Unawezaje kuprove kwamba walifanya kazi nzuri? Kama ni nzuri mbona wameachwa?

Estim wameprove beyond doubt kwamba wapo vizur hata kazi zinaonekana

Hivi nikikwambia kwamba unasumbuliwa na uislamu tu nitakuwa nakosea?
 
Expert wala sijui hoja yako hapa ni nini,hatuzungumzii wanufaika wa hizo huduma ni akina nani?

Hapa tunazungumzia kwanini waislamu nao wasipate hizo stahiki?
 
Expert wala sijui hoja yako hapa ni nini,hatuzungumzii wanufaika wa hizo huduma ni akina nani?

Hapa tunazungumzia kwanini waislamu nao wasipate hizo stahiki?

unarudi kule kule uliponiuliza kwa nini Christians hawafanyi biashara kama
waislamu, labda nikuulize waislamu walipewa chuo kikuu na B.Mkapa morogoro, wamekifanyia nini hicho chuo? waislamu wangapi wanapenda kwenda kusoma hapo?
 
unarudi kule kule uliponiuliza kwa nini Christians hawafanyi biashara kama
waislamu, labda nikuulize waislamu walipewa chuo kikuu na B.Mkapa morogoro, wamekifanyia nini hicho chuo? waislamu wangapi wanapenda kwenda kusoma hapo?
Naona unazalisha mambo mengine hapa,hiyo ishu ya Chuo imeingiaje expert wangu
 
Kwa zanzibar ni sehemu ambayo inajulikana waislamu wapo wengi,je kwa mazingira hayo ungetegemea nini?

Tuchukulie zanzibar ingekuwa labda ya wakristo walio wengi,je swala kama hilo lisingetokea?
 
Maswali: Qur-aan





Manufaa Gani Ya Ulevi Yaliyotajwa Katika Qur-aan Na Madhara Ya Kamari



Alhidaaya.com








SWALI:



Assalaamu alaikum warrahmatullahi wabarakatu, Katika suratul-bagarah ayah ya 219 inasema: Wanakuuliza juu ya ulevi na kamari. Sema: Katika hivyo zipo dhambi kubwa na manufaa kwa watu. Lakini dhambi zake ni kubwa zaidi kuliko manufaa yake. Swali langu ni hili: manufaa gani





JIBU:



AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho





Katika Aayah hii kuna msingi mkubwa wa kuharamishwa kwa vitu hapa duniani. Na hakika ni kuwa kujua kwetu hekima kuhalalishwa au kuharamishwa vitu si muhimu kwani tunajua kuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anahalalisha vizuri na kuharamisha vibaya. Vilivyo haramu vina madhara kwetu na halali ni maslahi kwetu. Ndipo Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Akatuambia:



الَّذِينَ يَتَّبِعُونَ الرَّسُولَ النَّبِيَّ الْأُمِّيَّ الَّذِي يَجِدُونَهُ مَكْتُوبًا عِندَهُمْ فِي التَّوْرَاةِ وَالْإِنجِيلِ يَأْمُرُهُم بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَاهُمْ عَنِ الْمُنكَرِ وَيُحِلُّ لَهُمُ الطَّيِّبَاتِ وَيُحَرِّمُ عَلَيْهِمُ الْخَبَائِثَ وَيَضَعُ عَنْهُمْ إِصْرَهُمْ وَالْأَغْلَالَ الَّتِي كَانَتْ عَلَيْهِمْ ۚ فَالَّذِينَ آمَنُوا بِهِ وَعَزَّرُوهُ وَنَصَرُوهُ وَاتَّبَعُوا النُّورَ الَّذِي أُنزِلَ مَعَهُ ۙ أُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ﴿١٥٧﴾

157. Wale wanomfuata Rasuli; Nabiy asiyejua kusoma wala kuandika ambaye wanamkuta ameandikwa kwao katika Tawraat na Injiyl, anawaamrisha mema na anawakataza munkari, na anawahalalishia vizuri na anawaharamishia maovu, na anawaondoshea mizigo yao (shariy’ah ngumu) na minyororo (vikwazo, taklifu) ilokuwa juu yao. Basi wale waliomwamini na wakamtukuza, na wakamnusuru na wakafuata nuru (Qur-aan) ambayo imeteremshwa pamoja naye; hao ndio wenye kufaulu. [Al-A’raa: 157]





Ama manufaa madogo ya kamari na vileo ni hapa hapa duniani. Manufaa ya kamari ni:



Kupata fedha kwa njia nyepesi na kuzitumia kwa mahitaji yake ya kibinafsi na familia.




