakini alibadilika.Yeye na huyo demu wake kiukweli baada ya hilo sekeseke inaonekana kabisa hawakuwa sawa na sikufahamu tatizo lilikuwa ni nin!.Sikutaka sana kuchimba na kuuliza uliza mambo ya ndani kwani ningeonekana mjuaji!,nilichoshukuru mimi ni kutoka nje na ile kesi iliisha!.


Baada ya kufika pale Sirari wanangu walitaka kufahamu ni kitu gani kilisababisha hadi kujikuta nipo mikononi mwa mapongo.Sasa sikutaka kuwaeleza ukweli ikabidi nifanye siri kabisa,nilichowaambia ni kwamba kuna mtu alikuwa akinidai na hivyo aliamua kunipeleka polisi,wao wakaamini hivyo kumbe haikuwa hivyo!.

Sasa ilipofika mida hiyo ya saa 10 alasiri,Gabi akawa amepigia simu na kweli akawa yupo pale Sirari na akaniambia tuonane kwenye ile bar tuliyokutana ile siku ya kwanza.
-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-


SEHEMU YA 10.
Niliondoka mdogo mdogo nikaelekea kwenye ile bar ambayo aliniambia ningemkuta hapo.Kweli,baada ya kufika hapo nilimkuta Gabi akiwa amekaa huku akiendelea kupiga beer yake pendwa ya Safari!.

Gabi "Uko poa?"

Mimi "Niko poa kaka"

Basi na mimi nikaagiza beer nikaanza kunywa huku tukiendelea kupiga stori za hapa na pale.Gabi bado alionekana kabisa kutokuwa na furaha tofauti na siku nyingine nilivyokuwa nimemzoea,yaani baada ya hilo sakata la sisi kukamatwa ni kama alikuwa hana mudi kabisa!.

Gabi "Mwanangu kwanza kabisa nikuombe samahani,maana jana tulishindwa kuzungumza kabisa kwasababu sikutaka kuzungumza mambo yetu mbele ya Eric(Bosi)"

Aliendelea "Vipi lakini uko Good?"

Mimi "Mimi niko Good kaka wala usijali"

Gabi " Unajua mwanangu asubuhi nimeshindwa kukupa hela kwasababu yule mwanamke amenikwaza sana"

Aliendelea "Hivi unajua yeye ndiye chanzo cha sisi kukaa ndani kaka!"

Mimi "Acha usiniambie kaka"

Gabi "Huwezi amini umughaka!"

Aliendelea "Usimuone na mitako ile ukadhani kichwani kuna akili,kichwani kabeba kamasi tu!"

Mimi "Mimi nilishangaa tu ananipigia simu ile juzi na akataka nije home kwako,lakini nilipokupigia simu yako kujiridhisha nikaona upo kimya kaka ndiyo ikabidi nije"

Gabi "Simu yako nilikuwa naiona lakini sikuweza kupokea kutokana ile hali ambayo nadhani uliikuta,isingekuwa rahisi!"

Aliendelea "Jambo la kushukuru tupo uraiani kaka,hayo mengine sidhani kama niyakutuumiza kichwa sana!"

Gabi "Unajua hiyo juzi nilikuwa nimetoka kuna mtu nilienda kuonana nae,sasa nikiwa huko nashangaa ananipigia simu akiwa analia,nikamuuliza kuna nini?,hasemi!"

Aliendelea "Ikabidi niwashe gari kurudi nyumbani maana nikadhani uenda wakurya wamemfanya kitu mbaya!"

Gabi "Ile nimefika ndani nashangaa nawekwa chini ya ulinzi,mwanangu hakuna siku nimemchukia yule mwanamke kama juzi!"


Aliendelea "Unajua mwanangu mimi nilikuwa mwalimu huko Babati sehemu moja inaitwa Haidomu,sasa kuna mambo mengi yalijizokeza hapo katikati hivyo nikawa nimetemana na uticha!"

Gabi "Sasa yule demu mimi nilifahamiana nae kipindi hicho hapo Haidomu,nikajikuta tunafahamiana na hatimae kuwa wapenzi!"

Gabi "Tumeishi kwa muda mrefu tu mpaka mimi kuja kufahamiana na Eric na ndiye akanipa mchongo huu ambao umenipa kila ninachokitaka,na huyu mwanamke anaelewa kila kitu kaka,siyo kwamba hajui!"

Aliendelea "Tukiwa pale babati,kuna siku sikachukua hela kaenda benki eti atumiwe kwenye akaunti yake!"

Mimi wakati huo naendelea kumsikiliza Gabriel tu na wala sikuwa mchangiaji!.


Gabi " Kibaya zaidi alichukua laki 5"

Mimi "Mbona zilikuwa nyingi sana"

Gabi "Kaka ninapokwambia hana akili siyo kwamba namdharau,hapana!,ni mwanamke wangu hilo nakubali lakini tatizo lake huwa hajiongezi,kila siku namwambia lakini haelewi!"

Aliendelea "Sasa alichokifanya Babati ndicho juzi ametaka kukifanya hapa,nimemuuliza ilikuwaje ananiambia eti alichukua laki moja kwenda kumtumia mtu kwa wakala,sasa inavyoonekana yule wakala baada ya kuzitambua zile pesa alipiga simu polisi"

Gabi "Na lenyewe lisivyokuwa na akili likabaki palepale mpaka wakalidaka!"

Mimi "Sasa kaka tutafanya kazi kweli kwa mazingira hayo?"

Gabi "Kaka nina mzigo!,we acha tu!"

Aliendelea "Sema tu kwamba hii ishu inamtandao mpana hivyo hata ukikamatwa kukaa ndani ni sekunde tu unakuwa umetoka"

Gabi "Sasa kitu ambacho nataka ufanye,nimekuja na mzigo na nitakukabidhi wote,wewe pambana mdogo mdogo na utakuwa unafanya kama tulivyokubaliana mwanzo!".

Basi ilipofika mida ya saa 1 usiku,Gabi akawa amenichukua kwenye ki-Corolla chake hadi nyumbani nilipokuwa naishi!,aliamua kushuka kabisa ili aingie ndani aone ninapoishi!.Sasa wakati anashuka akafungua buti ya gari akatoa begi ambalo siku zote alikuwa akihifadhia zile hela!.

Gabi "Kaka hapa kuna usalama kweli"

Mimi "Hapa kaka kila mtu na time yake,hakuna wakuda"

Gabi "Kama ndivyo basi hakuna shaka,jambo la muhimu ni wewe kuwa makini tu"

Basi baada ya mazungumzo,yeye akawa ameondoka na nikamsindikiza kisha akaniacha pale kijiweni na yeye akawa ameondoka kuelekea Tarime.Basi baada ya kuniacha hapo niliamua kurudi zangu geto kuzitathimini zile hela na kuzipangia mpango mkakati namna ya kuziingiza mtaani,nilianza kuzihesabu usiku ule ndipo nikapata jumla yake milioni 9.
Asubuhi kama kawaida kazi ya kuzingiza mtaani ikaendelea na nilikuwa nafanya kwa usiri mkubwa sana.Tangu lile jambo la kuswekwa ndani litokee sikutakaga kabisa kumwambia mshikaji wangu Mtatiro,niliamua kukaa nalo moyoni!.

Nakumbuka kila nilipokuwa nafanya kazi ikifika milioni 1,nilikuwa nampelekea jamaa chake na mimi kubaki nacha kwangu!.Kiukweli ile pesa japo ilikuwa haramu lakini ilikuwa tamu!.Kwa kipindi kile sikuona kabisa kazi nyingine ya kunipatia fedha nyingi na kwa haraka kama ile ya kubadili noti feki,japo nilijua ni kazi hatari lakini ilikuwa imenikolea mno!.

Sasa nakumbuka baada ya miezi kama miwili kupita huku nikiwa naendelea kukimbizana na zile hela hili ziishe niletewe nyingine,nikiwa pale kijiweni nikiendelea na kazi yangu ya upiga debe,kuna meseji ziliingia kwenye simu yangu kwa mfululizo!.Nilipochukua simu mfukoni na kutazama zilikuwa sms zilizokuwa zimetumwa na Gabriel!,basi ikabidi nifungue sms moja baada ya nyingine.

Sms 1 " Umughaka uko wapi?"

Sms 2 "Hizo hela unaweza kuzichoma moto muda huu?"

Sms 3 "Kama unaweza hebu ondoka kabisa hapo kwako na hizo hela"


Sasa baada ya kusoma zile sms kiukweli nilishituka sana,sasa nikakimbia kuweka vocha na kuanza kumpigia Gabriel lakini simu ikawa inaita tu haipokelewi!,baada ya kupiga sana akanitumia sms nyingine tena.

Sms "Nimekwambia kimbia kaka mambo yameharibika,tupo njiani tunakuja kwako!"


Aisee baada ya jamaa kuniambia wanakuja kwangu niliondoka nikikimbia kuelekea nyumbani kama kichaa,nilivuta picha umbali wa kutoka pale Tarime hadi Sirari nikaona kabisa kama gari ilikuwa na spidi kali,basi watakuwa wamebakiza hatua chache!.Nilipofika nyumbani nilifungua mlango kama vile mwizi,nilichukua lile begi nikavaa viatu nakutoka kisha nikaufunga mlango na kukimbia!.

Sasa kuna njia ilikuwa inakupeleka moja kwa moja mpaka mpakani(Mpaka wa Tanzania na Kenya),mimi nikaamua kuipita hiyo na sikutaka kwenda na ile njia kubwa ambayo ingetokezea kwenye lami kisha kijiweni.Nilikuwa nakimbia kama kichaa vile.

Baada ya mwendo mrefu kidogo nikajikuta nimeingia upande wa pili wa Kenya na sikutaka kabisa kuzubaa maana nilikuwa nimechanganyikiwa kabisa!.Sasa baada ya kufika ng'ambo ya pili ya upande wa Kenya pale mpakani Isebania,nilijaribu kuipiga ile namba ya Gabriel ikawa haipatikani!.Nilichokifanya nilichukua elfu 50 ya Tanzania nikaibadili pale mpakani kisha nikaenda stage(stand) nikapanda shuttle zilizokuwa zinakwenda Migori.

Sikufahamu nakwenda Migori kufanya nini lakini niliona bora kukimbia kuliko kukamatwa nikaozee gerezani,nilifahamu kile kitendo cha Gabriel kuniambia nikimbie kilikuwa ni kitendo cha hatari na uenda yeye tayari alikuwa mikononi mwa ndata!.
-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-SEHEMU YA 11.
Nililipa kiasi cha Ksh 50 kwenye Hiace(Shuttle) iliyokuwa ikielekea Kisumu na niliwaambia waniache Migori.Migori ni mji ambao ulikuwa ni mkubwa tu na hapo kabla sikuwahi kufika lakini katika stori za washikaji walikuwa wakidai ni mji ambao ulikuwa jirani sana na Isebania,nilichokua nimepanga ni kwamba nikifika hapo mji wa Migori nitajua cha kufanya,jambo la msingi ni kutoka kwanza hapo Sirari ambapo hali ya hewa ilikuwa imechafuka!.

Nikiwa kwenye gari nilikuwa nimekumbatia kile kibegi ambacho hakikuwa kizito na kiukweli nilikuwa kama nimepagawa na kuduwazwa na ile hali ya hofu niliyokuwa nayo!.Tulitumia takribani nusu saa mpaka dakika arobaini kufika hapo mjini Migori!.

Nilipofika nilishuka na nilitembea kuelekea juu kama narudi tena Sirari,sasa nilipofika kwa mbele nilikutana na jamaa nikamuuliza anielekeze ilipo Guest House ili niende nikapumzike,sasa kwa wale jamaa wao walikuwa wanaita Lodge,ulikuwa ukiuliza neno Guest House kidogo wanakushangaa,basi jamaa akawa amenionyesha Lodge moja ambayo haikuwa mbali na ile stage(stand).

Nilifika pale nikauliza vyumba nikaambiwa ni Ksh 350,nilichomoa hela nikawa nimempa kisha nikaonyeshwa chumba changu!.Kiukweli baada ya kuingia chumbani akili yangu ilitulia sasa!,niliingia bafuni kuoga na nilipomaliza nili lala sana na nimekuja kushituka ikiwa mida ya 12 jioni!,basi nikaamua kuamka ili niende kutafuta mahali walipokuwa wanauza msosi ili nitwange nirudi ndani,sasa nilijaribu kumuuliza yule jamaa wa pale mapokezi akawa amenionyesha kimgahawa ambacho hakikuwa mbali na lile eneo,sasa baadae nilikuja kufahamu kumbe mwenye ule mgahawa ndiye aliyekuwa mwenye ile Lodge!.

Nilipofika hapo Migori kiukweli kilichonichanganya ni namna ya kuitumia hela ya Kenya kiusahihi,kuna muda nadhani nilikuwa naibiwa kwasababu sikuwa na muda wa kuanza kuhesabu hesabu vichenji vilivyokuwa vinabaki!.

Sasa wakati natoka Sirari,kwenye lile begi nilikuwa na kiasi cha Tsh milioni 5,na sikufahamu nitazifanyia nini nikiwa hapo Migori!,Sasa asubuhi kulipokucha niliamka mida ya 4 asubuhi nikanawa uso na kupiga mswaki kisha nikaondoka kuelekea pale kwenye kile ki-mgahawa ili kupata chai!.Ule mgahawa ilionekana kwa lile eneo ulikuwa unauza sana kwasababu ile jioni na hata asubuhi nilipoingia nilikuta kuna watu wengi wakipata vyakula mbalimbali,sasa wakati nimeagiza chai na chapati nikiwa nasubiria,ghafla waliingia jamaa wawili wakiwa wamevaa makoti ya kijeshi na suruali za kijani huku wakiwa na bunduki!,nilipata hofu sana lakini nikawa mtulivu,sasa kumbe wale jamaa walikuwa ni askari wa Kikenya na ndivyo walivyokuwa wakivaa,haukupita muda waliongezeka na wengine wawili wakiwa na silaha kama wenzao!.Basi nao walikaa wakawa wameagiza chai wakaendelea kunywa!.

Muda huo nilijikausha kama sina habari na mtu,namshukuru Mungu pia na wao hawakuwa na habari na mtu!,walipomaliza walinyanyuka wakawa wameondoka,sasa nilikuja kugundua kumbe lile eneo nililokuwepo halikuwa mbali na kituo cha polisi hapo Migori na kituo chenyewe kilikuwa barabarani kabisa,niliona lile eneo si sahihi kwangu,hivyo nikapanga ikifika mchana niondoke lile eneo nikatafute Lodge nyingine ambayo itakuwa mafichoni kidogo!.

Kiukweli ile hela niliyokuwa nimebadili ilimalizika siku hiyo baada ya kutafuta Lodge nyingine iliyokuwa pembeni ya mji kama unaelekea Kisumu,sasa hofu ilianza kunijaa namna nitakavyoweza kusavaivu kwa kipindi chote nitakachokuwa huko!.

Ilipofika mida ya jioni nilitoka nikaelekea pale stendi kwa mguu na nilipofika jamaa walidhani ni abiria wakaanza kunichangamkia na niliwaeleza mimi si abiria,nilikaa pembeni kujaribu kuangalia namna wanavyofanyakazi lakini kila nikijaribu kuangalia mdau angalau nilete mazoea lakini hola!,kiukweli sikufahamu nitaishije yale mazingira ambayo sikuyazoea!.Utofauti niliuona pale stendi ni kwamba jamaa walionekana kujitahidi kuchangamka lakini bado washikaji na wahuni niliokuwa nikifanya nao kazi pale Sirari walikuwa wamewazidi wale wajaluo kwa uchangamfu!.
Basi siku hiyo niliamua kurudi zangu pale Lodge ambako nililala mpaka asubuhi,ilipofika mida ya saa 3 asubuhi nilitoka zangu nikarudi pale stendi kushangaa,sasa nikasogea zilipokuwa zinapaki gari za kuelekea Isebani,pale niliwakuta jamaa wanaongea kikurya hivyo nikajiona kabisa kama nipo Sirari,sasa kuna dogo alikuwa konda akiita abiria kwenye zile shuttle na alikuwa amevaa tisheti iliyokuwa na picha ya Chege na Temba huku ikiwa imeandikwa TMK WANAUME,sasa baada ya kumcheki kwa muda mrefu yule dogo ni kama alinivutia kwa namna alivyokuwa mchangamfu!,sasa baada ya kuitia ile shuttle na kujaza,nilimsogelea kutaka angalau mazoea nae ili ikiwezekana yeye ndiye aifanye ile kazi ya kubadili zile hela wakati nikiwa kule!.

Mimi "Mwanangu mambo niaje?"

Dogo "Ni bomba bro!"

Mimi "Una mrefu sana hapa eeh!"

Dogo "Yes bro tuko hapa kitambo!"

Sasa wakati naongea nae hakusita kuniuliza kama mimi ni Mtanzania maana ongea yangu na yake ilikuwa tofauti kabisa!.

Mimi "Unaitwa nani mwanangu?"

Dogo "Mimi naitwa Joe lakini wengi huniita Mkamilifu!"

Dogo "Na wewe bro majina yako nani?"

Mimi " Mimi naitwa Umughaka"

Dogo "Its your first time hapa Migori?"

Mimi "Hapana,huwa nakuja mara kibao tu!"

Dogo "Mi pia huwa nakwenda Sirare kwa jamaa zangu"

Sasa wao kwa kule badala ya kuita Sirari,wao walikuwa wakiita Sirare na hata shuttle zao zote za kuelekea Sirari zilikuwa zimeandikwa Sirare,nadhani ilikuwa ni lafudhi tu lakini walikuwa wakimaanisha Sirari!.Sasa dogo alionekana kupafahamu vizuri Sirari na hata maeneo baadhi niliyomtajia alionekana kuyafahamu!.

Sikutaka stori nyingi kwasababu sikuwa na hela ya kunivusha siku itakayofuata,nilitaka yeye ndiye akawe chambo wa kubadili zile hela na nilipanga endapo kikinuka basi ningechafua hapo Migori kuendelea kusonga mbele!.


Mimi "Hivi hapa ni maeneo gani wanabadili hela"

Dogo "Ooh kwani una haraka sana bro,huwezi subiri nimalize hii job then nikuonyeshe!"

Mimi "Sawa haina noma"

Basi dogo akaendelea kupambana na ile kazi ya kuita abiria mpaka akawa amejaza tena gari ya pili,hiyo ilikuwa mida ya saa 7 mchana!.

Dogo "Naweza kukuelekeza sasa"

Basi dogo akawa amenichukua mpaka kwenye jengo moja ambalo tukaingia ndani tukakuta maduka kibao,sasa mimi baada ya kuingia mle ndani kiukweli niliona siwezi kubadili zile hela kwenye mazingira yale kwasababu ningedakwa tu!.Sasa nilimchukua dogo nikatoka nae nje nikamwambia twende mpaka kwenye ile Lodge niliyofikia kisha nikamwambia nitamlipa hela ili kufidia muda wake!.Tulipofika kwenye ile Lodge nilimuacha dogo pale mapokezi nikamwambia anisubiri,nilifungua lile begi nikatoa laki moja kisha nikaitia mfukoni nikawa nimefunga kile chumba na kutoka nje!.

Mimi "Nakupa hizi hela naomba ukabadili sehemu nyingine tofauti na pale pa mwanzo kwasababu wale jamaa wanakata hela kubwa"

Dogo "Ok bro kuna jamaa mmoja yupo hapo ng'ambo nampelekea huwa ana-exchange pesa ya Tz,nikukute basi hapa"

Mimi "Nitakulipa vizuri ukifanya vizuri!"

Dogo "Sawa bro nikukute hapa,sa hii tu nakuja!"

Mimi "Uwe muaminifu"

Dogo "Ahahaha bro ndiyo maana nikaitwa Mkamilifu,we uliza watu wote kwa pale stage hakuna ambae hanijui!"

Mimi "Sawa nakusubiri".


Basi dogo alitoka akikimbia akielekea kwa huyo jamaa kubadili ile hela niliyompatia,ile hela kama nilivyosema hapo awali ya kwamba,ulikuwa ukiiangalia kiukweli hakukuwa na shaka yeyote kwamba ilikuwa ni pesa halali kwa matumizi,uenda kama ungeiweka kwenye mashine au ungekuwa na utambuzi wa hela feki ndipo ungeifahamu!.Nilipompa dogo ile hela nilikuwa nina mambo niliyokuwa nayafikiria kichwani,kama angekimbia basi kwangu isingeniuma kwasababu nilikuwa nazo za kutosha,na kama angefanikiwa kubadili basi ndiye angekuwa rafiki yangu kwa kipindi ambacho ningekuwa hapo,lakini pia kama wangemdaka nilipanga kutoweka kama kipanga!.

Basi baada ya kama nusu saa nikiwa pale nje,nilimuona dogo kwa mbali akiwa anakuja!.-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-SEHEMU YA 12.Niliendelea kumtazama dogo kwa makini asije kuwa anakuja na watu ili ikiwezekana nichukue hatua katika mbio!.Baada ya kujiridhisha ya kwamba alikuwa akija yeye mwenyewe nilikaa kwa kutulia nikiendelea kumsubiria!.

Dogo "Bro jamaa kasema akupatie ngapi!"

Mimi "Sijakuelewa!"

Dogo "Jamaa ameniambia waweza taka pesa ngapi kwa ile exchange!?"

