Kutoa Mimba - Hukmu Na Kafara Yake
Maswali: Zinaa-Liwati


SWALI:

Asalama aleykum, kwaunza tu napenda unipatie jawabu
la suwala langu inshaalla kama utakavoweza suala nini hukumu ya mwanamke ambae katowa mimba kabla mimba hiyo haijapulizwa roho? na nini kafara yake?




JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho


Kutoa mimba ikiwa ni kabla ya kupuliziwa roho au baada ya kupuliziwa roho kisheria ni haraam. Wakati unaokubalika kutoa mimba ni pale tu itakapokuwa kuna dharura za kisheria ndipo panaweza kukubalika tena kwa masharti yake.


Dharura hizo, ni kama kumehakikishika kuwa kuna uwezekana wa mama kufariki kwa kuwa na kiumbe hicho, au kuendelea kwake kuwa na mimba hiyo kutamletea mauti. Na isitoshe kukubalika huko, bali kumetakiwa uthibitisho huo utolewe na daktari mwenye kuaminika kabisa. Na muhimu kwanza atafutwe daktari Muislamu mwenye kuaminika, ikishindikana, basi daktari yeyote ambaye ni muaminifu sana.


Ama kuitoa mimba tu kwa sababu ya kutotaka mtoto, au kukhofia riziki yake, au malezi yake, au kuchelea gharama za maisha kama kumsomesha, kumvisha, au kumlisha n.k. hayo yote hayaruhusiwi kisheria kwani Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anasema:

“Wala msiwaue wana wenu kwa kuogopa umasikini. Sisi Tunawaruzuku wao na nyinyi. Hakika kuwaua hao ni khatia kubwa” [Al-Israa: 31]

“Wala msiwaue watoto wenu kwa sababu ya umasikini. Sisi Tunakuruzukuni nyinyi na wao” [Al-An'aam: 151]



Ingawa kuna baadhi ya Maulamaa wanaonelea kuwa inafaa kutoa mimba katika siku za arobaini za mwanzo, lakini iliyo sahihi zaidi ni kutokufaa kutoa katika hali zote ila kwa dharura kubwa kabisa inayokubalika katika sheria.

Ama katika hatua ya pili ya siku arobaini nyingine ambayo ni 'alaqah (kipande cha damu), au hatua ya tatu ya siku arobaini nyingine ambayo inajulikana kama ni 'mudhwgah' (kipande cha nyama), haitoruhusiwa kutolewa hiyo mimba hadi jopo la madaktari wenye kuaminika wathibitishe kuwa kweli kuendelea kuwepo mimba hiyo kutasababisha mama kufariki au ikiwa kumeonekana na kujulikana kuwa kiumbe (kijusi) hicho kimeshakufa tumboni ndipo katika hali hiyo kutaruhusika kutolewa baada ya kila njia kutumika kuondosha hatari hiyo kufeli.

Baada ya hatua hiyo ya tatu, na kufika miezi minne (siku mia na ishirini, yaani arobaini tatu) ambapo ndio roho itakuwa ishapuliziwa hicho kiumbe, hapo patakuwa haparuhusiki kabisa na ni madhambi makubwa kabisa ila kwa dharura kuu kabisa kama ilivyotajwa hapo nyuma, na tena kuwe kumefanyika juhudi kubwa za kuokoa hali sababishi (chenye kusababisha) na kwa hali hiyo kutakuwa kumetumika maslahi ya 'unafuu kati ya madhara mawili'. Na unafuu hapo ni uhai wa mama ambao ndio bora zaidi na wa msingi zaidi kuliko wa huyo kiumbe. Kwa sababu mama tayari kamili na anaishi na kuwepo kwake bado kuna matumaini ya kupatikana vizazi vingine, pia ni mwenye majukumu na wajibu katika maisha, na msimamizi wa nyumba, mlezi, n.k., hali hicho kiumbe kilichopo tumboni, hakina uhakika wa kuishi hadi kitakapozaliwa na haijulikani kama kitakapozaliwa kitakuwa hai au la, na pia kisicho na majukumu yoyote kwa wakati huo. Kwa hali hiyo, kati ya kulinda na kuokoa hali moja kati ya mbili, basi kumuokoa na kumlinda mama ni bora zaidi kuliko kile kilichoko tumboni.

Hali hiyo uliyoieleza, inaonyesha hakukuwa na dharura hiyo, na hivyo huyo mwanamke katenda kitendo kiovu ambacho sheria haikikubali kabisa. Tendo hilo la dhambi, linahitaji toba kwa mtendaji; toba ya dhati kabisa.

Ama kafara ya kitendo hicho, wametofautiana Maulamaa wakati wake na hata aina ya kafara yenyewe. Baada ya kutazama pande zote, lililo lenye nguvu ni kuwa, kabla ya kupuliziwa roho kiumbe (kijusi), hakulazimiki kutoa kafara (fidia), pamoja na kuwa kuna wanaoona kuwa inapaswa kutolewa. Lakini aliyefanya kitendo hicho anatakiwa atubu toba ya kweli na azidishe kufanya 'amali nyingi za kheri na kutoa sadaka sana kulipa maovu yake, kwani mema hufuta maovu.


Ama baada ya kupuliziwa roho, hakuna tofauti kukubaliwa kwake kuwepo na kafara au kutolewa fidia 'Diyah' (blood money). Baadhi ya Maulamaa wamesema kuwa kunatolewa fidia ya pesa kwa wale wenye kuhusiana na kiumbe hicho kwa kiasi cha gramu 213 za dhahabu, na wanalipwa wale wanaomrithi kile kiumbe (yaani kaka, dada au babu, bibi n.k. kulingana na sheria ya Mirathi), hatopewa yule aliyeshiriki kukitoa (kukiua) japo anaweza kumrithi. Na ikiwa wanaomrithi wakasamehe basi hakuna malipo. Kisha anatakiwa aache huru mtumwa (ikiwa inawezekana hilo), ikiwa haiwezekani au hakuna hali hiyo, basi anatakiwa afunge miezi miwili mfululizo ambayo ni kafara kwa ajili kuua.

Kama Asemavyo Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):

“Na haiwi Muumini kumuua Muumini ila kwa kukosea. Na mwenye kumuua Muumini kwa kukosea basi amkomboe mtumwa aliye Muumini, na atoe diya kuwapa jamaa za maiti, isipokuwa waache wenyewe kuwa ni sadaka. Na akiwa ni jamaa wa maadui zenu, hali yeye ni Muumini, basi ni kumkomboa mtumwa aliye Muumini. Na akiwa ni miongoni wa watu ambao pana ahadi baina yenu na wao basi wapewe diya watu wake na akombolewe mtumwa Muumini. Na asiye pata, basi afunge miezi miwili mfululizo, kuwa ni toba kwa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi na Mwenye hekima” [An-Nisaa: 92]

Hivyo, utaratibu wa kufanya kwa yule aliyetoa mimba baada ya siku mia na ishirini (miezi minne) yaani baada ya kupuliziwa roho, ni huu:

Kufanya toba ya kweli, na milango ya toba iko wazi hadi wakati karibu jua litakapochomoza upande wa magharibi (kabla halijachomoza), au wakati wa gharghar (roho itakapokuwa imefika kooni wakati wa kutolewa ‘mkoromo wa mauti’). Na masharti ya toba ni haya yafuatayo:
Kulipa fidia 'Diyah' (blood money);
Kafara kwa kukiua kiumbe, nayo ni kuacha huru mtumwa, au kufunga miezi miwili mfululizo.
Pia kutoa mimba kwa sababu imetokana na kitendo cha zinaa, ni jambo lisilokubalika kabisa. Kiumbe hakina makosa na tunajua kuwa habebi kiumbe madhambi ya mwengine. Allaah Anasema:

"Wala habebi mbebaji mzigo wa mwengine" [Al-An’aam: 164]

Na Amesema tena:

Na mbebaji habebi mzigo wa mwingine.)) [Faatwir 35:18]

Pia tukitazama kisa cha mwanamke wa ki-Ghaamidy aliyezini na akaenda kwa Mtue kutaka apewe adhabu ya mzinifu, na Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akamtaka aende hadi atakapozaa, na kasha akamrudisha tena hadi amnyonyeshe huyo mtoto na kisha mtoto alipokuwa mkubwa ndipo akatekeleza adhabu kwake. (Swahiyh Muslim). Tukio hilo linatuonyesha kuwa mtoto japo wa kitendo cha zinaa hairuhusiwi kabisa kuuliwa anapokuwa tumboni.

Na tufahamu kuwa kila kiumbe kinachozaliwa kinakuwa ni Muislam, na huenda huyo mtoto wa tendo la zinaa akawa Muislam bora sana kuliko wengi. Na Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aallihi wa sallam) anasema: "Kila mtoto anazaliwa katika hali ya fitwrah (maumbile ya asli; Uislam)..." imepokewa na al-Bukhaariy

Vilevile mwanamke ambaye amebakwa, haruhusiwi kutoa mimba yake kwa kauli yenye nguvu, ingawa baadhi ya Maulamaa wanasema anaweza kutoa katika siku zile arobaini za mwanzo ikiwa kuwa kwake na hiyo mimba kutamsababishia madhara katika jamii yake au kwa watu wake ima kwa kumtenga, kumsusa au hata kumuua kwa kigezo cha ‘kulinda hadhi’ ya familia au ukoo. Lakini, pamoja na sababu hizo, utakuta hazitoshi kuhalalisha kutoa mimba kwani kufanya hivyo, ni kutenda dhambi nyingine na inajulikana kuwa hicho kilichopo tumboni hakihusiki kwa njia moja au nyingine na jarima ile ya kubakwa mwanamke huyo, na maadam haikuwa ridhaa ya mwanamke kufanywa hivyo na alijitahidi kupambana na mbakaji/wabakaji akazidiwa, ni wajibu wake kukihifadhi hicho kiumbe na Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Atakilinda na kukijaalia kuwa ni chema na poza kwa mama yake. Na ikiwa mwanamke huyo hajaolewa, basi ni jambo jema kwa wanaume wa Kiislam kumsitiri na kumsaidia kumtoa katika mitihani hiyo iliyomkumba. Ama kama ana mume, basi mume wake ajitahidi japo ni vigumu sana, kusubiri na kukikubali kiumbe hicho ambacho hakina hatia yoyote ile. Na malipo makubwa yanawasubiri watu aina hiyo.

Wa Allaahu A’alam
 
Ana Rafiki Wa Kiume, Mama Yake Mdogo Anamtisha Kuwa

Akiolewa Naye Atamtangazia Kuwa Amezini Naye



Alhidaaya.com





Swali:



Asalam alekum warahmatulah wabarakatuh.