Ama manufaa ya vileo (pombe) ni kama yafuatayo:



Kudhaniwa na wanywaji kuwa inatoa dhiki na fikira kwa muda
Kutumika kuhifadhia baadhi ya vyakula.
Kusafisha sehemu za jeraha na kuua viini.
Kuondosha kinyesi.
Kudhaniwa na wanywaji kuwa inasisimua.
Kutumika katika mafuta aina ya virashio na manukato.




Hata hivyo, manufaa haya yanazidiwa na madhara yake mengi yaliyo dhahiri na yanayoathiri Dini, jamii na akili. Tunataja machache hapa:



Madhara ya kamari ni kama:



Kupoteza pesa kwa kushiriki kwenye mchezo huo ambao mara nyingi mtu hushindwa na huliwa pesa zake.
Kuingia kwenye uraibu wake na kujikuta kila wakati unapotezea muda huko na kushughulishwa nayo na kuacha ya muhimu ya ‘Ibaadah na familia.
Kufilisika.


Ama madhara ya pombe ni kama yafuatayo:



Kuacha nguzo za fardhi kama Swalaah, Swawm n.k.
Kukosa hayaa, heshima, ustaarabu, na kufanya matendo ya kipuuzi mara nyingi.
Kutoa maneno maovu, matusi.
Kugombana na watu.
Kutoa harufu mbaya mdomoni.
Kuharibu ndoa kwa kukosa kutimiza haki za mke na watoto.
Madhara kadhaa ya kuathiri afya ya mtu.




Na Allaah Anajua zaidi
 
Maswali: Qur-aan


Mazungumzo Ya Nabii Musa Na Al-Khidhwr Katika Suwrah Al-Kahf



Alhidaaya.com





SWALI:



Mimi Ningependa Kuuliza Suala Moja Tu. Katika Suwrah al-Kahf Kuna Masuala Ambayo Nabiy Muwsaa Alikuwa Anauliza Na Akipewa Majibu Na Yule Aliyefatana Nae. Tafadhali Naomba Ufafanuzi Wa Masuala Aliyokuwa Akiulizwa. Na Aliyemuuliza Ni Nani Yule?


Wabillahi Taufik.




JIBU:



AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho



Hakika masuala hayo yanapatikana katika Suwrah Al-Kahf (18) ambayo Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ametutaka tuwe tunaisoma kila Ijumaa ili tuepukane na fitina za Dajjaal. Masuala ambayo Nabiy Muwsaa (‘Alayhis-salaam) aliyomuuliza Khidhwr ni kama yafuatayo: Kwa nini akalitoboa jahazi, kumuua kijana asiye na hatia na kuusimamisha ukuta. Majibu ya masuala haya matatu yalikuwa:



أَمَّا السَّفِينَةُ فَكَانَتْ لِمَسَاكِينَ يَعْمَلُونَ فِي الْبَحْرِ فَأَرَدتُّ أَنْ أَعِيبَهَا وَكَانَ وَرَاءَهُم مَّلِكٌ يَأْخُذُ كُلَّ سَفِينَةٍ غَصْبًا ﴿٧٩﴾وَأَمَّا الْغُلَامُ فَكَانَ أَبَوَاهُ مُؤْمِنَيْنِ فَخَشِينَا أَن يُرْهِقَهُمَا طُغْيَانًا وَكُفْرًا ﴿٨٠﴾فَأَرَدْنَا أَن يُبْدِلَهُمَا رَبُّهُمَا خَيْرًا مِّنْهُ زَكَاةً وَأَقْرَبَ رُحْمًا ﴿٨١﴾وَأَمَّا الْجِدَارُ فَكَانَ لِغُلَامَيْنِ يَتِيمَيْنِ فِي الْمَدِينَةِ وَكَانَ تَحْتَهُ كَنزٌ لَّهُمَا وَكَانَ أَبُوهُمَا صَالِحًا فَأَرَادَ رَبُّكَ أَن يَبْلُغَا أَشُدَّهُمَا وَيَسْتَخْرِجَا كَنزَهُمَا رَحْمَةً مِّن رَّبِّكَ ۚ وَمَا فَعَلْتُهُ عَنْ أَمْرِي ۚ ذَٰلِكَ تَأْوِيلُ مَا لَمْ تَسْطِع عَّلَيْهِ صَبْرًا ﴿٨٢﴾