Mimi "Kwani jamaa huwa anabadili kiasi gani kwa kila Tsh 10,000!"

Dogo "Sikia bro kwanini nisikupeleke kwa huyo mjamaa ukaelewane nae!"

Mimi "Jamaa anafanyia kazi zake wapi?"

Dogo "Yuko tu hapo ng'ambo na hata siyo mbali!"

Mimi "Hakuna wanoko?"

Dogo "Ati unasema aje!?"

Mimi "Hakuna tatizo nikienda kwake?"

Dogo "Wala hakuna problem yeyote,jamaa yuko fiti tu!"


Sasa baada ya mazungumzo na yule dogo kumbe alimuachia huyo jamaa ile hela na jamaa akawa amemwambia aje aniulize ili kujua kwenye ile laki mimi angenipatia kiasi gani,basi kiukweli niliogopa sana na nikaona uenda ulikuwa ni mchongo wa mimi kudakishwa!.Lakini nilipompeleleza yule dogo sana akaniambia jamaa anauza vifaa vya magari,hivyo pia huwa anabadilishaga na hela!.Basi ili kuonekana sikuwa na wasiwasi nikamwambia dogo tuelekee kwa yule jamaa!.Tulitembea kwa takribani dakika 4 tukawa tumefika kwa yule jamaa ambaye alikuwa na duka la spare za magari!.Kiukweli niliamua kujiamini na niliamua kuiweka hofu kando,sasa yule jamaa alikuwa ni mkenya ambaye alionekana kiswahili kukifahamu vizuri japo kuna muda pia alikuwa akichapia!.

Jamaa "Mambo vipi bro"

Mimi "Poa kabisa"

Jamaa "Ni wewe ndiye umemwagiza Mkamilifu?"

Mimi "Yes ni mimi!"

Jamaa "Oooh hapo iko poa,maana hata sikumuelewa"

Aliendelea "Ulitaka sasa bro nikupee pesa ngapi?"

Mimi "Wewe huwa unabadili kiasi gani kwa kila Tsh 10,000?"

Jamaa "Mimi bro nitakupea Ksh 3500!"

Mimi "Ok sawa haina tatizo"

Basi kimoyo moyo nilikuwa namshukuru Mungu sana kukutana na yule jamaa maana kiukweli kama angekuwa mjuaji pale nisingechomoka!.Jamaa aliingia dukani akawa amenipa Ksh 3500 ambapo na mimi nilimpatia yule dogo Ksh 500.Sasa jamaa akaniambia kama nilikuwa ninapesa nyingine nimpelekee maana baada ya siku mbili alikuwa anatoka!,sasa yeye alichoamini ni kwamba kupitia hela ile angejipatia faida mara dufu,kuna muda nilikuwa naona kabisa natenda dhambi lakini sikuwa na namna kwasababu mimi nilichotaka ni pesa tu!.

Jamaa "Bro kama uko na pesa ingine waweza tu niletea nikubadilishie!"

Kimoyo moyo nikasema "wewe humjui umughaka vizuri,ngoja nikuonyeshe mimi ni nani".Basi nilimwambia ningerudi jioni kuleta hela kiasi fulani anichenjie.Basi tuliondoka na dogo huku tukiendelea kupiga stori za hapa na pale,nilimwambia dogo anionyeshe maduka ya nguo ili ninunue sweta nivae maana kwa kipindi kile kulikuwa na baridi ya kiaina hapo Migori!.Baada ya kununua sweta mimi nilirudi lodge na dogo akaelekea kuendelea na mishe zake!.

Sasa ilipofika mida ya saa 12 jioni sikumuoma dogo nikajua uenda atakuwa ametingwa na majukumu,basi nikachomoa tena mle kwenye begi shilingi laki moja nikaelekea kwa yule jamaa.Nilipofika jamaa alinipatia Ksh 3500 kama kawaida na kiukweli alikuwa akinishangaa sana na alitaka kufahamu kwa Tanzania nilikuwa natokea maeneo gani,mimi nilimdanganya ni mwenyeji wa Mwanza!.Kama nilivyosema hapo awali ya kwamba,baada ya kujishughulisha na hiyo shughuli haramu hata muonekano wangu ulibadilika sana na ulikuwa ukiniangalia huwezi amini kama mimi ni mpiga debe pale Sirari!.Sasa baada ya jamaa kunipatia ile hela nililipa pale lodge pesa ya siku mbili nikawa nimebaki na pesa kadhaa!.Nilitaka nikae pale Migori ndani ya siku 3 halafu nigeuke zangu Sirari ili nikaone kama mambo yalikuwa yamepoa!.Niliamini ya kwamba kama jamaa angetoka akaenda kubadili zile hela halafu wakamshitukia basi najua angemtafuta dogo Joe akawaleta pale Lodge nikapata kashikashi,hivyo nilipanga nichomoke mapema kabisa!.

Sasa kabla ya kuondoka nilinunua begi dogo la mgongoni kisha nikanunua na suruali ya jeans moja nikawa nimebadilisha,zile hela niliziweka kwenye lile begi la mgongoni pamoja na ile shati niliyokuwa nimevaa siku naingia hapo Migori,ile sweta na jeans nikavaa nikawa sasa na muonekano mpya!.Sasa siku naondoka nilienda kuonana na yule dogo Joe pale stendi nikamkabidhi lile begi nikampatia na hela kiasi cha elfu 50 ya Tanzania,sasa ilikuwa ni juu yake kuzibadili ili aionjoi maisha,kama walidamka basi ni yeye na mungu wake!.

Nilipanda zangu shuttle za Isebania nikageuka zangu.Nilipofika pale Isebania nilishuka nikaingia zangu kitaani kupita njia isiyokuwa rasmi kuingia Sirari,ile njia walikuwa wakiipita watembea kwa miguu hivyo hakukuwa na bugudha toka kwa mamlaka zote mbili!.Ilijulikana ya kwamba watu wa Kenya wanapita kuingia Tanzania na watanzania walikuwa wanaingia Kenya kununua bidhaa na mahitaji.Sasa nilipofika hapo Sirari,sikutaka kabisa kwenda moja kwa moja nyumbani,nilianzia kwanza kijiweni!.Nilipofika pale niliwakuta wadau wangu wakiwa wanaendelea na kazi huku wengine wakishangaa na kuniuliza ndani ya siku mbili tatu hizo nilikuwa wapi!.Mshikaji wangu Nyamori sikumuona hapo kijiweni hivyo nikaelekea dukani kwa yule mama kununua vocha ili nimpigie simu.

Nilimpigia simu yake ikawa inaita tu bila kupokelewa,basi nilipoona haipokelewi nikaamua kuachana nae,sasa ikabidi nimpigie Gabriel,nilipoipiga namba yake ikawa haipatikani!,nikarudia tena lakini haikupatikana!.Sasa sikutaka kumtafuta kabisa yule mwanamke wake kwasababu nilikuwa nakifahamu kichwa chake kilivyokuwa kibovu!.Nia ya mimi kumtafuta Gabriel nilitaka kujiridhisha kama yuko hewani ili anieleze kilitokea nini siku ile,sasa nilipomkosa niliamua kupiga kimya!.Sasa wakati nikiwa naendelea kutafakari,kuna mshikaji alikuwa mdau hapo kijiweni nae alikuwa mpiga debe,huyu alikuwa akiitwa Magesa!.Sasa jamaa akawa ananiambia kuna jamaa toka juzi alikuwa akinitafuta hapo kijiweni na hata asubuhi ametoka hapo kuniulizia!.

Mimi "Jamaa yukoje?"

Magesa "Ni jamaa mmoja hivi tolu halafu blaki!"

Mimi "Alikuwa anasemaje?"

Magesa "Aisee hata sijui maana juzi ameshinda hapa na hata leo pia amekuja lakini hakukaa!"

Mimi "Alikuwa na gari?'

Magesa " Sijajua kama ana gari maana hapa hakuja na gari"

Baada ya Magesa kuniambia vile kiukweli moyo wangu ulilipuka tena kwa hofu,kwa namna alivyozitaja sifa chache za huyo mtu nilijiridhisha kabisa ya kwamba hakuwa Gabriel.Sasa baada ya muda kidogo nikiwa pale kijiweni simu yangu ikawa inaita,kuangalia nikakuta ni Nyamori alikuwa akinipigia.

Nyamori "Mwanangu ulikuwa wapi?,mbona simu yako ilikuwa haipatikani!"

Mimi "Mwanangu nilienda hapo Migori mara moja"

Mimi " Nipo hapa kijiweni lakini sikuoni!"
Nyamori "Mi nilitoka niko Nyamongo tangu jana,kuna mzee tumemletea ng'ombe hivyo nitarudi jioni au kesho asubuhi"

Aliendelea "Sasa sikia,kuna jamaa mmoja ni askari namjua,toka juzi anakusarandia hapo kijiweni Mwanangu"

Basi baada ya jamaa kuniambia vile sikutaka kabisa kupoteza muda pale kijiweni nikawa nimeondoka,sasa ndipo nikaunganisha na yale maelezo ya magesa nikaona kumbe bado kulikuwa na msako unaoendelea kimya kimya!..

Nyamori " Mwanangu kwani kuna ishu gani?

Mimi "Mwanangu bado ni ile ishu ya deni!".

Nyamori "Kwanini usimwambie mshikaji uwe unamlipa kidogo kidogo mpaka umalize ili aache kukusumbua!"

Mimi "Nitajua cha kufanya Mwanangu!"

Yeye hakufahamu kwamba ni lile dili haramu ndilo lilikuwa likiniangaisha,alichofahamu na nilichomwambia ni kwamba nilikuwa ninadaiwa!.

Basi nikaondoka zangu nikawa natembea haraka uelekeo wa Tarime ili nikapande gari nielekee Tarime mjini,sasa sikutaka kunyooka na lami,nilipita pembezoni mwa barabara ili nikifika mbele nidandie gari mpaka Tarime!.Wazo la kurudi tena pale geto kwangu sikuwa nalo kabisa na niliamua kama ni vitu ngoja viozee ndani lakini si kwenda kujikamatisha!.

Sasa namshukuru Mungu nilifika Tarime na niliamua kupita njia nilizokuwa nazifahamu kuelekea nyumbani kwetu ambako Mzee miezi michache iliyopita alikuwa amenitimua!.Nilipofika hapo nyumbani nilimkuta binti ambaye nilikuwa simfahamu na nilipomuuliza wenyeji wameenda wapi akawa ameniambia Mzee hajui alipo kwenda ila mama yangu alikuwa ameenda sokoni na dogo Amos yeye alikuwa shule!,sasa niliondoka mdogo mdogo kuelekea sokoni ambako mama yangu alikuwa akifanyia biashara zake!.


-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-SEHEMU YA 13


Mimi "Mama nyakuru Mwita"

Mama "Tata sabhoke"

Ilikuwa ni heshima na salamu ambayo nilimpatia mama yangu baada ya kuwa nimefika hapo sokoni kwenye meza aliyokuwa akifanyia biashara!.

Mama "Ulienda wapi baba?"

Mimi "Nilikuwepo tu mama!"

Mama "Mbona umenenepa hivyo,au umepata kibarua huko baba!?"

Mimi "Nabangaiza tu hivyo hivyo!"

Mama "Nilimpigia mama yako mkubwa lakini akaniambia uliondoka na akajua labda ulirudi nyumbani"

Mimi "Mama nilienda kupambana na maisha yangu!".

Mama "Sasa baba utaendelea kuhangaika hivi hadi lini,rudi nyumbani mimi niliongea na baba yako na akasema hayo yameisha"

Mimi "Mama kwa umri huu siwezi kukaa tena pale nyumbani"

Mimi "Nilipita tu kuwasalimia"

Mama "Ulipita nyumbani?"

Mimi "Nimeanzia huko ndiyo nikaja hapa"

Mama "Dada yako alikuja na amemaliza kuondoka wiki iliyopita!"

Aliendelea "Chukua namba yake utawasiliana nae alisema ukirudi nikwambie umtafute"

Basi baada ya mazungumzo na mama nilichukua ile namba ya dada yangu mkubwa(Sarah)kisha nikaondoka zangu!.Mama yangu mara zote alikuwaga rafiki yangu kipenzi,pamoja na lile seke seke la mzee lakini bado alitaka nirudi pale nyumbani kitu ambacho kisingewezekana kwa wakati huo!.Sasa wakati naondoka nilimpigia dada yangu simu ili kumjulia hali maana tangu nilivyokuwa nimemaliza shule sikuwahi kuongea nae kwasababu yeye alikuwa ameolewa huko Mwanza!.

Sasa baada ya kuongea na dada kwa dakika kadhaa alishangaa sana kwa kile kitendo ambacho mzee alinifanyia na alilaumu sana kwanini nilishindwa kumshirikisha kwa muda wote huo nikawa kimya!.

Da'Sarah "Sasa sikuhizi unafanya kazi gani hapo Tarime?"

Sikutaka kabisa kumficha kitu dada nilimwambia niliamua kuwa mpiga debe angalau maisha yaendeleee,alinishangaa sana ya kwamba nawezaje kuwa na elimu halafu niende kupiga debe!.

Da'sarah "Nilimwambia baba ukweli na kama ni kuchukia ngoja achukie,haiwezekani pesa anamalizia kwa mama yake Robina halafu sisi tunahangaika!"

Aliendelea "Kwahiyo sasa ulikuwa unakaa wapi?"

Mimi "Niliamua kupanga hapo Sirari!"

Da'Sarah "Ngoja nimwambie shemeji yako aje akutumie nauli uje huku"

Aliendelea "Na huyo mzee wala usimwambie chochote,muacheni na hela zake,yeye si anaona mama yetu hana maana!"

Mimi "Mimi nishamsahau na wala sihitaji hata kumi yake!"

Mimi " Halafu dada kama huko kuna sehemu ya kufikia hilo suala la nauli kwangu alinisumbui,we hata usimsumbue shem we kama inawezekana hata leo nianze safari"

Da'Sarah " Sasa hivi kweli kuna gari za kutoka hapo kuja Mwanza?"

Mimi "Hilo suala wewe niachie mimi,mimi nikifika nitakwambia"

Da'Sarah " Sawa wewe panda gari uje kama una nauli na ngoja nimpigie shemeji yako simu muda huo!"

Ile kauli ya Dada kunitaka niende Mwanza nikama ilinisaidia maana mpaka wakati huo nilikuwa sielewi hatma yangu!.Basi nilielekea mpaka stendi ambako nilikuwa nikitembea kwa umakini na tahadhari kubwa ili nisije kujikuta naangukia mkoni mwa mapongo,wakati huo begi langu lilikuwa na hela lipo mgongoni sikutaka kabisa kuliachia!.Basi nilipofika pale stendi nilidandia Hiace za Musoma ambako nilipanga nikifika pale Zero zero( Makutano) nisubiri gari zinazoenda Mwanza kutokea Musoma mjini!.Nilifika pale Makutano mida ya saa 9 alasiri na nikatelemka kusubiri gari za Mwanza.

Sikutaka kupandia gari za Mwanza pale Tarime mjini maana kulikuwa na wajuaji wengi hivyo nikawa naogopa kukamatishwa!.Basi haukupita muda nikawa nimepanda gari za Mwanza na nikawasiliana na dada nikawa nimemjulisha nishapanda gari!.,Kiukweli akili yangu mpaka wakati huo ilikuwa inawaza mambo mengi sana,sikujali ya kwamba Sirari nimeacha vitu vyangu wala nini,mimi nilichojali ni usalama wangu na kama ni vitu niliona ningevifata hali ambapo ingetulia!.

Sasa wakati nikiwa kwenye gari nilimtafuta mshikaji wangu Mtatiro ambaye niliamini yupo Mwanza na nilipanga nikifika Mwanza tuonane!.


Mimi "Mwanangu vipi?"

Mtatiro "Mwanangu umekuwa adimu sana kama mate ya nyoka!"

Mimi "Ahahahaa ahahaaa,nambie mwanangu"

Mtatiro "Nimekutafuta juzi kati ulikuwa hupatikani!"

Mimi "Kuna mahali nilikuwepo mtandao ulikuwa haushiki kaka"

Mimi "Nipo njiani mwanangu nakuja M-Z-A"

Mtatiro "Unakuja lini,leo!?"

Mimi "Yeah nipo njiani"

Mtatiro "Umefika wapi?"

Mimi "Tukaribia Kiabakari"

Mtatiro "Mimi sipo Mwanza mwanangu"

Mimi "Ulirudi Tarime?"

Mtatiro "Hapana,nipo hapa Bunda kuna ki mgodi kimetema ndiyo tupo na brother"

Mimi "Duuu!"

Mtatiro "Mwanza unaenda kwa nani?"

Mimi "Naenda kwa sista Sarah!"

Mtatiro "Mwanangu achana na habari za Mwanza kwanza,we kama vipi telemkia hapo Bunda mimi nitakufata uje tuone kama tutapata chochote"


Sasa Mtatiro alinishawishi hadi nikajikuta tena safari ya Mwanza kama imetoweka moyoni mwangu,nilichokuwa namshukuru Mshikaji wangu Mtatiro alikuwaga kila fursa haachi kunishirikisha kama rafiki yake,iwe haramu au iwe halali,kiukweli kwenye hilo sitamsahau jamaa yangu(Kwasasa anaishi Uganda).

Mtatiro "We mwambie Konda akushushe kituo kinaitwa Nyasura"

Aliendelea "Akikushusha hapo Nyasura ndiyo itakuwa jirani na huku nilipo!"

Mimi "Sawa"

Basi safari ikawa inaishia Bunda ingawa nilishalipa nauli ya Mwanza moja kwa moja,sikuona taabu kwasababu bado fungu nilikuwa nalo la kutosha.Ingawaje pesa niliyokuwa nayo ilikuwa haramu lakini ilikuwa inanipa kujiamini kwingi sana!.

Baada ya safari ya dakika kadhaa tukawa tumefika pale Bunda na mimi kushushwa hapo Nyasura kama Mtatiro alivyokuwa amenielekeza!.Basi nilimpigia simu Mtatiro nikamueleza ya kwamba nishafika hapo Nyasura,jamaa akawa amenitaka nipumzike sehemu aje kunifuata maana alipokuwepo yeye kulikuwa na umbali mrefu kidogo!.
-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-SEHEMU YA 14.Baada ya kumsubiri Mtatiro hapo Nyasura kwa muda hatimaye nae akawa amekuja akiwa anaendesha baiskeli,kiukweli kama kawaida nilipokuwa nikionana na jamaa yangu huyo utani wa hapa na pale pia furaha kwa kiasi fulani ilichukua nafasi.


Mtatiro "Mwanangu unazidi kung'aa tu,naona Tarime imekukubali"

Mimi "Aah wapi mwanangu ni kuridhika tu!"

Mtatiro "Vipi lakini kina Monche na washikaji wengine wazima?"

Mimi "Mwanao Monche sijamcheki muda mrefu,siunajua tena mimi zangu muda mwingi huwa ni Sirari tu!"

Mimi "Nadhani atakuwepo!"

Mtatiro "Jamaa huwa nampigiaga simu hadi leo haipatikani"

Mimi "Uenda atakuwa alibadili simu"

(Monche alikuwa ni yule dereva wa ile Hiace ambayo Mtatiro alikuwa akifanyia kazi kabla hajaondoka kwenda Mwanza,hivyo walikuwa washikaji).

Wakati tunaondoka hapo Nyasura kuelekea huko walipokuwa kina Mtatiro,tuliamua kutembea ili kuendelea kupiga stori maana ilikuwa ni muda umepita sijaonana na jamaa,ile baiskeli japo ilikuwa na Carier(sehemu ya kukalia)lakini tuliona ni vema tutembee huku mastori yakiendelea.Tukiwa njiani niliamua kumwambia ukweli Mtatiro mambo yaliyokuwa yamenitokea kwasababu ukizangatia ni yeye ndiye aliyekuwa ameniunganisha na Gabriel.

Mtatiro "Jamaa sijaongea nae muda sana"

Aliendelea "Kwahiyo mlichomokaje?"

Mimi "We acha mwanangu!"

Mimi "Kuna jamaa anaitwa Eric ndiye aliyetuchomoa"

Mtatiro "Aah Eric nammanya mwanangu"

Aliendelea "Yule jamaa ndiye mwenye ile michongo na hata Gabriel ni mpambe tu!"

Mimi "Jamaa watakuwa wamemdaka maana baada ya kutoka Migori nilimtafuta lakini hapatikani!"

Mtatiro "Zile mishe zina njuruku(pesa) lakini ni hatari sana mwanangu,kila muda unakuwa macho kodo kama popo!"


Mimi "Mwanangu ninao mzigo kwenye begi!"

Mtatiro "Acha utani wewe!"

Mimi "Kwanini nikutanie!"

Mtatiro "Hebu tuone mwanangu!"

Nilishusha kile kibegi toka mgongoni nikawa nimempatia Mtatiro akawa amefungua na kutazama zile pesa ili ahakikishe nilichokuwa nakisema kama kina ukweli!.

Mimi "Hizo nilikimbia nazo kuingia Kenya ndo zimebaki!"

Mtatiro "Mwanangu hizi mbona zitatoka,we subiri uone!"

