Kupenda Futboli Ni Vibaya? Hukmu Ya Wanaoacha Swalaah Kwa Ajili ya Kutazama Mpira Wa Miguu?
Maswali: Mchanganyiko


SWALI:



Assalamu Aleykum Warrahmatullahi Wabarakatu.




Naomba kuuliza swali. Swali langu ni kama ifuatavyo; jee ni haramu kucheza, kuangaliya ama kuwa shabiki mkuu wa football? Sababu ya kuuliza swali hili ni kutaka kupata uhakika kuhusu swali hili. Kuna baadhi ya watu ambao wanapoteza wakati wao wote wakiwa wanaangaliya mpira na huku umewadiya wakati wa swala lakini hawaendi kuswali kwa sababu hawataki kupitwa na mchezo huwo.

Tafadhali nijibuni swala hili ili niweze kujadiliyana nao, shukran. Wa jazakummullahul kheir.





JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.



Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kupenda mpira au mchezo mwengine wowote ule.

Hakuna uharamu wowote kwa mtu kucheza mchezo wowote ule ambao unakwenda sambamba na shari’ah, kuangaliya au kuwa shabiki kwa mipaka ya Uislamu.




Tufahamu kuwa Uislamu ni Dini ya vitendo wala sio ya mawazo matupu. Inawachukulia wanaadamu kama wanaadamu. Kwa ajili hiyo, Uislamu ni Dini na dunia. Kuna namna nyingi ya michezo waliowekewa Waislamu na Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ili kujifurahisha na kujipumzisha, nayo kwa wakati huo yanaitayarisha nafsi zao kuweza kufanya ‘Ibaadah zao na wajibu wao kwa nashati kubwa zaidi na hima kubwa zaidi. Nyingi katika hizo ni Riyadha zinazowazoweza kupambana na mazito, na kuwatayarisha kwa vita vya Jihaad na kupigana kwa ajili ya Allaah Aliyetukuka. Katika michezo iliyo halali ni kama ifuatayo:



1. Mbio, naye Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anashindana na mkewe ‘Aa’ishah (Radhiya Allaahu ‘anha).

2. Miereka, naye Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alishindana na Rukaana na kumshinda (Abu Daawuud na Ahmad).

3. Kurusha mishale. Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliwapita Maswahaba (Radhiya Allaahu ‘anhum) wakishindana kurusha mishale, naye akawahimiza kwa kuwaambia: “Rusheni nami ni pamoja nanyi” (al-Bukhaariy).

4. Kucheza na mikuki.

5. Kupanda farasi.

6. Kuogelea pia kumehimizwa sana.

7. Kuwinda kwa kutumia ala kama mishale, mikuki na kwa sasa bunduki.



Uislamu pia umeweka kanuni za kijumla ya kuufanya mchezo wowote ule kuwa halali au haramu. Kanuni hizo ni kama zifuatazo:



1. Uhalali unategemea manufaa au hasara inayopatikana. Ikiwa manufaa ni makubwa zaidi mchezo utakuwa halali na lau itakuwa kinyume chake basi utakuwa ni haramu.

2. Mchezo wowote wenye kamari unakuwa ni haramu.

3. Isicheleweshwe Swalah kutoka kwa wakati wake kwa ajili ya mchezo wowote ule. Hatari hiyo inakuwa kubwa kwa kupoteza wakati na kujishughulisha watu kukosa kutekeleza wajibu wao.

4. Mchezaji ahifadhi ulimi wake wakati wa kucheza, asitukane na kutokwa na maneno machafu.

5. Mchezo kama wa ngumi ni mchezo uliokuwa haufai kwani kuna kudhuriuana uso ambako kumekatazwa na Mtume wetu (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na kuleta madhara ya ubongo na mifano ni mingi.

6. Mavazi yalingane na stara ya iliyowekwa kishari’ah. Haifai kuvaa vikaptula vinavyonyesha mapaja ya mwanaume kama ilivyo kwenye mpira wa miguu na mbio na pia nguo za kubana zenye kuonyesha maungo ya ndani kama kwenye michezo ya kukimbia, kuogelea, michezo ya viungo kama jimnastiki (sarakasi) n.k.

7. Wanawake hawakatazwi kucheza maadam wako wenyewe, na wawe wamevaa stara za kishari’ah. Hata hivyo wanawake haiwapendezei kucheza michezo ya nguvu iliyo kinyume na maumbile yao kama mieleka, mpira wa miguu na mingine ambao wanawake wa siku hizi wameanza kuiga.



Ikiwa moja katika masharti yaliyo juu haikutimizwa, basi mchezo huo utakuwa ni haramu. Hivyo, uhalali na uharamu wa kushabikia mchezo wa mpira itagemea na vigezo vilivyo juu. Na hapo umeuliza kwa uwazi kabisa kuwa watu wanaoshabikia mchezo huo huwa wanakosa Swalah, hivyo, kwa hali hiyo kunafanya kucheza kwa wakati huo na kutazama au kushabikia kuwa haramu.



Na Allaah Anajua zaidi
 
Meno Ya Dhahabu Ni Haramu Kubandika?
Maswali: Mchanganyiko



SWALI:

asalam alaikum, suali langu ni hili:mtu akibandika meno ya dhahabu ni haramu? Je, akisuali nayo swala itakubaliwa



JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako hili kuhusu mas-ala ya kutia meno ya dhahabu. Hakika ni kuwa meno ya dhahabu yanaweza kuwekwa na Muislamu kwa dharura inayokubalika kisheria. Hii ni kwa mujibu wa Hadiyth iliyosimuliwa na Arfajah bin As‘ad: Abdur-Rahmaan bin Tarafah alisema kuwa babu yake Arfajah ibn As‘ad (Radhiya Allaahu ‘anhu) alikatwa pua yake katika vita vya Kilaab, hivyo akatia pua ya fedha, lakini ikaanza kunuka. Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimuamuru atie pua ya dhahabu (Abu Daawuud, at-Tirmidhiy na an-Nasaa’iy). Hadiyth hii inatuonyesha jinsi Sheria yetu Tukufu inavyotazama maslahi ya mwanadaamu kwa kiwango kikubwa sana ili mwanadamu kama huyo asiwe ni mwenye kudhurika kwa chochote. Kwa minajili hiyo hata kile kitu ambacho ni haramu kikapewa ruhusa ili kusaidia kuleta nafuu kwa mwanadamu.

Kwa hiyo, ikiwa ipo dharura ya kisheria kutia jino la dhahabu kutakuwa hapana shida yoyote ile.

Na Allaah Anajua zaidi
 
Mwanamume Kuvaa Pete
Maswali: Mchanganyiko







SWALI:

Assalaam aleykum

KUVAA PETE: NINGEPENDA KUPATA JAWABU LA SWALA HILI "JEE, MWANAMME KUVAA PETE INAKUBALIKA KATIKA UISLAM"










JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Shukrani kwa suala lako hili ambalo huenda likawa linawatatiza wengi au baadhi.

Mwanamme Muislamu hakatazwi kuvaa pete ingawa si jambo la Sunnah kama wanavyodhania wengi kwa kujua kuwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa Sallam) alikuwa akivaa. Ni jambo lenye kuruhusiwa tu ikiwa mtu anataka kuvaa. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa Sallam) alikuwa havai kwa mapambo bali alikuwa akiitumia kama muhuri wake katika barua alizokuwa akiwaandikia watu mbalimbali.

Labda swali linaweza kujitokeza, je Muislamu mwanamme anafaa kuvaa pete aina gani au yoyote? Jibu la haraka ni: Hapana! Dalili yetu kuhusu hili ni zifuatazo:



1- Amesimulia Anas bin Maalik (Radhiya Allaahu ‘anhu) kuwa pete ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ilikuwa ya fedha yenye kijiwe cha Habasha ndani yake (Muslim).

2. ¨ Anas (Radhiya Allaahu ‘anhu) anahadithia tena: “Wakati mmoja Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliandika barua au alikuwa na wazo la kuandika barua. Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliambiwa kuwa wafalme hawaandiki barua mpaka ziwe na muhuri. Kwa hiyo, Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alifanya pete ya fedha iliyoandikwa ‘Muhammad RasuluLlaah – Muhammad Mjumbe wa Allaah’. Kama ninaangalia mng’aro wake mweupe mkononi mwa Mtume” (al-Bukhaariy).

3. Amesimulia Ibn ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘anhuma) kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa Sallam) alikuwa na pete ya fedha ambayo alikuwa anaivaa. Baadaye ilivaliwa na Abubakar, kisha ‘Umar na baadaye ‘Uthmaan mpaka ilipoanguka katika kisima cha Aris (al-Bukhaariy).

Pete isiyofaa kwa Muislamu mwanamme kuvaa ni ya shaba ya njano, chuma na dhahabu. Makatazo hayo ni kwa mujibu wa Hadiyth za bwana Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa Sallam).

1. Anasimulia Buraydah bin al-Haasib (Radhiya Allaahu ‘anhu) kuwa mtu mmoja alikuja kwa Mtume (Swalla ALlaahu ‘Alayhi wa aalihi wa sallam) akiwa amevaa pete ya shaba ya njano. Alimwambia: “Kwa nini nasikia harufu ya masanamu kwako?” Hivyo, aliitupa hiyo pete, akaja baadaye akiwa amevaa pete ya chuma. Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa Sallam) alimwambia: “Vipi nakuoa umevaa mapambo ya watu wa motoni?” Yule mtu aliitupa (hiyo pete) kisha aliuliza: “Ewe Mtume wa Allaah! Ni kifaa gani nitumie?” Akasema: “Tengeneza pete ya fedha, lakini wizani wake usizidi mithqaal moja” (Abu Daawuud).

2. Al-Baraa’ bin ‘Aazib (Radhiya Allaahu ‘anhu) amesema: Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ametuamuru mambo saba na ametukataza saba. … na ametukataza kuvaa pete ya dhahabu …”

(al-Bukhaariy na Muslim).

Tanbihi: ikiwa pete yako ya fedha ina maandishi ya jina la Allah au jina lolote katika majina ya Allaah inafaa unapoingia chooni uwe ni mwenye kuivua na kuiacha nje kama alivyokuwa akifanya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa Sallam).

Na Allah Anajua zaidi
 
Nifanye Nini Ili Niweze Kuipata Simu Yangu Iliyoibiwa Na Pia Iwe Fundisho Kwa Wezi Bila Ya Mimi Kuingia Katika Shirki?
Maswali: Mchanganyiko
SWALI

Asalaam alaykum warahmatulahi wabarakatuh mimi ni muislam nasoma chuo cha ualimu mhonda kiko morogoro, nimeibiwa simu ya mkononi ambayo niliipenda sana na niliinunua kwa gharama ya shilingi laki mbili na elfu ishirini, sasa simu hii imeibwa na mwanachuo mwenzangu hapa chuoni japo simjui hasa ni nani.

wako watu walionishauri niende kwa waganga wa kienyeji nikaona ni moja ya madhambi makubwa ambayo allah ameyakemea sasa nauliza nisome dua gani au nifanyeje ili simu yangu irudi na pia iwe fundisho kwani kuna wimbi la wizi sana. Nawapongeza kwa kazi nzuri mnayofanya, na ninajivunia alhidaya.

ALHIDAYA INAWAKUTANISHA WAISLAMU



JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.





Shukrani kwa swali lako kuhusu ufanye nini ili uipate tena simu yako uipendayo.

Hakika ni kuwa hakuna kisomo chochote ambacho Muislamu anaweza kusoma ili kukirudisha kitu chake kilichoibiwa.


Kitu cha pekee ambacho unaweza kufanya ni kumuomba Allaah Aliyetukuka kwa uwezo wake ulio mkubwa Akusahilishie kuipata kutoka kwa aliyeiba kwa njia Anayoitaka Yeye Mtukufu. Na jingine ni kumuombea aliyeiiba kwa kuwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Du’aa ya aliyedhulumiwa hairudi”.


Mbali na hayo, unatakiwa kama Muislamu uchukue tahadhari za ziada katika kuchunga mali zako. Tunamuomba Allaah Aliyetukuka Akufanye ni mwenye kuipata simu yako.




Na Allaah Anajua zaidi
 
Viumbe Gani Wameishi Duniani Bila Kukaa Matumboni Mwa Mama Zao?
Maswali: Mchanganyiko
SWALI:



Assalam aleikum Warmatullah Wabarakatu me ningependa kufahamu ni viumbe gani wameishi duniani bila ya kukaa matumboni mwa mama zao? WABILLAH TAWFIQ





JIBU:



Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.





Shukrani zetu kwa swali lako kuhusu viumbe walioishi duniani bila kukaa kwenye matumbo ya mama zao. Miongoni mwao ni:







Nabii Aadam (‘Alayhis Salaam).



Hawwaa, mke wa Nabii Aadam (‘Alayhis salaam).



Ngamia wa Nabii Shu’ayb (‘Alayhis Salaam).



Ndege waliokuja kumpiga Abraha na jeshi lake waliokuwa wamekuja Makkah kuvunja al-Ka’bah.








Na Allaah Anajua zaidi
 
Tofauti Ya Miezi Ya Kiislamu (Hijriyyah) Na Ya Miladi Zipi Sifa Zake?



Alhidaaya.com







SWALI:



Ni kwa nini miezi ya kiislamu inakuwa sanjari na miezi ya kimagharibi lakini inakuwa tofauti katika muda.

Naomba nakala ya kalenda iliyo na mchanganyiko wa miezi ya pande zote. Zipi sababu za kuitwa mwezi fulani na kisa cha kila mwezi au siku katika mwezi fulani, mfano: siku ya 9 na 10 mfungo nne nilipata kusimuliwa kuwa ndiyo Bani Israil waliangamizwa kwa kumuasi allah (Subhanahu wa Ta'ala).

Kwa nini kila mwezi una sifa zake na hakuna mfanano wa sifa na kama zipo ni zipi?

ALLAH (Subhanahu wa Taala) awalipe kwa yote myatendayo na wajaze kheri. In shaa Allah.





JIBU:



AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.





Tutajaribu kufafanua kwa kadiri tulivyolifahamu swali lako.



Mwanzo inatafaa tuelewe kuwa kuna tofauti ya msingi baina ya miezi ya Kiislamu na mingine. Miezi ya Kiislamu inafuatana na mwandamo wa mwezi ambao kila mwezi unakuwa na siku 29 au 30 ilhali miezi ya Kimagharibi inafuata jua, hivyo kufanya siku zake kuwa 28, 29 kwa Februari na kawaida ni 30 au 31. Kwa ajili hiyo, mwaka wa Kiislamu unakuwa na takriban siku 11 kidogo kuliko mwaka wa Kimagharibi.



Ama kuhusu miezi ya Kiislamu, Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Ndiye Aliyeifanya kuwa kumi na mbili, minne ikiwa ni mitukufu. Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema:



إِنَّ عِدَّةَ الشُّهُورِ عِندَ اللَّـهِ اثْنَا عَشَرَ شَهْرًا فِي كِتَابِ اللَّـهِ يَوْمَ خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ مِنْهَا أَرْبَعَةٌ حُرُمٌ ۚ ذَٰلِكَ الدِّينُ الْقَيِّمُ ۚ فَلَا تَظْلِمُوا فِيهِنَّ أَنفُسَكُمْ ۚ وَقَاتِلُوا الْمُشْرِكِينَ كَافَّةً كَمَا يُقَاتِلُونَكُمْ كَافَّةً ۚ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ مَعَ الْمُتَّقِينَ﴿٣٦﴾

Hakika idadi ya miezi mbele ya Allaah ni kumi na mbili katika hukmu ya makadirio ya Allaah, (tangu) siku Aliyoumba mbingu na ardhi. Kati ya hiyo, (iko miezi) minne mitukufu. Hivyo ndiyo Dini iliyo nyoofu. Basi msijidhulumu humo nafsi zenu (kwa kufanya maasi), na piganeni vita na washirikina wote kama wao wanavyokupigeni vita nyote. Na jueni kwamba Allaah Yu Pamoja na wenye taqwa. [At-Tawbah: 36]



Ama kuhusu nakala za kalenda kukutumia kwa njia ya mtandao inakuwa si wepesi kwani hizo zinachapishwa na kuuzwa katika miji na nchi tofauti. Kinachotakiwa ni wewe kwenda katika maduka yanayouza vitabu vya Kiislamu na kununua moja ili uweze kuwa nayo na kutazama unayoyahitaji. Au unaweza kuipata katika mitandao.