Ama jahazi, ilikuwa ya masikini wanaofanya kazi baharini. Basi nikataka kuitia dosari kwani mbele yao alikuweko mfalme anayechukua kila jahazi kwa kupora. Na ama ghulamu, walikuwa wazazi wake wawili Waumini. Basi Tukakhofu asiwatie mashakani kwa upindukaji mipaka ya kuasi na kufuru. Tukakusudia Rabb wao Awabadilishie aliye bora zaidi kuliko yeye aliyetakasika na aliyekuwa karibu zaidi kihuruma. Na ama ukuta, ulikuwa ni wa ghulamu wawili mayatima katika mji ule, na kulikuweko chini yake hazina yao, na baba yao alikuwa mwema. Basi Rabb wako Alitaka wafikie umri wa kupevuka na watoe hazina yao; ni rahmah kutoka kwa Rabb wako. Na sikufanya hayo kwa amri yangu. Hiyo ni tafsiri ya hakika ya yale ambayo hukuweza kuyavutia subira. [Al-Kahf: 79 – 82]



Aliyekuwa akimuuliza Nabii Muwsaa (‘Alayhis-salaam) ambaye ni Khidhwr wanazuoni wametofautiana kuhusu yeye alikuwa nani. Wengine wamesema kuwa alikuwa ni mja mwema kwa kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta‘aalaa):

عَبْدًا مِّنْ عِبَادِنَا آتَيْنَاهُ رَحْمَةً مِّنْ عِندِنَ

Mja miongoni mwa waja Wetu (Khidhr), Tuliyempa rahmah kutoka Kwetu,.. [Al-Kahf: 65]



Na wengine wakasema kuwa alikuwa Nabii kwa kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta‘ala):



..وَمَا فَعَلْتُهُ عَنْ أَمْرِي ۚ ذَٰلِكَ تَأْوِيلُ مَا لَمْ تَسْطِع عَّلَيْهِ صَبْرًا ﴿٨٢﴾

Na sikufanya hayo kwa amri yangu. Hiyo ni tafsiri ya hakika ya yale ambayo hukuweza kuyavutia subira. [Al-Kahf: 82]





Na Allaah Anajua zaidi
 
Maswali: Qur-aan



Mlio Wa Simu Wa Qur-aan Akisikia Asiye Muislamu Inafaa?



www.alhidaaya.com





SWALI:



Asalam Alaykum:



Swali langu ni kwamba, Kuna milio ya simu unapompigia mtu unaisikia wakati unamsubiri apokee (caller tune). Je kama Mkisto anakupigia na inakua anaisikia je ni sawa au? Nahitaji ufafanuzi wenu.





JIBU:



AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.





Hakika ni kuwa Muislamu hafai kuweka mlio wa simu kuwa wa Aayah au Suwrah ya Qur-aan kwani Qur-aan haikuteremshwa kwa lengo hilo. Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema:



شَهْرُ رَمَضَانَ الَّذِي أُنزِلَ فِيهِ الْقُرْآنُ هُدًى لِّلنَّاسِ وَبَيِّنَاتٍ مِّنَ الْهُدَىٰ وَالْفُرْقَانِ ۚ

Mwezi wa Ramadhwaan ambao imeteremshwa humo Qur-aan ili iwe mwongozo kwa watu na hoja bayana za mwongozo na pambanuo (la haki na batili). [Al-Baqarah: 185]





Na kisha Qur-aan haifai kusomwa katika sehemu fulani mojawapo ikiwa ni chooni. Mfano umeingia chooni na ikaanza kulia itabidi uizime lakini hasara tayari itakuwa imepatikana. Pia ikianza kulia nawe uishike, hata kabla ya kumalizika Aayah itakuwa ni utovu wa adabu.



Bonyeza kiungo kifautacho upate jibu lenye maelezo zaidi:



Kuweka Milio Ya Miziki Kwenye Simu Za Mkononi Au Qur-aan Inayosomwa Au Adhaana



Ama sauti ya Qur-aan kusikika na asiye Muislamu haina tatizo kabisa. Ikiwa asiye Muislamu anataka kujua kuhusu Uislamu licha ya kusikiliza hata kuisoma kwa kupatiwa tafsiri kwa lugha anayoielewa ndio bora na lengo.



Kwa hiyo, jambo hilo halina tatizo katika shari’ah.



Na Allaah Anajua zaidi
 
Nabiy Nuwh (alayhis-salaam) Na Kubashiriwa Ajenge Safina



Alhidaaya.com





SWALI:

Nahitaji kujua kuhusu Nabiy Nuwhu. (Radhwiyah Allaahu 'anhum).Hasa kuhusu kubashiriwa atengeneze safina.



Wabillah taufiq.