Basi baada ya mwendo mrefu huku tukiendelea kupiga mastori,Mtatiro akanitaka nipande kwenye baiskeli ili apige pedo(aendeshe) kwasababu bado kulikuwa kuna umbali tulipokuwa tukienda!.Baada ya muda tukawa tumefika hapo Kijijini ambako aliniambia kulikuwa na mgodi umetema,kiukweli palikuwa ni kijijini ambako hakukuwa pabaya sana maana karibia huduma zile muhimu zilipatikana hapo!.
Tulifika kwenye mji mmoja ambao ulikuwa na nyumba mbili za nyasi,Mtatiro akawa ameingiza baiskeli ndani akanitaka niweke lile begi ndani,akafunga ule mlango na kufuli akawa ameniambia tuelekee hapo kwenye hicho kimgodi!.Baada ya kufika pale mgodini tulikuta raia wanapambana kuchimba mashimo,kuna wengine walikuwa wamechimba mashimo marefu kiasi kwamba walikuwa hawaonekani,kuna ambao bado nilikuta waking'ang'ana kuchimba huku mashimo yakiwafika magotini!.Kiukweli kulikuwa na watu wengi sana huku kina mama wakiwa wanahangaika kubeba vifusi kwenye makarai na ndoo wakirundika mchanga kila mtu kwenye eneo aliloona kwake litakuwa salama kabisa.

Mtatiro alinipeleka mpaka kwenye shimo alimokuwa kaka yake na jamaa mmoja wakiendelea kuchimba,ile kazi ya uchimbaji haikuwa ya kitoto maana kulikuwa na vikokoto mshenzi kama vyote.

Sasa kwakuwa nilikuwa hapo ili kujaribu bahati yangu kwa upande huo wa madini,baada ya kumpa Hi brother ake Mtatiro nilikamata ndoo nikawa nasogeza ule mchanga pembezoni ya lile shimo!.Ile kazi tuliifanya hadi mida ya saa 3 usiku ndipo yule brother akasema tuondoke tukapumzike halafu kesho yake tungedamka mapema kuendelea!.Kiukweli familia ya kina Mtatiro haikuwaga na mambo mengi,nilichokuja kugundua ilikuwa ni familia yenye upendo sana,sema ndiyo hivyo tu hawakujaliwa kuwa na pesa!.


Ukweli ni kwamba,jamii yangu ya kikurya ni jamii ambayo huwa ina upendo na kuwajali watu wengine pia,ukiachilia tu yale madhaifu madogo madogo kama wanadamu wengine lakini wakurya ni kabila bora sana miongoni mwa makabila bora kwenye hii nchi!,yale madhaifu madogo madogo ya kupiga mwanamke,kukeketa na kuchinjana ovyo yalikuwaga ni kwasababu ya ukosefu wa elimu tu,sikuhizi hayo mambo kwa Tarime yamepungua na kama siyo kuisha kabisa baada ya watu kuelimika!.Tarime ni njema sana na atakaye na aende akajionee!.(Nilikuwa nachomekea tu ndugu zangu).

Tulipofika hapo nyumbani kwakuwa tulikuwa wanaume tupu,tulikoka moto tukaanza kupika ugali ambao tulikula na dagaa zilizokuwa zimepikwa mchana!.Namshukuru Mungu kulipokucha asubuhi Mtatiro alinipatia nguo zake ambazo zilikuwa zimechoka ili nivae twende tukapige kazi!.Kiukweli nilipofika hapo mgodini hiyo asubuhi tulikuta nyomi la watu kila mtu akiwa anapambana kwa upande wake!.Kama kawaida na sisi tukaanza kazi iliyotupeleka hapo,nikiwa nimekaa nasubiri udongo ili niupeleke maeneo husika,simu yangu ilianza kuita,ile nimeitoa mfukoni na kutazama nikakuta ni Da'Sarah alikuwa akinipigia!.


Da'Sarah "Mdogo wangu uko wapi?"

Mimi "Nisamehe Dada jana sikuwa na Vocha nikashindwa kukwambia niliteremkia hapa Bunda!"

Da'Sarah "Bunda tena umeenda kufanya nini!?"

Mimi "Hivi wale watoto wa mzee Marwa bado unawakumbuka?"

Da'Sarah "Marwa yupi?,yule jirani?"

Mimi "Eeh"

Da'Sarah "Mi namkumbuka yule mwanajeshi tu Ryoba"

Mimi "Sasa yupo mdogo wao ambae ni rika langu na ni rafiki yangu anaitwa Mtatiro,nilipita kumsalimia kaka yake anaumwa,alinipigia simu jana nikiwa kwenye gari nakuja hivyo nikaona niteremke kuja kumjulia hali!"


Niliamua kumdanganya dada yangu sababu ya mimi kuteremka pale Bunda ni kwenda kumuona kaka yake Mtatiro ambaye alikuwa mgonjwa ili asiendelee kunifikiria vibaya!.


Da'Sarah "Kwahiyo unakuja lini Mwanza!"

Mimi "Najitahidi dada nitawahi"

Da'Sarah "Uwahi kuja maana niliongea na shemeji yako akaniambia kuna muhindi alikuwa anatafuta mtu wa kusimamia boti zake za uvuvi"

Aliendelea "Siyo tumpange mtu kumbe na wewe huko una mambo yako!"

Mimi "Sawa dada nakuja"


Baada ya yale mazungumzo kazi zikaendelea kama kawaida,sasa lile eneo lilikuwa maarufu sana kama Nyasana Mgodini,kiumweli ni eneo lililokuwa limechanganya sana lakini jambo la ajabu hakukuwa na madini wala nini,maana Mtatiro alikuwa ananiambia wao wapo pale ndani ya mwezi na hakuna walichoambulia zaidi ya kupoteza hela tu!.


Mtatiro "Mwanangu hapa napo ni hasara tu,kila siku mara utasikia kuna kimkanda kimepita hapa,watu wakichimba kwenye hicho kimkanda hawaambulii kitu!"

Mimi "Kwani mlianza kuchimba lini?"

Mtatiro "Mimi nimekuja mwezi uliopita,lakini kina braza hapa wana miezi miwili,ndani ya miezi yote hiyo hawajawi hata kupata punje ya dhahabu!"

Mimi "Duuu!,mbona ni hatari"

Mtatiro "Kuna jamaa wao ndiyo walidai kuna mkanda umepita chini kutokea Geita,sasa watu wote hawa unao waona wanapambana kuutafuta mkanda!"

Mimi "Hakuna watu waliopata dhahabu hata mara moja?"

Mtatiro "Watu wanadai wanapata pata kimtindo lakini ukijaribu kuuliza waonyeshe walizopata hata huonyeshwi"

Aliendelea "Nishamshauri braza tuachane na hii biashara kichaa lakini hasikii,yeye bado anaamini kuna madini"


Kama kuna sehemu watanzania huwa wanapoteza muda na kulishana matango pori ni kwenye vimigodi uchwara,yaani unakuta wanaamini eneo husika kuna madini huku wakiendelea kupambana kwa nguvu na kupoteza pesa lakini mwisho wa siku wanaambulia patupu,na ndivyo ilivyokuwa hapo Nyasana,kuna muda unawaangalia ndugu zetu watanzania wanavyohangaika hadi huruma kwakweli,lile eneo ilikuwa inasemekana dhahabu ililipuka tu na watu wakaanza kujaa kwa wingi na kuanza kuchimba,sasa sikujua kama kuna wataalamu waliwahi kupima uwingi wa dhahabu ulioko pale ama la!.(Sijui kama hadi leo huo mgodi unafanya kazi).

Kuna muda tulikuwa tunatoka na mtatiro tunaingia mtaani kule kijijini tunabadili zile hela,tulipoona chenji kijijini hapo imekuwa ngumu tulikuwa tunaelekea pale senta ya Nyasura kupambana na ubadilishaji wa kununua bidhaa halisi na kurudishiwa chenji halali!.Kiukweli ile hela ikabaki chache sana!.

Kuna siku tukiwa tumetoka na Mtatiro tukiwa maeneo ya Bunda mjini kwenye mishe mishe hizo,simu yangu ikapigwa ikiwa ni namba ngeni!.

Mimi "Halloo"

Yeye "Mambo Umughaka"

Mimi "Poa,nani!"

Yeye "Hebu acha utani,kwahiyo namba yangu ushafuta!"-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-SEHEMU YA 15.Mimi "Sidhani kama ningekuuliza kama ningekuwa nayo!"

Yeye "Jamani!,ila wanaume nyie hamuaminikagi kabisa!"


Aliendelea "Yaani umughaka leo nakupigia simu unaniuliza mi nani!"


Mimi "Hii line nime renew ile ya kwanza ilipotea!"

Yeye "Haya bhana,mi Leah"

Kiukweli ile sauti ya huyo mwanamke ilikuwa ni sauti mpya kabisa katika masikio yangu,mimi sikutaka mambo mengi nikawa nimeamua tu kumdanganya ya kwamba line ilipotea nika renew hivyo majina nayo yakaenda na maji,sasa aliponitajia jina la Leah ndipo akazidi kunichanganya kabisa kwasababu hakuna mwanamke niliyekuwa nikifahamiana nae akiitwa Leah.Nilikuwa nikijaribu kuvuta picha alikuwa ni Leah wa wapi lakini picha inakataa!,sasa nilifahamu uenda wakati nikiwa pale Sirari na washikaji wakati tunapiga mtungi kuna demu nimewahi kuchukua namba yake lakini kwasababu ya pombe nikashindwa kuisevu,niliamua kubaki na hiyo tafakari moja tu ya kwamba uenda tulikutana kwenye mabar huko!.

Sikutaka kumkatisha ili asijisikie vibaya,mimi nikaungana nae na kumpokea kwa kauli iliyoonyesha kumfahamu!.


Mimi "Oooh! za siku!?"

Yeye "Nzuri tu,uko wapi!"

Mimi "Nipo kijiweni"

Yeye "Mmh unanidanganya!"

Mimi "Kweli!,nipo kijiweni"

Yeye "Nimepita nikusalimie lakini sijakuona"

Mimi "Kwani we unajua mi nafanyia wapi kazi?"

Yeye " Tuachane na maswali mengi bhana,tuonane basi"

Mimi "Lini?"

Yeye "Leo kama itawezekana"

Aliendelea "Lakini leo sitaki kwenda Guest nataka kuja kwako"


Kiukweli nilijaribu kuvuta picha alikuwa ni mwanamke gani huyo lakini bado sikupata majibu yanayoeleweka!,lakini pia katika maisha yangu pale Sirari kwa wakati ule sikumbuki kama niliwahi kulala na mwanamke Guest,mimi nilikuwaga napenda kampani na washikaji tu na kunywa bia mbili tatu lakini sikuwahi kabisa kuwa addicted na masuala ya wanawake mpaka ifike steji ya kulala nao kwenye magesti,mademu wengi tuliokuwa nao wakati huo walikuwa ni mademu wa washikaji zangu na ndiyo wengi nilikuwaga na namba zao kama mashemeji zangu!.

Ile nyumba ambayo nilikuwaga nimepanga pia sikuwahi kabisa kumpeleka mwanamke wa aina yeyote,sasa ilikuwa ajabu kuongea na huyo mwanamke na kuniambia eti " Lakini leo sitaki kwenda Guest" kana kwamba hata hiyo gesti yenyewe nishalala na mwanamke!.Fedha yangu kubwa iliishia kwenye Misosi na Kupiga pamba,kiukweli hadi leo ndivyo vitu vinanilia hela na wala si wanawake!,sina hobby kabisa na mademu ingawaje ninaye demu mzuri tu wa kiwango cha kimataifa!.

Niliamua kumpigia mshikaji wangu Nyamori ili pengine anieleze uenda angekuwa anamfahamu yule demu lakini pia akasema yeye alikuwa amfahamu,pia nikampigia mwanangu Magesa nikamuuliza kuhusu jina la huyo demu nae akasema hamjui,nilijaribu kumpepeleza Magesa ili anifahamishe uenda kuna demu amewahi kuja kunitafuta pale kijiweni kwa siku za karibuni lakini jamaa akasema hakuna!.Sasa niliamua kumshirikisha Mtatiro lile suala ndipo akaniambia inapaswa niwe makini uenda mapongo walikuwa wakiandaa mtego wa panya ili wanidake kupitia mwanamke.

Mtatiro "Hebu nipe hiyo namba tuone"

Nikampatia Mtatiro ile namba akajaribu kuipiga,alipoipiga bahati nzuri ikapokelewa na mwanaume lakini mtu aliyepokea ilionekana alikuwa kwenye kelele kama za watu wengi hivyo hawakuweza kusikilizana!.

Mtatiro "Hii namba inabidi uachane nayo maana wajinga watakuwa bado wanakusaka"

Aliendelea "Tena huyo demu akipiga we usipokee mkatie kabisa"

Sikuwa na shaka na maelezo ya jamaa yangu Mtatiro maana ni mtu ambaye mara zote alikuwaga akinishauri sana!.

Nilichokifanya nilikopi majina yote muhimu kwenye ile simu na kisha nikatoa ile line ya simu nikaitupa,kesho yake nikaenda kusajili line mpya ya Airtel. Baada ya kuona hapo Nyasana mambo hayanilipi niliamua kumwambia Mtatiro ya kwamba mi inabidi nieleke Mwanza kwa sista.Mtatiro nae ni kama alikuwa keshakata tamaa ila braza ake ndiye alionekana kikwazo kwake!.

Mtatiro "Mwanangu mi namuaga kama akikata kuondoka namuacha yeye apambane,atajua mwenyewe!".

Mtatiro alitaka arudi na yeye Mwanza akaangalie ishu nyingine maana pale kijijini ni kama alikuwa akipoteza muda,sasa aliniambia hapo Mwanza kuna nyumba ilikuwa imejengwa na kaka yao mkubwa ambaye alikuwa mwanajeshi na ndipo alipofikia,na huyo braza ake aliyekuwa hapo Nyasana mgodini pia alikuwa akiishi pale na familia yake kwakuwa hiyo nyumba haikuwa na mtu!.

Baada ya Mtatiro kumwambia huyo braza ake waondoke maana hapo ni kama alikuwa akipoteza muda lakini jamaa alikuwa haelewi kabisa,yeye alikuwa akisema lile eneo kuna madini na atabaki kukomaa,sisi kama tunaondoka basi tuondoke na yeye tumuache!.Hatukuwa na namna ilibidi sisi tuondoke kuitafuta Mwanza.Sasa mpaka wakati huo zile hela feki zilikuwa zimebaki Tsh milioni 1.8,na ambazo tulikuwa tumechenji na nyingine kutumia zikabaki halali laki 4.Hivyo zote halali na feki zilikuwa Tsh milion 2.2.

Tulipokuwa hapo Bunda tulinunua nguo na viatu pia mara kibao tulikuwa tukienda hapo mjini kupata beer na kula vizuri,hivyo kujikuta hela zinazidi kupukutika!.

Nilipofika Mwanza niliamua kutengana na Mtatiro,mimi nilielekea kwa sista aliyekuwa akiishi Meko na Mtatiro yeye akaelekea huko Usagara!.Nilimpatia jamaa yangu hela kama laki 6,feki nilimpa laki 4 na halali nikampatia laki 2 ili angalau zimsaidie atakapokuwa huko!.

Baada ya kufika hapo kwa sista kiukweli sikutaka kabisa kukaa,sasa shemeji alikuwaga akitoka kuna siku alikuwa akimaliza hata wiki ndipo anageuka pale nyumbani!.Nilimwambia sista aongee na shemeji ili amwambie yule muhindi kama bado ile kazi ipo nikaifanye lakini kwa bahati mbaya jamaa akasema ishapata mtu muda mrefu tu!.

Kuna siku shemeji akawa ameniambia niende akanifundishe kazi ya kusimamia wavuvi wake kwenye ile mitumbwi yake ili nitakapokuwa na ujuzi wa kutosha awe ananiachia usimamizi na yeye kuendelea na shughuli nyingine,nikawa nimekubali maana sikutaka kukaa tu hapo kwa shemeji nionekane mzigo!.

Tuliondoka na shemeji tukawa kama tunaelekea Musoma,sasa tulipofika Magu tulishuka,kuna gari ilikuja kumchukua pale tukawa tumeondoka hadi kisiwani huko ndani ndani, kile kisiwa kilikuwa kinaitwa kisiwa cha Ijinga,Aisee nilipofika hapo nilikuta kuna mitumbwi kama uchafu,kuna ambayo ilikuwa imefungwa injini za Yamahama na Honda,pia ipo mitumbwi ambayo ilikuwa ya kawaida tu!.

Baada ya kufika hapo shemeji akawa amemuita jamaa mmoja wakaanza kuongea!.

Shemeji "Aisee nimewaongezea mvuvi"

Jamaa "Aaah ndo huyu bwana eeh!"

Shemeji "Eeeh bhana mfundisheni kazi ni shemeji yangu"

Jamaa "Sawa bosi wangu"

Nilibaki kuduwaa na kushangaa maana niliambiwa naenda kusimamia mitumbwi lakini baada ya kufika kibao kimebadilika na kuitwa mvuvi!.-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-


SEHEMU YA 16Shemeji yangu kiukweli alikuwa na pesa isiyokuwa ya kawaida,hakuwa tajiri sana kiasi ambacho kingemuingiza miongoni mwa matajiri wa pale Mwanza, lakini alikuwa na uwezo na utajiri wa size ya kati!,nyumba aliyokuwa anakaa yeye na mkewe(dada Sarah)ilikuwa ya kwake ambayo aliijenga kwa fedha yake mwenyewe,pia alikuwa akimiliki gari aina ya Nissan Patrol Nyeusi.

Pia alikuwa ni mtu fulani aliyekuwa na viprinsipo vyake ambavyo kama ulikuwa hujamuelewa ungeona kama ni mateso kuishi nae,pesa yake mpaka ifikie hatua umeila basi ilikupasa umenyeke sana na jasho likutoke sana!.Hivyo hata wakati ananipeleka pale mwaloni na kumwambia yule bwana kwamba ningekuwa miongoni mwa wavuvi,nilikuja kumuelewa baadae maana mwanzo nilidhani kama alikuwa akinishushia heshima na kunidharau!.

Kwakuwa tulifika mida ya hapo Ijinga mida ya saa 10 jioni,yeye bwana shemeji baada ya kuwapa maelekezo wale jamaa na kuwaachia alicho waachia,aliondoka akatuacha.Sasa nilipouliza jamaa ameenda wapi yule jamaa aliyenipokea akadai anaelekea kwenye miradi yake mingine ambayo hata sikuifahamu!.

Wakati nimefika hapo sikufahamu kumbe kuna eneo jamaa walikuwa wakiendelea na mapishi bhana,sasa jamaa niliyekabidhiwa kwake kama kama mvuvi alinichukua akanitaka tusogee pembeni kidogo ambako kulikuwa na kibanda cha mabanzi na nyasi,nilipofika hapo nikakuta kundi la watu 7 wakiwa na miili iliyokuwa imejengeka vizuri kimisuli!,jamaa walikuwa wamevaa bukta tu huku vifua vikiwa wazi.Mimi pamoja na kakitambi kangu kalikokuwa kameanza kuchomoza kwa ajili ya beer na fedha haramu,nilijiona kwa wale jamaa siyo kitu kabisa kwa namna walivyokuwa wamejazia misuli!.Jamaa mmoja wapo kwenye wale watu nilisikia anamwambia yule jamaa niliyekuwa nae ya kwamba "Waukae angalia usije ukalala njaa!".
Kumbe yule jamaa niliyekuwa nae hilo ndilo lilikuwa jina lake,sasa sikuelewa kama ndilo alilopewa na wazazi wake au lilikuwa jina tu alilopewa na wale jamaa!.

Waukae "Aisee kazi mpya hii!"

Jamaa 1 "Ooh karibu mwanangu,huku ndiko nyumbani kwetu!"

Jamaa 2 "Town tulishakusahau,makazi yetu ni pamoja na samaki mwanangu!"

Wakati huo walikuwa wamekaa wamezunguka sufuria kubwa lililokuwa limefunikwa kwenye sinia kichwa chini miguu juu!,kuna jamaa mmoja alinyanyuka akaelekea ndani kwenye kile kinyumba akatoka na samaki 3 wakubwa ambao walikuwa kambale,samaki wale walikuwa wa kuchoma!,kumbe wao walishindwa kula muda ule walikuwa wakipiga stori wakimsubiri huyo Waukae.Jumla yetu pale ikafanya tukawa watu 9.

Tukauzunguka ule ugali lile sufuria likafuniliwa,aisee sikuwahi kushuhudia ugali wenye ukubwa ule toka nizaliwe,hiyo ndiyo ilikuwa mara ya kwanza kuona ugali uliokuwa mkubwa kwa kiwango kile,wale samaki wakaweka chini kwenye mfuko na kazi ya kuanza kufukuzana na matonge ikaanza rasmi!,mimi nilikula sana samaki kwakuwa nilikuwa nina hamu nao sana maana wakati nikiwa Sirari chakula changu kikubwa ilikuwa nyama na kichuri!.

Baada ya kushiba nilijisogeza kando nikawaacha jamaa wakiendeleza libeneke!.

Jamaa 1 "Mwanangu mbona unakimbia"

Mimi "Mwanangu niko fiti!"

Jamaa 2 "Huyu hana njaa muda bado!"

Ile kauli ya yule jamaa wa pili sikuielewa kwa wakati ule lakini kwa baadae ilikuwa na maana kubwa sana kwangu!.Niliondoka nikaelekea ziwani kwenda kunawa mikono!..