Ama kuhusu sababu ya kuitwa majina ya miezi ni Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Mwenye kujua zaidi kwani Yeye haulizwi Anayofanya, sisi ndio wenye kuulizwa.



Ama kuhusu siku zina tarehe na majina yake zilizopatiwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na Rasuli Wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Mfano ni:



1-Tarehe 10 wala sio tisa ya Mfungo Nne (yaani Al-Muharram). Siku hiyo inaitwa ‘Aashuraa nayo ni kwa ajili ya Bani Israaiyl wakati wa Nabiy Muwsaa (‘Alayhis Salaam) waliokolewa na Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) sio kuangamizwa kama ulivyo sema. Kwa ajili ya kuokolewa huko, wakawa wanafunga siku hiyo kama kutoa shukran kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa). Na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) naye akatuongezea tarehe tisa ambayo inayojulikana kama Taasuaa’ ili tufunge siku hizo mbili tutofautiane na Mayahudi.



2-Tarehe 9 ya Dhul-Hijjah inajulikana kama siku ya ‘Arafah, kwani katika siku hiyo Mahujaji wanasimama katika wangwa wa ‘Arafah ili kujikurubisha kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na kutimizia nguzo ya Hajj.



Miezi ya Kiislamu ina sifa tofauti kwa kupatiwa sifa hizo na Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na Rasuli Wake, ima kwa sababu ya kufanywa ‘Ibaadah miongoni mwa ‘Ibaadah kwa sababu nyingine yoyote ile.



Na Allaah Anajua zaidi
 
Vyuo Gani Vya Kwenda Kusoma Dini Nje?
Maswali: Mchanganyiko
Vyuo Gani Vya Kwenda Kusoma Dini Nje



www.alhidaaya.com





SWALI:



Assalamu Aleikum,

I will be coming for a holiday in Mombasa Kenya on the ....... for two months. Is there any place that you reccommend I could go and learn more about Islam for two these two months that i will be in Mombasa. I can read the Quran fluently but i need to learn the tajweed, Arabic language and other courses of Islam. My brother wants to go to Darul Mustafa in Tarim, Yemen for his Islamic Studies with Sh. Habib Ali Al Jifri, would you reccomend such a place or is there an alternative e.g. in Madina or Makkah.

Assalamu Aleikum





JIBU:



AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.





Kwenda kwako Kenya na kutaka kusoma 'ilmu tofauti ikiwemo mada ya lugha ya Kiarabu ni jambo zuri lakini muda wenyewe ni mfupi.



Kenya kuna ndugu wengi wanaofuata Manhaj Sahihi ambao unaweza kuulizia na ukaelekezwa kwao; cha msingi ni kuulizia nani wanaofuata na kulingania hii Dini kwa kufuata Manhaj ya Salafus Swaalih (Mwenendo wa Wema Waliotangulia kuanzia Maswahaba, Matabi'iyna na Waote waliowafuata wao kwa wema).



Nasaha zetu ni kuwa usiende kusoma huko kwenye huo ulichoeleza cha huyo mtu huko Tarim, kwani hao uliowataja ni Masufi wakubwa tena Wanachuoni wakubwa wameshatahadharisha kuwa ni watu wa bid’ah na matamanio na hata mafundisho yao yana aina za ushirikina na ghuluw (uvukaji mpaka wa Dini).



Hivyo, tunakunasihi ujihadhari na kaa mbali na vyuo kama ulivyovitaja na watu wake ambao wanamzulia Mtume na kueneza mafunzo ya upotofu.



Sehemu bora ya kusoma ni kwenye vyuo vya Kisalafi popote vilivyopo duniani, na sehemu zingine za kusoma ni Makkah na Madiynah, katika miji hiyo miwili mitukufu mtu atapata fadhila zaidi ya kufanya ‘Ibaadah katika Misikiti Mitukufu ambamo thawabu zake ni maradufu na pia kupata darsa za Mashaykh wakubwa humo ndani ya Misikiti hiyo mitakatifu mbali na masomo ya kawaida.





Na Allaah Anajua zaidi
 
Afanye Nini Ili Allaah Amsamehe Dhambi Na Aweze Kujikuribisha Kwake?
Maswali: Taqwa - Tazkiyyah


SWALI:

NAOMBA MUNIJUILISHE KITU GANI NIFANYE ILI NIWEZE KUNIKURUBISHA KWA MOLA WANGU NA ANIGHUFIRIE DHAMBI ZANGU. AU AMALI GANI NIFANYE ILI NIPATE HAYO



JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Kuhusu kufutiwa dhambi zako madamu una nia ya kutubia, jambo hili halina shaka kabisa kuwa lina uwezekano kwani dalili zake nyingi mno katika Qur-aan na Sunnah. Maswahaba walitia shaka kuhusu madhambi yao waliyotenda kabla ambayo ni makubwa zaidi kuliko yako nayo ni kuwa walikuwa ni wenye kumshirikisha Allaah kabla ya Uislamu. Lakini walipotaka ufafanuzi kuhusu madhambi yao, Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Akateremsha Aayah ifuatayo:

(( قُلْ يَا عِبَادِيَ الَّذِينَ أَسْرَفُوا عَلَى أَنفُسِهِمْ لَا تَقْنَطُوا مِن رَّحْمَةِ اللَّهِ إِنَّ اللَّهَ يَغْفِرُ الذُّنُوبَ جَمِيعًا إِنَّهُ هُوَ الْغَفُورُ الرَّحِيمُ))

((Sema: Enyi waja Wangu waliojidhulumu nafsi zao! Msikate tamaa na Rahma ya Allaah. Hakika Allaah Husamehe dhambi zote. Hakika Yeye ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu)) [Az-Zumar: 53]



Tafadhali ingia katika kiungo kifuatacho upate maelezo mengi mno kuhusu Tawbah ili upate kuridhika nafsi yako ikiwa utatubia kweli na uweze kubakia katika radhi za Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala):

Tawbah

Ama kuhusu kujikurubisha kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala), ni amali nyingi kabisa zisizokuwa na hesabu. Jambo la kwanza kabisa ni kutimiza Swalah zako tano kila siku. Kiungo kifuatacho pia kina maelezo marefu yatakayokupa umuhimu, fadhila na faida za Swalah, ambayo pindi ukiitimiza ipasavyo utaweza kuzidi kujiepusha na maouvu.

Swalah

Kisha fanya mema mengi ambayo yatafuta maovu yako na pia yatazidi kukurubisha kwa Mola wako Mtukufu kwani mema hufuta maovu kama Anavyosema Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala):

((إِنَّ الْحَسَنَاتِ يُذْهِبْنَ السَّيِّئَاتِ ذَلِكَ ذِكْرَى لِلذَّاكِرِينَ))

((Hakika ya mema huyaondosha maovu)) [Huud: 114]

Amka usiku katika thuluthi ya mwisho ya usiku uswali Tahajjud na umuombe Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Akusamehe madhambi yako na Akuongoze.

Jishughulishe na kumkumbuka Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) kila mara asubuhi na jioni, kwa kusoma Qur-aan, kusikiliza mawaidha, kutafuta elimu ya Dini yako, yote haya yatakupa faida ya dunia na Akhera. Elimu na manufa yote haya yanapatikana Alhidaaya, tembelea na fuata nasaha zetu ili Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Akuhidi katika njia iliyonyooka. .

Tunatumai kwamba utafuata nasaha zetu za dhati hizo na tunakuombea at-Tawfiyq na uongofu kutoka kwa Mola Mtukufu.

Na Allaah Anajua zaidi
 
Maswali: Taqwa - Tazkiyyah
Akiokota Tunda Shambani Mwa Mtu Ni Halaal Kwake?



www.alhidaaya.com









SWALI:



Masheikh wangu wa alhidaaya nataka muniwekee bayana hasa juu ya hili suali langu kwani linanipa mashaka sana juu ya kutaka kulifahamu na kuweza kuliwacha au kuendelea nalo. Hii ni kwa sababu baadhi ya masheikh ambao tayari nimewafika baadhi yao wanasema yakuwa si halali na wengine hulijuzisha kwa kusema kwamba (Milatul-biladi sharia). Swali: Mtu kupita katika shamba la watu na akakuta matunda yameanguka je, anayohaki ya kuchukua na kula hali ya kua ni halali kwake matunda hayo au si halali? Upande wowote uwao, naomba kupatiwa ushahidi kutoka katika kitabu na sunna za Mtume (s.a.w)





JIBU:



AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho





Kwanza kabla hatujajibu swali lako, tunakukumbusha kuwa unapoandika jina la Allaah au Nabiy, usifupishe mbele yake kwa kuweka (S.W.) au (S.A.W.) kama ilivyozoelekea na wengi, bali andika kwa kirefu maneno hayo bila ya kuyafupisha. Andika (Subhaanahu wa Ta'aalaa) baada ya kumtaja Allaah, na andika Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) au (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) baada ya kumtaja Nabiy. Hivyo ndivyo inavyopaswa, na ndio heshima zaidi na utukufu na ndivyo inavyotamkwa na si kama inavyofupishwa na wengi kimazoea au kivivu. Pia hiyo ni ‘ibaadha na ‘ibaadah inatakiwa ifanywe kwa namna iliyofundishwa na haifai kugeuza, kuongeza au kupunguza. Hali kadhalika Maswahaba walikuwa wakiandikiana barua na hakuna aliyekuwa akikatisha Salaam, wala kumswalia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) wala kumtukuza Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwenye barua zao. Tuige na tufuate nyendo zao tusalimike.





Hakika inayokubaliwa na kila mmoja wetu ni kuwa shamba si la anayetunda tunda lililoanguka bali ni la mtu mwengine. Lau lingekuwa ni shamba lake basi hangehitaji ruhusa kwa sababu ni miliki yake.



Ikiwa kitu si chako kisheria na hata kiakili huwezi kuchukua ila upawe idhini na mwenye shamba. Kwa hali hiyo ya ki Shariy’ah haitakuwa halali kwako kuchukua tunda lililoanguka katika shamba la mtu mwengine.



Hata hivyo, 'Urf (ada na desturi) ni miongoni mwa chimbuko la Shariy’ah katika Dini yetu tukufu. Ikiwa inafahamika na ni ada katika mji au kijiji unachoishi kuwa yafaa kwako kuchukua tunda lililoanguka basi kutakuwa hakuna tatizo lolote unapofanya hivyo, kwani hiyo itakuwa ni ada isiyopingana na Shariy’ah yetu.





Na Allaah Anajua zaidi
 
Alishika Dini Alipokuwa Hana Kazi Sasa Hana Muda Wa Kufanya ‘Ibaadah Na Anapotoa Nasaha Anaonekana Mjeuri
Maswali: Taqwa - Tazkiyyah


SWALI:



Assalamu aleikum warahmatullahi wabarakatuh - rehma za allah subhanahu wataala ziwe juu yenu. amin.



mimi ni mwanamke, nlikua nimeshika dini sanaa wakati nlipokua sijapata kazi, saivi nimepata kazi najitahidi nipate muda wa kusoma quran na kufanya ibada zangu nyingi lakini naposhika quran au kutaka kusoma tasbihi naingiwa na usingizi..wallah najitahidi kuongea na watu maneno mazuri anayopenda allah subhanahu wataala bado naambiwa mie mjeuri kwa kua watu wengi hawaapendi uwaendee kinyume na wanavotaka wao uende...nalia na naumia sana kuwa mbali na dini yangu na najiona nateseka sana sijui nifanyeje!

nataka niwe nauliza maswali yangu humu kwa wingi lakini yanachelewa kujibiwa basi hua sina mwengine wa kumwambia please nawaomba musichelewe kunijibu ndugu zanguni napata shida sana...ahsante.







JIBU:



Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.







Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kushika Dini wakati ambao ulikuwa huna kazi na kudorora katika ‘Ibaadah baada ya kupata kazi.

Awali ya yote tunasikitika kuona maswali yako yanachelewa kujibiwa lakini hilo liko nje ya uwezo wetu kwani maswali yanayokuja ni mengi. Na mfumo wetu wa kujibu ni kuanza na yale yaliyoletwa mwanzo kabla ya kuja kwa mengine. Huenda kuwa ulipotuma yalikuwa mengi na hatuwezi kuanza na yaliyochelewa na kuacha yaliyotumwa mwanzo. Kwa kila hali, tutajitahidi kufanya bidii ili tuweze kuyajibu kwa muda unaofaa, InshaAllaah.



Ama tukija katika swali lako ni kuwa kwa kila hali mwanaadamu na hasa Muislamu huwa anajaribiwa na Allaah Aliyetukuka kwa mitihani tofauti. Kukosa kazi ni mtihani na hivyo hivyo kupata kazi. Hata hivyo, sisi Waislamu tunatakiwa katika hali yoyote ile tuwe tunashikamana na Dini yetu kama inavyotakiwa. Ndio Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema:

“Ajabu kwa mambo ya Muumini, hakika mambo yote kwake ni kheri. Na hilo halipatikani ila kwa Muumini: Anapopatikana na furaha hushukuru na hiyo ikawa kheri kwake na anapopatikana na madhara husubiri, na hilo likawa kheri kwake” (Muslim).



Kila mtu tufahamu kuwa hupata Imani kwa kadiri ya Imani yake, na katika daraja hiyo ni Mitume na Manabii (‘Alayhimus Salaam) ambao mitihani yao ni mikubwa zaidi. Ni ada kwa wengi wanapokuwa hawana kazi au ni masikini kufanya ‘Ibaadah kwa wingi na kumuomba Allaah Aliyetukuka Awaondolee shida hiyo lakini pindi wanapopata kazi au kutajirika, basi humsahau Allaah moja kwa moja.

Jambo hili hutokea kwa sababu ya ukosefu wa Ikhlaasw na na Niyah njema. Mara nyingi unamuomba Allaah Aliyetukuka na kumuabudu ukingoni, mguu mmoja kwa Allaah na mwengine kwa Shaytwaan. Kwa ajili hiyo, Allaah Aliyetukuka Akatuambia:

“Na katika watu wapo wanaomuabudu Allaah kwa ukingoni. Ikimfikia kheri hutulia kwayo, na ukimfikia msukosuko hugeuza uso wake. Amekhasiri dunia na Akhera; hiyo ndiyo khasara iliyo wazi” (Al-Hajj 22: 11).



Kazi inatakiwa isimtoe mtu katika kufanya ‘Ibaadah. Ikiwa itakuwa hivyo, itakuwa afadhali kwa Muislamu aache kazi kuliko kuwa na kazi ambayo itampatia hasara hapa duniani na Kesho Akhera. Allaah Aliyetukuka Anatuzungumzia kuhusu Waumini wa kweli kweli:

“Watu ambao biashara wala kuuza hakuwashughulishi na kumdhukuru Allaah, na kushika Swalah, na kutoa Zakaah. Wanaikhofu Siku ambayo nyoyo na macho zitageuka” (An-Nuur 24: 37).

Na Akasema,

“Na itakapokwisha Swalah, tawanyikeni katika nchi mtafute fadhila za Allaah, na mkumbukeni Allaah kwa wingi ili mpate kufanikiwa” (Al-Jumu‘ah 62: 10).