JIBU:



AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho



Shukrani zetu za dhati kwa ndugu yetu aliyeulizwa swali hili kuhusu Nabiy aliyekuwa Uwlul-‘Azmi (wenye azima kubwa). Manabii hawa wakiwemo Nuwh, Ibraahiym, Muwsaa, ‘Iysa na Muhammad (‘Alayhimu-salaam) walipata mitihani mikubwa nao wakasubiri subra za kipekee.

Kawaida sifa uliyotaja kwa Nabiy Nuwh kwa kusema, Radhwiya Allaahu 'anhu ni kwamba sifa hiyo inatumika kwa Swahaba. Na 'anhum' ni wingi wa 'anhu' lakini unampomzungumzia Nabii mmoja basi unasema 'Alayhis-salaam', na wengi utasema 'Alayhim-Salaam'.



Swali linaonekana halikumalizika na huenda muulizaji alifanya haraka kulituma. ‘Alaa kulli haal tutajaribu kuelezea kulingana na ufahamu wetu wa swali hilo. NabiyNuwh (‘Alayhis-salaam) alitumwa na Allaah kwa watu wake, naye akawaelezea wazi kabisa kuwa yeye ni muonyaji anayewabainishia kila kitu. Jambo la kwanza alilowalingania ni wamuabudu Allaah Mmoja tu kwani wao hawana Rabb Mlezi mwengine. Na lau hawatafanya hivyo basi watakuwa ni wenye kupata adhabu kali sana.



Lakini kama kawaida wale makafiri wakubwa walikuwa ni wenye kumkejeli kwa kumwambia yeye ni mtu tu wa kawaida. Kwa hiyo, wakawa ni wenye kumkanusha na hasa kuwa wafuasi wa Nabiy (‘Alayhis-salaam) walikuwa ni wanyonge katika jamii hiyo. Aliwalingania kwa miaka 950 mpaka tufani ikawa ni yenye kuwafikia wakiwa katika hali hiyo ya dhulma na ukafiri. Nabiy Nuwh (‘Alayhis-salaam) hakutaka chochote kutoka kwao ila wamuamini Allaah lakini walikataa katakata. Walipochoshwa na Nabii Nuwh (‘Alayhis-salaam) walimwambia: "Umejadiliana nasi na umezidisha majadiliano yako nasi, basi tuletee unayotuahidi (adhabu); ukiwa miongoni mwa wanaosema kweli. Yeye aliwajibu kuwa Allaah Akitaka hilo ni jepesi kwake wala nyinyi hamtaweza kuzuilia hilo wala kumshinda.

Nabiy Nuwh (‘Alayhis-salaam) hakuchoka bali alizidi kutia juhudi kwa kuwalingania usiku na mchana, kwa siri, kwa kelele na dhahiri lakini walizidi kumkimbia na kuziba masikio yao ili wasimsikie kabisa.



Katika hali hiyo aliamriwa kuunda jahazi naye atakuwa ni mwenye kulindwa na wala asizungumze nao tena. Wakubwa wa kikafiri kila walipokuwa wakipita wakimcheka kwani waliona ajabu huyu Nabiy ataiendesha jahazi yake sehemu gani kwa kuwa nchi yao ilikuwa ni bara isiyokuwa na ziwa, mto wala bahari. Wakati Allaah Aliyetukuka Alipotaka kuleta adhabu Yake ardhi ilianza kufoka maji. Hapo aliamriwa apakie humo (katika jahazi) jozi moja ya kila mnyama (dume na jike), na watu wa nyumbani kwake ila wale watakaopitiwa na hukumu Yetu na walioamini. Walioamini pamoja naye walikuwa wachache sana.



Baada ya hapo waliamriwa wapande katika jahazi hilo kwa jina la Allaah. Mbingu ziliteremsha maji na pia mengine yalitoka chini ya ardhi na jahazi ikawa inakwenda kwenye mawimbi kama majabali. Wakati huo Nabiy Nuwh (‘Alayhis-salaam) alimwona mwanawe aliyekuwa akighariki, naye akamwambia aingie katika hiyo jahazi lakini mtoto akawa ni mwenye kukataa huku anasema atapanda juu ya mlima, lakini akawa ni mwenye kughariki na hiyo ndiyo iliyokuwa hatima yake kwa kukanusha pamoja na wale wote waliokufuru



Baada ya muda ardhi iliamriwa kumeza maji yote na mbingu nazo zikaamriwa zizuie kuteremsha mvua. Jahazi yenyewe ilisimama kwenye Mlima Judi ambako baada ya muda waliweza kutoka katika jahazi na kuanza maisha yao tena. Kulingana na baadhi ya tafsiri mlima huo upo kaskazini mwa Mosul au kaskazini mashariki mwa Jazirah ibn ‘Umar katika nchi (eneo) ya Kurdistan.