Mimi nilikuwa na boyfriend kwa muda mrefu kidogo. Mamake mdogo ambae ameshika dini sana na anaaminika katika familia yao kasema akiskia tunataka kufungua ndoa atawaambia ukoo mzima kama tumezini na atahakikisha ndoa haifungwi. Sisi tunajiamini kama hatujazini na ndoa yetu itakuwa halali lakini tunaogopa aibu ya kupakaziwa hili jambo ambalo halina ukweli wowote. Naomba ushauri wenu na In shaa Allaah Allaah atakulipeni. Tufanye nini ili tuweze kufanikisha ndoa yetu kwa misingi ya dini inavyosema kwasababu bado tunapendana sana.





Jibu:



AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.



Kabla hatujaingia katika swali lenyewe ambalo kwayo unajiweka katika hali ya kuonewa na mama mdogo wa rafiki yako wa kiume. Mwanzo tunataka kukukumbusha kuwa ni makosa kwa Muislamu kuwa na rafiki wa jinsia nyingine. Kwa maana hiyo, hufai wewe kama msichana Muislamu kuwa na rafiki wa kiume kwa muda mdogo hata kwa nukta moja au muda mrefu. Kuwa na rafiki ni njia ya kuingia katika zinaa hata ukisema kuwa hamjafanya chochote.



Allaah Aliyetukuka Anasema:

وَلَا تَقْرَبُوا الزِّنَىٰ ۖ إِنَّهُ كَانَ فَاحِشَةً وَسَاءَ سَبِيلًا ﴿٣٢﴾

Na wala msiikaribie zinaa. Hakika huo ni uchafu na njia mbaya kabisa. [Al-Israa: 32].



Na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ametuambia kuwa kila kiungo cha miili yetu, kama macho, mikono, miguu, masikio na kadhalika kinatekeleza zinaa kwa njia moja au nyingine. Macho zinaa yake ni kutazama, masikio ni kusikia, mikono ni kushika, yote yakiwa ni ya haramu yaliyokatazwa. Kwa hivyo, jambo la kwanza ambalo unatakiwa ufanye ni kutokutana na huyo rafiki yako wala kutokutana naye kwani huko ni kupata madhambi kwako.



Hatujui unamaanisha nini unaposema mama yake mdogo ameshika Dini? Kushika Dini ni kufuata maagizo ya Uislamu na kuacha makatazo yake. Kulingana na maelezo yako ni wazi kuwa inawezekana kuwa mama huyo ana Dini lakini bila ya elimu ambayo ni muhimu kukuza Dini yake. Kama angekuwa kweli ameshika Dini angemsaidia mtoto wake huyo kuweza kukamilisha Dini yake kwa kuoa mke anayempenda na kumtaka. Kitu ambacho huyo anayetaka kukuoa anafaa afanye ni kuja kwa wazee wako na kukuposa rasmi ikiwa kweli anakutaka. Ikiwa anataka kukuchezea basi atabaki kuwa ni rafiki yako tu kinyume cha shari’ah bila kuja kwenu.



Ikiwa anakutaka kweli anatakiwa huyo mume aje kwenu na kukuposa na kukuoa bila kujali watakayosema watu. Ikiwa kweli hamjazini Allaah Aliyetukuka Atawahifadhi kabisa na maneno ya watu. Ikiwa mama huyo atafanya jambo hilo atakuwa na dhambi kubwa sana mbele ya Allaah, kwani Aliyetukuka Anasema:



وَالَّذِينَ يَرْمُونَ الْمُحْصَنَاتِ ثُمَّ لَمْ يَأْتُوا بِأَرْبَعَةِ شُهَدَاءَ فَاجْلِدُوهُمْ ثَمَانِينَ جَلْدَةً وَلَا تَقْبَلُوا لَهُمْ شَهَادَةً أَبَدًا ۚ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ ﴿٤﴾

Na wale wanaowasingizia wanawake watwaharifu kisha hawaleti mashahidi wanne; basi wapigeni mijeledi themanini. Na wala msipokee ushahidi wao abadani. Na hao ndio mafasiki. [An-Nuwr: 4].



Hii Aayah inatakiwa aonyeshwe mama huyo kuonyesha dhambi kubwa anayofanya yeye na madhara kwake hapa duniani na kesho Aakhirah. Kungekuwa na Dola ya Kiislamu basi mama huyo angehitajika kuleta mashahidi wanne, akishindwa kufanya hivyo:



1. Ataadhibiwa kwa kupigwa bakora themanini.

2. Ushahidi wao hautakubaliwa tena, mpaka watubie kweli kweli.

3. Watakuwa ni miongoni mwa mafasiki, waliopotea njia.



Nasaha ambazo tunaweza kukupatia ni kama zifuatazo:



a. Mtake shauri Allaah Aliyetukuka kwa kuswali Swalah ya Istikhaarah



b. Je, kukataa kwa mama mdogo wa rafiki ni kwa ajili wewe hujashika Dini kama wanavyotaka? Hata kama hukushika Dini haimaanishi kuwa mama huyo anaweza kukusingizia mambo ambayo hujayafanya, hilo ni kosa kwake. Ikiwa unaona umeshika Dini inavyopasa unahitaji kuzungumza kwa mara ya mwisho na mchumba wako aweze kuzungumza na wazazi wake, wazee wengine au hata Mashaykh waweze kuzungumza na mama mdogo huyo kwa njia nzuri ili abadilishe msimamo wake kuhusu ndoa hiyo.



c. Je, huyo mume anayetaka kukuoa ameshika Dini inavyopasa? Ikiwa hakushika Dini utakuja kupata shida kwani hatajua haki zako kama inavyotakiwa katika Dini. Lau hujajua kuhusu hilo jaribu kumuulizia kwa wanaomjua ili usiingie katika tatizo. Usishike msemo wa Kiswahili unaosema kuwa kipendacho moyo ni dawa.



d. Taka shauri kwa wazazi wako na wazee na jamaa zako kuhusu suala hilo na utilie maanani ushauri wao.



Ukifanya hayo twataraji ya kwamba utapata kwa wepesi ufumbuzi wa tatizo lako hilo. Tunamuomba Allaah Aliyetukuka Akutimizie kila jema na zuri.





Na Allaah Anajua zaidi
 
Ana Tabia Za Kutazama Wanawake Na Picha Chafu

Anashindwa Kujizuia Nazo- Afanyeje?



Alhidaaya.com





Swali:



Nina tabia tatu Nimeshindwa kujizuia. Kuwatazama wanawake kwa matamanio. Kutazama picha zao kwenye t.v. Na kuwachezea. Yaani vitendo kabla ya jimai. Lakini si waingilii. Kila siku namuomba Rabb anitowe katika makosa haya nashukuru amenipa nguvu za kujizuia kuwaingilia lakini hayo matatu nimeshindwa na sababu kubwa ni kuwa yanapatikana kwa urahisi. Nifanye nini.





Jibu:



AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.





Awali ya yote ni kuwa mwanaadamu anaposema juu ya jambo lolote kuwa ameshindwa basi atashindwa kwa kuwa ashajiwekea udhaifu kuwa hawezi. Linalotakiwa ni kuwa na moyo thabiti na bila shaka Allaah Aliyetukuka Atakusaidia. Allaah Aliyetukuka Anasema:



إِنَّ اللَّـهَ لَا يُغَيِّرُ مَا بِقَوْمٍ حَتَّىٰ يُغَيِّرُوا مَا بِأَنفُسِهِمْ ۗ

Hakika Allaah Habadilishi yale yaliyoko kwa watu mpaka wao wenyewe wabadilishe yale yaliyomo katika nafsi zao. [Ar-Ra’d: 11].



Ikiwa unaweza kuchezecheza na wanawake bila ya kuzini nao ni kuwa wewe una uwezo wa kujizuia na hata hilo la kutazama televisheni na kuchezacheza na wanawake. Hiyo ni ishara tosha, hivyo fanya juhudi na Allaah Aliyetukuka Atakusaidia kwani Yeye Humsaidia mwenye kujisaidia.



Kisha linalotakiwa ni uwe mbali na vishawishi vyovyote ambavyo vinaweza kukuweka karibu na zinaa. Allaah Aliyetukuka Ametumia neno kali lenye uzito wa kumfanya mtu ajiepushe na uzinzi huo pale Aliposema:

وَلَا تَقْرَبُوا الزِّنَىٰ ۖ إِنَّهُ كَانَ فَاحِشَةً وَسَاءَ سَبِيلًا ﴿٣٢﴾

Na wala msiikaribie zinaa. Hakika huo ni uchafu na njia mbaya kabisa. [Al-Israa: 32].



Na kila wakati unapotaka kufanya kosa usitazame kosa lakini angalia unayemkosea. Wewe unamkosea Allaah Aliyetukuka, je, utamjibu nini utakaposimama mbele Yake Siku ya Qiyaamah siku ambayo hakutakuwa na mkalimani baina yako na Allaah Aliyetukuka.



Pia inaonyesha una wakati mwingi wa kupoteza, jaribu sana kujishughulisha na mambo ambayo yatakusahilishia kujiepusha na maovu hayo. Badala ya kuwa unapoteza wakati kwa kukaa na kutazama picha mbaya katika televisheni, nunua filamu za Kiislamu ambazo zitakufundisha kuhusu Dini yako na za mawaidha ambazo zitakuwa zinakukumbusha kuhusiana na wajibu wako juu ya hilo.



Chukua wakati mwingi katika kusoma Qur-aan, jua maana yake, zingatia yaliyo ndani, fanya juhudi kuyatekeleza hayo. Bila shaka ukifanya hayo utajikuta unakuwa karibu na Allaah Aliyetukuka na hivyo kujiepusha na mengi maovu.



Jikurubishe katika kufanya ‘Ibaadah na huku unamuomba Allaah Aliyetukuka kwa dhati Akuepushie matatizo hayo ya kujiingiza katika madhambi hayo makubwa. Na pia ulimi wako uwe na rutuba ya kumtaja Allaah Aliyetukuka kila wakati.



Tafadhali bonyeza viungo vifuatavyo upate maelezo na manufaa zaidi:



Anapenda Kuangalia Machafu Kisha Anatubu, Kisha Anarudia Tena, Naye Anachukiwa Jambo Hili



Nataka Kutubu Lakini Shaytwaan Kanivaa Nifanye Nini?



Kijana Anaishi Nchi Zenye Maasi Mengi, Anajaribu Kujizuia Anaomba Toba Kila Mara Anasumbuliwa Na Khofu Aliyonayo



Anajaribu Kufanya Mema Lakini Ana Tabia Chafu Ya Kuondosha Matamanio Kwa Mkono Na Vifaa, Afanyeje Kujiepusha Shaytwaan ?





Tunakuombea tawfiki katika kufanikisha kujiondoa katika hayo madhambi.