Kwa ajili ni lazima ufanye bidii na juhudi kubwa ya kuweza kufanya ‘Ibaadah, kwani kazi yako haitakuwa na baraka ikiwa hutamkumbuka Allaah Aliyetukuka. Kuongea na watu ni vizuri, hata hivyo unatakiwa ujirekebishe kwa kutekeleza ‘Ibaadah. Na njia rahisi ya kuweza kudumu katika ‘Ibaadah ni kuwa na marafiki wema, wazuri na walioshika Dini; kuwa na wakati wa kusoma Qur-aan, kujua maana yake na kujaribu kutekeleza. Na ukianza kusoma usisahau kujilinda kwa Allaah Aliyetukuka kutokana na Shaytwaan aliyelaaniwa. Jaribu kuleta Adhkaar za asubuhi na jioni na kabla ya kumpatia Muislamu mwenzio mawaidha, mwanzo jaribu kabisa kujirekebisha na kulifanyia kazi hilo ambalo una kasoro nalo. Kiburi na ujeuri vinaletwa na kuhisi kuwa wewe ni mkubwa wa daraja na hakuna akufikiyae kwa daraja na cheo. Kuondoa kiburi na ujeuri, jaribu kukaa na masikini, kuzungumza nao na wale ambao hawana kazi kwani wakati mmoja ulikuwa pamoja nao na ulikuwa na adabu aliyotufundisha Allaah Aliyetukuka na Mtume Wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).



Kuumia kwa kuambiwa wewe ni mjeuri na ikiwa si hivyo, hilo ni jambo la kawaida. Hata hivyo, ukitazama kuumia kwako pia angalia jinsi gani Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alivyoudhiwa mpaka akaambiwa kuwa yeye ni mchawi, mwenda wazimu na kadhalika.

Huo ni mtihani ikiwa huna sifa hiyo na ikiwa unayo basi fanya bidii ujirekebishe kabisa kuhusu hilo. Allaah Aliyetukuka Anatuambia:

“Hapana shaka Tutakujaribuni kwa chembe ya khofu, na njaa, na upungufu wa mali na watu na matunda. Na wabashirie wanaosubiri” (Al-Baqarah 2: 155).



Katika mtihani huo wako unatakiwa usubiri na uzidishe ‘Ibaadah ili upate kushinda na kufaulu.



Tunakuombea kwa Allaah Aliyetukuka na wewe nawe zidi kuomba ili upate kuupita mtihani ulio nao na uweze kurudi katika ‘Ibaadah.



Na Allaah Anajua zaidi
 
UJUMBE WA LEO :

“Watu ambao biashara wala kuuza hakuwashughulishi na kumdhukuru Allaah, na kushika Swalah, na kutoa Zakaah. Wanaikhofu Siku ambayo nyoyo na macho zitageuka” (An-Nuur 24: 37).
 
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn



باب فضل الجوع وخشونة العيش والاقتصار عَلَى القليل من المأكول والمشروب والملبوس وغيرها من حظوظ النفس وترك الشهوات

056-Mlango Wa Fadhila za Kuwa na Njaa na Maisha ya Kujinyima, na Kukusuru Kichache Katika Chakula na Vinywaji na Mavazi na Kujitenga na Maisha ya Fakhari na Kuacha Matamanio





Alhidaaya.com





قَالَ الله تَعَالَى:

فَخَلَفَ مِن بَعْدِهِمْ خَلْفٌ أَضَاعُوا الصَّلَاةَ وَاتَّبَعُوا الشَّهَوَاتِ ۖ فَسَوْفَ يَلْقَوْنَ غَيًّا ﴿٥٩﴾ إِلَّا مَن تَابَ وَآمَنَ وَعَمِلَ صَالِحًا فَأُولَـٰئِكَ يَدْخُلُونَ الْجَنَّةَ وَلَا يُظْلَمُونَ شَيْئًا ﴿٦٠﴾

Wakafuata baada yao waovu, walipoteza Swalaah na wakafuata matamanio; basi watakutana na adhabu motoni. Isipokuwa yule aliyetubu na akaamini na akatenda mema; basi hao wataingia Jannah na wala hawatodhulumiwa chochote. [Maryam: 59-60]



فَخَرَجَ عَلَىٰ قَوْمِهِ فِي زِينَتِهِ ۖ قَالَ الَّذِينَ يُرِيدُونَ الْحَيَاةَ الدُّنْيَا يَا لَيْتَ لَنَا مِثْلَ مَا أُوتِيَ قَارُونُ إِنَّهُ لَذُو حَظٍّ عَظِيمٍ ﴿٧٩﴾ وَقَالَ الَّذِينَ أُوتُوا الْعِلْمَ وَيْلَكُمْ ثَوَابُ اللَّـهِ خَيْرٌ لِّمَنْ آمَنَ وَعَمِلَ صَالِحًا وَلَا يُلَقَّاهَا إِلَّا الصَّابِرُونَ ﴿٨٠﴾

Akawatokea watu wake katika pambo lake. Wale wanaotaka uhai wa dunia wakasema: Ee laiti tungelipata mfano wa yale aliyopewa Qaaruwn, hakika yeye ana bahati kuu. Na wale waliopewa elimu wakasema: Ole wenu! Thawabu za Allaah ni bora zaidi kwa yule aliyeamini na akatenda mema. Na wala hazipati isipokuwa wenye kusubiri. [Al-Qaswasw: 79-80]



ثُمَّ لَتُسْأَلُنَّ يَوْمَئِذٍ عَنِ النَّعِيمِ ﴿٨﴾

Kisha bila shaka mtaulizwa Siku hiyo kuhusu neema. [At-Takaathur: 8]



مَّن كَانَ يُرِيدُ الْعَاجِلَةَ عَجَّلْنَا لَهُ فِيهَا مَا نَشَاءُ لِمَن نُّرِيدُ ثُمَّ جَعَلْنَا لَهُ جَهَنَّمَ يَصْلَاهَا مَذْمُومًا مَّدْحُورًا ﴿١٨﴾

Yeyote anayetaka (starehe za dunia) ipitayo upesi upesi Tunamharakizia humo Tuyatakayo, na kwa Tumtakaye. Kisha Tutamjaalia Jahannam aingie na kuungua hali ya kuwa mwenye kushutumiwa na kufukuziliwa mbali. [Al-Israa: 18]









Hadiyth – 1

وعن عائشة رضي الله عنها ، قالت : مَا شَبعَ آلُ مُحَمّد صلى الله عليه وسلم مِنْ خُبْزِ شَعِيرٍ يَوْمَيْنِ مُتَتَابِعَيْنِ حَتَّى قُبِضَ . متفقٌ عَلَيْهِ .

وفي رواية : مَا شَبعَ آلُ محَمّد صلى الله عليه وسلم مُنْذُ قَدِمَ المَدِينَةَ مِنْ طَعَامِ البُرِّ ثَلاثَ لَيَالٍ تِبَاعاً حَتَّى قُبِضَ.

Kutoka kwa 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) amesema: "Haikushiba familia ya Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) mkate wa shayiri siku mbili mfululizo hadi ameaga dunia (hali ilikuwa hivyo)." [Al-Bukhaariy na Muslim].

Na katika riwaayah nyingine: "Haikushiba familia ya Muhammad (Sawalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuanzia afike Madiynah kwa chakula cha ngano kwa siku tatu mfululizo mpaka ameaga dunia."





Hadiyth – 2

وعن عروة ، عن عائشة رضي الله عنها ، أنّها كَانَتْ تقول : وَاللهِ ، يَا ابْنَ أُخْتِي ، إنْ كُنَّا نَنْظُرُ إِلَى الهِلاَلِ ، ثُمَّ الهِلالِ : ثَلاَثَةُ أهلَّةٍ في شَهْرَيْنِ ، وَمَا أُوقِدَ في أبْيَاتِ رسول الله صلى الله عليه وسلم نَارٌ . قُلْتُ : يَا خَالَةُ ، فَمَا كَانَ يُعِيشُكُمْ ؟ قالت : الأَسْوَدَانِ التَّمْرُ وَالمَاءُ ، إِلاَّ أنَّهُ قَدْ كَانَ لرسول الله صلى الله عليه وسلم جِيرَانٌ مِنَ الأَنْصَارِ ، وكَانَتْ لَهُمْ مَنَائِحُ وَكَانُوا يُرْسِلُونَ إِلَى رسول الله صلى الله عليه وسلم مِنْ ألْبَانِهَا فَيَسْقِينَا . متفقٌ عَلَيْهِ .

Na imepokewa kutoka kwa 'Urwah, kutoka kwa 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kuwa yeye alikuwa anasema: "Naapa kwa Allaah! Ee kijana wa dadangu, tulikuwa tunaona mwezi, kisha mwezi mwingine, na kisha mwezi mwengine: Miandamo mitatu katika miezi miwili na hakukuwa kukiwashwa moto katika nyumba za Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)." Nikasema: "Ee halati yangu! Mlikuwa mkila nini?" Akasema: "Vitu Vyeusi viwili: Tende na maji isipokuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa na majirani wa ki-Answaar ambao walikuwa wakimletea Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) maziwa tuliokuwa tukinywa." [Al-Bukhaariy na Muslim]





Hadiyth – 3

وعن أَبي سعيد المقبُريِّ ، عن أَبي هريرة رضي الله عنهما: أَنَّهُ مَرَّ بِقَومٍ بَيْنَ أيدِيهمْ شَاةٌ مَصْلِيَّةٌ ، فَدَعَوْهُ فَأبَى أنْ يأْكُلَ . وقال : خرج رسول الله صلى الله عليه وسلم مِنَ الدُّنْيَا وَلَمْ يَشْبَعْ مِنْ خُبْزِ الشَّعيرِ . رواه البخاري .

Imepokewa kutoka kwa Abuu sa'iyd Al-Maqburiyy kutoka kwa Abuu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba mara moja alipita baina ya watu waliokuwa wakichoma mbuzi, walimuita lakini alikataa kula. Akasema: "Aliondoka Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) duniani na wala hakushiba hata siku moja makte wa mtama." [Al-Bukhaariy]





Hadiyth – 4

وعن أنس رضي الله عنه ، قَالَ : لَمْ يَأكُلِ النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم عَلَى خِوَانٍ حَتَّى مَاتَ ، وَمَا أكَلَ خُبْزاً مُرَقَّقاً حَتَّى مَاتَ . رواه البخاري .

وفي رواية لَهُ : وَلاَ رَأى شَاةً سَمِيطاً بعَيْنِهِ قَطُّ .

Imepokewa kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba amesema: "Hakula Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) juu ya meza mpaka akafariki. Na wa hakula mkate mzuri na laini mpaka akaaga dunia." [Al-Bukhaariy]

Katika riwaayah nyengine: "Wala hakumuona kabisa mbuzi mzima aliyechomwa."





Hadiyth – 5

وعن النعمان بن بشير رضي الله عنهما ، قَالَ : لَقَدْ رَأيْتُ نَبيَّكُمْ صلى الله عليه وسلم ، وَمَا يَجِدُ مِنَ الدَّقَلِ مَا يَمْلأُ بِهِ بَطْنَهُ . رواه مسلم .

Na imepokewa kutoka kwa an-Nu'maan bin Bashiyr (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba amesema: "Hakika nimemuona Nabiy wenu (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ambaye hakuweza kupata hata tende mbaya ambazo zitamshibisha." [Muslim]





Hadiyth – 6

وعن سهلِ بن سعد رضي الله عنه، قَالَ : مَا رَأى رسول الله صلى الله عليه وسلم النَّقِيَّ مِنْ حِين ابْتَعَثَهُ الله تَعَالَى حَتَّى قَبضَهُ الله تَعَالَى . فقِيلَ لَهُ : هَلْ كَانَ لَكُمْ في عَهدِ رسول الله صلى الله عليه وسلم مَنَاخِلُ ؟ قَالَ : مَا رَأى رسول الله صلى الله عليه وسلم مُنْخُلاً مِنْ حِينَ ابْتَعَثَهُ اللهُ تَعَالَى حَتَّى قَبَضَهُ اللهُ تَعَالَى ، فَقِيلَ لَهُ : كَيْفَ كُنْتُمْ تَأكُلُونَ الشَّعِيرَ غَيْرَ مَنْخُولٍ ؟ قَالَ : كُنَّا نَطحَنُهُ وَنَنْفُخُهُ ، فيَطيرُ مَا طَارَ ، وَمَا بَقِيَ ثَرَّيْنَاهُ . رواه البخاري .

Imepokewa kutoka kwa Sahl bin Sa'ad (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Hakuona mkate wa unga safi tangu Allaah Ta'aalaa Alipomtuma mpaka Allaah Ta'aalaa alipomfisha. Akauliza: "Je, katika zama za Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) mlikuwa na chekeche?" Akasema: "Hakuona Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kichungio tangu Allaah Ta'aalaa Alipomtuma hadi Allaah Ta'aalaa alipomfisha." Akauliza: "Mlikuwa mkila vipi shayiri isiochekechwa?" Akasema: "Tulikuwa tukiitwanga na kuipulizia, hupeperuka zinazopeperuka na kilichobaki tunakanda." [Al-Bukhaariy]





Hadiyth – 7

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه، قَالَ : خرجَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم ذَاتَ يَوْمٍ أَوْ لَيْلَةٍ ، فَإذَا هُوَ بأَبِي بَكْرٍ وَعُمَرَ رضي الله عنهما ، فَقَالَ : (( مَا أخْرَجَكُمَا مِنْ بُيُوتِكُما هذِهِ السَّاعَةَ ؟ )) قَالا : الجُوعُ يَا رسول الله . قَالَ : (( وَأنَا ، وَالَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ ، لأخْرَجَنِي الَّذِي أخْرَجَكُما ، قُوما )) فقَامَا مَعَهُ ، فَأتَى رَجُلاً مِنَ الأَنْصَارِ ، فَإذَا هُوَ لَيْسَ في بيْتِهِ ، فَلَمَّا رَأَتْهُ المَرْأَةُ ، قالت : مَرْحَبَاً وَأهلاً .فقال لَهَا رسول الله صلى الله عليه وسلم🙁( أيْنَ فُلانُ ؟ )) قالت : ذَهَبَ يَسْتَعْذِبُ لنَا المَاءَ . إِذْ جَاءَ الأَنْصَارِيُّ ، فَنَظَرَ إِلَى رسول الله صلى الله عليه وسلم وَصَاحِبَيْهِ ، ثُمَّ قَالَ : الحَمْدُ للهِ ، مَا أَحَدٌ الْيَوْمَ أكْرَمَ أضْيَافاً مِنِّي ، فَانْطَلَقَ فَجَاءهُمْ بِعِذْقٍ فِيهِ بُسْرٌ وَتَمْرٌ وَرُطَبٌ ، فَقَالَ : كُلُوا ، وَأَخَذَ الْمُدْيَةَ ، فَقَالَ لَهُ رسول الله صلى الله عليه وسلم: (( إيْاكَ وَالْحَلُوبَ )) فَذَبَحَ لَهُمْ ، فَأكَلُوا مِنَ الشَّاةِ وَمِنْ ذَلِكَ العِذْقِ وَشَرِبُوا . فَلَمَّا أنْ شَبِعُوا وَرَوُوا قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم لأَبي بَكْر وَعُمَرَ رضي الله عنهما : (( وَالَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ ، لَتُسْأَلُنَّ عَنْ هَذَا النَّعِيمِ يَوْمَ القِيَامَةِ ، أَخْرَجَكُمْ مِنْ بُيُوتِكُمُ الْجُوعُ ، ثُمَّ لَمْ تَرْجِعُوا حَتَّى أصَابَكُمْ هَذَا النَّعيمُ )) رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba amesema: Alitoka Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) siku moja au usiku, akakutana na Abuu Bakr na 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhummaa) Akasema: "Nini kilichowatoa katika majumba yenu saa hii?" Wakasema: "Njaa ee Rasuli wa Allaah." Akasema: "Naapa kwa ambaye nafsi yangu iko mkononi Mwake, mimi pia kimenitoa nyumbani kwangu kilichowatoa nyie, simameni" Wakasimama pamoja naye Akaja mtu wa Ki-Answaar, lakini hakuwa nyumbani kwake. Mkewe alipowaona, alisema: "Karibuni sana." Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akamuuliza: "Fulani yuko wapi?" Akasema: "Amekwenda kututekea maji." Mara akarudi yule Answaar akamwangalia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na rafiki zake, kisha akasema: "Alhamdulillaah." Hakuna leo mwenye wegeni watukufu kuniliko." Akatoka na kurudi huku amekuja na kitagaa chenye tende mbivu na mbichi. Akasema: "Kuleni naye" akachukua kisu kuwachinjia mbuzi. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia: "Usichinje mwenye maziwa." Wakala mbuzi waliochinjiwa, wakala na tende na kunywa maji. Waliposhiba na kukata kiu, Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliwaambia Abu Bakr na 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa): "Naapa kwa ambaye nafsi yangu iko mikononi Mwake, Mtaulizwa neema hii Siku ya Qiyaamah. Lililowatoeni majumbani mwenu ni njaa, lakini kabla ya kurudi (majumbani kwenu) mmepata neema hii." [Muslim]