Walipomaliza kula ugali ambao haukubaki hata punje,ndipo kila mtu alinyanyuka na kuendelea na mambo yake,mimi niliendelea kushangaa kwa kuwa ndiyo ilikuwa mara yangu ya kwanza kufika ziwani kabisa na kusogelea maji ya ziwani,mara zote nimekuwa nikiliangalia lile Ziwa Victoria kwa mbali tu na sikuwahi kabisa kulisogelea kwa karibu hadi kuyagusa maji yake!.

Ilipofika mida ya saa 12 jioni niliona wale jamaa wakianza kubeba nyavu pamoja na makarabai na kupelekea kwenye ile mitumbwi,Zoezi lile lilifanyika kwa haraka na ndipo wengine wakawa wanavaa masweta na nguo za kazi,kuna jamaa wengine wao walibaki kama walivyokuwa tu hapo awali!.

Baada ya muda giza nalo likaanza kutanda,ndipo Waukae akawa ameniambia nivue suruali nibaki na bukta pamoja na tisheti kisha nizame kwenye mtumbwi!.

Sasa kumbe ili mitumbwi mingine mingi niliyoiona ilikuwa ya watu wengine,wale jamaa tuliokuwa nao pale tunakula,waliokuwa wafanyakazi wa shemeji walikuwa 4,hivyo ukiniweka mimi pamoja na Waukae tulikuwa jumla 6,wale wengine walikuwa wa mitumbwi mingine!.

Tuligawana watu watatu kwa kila mtumbwi na kisha ikawashwa tukaondoka!.Hakuna siku ambayo sitokuja kuisahau kama hiyo maana ndiyo ilikuwa siku yangu ya kwanza kupanda mtumbwi pia ilikuwa siku ya kwanza kusafiri ziwani,muda huo kiukweli ziwa lilikuwa limetulia sana na hakukuwa na mawimbi.Baada ya mwendo mrefu kuelekea katikati ya ziwa Victoria,nilikuwa nikigeuka nyuma naziona taa za pale kijijini mwaloni kwa mbali sana,pia kwa umbali ule ilifanya tukawa tunaona mianga ya taa kutoka vijiji vingine vilivyokuwa kando ya ziwa!.
Baada ya kufika walipoona panawafaa kushusha nyavu,zile boti zikawa zimezimwa na kulikuwa na utulivu wa hali ya juu,mawazo yangu yalikuwa yanakwenda mbali zaidi na kujikuta nawaza endapo tukizama itakuwaje,lakini kwa upande wa wale jamaa wao hawakuwa na hofu kabisa!.

Zile nyavu zikaanza kushushwa taratibu kutoka kwenye ile boti yetu,nyavu zilipokwisha kushushwa zote,ndipo nilimuona Waukae anachukua kopo moja kubwa la Toss(ambalo lilikwisha sabuni) lilikuwa na maji ndani yake akalifungua kisha akawa anachota yale maji kwa mkono kisha anayatupa ziwani huku akinuia jambo fulani!,sasa kwakuwa nilikuwa mtu mzima niligundua ya kwamba ile ilikuwa ni dawa na alichokuwa kuwa anafanya ni kama vile walipewa masharti na mganga,lile jambo lilikuwa likifanyika siku zote ambazo nilikuwa hapo Mwaloni na ilikuwa ni lazima lifanyike!.Na hata ule mtumbwi mwingine pia lilifanyika jambo hilo!.

Baada ya hapo tulitulia humo ndani ya mitumbwi hadi mida ya saa 10,sasa mimi nilifahamu ya kwamba tukishatupa zile nyavu tungerudi mwaloni hadi kesho yake ndipo kazi ifanyike kumbe haikuwa hivyo!.Ilipofika hiyo mida saa 10 ndipo sasa tukaanza kuvuta zile nyavu!,nilichokuja kugundua ni kwamba,wale jamaa hawakujazia ile miili yao misuli kwasababu ya kunyanyua nondo(vyuma vya Gym)bali walijaza kwasababu ya kuvuta zile nyavu!,aisee asikwambie mtu,ingawa kulikuwa kuna baridi na hali ya hewa isiyokuwa ya joto lakini mimi nilichuruzika jasho kama nilikuwa nakimbizwa!.

Mahala popote ukiwa unawaona wavuvi nakuomba wapigie saluti,ile kazi haikuwa ya kitoto kama watu wazaniavyo!.

Basi baada ya kuvuta zile nyavu kwa muda,ndipo na samaki nao waliokuwa wamenaswa na zile nyavu wakaanza kujitikisa na kurukaruka!,kwa upande wangu niliendelea kushangaa sana kwasababu ilikuwa ni kitu kipya!.Hiyo siku tulipata samaki wengi sana na kitu ambacho niliendelea kukishangaa sana ni kitendo cha kumvua samaki aina ya Sangara mwenye ukubwa na kimo kama cha mtoto wa miaka 6.Niliuliza nikaambiwa huyo ni cha mtoto,kuna siku huvuliwa Sangara mwenye kimo cha mtu mzima ingawaje huwa ni mara chache lakini hutokeaga!.

Ilipofika mida ya saa 12 asubuhi baada ya kuifanya ile kazi kwa muda mrefu,mashine ziliwashwa na kurudi mwaloni huku tukiwa na rundo la samaki wakubwa na wadogo!.Tulipofika Mwaloni tulikuta kulikuwa na gari kubwa ambalo lilikuwa rasmi kwa ajili ya kubeba na kuhifadhi samaki!.Haukupita muda nikawa nimemuona na shemeji pia!.

Tuliwashusha wale samaki kwenye chombo kisha wakawa wanapimwa uzito,waliokuwa wakubwa wa size iliyotakiwa waliipakiwa kwenye ile gari,na waliobaki waliwekwa kwenye madumu kisha kuna land-rover lilikuja kuwachukua!.

Baada ya kuifanya ile kazi kwa muda wa mwezi mmoja nikaanza kuizoea,sasa kuna siku nikawa napiga mastori na Waukae ambaye tayari alishakuwa mtu wangu wa karibu sana!.Wao ilipofika mwisho wa Mwezi walikuwa wakilipwa kwa makubaliano walioyafahamu wao,lakini sikulipwa chochote,sasa nikafahamu uenda shemeji atakuwa hela yangu anampatia Dada yangu uenda alidhani kwa pale kijijini ningeitumia vibaya,kilichokuwa kinanisaidia ilikuwa ni ile hela yangu ambayo bado nilikuwa nayo.

Waukae "Unadhani bila vile utapata samaki!?"

Aliendelea "Utarudi na mitumbwi ikiwa inakukodolea macho!"

Mimi "Kwahiyo ni kila mtu mwenye mtumbwi anafanya?"

Waukae "Ni ujanja wako tu,wapo ambao wanamtegemea Mungu lakini huwa hawasaidii wanaishia kupata hasara na kuuza injini!"

Mimi "Kwani Injini inauzwaje!"

Waukae "Injini ipi sasa,maana kuna hiyo Yamaha na Honda!"

Mimi "Kwani zinatofautiana bei!?"

Waukae "Hiyo Yamaha ina bei yake na Honda pia ina bei yake"

Mimi "Nzuri ni ipi kaka?"

Waukae "Yamaha ina sipidi ila Honda ina nguvu na hata bei yake imesimama"

Ile mitumbwi ya shemeji yeye alikuwa amefunga injini za Honda,lakini mitumbwi karibia mingi ilikuwa na injini za Yamaha!.

Waukae "Yaani hapa bila dawa unadhani unatoboa!"

Aliendelea "Hivi Masangara ni shemeji yako kabisa eti!"

Mimi "Masangara ndiyo nani?"

Baada ya kuuliza Masangara ndiyo nani yule jamaa akaanza kucheka sana kana!.
Waukae "Sisi tunamjua kwa jina la Masangara"

Mimi "Ni shemeji yangu ila hilo jina sikuwahi kulifahamu"

Waukae "Huku watu wanamjua kwa jina hilo"

Waukae alikuwa ni msukuma bila hata kuuliza kwasababu ongea yake na rafudhi yake vilitosha kukuaminisha pasipo shaka!.

Baada tena ya kupiga kazi kwa mwezi mmoja uliofuata wenzangu wakalipwa hela nzuri tu lakini kwangu ikawa hola!.Sikuelewa sababu za shemeji kutokunilipa ilikuwa ni nini wakati nilikuwa nafanya kazi sawa na akina waukae!.Niliamua kuweka vocha kwenye kiswanswadu changu na kumpigia Dada Sarah na kujifanya namsalimia ili nione uenda angeniambia shemeji huwa anamuachia hela yangu!,baada ya mazungumzo nikaona yuko kimya sikutaka kumuuliza maana niliona nikimuuliza na akajua kumbe mumewe anipatii chochote kitu ningewachonganisha,hivyo nikaamua kukaa kimya!.

Ndani ya mwezi huo nilipokuwa nimejifunza na kuielewa ile kazi na namna ilivyokuwa inapesa ndefu,niliamua kumpigia simu Maanangu Mtatiro.


-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-
SEHEMU YA 17.Mtatiro "Mwanangu mimi unadhani kwanini sitaki kukaa kwa ndugu!"

Aliendelea "Tatizo ukiongea unaweza kuonekana mbaya wakati unadai chako"

Mimi "Nakomaa sana mwanangu na huku kuna baridi kishenzi,lakini jamaa hilo halioni"

Mimi "Ngoja niangalie hali itakavyokuwa nikiona miyeyusho nachafua!"

Mtatiro "Wewe ukiweza njoo tukapambane minadani mwanangu!"

Aliendelea "Kuna hela nasubiri braza anipe nianze kukimbizana minadani!"

Aliendelea "Kwani ule mzigo uliisha kabisa?"

Mimi "Bado upo kaka lakini kidogo"

Mtatiro "Kama ngapi imesalia!"

Mimi "Ipo kama laki 6"

Mtatiro "Hapo ukichenji utabaki na kasalio kidogo,hebu ngoja wiki hii nicheki braza akinitumia tuangalie tusepe wapi!"

Mimi "Poa mwanangu!"

Yalikuwa ni maongezi kati yangu na rafiki yangu wa damu Mtatiro,huyu jamaa alikuwaga zaidi ya ndugu,mambo yote muhimu nilikuwa nikimshirikisha na yeye pia alikuwaga akinishirikisha mambo yake,nilipokuwa nafeli aliumia sana kama ndugu kwasababu tulipendana sana!.

Basi niliamua kupambana na ile kazi ya uvuvi lakini ilifika mahali nikakata tamaa kutokana na kutopata malipo,niliendelea kusubiri uenda ningepewa ile kazi ya usimamizi kama nilivyokuwa nimeahidiwa lakini ikawa hola,niliamua kuwa mvumilivu maana ndani ya mwezi huo rafiki yangu Mtatiro yeye alianza kazi ya kuuza mitumba huko minadani lakini mimi nikamwambia ngoja kwanza nisikilizie hali itakavyokuwa.

Sasa nakumbuka siku moja nikiwa hapo ziwani nimepauka sina hili wala lile,simu ya Mtatiro iliita nami nikaipokea!.

Mtatiro "vp mwana?"

Mimi "Shwari mwanangu"

Mtatiro "Bado upo mwaloni?"

Mimi "Bado nakomaa mwanangu!"

Mtatiro "Mwanangu leo Gabriel amenipigia simu!"

Mimi "Acha utani mwanangu!"

Mtatiro "Kweli mwanangu kwanini nikutanie!"

Mimi "Duuu!,jamaa yupo uraiani?"

Mtatiro "Kwanza anakuulizia kinoma!"

Aliendelea "Nimemwambia uko Mwanza na anasema anakutafuta sana upatikani,nikamwambia Umughka alishabadili namba siku nyingi"

Mimi "Jamaa anasemaje sasa"

Mtatiro "Hatujapiga sana stori maana alikuwa anakuulizia sana,ila ameniambia anakuja Mwanza na amesema tufanye juu chini tuonane!"

Aliendelea "Mwanangu leo nipo hapa Katoro nilikuja kuleta mzigo ila jioni nageuka Mwanza!"

Mimi "Vipi kazi inalipa!"

Mtatiro "Watu wa huku wanavaa sana maspesho mwanangu,yaani najilaumu kuchukua hii mitumba!"

Aliendelea "Ila wapo wanaonunua tu kiaina!"

Aliendelea "Nikirudi jioni Mwanza nitakucheki"

Mtu niliyekuwa nikiunga bando napiga nae stori nyingi alikuwa ni mshikaji wangu Mtatiro pamoja na wanangu wa Tarime!.Kiukweli baada ya kuona mambo hapo mwaloni yanakuwa magumu niliamua kuondoka kurudi kwa sista ili nione la kufanya,sikutaka kuendelea kukaa sehemu ambayo nilikuwa nikifurahia kula samaki na ugali wakati mfukoni hakuna chochote,nilishazoea kushika hela kwa sana tu kwa wakati huo,kile kitendo cha shemeji kunifanyisha kazi ya uvuvi kwa takribani miezi mitatu pasipo malipo sikukiafiki hata kidogo.Nilipofika kwa sista sikutaka kumwambia kwamba mumewe alikuwa hanilipi ili kujiepusha na uchonganishi,nilifahamu uenda ningemwambia pengine angenihisi mimi ni mvivu tu ambaye sipendi kufanya kazi na nishazoea kuzurura!,hivyo nikaamua kupiga kimya!.

Nilipotoka kule mwaloni Magu niliondoka tu kama naelekea mjini Magu na ningerudi baadae lakini haikuwa hivyo,hakuna mtu niliyemuaga maana wao walidhani nafika tu mjini halafu ningerejea!.Sasa kuna muda shemeji alikuja pale nyumbani kutoka huko kwenye shughuli zake na akashangaa kuniona pale akidhani uenda muda ule ningekuwa mwaloni!.

Hiyo ilikuwa ni baada ya kupita siku 3 baada ya mimi kutoka huko!,jamaa alikuwa amechukia sana lakini nahisi alishindwa kuongea sababu ya mkewe,mimi ile hali niliiona na kwasababu nilikuwa mtu mzima niliamua kujiongeza ili kuepusha mambo mengi!.Haiwezekani nikufanyie kazi miezi yote hiyo ushindwe kunilipa halafu bado niendelee na kazi!,yeye alidhani mimi kwenda kwake ndiyo sasa aanze kunitumikisha kama punda,nilikuja kugundua kumbe hata lile suala la kumwambia sista kwamba kuna muhindi alikuwa akihitaji usimamizi kwenye mitumbwi yake zilikuwa ni fiksi tu,hakukuwa na muhindi wala bibi yake na mihindi!.

Nadhani mwanzo kama mtakumbuka nilisema ya kwamba,ninao ndugu kibao tu hapa mjini Dar es salaam lakini huwa nawapotezea kwasababu wengi wao wanajifanya matawi ya juu huku wakiwa na nyodo pamoja na dharau kibao!.,Huyo shemeji na dada yangu kwasasa wanaishi Dar es salaam lakini sijawahi kuthubutu kukaanyaga kwao kwasababu jamaa ana roho mbaya mno!,simsemi vibaya lakini hapendi ndugu wa mwanamke!,Maza mwenyewe alishakata miguu kuja kwa binti yake baada ya kuona hali ya jamaa anavyokuwa akitembelewa na ndugu wa mke!.Mimi nampenda sana jamaa kama navyowapenda watu wengine na namuheshimu lakini sitaki kabisa kujishobokesha,napambana tu kivyangu,nikiwaga nina shida za hapa na pale huwa nina wasiliana na sista basi inatosha!.

Basi baada ya kuona yale mazingira sitoyaweza,nilimwambia dada yangu kuna mahali nimeona nikajaribu maisha kwasababu yale maisha ya kisiwani yamenishinda!.Dada aliamini ni kweli maisha ya kule yamenishinda lakini kiukweli haikuwa hivyo!,niliamua nifunike kombe mwanaharamu apite!.

Kweli!,Dada yangu nakumbuka alinipatia shilingi laki moja na akaniambia nikiwa napata tatizo niwe namjulisha!.Nilimpigia mshikaji wangu Mtatiro akawa ameniambie nipande gari za kuelekea Usagara nitamkuta ananisubiri maeneo yale!.
Nilifanikiwa kufika na nikamkuta Mtatiro ambaye tuliongozana nae mpaka kwenye nyumba ya kaka yake aliyokuwa akiishi yeye na familia ya kaka yake tuliyemuacha Bunda akikomaa na madini!.Ile nyumba ilikuwa na braz ake aliyekuwa mwanajeshi wakati huo huko Kigoma!.

Siku nazo hazikuganda zikawa zinapepea kama upepo,sasa nakumbuka siku moja tukiwa katika mihangaiko mnadani kwenye kijiji kimoja kilichopo huko Geita kinachoitwa Nzera,nikapigiwa simu na mshikaji wangu Magesa ambaye aliniambia ya kwamba,yule mzee aliyekuwa akimiliki ile nyumba niliyokuwa nimepanga pale Sirari amekuwa akienda pale kijiweni kunitafuta bila mafanikio,sababu ya yeye kunitafuta ilikuwa ni kuhusu kodi yake ya nyumba,nilichofanya nilimwambia Magesa kama anaweza aende anihamishie vile vitu na ningevikuta kwake kwasababu yeye alikuwaga amejenga japo nyumba ilikuwa kama pagale tu maana kuna vyumba vingine vilikuwa havijaisha!.

Mimi "Mwanangu nitakutumia hela ya kubebea wewe nisaidie nitavikuta kwako!"

Magesa "Kwani huko ulipo utachukua muda mrefu?"

Mimi "Naweza kuchelewa kaka,ndiyo maana nakuomba unisaidie!"

Mimi "Unavyoweza kuvitumia wewe tumia kaka ilimradi visiaribike tu!"

Magesa "Sawa haina noma,we kama itawezekana nitumie hela ya usafiri nitavifata!"

Baada ya yale mazungumzo niliendelea kupiga mwano kuita wateja wa kununua mavazi pale mnadani!.

Sasa baada ya mwezi kukatika baada ya mimi kuanza kuifanya ile shughuli ya uuzaji wa mitumba huku mimi na Mtatiro tukiendelea kuzunguka katika minada mbalimbali huko vijijini,siku moja Gabriel alimpigia simu Mtatiro na akawa amesema inapaswa tuonane haraka!.

Kweli,baada ya kutoka kwenye mnada mmoja huko Sengerema tuliamua kesho yake hatutoenda mnadani bali tungeenda kumuona Gabriel.Kesho yake mida ya saa 4 asubuhi tuliondoka kuelekea Nyakato ambako Gabi alikuwa amemwambia Mtatiro tukifika hapo tumwambie!.

Tulipofika Mtatiro alimpigia simu Gabi akawa amemwambia tumefika hapo Nyakato,jamaa alimwambia tusubiri hapo kuna gari ilikuwa inakuja kutuchukua.

Hazikupita hata nusu kuna jamaa akawa amempigia simu Mtatiro akimuomba amuelekeze mahali tulipokuwa tumesimama ili asogee kutuchukua,baada ya maelekezo tukaona Gari land cruiser hard top la njano likiwa na vioo vyeusi likisimama na dereva akitufanyia ishara ya kutakiwa tupande tuondoke!.-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-SEHEMU YA 18.Muda si mrefu tulifika kwenye nyumba fulani ambayo ilikuwa ndani ya geti,geti lilifunguliwa ndipo tukazama ndani.Dereva yule aliteremka akawa anatuongoza kuelekea ndani.Mazingira yale yalikuwa yametulia sana na nyumba ile ilikuwa pembezoni mwa mlima!.


Gabi "Ooh wanaume wapambanaji wa kikurya!"

Gabi alipotuona alifurahi sana na kiukweli tulikumbatiana kwa furaha!.Nilimshangaa sana Gabi safari hii kwasababu alikuwa amebadilika sana tofauti na miezi michache iliyokuwa imepita,safari hii alikuwa ameachia ndevu kidevuni mwake na mashavuni kiasi kwamba kuficha uhalisia wake ambao nilikwisha kuuzoea!.

Gabi "Vipi wewe mbona hupatikanagi!?"

Mimi "Nilibadili namba kaka"

Gabi "Mambo yanakwendaje lakini!"

Mimi "Tupo tunapambana kaka"

Gabi "Jamaa bhana walinishikiria kwa siku kadhaa ila walitema nyongo!"

Mimi "Walikuja mpaka pale kwako au ilikuwaje kaka"

Gabi "By the way ni stori ndefu lakini niwaambie kitu,Kama huna hela utakufa njaa lakini mwenye hela huchelewa tu kula ila hafi njaa"

Aliendelea "Pesa ndo kila kitu"

Gabi "Vipi lakini mwanangu ule mzigo ilikuwaje?"

Mimi "Kaka ulivyoniambia mko njiani mnakuja mimi nilitoroka nao nikafika mahali nikauchoma moto!"


Gabi "Ahahaha ya kwamba Mkurya ulisanda,sio!"

Aliendelea "Wala usijali yale tuliyamaliza,tunachopaswa kufanya ni kuangalia yaliyoko mbele yetu!"


Gabi "Siku hizi mnafafanya shughuli gani aisee!"


Mtatiro "Braza tunapambana na mitumba"

Gabi "Sasa hiyo inawalipa kweli!?"

Aliendelea "Hebu ngoja kwanza niwaambie wawalete msosi mtandike wanangu!"