Na Allaah Anajua zaidi
 
Anafanya Kitendo Cha Siri Kisha Anatubu Kisha Anarudia

Tena, Hadi Anaacha Kuswali, Vipi Aache Maasi Haya



Alhidaaya.com





Swali:



Assalam Aleykum Enyi ndugu zangu Waislam Kwana kabla sijauliza Swali Langu ningependa Kuwapongeza kwa kufungua Tovuti hii yenye Kuelimisha wanaopenda dini ya Kiislam mi nina Swali ngependa Kuwauliza na nitafurahi mtakavyonjibu



Nini Athari ya Alieapa Kwamba Hatorudia Jambo Halafu Akarudia Mara Mbili Lakini Mtu Huyo Huyo Bado Anania Aongoke Lakini Matamanio Ya Mwili Hayamuachi? Na Anataka Msamaha Kutoka Kwa Rabb Wake. Mfano mimi huwa nina matamanio sana ya kuingiliana Kimwili na msichana nimejitahidi nimeacha lakini nimeshindwa kuacha Musterbation na niliapa kwamba najuta kwa ninayo fanya ee Rabb Niongoze na sitarudia tena lakini nimerudia mara mbili jee nifanye vp kurudia kwangu hunifanya muda mwingine nisi swali Kabisa Nisaidieni ndugu zangu Lakini nahitaji Maghfira kutoka kwa Rabb wangu. Masalaam





Jibu:



AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.



Fahamu ndugu yetu kuwa Allaah Aliyetukuka ni Msamehevu sana, Naye Anasamehe kila jambo kama Alivyosema:



قُلْ يَا عِبَادِيَ الَّذِينَ أَسْرَفُوا عَلَىٰ أَنفُسِهِمْ لَا تَقْنَطُوا مِن رَّحْمَةِ اللَّـهِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ يَغْفِرُ الذُّنُوبَ جَمِيعًا ۚ إِنَّهُ هُوَ الْغَفُورُ الرَّحِيمُ﴿٥٣﴾

Sema: Enyi waja Wangu ambao wamepindukia mipaka juu ya nafsi zao: Msikate tamaa na rahmah ya Allaah; hakika Allaah Anaghufuria dhambi zote; hakika Yeye Ndiye Mwenye kughufuria, Mwenye kurehemu. [Az-Zumar: 53].



Kwa hiyo, mwanzo usikate tama na ni lazima uwe na azma yenye nguvu. Ukiwa na sifa hizo pamoja na kumuomba Allaah Aliyetukuka basi yatakusaidia kabisa katika kujiondoa na madhambi hayo. Huenda pia una marafiki wabaya ambao wanaokushawishi kuliendea hilo ovu ambalo limekatazwa na Allaah Aliyetukuka. Ikiwa unaweza kutimiza masharti haya, basi msamaha wako kutoka kwa Allaah Aliyetukuka una dhamana:



1. Kujiondoa katika maasiya hayo.

2. Ajute sana katika kufanya kosa hilo.

3. Aazimie kutolirudia tena kosa hilo.



Uchu huo wa matamanio huenda ukawa unakuja kwa sababu huna mke. Kwa hiyo, unatakiwa ufanye juhudi za kutafuta mke ili uweze kukidhi mahitaji yako ya kimwili kwa njia ya halali. Kisha pia usiwe ni mwenye kuapa apa kila wakati, bali weka nia nzuri kabisa wala usiape kwani kuapa kunahitajia kafara ikiwa hujatekeleza kiapo chako.



Ili kupunguza matamanio yako inabidi pia uwe ni mwenye kufunga kama alivyoagiza Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Kufanya hivyo kutafanya matamanio yako yapungue kwa kiasi kikubwa. Na kufanya kosa la kujichua isikupelekee kuacha Swalah kwa hali yoyote ile. Shikamana na Swalah kwa hali zote na huku unamnyenyekea Allaah Aliyetukuka ili Akuondolee tatizo hilo.



Yaonyesha kuwa yamini uliyoweka si ya upuuzi bali ni ya kweli kweli. Kwa ajili hiyo kuonyesha kuwa kweli unataka kurudi kwa Allaah Aliyetukuka inatakiwa na inafaa utoe kafara iliyolezewa katika Aayah iliyo chini. Allaah Aliyetukuka Anasema:



لَا يُؤَاخِذُكُمُ اللَّـهُ بِاللَّغْوِ فِي أَيْمَانِكُمْ وَلَـٰكِن يُؤَاخِذُكُم بِمَا عَقَّدتُّمُ الْأَيْمَانَ ۖ فَكَفَّارَتُهُ إِطْعَامُ عَشَرَةِ مَسَاكِينَ مِنْ أَوْسَطِ مَا تُطْعِمُونَ أَهْلِيكُمْ أَوْ كِسْوَتُهُمْ أَوْ تَحْرِيرُ رَقَبَةٍ ۖ فَمَن لَّمْ يَجِدْ فَصِيَامُ ثَلَاثَةِ أَيَّامٍ ۚ ذَٰلِكَ كَفَّارَةُ أَيْمَانِكُمْ إِذَا حَلَفْتُمْ ۚ وَاحْفَظُوا أَيْمَانَكُمْ ۚ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ اللَّـهُ لَكُمْ آيَاتِهِ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ ﴿٨٩﴾

Allaah Hatokuchukulieni kwa viapo vyenu vya upuuzi, lakini Atakuchukulieni kwa (kuvunja) viapo mlivyoapa kwa niyyah mlioifunga thabiti. Basi kafara yake ni kulisha maskini kumi chakula cha wastani mnachowalisha ahli zenu, au kuwavisha nguo, au kuacha huru mtumwa. Lakini asiyeweza kupata (katika hayo), basi afunge Swiyaam siku tatu. Hiyo ndio kafara ya viapo vyenu mnapoapa. Na hifadhini yamini zenu. Hivyo ndivyo Allaah Anavokubainishieni Aayaat (na hukmu) Zake ili mpate kushukuru. [Al-Maaidah: 89].





Na Allaah Anajua zaidi
 
Maswali: Maasi


Anajaribu Kufanya Mema Lakini Ana Tabia Chafu Ya Kuondosha Matamanio Kwa Mkono Na Vifaa, Afanyeje Kujiepusha Shaytwaan ?



Alhidaaya.com



Swali:



Assalam alaikum



Naomba munisaidie kuhusu suala hili. Mr X anapata taabu sana kuhusu matamanio ya nafsi yake yeye mwenyewe yaani anajitamani yeye mwenyewe, kwa njia ya mikono yake na baadhi ya vitu vingine vya kumpa yeye hamu ya kutimiza haja yake. Na huyo Mr. X kashaoa na mkewe anamtimizia haja zake kama inavyostahiliwa kutimiziwa lakini yeye bado anapokua peke yake humkufuru Allaah Subhaanahu wa Ta'aalaa, kwa kujitamani yeye mwenyewe au kuangalia baadhi ya mambo ya matamanisho ili atimize azma yake. Na vilevile Mr X anajitahidi kujikurubisha katika kumtii Allaah Subhaanahu wa Ta'aalaa, kama kusali sala zote tano baadhi huzisali Msikitini na baadhi huzisali Nyumbani na wakati mwingine hujitahidi kuhudhuria darsa mbalimbali na kuwakataza watu kutokufanya mabaya asioyataka Allaah Subhaanahu wa Ta'aalaa. Na yote hayo machafu anayoyafanya anajua hasa kua hivi ninavyofanya sio mwenendo unaokubalika katika imani ya kiislam, lakini anajikuta ni mwingi wa kufanya hayo mambo machafu mpaka anajiona kua yeye kama katekwa kijinsia kimaumbile, maana anajua kama vibaya na ndani ya moyo wake halipendi, na mema anajitahidi kufanya lakini haya mabaya ndio yameshamiri zaidi. Sasa Afanye Nini Mpaka Amshinde Huyu Iblisi Aliyemkabili?



Naomba Tumsaidie MR X



Shukran





Jibu:



AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.



Hakika ni kuwa mwanaadamu ana maumbile ya kutamani na kufanya maovu. Maovu yanavutia na yanazidi kujikita katika maisha ya mwanaadamu kwa njia moja au nyingine. Baadhi yake ni kutokana na mtu kuwa mbali na Allaah Aliyetukuka kwa matendo na maneno, kutojiweka katika kufuata Sunnah za Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), kufuata matamanio, upungufu wa Imani, kuwa na marafiki wabaya, kutoishi na Qur-aan, kuwa na wakati mwingi wa faragha, kutokumbuka mauti na mengineyo.



Kwa kuwa nafsi inaamrisha mabaya inabidi Muislamu ajitahidi kujitoa katika nafsi mbaya, kuifikia nafsi yenye kujilaumu na hatimaye kupanda na kufika katika nafsi iliyotulia. Allaah Aliyetukuka Anasema:



وَمَا أُبَرِّئُ نَفْسِي ۚ إِنَّ النَّفْسَ لَأَمَّارَةٌ بِالسُّوءِ إِلَّا مَا رَحِمَ رَبِّي ۚ إِنَّ رَبِّي غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٥٣﴾

Na siitoi hatiani nafsi yangu. Hakika nafsi ni yenye kuamrisha sana maovu isipokuwa ambayo Rabb wangu Ameirehemu. Hakika Rabb wangu ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu. [Yuwsuf: 53].



Hata hivyo kulingana na maelezo juu ya kumhusu huyo ndugu, inaonekana kuwa yupo baina ya nafsi inaoamrisha maovu na ile yenye kujilaumu. Na kwa ajili hiyo ni lazima ajinasue kutoka katika hali hiyo ambayo si nzuri na itamfikisha mahali ambapo ni pabaya.



Kulingana na maelezo inaonyesha kuwa ameshindwa kujizatiti na kujiondoa katika mabaya mbali ya kuwa yeye anaamrisha mema. Na lau atakuwa ni mwenye kuzingatia Aayah zifuatazo basi huenda zikamtoa kwa aliyonayo. Allaah Aliyetukuka Anasema:



يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لِمَ تَقُولُونَ مَا لَا تَفْعَلُونَ﴿٢﴾كَبُرَ مَقْتًا عِندَ اللَّـهِ أَن تَقُولُوا مَا لَا تَفْعَلُونَ﴿٣﴾

Enyi walioamini! Kwanini mnasema yale msiyoyafanya? Ni chukizo kubwa mno mbele ya Allaah kwamba mnasema yale msiyoyafanya. [Asw-Swaff: 2 – 3].



Na pia kutazama Hadiyth zinazozungumzia adhabu anayopata mwenye kuamrisha mema naye akawa anafanya mabaya. Tukumbuke Hadiyth ya Usaamah bin Zayd bin al-Haarith (Radhwiya Allaahu ‘anhuma) kuwa amemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema:



"Ataletwa mtu Siku ya Qiyaamah, naye ataingizwa Motoni. Matumbo yake yatatoka nje, naye atayashikilia akiwa anazunguka kama anazunguka punda kwa mtambo. Watu wa Motoni watakusanyika na kusema: ‘Ee fulani una nini? Si ulikuwa ukiamrisha mema na kukataza mabaya?’ Atasema: ‘Ndio, nilikuwa nikiamrisha mema lakini siyafanyi na nikikataza mabaya, nami nikiyaendea” [Ahmad, al-Bukhaariy na Muslim]. Ikiwa atakumbushwa kuhusu hayo huenda yakamfanya ajirekebishe.