Mazingatio kwetu ni mengi lakini yaliyo muhimu ni:



Allaah Aliyetukuka ni Muweza wa kufanya jambo lolote.
Hatima ya makafiri mbali na nguvu zao, ni mbaya, hapa duniani na kesho Aakhirah.
Ujamaa na watu wema hautakufalia kitu ikiwa wewe mwenyewe hutakuwa mwema.
Waumini wasiwe wasivunjike moyo na kujiona kuwa wao ni wanyonge.


Kwa ziada tunaweza kutazama Suwrah zifuatazo:

Huwd: 25-48

Al-A'raaf: 59 -64

Al-Muuminuun: 23 - 30

Ash-Shu'araa: 105 – 122

Nuwh: 71





Na Allaah Anajua zaidi
 
Nani Aliyepanga Suwrah, Aayah Na Nani Aliyetoa Majina ya Suwrah?



Alhidaaya.com





SWALI:



Swali La Kwanza:



Asslaam aleykum,

Ni nani aliezipanga suwrah za Qur-an katika mpango tunaouona sasa. Ni kwa nini na kuna hikma gani. Ikiwa Suwrah Al-Baqarah imeteremshwa Madina kwa nini iwe ya pili katika msahafu na isiwe ya 86, kwani za mwanzo zilianza kuteremshwa Makkah?



Swali La Pili:

Shekh, naomba tafadhali maelezo nani aliyetoa majina ya sura za qurani? Vipi zimepangwa aya ikiwa Qurani imeteremshwa kidogo kidogo kuanzia iqra hadi aya za mwisho kabla kufa Nabiy maana naona imeanza Alhamdu na kumalizikia Qul-audhu.





JIBU:



AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho



Ni jambo linaloeleweka kuwa hakuna jambo lolote la Uislamu isipokuwa lina hekima kubwa ni sawa tunazijua hizo hekima au la.



Mpangilio wa Qur-aan na majina yake yamepangwa na Yeye Mwenyewe Allaah Mwenye hekima na busara kubwa. Tufahamu kuwa Qur-aan yote ilikuwa imehifadhiwa na Allaah Aliyetukuka katika sehemu inayoitwa Lawhul Mahfuudh na kisha kuteremshwa yote usiku wa al-Qadr katika mwezi wa Ramadhwaan hadi wingu wa duniani. Kutoka hapo Jibriyl ('Alayhis Salaam) akawa ni mwenye kupatiwa amri na Aliyetukuka kumteremshia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'Alayhi wa aalihi wa sallam) kidogo kidogo kwa miaka 23 kulingana na mahitajio.



Kila ilipokuwa inateremshwa Surah au baadhi ya Aayah Jibriyl ('Alayhis Salaam) kwa maagizo kutoka kwa Allaah Aliyetukuka alikuwa akimuamuru Nabiy (Swalla Allaahu 'Alayhi wa aalihi wa sallam) aiweke mahali kadhaa na jina la Suwrah liwe kadhaa. Baada ya kuhama Madiynah, Jibriyl alikuwa akija kila Ramadhwaan kumsikiliza Nabiy (Swalla Allaahu 'Alayhi wa aalihi wa sallam) kisomo cha Qur-aan. Na ule mwaka aliokufa, Jibriyl alikuja mara mbili na mara ya mwisho Zayd bin Thaabit (Radhwiya Allaahu 'anhu) alikuwepo.



Hivyo, alivyoaga dunia (Swalla Allaahu 'Alayhi wa aalihi wa sallam), Swahaba (Radhwiya Allaahu 'anhum) waliandika Qur-aan kama walivyofundishwa na kuagiziwa na Nabiy (Swalla Allaahu 'Alayhi wa aalihi wa sallam). Hata wale waandishi wa Nabiy (Swalla Allaahu 'Alayhi wa aalihi wa sallam) walikuwa wakipatiwa maagizo hayo.



Ama kuhusu Suwrah Al-Baqarah kuwa ni ya 86 si kweli na huenda kuwa ndugu yetu akawa amekosea katika ubinaadamu wake. Na hilo si la ajabu. Hakika ni kuwa Suwrah Al-Baqarah ni Suwrah ya 87 kuteremshwa na ya kwanza kuteremka Madiynah. Surwah ya mwisho kuteremshwa Makkah ilikuwa ni ya 86 nayo ni Suratul Mutwaffifiyn (83).