Baada ya muda chakula kililetwa na mama mmoja wa makamo ambaye kimuonekano alikuwa na miaka zaidi ya Hamsini,basi tulianza kula kile chakula wakati huo Gabriel hakiwa hayupo sebuleni,alirudi tukiwa tumemaliza kula na akatutaka tutoke kuelekea town tukapate bia mbili tatu!.
Tulipanda ile Land cruiser tukaondoka kuelekea mjini ambapo tulifikia Hotel ya kifahari ya Gold crest,Tulipofika pale tulipanda kwenye lift ambayo ilituvuta kwenda juu kabisa mwisho wa lile jengo,tuliingia kwa juu ambako nilikuta kuna uwazi wa kutosha huku watu wakiwa wanapata vyakula na vinywaji!.

Ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kuingia kwenye Hotel ya kifahari iliyokuwa hapo Mwanza,kiukweli nili enjoy sana maana mandhari yote ya jiji la Mwanza ilikuwa ikionekana hapo.Tulitafuta meza yetu tukawa tumekaa,Gabi aliagiza pombe Kali mchupa mkubwa na akawa ametutaka na sisi kila mmoja kuagiza tulichokuwa tunakunywa!.

Mtatiro akawa ameniambia tuagize li Jack Daniel chupa kubwa ili tulichape wawili,hivyo ndivyo tulivyofanya!.Hapo kabla sikiwahi kunywa pombe kali,nilikuwa nikinywa vibia vyangu kadhaa natulia,hiyo ndiyo ilikuwa mara ya kwanza kunywa pombe kali!.Yule dereva yeye alikuwa akinywa maji muda wote tuliokuwa hapo.

Baada ya pombe kuanza kukolea,maongezi nayo yalichukua nafasi!.

Gabi "Wanangu mimi huwa nawakubali sana katika mapambano!"

Aliendelea "Nyie ni miongoni mwa marafiki zangu wakubwa na sitowaacha ndugu zangu!"

Gabi "Jioni kuna mahali nataka twende ndugu zangu!"

Mtatiro "Kuna dili jipya kaka?,wewe tupe dili sisi tupige tunachotaka ni hela!"

Gabi "Hilo wala msijali,nyie ni wanangu wa damu lazima kila dili niwe nawakumbuka!"

Baada ya kupiga mtungi kwa muda mrefu,Gabi alimwambia yule dereva aondoke atuache na sisi tungechukua taksi kwasababu tulikuwa na safari nyingine!.Baada ya yale mazungumzo nikiona Gabi anatoa pochi iliyokuwa imesheheni noti za elfu kumi kumi akachomoa elfu 50 akamkabidhi jamaa huku akimwambia atampigia simu!.


Gabi "Wanangu sikieni,huyo dogo ni mtoto wa dingi mdogo na pale alipowaleta ni nyumbani kwao,ingawaje pia wana nyumba nyingine Arusha ambako wanakaa ndugu zake na wadogo zake!"

Aliendelea "Dingi yake ni marehemu na baada ya kugawiwa pesa za urithi dogo akaona aje amalizie hiyo nyumba ya Mwanza aishi yeye na ile ya Arusha awaachie wadogo zake!"

Mtatiro "Anapiga ishu gani?"

Gabi "Dogo anasema anagereji ila sijajua ipo maeneo gani,alichezea sana hela dogo msimuone vile,hilo li cruiser alinunua tukamshauri alipeleke Arusha lipige kazi lakini naona kama haelewi!"


Basi baada ya mazungumzo hayo huku tukiendelea kukata maji machungu!,ilipofika mida ya saa 1 usiku tulionodoka kutafuta Taksi na kuelekea maeneo ambayo Gabi alikuwa akiyafahamu!.Tulifika kwenye nyumba moja ambayo ilikuwa kimya sana hata kabla nilidhani haikuwa na umeme kumbe taa zilikuwa zimezimwa!,baada ya ile Taksi kuondoka Gabi alipiga simu akazungumza na mtu mmoja ambaye bila kuchelewa alitufungulia geti tukazama ndani.

Tulipoingia ndani tulipelekwa hadi sebuleni ambapo nako hakukuwa na mwanga wa taa ila baada ya kukaa kwenye kochi ndipo taa ya sebuleni iliwashwa,sasa baada ya ile taa kuwashwa kulikuwa na jamaa wawili pale sebuleni ambao walikuwa wamejengeka vizuri mno kimisuli huku usoni mwao hakukuwa hata na chembe ya tabasamu!.Tulipoingia ndani,Gabi yeye moja kwa moja alipitiliza ndani huko vyumbani na hatukufahamu alienda kufanya nini!.

Baada ya muda alikuja Gabriel akiandamana na Jamaa mmoja aliyekuwa amenyoa upara,pia hakuwa na ndevu hata kidogo maana zote alikuwa amezipiga wembe!.

Gabi "Aisee mnaweza kutupisha kidogo tunamazungumzo"

Wale jamaa wawili tuliowakuta hapo walinyanyuka wakawa wameondoka kuelekea huko ndani!.

Gabi "Mkuu hawa ndio vijana niliokueleza tangu wiki iliyopita tukiwa Arusha!"

Aliendelea "Huyu anaitwa Mtatiro na huyu anaitwa Umughaka"

Gabi "Ni wakurya majasiri sana kama nilivyokwambia"
Aliendelea "Ndugu zangu huyu ni bosi wangu bila shaka pia atakuwa bosi wenu"

Gabi "Nadhani bosi karibu uzungumze chochote!"

Yule tuliyeambiwa ni bosi wa Gabi alianza kutuangalia kwa makini sana huku akitukazia macho kiasi kwamba kila mtu kama alianza kuingiwa na hofu!.


Bosi "Nyie ni Wakurya kutokea wapi bhana!"


Mtatiro "Tumetokea Tarime"

Bosi "Tarime ni kubwa"

Mtatiro "Wote tunatokea sehemu moja pale Tarime mjini"

Bosi "Ninaposema Tarime nahitaji kujua jina la kijiji au mtaa mnaotokea!"

Mtatiro "Tunatokea Rebu"

Bosi "Wewe una miaka mingapi?"


Mimi "Nina miaka 23"

Bosi " Na wewe?"

Mtatiro "Mi nina miaka 27"

Bosi "Mmewahi kufanya kazi gani ambayo ilitishia kuyakatisha maisha yenu uhai!?"


Baada ya hilo swali tulibaki kujiuma uma ndipo Gabi akaingilia kati kusaidia kujibu!.

Gabi "Bosi hawa wote nilikuwa nafanya nao ile kazi ndiyo maana nina waamini!"

Bosi "sawa,bila shaka umewaambia!"

Gabi "Hapana mkuu sijawaambia chochote"

Bosi "Ilipaswa uwaambie ili mwenye kuamua aamue,sitaki mtu mwenye roho ya kike kwenye kazi zangu!"

Aliendelea "Sasa nyie nisikilizeni kwa makini,naitwa Afande........,je mmewahi kutumia bunduki?"

Baada ya kutaja neno bunduki kiukweli akili yangu ilitaka kuchanganyikiwa,nilijikuta kale kapombe nilikokuwa nimekunywa kote kalikata!.Mimi niliitikia kwa kutikisa kichwa kuashiria hapana lakini Mtatiro alimjibu!.


Mtatiro "Hapana"

Bosi "Je mko tayari kutumia bunduki?"


Mimi nilisita kuitikia ila mwenzangu Mtatiro alikuwa na ujasiri sana kujibu like swali!.

Mtatiro "Ndiyo mimi nipo Tayari!"

Bosi "Na wewe je?"

Baada ya Mtatiro kujibu lile swali na mimi nikajikuta namfuatisha Mtatiro.

Mimi "Nipo Tayari!"

Bosi "Sasa nyie ndiyo wakurya ninao wafahamu,nimewapenda!"

Baada ya yale mazungumzo yule bosi aliondoka akarudi ndani akasema tumsubiri kwanza anarudi!.


-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-SEHEMU YA 19.


Baada ya muda wa nusu saa yule Bosi alirudi akiwa na jamaa mmoja wa wale jamaa wawili tuliowakuta pale sebuleni kabla hawajaambiwa watupishe kwa ajili ya mazungumzo!.

Alimwambia yule jamaa "Kaa pale"

Bosi "Hawa ni watu wa kazi,ni wakurya wakwenu huko!"

Basi yule jamaa akaanza kutuongelesha lugha ya kikurya huku akituuliza maswali na sisi tukimjibu kwa ufasaha,sasa baada ya kujiridhisha ya kwamba tulikuwa wakurya,akamwambia Bosi kwamba ni kweli sisi ni Wakurya.

Bosi "Sawa naomba utupishe!"

Yule jamaa akanyanyuka akaondoka akatuacha pale sebuleni!.

Bosi "Kazi nitakayowapa itawatoa kwenye umasikini na hizi shida ndogo ndogo mtazisahau!"

Aliendelea "Pesa yetu ipo mikononi mwa watu hivyo inapaswa irudi kwetu!"

Bosi "Mimi nitawalinda wala msijali!"

Aliendelea "Kanuni huwa ni pasu kwa pasu kwa kitakachopatikana!"

Bosi "Endapo kikinuka jisalimishe au tetea uhai wako,Yeyote atakaye kuwa kikwazo huyo ni halali yako!"

Muda wote wa mazungumzo nilikuwa naona Mtatiro akitikisa kichwa kana kwamba yale maneno yalikuwa yakimuingia sana na yeye kuyakubali!.Mimi kiukweli niliingia uoga sana lakini nilikuwa tayari kumfuata Mtatiro atakachokiamua yeye!.

Bosi "Kufa na siri hapa si hiari ni lazima,fanya ufanyavyo usije ukathubutu kumtaja mtu endapo ukiwa mikononi mwa wendawazimu(Mapongo)"


Aliendelea "Kitakachopatikana narudia tena itakuwa pasu kwa pasu!"

Bosi "Sasa tutaondoka wote kuelekea Arusha,lakini kabla ya kwenda huko mtaondoka na jamaa kwanza mkatengenezwe ndipo tuondoke!"

Aliendelea "Nyinyi ni wanaume bhana,haya ni maisha tu,pesa ndiyo kila kitu na hivyo lazima zirudi mikononi mwetu!"

Bosi "Gabriel mwambie Doto Akupatie milioni mbili uniletee"

Gabi ambaye muda wote alikuwa kimya akimsikiliza bosi wake,alinyanyuka akaelekea huko ndani ambako aliagizwa!.

Baada ya dakika 1 alirejea na bunda mbili ambayo kila moja ilikuwa na milioni moja!.

Bosi "Kamata hii"

Mimi nikapewa bunda moja na Mtatiro nae akakabidhiwa bunda lake!.

Bosi "Hizo ni pesa mtakazo tumia kutatua shida ndogo ndogo!"

Aliendelea "Nadhani utaratibu mwingine Gabriel atawaeleza,nendeni mjipange ili ikiwezekana kesho au kesho kutwa muondoke mkatengenezwe kabla ya kwenda Arusha"


Kiukweli ile pesa ilikuwa ni kama vile sumaku,maana baada ya kuipokea ile hela niliona kama nilichelewa kwenye utajiri!.Tulinyanyuka tukamuaga yule jamaa na taa ikazimwa sisi tukatoka nje!.Tulipofika nje tulitembea kuitafuta barabara ambapo ilitulazimu kutafuta Taksi ili tuondoke!.

Gabi "Nyie ni wanangu ni lazima niwaambie ukweli,mara zote huu ni mchongo ambao nikiufanya,kule kwenye zile pesa bandia pia natafuta tu maisha lakini kiukweli maisha yako huku!"

Aliendelea "Siwezi kuwashikisha dili mbovu!"

Gabi "Huyo mliyekuwa mnaongea nae ni Askari lakini mpelelezi!"

Aliendelea "Si mko tayari ndugu zangu tupambane huku?"

Mtatiro "Mi nilitaka kumwambia anikabidhi chuma niingie mzigoni hata muda huu,nishachoka kudharauliwa!"


Gabi "Usiwe na haraka Mtatiro,nyie jiandaeni kesho kuna mahali mtapelekwa na jamaa ili mkitoka huko muwe kamili gado"

Sasa kwakuwa Mtatiro alilidhia ile kazi kwa moyo mweupe,kiukweli na mimi nilijikuta nakubali kwasababu nilikuwa namkubali sana jamaa yangu!.

Muhimu:-

(Yule tuliyeambiwa ni mpelelezi kiukweli hakuwa Askari wala mpelelezi,nilikuja kugundua baadae jamaa alikuwa ni mafia wa hatari na alikuwa akisakwa na jeshi la polisi sana,sasa nilichokuwa nikijipa moyo ni kwamba,kwakuwa alikuwa askari sikuhofia chochote maana nilijua endapo kikitokea cha kutokea tungesaidika,kumbe ile ilikuwa ni zuga tu wanaume tuingie mkenge,sitomtaja jina kwasababu maalumu na hata hivyo jamaa kwasasa ni marehemu).

Gabi "Umughaka mbona kama huna amani mwanangu"

Mimi "Mimi niko fiti kaka"

Gabi "Au unahofu?,mbele ya chuma hakunaga hofu kaka ile subiri uishike ndiyo utaniambia!"

Mimi "Kwahiyo chuma tunapewa lini?

Gabi "Msiwe na haraka,chuma zipo tutazikuta Arusha!"

Aliendelea "Hamuwezi kupewa chuma mpaka mkatolewe uoga ndugu zangu!"

Mtatiro "Mimi si muoga kaka labda Umughaka"

Baada ya ile kauli ya Mtatiro tukajikuta wote tunacheka sana!,basi sisi tulifanikiwa kuondoka tukawa tumeagana na Gabi na kukubaliana asubuhi tungeonana ili kuondoka tulikoambiwa tungeenda ili kutengenezwa kutolewa uoga!.

Tulipofika nyumbani kiukweli kila mtu alianza kuhesabu hela zake na kukuta ilikuwa milioni moja moja!.Mazungumzo yalichukua nafasi pale ndani na kiukweli Mtatiro alikuwa akiniambia sisi ni watoto wa kiume hatuna budi kupambana kwenye madili makubwa ya hela ili tufanikiwe katika maisha!.Ndugu yangu Mtatiro alikuwaga ni jasiri sana na asiyekuwa na chembe ya aibu na uoga!,alikuwaga akiamua kitu basi hakuna kurudi nyuma,ile roho ya ujasiri na isiyokuwa na uoga ndiyo Mtatiro aliniambukiza na mimi pia hata leo!.Mtatiro alikuwa ameamua liwalo na liwe,yeye alichokuwa akitaka ni pesa tu,hakutaka kusikia mambo mengine kabisa!.

Asubuhi kulipokucha Mtatiro alinishauri twende kwanza tukanunue nguo na viatu ili tuwe kila wakati tunapendeza!,sasa hakufahamu hayo ndiyo yalikuwaga mambo yangu,kiukweli nilifanya mambo yote hayo ili nipate pesa ya kula vizuri na kuvaa vizuri tu!.Baada ya lile zoezi la kununua viwalo,tukaianza safari ya kuelekea kitangiri ambapo yalikuwa makazi ya muda yule jamaa.

Tulipofika nje ya geti Mtatiro alimpigia simu Gabi akawa amekuja kutufungulia geti na kuzama ndani!.Tulipofika hapo ndani hatukumkuta yule bosi wa Gabi ila tulimkuta jamaa mmoja ambaye hakutaka tupoteze muda bali tuanze safari!.

Jamaa "Si mko Tayari!?"

Sisi " Ndiyo"

Jamaa "Ok tuondoke"

Tuliondoka kuelekea nje ambapo alianza kuwasiliana na mtu kwenye simu akimaambia asogee maeneo tuliyokuwepo ili tuondoke!.Baada ya muda mfupi gari aina ya Noah Ace ikawa imefika pale na aliyekuwa akiendesha alikuwa Demu!.Tulipanda kwenye ile gari sisi tukakaa katikati na yule jamaa akawa amekaa mbele!.Sasa tulimpa hai yule demu lakini hakutoa ushirikiano ikabidi tukaushe!.

Ndani ya ile gari hakuna mtu aliyezungumza na mwenzie zaidi ya mikausho mikali.-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-
SEHEMU YA 20.Gari ilitembea tukaikamata njia ya Sirari,sasa tukawa kama tunaelekea Musoma.Yule jamaa akamwambia yule demu aliyekua akiendesha gari ya kwamba inapaswa tuweke kituo kwanza Lamadi tukapate msosi kisha ndiyo tuondoke.

Baada ya kufika lamadi na kupata Msosi tuliondoka kuelekea Bariadi,sikuwahi kufika bariadi ni hiyo ndiyo ilikuwa mara yangu ya kwanza kufika huko,sasa baada ya kuiacha bariadi tulianza kuingia vijijini huko ndani ndani ambako sikuvifahamu kwa haraka maana sikuwa mwenyeji huko.

Kituo chetu cha mwisho kilikuwa kwenye kijiji cha Mwanaungu ambako baada ya kushushwa hapo,yule jamaa alimwambia yule demu kwamba amsubiri kwanza atupeleke halafu waondoke!.

Mtatiro "Mwanangu kwahiyo mnatuacha?"

Jamaa "Tutarudi kuwachukua ondoa shaka!"

Tulitembea kwa umbali mrefu kidogo hatimaye tukafika kwenye mji mmoja ambao ulikuwa umezungushiwa minyaa ya kutosha,baada ya kufika hapo tulikuta kuna vijumba vingi vya nyasi huku kukiwa na watu ambao wengine walikuwa wamelala kwenye majamvi huku wengine wakiendelea na shughuli zao!.Kuna mwanamke akaja kutupokea kwa salamu ya kisukuma huku akipiga magoti,sasa mimi kwakuwa nilikaa usukumani kwa kipindi fulani wakati baba yangu mdogo akiwa headmaster,ile salamu haikunipa taabu kabisa!,na siyo salamu tu,naweza kukizungumza kisukuma ingawaje cha kuombea maji!.

Baada ya ile salamu yule mwanamke alituletea viti ambavyo havikuwa na watu kwa wakati huo.Basi baada ya muda mfupi yule mwanamke akaja na daftari akatutaka kila mmoja wetu kutaja jina lake na kuandikwa,sasa tulipoandikwa akatuchania vikaratasi vikiwa na namba,mimi nilipewa namba 16 na Mtatiro akapewa namba 17,yule jamaa yeye akamwambia yule mwanamke kwamba anahitaji kuonana na Mwami(Ng'wana Mwami).Yule mwanamke akamtaka asubiri kwanza.

Baada ya muda yule mwanamke akaja akamuita yule jamaa akampeleka mpaka kwenye kinyumba cha nyasi kilichokuwa kikubwa kati ya vile vinyumba tulivyovikuta pale.Baada ya muda yule jamaa akatoka akaja akatuambia angerudi baada ya siku mbili,hatukujua alipoingia mle ndani alienda kuzungumza kitu gani na huyo aliyekuwa humo ndani!.Jamaa aliondoka akatuacha pale,hiyo ilikuwa mida ya mchana saa 7.

Ilipofika mida ya saa 10,kuna mwanamke alitoka kwenye kile kijumba huku akijinyoosha kana kwamba alikuwa amechoka sana!.Alianza kuwazungukiwa watu kadhaa waliokuwa pale nje huku akiongea nao kisukuma na kiswahili!.Alipofika kwetu alitusalimia kisukuma na kama kawaida nami nilimuitikia kisukuma,sasa Mtatiro halikuwa haelewi kabisa hata salamu ndipo nilimwambia yule mama ya kwamba mwenzangu haelewi kisukuma,aliamua kumsalimu kiswahili kisha akaendelea na watu wengine!.Yule mama ndiye aliyekuwa mwenyeji wetu na alikuwa mganga!.

Mtatiro "Mwanangu kisukuma kumbe unakipiga fresh"

Mimi "Nimekaa nao,dingi yangu mdogo alikuwa headmaster shule moja huko Tabora hivyo nilikinyaka kiasi fulani"

Ilipofika mida ya saa 12 jioni kuna watu takribani 7 ambao walikuwa wanaume 3 na wanawake 4 waliingia pale nyumbani huku wakiwa wamebeba majembe,mimi nilidhani ni ndugu tu wanaoishi hapo kumbe walikuwa wateja wa huyo mama.Sasa utaratibu ulikuwa ni kwamba,unapofika kwa huyo mama unapewa namba kama sisi tulivyopewa,wakati ukiendelea kusubiri ili namba yako iitwe ilipaswa kila kunapokucha ukamate jembe umfuate mwenyeji akakuelekeze shamba la kulima na ulikuwa unapewa kipande chako ili upambane nacho,na kipande chenyewe hakikuwa cha kitoto,yaani kama ukimaliza kile kipande ndipo unaambiwa sasa umekolifai kupatiwa matibabu na yule mama.Sasa wakati unasubiri matibabu ndipo mnaitwa kwa namba ambazo hata sisi tulipewa.(Yule mganga alikuwa mjanja sana,badala ya kulima mashamba yake,sisi wapumbavu ambao tulifahamika kama wateja wake ndio tuliomlimia wakati yeye akiwa ametulia nyumbani,Daaah!,na kila mtu aliyefika hapo kwake ni lazima ilikuwa akamatishwe jembe aingie shambani!).