Hadiyth – 8

وعن خالد بن عُمَيْر العَدَوِيِّ ، قَالَ : خَطَبَنَا عُتْبَةُ بنُ غَزْوَانَ ، وَكَانَ أمِيراً عَلَى البَصْرَةِ ، فَحَمِدَ الله وَأثْنَى عَلَيْهِ ، ثُمَّ قَالَ : أَمَّا بَعْدُ ، فَإِنَّ الدُّنْيَا قَدْ آذَنَتْ بِصُرْمٍ ، وَوَلَّتْ حَذَّاءَ ، وَلَمْ يَبْقَ مِنْهَا إِلاَّ صُبَابَةٌ كَصُبَابَةِ الإنَاءِ يَتَصَابُّهَا صَاحِبُهَا ، وَإِنَّكُمْ مُنْتَقِلُونَ مِنْهَا إِلَى دَارٍ لاَ زَوَالَ لَهَا ، فَانْتَقِلُوا بِخَيرِ مَا بِحَضْرَتِكُمْ ، فَإِنَّهُ قَدْ ذُكِرَ لَنَا أنَّ الحَجَرَ يُلْقَى مِنْ شَفِيرِ جَهَنَّمَ فَيَهْوِي فِيهَا سَبْعِينَ عَاماً ، لاَ يُدْرِكُ لَهَا قَعْراً ، وَاللهِ لَتُمْلأَنَّ أَفَعَجِبْتُمْ ؟! وَلَقدْ ذُكِرَ لَنَا أنَّ مَا بَيْنَ مِصْرَاعَيْنِ مِنْ مَصَارِيعِ الْجَنَّةِ مَسيرَةُ أرْبَعِينَ عَاماً ، وَليَأتِيَنَّ عَلَيْهَا يَوْمٌ وَهُوَ كَظِيظٌ مِنَ الزِّحَامِ ، وَلَقَدْ رَأيْتُنِي سَابعَ سَبْعَةٍ مَعَ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، مَا لَنَا طَعَامٌ إِلاَّ وَرَقُ الشَّجَرِ ، حَتَّى قَرِحَتْ أشْدَاقُنَا ، فَالتَقَطْتُ بُرْدَةً فَشَقَقْتُهَا بَيْنِي وَبَيْنَ سَعْدِ بْنِ مَالِكٍ ، فاتَّزَرْتُ بِنِصْفِهَا ، وَاتَّزَرَ سَعْدٌ بِنِصْفِهَا ، فَمَا أصْبَحَ اليَوْمَ مِنَّا أحَدٌ إِلاَّ أَصْبَحَ أمِيراً عَلَى مِصرٍ مِنَ الأَمْصَارِ ، وَإنِّي أعُوذُ بِاللهِ أنْ أكُونَ فِي نَفْسِي عَظِيماً ، وَعِنْدَ اللهِ صَغِيراً .

رواه مسلم .

Na imepokewa kutoka kwa Khaalid bin 'Umayr Al-'Adawiy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba amesema: Alituhutubia 'Utbah bin Ghazwaan (Radhwiya Allaahu 'anhu) naye alikuwa ni Amiri wa Basrah. Alimuhimidi Allaah na kumtukuza, kisha akasema: "Ama baada ya hayo! Kwa hakika dunia inatangaza kumalizika kwake na imegeuza uso wake na inakimbia kwa haraka sana. Dunia imebakia ndogo sana kama mfano wa matone yanayobaki baada ya mtu kunywa maji kutoka kwenye chombo. Wapenzi wa dunia wanakunywa matone hayo. Na hakika nyinyi mtakuwa ni wenye kuhamishwa kutoka katika nyumba yenye kudumu milele. Hivyo, yakinisha kuwa utakwenda huko na vile vitu vizuri kabisa ulivyonavyo. Tumeelezwa ya kwamba jiwe litakuwa ni lenye kurushwa kwenye mdomo wa Jahanamu ambalo litachukua miaka sabiini kufika chini. Naapa kwa Allaah kuwa sehemu hiyo itajazwa (na watu waovu). Je, mnastaajabu? Na hakika tuliambiwa ya kwamba masafa baina ya mbao mbili za mlango wa Peponi ni mwendo wa miaka arobaini. Mbali ya hiyo itafika siku ambapo halaiki ya watu itajaa kwenye mlango huo. Nakumbuka nilipokuwa mmoja wa watu saba waliokuwa pamoja na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) wakati ambao hatukuwa na chochote cha kula ila majani ya miti mpaka midomo yetu ikapata majeraha ya kupasuka pasuka. Hata hivyo nilipata kitambara ambacho nilikikata vipande viwili, kimoja nikatumia mimi na nusu ya pili nikampatia Sa'ad bin Maalik (Radhwiya Allaahu 'anhu). Ama leo kila moja miongoni mwetu ni Amiri wa mji miongoni mwa miji. Na kwa hakika mimi, najilinda kwa Allaah kwa hilo, kuwa katika nafsi yangu kujiona mtukufu na mbele ya Allaah nikawa mdogo sana." [Muslim]





Hadiyth – 9

وعن أَبي موسى الأشعري رضي الله عنه، قَالَ : أخْرَجَتْ لَنَا عَائِشَةُ رضي الله عنها كِسَاءً وَإزاراً غَلِيظاً ، قالَتْ : قُبِضَ رسول الله صلى الله عليه وسلم في هَذَيْنِ . متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Abuu Muwsaa Al-Asha'ariy kwamba amesema: "Alituonyesha 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kitambara na kikoi kigumu, akasema: 'Ameaga dunia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akiwa na nguo hizi mbili pekee." [Al-Bukhaariy na Muuslim]





Hadiyth – 10

وعن سعد بن أَبي وقاص رضي الله عنه، قَالَ : إنِّي لأَوَّلُ الْعَرَبِ رَمَى بِسَهْمٍ في سَبِيلِ الله ، وَلَقَدْ كُنَّا نَغْزُو مَعَ رسول الله صلى الله عليه وسلم مَا لَنَا طَعَامٌ إِلاَّ وَرَقُ الْحُبْلَةِ ، وَهذَا السَّمُرُ ، حَتَّى إنْ كَانَ أحَدُنَا لَيَضَعُ كَمَا تَضَعُ الشَّاةُ مَا لَهُ خَلْطٌ . متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Sa'ad bin Abuu Waqqaas (Radhwiya Allaah 'anhu) kwamba amesema: "Mimi nilikuwa Muarabu wa kwanza kurusha mshale katika njia ya Allaah. Tulikuwa tukipigana (katika Jihad) pamoja na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) hatuna kabisa chakula isipokuwa majani ya miti ya jangwani (kama acacia). Hivyo kukifanya choo chetu kuwa kigumu kama kinyesi cha mbuzi." [Al-Bukhaariy na Muslim]





Hadiyth – 11

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( اللَّهُمَّ اجْعَلْ رِزْقَ آلِ مُحَمّدٍ قُوتاً )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Ee Allaah! Ijaalie riziki ya familia ya Muhammad iwe ni yenye kutosha." [Al-Bukhaariy, Muslim na At-Tirmidhiy]





Hadiyth – 12

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه، قَالَ : وَاللهِ الَّذِي لاَ إِلهَ إِلاَّ هُوَ ، إنْ كُنْتُ لأَعْتَمِدُ بِكَبِدِي عَلَى الأَرْضِ مِنَ الجُوعِ ، وَإنْ كُنْتُ لأَشُدُّ الحَجَرَ عَلَى بَطنِي مِنَ الْجُوعِ . وَلَقَدْ قَعَدْتُ يَوماً عَلَى طَرِيقِهِمُ الَّذِي يَخْرُجُونَ مِنْهُ ، فَمَرَّ بِي النبي صلى الله عليه وسلم ، فَتَبَسَّمَ حِيْنَ رَآنِي ، وَعَرَفَ مَا فِي وَجْهِي وَمَا فِي نَفْسِي ، ثُمَّ قَالَ : (( أَبَا هِرٍّ )) قُلْتُ : لَبَّيْكَ يَا رسول الله ، قَالَ : (( الْحَقْ )) وَمَضَى فَاتَّبَعْتُهُ ، فَدَخَلَ فَاسْتَأذَنَ ، فَأَذِنَ لِي فَدَخَلْتُ ، فَوَجَدَ لَبَنَاً في قَدَحٍ ، فَقَالَ : (( مِنْ أَيْنَ هَذَا اللَّبَنُ ؟ )) قَالُوا : أهْدَاهُ لَكَ فُلانٌ – أَو فُلانَةٌ – قَالَ : (( أَبَا هِرٍّ )) قلتُ : لَبَّيْكَ يَا رسول اللهِ ، قَالَ : (( الْحَقْ إِلَى أهْلِ الصُّفَّةِ فَادْعُهُمْ لِي )) قَالَ : وَأهْلُ الصُّفَّة أضْيَافُ الإِسْلاَمِ ، لاَ يَأوُونَ علَى أهْلٍ وَلاَ مَالٍ وَلاَ عَلَى أحَدٍ ، وَكَانَ إِذَا أتَتْهُ صَدَقَةٌ بَعَثَ بِهَا إلَيْهِمْ ، وَلَمْ يَتَنَاوَلْ مِنْهَا شَيْئاً ، وَإِذَا أتَتْهُ هَدِيَّةٌ أرْسَلَ إلَيْهِمْ ، وَأصَابَ مِنْهَا ، وأشْرَكَهُمْ فِيهَا . فَسَاءنِي ذَلِكَ ، فَقُلْتُ : وَمَا هَذَا اللَّبَنُ في أهْلِ الصُّفَّةِ ! كُنْتُ أحَقُّ أنْ أُصِيبَ مِنْ هَذَا اللَّبَنِ شَرْبَةً أتَقَوَّى بِهَا ، فَإذَا جَاءُوا وَأمَرَنِي فَكُنْتُ أنَا أُعْطِيهِمْ ؛ وَمَا عَسَى أنْ يَبْلُغَنِي مِنْ هَذَا اللَّبَنِ . وَلَمْ يَكُنْ مِنْ طَاعَةِ اللهِ وَطَاعَةِ رسول الله صلى الله عليه وسلم بُدٌّ ، فَأَتَيْتُهُمْ فَدَعَوْتُهُمْ ، فَأقْبَلُوا وَاسْتَأذَنُوا ، فَأَذِنَ لَهُمْ وَأخَذُوا مَجَالِسَهُمْ مِنَ الْبَيْتِ ، قَالَ : (( يَا أَبَا هِرٍّ )) قُلْتُ: لَبَّيْكَ يَا رسول الله ، قَالَ : (( خُذْ فَأعْطِهِمْ )) قَالَ : فَأخَذْتُ القَدَحَ ، فَجَعَلْتُ أُعْطِيهِ الرَّجُل فَيَشْرَبُ حَتَّى يَرْوَى ، ثُمَّ يَرُدُّ عَلَيَّ الْقَدَحَ ، فَأُعْطِيهِ الرَّجُلَ فَيَشْرَبُ حَتَّى يَرْوَى ، ثُمَّ يَرُدُّ عَلَيَّ الْقَدَحَ ، فَأُعْطِيهِ الرَّجُلَ فَيَشْرَبُ حَتَّى يَرْوَى ، ثُمَّ يَرُدُّ عَلَيَّ الْقَدَحَ حَتَّى انْتَهَيْتُ إِلَى النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم ، وَقَدْ رَوِيَ الْقَوْمُ كُلُّهُمْ ، فَأخَذَ الْقَدَحَ فَوضَعَهُ عَلَى يَدِهِ ، فَنَظَرَ إليَّ فَتَبَسَّمَ ، فَقَالَ : (( أَبَا هِرٍّ )) قُلْتُ : لَبَّيْكَ يَا رسول الله ، قَالَ : (( بَقيتُ أنَا وَأنْتَ )) قُلْتُ : صَدَقْتَ يَا رسول الله ، قَالَ : (( اقْعُدْ فَاشْرَبْ )) فَقَعَدْتُ فَشَرِبْتُ ، فَقَالَ (( اشْرَبْ )) فَشَرِبْتُ ، فَمَا زَالَ يَقُولُ : (( اشْرَبْ )) حَتَّى قُلْتُ: لا ، وَالَّذِي بَعَثَكَ بِالحَقِّ لاَ أجِدُ لَهُ مَسْلكاً ! قَالَ: (( فَأرِنِي )) فَأعْطَيْتُهُ الْقَدَحَ ، فَحَمِدَ الله تَعَالَى ، وَسَمَّى وَشَرِبَ الفَضْلَةَ . رواه البخاري .

Na imepokewa kutoka kwa Abuu Huraiyrah amesema: ""Naapa kwa ambaye hapana Mola isipokuwa Yeye, nilikuwa naegemeza tumbo langu ardhini kwa njaa, nikifunga jiwe tumboni mwangu kwa njaa. Siku moja nilikaa juu ya njia yao wanayotokea. Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipita akatabasamu aliponiona, akajua kilicho usoni mwangu na yaliyo nafsini mwangu. Alisema: "Abuu Hirr." Nikasema: "Ee Rasuli wa Allaah." Akasema: "Nifuate." Aliondoka nikamfuata. Akabisha hodi akakaribishwa, akaniruhusu kuingia. Akakuta maziwa ndani ya jagi akasema: "Kutoka wapi haya maziwa?" Wakasema: "Fulani amekuzawadia." Akasema: "Abuu Hirr." Nikasema: "Labbayka, ee Rasuli wa Allaah." Akasema: "Nenda kaite watu wa Swuffah." Akasema: "Watu wa Swuffah ni wageni wa Waislamu, hawana isipokuwa jamaa, mali, wala yoyote," Alikuwa akipata swadaqah anawapelekea, hakutumia chochote humo. "Na anapopata zawadi anawapelekea naye anakula humo, na kuwashirikisha humo, Likaniumiza hilo, nikauliza: "Maziwa gani haya kwa watu wa Suwffah?" Nilikuwa na haki zaidi kupata haya maziwa ili yanipe nguvu. Watakapofiks ataniamuru kuwaandalia, pengine yasinifikie maziwa haya, hakukuwa na budi isipokuwa kutii amri ya Allaah na Rasuli Wake." Nilikwenda kuwaita, wakabisha hodi, wakaruhusiwa, wakakaa sehemu yao. Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: "Abuu Hirr." Nikasema: "Labbayka, ee Rasuli wa Allaah." Akasema: "Chukua haya maziwa uwape." Akasema: "Nikachukua kikombe nikaanza kumpa wa kwanza, alikunywa hadi akatosheka. Kisha akanirudishia kikombe, nikampa mwengine hunywa mpaka anatosheka. Kisha hunirudishia kikombe kikamfikia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) wote wamemaliza kunywa. Nabiy akachukua kikombe mkononi mwake akanitazama akatabasamu, akasema: "Abuu Hirr." Nikasema: "Labbayka, ee rasuli wa Allaah." Akasema: "Tumebaki mimi na wewe." Nikasema: "Ndio, ee Rasuli wa Allaah." Akasema: "Kaa unywe." Nikakaa nakunywa." Akasema: "Kunywa." Nami nikanywa. Hakuacha kusema "Kunywa." Mpaka ikafika wakati nikasema: "Laa, naapa aliyekutuma kwa haki sina nafasi yake." Akasema: "Nipe." Nikampa kikombe, akamuhimidi Allaah, akasema: "Bismillaah, akanywa maziwa yaliyobakia." [Al-Bukhaariy]





Hadiyth – 13

وعن محمد بن سيرين ، عن أَبي هريرة رضي الله عنه، قَالَ : لَقَدْ رَأيْتُنِي وَإنِّي لأَخِرُّ فِيمَا بَيْنَ مِنْبَرِ رسولِ الله صلى الله عليه وسلم إِلَى حُجْرَةِ عائِشَةَ رضي الله عنها مَغْشِيّاً عَلَيَّ ، فَيَجِيءُ الجَائِي ، فَيَضَعُ رِجْلَهُ عَلَى عُنُقِي ، وَيَرَى أنِّي مَجْنُونٌ وَمَا بِي مِنْ جُنُونٍ ، مَا بِي إِلاَّ الْجُوعُ . رواه البخاري.