Na Allaah Anajua zaidi
 
Nataka Kujua Matumizi Na Fadhila Za Suwrah Yaasiyn na Ayatul-Kursiy



Alhidaaya.com





SWALI:



Nataka kujua matumizi na fadhila za Suwrah Yaasiyn na Ayatul Kursiy



Nina matumaini nitaafahamishwa vizuri nawatakia kila la kheri waislam wenzangu




JIBU:



AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.





Watu wanaifanyia vishindo Suwrah Yaasiyn na wakabuni na kutumia Hadiyth dhaifu na ndipo limewafanya Waislamu kuipa nyongo Qur-aan nzima na wakawa wanaisoma Suwrah hii peke yake na nyingine chache. Hii ni kinyume na agizo la kuisoma Qur-aan pole pole na kidogo kidogo kuanzia Suwratul-Faatihah hadi An-Naas. Hadyith nyingi kuhusu fadhila za Suwrah hii ni dhaifu na za kuzushwa.





Miongoni mwa Hadiyth hizo kuhusu fadhila ya Suwrah hiyo ya Yaasiyn ni ile ya at-Tirmidhiy inayosema: “Kila kitu kina moyo wake, na moyo wa Qur-aan ni Yaasiyn. Atakayeisoma mara moja, Allaah Atamuandikia thawabu za kwamba ameisoma Qur-aan yote mara kumi.” Mwenyewe At-Tirmidhiy papo hapo alipoitaja alisema kuwa hii ni Hadiyth ngeni, yaani aina ya Hadiyth dhaifu.



Nyingine ni ile inayosema: “Kuisoma Yaasiyn kunampa msomaji alilolikusudia”. Hii ndiyo kabisa haina nguvu hata chembe wala tamko hili si la Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).



Ama Aayatul-Kursiy (2: 255) ni Aayah Tukufu kabisa kutokana na dalili.



Kutoka kwa ‘Abdullaahi bin Rabaah Al-Answaariy kutoka kwa ‘Ubayy bin Ka’ab ambaye amehadithia: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Yaa Abal-Mundhir! Hivi unajua ni Aayah gani ndani ya Kitabu cha Allaah kuwa ni adhimu kabisa?” Akasema: Nikasema: Allaah na Rasuli Wake ni wajuzi zaidi. “Yaa Abal-Mundhir! Hivi unajua ni Aayah gani ndani ya Kitabu cha Allaah kuwa ni adhimu kabisa?” Akasema: Nikasema: "Allaah, hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye, Aliyehai daima, Msimamia kila kitu". (mpaka mwisho wa Aayah). Akasema Ubayy: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akanipiga kifuani kisha akasema: “Wa-Allaahi upongezwe kwa ‘ilmu yako yaa Abal-Mundhir.” [Muslim] na katika mapokezi ya Ahmad imeendelea: “Naapa kwa Ambaye nafsi yangu imo Mikononi Mwake, Aayah hii ina ulimi na midomo miwili ambao inamtukuza Mfalme (Allaah) katika mguu wa Arsh.” [Muslim (810), Swahiyh At-Targhiyb (1471)]



Anahimizwa kila Muislamu kuihifadhi na kuisoma nyakati nyingi kwani zimekuja Hadiyth nyingi juu ya fadhila zake. Miongoni mwa Hadiyth ni:



1-Kabla ya Kulala Kupata Hifadhi ya Shaytwaan:



Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Mwenye kuisoma anapokuwa kitandani (kwa ajili ya kulala) hakika atakuwa katika hifadhi ya Allaah wala hatakaribiwa na shaytwaan mpaka kupambazuke” [al-Bukhaariy].



2-Kuisoma Asubuhi Na Jioni Kwa Ajili Ya Kinga;



“Atakayeisoma anapoamka asubuhi itamkinga na majini mpaka itakapofika jioni. Na atakayeisoma jioni atakingwa nao mpaka asubuhi.” [Al-Haakim (1/562) Taz. Swahiyh At-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/273)]



Pia,



”Atakayezisoma mara tatu asubuhi na jioni zitamtosheleza kwa kila kitu.” [Abuu Daawuwd (4/322) [5082], At-Tirmidhiy (5/567) [3575], Taz. Swahiyh At-Tirmidhiy (3/182)]



3-Kuisoma Kila Baada Ya Swalaah Kupata Kuingizwa Jannah:



Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Mwenye kuisoma baada ya kila Swalah hakitomzuia kuingia Jannah isipokuwa kifo”. [Swahiyh Al-Jaami’ (5/339) [6464], na Silsilat Al-Ahaadiyth As-Swahiyhah (2/697) [972].