Mimi na Matatiro tulikomaa na vipande vyetu ambavyo tulivianza siku iliyofuata kwasababu siku tuliyofika tulikuwa tumechelewa,bahati nzuri ilikuwa ni palizi na hakukuwa na nyasi sana!.Siku hiyo tulipomaliza kupalilia lile shamba ilikuwa mida ya saa 9 alasiri,tuliporudi hapo nyumbani kiukweli tulikuwa tumechafuka miguu na kunuka majasho hatari,sasa nilimfuata yule mama aliyetupokea siku ile nikawa nimemwambia atupatie maji ili tuoge,alituambia inapaswa tuwasubiri wenzetu ambao nao walikuwa hawajamaliza sehemu zao ili tupate chakula kwa pamoja kisha ndio tuoge!.

Wale walipotoka huko shambani,tulitengewa ugali wa udaga kwa na furu wa kuchemsha.Sasa tulipaswa kukaa watu watatu watatu kwa ajili ya chakula,mimi nilikaa na Mtatiro kama kawaida pamoja na jamaa mmoja ambaye alikuwa mteja kama sisi!.Siku hiyo ikapita kapa bila kuitwa namba lakini kuna watu wao waliitwa wakaendelea kupewa huduma kama kawaida!.

Siku iliyofuata tukaitwa majina watu kama wanne,sasa kwakuwa mimi na Mtatiro tulikuwa na shida moja ilibidi tuambiwe tusubiri kwanza amalizane na wale wa wawili.Zamu yetu ilifika na tukaitwa ndani kwa yule mama,hatukujieleza hata kidogo bali tulipoingia ndani alitutaka tuvue shati ili kitendo cha kupigwa chale kuchukue nafasi!.

Yule mama alitupiga chale kwa kutumia kisu kilichokuwa kikali kama wembe,alituchanja kila sehemu aliyoona yeye inafaa,baada ya hapo alituchanja pia kwenye ulimi kila mtu!.Alipomaliza kutuchanja na kutupaka dawa,alichukua kitu kilichokuwa kimefungwa na kukazwa sana na kutakiwa kila mmoja akivae kiunoni,ile alituambia ni irizi na asije akatokea mtu akaivua,alisema endapo ikitokea ukaivua basi usije ukamlaumu!.

Mpaka wakati huo hatukufahamu kwa huyo mganga tulipelekwa kufanya nini,ingawa tuliambiwa tulikuwa tunakwenda kutengenezwa ili hatukujua ule utengenezwaji ulikuwa na faida gani katika ile kazi yetu mpya ambayo tungeianza siku chache zilizokuwa mbele yetu!.Yule mama alituambia ya kwamba,ile irizi haikupaswa kabisa kutolewa kiunoni hata iweje.

Basi baada ya kumaliza ile shughuli tulitoka nje tukaendelea kumsubiri jamaa aliyetuambia angekuja kutuchukua!.Ile siku jamaa hakutokea kabisa,hivyo ikatubidi tulale tena kwa yule mama.Yale mazingira yalikuwa ya hovyo sana lakini ilibidi tukubaliane na hali kwasababu tuliitamani pesa!.Ilipofika mida ya saa 5 asubuhi siku iliyofuata yule jamaa alirudi kutuchukua na kisha tukaondoka,sasa tulipoingia kwenye ile Noah tulikuta kuna mabegi kadhaa na kulikuwa na jamaa mmoja akiwa amekaa siti za abiria,dereva alikuwa ni yuleyule demu ambaye alikuwaga azungumzi na mtu!.

Jamaa "Wanangu safari ni moja kwa moja Arusha"

Mtatiro "Kaka mngeturudisha kwanza tukachukue nguo"

Jamaa "Nguo sio sehemu ya kuwazia,utazikuta huko"

Basi hatukuwa na swali,tuliamua kukausha na safari kuanza.Tulitembea sana na hatimaye tukaikamata lami kuelekea Musoma,baada ya kuivuka lamadi kwa mbele,tukaikamata geti la Ndabaka linaloingia Serengeti.-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-SEHEMU YA 21.Haikuwa safari ya kitoto hata kidogo,tuliingia pale Arusha saa 3 usiku.Hii haikuwa mara yangu ya kwanza kufika Arusha,japo nimefika mara kadhaa lakini sikuwahi kuwa mwenyeji,mara zote wakati naenda shule Tanga nilikuwa nikipita Arusha.Baada ya kufika Arusha mjini yule jamaa akawa ametuambia inapaswa tupate chakula mahali fulani ili tukimaliza tuondoke kwakuwa tulipokuwa tukienda hakukuwa na chakula wala mtu wa kukipika!.

Tulipomaliza kula tuliondoka zetu kuelekea ambako mimi na Mtatiro tulikuwa hatupajui.Baada ya muda ile gari ikaanza kupiga honi baada ya kufika mbele ya nyumba ambayo ilikuwa na geti;geti lile lilifunguliwa kisha gari ikaingia ndani.Tuliteremka huku tukiendelea kushangaa shangaa ndipo yule jamaa akaja akatuambia tumfuate,tulielekea ndani ambako tulionyeshwa chumba cha kulala ambacho kilikuwa na vitanda 2.

Wakati ule kiukweli hakuna mtu tuliyemkuta pale kwenye ile nyumba zaidi ya yule mtu aliyetufungulia lile geti,sasa kumbe baada ya ile Noah kutuacha pale wao waliondoka na hakuelewa walienda kulala wapi.Asubuhi mida ya saa 2 yule jamaa tuliyetoka nae Mwanza alikuja kutuchukua na kutuambia inapaswa tuondoke!.Tuliondoka kuelekea Tengeru hatimaye tukafika kwenye nyumba moja ambayo tulimkuta yule bosi wake na Gabi akiwa na jamaa wawili,miongoni mwa wale jamaa tulikuwa nae Mwanza ila yule mmoja sikumfahamu,sasa ilifanya idadi yetu kuwa watu wanne ukimuondoa yule Bosi.Yule bosi alimuita yule jamaa tuliyekuja nae wakaanza kuzungumza kitu ambacho hatukukilewa,sasa baada ya yale mazungumzo jamaa alitoka akawa ameondoka,baada ya muda kuna jamaa mmoja miongoni mwa wale tuliowakuta alikuja akawa ametuuliza mimi na Mtatiro tunavaa viatu namba ngapi kila mmoja.

Baada ya kumueleza size ya namba ya viatu tulizokuwa tunavaa,jamaa aliondoka.Haukupita muda akawa amerudi na viatu aina ya safari boot ambazo kila mtu alipaswa kuchukua size yake!.Sasa ilipofika mida ya jioni yule jamaa tuliyetoka nae Mwanza alirudi akiwa kwenye gari aina ya Mark 2 nyeupe iliyokuwa na tinted,ile gari iliingia mpaka pale ndani kisha jamaa akawa ametelemka na begi jeusi ambalo lilionekana lilikuwa zito.

Jamaa "Aisee hebu njoeni ndani mara moja"

Baada ya kufika ndani,jamaa hakutaka kupoteza muda,alifungua lile begi ambalo lilikuwa na nguo kadhaa akawa amezitoa na kututaka kila mmoja ajaribu itakayo mtosha.Mimi zilizonitosha ilikiwa ni jeans mbili pamoja na cadet moja iliyokuwa nzito,Mtatiro yeye kwakuwa alikuwa na mwili mkubwa kidogo,alipata nguo ambazo ziliendana na mwili wake vizuri.

Sasa baada ya hapo jamaa alituambia tukae chini kisha akawa ametoa bunduki iliyokuwa kwenye lile begi!.Sikufahamu ile bunduki ilikuwa ni aina gani kwasababu sikuwa mtaalamu wa bunduki kwa wakati huo,ile bunduki ilikuwa ni fupi kisha ikawa imekazwa kwa mapira katikati.Sasa baada ya kuitoa ile bunduki yule jamaa alituambia tumsubiri yule aliyekuwa bosi wa Gabi anakuja.

Yule bosi baada ya kurudi na yeye hiyo mida ya saa 2 usiku pia alikuwa na bunduki ambayo niliifahamu ilikuwa SMG.

Bosi "Msiogope bhana haya ni mambo ya kawaida"

Aliendelea "Jamaa yenu mtamkuta Kahama anawasubiri,pale kuna mtu ana hela zangu itapaswa mkazichukue"

Aliendelea "Hii Mashine ningekupatia wewe(Mtatiro)lakini nahitaji kwanza muda"

Aliendelea "Jipe atawapa hiyo nyingine mtaondoka nayo kwenda Kahama halafu hii kuna mtu mtaongozana nae ndiyo atakuwa nayo"

Aliendelea "Sasa naomba simu zenu mziache hapa maana huko hampaswi kwenda na simu"

Basi tulichukua zile simu tukawa tumemkabidhi yule aliyeitwa Bosi.Kumbe muda huo ambao sisi tulikuwa hapo Arusha,Gabi yeye alikuwa Kahama mkoani Shinyanga ambako hatukufahamu alikwenda kufanya shughuli gani!.

Bosi "Nyie mtaondoka kesho kutwa,kaeni hapa mpumzike kwanza"

Baada ya yale mazungumzo,yule Bosi aliondoka na yule jamaa tuliyetoka nae Mwanza wakawa wametuacha pale kwenye ile nyumba tukiwa pamoja na wale jamaa wawili tuliowakuta.

Kweli!,baada ya siku mbili tuliondoka asubuhi na mapema,ilikuwa mida ya saa 10 usiku ndipo tuliianza safari kuelekea Kahama mkoani Shinyanga,mimi kiukweli sikuelewa kilichokuwa kimetupeleka Arusha ilikuwa ni kitu gani maana hata bunduki zenyewe hatukupewa kwa muda huo bali tuliishia tu kuonyeshwa na kupewa maelekezo,sikuweza kuhoji sana niliamua tu kutulia maana nilikubali mwenyewe kujiingiza kwenye genge la ujambazi!.
Tuliondoka na ile Toyota Mark 2 ambayo tulikuwa mimi na Mtatrio pamoja na yule jamaa tuliyetoka nae Mwanza ambaye alifahamika kwa jina la Jipe,sikujua kama ndilo jina lake halisi lakini hata sisi baada ya kuzoeana tulikuwa tukimuita hivyo!.Dereva aliyekuwa akiendesha ile gari kiukweli alikuwa jamaa fulani wa kawaida sana na mwembamba lakini alikuwa dereva mzuri sana,nakumbuka ile gari ilikuwa ikitembea mpaka unahisi inapaa!.

Baada ya safari ndefu hatimaye tukafika Kahama,sasa tulipofika maeneo ya mgodi wa buzwagi,tuliingia kushoto tukaikamata barabara ya vumbi kuelekea Mwendakulima kwa ndani ndani huko.

Haukupita muda tukawa tumefika kwenye nyumba moja ambayo haikuwa na geti lakini ilikuwa imejitenga mbali na nyumba nyingine,sasa tulipofika hapo ndipo tukakutana na Gabriel ambaye baada ya sisi kuteremka kwenye ile gari alimchukua pembeni yule jamaa wakaanza kuzumngumza!.

Baada ya yale mazungumzo Gabi alituambia tuingie ndani huku yule jamaa akibeba lile begi lililokuwa na silaha kuingia nalo ndani!.Tulipiga stori na Gabi huku yeye akiendelea kutupa moyo kwamba yale mambo yalikuwa ni kawaida tu na hatukupaswa kuwa na hofu!.

Siku iliyofuata ilipofika saa 6 usiku,yule jamaa alituambia mimi na Mtatiro tutaongozana nae kuelekea mahali fulani,sasa alimpatia Mtatiro ile bunduki iliyokuwa imefungwa na mapira kwa nguvu sana na yeye akachukua ile SMG.

Jipe "Mtakuwa manafuata maelekezo yangu kila nitakachokuwa nawaambia!"

Mtatiro "Sawa"
Jipe "Hiyo silaha tayari risasi iko chemba,hivyo kuwa makini!"

Aliendelea "Gabriel atabaki hapa kuweka mambo sawa,sisi tutaondoka na tutawahi kurudi,kule tukifika hakuna kusubiri,tunaenda kufata kilichotupeleka!"

Jipe "Wewe jamaa(mimi)utakuwa kando yetu na utafanya nitakachokuwa nakwambia"

Mimi "Sawa"

Mtatiro alivyokuwa ameishika ile silaha ungemuangalia kwa haraka haraka ungezani uenda alikuwa askari mwenye uzoefu wa miaka mingi,jamaa alikuwaga jasiri sana alikuwa mtu ambaye ulikuwa ukimpatia maelekezo mara ya kwanza basi hurudii tena maana alikuwa na kichwa chepesi!.Mpaka muda huo ukweli ni kwamba,Mtatiro ndiye aliyenishawishi hadi na mimi kujikuta naingia mkenge!,sikuwa na namna ilipaswa nitafute pesa!.-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-SEHEMU YA 22.


Tuliondoka na gari lile eneo kuelekea ambako tuliambiwa tunakwenda kuchukua pesa ya Bosi.Ile gari baada ya kutembea kwa umbali mrefu hatimaye ilisimama kando ya barabara ya vumbi na ndipo yule jamaa(Jipe)akatutaka tuteremke!.

Jipe "Katusubiri pale mbele ya lile karavati"

Jipe alimwambia yule dereva azime taa kisha akatusubiri kwenye karavati lililokuwa mbele!.Jamaa aliongoza na sisi kumfuata nyuma,mtatiro na Jipe ambao walikuwa na silaha,walikuwa wamevaa makoti marefu ambayo yalifanya zile silaha walizokuwa nazo kutokuonekana kwa urahisi!,sasa baada ya kutembea kwa umbali mrefu kidogo hatimae tukafika kwenye nyumba moja ambayo haikuwa na geti wala fensi!,jamaa alisogea hadi mlangoni akaanza kusukuma ule mlango kana kwamba ulikuwa wazi,baada kusukuma ule mlango na kuzunguka ile nyumba,jamaa alitoa simu akampigia Gabi,baada ya mazungumzo jamaa alitwambia tuondoke haraka maana kumbe tuliingia chaka,eneo lililokusudiwa halikuwa hilo!,tulitembea kwa haraka kuifuata ile gari na hatimaye tukaianza safari kuelekea kulipokusudiwa!.Wakati huo wote mimi sikuwa na silaha zaidi ya kuwafuata nyuma Jipe na Mtatiro ambao wao ndio walikuwa na Silaha!.

Baada ya safari ya dakika kadhaa tukawa tumefika kwenye eneo ambalo lilikuwa na nyumba kadhaa ambazo ilionyesha kabisa walioishi eneo hilo walikuwa na vyanzo vizuri vya Mapato.

Jipe "Kila mtu ajifunge vitambaa"

Aliendelea "Nitakachosema ndicho mtakachokifanya"

Sisi "sawa"

Tuliteremka kwenye ile gari tukaanza kutembea kuelekea kwenye nyumba iliyokusudiwa;Lile eneo lilikuwa limetulia sana kwa wakati huo maana ilikuwa yapata mida ya saa 7 usiku.Tulipofika nje ya geti Jipe alipanda ukuta akawa ameruka kwa ndani,sasa wakati jamaa akiwa ndani nikasikia sauti ya mbwa akibweka kwa nguvu sana,jamaa hakutaka kupoteza muda,nilisikia sauti ya risasi ikipigwa na yule mbwa sikumsikia tena!.

Jipe "Ingieni ndan"

Jipe alituambia kwa sauti kubwa iliyoonyesha msisitizo,basi tulipanda ule ukuta tukaruka kwa ndani!.Baada ya kuingia ndani ndipo jamaa akawa anaangalia namna ya kufanya ili tuingie ndani!.Jipe alianza kupiga lile geti la chuma kwa risasi hadi likaachia ukawa sasa umebaki mlango wenyewe!.Kiukweli mara ya kwanza nilitaka kukimbia baada ya zile sauti za ile bunduki zenye kishindo kikubwa,nilibaki kumtazama Jipe muda huo ambao hakuwa na mchezo kabisa!.

Sasa nilianza kusikia kwa ndani sauti za watu wakilia na kuomba msaada,mahali ilipokuwa ile nyumba kulikuwa na nyumba nyingine ambazo hakukuwa na mtu aliyetoka nje hata mmoja.Wakati jamaa akipambana ili ule mlango ufunguke tuzame ndani,kuna sauti ya kiume ilikuwa inasikika kwa ndani ikisema "Atakaye ingia huyo ni halali yangu!".

Jipe "Hebu nipe hiyo silaha,kamata hii"

Alichukua ile silaha ya Mtatiro akaanza kupiga risasi kwenye kitasa cha ule mlango hadi ukaachia!.Baada ya kitasa kuachia aliusukuma ule mlango kulekea ndani kisha na jamaa akawa ameingia ndani!.

Jipe "Ingieni ndani"

Tuliingia ndani ambako tulifika sebuleni na hatukukuta mtu hata mmoja,sasa jamaa akamrudishia Mtatiro silaha yake kisha akachukua ya kwake ambayo Mtatiro alikuwa nayo!.Jamaa alikuwa jasiri sana na ilionekana hata lile tukio halikuwa la mra ya kwanza,inaonekana alishayafanya sana yale matukio na ndiyo maana alikuwa akijiamimi sana!.Tulitembea kuelekea vyumbani ambako jamaa alituambia tufuatane nae!.Ile silaha ndugu zangu ioneni tu askari wamebeba lakini ni hatari sana,sikuwahi kabisa kusikia ikipigwa karibu,siku hiyo ndiyo nilifahamu kwanini silaha ni hatari sana hadi serikali kupambana na wahalifu!.Pia ni kitu ambacho ukiwa nacho kinakupatia kujiamini kupita maelezo,namna ambazo jamaa alikuwa akijiamini tulivyofika pale haikuwa na mfano,wewe fikiria ile sauti iliyosema "Atakaye ingia ndani huyo ni halali yangu" lakini hakujali kitu!.

Jipe "Magige fungua mlango mwenyewe"

Aliendelea "Nikifungua mimi umeumia"

Sasa kuna sauti ya kiume ikasikika ndani ya chumba ikiwa inajitetea!.

Sauti ya kiume "Tafadhali nawaomba mchukue chochote msiniue!"

Jipe "Fungua mlango unanipotezea muda msenge wewe!"

Basi yule jamaa aliyekuwa chumbani alifungua ule mlango.Baada ya kufunguliwa ule mlango Jipe aliusukuma kwa mguu kwa nguvu ukawa umejifungua zaidi!.Sasa nilibaki kushangaa kwasababu wakati tukiwa nje nilisikia huyo jamaa akisema atakaye ingia ndani atakuwa halali yake nikadhani uenda alikuwa na silaha kumbe ilikuwa zuga tu!.Tulipoingia ndani tulimkuta jamaa akiwa na mwanamke pamoja na dada mmoja na watoto watatu,wa kike wawili na wa kiume mmoja,jumla yao kufanya kuwa watu sita!.

Jipe "Pesa ziko wapi?"

Aliendelea "Usinipotezee muda nataka pesa"

Jipe "Lale chini sitaki mniangalie wapumbavu nyie"

Baada ya kusema vile,niliona yule mwanamke anawakusanya wanae na kulala chini huku wakifunika nyuso zao chini!.Sasa yule jamaa akawa kama anategea kujibu lile swali la wapi pesa ilipo,Jipe alikoki ile silaha akamtandika ya mguuni yule jamaa akaendelea kulia kwa maumivu makali pale chini.

Jipe " Nimekwambia nataka pesa usinipotezee muda"

Baada ya kuona hali inaweza kuwa mbaya zaidi ndipo yule mwanamke akapiga kelele huku akilia akisisitiza tusiwaue na akaeleza pesa ilipo!.Alinyanyuka tukaongozana nae kuelekea jikoni ambako pembeni kulikuwa na stoo!".

Yule mwanamke "Pesa hiyo hapo chini ya vigae!"

Jipe "Oya hebu funua vigae hivyo utoe hiyo hela"

Niliingia ndani ya kile chumba ambacho kilikuwa stoo nikaanza kutoa vile vigae ambavyo vilikuwa vimewekwa juu ya mzigo kwenye gunia.Nilifanya haraka sana maana hatukutaka kupoteza muda kabisa lile eneo!.Nilipofurumusha vile vigae chini,ndipo nikafikia gunia lililokuwa limejaa manguo ikabidi nilinyanyue nikalitoa mle stoo!.

Nilianza kuyatoa yale manguo yaliyokuwa kwenye lile gunia hatimae nikazifikia pesa ambazo zilikuwa nyingi zimefungwa kwenye mabunda ya elfu tano tano na elfu kumi kumi!.

Jipe "Beba tuondoke"

Nikabeba lile gunia na kuondoka eneo la tukio kuifuata ile Mark 2 iliyokuwa imepaki mbali kidogo ikitusubiri.Tuliondoka yale maeneo kwa spidi kali kuikamata njia ya Mwanza na safari ikaanza.Tulitembea kwa spidi kali hadi maeneo ya mgodi ule wa Buzwagi kisha kuikamata njia ya kuelekea eneo tulilokuwa tumemuacha Gabi,baada ya kufika pale jamaa aliniambia nikimbie haraka kumuita Gabi ili tuondoke.Gabi alitoka ndani kwa spidi kali baada ya kumshitua kisha tukaingia kwenye gari na kuondoka lile eneo.

Jipe "Mwanangu hakikisha risasi inakuwa chemba,hatujui kilichoko mbele yetu"

Mtatiro "Iko sawa tayari"

Ile gari ilikuwa inatembezwa kwa spidi kali huku ikiwa imezimwa taa,sasa kuna mahali tulifika Jipe akamwambia dereva asimamishe gari kwanza,gari iliposimamishwa akaniambia nikae siti ya mbele yeye arudi nyuma akae na Mtatiro.