Imepokewa kutoka kwake Muhammad bin Siiyriyn kutoka kwa Abuu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: "Nilijiona naanguka baina ya mimbari ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na chumba cha 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) na kupoteza fahamu, anapita mtu anaweka mguu wake shingoni mwangu, akidhani mimi ni mwenda wazimu. Ns mimi si mwenda wazimu isipokuwa njaa." [Al-Bukhaariy]





Hadiyth – 14

وعن عائشة رضي الله عنها ، قالت : تُوُفِّي رسول الله صلى الله عليه وسلم وَدِرْعُهُ مَرْهُونَةٌ عِنْدَ يَهُودِي في ثَلاثِينَ صَاعاً مِنْ شَعِير . متفق عَلَيْهِ .

Na imepokewa kutoka kwa 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kwamba amesema: "Alifariki Rasuli wa Allaah (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na dir'a (nguo ya chuma inayotumiwa katika vita) yake ameiweka rahani kwa Myahudi kwa Swaa' (takriban kilo mbili na nusu) thelathini za shayiri." [Al-Bukhaariy, Muslim na An-Nasaai]





Hadiyth – 15

وعن أنسٍ رضي الله عنه، قَالَ : رَهَنَ النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم دِرْعَهُ بِشَعِيرٍ ، وَمَشَيْتُ إِلَى النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم بخُبْزِ شَعِيرٍ وَإهَالَة سَنِخَةٍ ، وَلَقَدْ سَمِعْتُهُ يَقُولُ : (( مَا أصْبَحَ لآلِ مُحَمّدٍ صَاعٌ وَلاَ أمْسَى )) وَإنَّهُمْ لَتِسْعَةُ أبيَات . رواه البخاري .

Imepokewa kwa Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba amesema: "Aliweka rehani Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) dir'a yake kwa shayiri, nikamchukulia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) mkate wa shayiri na samli, Nimemsikia anasema: "Haijapambazuka Familia ya Muhammad ikiwa na pishi ya chakula wala kuchwewe." Na hizo ni nyumba tisa." [Al-Bukhaariy]





Hadiyth – 16

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، قَالَ : لَقَدْ رَأَيْتُ سَبْعِينَ مِنْ أَهْلِ الصُّفَّةِ ، مَا مِنْهُمْ رَجُلٌ عَلَيْهِ ردَاءٌ ، إمَّا إزَارٌ وَإمَّا كِسَاءٌ ، قَدْ رَبَطُوا في أعْنَاقِهِم مِنْهَا مَا يَبْلُغُ نِصْفَ السَّاقَيْن ، وَمِنْهَا مَا يَبْلُغُ الكَعْبَيْنِ فَيَجْمَعُهُ بِيَدِهِ كَرَاهِيَةَ أنْ تُرَى عَوْرَتُهُ . رواه البخاري .

Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: "Nimeona Swahaaba sabiini miongoni mwa watu wa Swuffah, hakuna mtu miongoni mwao mwenye kikoi, shuka, wamezifunga katika shingo zao. Kuna zinazofika nusu ya miguu, nyingine kwenye fundo mbili, hivyo huzishika mkononi mwake kuchukia uchi wao kuonekana." [Al-Bukhaariy]





Hadiyth – 17

وعن عائشة رضي الله عنها ، قالت : كَانَ فِرَاشُ رسول الله صلى الله عليه وسلم مِنْ أُدْمٍ حَشْوُهُ لِيفٌ . رواه البخاري .

Imepokewa kutoka kwake 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kwamba amesema: "Godoro la Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) lilikuwa limetengenezwa kwa ngozi iliyotiwa magamba ya mtende." [Al-Bukhaariy]







Hadiyth – 18

وعن ابن عمر رضي الله عنهما، قَالَ : كُنَّا جُلُوساً مَعَ رسول الله صلى الله عليه وسلم، إِذْ جَاءَ رَجُلٌ مِنَ الأنْصَارِ ، فَسَلَّمَ عَلَيْهِ ، ثُمَّ أدْبَرَ الأَنْصَاريُّ ، فَقَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( يَا أخَا الأنْصَارِ ، كَيْفَ أخِي سَعْدُ بْنُ عُبَادَةَ ؟ )) فَقَالَ : صَالِحٌ ، فَقَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( مَنْ يَعُودُهُ مِنْكُمْ ؟ )) فَقَامَ وَقُمْنَا مَعَهُ ، وَنَحْنُ بضْعَةَ عَشَرَ ، مَا عَلَيْنَا نِعَالٌ ، وَلاَ خِفَافٌ ، وَلاَ قَلاَنِسُ ، وَلاَ قُمُصٌ ، نَمْشِي في تِلك السِّبَاخِ ، حَتَّى جِئْنَاهُ ، فَاسْتَأْخَرَ قَوْمُهُ مِنْ حَوْله حَتَّى دَنَا رسول الله صلى الله عليه وسلم وَأصْحَابُهُ الَّذِينَ مَعَهُ . رواه مسلم .

imepokewa kutoka kwa Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba amesema: "Tulikuwa tumekaa pamoja na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipokuja mtu kutoka kwa Answaar na kumsalima Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Kisha yule Answaar akawa anaondoka, Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akauliza: "Ee ndugu yangu wa Ki-Answaar, ndugu yangu Sa'ad bin 'Ubaadah yu hali gani?' Akasema: "Hali yake ni nzuri." Akasema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Nani atakayemzuru miongoni mwenu?" Alisimama na tukasimama pamoja naye. Na sisi tulikuwa kumi, na hakuna miongoni mwetu aliyekuwa na viatu au soksi za ngozi, wala kofia au shati. Tulikuwa tunatembea katika hali hiyo mpaka tukafika katika nyumba ya Sa'ad. Watu wake wa nyumbani (familia yake) walitupatia nafasi mpaka Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaaba zake waliokuwa pamoja naye wakapata nafasi ya kuja karibu yake." [Muslim]





Hadiyth – 19

وعن عِمْرَان بنِ الحُصَيْنِ رضي الله عنهما ، عن النبي صلى الله عليه وسلم ، أنّه قَالَ : (( خَيْرُكُمْ قَرْنِي ، ثُمَّ الَّذِينَ يَلُونَهُمْ ، ثُمَّ الَّذِينَ يَلُونَهُمْ )) قَالَ عِمْرَانُ : فَمَا أدْري قَالَ النبي صلى الله عليه وسلم مَرَّتَيْنِ أَو ثَلاَثاً (( ثُمَّ يَكُونُ بَعْدَهُمْ قَوْمٌ يَشْهَدُونَ وَلاَ يُسْتَشْهَدُونَ ، وَيَخُونُونَ وَلاَ يُؤْتَمَنُونَ ، وَيَنْذِرُونَ وَلاَ يُوفُونَ ، وَيَظْهَرُ فِيهمُ السَّمَنُ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwake 'Imraan bin Al-Huswaiyn (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mbora wenu ni (watu wa) karne yangu, kisha wanaowafuata, kisha wanaowafuata, kisha wanaowafuata, Akasema 'Imraan: "Sijui Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ameisema mara mbili au mara tatu. Kisha watakuja baada yao watu watashuhudia wala hawatakiwi kushuhudia, wanakhini wala hawaaminiwi, utadhihiri miongoni mwao umeme (walionenepa)." [Al-Bukhaariy na Muslim]





Hadiyth – 20

وعن أَبي أُمَامَة رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( يَا ابْنَ آدَمَ ، إنَّكَ أنْ تَبْذُلَ الفَضْلَ خَيرٌ لَكَ ، وَأنْ تُمسِكَهُ شَرٌ لَكَ ، ولاَ تُلاَمُ عَلَى كَفَافٍ ، وَابْدأ بِمَنْ تَعُولُ )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن صحيح )) .

Imepokewa kutoka kwa Abuu Umamah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Ee mwanadamu! Hakika lau utatoa fadhila (hela) za ziada itakuwa bora kwako, na kuzuilia (kutotumia) ni shari kwako. Hutalaumiwa kuwa na hela kwa kadiri ya mahitaji yako. Na anza kuitumia kwa wale wenye haki kwako." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]





Hadiyth – 21

وعن عُبيْدِ الله بنِ محْصن الأَنصَارِيِّ الخطميِّ رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( مَنْ أصْبَحَ مِنْكُمْ آمِناً في سربِهِ ، مُعَافَىً في جَسَدِهِ ، عِنْدَهُ قُوتُ يَوْمِهِ ، فَكَأنَّمَا حِيزَتْ لَهُ الدُّنْيَا بِحَذَافِيرِهَا )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .

Imepokewa kutoka kwa 'Ubaydullaah bin Muhswan Al-Answaariy Al-Khutwamiy kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Yeyote atakaye pambazukiwa (atakaye inuka asubuhi) akiwa yu salama wa nafsi yake (au familia yake), akiwa na siha mzuri ya mwili wake, anacho chakula cha siku yake hiyo. Mwenye hayo ni kama ambaye amepatiwa dunia na vilivyomo ndani yake." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]







Hadiyth – 22

وعن عبد الله بن عَمْرو بنِ العاص رضي الله عنهما : أن رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( قَدْ أفْلَحَ مَنْ أسْلَمَ ، وَكَانَ رِزْقُهُ كَفَافاً ، وَقَنَّعَهُ اللهُ بِمَا آتَاهُ )) رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa 'Abdillaah bin 'Amru bin Al-'Aas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakika amefanikiwa aliyesilimu na ikiwa riziki yake ni yenye kumtosha na akakinaika kwa anachopewa na Allaah." [Muslim]





Hadiyth – 23

وعن أَبي محمدٍ فضَالَة بن عبيدٍ الأنصاريِّ رضي الله عنه: أنه سمع رسول الله صلى الله عليه وسلم، يقول : (( طُوبَى لِمَنْ هُدِيَ لِلإسْلاَمِ ، وَكَانَ عَيْشُهُ كَفَافاً وَقَنِعَ )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن صحيح )) .

Imepokewa kutoka kwa Abuu Muhammad Fadhwalah bin 'Ubayd Al-Answaariy (Radhwiya Allaah 'anhu) kuwa amemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Habari njema kwa anayeongoka na kusilimu na akapata rizki ya kumtosha mahitaji yake na akakinai kwa hilo." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]





Hadiyth – 24

وعن ابن عباس رضي الله عنهما ، قَالَ : كَانَ رسول الله صلى الله عليه وسلم يَبيتُ اللَّيَالِيَ الْمُتَتَابِعَةَ طَاوِياً ، وَأهْلُهُ لاَ يَجِدُونَ عَشَاءً ، وَكَانَ أكْثَرُ خُبْزِهِمْ خُبزَ الشَّعيرِ . رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن صحيح )) .

Na imepokewa kutoka kwa Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba amesema: "Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akilala akiwa na shida ya njaa kwa masiku marefu yenye kufuatana na familia yake haina chochote cha kula usiku. Na mara nyingi mkate waliokuwa wakitumia ni mkate wa shayiri." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]





Hadiyth – 25

وعن فُضَالَةَ بن عبيدٍ رضي الله عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم كَانَ إِذَا صَلَّى بِالنَّاسِ ، يَخِرُّ رِجَالٌ مِنْ قَامَتِهِمْ في الصَّلاةِ مِنَ الخَصَاصَةِ – وَهُمْ أصْحَابُ الصُّفَّةِ – حَتَّى يَقُولَ الأعْرَابُ : هؤُلاء مَجَانِينٌ . فَإذَا صلَّى رسول الله صلى الله عليه وسلم انْصَرَفَ إلَيْهِمْ ، فَقَالَ : (( لَوْ تَعْلَمُونَ مَا لَكُمْ عِنْدَ اللهِ تَعَالَى ، لأَحْبَبْتُمْ أنْ تَزْدَادُوا فَاقَةً وَحَاجَةً )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديث صحيح )) .

Imepokewa kutoka kwake Fadhwalah bin 'Ubayd (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba, Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiswalisha watu wakianguka chini baadhi ya watu wa Swuffah kwa sababu ya njaa kali mpaka wakawa wanasema Mabedui: "Hawa ni wenda wazimu." Alipokamilisha Swalah Rasuli wa Allaah alikuwa akiwaendea na kuwaambia: "Lau mngejua yaliyoko (katika thawabu) kwa Allaah Ta'aalaa, mngependa hali ya njaa kali ikaongezeka." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]





Hadiyth – 26

وعن أَبي كريمة المقدام بن معد يكرِبَ رضي الله عنه ، قَالَ : سَمِعْتُ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم ، يقول : (( مَا مَلأَ آدَمِيٌّ وِعَاء شَرّاً مِنْ بَطْنٍ ، بِحَسْبِ ابنِ آدَمَ أُكُلاَتٌ يُقِمْنَ صُلْبَهُ ، فإنْ كانَ لا مَحالةَ فثُلُثٌ لِطَعَامِهِ ، وَثُلُثٌ لِشَرابِهِ ، وَثُلُثٌ لِنَفَسه )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .

Imepokewa kutoka kwa Abu Kariymah Al-Miqdaam bin Ma'di Yakrib (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: "Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Hajajaza mwanadamu chombo kiovu zaidi kuliko tumbo lake. Inamtosha mwanadamu tonge la kuufanya mgongo usimame wima. Ikiwa hapana budi ila kula hicho chakula basi thuluthi ya tumbo iwe kwa chakula na thuluthi kwa kinywaji na thuluthi kwa nafsi yake (pumzi)." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan].