4-Ina Jina Tukufu Kabisa Ndani Yake Ambalo Unapoomba Hutakaqabaliwa:



Abuu Umaamah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amehadithia kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ”Jina Tukufu kabisa la Allaah Ambalo likiombewa kwalo Anaitikia limo katika Suwrah tatu; Al-Baqarah, Aal-‘Imraan, na Twaahaa’. [At-Tirmdhiy, Silsilah Asw-Swahiyhah (746)] Na mapokezi mengineyo yaliyothibitisha kuhusu Ismul-A’dhwam (Jina tukufu kabisa).





Na Hadiyth nyingine ni kule kufundishwa Abuu Hurayrah (Radhwiya-Allaahu ‘anhu) na shaytwaan kisha Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: “Amesema kweli japokuwa yeye ni muongo.” [Al-Bukhaariy na Muslim]



Kwa hivyo hizi ni baadhi ya Hadiyth zinazoonyesha fadhila za Ayatul-Kursiy. Hakika itakuwa ni muhimu kwetu kuweza kuihifadhi na kuisoma kila wakati ambao umesuniwa kufanya hivyo ili tupate ulinzi na faida zake kutoka kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)





Na Allaah Anajua zaidi
 
Ni Kweli Mwenye Kuhifadhi Qur-aan Haozi Kaburini?



Alhidaaya.com





SWALI:

Shukran Allaah Awajazi Kila La Kheri Kwa Kazi Yenu. Mtu Akiwa Hafidhul Qur-aan Akifa Huwa Haozi Nauliza Ni Quran Yote Ama Kuhifadhi Baadhi Ya Suwrah Ama Juzu Fulani Anaingia Mtu Katika Fadhla Hii.

Fi Amanillah

Sister In Islam.




JIBU:


AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho



Mwanzo tufahamu fadhila za Qur-aan ni muhimu, kubwa na nyingi, lakini ifahamike kuwa fadhila hizi zinatokana na maelezo tuyopewa na Allaah (Subhaanahu wa Ta‘aalaa) na Nabiy Wake, Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anatuelezea yafuatayo katika ubora wa Qur-aan:



1. Amesema Abu Umaamah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba amemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: “Isomeni Qur-aan kwani hakika itakuja Siku ya Qiyaama kumuombea Swahibu yake (aliyeisoma)” (Muslim).



2. Na amesema an-Nawwaas bin Sam‘aan (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: “Siku ya Qiyaama italetwa Qur-aan pamoja na wale waliokuwa wakifuata maagizo yake duniani. Itamtangulia Suwrah Al-Baqarah na Aal ‘Imraan zikimtetea Swahibu yake (wale waliokuwa wakizisoma katika maisha yao)” (Muslim na at-Tirmidhiy).



3. Na imepokewa kwa ‘Uthmaan bin ‘Affaan (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Mbora wenu ni yule aliyejifunza Qur-aan na akaifundisha” (al-Bukhaariy, Abu Daawuud na at-Tirmidhiy).



4. Na imepokewa kutoka kwa mama wa waumini ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Yule ambaye anasoma Qur-aan naye ni mahiri katika hilo, atakuwa pamoja na Malaika na Rusuli watukufu wenye kutii na yule ambaye anasoma Qur-aan na huku anaona ugumu na anapata shida, atapata malipo mawili” [Al-Bukhaariy, Muslim, at-Tirmidhiy na Ibn Maajah].



5. Na imepokewa kwa Abu Musa al-Ash‘ariy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Mfano wa Muumini ambaye anasoma Qur-aan ni kama mfano wa mbalungi, harufu yake ni nzuri na ladha yake ni nzuri, na mfano wa Muumini ambaye hasomi Qur-aan mfano wake ni kama tende, haina harufu na ladha yake ni tamu. Na mfano wa mnafiki ambaye anasoma Qur-aan ni kama mfano wa mrehani, harufu yake ni nzuri na ladha yake ni chungu; na mfano wa mnafiki ambaye hasomi Qur-aan ni kama mfano wa handhala, hauna harufu na ladha yake ni chungu” [Al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuud, at-Tirmidhiy na an-Nasaa’iy].



6. Na imepokewa kwa ‘Umar bin al-Khatwaab (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Hakika Allaah Atawanyanyua watu kwa Kitabu hichi na kuwatweza kwayo wengine” (Muslim).



7. Na imepokewa kwa Ibn ‘Umar (Radhwiya Allaahu ‘anhuma) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Hakuna husuda isipokuwa katika mambo mawili: Mtu aliyepewa na Allaah Qur-aan, akawa anaisoma nyakati za usiku na nyakati za mchana; na mtu aliyepewa na Allaah , naye akaitoa hiyo nyakati za usiku na nyakati za mchana” (al-Bukhaariy na Muslim). malimali



8. Na amesema al-Baraa’ bin ‘Aazib (Radhwiya Allaahu ‘anhu): Mtu mmoja alikuwa anasoma Suwrah Kahf na kulikuwa na farasi aliyekuwa amefungwa karibu yake kwa kamba mbili, ukamfunika yeye ukungu (wingu) na farasi wake akawa anaogopa huku anaruka ruka na kumkimbia. Kulipopambazuka alikwenda kwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na kumweleza kisa hicho. Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimwambia: “Hiyo ni as-Sakiynah (utulivu) unaoteremka kwa ajili ya Qur-aan” [al-Bukhaariy, Muslim na at-Tirmidhiy]

.

9. Na imepokewa kwa Ibn Mas‘uud (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Mwenye kusoma herufi kutoka kwa Kitabu cha Allaah atapata ujira mmoja, na ujira huu ni sawa na kumi mfano wake. Wala sisemi kuwa Alif Laam Miym ni herufi moja lakini Alif ni herufi na Laam ni herufi na Miym ni herufi” (At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh na ameipokea ad-Daarimiy nayo ni Sahihi).



10. Na imepokewa kwa Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu ‘anhuma) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Hakika yule ambaye kwamba hana moyoni mwake (yaani hakuhifadhi) chochote katika Qur-aan ni kama nyumba iliyohamwa” (At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh na ameipokea Ahmad, al-Haakim na ad-Daarimiy).



11. Na imepokewa kwa ‘Abdullaah bin ‘Amru bin al-‘Aasw (Radhwiya Allaahu ‘anhuma) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Ataitwa Swahibu (msomi) wa Qur-aan Siku ya Qiyaama na ataambiwa: ‘Soma Qur-aan na upande kuelekea (mbingu za juu) na usome kama ulivyokuwa ukisoma duniani kwani daraja yako itakuwa ni kwa ile Aayah ya mwisho utakayosoma’ [Abu Daawuud na At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadityh Hasan Swahiyh na imepokewa na Ahmad na Isnadi yake ni Hasan]”.



Hizi ni baadhi ya fadhila kutoka katika Sunnah zilizo sahihi. Bila shaka zipo fadhila za kusoma Aayah na surah Fulani zilizomo katika Qur-aan. Hata hivyo, wapo watu ambao wamebuni Hadiyth ili kuonyesha utukufu ambao haumo kabisa katika Qur-aan. Mfano ni ile inayosemekana ni Hadiyth lakini ni ya kubuni: “Msomaji wa Qur-aan hawi mzulufu”.



Ama fadhila hii kwa mwenye kuhifadhi Qur-aan kuwa hataoza haijapatikana katika Hadiyth zilizo sahihi. Hakika wale ambao miili yao haitaoza kwa Hadiyth sahihi ni Rusuli. Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:



"Allaah Aliyetukuka, Ameiharamisha ardhi kula miili ya Manabii" [Muslim, Abu Daawuud, an-Nasaaiy na Ibn Maajah kutoka kwa Aws bin Aws (Radhwiya Allaahu ‘anhu)].



Na katika Hadiyth nyingine Abu Dardaa’ (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Niswalieni Ijumaa kwani kufanya hivyo kunashuhudiwa. Malaika wapo kwayo, na hakuna atakayeniswalia bila Swaalah yake hiyo kuletwa kwangu mpaka anakaposimama. Nikamuuliza: ‘Je, hayo pia yatakuwa baada ya kuaga dunia kwako?’ Akasema: ‘Allaah Ameiharamisha ardhi kuila miili ya Manabii’. Hivyo, Rasuli wa Allaah yu hai (uhai wa maisha ya Barzakh) na anaruzukiwa sana” [at-Tirmidhiy na Ibn Maajah].



Kuhifadhi Qur-aan kuna fadhila zake lakini pamoja na kufuata maagizo yaliyomo ndani yake na kukatazika na maharamisho. Kuhifadhi bila kufuata inakuwa haina fadhila kwani Qur-aan yenyewe itakuwa inakulaani nawe huna hata habari kwa yale matendo unayoyafanya.





Na Allaah Anajua zaidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…