Jipe "Washa taa tuondoke"

Dereva aliwasha taa na safari ikaanza,sasa tulipofika karibu na tinde,Jipe akatoa maelekezo ya kwamba,endapo kuna mtu akatokea akasimamisha gari ahakikishe hasimami!.Namshukuru Mungu pale tinde tulipita salama kabisa,sasa tulipofika mbele kabisa kuikaribia shinyanga jamaa akachukua zile bunduki akanyanyua siti walizokuwa wamekalia akaziweka,kisha tukaondoka kwa spidi kali!.Njiani hatukusumbuliwa kabisa.Tuliingia Mwanza mida ya saa 9 usiku hadi kule kwenye ile nyumba siku ya kwanza tulipoenda na Gabi!.-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-
SEHEMU YA 23.Baada ya gari kuingia ndani ya ile nyumba,Gabi alishuka na zile hela kwenye lile gunia na Jipe alifunua zile siti akatoa silaha kisha tukaingia wote ndani,baada ya kufika ndani yule dereva hakukaa sana akawa ameondoka!.Kiukweli zile hela zilikuwa nyingi mno zaidi ya milioni 50,maana tangu nilivyoanza kushika hela japo nilizoshika nyingi zilikuwa za bandia lakini nilikuwa ninafahamu bunda likiwa na milioni 1 au zaidi,zile za kwenye ule mfuko kiukweli zilikuwa nyingi na nina hakika zilizidi milioni hamsini.

Tuliamua kukaa kimya kwenye ile nyumba huku kila mmoja akitafakari kivyake kichwani mwake!,hakukuwa kabisa na muda wala hamu ya kupata usingizi!.

Sasa ilipofika mida ya saa 1 asubuhi alitokea yule bosi wake na Gabi ambaye hakuwepo hapo nyumbani na nakumbuka alikuja na kale kadada kalikokuwa kadereva tulipoenda Arusha.Baada ya kufika alikuja moja kwa moja hadi sebuleni ambapo mimi na Mtatiro tulikuwa tumejiegesha kwenye makochi.

Bosi "Jipe yuko wapi?"

Mtatiro "watakuwa huko ndani!"

Basi yule bosi aliingia ndani vyumbani huko na baada ya muda akawa ametoka akiwa ameongozana na Gabi pamoja na Jipe aliyekuwa amebeba lile fuko lililokuwa na hela!.
Bosi "Mlizihesabu?"

Jipe "Hapana bosi hatukuwa na muda huo na tumefika muda si mrefu"

Bosi "Kwanini mlimpiga jamaa risasi?"

Jipe "Alitaka kuleta ubishi bosi na sisi tulitaka kuwahi!"

Bosi "Sawa ni jambo jema ila niliwahi kukwambia uwe unaangalia na mazingira Jipe,usiwe unatumia tu risasi hata ambapo unaona hakuna uhitaji,hizo risasi nazipata kwa gharama sana!"

Aliendelea "Tukiwa Namanga nimewahi kukwambia ikiwezekana risasi itumike kwa wabishi tu na wasenge(Askari)lakini hao watu wa kawaida unaweza ukatumia kuwatishia tu wakatoa mzigo"

Bosi "Utawapa maelekezo hawa marafiki zangu pia namna ya kutumia risasi,si kila mahali!"

Baada ya yale mazungumzo yule bosi alizimwaga zile hela chini,hakika zilikuwa hela nyingi sana kama nilivyosema zilikuwa zaidi ya milioni 50.Sasa baada ya kuzihesabu zile hela alimwambia Gabi alete begi waweke zile hela,Gabi aliingia chumbani akaleta begi ambalo waliziweka zile hela.

Bosi "Kamateni hizo mtagawana wewe na mwenzio"

Aliendelea "Niliwaambia siri kwetu ni kitu muhimu kuliko hii pesa,bila shaka mnakumbuka!".

Mtatiro "Tunakumbuka bosi"

Bosi "Sawa,nawaamini sana"

Basi Mtatiro akachukua zile hela akaanza kuzihesabu na kupata jumla yake milioni 1.9 aambazo ilipaswa tuzigawane mimi na yeye.Nilimwambia Mtatiro azitie mfukoni na tungezigawana baadae.Baada ya kuchukua zile hela,Gabi alituambia wao walikuwa wanatoka kuna mahali wanaelekea na alitutaka tuondoke kurudi maskani ili tukapumzike na wakirudi angetushitua kwenye simu.

Mtatiro alimwambia simu zetu tuliziacha Arusha na hivyo hatukuwa na mawasiliano kwa wakati huo.Gabi alimuuliza yule bosi kuhusu mawasiliano na bosi wake akasema tununue simu mpya kisha tumwambie gharama tutakayoitumia kununulia hizo simu ili aturejeshee,sasa nakumbuka Gabi alimwandikia Mtatiro namba yake akasema tukishanunua simu Mtatiro ampigie.

Walipoondoka na ile Noah na sisi tuliamua kuondoka zetu kurejea kule Usagara kwenye nyumba ya braza ake na Mtatiro walipokuwa wakikaa.

Mtatiro "Hivi jamaa si alituambia tukipata pesa tutakuwa tunagawana pasu kwa pasu!"

Aliendelea "Sasa mbona wametupa milioni 1.9?"

Mimi "Mwanangu siungemuuliza Gabi?"

Mtatiro "Mimi nilidhani labda wamekosea hivyo nilitaka kuona labda wangetuongeza nyingine"

Mimi "Hata hivyo hii ni siku ya kwanza Mtatiro pia siunakumbuka alisema hela niya kwake"

Mtatiro "wewe ngoja tukanunue simu,nitamuuliza Gabi"


Baada ya muda ndipo nilikuja kugundua kumbe yule jamaa ambaye tulienda kwake kufanya tukio alikuwa mfanyabiashara wa madini hapo Kahama.Kiukweli niliumia sana moyo kwa kile kitendo tulichokuwa tumekifanya lakini tayari nilikuwa mikononi mwa watu wabaya wasiokuwa na huruma!.

Baada ya kuwa tumenunua zile simu,Mtatiro alimpigia Gabi simu na akamwambia wao wako Arusha wangerejea baada ya siku 3,hivyo alimwambia jamaa akifika tutaonana tuzungumze mambo mengi!.Kweli!,Baada ya wiki kupita tangia tufanye lile tukio,Gabi alimtafuta Mtatiro akawa amesema tunapaswa kuonana nae!.Tuliondoka tukaelekea mjini pale tulipokutana siku ya kwanza Golden Crest.

Gabi "Wanangu si mko lakini!"

Mtatiro "Tuko poa kaka"

Gabi "Tulienda Arusha mara moja,nimerudi mimi na Jipe ila mkuu kabaki atakuja wiki ijayo"

Mtatiro "Vipi nyie mlipewa chenu?"

Gabi " Yeah kila mtu alipewa chake!"

Mtatiro "Lakini bosi alisema tutakuwa tunatoka pasu kaka"

Gabi "Mwanangu pesa bado zipo nyingi mno,hiyo ni rasha rasha tu!"

Aliendelea "Unajua yule Magige waliwahi kufanya na mkuu biashara,sasa nadhani kuna udhurumaji ulifanyika ndiyo maana mkuu alitaka tuzifate pesa zake"

Gabi "Pesa bado zipo nyingi kaka wala hata usiwaze kwa hilo!"

Basi baada ya yale mazungumzo ya Gabi ni kama alituliza presha ya Mtatiro.Tulimaliza pale yale mazungumzo kisha tukaanza kupata beer ambapo tuliondoka mida ya saa 3 usiku.
Nakumbuka tulikaa mtaani wiki 2 bila kazi,na wiki ya tatu ilipoanza,Gabi alitutafuta kwenye simu akatuambia tuelekee kule mjengoni ili kuona tunajipangaje namna ya kutoka kuelekea kwenye uvamizi tena!.

Tulipofika pale kama kawaida tulimkuta Gabi,Jipe pamoja na jamaa mmoja ambaye ndiye alikuwaga akibaki pale kwenye ile nyumba,sasa baada ya muda alikuja yule demu aliyekuwa akiendesha ile Noah.

Jipe "Mko poa wanangu"

Mtatiro "Si tuko poa kaka,umetutenga sana"

Jipe 'Safari hii tutatoka wote jamaa zangu"

Aliendelea "Nyie ndio wanangu siwezi kuwatupa"

Mtatiro "Sawa,tupe mchongo"

Jipe " Tutaondoka leo usiku kuelekea Geita tutaenda kupitia Kahama ndiko hakuna hakuna wakuda,tukifika kuna nyumba tutafikia kisha tutapumzika hapo halafu kesho tutaifanya kazi itakayotupeleka hapo"

Aliendelea "Simu zote tutaziacha hapa na pia kama kuna mtu anavyo vitambulisho itabidi aviache hapa,kule tutaenda kama tulivyoenda Kahama,hatupaswi kuwa na chochote zaidi ya masihine!"

Jipe "Gabi wewe nadhani una maelekezo kutoka kwa bosi hivyo unajua cha kufanya"

Aliendelea "Wewe Kamange unaijua kazi yako,nimemaliza!"

Basi baada ya yale maelekezo kila mmoja alisubiri ifike usiku ili tuianze safari!.
-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-


SEHEMU YA. 24.Kamange ndiye aliyekuwa dereva kwenye ile Noah na mara zote alikuwaga hana kabisa stori na mtu!.Tulifanikiwa kufika Geita salama kabisa mida ya saa 6 usiku tukipitia njia ya Kahama,kwa mujibu wa malekezo ya Jipe ni kwamba,endapo tungepitia Kigongo/Busisi yawezekana kabisa tungeweza kugundulika kwenye ukaguzi,hivyo kwakuwa hatukuwa na haraka,jamaa akasema tupitie Kahama.

Baada ya kufika Geita usiku huo,aliyekuwa akituelekeza mahali pa kwenda alikuwa ni Jipe ambaye yawezekana aliifahamu vizuri ile mitaa ya Geita na viunga vyake,binafsi ukiacha siku tuliyoenda na Mtatiro kwenye mnada wa kuuza mitumba huko kwenye kijiji cha Nzera,sikuwahi tena kufika Geita hadi siku hiyo.Sasa Jipe alikuwa akimpatia yule demu dereva maelekezo namna ya kuifata njia yenye uelekeo sahihi wa kutufikisha tunakokwenda!.Haukupita muda tukawa tumefika kwenye nyumba ambayo haikuwa na fensi wala geti,sasa ile nyumba ilikuwa mbali kidogo kutokea pale mjini!.

Mimi,Mtatiro na Jipe tuliteremka wakati huo huo Gabi na Yule demu waliondoka na gari wakaahidi wangerudi kesho asubuhi!.Jipe alianza kugonga mlango wa ile nyumba hatimae mwenyeji akawa amefungua mlango.

Jipe "wachamawe sengi"

Yule mama "Wachatata"

Jipe "Mwasibhao"

Yule "Chasibhao lata,jendeyo"

Jipe "Ni jakisi sengi"


Jipe alinyanyua lile begi ambalo lilikuwa na silaha kwa chini na juu likiwa na nguo baadhi tukawa tumeingia ndani.

Jipe "Aisee huyu ni Shangazi yangu anaishi hapa Geita ni mwalimu,hivyo jisikieni huru"

Aliendelea "Shangazi,hawa ndiyo wale marafiki zangu ambao nilikwambia tunapita kulala hapa halafu kesho tunaelekea Nyarugusu"

Yule mama "Sawa baba,hapa ni kwenu,usijali"

Aliendelea "Mtalala kwenye hicho chumba wanangu"

Yule mama baada ya maongezi ya dakika kadhaa alituacha pale sebuleni akawa ameingia chumbani kwake kulala.

Jipe "Twendeni tukapige mbonji wazee"


Basi tuliingia chumbani tukawa kulala hadi asubuhi,ilipofika asubuhi Jipe aliamka akawa ameondoka pale kwa shangazi yake na akatutaka tusitoke hadi ile gari itakapokuja kutuchukua.Wakati tukiwa hapo kwa huyo mama,Mtatiro alianza kuniambia anajisikia vibaya sana na hali yake si nzuri!.

Mimi "Shida ni nini kwani?"

Mtatiro "Yaani nahisi tu baridi na najisikia kizinguzungu!"

Aliendelea "Ila niko poa wala usijali"

Mimi "Au nikakuchukulie panadol"

Mtatiro "Ngoja jamaa arudi umwambie"

Baada ya muda Jipe alirudi akatutaka tukapande gari tuondoke zetu,nilijaribu kumshirikisha hali ya mshikaji wangu Mtatiro akaniambia watamnunulia dawa tukifika tulikopaswa kwenda!.Tulipotoka nje,yule mama hatukumkuta bali tuliwakuta mabinti wawili wakubwa wakiwa wanaendelea na shughuli zao.

Jipe "Mi naondoka,mtamwambia Shangazi nitarudi"

Binti "Sawa kaka"


Tuliondoka na kushika njia kama tunarudi Mwanza,kuna mahali tulifika tukaikamata barabara ya vumbi iliyokuwa inatutoa nje ya ule mji wa Geita,baada ya kutembea kwa umbali mrefu kidogo hatimaye tukafika kwenye nyumba moja iliyokuwa na tofauli za kuchoma,ambapo Jipe alishuka akaenda kufungua ile nyumba kisha akatutaka tuteremke na kuingia ndani!.Baada ya kufika ndani Jipe akaanza kutoa maelekezo kwa kila mmoja!.

Jipe "Jamani hapa ndipo tutakaa mpaka usiku wa leo,na tukimaliza kufanya kilichotuleta tunaondoka leoleo!"

Aliendelea "Gabi nadhani nenda nilikokwambia"

Jipe "Kamange hakikisha hiyo gari ni nzima,kama kuna tatizo ipeleke gereji muda huu!"

Kamange "Gari inawasubiri nyinyi tu!"

Jipe "Ok,sawa"

Jipe alitoa hela kidogo akawa amempa yule demu aende pharmacy akamnunulie Mtatiro Panadol ili kuondoa ile hali ya sintofahamu aliyokuwa nayo.Sasa kwakuwa ile nyumba ilikuwa na vyombo vya kupikia,Jipe alishauri zikanunuliwe dagaa na unga tuje tukorofishe ili tuweze kupata chakula,na hivyo ndivyo tulivyofanya.
Ilipofika mida ya Saa 1 usiku hali Mtatiro ilizidi kuwa mbaya hata baada ya kumeza vidonge,yeye kwa maelezo yake alikuwa akidai anaihisi baridi na kujisikia vibaya mwili mzima.

Jipe "Kwahiyo sa itakuwaje mwanangu"

Aliendelea "Chuma utaweza kushika?"

Mtatiro "Kwani tunaondoka sa hivi?"

Jipe "Mida inakaribia"

Mtatiro "Ngoja tuone"

Sasa ilipofika mida ya saa 4 usiku kuelekea saa 5,Jipe baada ya kuona hali ya Mtatiro haikuwa ya kuridhisha alinipatia maelekezo!.

Jipe "Umughaka utashika chuma ya Mtatiro"

Mimi "Sawa"

Jipe "Usifanye tofauti na nitakachokwambia"

Mimi "Sawa"

Baada ya nusu saa tukiwa tupo tayari kuondoka,simu ya Jipe ilikuwa ikiita,jamaa aliipokea akaanza kuzungumza.Sasa aliyekuwa amepiga ile simu alikuwa Gabi ambaye yaelekea alikuwa akimpatia maelekezo Jipe.

Jipe "Kamange yuko wapi?"

Mimi "Nadhani atakuwa kwenye gari!"

Jipe "Twendeni"

Aliendelea "Tukitoka huko ni kuondoka tu kurudi Mwanza,hatuna muda wa kupoteza!"

Baada ya kutoka nje ya ile nyumba,Jipe alifunga kofuli kisha ufunguo akauweka juu ya mlango kwenye venti.Tuliondoka lile eneo kuelekea ambako walikuwa wakipafahamu Jipe na Gabi,sisi wengine ilikuwa ni wafuata maelekezo tu.Haukupita muda tukawa tumefika kwenye nyumba zilizokuwa mtaa wa kifahari kweli kweli.

Jipe "Umughaka ile nyumba yenye geti jeusi unaiona?"

Mimi "Ile ya mbele?"

Jipe "Ukiacha hiyo yenye paa refu,ile yenye geti jeusi siunaiona?"

Mimi "Ndiyo"

Jipe "Ok,hakikisha ukifika wewe gonga na wakiuliza nani waambie mimi respis geti,wakifungua tu hiyo kazi nyingine niachie mimi!"

Aliendelea "Kamange nyuma ya hii nyumba kuna njia isiyo rasmi,nenda kapaki hapo tunakukuta"

Kamange "Gabi yuko wapi?"

Jipe "Tutamkuta mbele"

Kamange "Mjulishe kabisa akae standby,sitaki lawama"


Mimi na jipe tulitelemka kwenye ile Noah huku tukiwaacha Kamange na Mtatiro ambaye hali yake haikuwa nzuri.Ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kuikamata silaha na kiukweli ilikuwa nzito kwa kiasi chake.

Nilichukua kitambaa cha kiujifunika nikakiweka mfukoni huku ile silaha nikiwa nimeiweka kwenye ndani ya koti.Nilipofika kwenye lile geti nilianza kugonga kwa nguvu mara kadhaa!.Wakati nilipokuwa nikigonga lile geti Jipe alikuwa pembeni huku akiwa makini sana.

Sauti ya mwanaume "Naniii !?"

Mimi "Mimi Respis"

Sauti "Nakuja"

Haukupita sekunde 20 lile geti lilifunguliwa kisehemu kidogo kile ch a watu kupita.Geti lilipofunguliwa tu Jipe alisukuma kwa nguvu huku akitoa silaha na kumuonyeshea yule jamaa.Jamaa alitaka kupiga kelele lakini Jipe alimdhibiti akamwambia akipiga kelele atamuua!.

Jipe "Ingia ndani fasta na ufunge hilo geti!"


Jipe alimchukua yule jamaa akiiingia nae ndani huku na mimi nikiwa nyuma nimeshika ile silaha iliyokuwa imenipatia kiburi kisichokua cha kawaida.

Jipe "Kaka yako yuko wapi?"

Yule jamaa "Braza amesafiri"

Jipe "Upo na nani humu ndani?"

Jamaa "Nipo na shemeji yangu pamoja na mdogo wake"

Jipe "Umughaka kaa tayari kwa lolote,ukiona hatari ruksa kuua"

Mimi "Sawa"

Jipe alimchukua yule jamaa ambaye alikuwa akitetemeka kama kashikwa na degedege kisa kuona ile SMG,baada ya muda Jipe alirudi na watu watatu pale sebuleni huku yule mwanamke akiwa ndani ya chupi tu.Alikuwa mwanamke,yule jamaa aliyetufungulia geti pamoja na dogo mmoja wa kiume ambaye kimuonekano alikuwa na miaka 12.

Jipe " Laleni chini mfunike sura zenu"

Aliendelea "wewe mume wako yuko wapi"

Mwanamke "Amesafiri"

Jipe "Kwenda wapi?"

Mwanamke "Ameenda Dar"

Jipe "Nataka pesa,ziko wapi?"

Mwanamke "pesa huwa tunapeleka benki,tafadhali msinifanye chochote twendeni benki nikawapatie"

Jipe "Wewe nitakupasua ubongo,nahitaji pesa wewe unaleta ujinga!"

Mwanamke "Hapa kipo kiasi kidogo,tafadhali usiniue"

Yule mwanamke alikuwa anaongea huku machozi yakimtoka kama mvua,wakati fulani huruma ilikuwa ikiniingia lakini sikuwa na namna!.

Jipe "Zipo shilingi ngapi wewe acha kutupotezea muda!"

Kabla mwanamke hajajibu swali,Jipe alimnyanyua akawa amerudi nae huko chumbani,wakati huo mimi pale sebuleni niliendelea kuwachunga wale madogo huku silaha ikiwa tayari kwa lolote.Baada ya muda Jipe alirudi pale sebuleni akiwa na kanga iliyokuwa imejaa pesa,ile kanga namna ilivyokuwa imefungwa ni kama furushi la nguo chafu.

Jipe aliwaambia wale madogo wasimame wote na tulielekea chumbani ambako aliwaambia waingie chini ya uvungu kisha akafunga mlango kwa nje na funguo.

Baada ya hapo tuliingia kwenye kile chumba cha yule mwanamke na kupekua kika mahali lakini hatukupata pesa nyingine.

Jipe "Ingia chini ya uvungu,ole wako upige kelele ndipo utajua mimi ni nan!"

Yule mwanamke aliingia chini ya uvungu kama kafukuzwa,ndipo jipe alichukua funguo akafunga mlango kwa nje akaniambia tusepe.Tulitoka ndani haraka kuifata ile Noah iliyokuwa imepaki nyuma ya ile nyumba,tuliingia ndani na kuondoka haraka sana lile eneo.

Baada ya mwendo mrefu kidogo huku tukiiacha Geita,kuna mahali tulifika Jipe akamwambia yule demu asimamishe gari.Jipe alitoa simu akaanza kupiga.

Jipe "Uko maeneo gani wewe?"

Aliendelea "Subiri hapo njiani tumekaribia"

Sasa kumbe alikuwa amempigia Gabi akitaka kujua yupo maeneo gani.Baada ya mwendo ambao haukuzidi dakika 3 tulimuona Gabi akiwa barabarani ndipo gari ikasimama akapanda tukaondoka zetu.