Hadiyth – 27

وعن أَبي أُمَامَة إياسِ بن ثعلبةَ الأَنْصَارِيِّ الحارثي رضي الله عنه ، قَالَ : ذَكَرَ أصْحَابُ رسول الله r يَوماً عِنْدَهُ الدُّنْيَا ، فَقَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( ألاَ تَسْمَعُونَ ؟ ألاَ تَسْمَعُونَ ؟ إنَّ البَذَاذَةَ مِنَ الإِيمَانِ ، إنَّ البَذَاذَةَ مِنَ الإِيمَانِ )) يَعْنِي : التَّقَحُّلَ . رواهُ أَبو داود

Imepokewa kutoka kwa Abu Umaamah Iyaas bin Tha'labah Al-Answaariy Al-Haarithiy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba amesema: Siku moja Sahaabah wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) walimtajia kuhusu dunia mbele yake. Akasema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Je,hamjasikia? Je, hamjasikia? Hakika kuupa nyongo ulimwengu ni katika Imaani. Hakika kuupa nyongo ulimwengu ni katika Imaani (kwa kuacha fakhari katika mavazi na mengineo)." [Abu Daawuud]





Hadiyth – 28

وعن أَبي عبد الله جابر بن عبد الله رضي الله عنهما ، قَالَ : بَعَثَنَا رسول الله صلى الله عليه وسلم ، وَأمَّرَ عَلَيْنَا أَبَا عُبَيْدَةَ رضي الله عنه ، نَتَلَقَّى عِيراً لِقُرَيْشٍ ، وَزَوَّدَنَا جِرَاباً مِنْ تَمْرٍ لَمْ يَجِدْ لَنَا غَيْرَهُ ، فَكَانَ أَبو عُبيدَةَ يُعْطِينَا تَمْرَةً تَمْرَةً ، فَقيلَ : كَيْفَ كُنْتُمْ تَصْنَعُونَ بِهَا ؟ قَالَ : نَمَصُّهَا كَمَا يَمَصُّ الصَّبي ، ثُمَّ نَشْرَبُ عَلَيْهَا مِنَ الْمَاءِ ، فَتَكْفِينَا يَوْمَنَا إِلَى اللَّيْلِ ، وَكُنَّا نَضْرِبُ بِعِصيِّنَا الخَبَطَ ، ثُمَّ نَبُلُّهُ بِالماءِ فَنَأكُلُهُ . قَالَ : وَانْطَلَقْنَا عَلَى سَاحِلِ الْبَحْرِ ، فَرُفِعَ لَنَا عَلَى سَاحِلِ الْبَحْرِ كَهَيْئَةِ الكَثِيبِ الضَّخْمِ ، فَأَتَيْنَاهُ فَإذَا هِيَ دَابَّةٌ تُدْعَى الْعَنْبَرَ ، فَقَالَ أَبو عُبَيْدَةَ : مَيْتَةٌ ، ثُمَّ قَالَ : لا ، بَلْ نَحْنُ رُسُلُ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم ، وفي سبيل الله وَقَدِ اضْطُرِرْتُمْ فَكُلُوا ، فَأقَمْنَا عَلَيْهِ شَهْراً ، وَنَحْنُ ثَلاَثُمِئَةٍ حَتَّى سَمِنَّا ، وَلَقَدْ رَأيْتُنَا نَغْتَرِفُ مِن وَقْبِ عَيْنِهِ بِالقِلاَلِ الدُّهْنَ وَنَقْطَعُ مِنْهُ الفِدَرَ كالثَّوْرِ أَوْ كَقَدْرِ الثَّوْرِ ، وَلَقَدْ أَخَذَ مِنَّا أَبو عُبَيْدَةَ ثَلاثَةَ عَشَرَ رَجُلاً فَأقْعَدَهُمْ في وَقْبِ عَيْنِهِ وَأخَذَ ضِلْعاً مِنْ أضْلاَعِهِ فَأقَامَهَا ثُمَّ رَحَلَ أعْظَمَ بَعِيرٍ مَعَنَا فَمَرَّ مِنْ تَحْتهَا وَتَزَوَّدْنَا مِنْ لَحْمِهِ وَشَائِقَ ، فَلَمَّا قَدِمْنَا المَدِينَةَ أَتَيْنَا رسول الله صلى الله عليه وسلم فَذَكَرْنَا ذَلِكَ لَهُ ، فَقَالَ : (( هُوَ رِزْقٌ أخْرَجَهُ اللهُ لَكُمْ ، فَهَلْ مَعَكُمْ مِنْ لَحْمِهِ شَيْءٌ فَتُطْعِمُونَا ؟ )) فَأرْسَلْنَا إِلَى رسول الله صلى الله عليه وسلم مِنْهُ فَأكَلَهُ . رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Abu 'Abdillaah Jaabir bin Abdillaah (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) amesema: "Alitutuma Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), amiri alikuwa Abu 'Ubaydah (Radhwiya Allaahu 'anhu), ili kuteka msafara wa Makureshi. Akatupa mfuko wa tende bila kitu kingine. Abu 'Ubaydah akawa akimpa kila mmoja watu tende moja moja tu. Akaulizwa: 'Mlikuwa mnaifanya nini?, Akasema: 'Tulikuwa tunainyonya kama anavyonyonya mtoto mchanga, kisha tukinywamaji. Ilikuwa ikitutosha mchana hadi usiku. Tulikuwa tukikata majani kwa fimbo, tukizitia kati maji na kuzila.' Akasema: 'Tulikwenda tukafika ufukweni ikanyanyuliwa kwetu katika huo ufuo wa bahari mfano wa kichuguu kikubwa. Tukakijia kumbe ni mnyama anayeitwa nyangumi.' Abu 'Ubaydah akasema: 'Huyu ni maiti.' Kisha akasema: 'Bali sisi ni wajumbe wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na tuko katika njia ya Allaah, na hii ni dharura kwa hivyo kuleni.' Tukamla mwezi mzima, nasi ni mia tatu hadi tukanenepa. Tulikuwa tukimtoa mafuta jichoni na kujaza viriba vya ngozi, tunakata nyama kama ng'ombe dume au mfano wake. Abu 'Ubaydah alikalisha watu kumi na tatu kwenye shimo la jicho lake. Akatoa mfupa wa mbavu yake na kuusimamisha na kupitisha ngamia mrefu zaidi chini yake. Wakati tunarudi tulichukua mapande makubwa na kuyachemsha kwa ajili ya chakula chetu. Tulipofika Madiynah tulikwenda kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na tukamtajia hayo, Akasema: "Hiyo ni riziki Allaah amekutoleeni, je mna chochote katika nyama yake mtupe" Tulimpa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) sehemu yake akaila." [Muslim]





Hadiyth – 29

وعن أسماء بنتِ يزيد رضي الله عنها ، قالت : كَانَ كُمُّ قَمِيصِ رسول الله صلى الله عليه وسلم إِلَى الرُّصْغِ . رواه أَبو داود والترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .

Na imepokewa kutoka kwa Asmaa' bint Yaziyd (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kwamba amesema: "Mikono ya shati la Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ilikuwa ikifika mpaka kwenye kiungo cha viganja." [Abu Daawuud na At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]







Hadiyth – 30

وعن جابر رضي الله عنه ، قَالَ : إنَّا كُنَّا يَوْمَ الْخَنْدَقِ نَحْفِرُ ، فَعَرَضَتْ كُدْيَةٌ شَدِيدَةٌ ، فَجَاؤُوا إِلَى النبي صلى الله عليه وسلم ، فقالوا : هذِهِ كُدْيَةٌ عَرَضَتْ في الخَنْدَقِ . فَقَالَ : (( أنَا نَازِلٌ )) ثُمَّ قَامَ ، وَبَطْنُهُ مَعْصُوبٌ بِحَجَرٍ ، وَلَبِثْنَا ثَلاَثَة أيّامٍ لاَ نَذُوقُ ذَوَاقاً فَأخَذَ النبي صلى الله عليه وسلم المِعْوَلَ ، فَضَرَبَ فَعَادَ كَثيباً أهْيَلَ أَو أهْيَمَ ، فقلت : يَا رسول الله ، ائْذَنْ لي إِلَى البَيْتِ ، فقلتُ لامْرَأتِي : رَأيْتُ بالنَّبيِّ صلى الله عليه وسلم شَيئاً مَا في ذَلِكَ صَبْرٌ فَعِنْدَكِ شَيْءٌ ؟ فقالت : عِنْدي شَعِيرٌ وَعَنَاقٌ ، فَذَبَحْتُ العَنَاقَ وَطَحَنْتُ الشَّعِيرَ حَتَّى جَعَلْنَا اللَّحْمَ في البُرْمَةِ ، ثُمَّ جِئْتُ النبي صلى الله عليه وسلم ، وَالعَجِينُ قَدِ انْكَسَرَ ، وَالبُرْمَةُ بَيْنَ الأثَافِيِّ قَدْ كَادَتْ تَنْضِجُ ، فقلتُ : طُعَيْمٌ لي ، فَقُمْ أنْتَ يَا رسول اللهِ وَرَجُلٌ أَوْ رَجُلانِ ، قَالَ : (( كَمْ هُوَ )) ؟ فَذَكَرْتُ لَهُ ، فَقَالَ : (( كثيرٌ طَيِّبٌ قُل لَهَا لاَ تَنْزَع البُرْمَةَ ، وَلاَ الخبْزَ مِنَ التَّنُّورِحتى آتِي )) فَقَالَ : (( قُومُوا )) ، فقام المُهَاجِرُونَ وَالأنْصَارُ ، فَدَخَلْتُ عَلَيْهَا فقلتُ : وَيْحَكِ قَدْ جَاءَ النبيُّ صلى الله عليه وسلم وَالمُهَاجِرُونَ وَالأنْصَارُ ومن مَعَهُمْ ! قالت : هَلْ سَألَكَ ؟ قُلْتُ : نَعَمْ ، قَالَ : (( ادْخُلُوا وَلاَ تَضَاغَطُوا )) فَجَعَلَ يَكْسرُ الخُبْزَ ، وَيَجْعَلُ عَلَيْهِ اللَّحْمَ ، وَيُخَمِّرُ البُرْمَةَ وَالتَّنُّور إِذَا أخَذَ مِنْهُ ، وَيُقَرِّبُ إِلَى أصْحَابِهِ ثُمَّ يَنْزعُ ، فَلَمْ يَزَلْ يِكْسِرُ وَيَغْرِفُ حَتَّى شَبِعُوا ، وَبَقِيَ مِنْهُ ، فَقَالَ : (( كُلِي هَذَا وَأهِدي ، فَإنَّ النَّاسَ أصَابَتْهُمْ مَجَاعَةٌ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

وفي رواية قَالَ جابر : لَمَّا حُفِرَ الخَنْدَقُ رَأيْتُ بالنبيِّ صلى الله عليه وسلم خَمَصاً ، فَانْكَفَأْتُ إِلَى امْرَأتِي ، فقلت : هَلْ عِنْدَكِ شَيْءٌ ؟ فَإنّي رَأيْتُ برسول الله صلى الله عليه وسلم خَمَصاً شَديداً ، فَأخْرَجَتْ إلَيَّ جِرَاباً فِيه صَاعٌ مِنْ شَعِيرٍ ، وَلَنَا بَهِيمَةٌ دَاجِنٌ فَذَبَحْتُهَا ، وَطَحَنتِ الشَّعِيرَ ، فَفَرَغَتْ إِلَى فَرَاغي ، وَقَطَعْتُهَا في بُرْمَتها ، ثُمَّ وَلَّيْتُ إِلَى رسول الله صلى الله عليه وسلم ، فقالت : لاَ تَفْضَحْنِي برسول الله صلى الله عليه وسلم وَمَنْ مَعَهُ ، فَجئتهُ فَسَارَرْتُهُ ، فَقُلْتُ : يَا رسول الله ، ذَبَحْنَا بهيمَة لَنَا ، وَطَحَنْتُ صَاعاً مِنْ شَعِيرٍ ، فَتَعَالَ أنْتَ وَنَفَرٌ مَعَكَ ، فَصَاحَ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، فَقَالَ : (( يَا أهلَ الخَنْدَقِ : إنَّ جَابِراً قَدْ صَنَعَ سُؤْراً فَحَيَّهَلا بِكُمْ )) فَقَالَ النبي صلى الله عليه وسلم : (( لاَ تُنْزِلُنَّ بُرْمَتَكُمْ وَلاَ تَخْبزنَّ عَجِينَكُمْ حَتَّى أجِيءَ )) فَجِئْتُ ، وَجَاءَ النبي صلى الله عليه وسلم يَقْدُمُ النَّاسَ ، حَتَّى جِئْتُ امْرَأتِي ، فقالَتْ : بِكَ وَبِكَ ! فقُلْتُ : قَدْ فَعَلْتُ الَّذِي قُلْتِ . فَأخْرَجَتْ عَجِيناً ، فَبسَقَ فِيهِ وَبَاركَ ، ثُمَّ عَمَدَ إِلَى بُرْمَتِنا فَبصَقَ وَبَارَكَ، ثُمَّ قَالَ: (( ادْعِي خَابزَةً فَلْتَخْبِزْ مَعَكِ ، وَاقْدَحِي مِنْ بُرْمَتِكُمْ ، وَلاَ تُنْزِلُوها )) وَهُم ألْفٌ ، فَأُقْسِمُ بِالله لأَكَلُوا حَتَّى تَرَكُوهُ وَانْحَرَفُوا ، وَإنَّ بُرْمَتَنَا لَتَغِطّ كَمَا هِيَ ، وَإنَّ عَجِينَنَا لَيُخْبَزُ كَمَا هُوَ .

Imepokewa kutoka kwa Jaabir (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Siku ya Khandaq tulikuwa tunachimba pakatokea jiwe gumu, wakaja kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) wakasema: 'Jiwe limedhihiri katika Khandaq' akasema: "Mimi nitateremka." Kisha akasimama na tumbo lake limefungwa jiwe. Tulikaa siku tatu bila kuonja chakula. Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akachukua mtaimbo akalipiga likawa kichuguu laini, au mchanga. Nikasema: "Ee Rasuli wa Allaah! Niruhusu niende nyumbani." Nilimwambia mke wangu: "Nimemuona Nabiy (Swalla Allaau 'alayhi wa aalihi wa sallam) katika hali ambayo siwezi kuvumilia. Una chochote?" Akasema: "Ipo shayiri na mwana mbuzi." Nilimchinja mbuzi na kutwanga shayiri hadi tukaiweka nyama katika chungu. Baada ya hapo nilikuja kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) mchunzi ukiwa unatokota na unga wa shayiri umekandwa na tayari kutiwa katika tanuri. Nilimwambia: "Nimeandaa chakula. Njoo wewe na mtu au watu wawili." Akasema: "Huo unatosha kiasi gani?" Nikamtajia. Akasema: "Wengi ni bora, mwambie mkeo asiepue chungu, motoni wala mikate katika tanuri hadi nije." Kisha akawambia Swahaba zake: "Twendeni." Wakasimama Muhaajiruun na Answaar. Nikaingia kwa mke wangu nikamwambia: "Umebarikiwa! Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), Muhaajiruun na Answaar wote wanakuja." Akasema: "Je, alikuuliza?" Nikasema: "Ndio." Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alifika hapo na kuwaambia Swahaba zake: "Ingieni wala msisongamane." Akawa anakata mikate, na juu yake anaweka nyama. Anatoa mchuzi kwenye chungu na mikate kutoka kwa tanuri, kisha akaifunika na kuwapa Swahaba zake. Kisha anarudia, hakuacha hilo mpaka wakashiba na kikabaki. Akasema: "Kula hiki chakula na ukigawe, kwani watu wamepata njaa." [Al-Bukhaariy na Muslim]

Katika riwaayah: Jaabir amesema: "Khandaq lilipofukuliwa, nilimuona Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ana njaa. Hivyo nilikwenda kwa mke wangu na kumuuliza: "Una kitu chochote kwani nimemuona Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ana njaa kali?" Alitoa mkoba wenye pishi ya shayiri, nasi tuna mwana mbuzi. Nikamchinja, mke wangu akakanda shayiri na akaoka mkate. Nikaikata nyama na kuitia chunguni. Kisha nilikwenda kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), Akaniambia mke wangu: "Usinifedheheshe kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na walio pamoja naye." Nilikuja kwake na kumnong'oneza nikasema: "Ee Rasuli wa Allaah! Tumechinja mnyama wetu, na tuna pishi ya shayiri, njoo wewe kikundi pamoja nawe." Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), akaita: "Enyi watu wa Khandaq! Hakika Jaabir ameandaa karamu kwa hivyo nyote njooni." Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: "Msiepue chungu wala msiitoe mikate yenu mpaka nije." Nilirudi nyumbani Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akaja anaongoza watu. Nilimjia mke wangu. Akasema: "Kwako wewe." Nikasema: "Nimefanya ulivyoniamuru." Mke wangu alileta mkate, na Nabiy akautia mate yake na kuubariki, kisha akaenda kwenye chungu akatema ndani yake na kukibariki. Kisha akasema: "Muite muokaji aoke pamoja nawe, na toeni mchuzi kwenye chungu, wala msikiinue chungu (motoni)." Wao ni elfu. Naapa kwa Allaah! Walikula mpaka wakakiacha wakaondoka. Chungu chetu kimejaa kama kilivyokuwa, na ngano yetu iko kama mwanzo.