Huyo ndugu anahitaji ushauri nasaha kwa yale anayokumbana nayo. Inatakikana akalishwe chini na kuzungumziwa kwa anayoyafanya na jinsi ya kujitoa, kwani akitopigana na nafsi yake itampeleka mahali pabaya. Kwa kutazama yanayomfika, twaona lau atafanya yafuatayo, basi ataweza kujiondoa katika madhambi hayo:



Allaah Aliyetukuka Anasema:




1. Inaonyesha ana wakati wa faragha mwingi sana ndio anapatia fursa ya kufanya hayo ya madhambi. Na dawa tayari tumepatiwa, nayo ni kujaribu kuwa na mtu na hasa mke wake anapokuwa nyumbani. Hii itamsaidia endapo anajihisi kutekeleza zinaa ya mkono amwite mkewe aweze kustarehe naye. Na ikiwa mkewe hayupo nyumbani basi ajipatie jambo la kumshughulisha hapo nyumbani au nje ili asiipate hiyo faragha. Hapo nyumbani itakuwa ni kumsaidia mkewe kazi za usafi au kufanya shughuli nyengine yoyote ambayo itampatia yeye thawabu na kupata mapenzi ya mkewe. Ikiwa hilo lamshinda, basi atoke nje ya nyumba na kwenda kufanya mazoezi. Hilo linaweza kupatikana kwa kwenda uwanjani au gym na kadhalika. Kwa kuwa akiwa faragha anafanya vitu ambavyo vinamlipua, atumie wakati wake kwa kutazama video za mawaidha na vipindi vyenye kufaidisha.


2. Kwa mtu mwenye matamanio kama hayo, mbali na kuwa mmesema kuwa mkewe anamtimizia haja za kumstarehemesha inaonekana kuwa yeye mwenyewe hafikii kilele. Mke anaweza kweli akaona hivyo lakini shahawa ya mume imepita hilo. Hivyo, inatakiwa ashauriwe mume aoe mke mwengine wa kuweza kujaliza kwa yale asiyoyapata kwa mke wa kwanza.


3. Inabidi ajizoezeshe kufunga kwani kufunga kunaondoa hayo matamanio ya ziada ya mwanamme. Awe na ada ya kufunga Jumatatu na Alkhamiys.


4. Kuwa na marafiki wema na wazuri ambao watakuwa kioo kwake na kumnasihi katika hayo mambo na mengineyo.


5. Kuisoma Qur-aan kwa kuielewa na kujaribu kuitia kimatendo maishani mwake.


6. Kukumbuka mauti na kuwa siku moja atasimamishwa mbele ya Allaah Aliyetukuka na hakutakuwa na mkalimani baina yake na Rabb Wake.


7. Kutaamali zile adhabu ambazo anatarajiwa kuzipata kwa kufanya kinyume na anayoamrisha. Hasa aitaamali hiyo Hadiyth tuliyoitaja hapo juu.


8. Awe kila wakati anaomba kinga kutoka kwa Allaah Aliyetukuka hasa anapopata zile pepesi za Shaytwaan na wasiwasi wake.


9. Awe anasoma zile Adhkaar za asubuhi na jioni na kumuomba kwa dhati Allaah Aliyetukuka kumuondoshea hayo.


10. Afanye juhudi kubwa kujirekebisha, kwani Allaah Aliyetukuka Humsaidia anayejisaidia.



Allaah Aliyetukuka anasema:

إِنَّ اللَّـهَ لَا يُغَيِّرُ مَا بِقَوْمٍ حَتَّىٰ يُغَيِّرُوا مَا بِأَنفُسِهِمْ ۗ

Hakika Allaah Habadilishi yale yaliyoko kwa watu mpaka wao wenyewe wabadilishe yale yaliyomo katika nafsi zao. [Ar-Ra‘d: 11].



Bonyeza viungo vifuatavyo upate maelezo zaidi:



Nini Hukumu Ya Kujichua Sehemu Za Siri Au Kujisaga?.



Kutumia Kitu Kujitoa Matamanio Nini Hukmu Yake



Na tunatarajia kwa tawfiki ya Allaah Aliyetukuka atakuwa ni mwenye kutengea katika yaliyo bora na ya kheri zaidi.



Na Allaah Anajua zaidi
 
Maswali: Maasi




Analewa Sana Ila Mwezi Wa Ramadhwaan Anaacha Kisha Anarudia Tena Baadae Nini Hukmu Yake?



Alhidaaya.com



Swali:



Assalam alaykum



Swali, mtu anaekunya sana pombe, halafu ukifika mwezi mtukufu, ramazani anastop kunywa pombe kwa sababu ya kufunga mwezi mtukufu, mwezi ukiisha analudia pombe, nini hatima yake.





Jibu:



AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.



Unywaji wa pombe una madhara makubwa hapa duniani na Kesho Aakhirah. Allaah Aliyetukuka Anatuambia yafuatayo:



يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّمَا الْخَمْرُ وَالْمَيْسِرُ وَالْأَنصَابُ وَالْأَزْلَامُ رِجْسٌ مِّنْ عَمَلِ الشَّيْطَانِ فَاجْتَنِبُوهُ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ ﴿٩٠﴾

Enyi walioamini! Hakika pombe na kamari na masanamu na kutazamia kwa mishale ya kupigia ramli; ni najisi na chukizo kutokana na kitendo cha shaytwaan; basi jiepusheni navyo, mpate kufaulu.



إِنَّمَا يُرِيدُ الشَّيْطَانُ أَن يُوقِعَ بَيْنَكُمُ الْعَدَاوَةَ وَالْبَغْضَاءَ فِي الْخَمْرِ وَالْمَيْسِرِ وَيَصُدَّكُمْ عَن ذِكْرِ اللَّـهِ وَعَنِ الصَّلَاةِ ۖ فَهَلْ أَنتُم مُّنتَهُونَ ﴿٩١﴾

Hakika shaytwaan anataka kukutilieni baina yenu uadui na bughudha katika pombe na kamari na akuzuieni kumdhukuru Allaah na Swalaah; basi je mtakoma? [Al-Maa’idah: 90 – 91]



Ulevi umeelezwa hapa kama uchafu, uchafu unaofanana na kamari, kuabudu masanamu na kupiga ramli. Ulevi unatia uadui baina ya watu, chuki na unamzuia mtu kutekeleza ‘Ibaadah ya kumdhukuru Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) na kuswali kwa ajili Yake. Mlevi mara nyingi huwa haswali na hupuuza mengi pamoja na kujiingiza katika madhara makubwa sana.



Ama kuhusu hilo, Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

"Mwenye kunywa pombe duniani, kisha hakuleta toba, atanywima Aakhirah" [Al-Bukhaariy na Muslim]



Hadiyth hii inamaanisha kuwa mlevi anayaendelea na ulevi wake, na akakosa kuomba maghfira kabla ya kufa kwake hatokuwa ni mwenye kuipata Aakhirah. Hii inatuleta katika masharti ya tawbah. Ni hakika kuwa ili tawbah kukubaliwa ni lazima Muislamu atekeleze masharti kadhaa. Ikiwa kosa lake linaingiliana na haki ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) basi mwenye kutubia anatakiwa atimize masharti matatu, nayo ni kama yafuatayo:



1. Aache maasiya kabisa.

2. Ajute kufanya maasiya.

3. Aazimie kuwa hatorudia tena maasiya hayo.



Lakini inavyoonekana huyu mlevi ni kama anamcheza shere Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) kwa kuacha mwezi wa Ramadhwaan peke yake, akidhani kwamba Allaah ni wa Ramadhwaan pekee. Kwa minajili hiyo, hajatimiza masharti ya kukubaliwa tawbah, hivyo kuingia katika kughadhibikiwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa).





Na Allaah Anajua zaidi
 
Maswali: Maasi


Anaweza Kufuta Picha Za Ngono Katika Kompyuta Ya Mwenziwe Bila ya Ruhusa?





Alhidaaya.com





Swali:

Hongereni kwa program hii nimeikubali Allaah awazidishie mtoe bora zaidi ya hivi KEEP IN TOUCH MY FELLOW MUSLIMS je kuna tatizo lolote kufuta ie delete mambo ya kipuuzi like phonographs kwenye computer ya mtu bila ya kumtaarifu muhusika ie mwenye computer au bila yeye mwenyewe kukuruhusu sorry for this question if not good for you.



Jibu:



AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.



Hakika ni kuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na Nabiy Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) wametuhimiza sana mas-ala ya kuamrisha mema na kukataza mabaya. Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema:

ادْعُ إِلَىٰ سَبِيلِ رَبِّكَ بِالْحِكْمَةِ وَالْمَوْعِظَةِ الْحَسَنَةِ ۖ وَجَادِلْهُم بِالَّتِي هِيَ أَحْسَنُ ۚ

Lingania katika njia ya Rabb wako kwa hikmah na mawaidha mazuri. Na jadiliana nao kwa ambayo ni mazuri zaidi. [An-Nahl: 125].



Na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:



"Yeyote katika nyinyi atakayeona munkari naubadilishe kwa mkono wake; na akiwa hawezi basi afanye hivyo kwa ulimi wake; na akiwa hawezi basi afanye kwa moyo wake na huo ni udhaifu wa Imani" (Muslim).



Nguvu zinatumika kwa yule aliye chini yako kama mtoto wako au watoto unaowalea na wengineo kama mtu ambaye yupo chini ya usimamizi wako au unamlea n.k., lakini ikiwa ni rafiki yako ni lazima ubadilishe munkari kwa busara na kumkinaisha. Kuifuta pekee haitoshi kwani akiona haipo atairudisha nawe pia utakuwa umeingia makosani kidini. Na pia huenda ikamfanya mwenzio azidi kurudia hayo maovu badala ya kukubali nasaha kwa kuchukia kuingiliwa katika mambo yake ya kibinafsi Pia ufahamu kuwa hairuhusiwi kuingia katika nyumba au vitu vya watu bila idhini yao. Jambo la busara ni wewe uzungumze naye huku ukimueleza na kumfahamisha makosa hayo katika Dini. Akikinaika na hilo nawe utapata ujira na kama hakukubali kuhusu hilo wewe jukumu lako litakuwa limekwisha isipokuwa utahitajika kumnasihi tena na tena na tawfiki inatoka kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa). Hata kama hatakubali unayomwambia wewe utakuwa na ujira wako kwa ukamilifu.



Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema:

وَذَكِّرْ فَإِنَّ الذِّكْرَىٰ تَنفَعُ الْمُؤْمِنِينَ ﴿٥٥﴾

Na kumbusha, kwani ukumbusho huwafaa Waumini. [Adh-Dhaariyaat: 56]. Na anasema Allaah Subhaanahu wa Ta'aalaa:



وَمَا أُرْسِلُوا عَلَيْهِمْ حَافِظِينَ ﴿٣٣﴾

Na wao hawakutumwa kuwa ni walinzi juu yao. [Al-Mutwaffifyn: 33].



