#MakalaNo: 085
💡 (
"لا وتران في ليلة" )⁉️
🌑 HAKUNA WITRI MBILI KATIKA USIKU MMOJA.
📌 عن طلق بن علي قال: سمعت رسول الله ﷺ يقول : ( لا وتران في ليلة ).
📚
رواه الترمذي ٤٧٠ / وصححه الألباني في صحيح الجامع ٧٥٦٧
Kutoka kwa
Twaaliq bin Alliy Amesema nimemsikia Mtume ﷺ akisema: Hakuna witri mbili katika usiku mmoja.
"ما معنى حديث ( لا وتران في ليلة)"
Nini maana ya hakuna witri mbili katika usiku mmoja?
📌قال الشيخ محمد بن صالح العثيمين رحمه الله تعالى:
Amesema Sheikh Muhammad bin Uthaymiyn - Allah amrehemu:
معناه أنه لا يشرع للإنسان أن يوتر مرتين في الليلة الواحدة لأن الوتر إنما يقصد به ختم الصلاة بالوتر وإذا ختمت بوتر فلا وجه للإيتار مرة ثانية.
Maana yake ni kuwa si sheria kwa mtu kuswali witri mara mbili katika usiku mmoja kwa sababu witri hukusudiwa kuhitimisha swala kwa witri na itakapo hitimishwa kwa witri hakuna sura ya kuweza kuleta witri kwa mara ya pili.
📕
فتاوى نور على الدرب
📌 قال ابن حزم رحمه الله تعالى:
Amesema Ibn Hazm - Allah amrehemu:
الوتر آخر الليل أفضل؛ ومن أوتر أوله فحسن, والصلاة بعد الوتر جائزة, ولا يعيد وتراً آخر .
Witri mwisho wa usiku ni bora na mwenye kuileta mwanzoni ni vizuri na swala baada ya witri inafaa na harudii kuswali witri.
📚
المحلى ٩٢/٢/٩٣
📌وقال الشيخ ابن باز رحمه الله:
Na amesema Sheikh ibnu Baaz - Allah amrehemu;
من أوتر في أول الليل وتيسر له القيام في آخر الليل صلى ما تيسر شفعاً ركعتين ركعتين ولا يعيد الوتر بل يكفيه الوتر الأول لقوله صلى الله عليه وسلم: "لا وتران في ليلة".
Mwenye kuswali witri mwanzoni mwa usiku na akawepesika kusimama mwishoni mwa usiku huswali kitakachokuwa chepesi kwake rakaa mbili mbili na wala harudii witri bali itamtosha witri ya mwanzo kwa kauli yake Mtume ﷺ "hakuna witri mbili katika usiku mmoja."
📚
[مجموع فتاوۍابن باز رحمه الله 11/311)]
📝 Mfasiri: Ustadhi Abuu Mujtaba Ahmad Mwinyiwiwa - Allâh amuhifadhi.
🗓 Tarehe: 04-RAMADHANI-1445H
ALKHAMISI 14-MARCH-2024H
🇹🇿 Sehemu: Kibaha - Pwani - Tanzania.
⛔️ Huruhusiwi kubadili chochote katika makala hii, sambaza kama ulivyoipokea.
🌐 Ungana nasi katika Channel yetu ya WhatsApp kupitia kiunganishi hiki: Manhaj Online TV
____________________________
📂 NB: Usisahau kusubscribe channel yetu ya Youtube
@manhajonlinetv kisha bonyeza alama hii "🔔" ili uwe wa kwanza kupata video zetu.
》
Manhaj Online TV
•┈┈•◈◉✹❒
Sambaza ❒✹◉◈•┈┈•