Hadiyth – 31

وعن أنسٍ رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ أَبو طَلْحَةَ لأُمِّ سُلَيمٍ : قَدْ سَمِعْتُ صَوْتَ رسول الله صلى الله عليه وسلم ضَعيفاً أعْرِفُ فيه الجُوعَ ، فَهَلْ عِنْدَكِ مِنْ شَيْءٍ ؟ فَقَالَتْ : نَعَمْ ، فَأخْرَجَتْ أقْرَاصاً مِنْ شَعِيرٍ ، ثُمَّ أخَذَتْ خِمَاراً لَهَا ، فَلَفَّتِ الخُبْزَ بِبَعْضِهِ ، ثُمَّ دَسَّتْهُ تَحْتَ ثَوْبِي وَرَدَّتْنِي بِبَعْضِهِ ، ثُمَّ أرْسَلَتْني إِلَى رسولِ الله صلى الله عليه وسلم ، فَذَهَبتُ بِهِ ، فَوَجَدْتُ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم ، جَالِساً في المَسْجِدِ ، وَمَعَهُ النَّاسُ، فَقُمْتُ عَلَيْهمْ، فَقَالَ لي رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( أرْسَلَكَ أَبو طَلْحَةَ ؟ )) فقلت : نَعَمْ ، فَقَالَ : (( ألِطَعَامٍ ؟ )) فقلت : نَعَمْ ، فَقَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( قُومُوا )) فَانْطَلَقُوا وَانْطَلَقْتُ بَيْنَ أيْدِيهِمْ حَتَّى جِئْتُ أَبَا طَلْحَةَ فَأخْبَرْتُهُ ، فَقَالَ أَبو طَلْحَةَ : يَا أُمَّ سُلَيْمٍ ، قَدْ جَاءَ رسول الله صلى الله عليه وسلم بالنَّاسِ وَلَيْسَ عِنْدَنَا مَا نُطْعِمُهُمْ ؟ فَقَالَتْ : الله وَرَسُولُهُ أعْلَمُ . فَانْطَلَقَ أَبو طَلْحَةَ حَتَّى لَقِيَ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم ، فَأقْبَلَ رسول الله صلى الله عليه وسلم مَعَهُ حَتَّى دَخَلاَ ، فَقَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( هَلُمِّي مَا عِنْدَكِ يَا أُمَّ سُلَيْمٍ )) فَأتَتْ بِذلِكَ الخُبْزِ ، فَأمَرَ بِهِ رسول الله صلى الله عليه وسلم فَفُتَّ ، وَعَصَرَتْ عَلَيْهِ أمُّ سُلَيْمٍ عُكّةً فَآدَمَتْهُ، ثُمَّ قَالَ فِيهِ رسول الله صلى الله عليه وسلم مَا شَاءَ اللهُ أنْ يَقُولَ ، ثُمَّ قَالَ : (( ائْذَنْ لِعَشْرَةٍ )) فأذنَ لَهُمْ فَأكَلُوا حتى شَبِعُوا ثُمَّ خَرَجُوا ، ثُمَّ قَالَ : (( ائْذَنْ لِعَشْرَةٍ )) فأذِنَ لهم حَتَّى أكَلَ الْقَوْمُ كُلُّهُمْ وَشَبِعُوا وَالقَوْمُ سَبْعُونَ رَجُلاً أَو ثَمَانُونَ . متفقٌ عَلَيْهِ .

وفي رواية : فَمَا زَالَ يَدْخُلُ عَشرَة ، وَيخرجُ عشرةٌ حَتَّى لَمْ يَبْقَ مِنْهُمْ أحَدٌ إِلاَّ دَخَلَ ، فَأكَلَ حَتَّى شَبعَ ، ثُمَّ هَيَّأهَا فَإذَا هِيَ مِثْلُهَا حِيْنَ أكَلُوا مِنْهَا .

وفي رواية : فَأَكَلُوا عَشرَةً عَشرةً ، حَتَّى فَعَلَ ذَلِكَ بِثَمَانِينَ رَجُلاً ، ثُمَّ أكَلَ النبيُّ صلى الله عليه وسلم بَعْدَ ذَلِكَ وَأهْلُ البَيْتِ ، وَتَرَكُوا سُؤْراً .

وفي رواية : ثُمَّ أفْضَلُوا مَا بَلَغُوا جيرانَهُمْ .

وفي رواية عن أنس ، قَالَ : جِئتُ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم يوماً ، فَوَجَدْتُهُ جَالِساً مَعَ أصْحَابِه ، وَقَدْ عَصَبَ بَطْنَهُ ، بِعِصَابَةٍ ، فقلتُ لِبَعْضِ أصْحَابِهِ : لِمَ عَصَبَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم بَطْنَهُ ؟ فقالوا : مِنَ الجوعِ ، فَذَهَبْتُ إِلَى أَبي طَلْحَةَ ، وَهُوَ زَوْجُ أُمِّ سُلَيْمٍ بِنْت مِلْحَانَ ، فقلتُ : يَا أبتَاهُ ، قَدْ رَأيْتُ رسول الله صلى الله عليه وسلم عَصَبَ بَطْنَهُ بِعِصَابَةٍ ، فَسَألْتُ بَعْضَ أصْحَابِهِ ، فقالوا : من الجُوعِ . فَدَخَلَ أَبو طَلْحَةَ عَلَى أُمِّي ، فَقَالَ : هَلْ مِنْ شَيءٍ ؟ قالت : نَعَمْ ، عِنْدِي كِسَرٌ مِنْ خُبْزٍ وَتَمَرَاتٌ ، فَإنْ جَاءنَا رسول الله صلى الله عليه وسلم وَحْدَهُ أشْبَعْنَاهُ ، وَإنْ جَاءَ آخَرُ مَعَهُ قَلَّ عَنْهُمْ ... وَذَكَرَ تَمَامَ الْحَدِيثِ .

Kutoka kwa Anas amesema: Abuu Twalhah alimwambia Ummu Sulaym (Radhwiya Allaahu 'anhaa): "Nimesikia sauti ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ni dhaifu, najua ana njaa. Una chochote?" Akasema: "Ndio." Akatoa mikate ya shayiri, kisha akachukua khimaar yake na kufinika mkate kwa sehemu yake, na kuificha ndani ya nguo yangu, kisha akanituma kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) nikaenda nao, nikamkuta Rasuli wa Allaah amekaa Msikitini pamoja na watu. Nilisimama mbele yao, Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: "Umetumwa na Abuu Twalhah?" Nikasema: "Ndio." Akasema: "Je, ni chakula?" Nikasema: "Ndio." Akasema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Inukeni" Wakaondoka, nikatembea mbele yao, hadi nikamfikia Abuu Twalhah (Radhwiya Allaahu 'anhu) nilimwarifu yaliyojiri Msikitini. Abuu Twalhah akasema: "Ee Umm Sulaym! Hakika Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amekuja na watu nasi hatuna cha kuwalisha." Akasema: "Allaah na Rasuli Wake wanajua zaidi." Abuu Twalhah alitoka mpaka akakutana na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), naye alifuatana na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) hadi wakaingia nyumbani. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: "Ee Umm Sulaym! Lete ulichonacho." Akaleta mikate, Rasuli wa Allaah akaamuru ikakatwa katwa. Umm Sulaym akaitia siagi kwenye chupa kutayarisha mchuzi. Kisha Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alisema alichomjaalia Allaah kusema, kisha akasema: "Waruhusuni watu kumi." Wakaruhusiwa wakala mpaka wakashiba, kisha wakatoka. Kisha akasema: "Waruhusuni watu kumi." Wakaruhusiwa wakala mpaka wakashiba, kisha wakatoka. Kisha akasema: "Waruhusuni watu kumi." Wakaruhusiwa wakala mpaka wakashiba, kisha wakatoka. Na idadi ya watu ilikuwa ni sabiini au themanini. [Al-Bukhaariy na Muslim].

Katika riwaayah: "Hawakuacha kuingia kumi, na kutoka kumi mpaka hakubakia wakamalizika wote yoyote isipokuwa aliingia, akala hadi akashiba. Kisha wakakikusanya kikawa mfano wa kilicholiwa walipoanza kula."

Katika riwaayah: "Wakala watu kumi kumi mpaka wakafika themanini. Kisha akala Nabiy (swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), baadae ahlul bayt, wakaacha mabaki.

Katika riwaayah: "Kisha kilichobakia kiligawiwa majirani."

Katika riwaayah ya Anas amesema: "Nilimjia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) siku moja, Nikamkuta amekaa na Swahaba zake, Amefunga tumbo lake kwa mkanda; Nikauliza baadhi ya Swahaba zake: "Kwa nini Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amefunga tumbo lake?" Wakasema: "Kutokana na njaa." Nikaenda kwa Abuu Twalhah, mume wa Umm Sulaym bint Milhaan nikamwambia: "Ee babangu! Nimemwona Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amefunga tumbo lake kwa mkanda, Nikauliza baadhi ya Swahaba zake wakasema: "NI kutokana na njaa." Abuu Twalhah akaingia kwa mamangu, akasema: kumwambia: "Kuna chochote?" Akasema: "Ndio, nina vipande vya mkate na tende. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akitujia peke yake tutamshibisha, Akija mwingine pamoja nae kitakuwa kidogo." Akataja Hadiyth kamili.
 
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn



باب القناعة والعَفاف والاقتصاد في المعيشة والإنفاق وذم السؤال من غير ضرورة

57-Mlango Wa Kukinai, Utohara na Kukusuru Katika Maisha na Kutoa na Uovu Wa Kuomba Bila Ya Dharura



Alhidaaya.com







قَالَ الله تَعَالَى:

وَمَا مِن دَابَّةٍ فِي الْأَرْضِ إِلَّا عَلَى اللَّـهِ رِزْقُهَا ﴿٦﴾

Na hakuna kiumbe chochote kitembeacho katika ardhi isipokuwa riziki yake iko kwa Allaah; [Huwd: 6]



لِلْفُقَرَاءِ الَّذِينَ أُحْصِرُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ لَا يَسْتَطِيعُونَ ضَرْبًا فِي الْأَرْضِ يَحْسَبُهُمُ الْجَاهِلُ أَغْنِيَاءَ مِنَ التَّعَفُّفِ تَعْرِفُهُم بِسِيمَاهُمْ لَا يَسْأَلُونَ النَّاسَ إِلْحَافًا ۗ ﴿٢٧٣﴾

(Swadaqah ni) Kwa ajili ya mafakiri waliozuilika katika njia ya Allaah hawawezi kwenda huku na kule katika ardhi (kutafuta rizki); asiyewajua huwadhania kuwa ni matajiri kutokana na staha ya kujizua kwao, unawatambua kwa alama zao, hawaombi watu kwa ung’ang’anizi. [Al-Baqarah: 273]



وَالَّذِينَ إِذَا أَنفَقُوا لَمْ يُسْرِفُوا وَلَمْ يَقْتُرُوا وَكَانَ بَيْنَ ذَٰلِكَ قَوَامًا ﴿٦٧﴾

Na wale ambao wanapotoa huwa hawafanyi israfu na wala hawafanyi uchoyo na wanakuwa wastani baina ya hayo. [Al-Furqaan: 67]



وَمَا خَلَقْتُ الْجِنَّ وَالْإِنسَ إِلَّا لِيَعْبُدُونِ ﴿٥٦﴾ مَا أُرِيدُ مِنْهُم مِّن رِّزْقٍ وَمَا أُرِيدُ أَن يُطْعِمُونِ ﴿٥٧﴾

Na Sikuumba majini na wana Aadam isipokuwa waniabudu. Sitaki kutoka kwao riziki yoyote, na wala Sitaki wanilishe. [Adh-Dhaariyaat: 56-57]







Hadiyth – 1

عن أَبي هريرة رضي الله عنه ، عن النبي صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( لَيْسَ الغِنَى عَن كَثرَةِ العَرَض ، وَلكِنَّ الغِنَى غِنَى النَّفْسِ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) toka kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Utajiri si wingi wa mali, lakini utajiri ni kutosheka katika nafsi." [Al-Bukhaariy na Muslim]





Hadiyth – 2

وعن عبد الله بن عمرو رضي الله عنهما : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( قَدْ أفْلَحَ مَنْ أسْلَمَ ، وَرُزِقَ كَفَافاً ، وقَنَّعَهُ الله بِمَا آتَاهُ )) رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa 'Abdillaah bin 'Amruw bin Al-'Aaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakika amefanikiwa aliyesilimu na ikawa riziki yake ni yenye kumtosha na akakinaika kwa anachopewa na Allaah." [Muslim]





Hadiyth – 3

وعن حكيم بن حزام رضي الله عنه ، قَالَ : سألتُ رسول الله صلى الله عليه وسلم فَأعْطَانِي ، ثُمَّ سَألْتُهُ فَأَعْطَانِي ، ثُمَّ سَألْتُهُ فَأعْطَانِي ، ثُمَّ قَالَ : (( يَا حَكِيم ، إنَّ هَذَا المَالَ خَضِرٌ حُلْوٌ ، فَمَنْ أخَذَهُ بِسَخَاوَةِ نَفسٍ بُورِكَ لَهُ فِيهِ ، وَمَنْ أخَذَهُ بإشرافِ نَفسٍ لَمْ يُبَارَكْ لَهُ فِيهِ ، وَكَانَ كَالَّذِي يَأكُلُ وَلاَ يَشْبَعُ ، وَاليَدُ الْعُلْيَا خَيْرٌ مِنَ اليَدِ السُّفْلَى )) قَالَ حكيم : فقلتُ : يَا رسول الله ، وَالَّذِي بَعَثَكَ بِالحَقِّ لاَ أرْزَأُ أحَداً بَعْدَكَ شَيْئاً حَتَّى أُفَارِقَ الدُّنْيَا ، فَكَانَ أَبُو بَكْرٍ رضي الله عنه يَدْعُو حَكيماً لِيُعْطِيَه العَطَاء ، فَيَأبَى أنْ يَقْبَلَ مِنْهُ شَيْئاً ، ثُمَّ إنَّ عُمَرَ رضي الله عنه دَعَاهُ لِيُعْطِيَه فَأَبَى أنْ يَقْبَلَهُ . فقالَ : يَا مَعْشَرَ المُسْلِمِينَ ، أُشْهِدُكُمْ عَلَى حَكيمٍ أنّي أعْرِضُ عَلَيْهِ حَقَّهُ الَّذِي قَسَمَهُ اللهُ لَهُ في هَذَا الفَيء فَيَأبَى أنْ يَأخُذَهُ . فَلَمْ يَرْزَأْ حَكيمٌ أحَداً مِنَ النَّاسِ بَعْدَ النبي صلى الله عليه وسلم حَتَّى تُوُفِّي . متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Hakiym bin Hizaam (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: "Nilimuomba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) naye akanipatia, kisha nikamwuomba mara nyengine, naye akanipa. Kisha nikamuomba tena naye akanipatia. Hapo akaniambia: "Ee Hakiym! Hakika hii mali ni kijani na ni tamu. Mwenye kuichukua kwa nafsi ya upaji atabarikiwa, na mwenye kuichukua kutaka nayo utukufu hatabarikiwa. Naye anakuwa mfano wa mlaji asiyeshiba. Na mkono wa juu ni bora kuliko mkono wa chini." Akasema Hakiym (Radhwiya Allaahu 'anhu) nikasema: "Ee Rasuli wa Allaah! Naapa kwa aliyekutuma kwa haki, sitamuomba yeyote mpaka nitakapoaga dunia." Abuu Bakr (Radhwiya Allaahu 'anhu) alikuwa akimuiita Hakiym ampe, anakataa kupokea. Kisha "Umar (Radhwiya Allaahu 'anhu) alimuiita ampe akakataa kupokea. 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhu) alisema: "Enyi kongamano la Waislamu! Shuhudieni kuwa juu ya Hakiym kuwa nilimpa haki yake aliyomgawia Allaah katika ngawira amekataa kuichukua." Hivyo Hakiym hakumuomba yoyote baada ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) mpaka amekufa." [Al-Bukhaariy, Muslim, At-Tirmidhiy na An-Nasaai]







Hadiyth – 4

وعن أَبي بردة ، عن أَبي موسى الأشعري رضي الله عنه ، قَالَ : خَرَجْنَا مَعَ رسول الله صلى الله عليه وسلم في غَزاةٍ وَنَحْنُ سِتَّةُ نَفَرٍ بَيْنَنَا بَعِيرٌ نَعْتَقِبُهُ ، فَنقِبَت أقدَامُنَا وَنَقِبَت قَدَمِي ، وسَقَطت أظْفَاري ، فَكُنَّا نَلُفُّ عَلَى أرْجُلِنا الخِرَقَ ، فَسُمِّيَت غَزْوَةَ ذَاتِ الرِّقَاعِ لِمَا كُنَّا نَعْصِبُ عَلَى أرْجُلِنَا مِنَ الخِرَقِ ، قَالَ أَبُو بُردَة : فَحَدَّثَ أَبُو مُوسَى بِهَذَا الحَدِيثِ ، ثُمَّ كَرِه ذَلِكَ ، وقال : مَا كُنْتُ أصْنَعُ بِأنْ أذْكُرَهُ ! قَالَ : كأنَّهُ كَرِهَ أنْ يَكُونَ شَيْئاً مِنْ عَمَلِهِ أفْشَاهُ . متفقٌ عَلَيْهِ .