Na Anasema tena:

فَذَكِّرْ إِنَّمَا أَنتَ مُذَكِّرٌ ﴿٢١﴾لَّسْتَ عَلَيْهِم بِمُصَيْطِرٍ ﴿٢٢﴾

Basi kumbusha! Hakika wewe ni Mkumbushaji. Wewe si mwenye kuwadhibiti. [Al-Ghaashiyah: 21 – 22].



Tukumbuke pia kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa salaam) amesema:



"Miongoni mwa uzuri wa Uislamu wa mtu ni kuacha lisilomkhusu" [at-Tirmidhiy, nayo ni Hadiyth Hasan].



Nia yako na malengo ni mazuri sana, lakini ni vyema ufuate utaratibu wa sawa ili kupatikane natija nzuri inshaAllaah. Hata hivyo, ikiwa unahisi ukifuta hatoweka tena au kupata tena na kuweka, na hakutoleta matatizo, basi ni bora kufanya hivyo





Na Allaah Anajua zaidi
 
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn



باب النهي عن سؤال الإمارة واختيار ترك الولايات إذا لَمْ يتعين عليه أَوْ تَدْعُ حاجة إِلَيْهِ

081-Mlango Wa Kukatazwa Kuomba Uongozi na Kuchagua



Alhidaaya.com





قَالَ الله تَعَالَى:

تِلْكَ الدَّارُ الْآخِرَةُ نَجْعَلُهَا لِلَّذِينَ لَا يُرِيدُونَ عُلُوًّا فِي الْأَرْضِ وَلَا فَسَادًا ۚ وَالْعَاقِبَةُ لِلْمُتَّقِينَ ﴿٨٣﴾

Hiyo ni nyumba ya Aakhirah, Tunaijaalia kwa wale wasiotaka kujitukuza katika ardhi na wala ufisadi. Na hatima njema ni kwa wenye taqwa. [Al-Qaswasw: 83]







Hadiyth – 1

وعن أَبي سعيدٍ عبدِ الرحمانِ بن سَمُرَة رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ لي رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( يَا عَبْدَ الرَّحمان بن سَمُرَةَ ، لاَ تَسْأَلِ الإمَارَةَ ؛ فَإنّكَ إن أُعْطِيتَهَا عَنْ غَيْرِ مَسْألَةٍ أُعِنْتَ عَلَيْهَا ، وَإنْ أُعْطِيتَهَا عَنْ مَسْألَةٍ وُكِلْتَ إِلَيْهَا ، وَإِذَا حَلَفْتَ عَلَى يَمِينٍ ، فَرَأيْتَ غَيْرَهَا خَيْراً مِنْهَا ، فَأتِ الَّذِي هُوَ خَيْرٌ وَكَفِّرْ عَنْ يَمِينكَ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Abu Sa'iyd 'Abdir-Rahmaan bin Samurah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Aliniambia mimi Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Ee 'Abdir-Rahmaan bin Samurah! Usiombe uongozi, hakika kama utapewa bila kuuomba utasaidiwa juu yake, na ukipewa kwa kuuomba utatelekezwa nao, na ukiapa juu ya yamini na ukaona vinginevyo ni bora basi lete ambalo ni kheri na toa kafara la yamini yako." [Al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuud, At-Tirmidhiy, An-Nasai na Ahmad].





Hadiyth – 2

وعن أَبي ذرٍّ رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( يَا أَبَا ذَرٍّ ، إنِّي أرَاكَ ضَعِيفاً ، وَإنِّي أُحِبُّ لَكَ مَا أُحِبُّ لِنَفْسِي . لاَ تَأمَّرَنَّ عَلَى اثْنَيْنِ ، وَلاَ تَوَلَّيَنَّ مَالَ يَتِيمٍ )) رواه مسلم .

Toka kwa Abu Dharr amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliniambia: "Ee Aba Dharr! Hakika mimi nakuona udhaifu, Hakika mimi nakupendelea nipendelealo nafsi yangu. Usitake uongozi hata kuongoza watu wawili wala usisimamie mali ya yatima." [Muslim]





Hadiyth – 3

وعن أَبي ذرٍّ رضي الله عنه ، قَالَ : قُلْتُ : يَا رسول الله ، ألا تَسْتَعْمِلُني ؟ فَضَرَبَ بِيَدِهِ عَلَى مَنْكِبي ، ثُمَّ قَالَ : (( يَا أَبَا ذَرٍّ ، إنَّكَ ضَعِيفٌ ، وإنّها أمانةٌ ، وَإنَّهَا يَوْمَ الْقِيَامَةِ خِزْيٌ وَنَدَامَةٌ ، إِلاَّ مَنْ أخَذَهَا بِحَقِّهَا ، وَأدَّى الَّذِي عَلَيْهِ فِيهَا )) رواه مسلم .

Toka kwa Abu Dharr (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Nilisema: Ee Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): Kwa nini hunipi uongozi? Akanipiga Kofi kwa mkono wake mabega yangu, kisha akasema: "Ee Abu Dharr! Hakika wewe ni dhaifu, na hiyo ni amana, nao Siku ya Qiyaamah ni hizaya na majuto, ila mwenye kuuchukua kwa haki yake, na akatekeleza yanayo pasa ndani yake." [Muslim]





Hadiyth – 4

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( إنَّكُمْ سَتَحْرِصُونَ عَلَى الإمَارَةِ ، وَسَتَكونُ نَدَامَةً يَوْمَ القِيَامَةِ )) رواه البخاري .

Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu)kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakika nyinyi mutakuwa munapupia uongozi na utakuwa juu yenu Siku ya Qiyaamah ni majuto." [Al-Bukhaariy]
 
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn



باب حث السلطان والقاضي وغيرهما من ولاة الأمور عَلَى اتخاذ وزير صالح وتحذيرهم من قرناء السوء والقبول منهم

082-Mlango Wa Kuhimizwa Viongozi, Maqdhi na Wengineo Kuchagua Washauri na Mawaziri Wazuri na Wema na Kuonywa Kuwa na Marafiki Wabaya na Kuwakubali



Alhidaaya.com



قَالَ الله تَعَالَى:

الْأَخِلَّاءُ يَوْمَئِذٍ بَعْضُهُمْ لِبَعْضٍ عَدُوٌّ إِلَّا الْمُتَّقِينَ﴿٦٧﴾

Marafiki wapenzi Siku hiyo watakuwa maadui wao kwa wao isipokuwa wenye taqwa. [Az-Zukhruf: 67]





Hadiyth – 1

وعن أَبي سعيدٍ وأبي هريرة رضي الله عنهما : أنَّ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( مَا بَعَثَ اللهُ مِنْ نَبِيٍّ ، وَلاَ اسْتَخْلَفَ مِنْ خَليفَةٍ إِلاَّ كَانَتْ لَهُ بِطَانَتَانِ : بِطَانَةٌ تَأمُرُهُ بالمَعْرُوفِ وتَحُضُّهُ عَلَيْهِ ، وَبِطَانَةٌ تَأمُرُهُ بالشَّرِّ وَتَحُضُّهُ عَلَيْهِ ، وَالمَعْصُومُ مَنْ عَصَمَ اللهُ ))رواه البخاري .

Kutoka kwa Abu Sa'iyd na Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Allaah hakumtuma Nabiy yeyote wala hakumchagua Khalifa isipokuwa walikuwa na washauri wawili, mmoja alikuwa akimuamrisha mema na akimhimiza kwayo na mwengine akimuamrisha shari na kumhimiza kwayo. Na mtu asiyekuwa na hatia ni yule anayehifadhiwa na Allaah kutofanya madhambi." [Al-Bukhaariy].





Hadiyth – 2

وعن عائشة رضي الله عنها ، قالت : قَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( إِذَا أرَادَ اللهُ بِالأَمِيرِ خَيْراً ، جَعَلَ لَهُ وَزِيرَ صدقٍ ، إنْ نَسِيَ ذَكَّرَهُ ، وَإنْ ذَكَرَ أعَانَهُ ، وَإِذَا أرَادَ بِهِ غَيْرَ ذَلِكَ جَعَلَ لَهُ وَزِيرَ سُوءٍ ، إنْ نَسِيَ لَمْ يُذَكِّرْهُ ، وَإنْ ذَكَرَ لَمْ يُعِنْهُ )) رواه أَبُو داود بإسنادٍ جيدٍ عَلَى شرط مسلم .

Imepokewa kutoka kwa 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Allaah anapoktakia kheri kiongozi, anamjalia yeye waziri mkweli (mzuri) ambaye anamkumbusha anaposahau na anapokumbuka basi humsaidia. Na anapomtakia kinyume na hilo (yaani shari), anamjaalia waziri mbaya ambaye hamkumbushi anaposahau na anapokumbuka basi hamsaidii." [Abuu-Daawuud, na Isnaad yake ni Jayd (nzuri) kwa sharti ya Muslim].
 
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn



باب النهي عن تولية الإمارة والقضاء وغيرهما من الولايات لمن سألها أَوْ حرص عليها فعرَّض بها

083-Mlango Wa Kukataza Kumpatia Uongozi na Ukadhi na Nyadhifa Nyinginezo za Uongozi kwa Mwenye Kuomba Ama Kupupia



Alhidaaya.com





عن أَبي موسى الأشعريِّ رضي الله عنه ، قَالَ : دَخَلْتُ عَلَى النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم أنَا وَرَجُلانِ مِنْ بَنِي عَمِّي ، فَقَالَ أحَدُهُمَا : يَا رسول الله ، أمِّرْنَا عَلَى بَعْض مَا ولاَّكَ اللهُ (عزّ وجلّ) ، وقال الآخَرُ مِثلَ ذَلِكَ ، فَقَالَ : (( إنَّا وَاللهِ لاَ نُوَلِّي هَذَا العَمَلَ أحَداً سَألَهُ ، أَوْ أحَداً حَرَصَ عَلَيْهِ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Abuu Muwsaa Al-Ash'ariy (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Nilienda kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) nikiwa na watu wawili katika watoto wa ami zangu. Akasema mmoja wao: "Ee Rasuli wa Allaah! Tupe uongozi kwa baadhi ya aliyokutawalisha Allaah ('Azza wa Jalla)." Mwingine akasema mfano wake, Akasema: "Wa-Allaahi, sisi hatumpi kazi yeyote anayeomba au yeyote mwenye kuonyesha dalili ya kupupia." [Al-Bukhaariy, Muslim na An-Nasai].
 
Alhamdulillah tumemaliza kusoma kitabu chetu cha Riyaadhw Asw-Swaalihiyn katika maudhui mbali mbali

Huenda tutakutana nacho tena katika maudhui mengine

..........................................................................................................
 