Jipe "Umefanikisha"

Gabi "Kama kawa"

Sikuelewa ni kitu gani ambacho Gabi alikuwa akikifanya muda huo huko alipokuwa,hiyo ilibaki ni siri yake yeye na Jipe.

Tulifanikiwa kufika Mwanza saa 11 alfajiri ambako moja kwa moja tulipitiliza hadi kwenye ile nyumba ambayo ndipo yalikuwa makazi yetu ya mipango mikakati.

Ilipofika mida ya saa 2 asubuhi,Jipe alitupatia kila mmoja wetu mimi na Mtatiro laki 5,sikufahamu wale wengine walipewa kiasi gani maana sisi tuliondoka zetu!.Kiukweli ile pesa iliyokuwa imefungwa kwenye ile kanga sikufahamu ilikuwa kiasi gani maana kule Geita hatukuwa na muda wa kuhesabu,na hata tulivyofika hapo kwenye hiyo nyumba,Jipe na Gabi waliingia chumbani na lile furushi!.


Mtatiro "Hawa wasenge ngoja uje uone"

Mimi "Kwanini?"

Mtatiro "Wewe unaona makubaliano yetu yanatekelezwa?"

Aliendelea "Hawanijui vizuri,siwezi kuweka roho yangu rehani halafu unilipe laki 5"


Ile hela Mtatiro aliniambia tuiweke kwenye mtaji wa mitumba ili tuzidi kuizungusha .Sasa nakumbuka siku moja tukiwa pale Hungumahlwa kwenye harakati za kupambana na mitumba,ghafla hali ya mshikaji wangu mtatiro ilibadilika na akaniambia yeye inabidi arudi nyumbani akatafute dawa ameze ili hali itengemae,tulikubaliana tungeonana nyumbani!.

Ilipofika mida ya saa 8 mchana nilipigiwa simu,nilipotoa ile simu mfukoni nikakuta ilikuwa namba ya Mtatiro akinipigia,lakini baada ya kupokea nikakuta si yeye akiongea!.

Sauti "Hallo!"

Mimi "Hallo"

Sauti "Wewe bila shaka ni Umughaka"

Mimi "Ndiyo"

Sauti "Hebu kama unaweza njoo hapa Bugando"

Mimi "Niko mbali kidogo"

Sauti "Uko nje ya Mwanza?"

Mimi "Nipo Hungumalwa"

Sauti "Jitahidi ufike haraka"

Sikutaka kupoteza muda pale mnadani,nilichukua mzigo wangu nikaufunga nikaenda kuupakia kwenye fuso ambalo mara zote tulikuwaga tukipakia mizigo yetu kisha nikampatia dereva maagizo mahali pa kwenda kuushusha.Niliondoka hapo Hungumalwa na nikafanikiwa kufika Bugando mida ya saa 11 jioni.Sasa nilipofika niliipiga ile namba ya Mtatiro na hatimae ikapokelewa na yule yule mtu aliyekuwa amenipigia,alinielekeza mahali alipokuwa ndipo nikamfuata.Kumbe yule mtu alikuwa ni daktari na alitaka kunipatia taarifa ya Mtatiro.
Kiukweli nilianza kuingiwa na hofu sana kwasababu Mshikaji wangu Mtatiro aliondoka akiwa anajiweza kutembea sasa sikujia ni kitu gani kilikuwa kimempata.

Niliingia hadi kwenye chumba alichokuwa ameniambia niingie,nilipoingia nilimkuta Mtatiro pia yupo akiwa amekaa kwenye kiti,baada ya kumuona Mtatiro pale kwenye kiti angalau moyo wangu ulitulia.

Jamaa(Daktari) "Mambo vipi kaka"

Mimi "Safi kabisa kaka"

Jamaa "Karibu kiti kiti"

Aliendelea "Bila shaka huyu unamfahamu"

Mimi "Ndiyo"

Jamaa "Ni nani yako?"

Mimi "Ni rafiki zaidi ya ndugu"

Jamaa "Kwahiyo mnaaminiana?"

Mimi "Ndiyo"

Jamaa "Sasa mimi nimekuita hapa kwa ridhaa ya huyu ndugu yako,maana nilimwambia aniitie ndugu yake wa karibu ndipo akasema nikutafute wewe,bila shaka hali yake unaiona"

Aliendelea "Amewahi kukwambia kinachomsibu?"

Mimi "Hapana kwakweli"

Jamaa "Sawa,Bwana Mtatiro,ni vema rafiki yako akafahamu kinachokusibu atakuwa msaada kwako kama hutojali!"

Mtatiro "Haina tatizo dokta wewe mwambie huyu ni rafiki yangu tunapendana na kuheshimiana!"

Jamaa "Sawa,sasa bwana mimi nimekuita hapa kwa ajili ya huyu ndugu yako,ndugu yako ni muathirika wa virusi vya Ukimwi na kama ulivyoutaratibu mgonjwa anapopimwa na kugundulika na hilo tatizo huwa tunamuanzishia utaratibu wa kuanza matibabu"

Aliendelea "Ndugu yako huyu alianza dozi kama kawaida lakini kuna muda huwa anategea sana kuja kuchukua dawa mara zile tulizompa zinapokwisha,hivyo inamuondolea ufanisi wa afya yake,pia kwakuwa wewe upo hapa naomba uwe unamshauri asiwe mtu wa kunywa sana pombe,si nzuri kwa afya yake!"

Niliendelea kumsikiliza yule daktari kwa makini wakati huo moyo wangu ulikuwa unauma sana,sikutaka kuonyesha hadharani pengine ningemfanya mshikaji wangu aliyekuwa akiniamini Mtatiro ajisikie vibaya,nilikuwa makini sana ili nisije kuleta sintofahamu!.

Jamaa "Sasa naomba hizi dawa nazompatia hapa,hakikisha kila siku anameza kwa masaa yale yale atakayojipangia yeye ili kuweza kumjengea kinga imara dhibi ya mashambulizi nyemelezi"

Aliendelea "Naomba umsimamie awe anameza dawa kila siku na kama nimivyokwambia umshauri aache pombe,pia azingatie lishe bora!"


Baada ya mazungumzo tulitoka nje na Kuondoka zetu nyumbani,nilikuwa namlaumu sana rafiki yangu Mtatiro kwanini aliacha kuzingatia dawa wakati alilifahamu tatizo lililokuwa likimkabili,kiukweli sikumuonyesha chuki bali nilimpenda sana rafiki yangu na nilitaka afanye vema zaidi ili afya yake iendelee kuimarika.Sikumbagua bali niliendelea kumshauri na kumfanya awe na furaha muda wote kama rafiki yangu.-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-/-SEHEMU YA 25."Wewe ni mtu muhimu sana kwangu Mtatiro na umekuwa sehemu ya furaha katika maisha yangu,ulinipokea na kunisaidia wakati mzee aliponitimua nyumbani,hukuniacha katika matatizo bali ulinishika mkono kama kijana mwenzio hivyo na mimi sitokuacha rafiki yangu" ni maneno niliyokuwa nikimwambia rafiki yangu wa damu Mtatiro ili aendelee kuwa na amani kabisa.

USHAURI

Kuishi na Virusi vya Ukimwi si mwisho wa maisha na uhai,kama kuna kitu nakichukia katika maisha yangu ni ubaguzi huu unaofanywa kwa hawa ndugu zangu,haya ni maisha tu na tunapaswa kupendana,unaweza ukawa muaminifu na bado mumeo/mkeo akakuletea ugonjwa,hivyo hatupaswi kuwanyooshea wengine vidole kana kwamba ni wadhambj kuliko sisi,tuache dharau za kijuaji na kebehi zisizo na msingi!.
Ndugu zangu pia niwaombe mzingatie dawa kwa wakati ili ziweze kuwafubaza virusi angalau unapokutana na mwenzako usimuambikize ili muendelee kufurahia maisha,jambo la msingi ni wewe mwenyewe kuacha kujibagua,jikubali na songa mbele!.Acha starehe za kijinga,panga mipango yako na timiza ndoto zako,usiwe mlevi kupita kiasi na hakuna sababu ya kuwaambukiza wengine kwa makusudi,wapende watu wote.Pia achana na imani za mitume na manabii kwamba wakupatie maji au mafuta utumie kisha uache dawa,achana kabisa na hizo imani mfu,wewe muombe Mungu atakusikia,kama akipenda anaweza kuuondoa huo ugonjwa na kama akiona inafaa wewe kuendelea nao basi Mshukuru na endelea kuishi,hata kama ukimuomba Mungu na ugonjwa usitoke lakini Mungu bado atabaki kuwa mwema hivyo usikate tamaa.

Basi baada ya afya ya rafiki yangu kipenzi Mtatiro kuimalika tuliendelea na kazi yetu ya kuuza mitumba sehemu na vijiji mbalimbali vya kanda ya ziwa.Nakumbuka siku moja Gabi alimpigia simu Mtatiro akawa amemuambia inapaswa tuonane ili tupange mikakati ya kuelekea maeneo kama kawa.Kweli,tuliondoka siku iliyofuata kuelekea kule yalipokuwa makazi ya muda ilipokuwa inasukwa mipango kabla.Tulipofika pale ndani tulimkuta Gabi kama kawaida akiwepo Jipe na jamaa yule dereva tuliyeenda nae kwenye tukio kahama.

Jipe "Wanangu mko poa"

Mtatiro "Tuko fiti kaka"

Jipe "Sasa Kesho safari ni Kagera"

Aliendelea "Si mko vizuri?"

Mtatiro "Sisi tuko tayari hata leo kaka ni nyinyi tu!"

Jipe "Sawa,Gabriel atatangulia leo halafu sisi kesho jioni tutaondoka"

Basi baada ya yale mazungumzo Jipe akatutaka tujitayarishe kwa ajili ya safari kesho yake.Mimi na Mtatiro tuliamua kurudi nyumbani huku Mtatiro akiapa na kusema safari hii wakijidai kutudhurumu basi ama zake ama zao!.

Siku iliyofuata mida ya saa 7 mchana tulikuwa tushafika eneo la tukio na ndipo tukakamata Noah na kuianza safari ya kuelekea mkoa wa Kagera,kwenye gari nilikuwa mimi na Mtatiro wakati huo jipe akiwa amekaa kwa mbele pamoja na yule jamaa dereva!.Tuliingia Kagera mida ya saa 12 asubuhi siku iliyofuata,njia tuliyotumia ni ileile ya kupitia Kahama huku tukiwa makini kupita maelekezo,Jipe alikuwa ametoa maelekezo ya kwamba,yeyote atakaye jiingiza mkenge basi ingekuwa ni halali yetu!.
Baada ya kufika Kagera,Jipe aliwasiliana na Gabi ambaye alimuelekeza maeneo ambayo tungemkuta,nakumbuka tuliikamata njia na uelekeo wa Bukoba mjini,nje kidogo ya mji tukamkuta Gabi.

Gabi "wazee kwa huku itabidi tuzunguke kidogo muda uende kwasababu hatuna makazi,na ikifika mida tutaitana tufanye kilichotuleta".

Kwakuwa mimi na Mtatiro ndiyo ilikuwa mara yetu ya kwanza kufika Kagera ilibidi tukae kwenye ile gari maana hatukutaka kucheza mbali tukajichanganya na ukizangatia hatukuwa na simu!.Dereva alitafuta maeneo ambayo hayakuwa na shughuli nyingi za watu akapaki gari hapo!.

Ilipofika mida ya saa 10 jioni mvua ikaanza kunyesha kama masikhara lakini muda ulipozidi ndipo hali ilizidi kuwa mbaya,tangu nizaliwe sijawahi kuona radi zikipiga kama siku hiyo,ile mvua ilikuwa na radi si mchezo hadi uoga ukawa unaniingia!.Kadiri muda ulivyozidi ndivyo mvua nayo ilizidi kuongeza spidi na nilikuwa naona Jipe anaomba iendelee kunyesha vilevile isikatike.Sasa ikafika mida ya saa 12 ikapungua ikawa inanyesha kidogo sana,tulikuwa ndani ya gari wakati huo tukiendelea kuvuta muda.Ilipofika mida ya saa 3 usiku mvua ikaanza tena kunyesha kama mwanzo.

Jipe "Huu ni muda sasa"

Aliendelea "Aisee wewe utaenda kutusubiri mahali nitakapokuelekeza"

Jipe "Wengine wote tutaongozana na mtafanya kila nitakachowaambia"

Basi ile gari ikaanza kuondoka kuelekea uelekeo wa Bukoba Mjini,kuna mahali tulifika ambapo kwa umbali kama wa mita 500 kulikuwa na sheli(sitoitaja),dereva alitakiwa kuzima taa na kugeuza gari atusubiri hapo!.Kila mmoja alikuwa tayari kwa ajili ya makabiliano.
Muda huo ilikuwa ni saa 4 usiku lakini kulikuwa na mvua kubwa sana,tulipofika kwenye ile sheli baada ya Jipe kuchomoa SMG kuna mlinzi alimuona akaanza kukimbia kama mwehu huku akiwa na gobole,Jipe hakutaka kumpotezea muda,alipiga risasi ya mgongoni yule mlinzi akawa amedondoka chini.

Jipe "Mtatiro kusanya hao wauza mafuta wote"

Jipe aliingia ndani kwenye vyumba vilivyokuwa kando ya ile sheli huku akiniambia niongozane nae.Pale nje Mtatiro na Gabi waliendelea kuwadhibiti wale wauza mafuta na kuchukua hela huku wakiwa chini ya ulinzi mkali.

Jipe "Toa pesa wewe la sivyo nitakuua"

Jipe alikuwa akimwambia dada mmoja kibonge ambaye tulimkuta mle ndani wakati huo akimnyooshea mtutu wa bunduki.Yule dada alifungua boksi moja lilikuwa la mbao na kulikuwa na noti za kutosha,sasa kulibeba lile boksi mwenyewe kidogo likawa zito,Jipe akamuamuru yule demu atupatie mfuko,yule demu alitoa mfuko mmoja ambao ulikuwa kama shuka ambao ulikuwa umechakazwa na rangi ya maoili!,niliukamata ule mfuko haraka nikaanza kuchukua zile hela haraka sana,sikutaka kabisa kuhangaika na silva maana jipe alisema nitemane nazo,baada kumaliza zile hela,Jipe alimuamuru yule demu alale chini na asijaribu kuinua kichwa kwani atamuua,tuliondoka chap mle ndani kuelekea nje ambapo tuliwakuta Gabi na Mtatiro wakiwa wanatusubiri!.

Tulikimbilia gari na tulipofika dereva aliondoka kwa spidi kali sana lile eneo,wakati huo bado mvua ilikuwa ikiendelea kunyesha sana.Wakati tupo njiani,Jipe alimpigia simu yule demu Kamange na kumtaka achukue ile gari Mark 2 atukute Geita.Ile Noah ilitembea vibaya mno usiku huo na tulifanikiwa kufika Geita mida ya saa 8 Usiku,Jipe akawa amemwambia Gabriel na dereva ya kwamba wao watangulie Mwanza halafu sisi tungeisubiri ile Mark 2.

Kweli,Kesho yake mida ya saa 4 asubuhi yule demu akawa amefika pale Geita kutuchukua tukawa tumeondoka,Tuliingia Mwanza mida ya saa 11 jioni.Tuliwakuta kina Gabi wao wameshafika,sasa tulipofika Mtatiro alimwambia Jipe ya kwamba pesa tulizopora ziletwe zihesabiwe ili kila mtu afe na chake,nadhani wao walidhani Mtatiro anatania lakini jamaa alikuwa serious sana,sikuwahi kufahamu kama Mtatiro akikasirika anakuwa vile aisee,mara zote mimi nimekuwa nikimuona akiwa kawaida nikawa namchukulia poa,siku hiyo ndiyo niliiona rangi halisi ya yule mkurya.

Mtatiro "Haiwezekani tupore pesa halafu nyie muwe mnagawana nyingi na sisi mnatupa kidogo,mkitaka damu leo imwagike ficheni hizo hela muone!"

Jipe "Hakuna atakayedhurumiwa hata mmoja"

Mtatiro "Mbona juzi mmetunyenga?"

Jipe "Yale yalikuwa ni maelekezo ya bosi"

Mtatiro "Basi mwambieni leo kila mtu anapata pasu,sitaki ufara!"

Baada ya jamaa kuona Mtatiro yuko serious,Jipe alimwambia Gabi walete zile pesa ili kila mmoja apewe haki yake.Kweli,mimi na Mtatiro kila mmoja alipata mioni 6,na wao pia walipata kama sisi.Tuliamua kuondoka zetu baada ya kupokea mgao wetu.

Mtatiro "Mwanangu kama ni hela ya mtaji tushapata,tuachane na hizi habari wao kama wanaendelea ngoja waendelee"

Aliendelea "Cha kufanya tukafungue duka la jumla tuachane na mitumba"

Mtatiro "Au wewe unaonaje mwanangu?"

Mimi "Kwanini tusifungue duka la vipodozi?"

Mtatiro "Eti eeeh,sawa?"

Baada ya kupata ile hela kweli tuliachana na biashara ya mitumba na tukafungua duka la vipodozi yale yale maeneo ya Usagara tukaanza kupambana,nakumbuka Mtatiro alikuwaga anafuata vipodozi Uganda kwasababu huko ndiko vilikuwa vinapatikana kwa bei ya chini,kiukweli tulipiga sana hela na maisha yetu yalianza kubadilika mdogo mdogo,ilifika sehemu tukahama pale kwa braza ake Mtatiro kila mmoja akaenda kupange geto lake mwenyewe!.

Nakumbuka siku moja Mtatiro akaja kuniambia kwamba Gabi anampigia simi twende kuna mchongo wenye hela kubwa tukapige.

Mimi "Umemwambiaje!"

Mtatiro "Mi nimemwambia kwasasa tunashughuli zetu,wao kama wanaendelea waendelee!"

Aliendelea "Jamaa baada ya kumwambia ananiambia kwamba tunataka kuwachoma,hivyo tujiangalie tutaumia"

Mimi "Sasa itakuwaje?"

Mtatiro "wale hawawezi kututisha we tulia"

Basi baada ya jamaa kuona hatuwapi tena ushirikiano wakaamua kutokutushirikisha kwenye michongo yao tena lakini walikuwa wamechukia sana baada ya sisi kuachana nao.Baada ya miezi kadhaa kupita,kuna siku Mtatiro akaja kuniambia amesikia habari mahali kuna majambazi wamedakwa wengine wameuawa huko Mbeya na mmoja wapo wa waliodakwa ni Gabi,sasa baada ya kuifatilia ile habari ni kweli kabisa ilikuwa Jipe na majambazi kadhaa wenzie waliuawa palepale eneo la tukio.

Kumbe walienda kumpora mfanyabiashara mmoja mwenye asili ya India ambaye ndani ya gari alikuwa na madini pamoja na pesa alizokuwa akizitoa huko Chunya kuelekea Mbeya,sasa wao hawakujua yule mfanyabiashara alikuwa na eskoti ya askari kadhaa,yawezekana walijua hilo ila wakajifanya wabishi kwakuwa walikuwa na silaha.Walikufa majambazi wawili na mmoja akiwa Jipe huku Gabi na mwingine mmoja wakisalimu amri.

Gabi alifungwa miaka the thelathini gerezani na mwaka juzi nimetoka kumuona pale gereza la Ruanda Mbeya.Jamaa amechoka sana na aliponiona mara ya kwanza alionyesha huzuni lakini hakuwa na namna ndo hivyo ishatokea.Aliniambia yule aliyekuwa bosi wake alikimbilia huko Kenya kuanzisha maisha huko.Huwa namtembelea jamaa nikipata nafasi,na siachi kumtia moyo na kumfariji,namwambia ashukuru akufa,maadam yuko hai basi atatoka tu gerezani na ataendelea na maisha yake ingawaje atakuwa amepoteza muda.

Mimi na Mtatiro lile duka la vipodozi tuliuza na kila mmoja akaendelea na biashara zake,Mtatiro aliondoka kwenda Uganda kwa anko wake hadi leo anaishi huko.Mimi niliamua kurudi Tarime Sirari nikafungua duka nikaanza kukimbiza,kuna mtoto wa dingi mkubwa anaishi Dar es salaam alikuwa anafanya biashara ya vyombo akaniambia nije tuungane tufanye biashara kwa kua inalipa sana,hivyo nikaondoka Tarime kuja Dar,kufika nikampatia jamaa zaidi ya milioni 9 akanidhurumu hadi leo,niliamua kumuachia Mungu nikaanza kupambana upya kutafuta mtaji,nilipopata mtaji nikanunua bodaboda yangu ambayo ndiyo inaniingizia kipato kwa hapa mjini.


Nawapenda sana.


MWISHO.
 
portrait-chicken-poultry-hen.jpg
 
Nisikuchoshe na usinichoshe,tusichoshane!.


Kwenye haya maisha kuna wakati huwa ninakaa chini na kusema "Kama sikufa kipindi kile,basi siwezi kufa mpaka Mungu atakaporuhusu". Nadhani wengi mtakumbuka ni siku chache tu zimepita nimeandika kisa cha maisha ambayo nilikutana nayo wakati nikiwa
Hii ina vipande vingapi ? Tujiandae kabisaa maana vidole vyako vinapima chumvi ya uandishi mzuri sana..... Wacha twende nayoo mpaka mwisho
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom