RC kutangaza jiwe linalocheza | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

RC kutangaza jiwe linalocheza

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by nngu007, Apr 11, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Apr 11, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  na Jovither Kaijage, Ukerewe  MKUU wa Mkoa wa Mwanza, Abbas Kandoro, ameshangazwa na kushitushwa na jiwe la ajabu lililopo katika Kijiji cha Nyamanga katika Kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe, linaloimbiwa na kucheza na kuahidi kulitangaza ili liweze kuchangia pato la taifa.
  Ahadi hiyo aliitoa juzi baada ya kutembelea jiwe hilo vikiwemo vivutio kadhaa vya utalii vilivyopo katika Wilaya ya Ukerewe ambapo pia aliziagiza halmashauri za wilaya mkoani humo kutambua na kutunza vivutio hivyo kwa faida ya vizazi vijavyo.
  Akiwa eneo la jiwe hilo lililo kando ya Ziwa Victoria, Kandoro alishuhudia jiwe hilo linalokadiriwa kuwa na uzito wa tani 2,000 likiimbiwa na kucheza, kitendo ambacho kilishangaza wengi waliofika kushuhudia maajabu hayo. Mmoja wa wana ukoo wa Rwakatimba wanaotunza mila na desturi ya jiwe hilo, mzee Magesa Makolokolo (90), mbali ya kueleza historia yake pia ndiye mwenye jukumu la kuimbia jiwe hilo licheze. Katika taarifa yake pia aliomba serikali imsaidie gharama za uendeshaji na kutunza mila hiyo, kwa kuwa kila mwaka linafanyiwa tambiko linaloghalimu sh 300,000 na wakati mwingine hushindwa kutimiza sharti hilo kwa kukosa fedha.
   
 2. fige

  fige JF-Expert Member

  #2
  Apr 11, 2011
  Joined: Jul 4, 2010
  Messages: 376
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Napendekeza jiwe liingizwe kwenye maajabu ya dunia
   
 3. Mtumishi Mkuu

  Mtumishi Mkuu JF-Expert Member

  #3
  Apr 11, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 260
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Hebu mdau ambae amelishuhudia atumwagie ushahidi hapa na sisi tuone na kuamini!
   
 4. Ibrahim K. Chiki

  Ibrahim K. Chiki Verified User

  #4
  Apr 11, 2011
  Joined: Apr 5, 2011
  Messages: 594
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Tanzania kwa uchawi tuu, hatujambo...duuu.
   
 5. L

  Leornado JF-Expert Member

  #5
  Apr 11, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,534
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Hili litakuwa ajabu kuu la dunia. RC asije akakurupuka kumbe ni mambo ya mazingaombwe.
  Bora akae :tape:.
   
 6. Avatar

  Avatar JF Gold Member

  #6
  Apr 11, 2011
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 676
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 35
  Mh!... Siamini!
   
 7. m

  mwabaluhi JF-Expert Member

  #7
  Apr 11, 2011
  Joined: Oct 16, 2010
  Messages: 561
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nishawahi kusikia habari za jiwe hili hapo kabla
   
 8. Mzee Wa Rubisi

  Mzee Wa Rubisi JF-Expert Member

  #8
  Apr 11, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,754
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145

  ingia kwenye blog ya gsengo utapata picha ya ziwe hilo
   
 9. Mzee Wa Rubisi

  Mzee Wa Rubisi JF-Expert Member

  #9
  Apr 11, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,754
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145

  watu wa ukelewe ni kitu cha kawaida
   
 10. Mzee Wa Rubisi

  Mzee Wa Rubisi JF-Expert Member

  #10
  Apr 11, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,754
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145

  mbona Jk alifika pale akawaambia wamekalia uchumi na hakuwasaidi
   
 11. kakuruvi

  kakuruvi JF-Expert Member

  #11
  Apr 11, 2011
  Joined: Sep 2, 2009
  Messages: 646
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Hilo Jiwe ndio hili kwa mujibu wa G.Sengo

  [​IMG]
   
 12. Mental Retard

  Mental Retard Member

  #12
  Apr 11, 2011
  Joined: Mar 9, 2008
  Messages: 33
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 15
   
 13. Gurta

  Gurta JF-Expert Member

  #13
  Apr 11, 2011
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 2,246
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
   
 14. b

  babayaro New Member

  #14
  Apr 11, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  TBC au strar tv kama sikoseai waliwahi kulionyesha kama miezi miwili iliyopita
   
 15. Shomari

  Shomari JF-Expert Member

  #15
  Apr 11, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,107
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  haya masuala ni ya Kisayansi na Kijiografia zaidi, sio kupiga mluzi, wabongo tunapenda sana njia za mkato. eti kupiga mluzi!!
   
 16. W

  We can JF-Expert Member

  #16
  Apr 11, 2011
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 681
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  I think there could be NO miracle here! The rock is experiencing unstable equilibrium in its state of rest. Its centre of gravity is mostlikely in such a way that it is not at the centre of the body. Remember your O-Level physics, you can have stable and unstable equilbrium...

  The rock is like pivoted somewhere due to erosion at its base. As this erosion continues for some years (say hundreds from now), the base can be flattened and it will, with time come to its rest (no more simple harmonic mitions).

  The question of siging for the rock is impractical. What i can guess is that before someone signs, a small force must be applied against the rock for its to start moving to and fro. When unstable (as stated above), a little energy is needed to make it start moving, even a 4 yr old boy / girl can make it move. So, i think before the person signs, he/she applies a little energy that may note be considered significant! It is...!

  If you want to prove what i am saying, live a litle more hundreds of years or a bit less....!
   
 17. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #17
  Apr 12, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,223
  Likes Received: 1,412
  Trophy Points: 280
  Tani 2,000?
   
 18. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #18
  Apr 12, 2011
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  ni jiwe la tambiko hilo. Haliwezi kuwa
   
 19. N

  NYAMLENGWA Member

  #19
  Apr 12, 2011
  Joined: Mar 8, 2011
  Messages: 41
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kwel mkuu hlo jiwe lipo na likiimbiwa linacheza na ni la zaman nashangaa habari ndio zinaenea
   
 20. Labata

  Labata Member

  #20
  Apr 12, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwenyewe nashangaa same thing, yani kuna matatizo muhimu katika hii nchi watu wanazungumzia babu,dada,bibi,kaka, sasa JIWE??!!!
  Are we serious eti jiwe
   
Loading...