UONGOZI NI DHAMANA KUBWA

Tumesoma hapo katika kitabu chetu ambacho tumekimaliza katika mlango wa kutopupia kuomba Uongozi

Rasul swalla aallahu aliyhi wa aalih wa sallam amesema mtu akipewa pasina kuuomba hakika atasaidiwa na Allah na yule atakaye omba itakuwa kinyume chake

Lakini hatuna budi kufahamu kuwa hakika Uongozi ni dhamana na mtu atakuja kuulizwa siku ya kiama,kama tunavyosoma katika hadith

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( إنَّكُمْ سَتَحْرِصُونَ عَلَى الإمَارَةِ ، وَسَتَكونُ نَدَامَةً يَوْمَ القِيَامَةِ )) رواه البخاري .

Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu)kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakika nyinyi mutakuwa munapupia uongozi na utakuwa juu yenu Siku ya Qiyaamah ni majuto." [Al-Bukhaariy]

Kwahiyo kuna baadhi ya watu hakika hiyo siku ya hukumu watakuja kuwajibika mbele ya Allah kwa uongozi wao

Kwahiyo kabla hujawa kiongozi tambua kwamba hakika hiyo ni dhamana na utakuja kuulizwa ni kiasi gani ulitekeleza uongozi wako

Jiulize je unataka uongozi kwa maslahi yako binafsi au kwa maslahi ya umma mzima?

Je unaweza kufanya uadilifu kwa unao waongoza?

Je utakuwa mpole na mwenye huruma kwa wale unao waongoza au utakuwa mkali tu?

Kumbuka Nabii swalla aallahu alaiyhi wa sallam anasema hakika jambo lolote halitakuwa na upole ila litakuwa zuri na jambo lolote halitakuwa na ukali ila litaharibika

Haimaanishi kwamba kuna nyakati hautahitajika kuwa mkali laa! Utakuwa mkali kwasababu maalumu kama kuna uzembe na mambo kama hayo,lakini muda mwingi ushikamane na upole,toa nasaha kwa walio chini yako pale unapo warekebisha na kuyaweka mambo sawa
 
UJUMBE WA LEO :

Penda kuwa karibu na watu ambao watakukumbusha akhera yako
 
00-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! Utangulizi


إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيمٌ



Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!



00-Utangulizi



Alhidaaya.com






بِسْمِ الله الرَّحْمنِ الرَّحِيم



الْحمْدُ لِلَّه وَالصَّلاةُ وَالسِّلامُ عَلى خَاتم الأنْبِيَاء وَالْمُرْسَلِين، الْمَبْعُوثُ رَحْمَةً لِلْعَالَمِين، مُحَمَّد وَعَلى آلِه وَأصْحابِه أجْمَعِين وَمَنْ تَبِعَهُمْ بِإِحْسَانٍ إِلَى يَوْمِ الدِّينِ.

Himdi Anastahiki Allaah, Swalaah na salaam zimfikie Nabiy na Rasuli wa mwisho, aliyetumwa awe rahmah kwa walimwengu, Muhammad, pamoja na ahli zake na Maswahaba zake wote, na wanaowafuata kwa ihsaan mpaka Siku ya Malipo.





Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيمٌ ﴿١٣﴾

hakika shirki ni dhulma kubwa mno [Luqmaan: 13]





Kinyume ya shirki ni Tawhiyd ambayo ni kumpwekesha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) katika Rubuwbiyyah (Uola) Uluwhiyyah (‘ibaadah) Yake na katika Asmaa na Swifaat (Majina na Sifa nzuri) Zake. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):



وَلَقَدْ أُوحِيَ إِلَيْكَ وَإِلَى الَّذِينَ مِن قَبْلِكَ لَئِنْ أَشْرَكْتَ لَيَحْبَطَنَّ عَمَلُكَ وَلَتَكُونَنَّ مِنَ الْخَاسِرِينَ﴿٦٥﴾

Kwa yakini umefunuliwa Wahy na kwa wale walio kabla yako kwamba: “Ukifanya shirki bila shaka zitaporomoka ‘amali zako na bila shaka utakuwa miongoni mwa waliokhasirika.”



بَلِ اللَّـهَ فَاعْبُدْ وَكُن مِّنَ الشَّاكِرِينَ﴿٦٦﴾

Bali Allaah Pekee mwabudu, na uwe miongoni mwa wenye kushukuru. [Az-Zumar: 65-66]





Waislamu wengi wako katika hali ya kumshirikisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa); wengine wakiwa wanatambua hatari zake, na wengine wakiwa hawatambui kuwa wanamshirikisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa), kwa sababu baadhi ya ‘amali zinazotendwa zinaonekana kuwa kama ni nzuri na hali zimeingia shirki ndani yake.



Imaam Muhammad bin ‘Abdil-Al-Wahhaab amesema katika Al-Qawaaid Al-Arba’: “Kwamba washirikina wa zama zetu ni waovu zaidi (shirki zao ni kubwa zaidi) kuliko washirikina wa awali, kwa sababu, wa awali walimshirikisha Allaah katika raha, lakini wakizitakasa ‘Ibaadah zao wakati wa shida. Ama washirikina wa sasa, shirki zao ni wakati wote, wakiwa katika raha au katika shida … na dalili ni kauli Yake Ta’aalaa:



فَإِذَا رَكِبُوا فِي الْفُلْكِ دَعَوُا اللَّـهَ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ فَلَمَّا نَجَّاهُمْ إِلَى الْبَرِّ إِذَا هُمْ يُشْرِكُونَ ﴿٦٥﴾

Wanapopanda merikebu humwomba Allaah wakiwa wenye kumtakasia Yeye Dini, lakini Anapowaokoa katika nchi kavu, tahamaki hao wanamshirikisha. [Al-‘Ankabuwt: 65]



Kwa hiyo, kuna umuhimu mkubwa wa Waislamu kujifunza somo hili ili kujitahadharisha na hatari zake ili waweze kufunga milango na njia zote kubwa na ndogo za shirki. Makala hizi In Shaa Allaah zitaweza kutambulisha na kubainisha matendo mengi yanayomshirikisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na namna ya kuyaepuka, ili Muislamu abakie katika amri ya Muumba wake Ambaye Ameamrisha kuabudiwa Yeye Pekee bila ya kumshirikisha. Kumshirikisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) ni katika dhambi kubwa mno kama alivyobainisha Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):



عَنْ اِبْنِ مَسْعُودٍ ‏ رضى الله عنه ‏ قَالَ سَأَلْتُ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم: أَيُّ اَلذَّنْبِ أَعْظَمُ؟ قَالَ: ((أَنْ تَجْعَلَ لِلَّهِ نِدًّا, وَهُوَ خَلَقَكَ))‏

Imepokelewa kutoka kwa ibn Mas-‘uwd (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ambaye amesema: “Nilimuuliza Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): Je, dhambi ipi kubwa mno?” Akasema: ((Kumfanyia Allaah mlinganishi (wa kumshirikisha) na hali Yeye Amekuumba)) [Al-Bukhaariy, Muslim]



Nukta chache zifuatazo ni mukhtasari wa hatari za kumshirikisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):





1. Shirki inaharibu ‘amali za mtu. Dhambi hii kubwa walitahadharishwa Rasuli wa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwa ukali mno pale Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anaposema:



وَلَوْ أَشْرَكُوا لَحَبِطَ عَنْهُم مَّا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿٨٨﴾

Na kama wangemshirikisha bila shaka yangeporomoka yale waliyokuwa wakitenda. [Al-An’aam: 88]





2. Shirki ni dhambi pekee ambayo Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Haisamehe isipokuwa tu mtu akirudi kutubia Kwake. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

إِنَّ اللَّـهَ لَا يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَاءُ ۚ وَمَن يُشْرِكْ بِاللَّـهِ فَقَدْ ضَلَّ ضَلَالًا بَعِيدًا﴿١١٦﴾

Hakika Allaah Haghufurii kushirikishwa; lakini Anaghufuria yasiyokuwa hayo kwa Amtakae. Na yeyote atakayemshirikisha Allaah basi kwa yakini amepotoka upotofu wa mbali. [An-Nisaa: 116]





3. Shirki inamtoa mtu nje ya Uislamu!



Imeelezwa shirki kuwa ni miongoni mwa matendo yanayomtoa mtu nje ya Uislamu, kama ilivyo katika Nawaaqidhw Al-Islaam cha Imaam Muhammad ibn Al-Wahhaab (Rahimahu-Allaah).



Na miongoni mwa mengi wanayotenda baadhi ya Waislamu ni kumwendea kahini anayetabiri mambo ya ghayb; elimu ambayo hakuna aijuae isipokuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa). Hatari ya tendo hili ni kama alivyotahadharisha Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):



وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ) عَنِ النَّبِيِّ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) قَالَ: ((مَنْ أَتَى كَاهِنًا، فَصَدَّقَهُ بِمَا يَقُولُ فَقَدْ كَفَرَ بِمَا أُنْزِلَ عَلَى مُحَمَّدٍ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ)) رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ

Imepokewa toka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kutoka kwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Atakayemkaribia kahini na kuamini anayoyasema basi amekanusha aliyoteremshiwa Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم)) [Abu Daawuwd]





4-Mwenye kumshirikisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) ni mwenye hatima mbaya mno ya makazi ya Moto. Ametahadharisha hilo Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

إِنَّهُ مَن يُشْرِكْ بِاللَّـهِ فَقَدْ حَرَّمَ اللَّـهُ عَلَيْهِ الْجَنَّةَ وَمَأْوَاهُ النَّارُ ۖ وَمَا لِلظَّالِمِينَ مِنْ أَنصَارٍ﴿٧٢﴾

Hakika mwenye kumshirikisha Allaah bila shaka Allaah Atamharamishia Jannah, na makazi yake yatakuwa ni motoni. Na madhalimu hawatopata yeyote mwenye kunusuru.” [Al-Maaidah: 72]



Tunataraji tawfiyq ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) makala hizi ziwazidishie elimu yenye manufaa Waislamu kuhusiana na somo hili na Atuepushe sote kumshirikisha Yeye Subhaanahu wa Ta’aalaa.
 
01-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Maana Ya Dhulma Na Shirki


إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيمٌ



Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!



01- Maana Ya Dhulma Na Shirki



Alhidaaya.com




Maana ya dhulma ni kuweka kitu mahali pasipo pake. Hivyo anayeabudu au kumwomba asiyekuwa Allaah atakuwa ameilekeza ‘ibaadah yake kwa asiyestahiki.



Maana ya shirki ni kumwekea Allaah mshirika katika Ar-Rubuwbiyyah (Uola) Wake au Uluwhiyyah (‘Ibaadah) Yake au Asmaa na Swifaat Zake.



عَنْ عبد الله بن مسعود رضي الله عنه قال: لَمَّا نَزَلَتْ هَذِهِ الآيَةُ: الَّذِينَ آمَنُوا وَلَمْ يَلْبِسُوا إِيمَانَهُم بِظُلْمٍ، شَقَّ ذَلِكَ عَلَى النَّاس وَقَالُوا: أَيُّنَا لَمْ يَظْلِمْ نَفْسَهُ؟! فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((إنَّه لَيْسَ كَمَا تَعنُون! ألَمْ تَسْمَعوا ما قال الْعبْد الصَّالح؟ يَا بُنَيَّ لَا تُشْرِكْ بِاللَّـهِ ۖ إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيمٌ- إنَّما هُو الشِّرْك))

Imepokelewa kutoka kwa ‘Abdullaah bin Mas‘uwd (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ambaye amesema: Ilipoteremshwa Aayah hii: Wale walioamini na hawakuchanganya iymaan zao na dhulma; [An-An’aam: 82] Iliwatatiza watu wakasema: “Nani katika sisi hajadhulumu nafsi yake?” Akasema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): ((Si kama vile mnavyomaanisha! Hamsikii pale mja mwema aliposema: “Ee mwanangu! Usimshirikishe Allaah, hakika shirki ni dhulma kubwa mno!” [Luqmaan: 13] Hakika hiyo ni shirk.)) [Ahmad na riwaayah zinazofanana katika Al-Bukhaariy na wengineo]



Shaykh Al-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema: “Hakika kila Alichokikataza Allaah kinarejea katika dhulma na kila Alichokiamrisha kinarejea katika uadilifu, na ndio maana Allaah (Tabaaraka wa Ta’aalaa) Anasema:

لَقَدْ أَرْسَلْنَا رُسُلَنَا بِالْبَيِّنَاتِ وَأَنزَلْنَا مَعَهُمُ الْكِتَابَ وَالْمِيزَانَ لِيَقُومَ النَّاسُ بِالْقِسْطِ

Kwa yakini Tuliwapeleka Rusuli Wetu kwa hoja bayana, na Tukateremsha pamoja nao Kitabu na Miyzaan (shariy’ah) ili watu wasimamie kwa uadilifu. [Al-Hadiyd: 25]



Akajulisha kwamba Ametuma Rasuli na Ameteremsha Kitabu na shariy’ah kwa ajili ya watu wasimamie uadilifu” [Majmuw’ Al-Fataawa li Ibn Taymiyyah (18/157)]



Kumshirikisha Allaah aghlabu ni katika Uluwhiyyah Yake kwa kumwomba asiyekuwa Allaah, au kuelekeza aina yoyote ya ‘ibaadah kwa asiyekuwa Allaah kama kuchinja, kuweka nadhiri, kuapa, kukhofu na kutaraji, kutawakkal, istighaathah (kuomba uokozi au kinga) au kujikurubisha na yeyote au chochote kile kisichokuwa Allaah.



Vile vile kumlinganisha Allaah na viumbe. Anasema Allaah:

يَا أَيُّهَا النَّاسُ اعْبُدُوا رَبَّكُمُ الَّذِي خَلَقَكُمْ وَالَّذِينَ مِن قَبْلِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ ﴿٢١﴾

Enyi watu! Mwabuduni Rabb wenu Ambaye Amekuumbeni na wale wa kabla yenu mpate kuwa na taqwa.



الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ الْأَرْضَ فِرَاشًا وَالسَّمَاءَ بِنَاءً وَأَنزَلَ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً فَأَخْرَجَ بِهِ مِنَ الثَّمَرَاتِ رِزْقًا لَّكُمْ ۖ فَلَا تَجْعَلُوا لِلَّـهِ أَندَادًا وَأَنتُمْ تَعْلَمُونَ ﴿٢٢﴾

Ambaye Amewafanyieni ardhi kuwa ni tandiko na mbingu kuwa ni paa, na Akateremsha kutoka mbinguni maji, Akawatolea kwayo matunda kuwa ni riziki zenu. Basi msimfanyie Allaah waliolingana naye na hali ya kuwa nyinyi mnajua. [Al-Baqarah: 21-22]



Na Anasema pia Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

وَجَعَلُوا لِلَّـهِ أَندَادًا لِّيُضِلُّوا عَن سَبِيلِهِ

Na wakamfanyia Allaah walinganishi ili wapoteze (watu) na njia Yake. [Ibraahiym: 30]



Na Anasema pia (سبحانه وتعالى):

قُلْ أَئِنَّكُمْ لَتَكْفُرُونَ بِالَّذِي خَلَقَ الْأَرْضَ فِي يَوْمَيْنِ وَتَجْعَلُونَ لَهُ أَندَادًا ۚ ذَٰلِكَ رَبُّ الْعَالَمِينَ﴿٩﴾

Sema: “Je, hivi nyinyi mnamkufuru Yule Aliyeumba ardhi kwa siku mbili, na mnamfanyia waliolingana Naye? Huyo Ndiye Rabb wa walimwengu.” [Fusw-Swilat: 9]
 
02-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Shirki Ni Aina mbili Na Tofauti Zake


إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيمٌ

Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!

02- Shirki Ni Aina mbili Na Tofauti Zake

Alhidaaya.com





Shirki ni aina mbili; shirki kubwa na shirki ndogo.



1-Shirki Kubwa inamtoa mtu nje ya Uislamu, ‘amali zake zote zinaporomoka, mwenye kumshirikisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwa shirki kubwa huwa ni halali damu yake, na mali yake na ni mwenye kudumu Motoni ikiwa hatotubia kabla ya kufariki kwake. Na dhambi ya shirki kubwa ni dhambi pekee ambayo Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Hamsamehi mja atakapokufa bila kutubia. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):



إِنَّ اللَّـهَ لَا يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَاءُ ۚ

Hakika Allaah Haghufurii kushirikishwa; lakini Anaghufuria yasiyokuwa hayo kwa Amtakae. [An-Nisaa: 48]



Shirki kubwa ni kuelekeza ‘ibaadah na kuomba du’aa kwa asiyekuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa). Washirikina wao ndio kabisa hawamwabudu Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) japokuwa huenda wengine wanaamini kuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Ndiye Muumba kama walivyoamini hivyo washirikina wa Makkah. Shirki yao imethibiti katika Uluwhiyyah (‘ibaadah) pale walipoabudu masanamu wakidai kuwa yanawakurubisha kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kama ilivyotajwa katika Qur-aan:



وَالَّذِينَ اتَّخَذُوا مِن دُونِهِ أَوْلِيَاءَ مَا نَعْبُدُهُمْ إِلَّا لِيُقَرِّبُونَا إِلَى اللَّـهِ زُلْفَىٰ

na wale waliojichukulia badala Yake walinzi (wakisema): “Hatuwaabudu isipokuwa ili wapate kutukurubisha kwa Allaah tumkaribie” [Az-Zumar: 3]



Wengine ndio wamemshirikisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na viumbe Vyake wakawafanya ni ilaah (waabudiwa) wao. Juu ya hayo, Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anamghufuria yeyote yule anayerudi kutubia Kwake baada ya kufuru na shirki kubwa kama hizo. Dalili ni kauli zifuatazo katika Qur-aan:



لَقَدْ كَفَرَ الَّذِينَ قَالُوا إِنَّ اللَّـهَ هُوَ الْمَسِيحُ ابْنُ مَرْيَمَ ۖ وَقَالَ الْمَسِيحُ يَا بَنِي إِسْرَائِيلَ اعْبُدُوا اللَّـهَ رَبِّي وَرَبَّكُمْ ۖ إِنَّهُ مَن يُشْرِكْ بِاللَّـهِ فَقَدْ حَرَّمَ اللَّـهُ عَلَيْهِ الْجَنَّةَ وَمَأْوَاهُ النَّارُ ۖ وَمَا لِلظَّالِمِينَ مِنْ أَنصَارٍ﴿٧٢﴾

Kwa yakini wamekufuru wale waliosema: “Hakika Allaah ni Al-Masiyh mwana wa Maryam.” Na Al-Masiyh alisema: “Enyi wana wa Israaiyl! Mwabuduni Allaah, Rabb wangu na Rabb wenu. Hakika mwenye kumshirikisha Allaah bila shaka Allaah Atamharamishia Jannah, na makazi yake yatakuwa ni motoni. Na madhalimu hawatopata yeyote mwenye kunusuru.”



لَّقَدْ كَفَرَ الَّذِينَ قَالُوا إِنَّ اللَّـهَ ثَالِثُ ثَلَاثَةٍ ۘ وَمَا مِنْ إِلَـٰهٍ إِلَّا إِلَـٰهٌ وَاحِدٌ ۚ وَإِن لَّمْ يَنتَهُوا عَمَّا يَقُولُونَ لَيَمَسَّنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿٧٣﴾

Kwa yakini wamekufuru wale waliosema: “Hakika Allaah ni watatu wa utatu.” Na hali hapana Muabudiwa wa haki isipokuwa Ilaah Mmoja Pekee. Na wasipoacha yale wanayoyasema, bila ya shaka itawagusa wale waliokufuru miongoni mwao adhabu iumizayo.



أَفَلَا يَتُوبُونَ إِلَى اللَّـهِ وَيَسْتَغْفِرُونَهُ ۚ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٧٤﴾

Je, hawatubii kwa Allaah na wakamwomba maghfirah? Na Allaah ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu. [Al-Maaidah: 72-74]



2-Shirki Ndogo: Hii inajulikana kama riyaa, nayo ni kufanya ‘ibaadah au kutenda amali lakini kwa niyyah ya kujionyesh a kwa watu. Shirki hii haimtoi mtu nje ya Uislamu bali ‘amali zake huporomoka na, ni mwenye kuadhibiwa Motoni kwa kadiri ya madhambi yake.



Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amewahofia Swahaabah aina hii ya shirki:



عن مَحْمُودِ بْنِ لَبِيدٍ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إنَّ أخوَفَ ما أخافُ عليكم الشِّركُ الأصغرُ، قالوا: وما الشِّركُ الأصغر؟ قال: الرِّياءُ، يقولُ اللهُ عزَّ وجلَّ لأصحابِ ذلك يومَ القيامةِ إذا جازَى النَّاسَ اذهبوا إلى الَّذين كنتم تُرائون في الدُّنيا فانظُروا هل تجِدون عندهم جزاءً؟" - صححه الألباني في السلسلة الصحيحة(951 )

Imepokelewa kutoka kwa Mahmuwd bin Labiyd ambaye amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: Hakika ninachokihofia kwenu zaidi ni shirki ndogo. Wakasema: Ni ipi hiyo shirki ndogo? Akasema: Ar-Riyaa. Allaah ('Azza wa Jalla) Atawaambia watu wa Siku ya Qiyaamah pale watakapolipwa watu jazaa: Nendeni kwa wale mliokuwa mkijionyesha kwa ‘amali zenu duniani kisha tazameni je, mtakuta kwao jazaa? [Ahmad na ameisahihisha Shaykh Al-Albaaniy katika Silsilat Al-Hadiyth Asw-Swahiyhah (951)]
 
03-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Shirki Ndogo - Riyaa (Kujionyesha)


إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيمٌ

Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!



03- Shirki Ndogo : Riyaa (Kujionyesha)



www.alhidaaya.com





‘Amali zote zinahitaji kutangulizwa na niyyah safi. Hadiyth mashuhuri ambayo ‘Ulamaa wamesema kuhusu Hadiyth hii kwamba ni nusu ya ya Dini kama alivyosema Imaam Abu Daawuwd, kwani Dini inakusanya vilivyo dhahiri kama vitendo na visivyo dhahiri kama niyyah.

إِنَّما الأَعْمَالُ بالنِّيَّاتِ وإنَّما لكُلِّ امْرِىءٍ ما نَوَى،

Hakika ‘amali inategemea (malipo) kwa niyyah na kila mtu atapata kwa mujibu wa kila alichotilia niyyah. [Al-Bukhaariy, Muslim]





Imaam Ash-Shaafi’iy naye kasema Hadiyth hii ni nusu ya elimu. Naye Imaam Ahmad na Imaam Ash-Shaafi’iy wamesema Hadiyth hii inakusanya moja ya tatu ya elimu. Imaam Al-Bayhaqiy akafafanua maneno yao hayo kwa kusema, “Hayo ni kwa sababu, mtu huchuma thawabu kwa moyo wake, ulimi na mwili wake. Hivyo, niyyah inahusiana na moja ya viungo hivyo vitatu. [Ibn Hajr, Fat-h Al-Baariy, mj. 1, uk. 11]



Na sharti za kupokelewa ‘amali za mja ni ikhlaasw, niyyah safi ya ‘amali kwa kufuata amri ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kama Anavyoamrisha:



وَمَا أُمِرُوا إِلَّا لِيَعْبُدُوا اللَّـهَ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ حُنَفَاءَ وَيُقِيمُوا الصَّلَاةَ وَيُؤْتُوا الزَّكَاةَۚ وَذَٰلِكَ دِينُ الْقَيِّمَةِ ﴿٥﴾

Na hawakuamrishwa isipokuwa wamwabudu Allaah wenye kumtakasia Dini, wenye kujiengua na upotofu kuelemea Dini ya haki na wasimamishe Swalaah na watoe Zakaah; na hiyo ndiyo Dini iliyosimama imara. [Al-Baayyinah: 5]





Na Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):



فَمَن كَانَ يَرْجُو لِقَاءَ رَبِّهِ فَلْيَعْمَلْ عَمَلًا صَالِحًا وَلَا يُشْرِكْ بِعِبَادَةِ رَبِّهِ أَحَدًا ﴿١١٠﴾

Hivyo anayetaraji kukutana na Rabb wake, basi na atende ‘amali njema na wala asimshirikishe yeyote katika ‘ibaadah za Rabb wake.” [Al-Kahf: 110]



Yaani asifanye riyaa (kujionyesha) ‘amali zake kwa watu kama Swalaah, Hajj, Swawm, Zakaah, Swadaqah, kusoma Qur-aan, kufanyia watu wema na ihsaan kwa ajili ya kusifiwa, kujitukuza au kuonekana ni mwema na sifa kama hizo za riyaa.



Na Rasuli wa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) aliwatahadharisha Swahaabah (Radhwiya Allaahu ‘anhum) kuhusu riyaa. Siku ya Qiyaamah pindi mtu atakapokuja na ‘amali zake itatambulikana kama zilikuwa za ikhlaasw au za riyaa kwani Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema katika Hadiyth:



عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه) قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ (صلى الله عليه وآله وسلم): ((إِنَّ اللَّهَ لاَ يَنْظُرُ إِلى أجْسمِكُمْ وَلاَ إِلَى صُوَرِكُمْ وَلَكِنْ يَنْظُرُ إِلَى قُلُوبِكُمْ)) رواه مسلم

Imepokelewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ambaye amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hakika Allaah Hatazami viwiliwili vyenu wala sura zenu, lakini Anatazama nyoyo zenu)). [Muslim]



Nyoyo ndizo zitakazodhihirisha ikhlaasw ya mtu kwani humo ndipo kunapofichika shirki kama ilivyobainishwa katika Hadiyth ifauatayo:



عَنْ أَبِي سَعِيدٍ، قَالَ: خَرَجَ عَلَيْنَا رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَنَحْنُ نَتَذَاكَرُ الْمَسِيحَ الدَّجَّالَ، فَقَالَ: ((أَلا أُخْبِرُكُمْ بِمَا هُوَ أَخْوَفُ عَلَيْكُمْ عِنْدِي مِنَ الْمَسِيحِ الدَّجَّالِ؟)) قَالَ: قُلْنَا: بَلَى! فَقَالَ: ((الشِّرْكُ الْخَفِيُّ، أَنْ يَقُومَ الرَّجُلُ يُصَلِّي، فَيُزَيِّنُ صَلاتَهُ، لِمَا يَرَى مِنْ نَظَرِ رَجُلٍ)) سنن ابن ماجه (4204).

Imepokelewa kutoka kwa Abu Sa’iyd (Radhwiya Allaahu 'anhu) ambaye amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu alayhi wa aalihi wa sallam) alikuja kwetu wakati tulikuwa tukijadiliana kuhusu Dajjaal, akasema: ((Je, niwajulisheni kile nikikhofiacho zaidi kwenu kuliko hata (hatari za) Dajjaal?)) Tukasema: Ndio. Akasema: ((Basi ni shirki iliyojificha. Mtu anasimama kuswali, anaipamba na kuiremba Swalaah yake kwa kujua kuwa kuna watu wanamtazama)) [Sunan Ibn Maajah (4204)]



Hiyo ni kama sifa ya wanafiki wanaomhadaa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kama Anavyosema:



إِنَّ الْمُنَافِقِينَ يُخَادِعُونَ اللَّـهَ وَهُوَ خَادِعُهُمْ وَإِذَا قَامُوا إِلَى الصَّلَاةِ قَامُوا كُسَالَىٰ يُرَاءُونَ النَّاسَ وَلَا يَذْكُرُونَ اللَّـهَ إِلَّا قَلِيلًا ﴿١٤٢﴾

Hakika wanafiki (wanadhani) wanamhadaa Allaah, na hali Yeye (Allaah) Ndiye Mwenye kuwahadaa. Na wanaposimama kuswali husimama kwa uvivu, wakijionyesha kwa watu na wala hawamdhukuru Allaah isipokuwa kidogo tu. [An-Nisaa: 142]
 
Dada Mmoja Karitadi, Wengine Wanaishi Na Wanaume Wakiristo, Je, Akate Mahusiano Nao?
Maswali: familia-Jamii
SWALI:



Asalaam aleykum warahmatullah wabarakatuh



[1] Naomba kupata ufafanuzi;kuna mdogo wangu wa kike tumechangia mama alibadilisha dini na kuwa mkristo na kufunga ndoa ya kikristo na wakati huo mama yetu alikuwa hai;mimi na ndugu zangu wa kiume hatukujihusisha na swala la hiyo ndoa japo aliyefariki mama alikasirika sana akaona kama hatumtendei haki huyo mdogo wetu na yeye pia, hata hivyo mimi binafsi nilimkanya kabla huyu mdogo wangu akadai mama ndio amemshauri wakati huo alikuja kwangu kutaka ushauri na kunidanganya hajabadili dini kumbe alishabadili na walikuwa kataka mipango ya ndoa; hata hivyo ndugu zangu na mimi hatukanyagi kwake wala yeye haji kwetu sisi wote ambao tulipinga swala la kubadilsha dini na yeye kutoka katika uislam.

[2] Kuna dada zangu wengine nimechangia nao baba wapo wawili wao nao wanaishi na wanaume wakristo na wamezaa nao ila hawajafunga ndoa, mimi huwa nakwenda kwao kwani bado ni ngugu zangu kwa damu na imani, je nafanya makosa kuwatembelea kwani hata wao kwangu wanakuja? Shekhe naomba majibu kwa haraka kidogo ili niyafanyie kazi.









JIBU:



Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.





Shukrani zetu za dhati kwa swali lako zuri kuhusu dada aliyeritadi na dada walioolewa na Wakristo.





Hakika masuala haya mawili ni nyeti sana kwa wakati wetu huu wa ulimwengu. Kwa kuwa tunakumbana na mambo hayo katika majarida na vyombo vya habari na kwa ajili hiyo tunaiga bila kujua ukweli na uhakika wa masuala hayo.



Kuritadi ni jambo baya katika Uislamu kwani linakuingiza mtu Motoni ikiwa hatorudi tena katika Dini. Lau kungekuwa na dola ya Kiislamu basi dada kama huyo au Muislamu yeyote anayefanya hivyo itabidi achukuliwe hatua na serikali kwa kumfanyia Da‘wah na kumnasihi ili arudi katika Dini ya Fitwrah (maumbile ya asli). Kwa kuwa dola hiyo haipo shughuli hiyo inabidi ifanywe nanyi huku mukizingatia maadili ya ulinganizi na nasaha.

Hamtopenda dada yenu apate shida hapa duniani na Kesho Akhera. Ikiwa sisi hatupendelei hilo basi nasi pia tusimuache dada yetu aelekee paovu. Itabidi mtumie busara na hekima ya kuweza kumvutia tena katika Uislamu kwa njia zote. Kwa kwenda kuzungumza naye, kuwatuma watu wenye ujuzi wa dini, kumtumia vitabu na hata kaseti. Ikiwa atang’ang’ania katika ukafiri wake itabidi wakati huo mukate mahusiano naye ya moja kwa moja lakini baada ya kutumia mbinu zote muwezazo za kumrudisha katika Uislamu.



Hakika ni makosa makubwa kwa dada Muislamu kukaa na asiyekuwa Muislamu kwa njia yoyote ile. Hiyo kisheria ni zinaa ambayo ni dhambi kubwa katika Uislamu. Na hata kama wangeolewa, kisheria pia hakuna ndoa baina ya binti Muislamu na mume kafiri, ndoa ya namna hiyo haitambuliki kuwa ni ndoa. Kwa njia hiyo pia itakuwa ni zinaa kisheria. Jambo ambalo mnafaa kufanya sio tu kutembeleana bali kuwalingalia dada zako waachane na wanaume hao kwani wapo katika njia iliyo mbaya. Inafaa mtumie njia mbalimbali za Da‘wah ili kuwavutia tena warudi katika Uislamu. Pia muwatumie watu wenye elimu kuliko nyinyi ili waende kuzungumza nao, kuwatumia vitabu, makala, kaseti kuhusu mambo tofauti ya Uislamu yakiwemo hayo waliyo nao wao. Ikiwa wataendelea na hayo waliyo nayo itabidi kwa madhambi hayo mkate uhusiano nao kwani kufanya hivyo huenda wakatia fahamu na kurudi katika njia ya sawa.



Na Allaah Anajua zaidi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…