Na imepokewa kutoka kwa Abuu Burdah kwa Abuu Muwsaa Al-'Ash'ariy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa: Tulikuwa pamoja na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuelekea vitani, tulikuwa watu sita tukipanda ngamia mmoja kwa zamu. Nyayo zetu zilipasuka, miguu yangu ikapasuka kucha zangu za miguu zikatoka. Ili kufunika majeraha, tulifunga miguu yetu matambara, kwa hiyo vikaitwa Dhaatur Riqaai, kwa sababu ya kufunga matambara miguuni mwetu. Akasema Abuu Burdah: "Abuu Muwsaa alihadithia kisa hiki kisha akachukia hilo, akasema: Sikufanya hilo ilinikumbukwe." Akasema: "Kana kwamba amechukia kufichua matendo yake (ya Jihaad) [Al-Bukhaariy na Muslim]





Hadiyth – 5

وعن عمرو بن تَغْلِبَ – بفتح التاء المثناة فوق وإسكان الغين المعجمة وكسر اللام - رضي الله عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم أُتِي بِمالٍ أَوْ سَبْيٍ فَقَسَّمَهُ ، فَأعْطَى رِجَالاً ، وَتَرَكَ رِجَالاً ، فَبَلغَهُ أنَّ الَّذِينَ تَرَكَ عَتَبُوا ، فَحَمِدَ اللهَ ، ثُمَّ أثْنَى عَلَيْهِ ، ثُمَّ قَالَ : (( أمَّا بعْدُ ، فَواللهِ إنِّي لأُعْطِي الرَّجُلَ وَأدَعُ الرَّجُلَ ، وَالَّذِي أدَعُ أحَبُّ إلَيَّ مِنَ الَّذِي أُعْطِي ، وَلَكِنِّي إنَّمَا أُعْطِي أقْوَاماً لِمَا أرَى في قُلُوبِهِمْ مِنَ الجَزَعِ وَالهَلَعِ ، وَأكِلُ أقْوَاماً إِلَى مَا جَعَلَ اللهُ في قُلُوبِهم مِنَ الغِنَى وَالخَيْرِ ، مِنْهُمْ عَمْرُو بنُ تَغْلِبَ )) قَالَ عَمْرُو بنُ تَغْلِبَ : فَوَاللهِ مَا أُحِبُّ أنَّ لِي بِكَلِمَةِ رسول الله صلى الله عليه وسلم حُمْرَ النَّعَم . رواه البخاري .

Imepokewa kutoka kwa 'Amruw bin Taghlib (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba aliletewa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) mali au ngawira akaigawa. Aliwapa baadhi ya watu na kuwaacha wengine. Ikamfikia kwamba ambao amewaacha wamelalamika, Basi Akamhimidi Allaah, Akamsifu, kisha akasema: "Amma Ba'ad, Wa-Allaahi! Mimi nampa mtu na namuacha mwingine, ninayemnyima nampenda zaidi kuliko ninayempa. Ninawapa watu niwaonao mioyoni mwao babaiko na papara, na wengine nawaegemeza kwenye majaliwa ya Allaah mioyoni mwao, ukwasi na kheri, miongoni mwao ni 'Amruw bin Taghlib." Akasema 'Amruw bin Taghlib (Radhwiya Allaahu 'anhu) : "Naapa kwa Allaah! Sipendi mbadala wa maneno ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) hata kwa ngamia wekundu, (ambao walikuwa wakithaminiwa sana na Waarabu)." [Al-Bukhaariy]





Hadiyth – 6

وعن حكيم بن حزام رضي الله عنه : أنَّ النَّبيَّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( اليَدُ العُلْيَا خَيْرٌ مِنَ اليَدِ السُّفْلَى ، وَابْدَأْ بِمَنْ تَعُولُ ، وَخَيْرُ الصَّدَقَةِ مَا كَانَ عَنْ ظَهْرِ غِنىً ، وَمَنْ يَسْتَعْفِفْ يُعِفُّهُ الله ، وَمَنْ يَسْتَغْنِ يُغنهِ الله )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwake Hakiym bin Hizaam: Kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mkono wa juu ni bora kuliko mkono wa chini, anza kwa wanaokutegemea. Na bora ya swadaqah ni ilio nje ya kujitosha, Mwenye kujichunga Allaah atamwezesha. Na Mwenye kujitosha Allaah atamtosha." [Al-Bukhaariy na Muslim]





Hadiyth – 7

وعن أَبي عبد الرحمان معاوية بن أبي سفيان رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( لاَ تُلْحِفُوا في الْمَسْأَلَةِ ، فَوَاللهِ لاَ يَسْأَلُنِي أَحَدٌ مِنْكُمْ شَيْئاً ، فَتُخْرِجَ لَهُ مَسْأَلَتُهُ مِنِّي شَيْئاً وَأنَا لَهُ كَارهٌ ، فَيُبَارَكَ لَهُ فِيمَا أعْطَيْتُهُ )) رواه مسلم .

Na imepokewa kutoka kwa Abuu Sufyaan |Swakhr bin Harb (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Msing'ang'anie katika kuuliza. Wa-Allaahi! Haniombi miongoni mwenu chochote, na nikampatia hicho alichoomba nami nachukia habarikiwi katika nilichompa." [Muslim]





Hadiyth – 8

وعن أَبي عبدِ الرحمان عوف بن مالِك الأَشْجَعِيِّ رضي الله عنه ، قَالَ : كُنَّا عِنْدَ رسول الله صلى الله عليه وسلم تِسْعَةً أَوْ ثَمَانِيَةً أَوْ سَبْعَةً ، فَقَالَ : (( ألاَ تُبَايِعُونَ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم )) وَكُنَّا حَديثِي عَهْدٍ ببَيْعَةٍ ، فَقُلْنَا : قَدْ بَايَعْنَاكَ يَا رسولَ اللهِ ، ثمَّ قالَ : (( ألا تُبَايِعُونَ رسولَ اللهِ )) فَبَسَطْنا أيْدينا ، وقلنا : قدْ بايعناكَ فَعَلامَ نُبَايِعُكَ ؟ قَالَ : (( عَلَى أنْ تَعْبُدُوا اللهَ وَلاَ تُشْرِكُوا بِهِ شَيْئاً ، وَالصَّلَوَاتِ الخَمْسِ وَتُطِيعُوا الله )) وأَسَرَّ كَلِمَةً خَفِيفَةً (( وَلاَ تَسْألُوا النَّاسَ شَيْئاً )) فَلَقَدْ رَأيْتُ بَعْضَ أُولئِكَ النَّفَرِ يَسْقُطُ سَوطُ أحَدِهِمْ فَمَا يَسأَلُ أحَداً يُنَاوِلُهُ إيّاهُ . رواه مسلم .

Na imepokewa kutoka kwake Abuu 'Abdir-Rahmaan 'Awf bin Maalik Al-Ashja'iy (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema kuwa: Tulikuwa pamoja na Rasuli wa Allaah watu wa tisa au nane au saba, akasema: "Kwa nini hamum-bai' Rasuli wa Allaah? Tukanyoosha mikono yetu tukasema: Tumekubali (Bay'ah) ee Rasuli wa Allaah? Je, tukuba'i juu ya nini?" Akasema: "Juu ya kumuabudu Allaah wa msimshirikishe na chochote, na Swalaah tano, hafifu: (taratibu): "Wala msiwaombe watu chochote." Hakika nimeona baadhi ya watu hao hata akaiangukwa na kikoto (kiboko), haombi yoyote kumuokotea." [Muslim]





Hadiyth – 9

وعن ابن عمر رضي الله عنهما: أنَّ النَّبيَّ صلى الله عليه وسلم، قَالَ: (( لاَ تَزَالُ الْمَسْأَلةُ بأَحَدِكُمْ حَتَّى يَلْقَى الله تَعَالَى وَلَيْسَ في وَجْهِهِ مُزْعَةُ لَحْمٍ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwake Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Itabaki kuomba kwa mmoja wenu hadi atakapokutana na Allaah Ta'aalaa na hana katika uso wake kipande cha nyama." [Al-Bukhaariy, Muslim na An-Nasaai]





Hadiyth – 10

وعن ابن عمر رضي الله عنهما : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم قَالَ وَهُوَ عَلَى المِنْبَرِ ، وَذَكَرَ الصَّدَقَةَ وَالتَّعَفُّفَ عَنِ الْمَسْأَلَةِ : (( اليَدُ العُلْيَا خَيْرٌ مِنَ اليَدِ السُّفْلَى ، وَاليَدُ العُلْيَا هِيَ المُنْفِقَةُ ، وَالسُّفْلَى هِيَ السَّائِلَةُ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Na imepokewa kutoka kwa Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alizungumza kuhusu swadaqah na kutoomba akiwa juu ya minbar na akasema: "Mkono wa juu ni bora kuliko mkono wa chini. Mkono wa juu ni wenye kutoa na wa chini ni wenye kuomba." [Al-Bukhaariy na Muslim]





Hadiyth – 11

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( مَنْ سَألَ النَّاسَ تَكَثُّراً فإنَّمَا يَسْألُ جَمْراً ؛ فَلْيَسْتَقِلَّ أَوْ لِيَسْتَكْثِرْ )) رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye kuomba watu ili mali yake iongezeke, hakika yeye anaomba kaa la moto. Hivyo ni juu yake ima kupunguza au kuongeza." [Muslim]





Hadiyth – 12

وعن سَمُرَةَ بنِ جُنْدبٍ رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( إنَّ المَسْأَلَةَ كَدٌّ يَكُدُّ بِهَا الرَّجُلُ وَجْهَهُ ، إِلاَّ أنْ يَسْأَلَ الرَّجُلُ سُلْطاناً أَوْ في أمْرٍ لاَ بُدَّ مِنْهُ )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن صحيح )) .

Imepokewa kutoka kwake Samurah bin Jundub (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakika kuomba inamjeruhi mtu uso wake isipokuwa anapomuomba mtu sultani au kwa jambo ambalo hapana budi (ila kuomba)." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]





Hadiyth – 13

وعن ابن مسعود رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( مَنْ أصَابَتْهُ فَاقَةٌ فَأنْزَلَهَا بالنَّاسِ لَمْ تُسَدَّ فَاقَتُهُ ، وَمَنْ أنْزَلَهَا باللهِ ، فَيُوشِكُ اللهُ لَهُ بِرِزْقٍ عَاجِلٍ أَوْ آجِلٍ )) رواه أَبُو داود والترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .

Imepokewa kutoka kwa Ibn Mas'uwd (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Yeyote mwenye kupatwa na shida (kama njaa na ufakiri), kisha akaipeleka kwa watu ili wamsaidie, shida yake hiyo haitaondoka (kutaka uasidizi) kwa Allaah basi ataondoshewa na Allaah kwa haraka na kupatiwa riziki kwa wakati wa karibu au baadae." [Abuu Daawud na At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]





Hadiyth – 14

وعن ثوبان رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( مَنْ تَكَفَّلَ لِي أنْ لاَ يَسْأَلَ النَّاسَ شَيْئاً ، وَأتَكَفَّلُ لَهُ بِالْجَنَّةِ ؟ )) فقلتُ : أنَا ، فَكَانَ لاَ يَسْأَلُ أحَداً شَيْئاً . رواه أَبُو داود بإسناد صحيح .

Imepokewa kutoka kwake Thawbaan (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Yeyote atakaye nidhaminia kwamba hatamuuliza (kuomba) mtu yeyote kwa kitu chochote basi kwake nitamdhaminia Pepo. Nikasema: 'MImi.' Baada ya hapo hakumuomba (yaani Thawbaan) mtu yoyote kitu chochote." [Abuu Daawud kwa Isnaad iliyo Swahiyh]





Hadiyth – 15

وعن أَبي بِشْرٍ قَبيصَةَ بنِ المُخَارِقِ رضي الله عنه ، قَالَ : تَحَمَّلْتُ حَمَالَةً فَأتَيْتُ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم أسْأَلُهُ فِيهَا ، فَقَالَ : (( أقِمْ حَتَّى تَأتِيَنَا الصَّدَقَةُ فَنَأمُرَ لَكَ بِهَا )) ثُمَّ قَالَ : (( يَا قَبيصةُ ، إنَّ المَسْأَلَةَ لاَ تَحِلُّ إِلاَّ لأَحَدِ ثلاثَةٍ : رَجُلٌ تحمَّلَ حَمَالَةً ، فَحَلَّتْ لَهُ المَسْأَلَةُ حَتَّى يُصِيبَها ، ثُمَّ يُمْسِكُ ، وَرَجُلٌ أصَابَتْهُ جَائِحَةٌ اجْتَاحَتْ مَالَهُ ، فَحَلَّتْ لَهُ الْمَسْأَلَةُ حَتَّى يُصِيبَ قواماً مِنْ عَيش - أَوْ قَالَ : سِدَاداً مِنْ عَيْشٍ - وَرَجُلٌ أصَابَتْهُ فَاقَةٌ ، حَتَّى يَقُولَ ثَلاَثَةٌ مِنْ ذَوِي الحِجَى مِنْ قَوْمِه : لَقَدْ أصَابَتْ فُلاناً فَاقَةٌ . فَحلَّتْ لَهُ الْمَسْأَلَةُ حَتَّى يصيب قواماً من عيش ، أَوْ قَالَ : سداداً من عيشِ ، فما سِوَاهُنَّ مِنَ المسألَةِ يَا قَبِيصَةُ سُحْتٌ ، يَأكُلُهَا صَاحِبُهَا سُحْتاً )) رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Abuu Bishr Qabiyswah bin Al-Mukhaariq amesema: Nilibeba dhamana ya fidia ya mauaji. Nilimwendea Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kumuulizia hilo. Akasema (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Ngojea mpaka itujie swadaqah tutakuamrishia chochote." Kisha akasema: "Ee Qabiyswah! Hakika kuomba si halali ila kwa moja ya matatu: Mtu anayedaiwa, ni halali kwake kuomba hadi alipate, kisha ajizuie; Na mtu amepata maafa mali yake ikaharibika ni halali kwake kuomba mpaka apate msimamo katika maisha- au alisema:' "Kukidhi maisha." Na mtu amepata ufukara, mpaka waseme watu watatu wenye akili katika watu wake: 'fulani amepata njaa.' Ni halali kwake kuomba mpaka apate msimamo wa maisha au alisema, "Kukidhi maisha." Wasiokuwa hawa kuomba ee Qabiyswah ni haramu, anaekula anakula haramu." [Muslim]





Hadiyth – 16

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( لَيْسَ المسكينُ الَّذِي يَطُوفُ عَلَى النَّاسِ تَرُدُّهُ اللُّقْمَةُ وَاللُّقْمَتَانِ ، وَالتَّمْرَةُ وَالتَّمْرَتَانِ ، وَلكِنَّ المِسكينَ الَّذِي لاَ يَجِدُ غِنىً يُغْنِيهِ ، وَلاَ يُفْطَنُ لَهُ فَيُتَصَدَّقُ عَلَيْهِ ، وَلاَ يَقُومُ فَيَسْألَ النَّاسَ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Masikini si yule anaeranda kwa watu anarudishwa kwa tonge moja au mbili, tende moja na tende mbili, Ila masikini ni asiyepata cha kumtosheleza wala hakuna anayemjua ili ampe swadaqah, wala hasimami kuomba watu." [Al-Bukhaariy na Muslim].
 
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn



باب جواز الأخذ من غير مسألة وَلاَ تطلع إليه

058-Mlango Wa Ruhusu ya Kuchukua Kitu Bila Kuomba



Alhidaaya.com





عن سالم بن عبد الله بن عمر ، عن أبيه عبد الله بن عمر ، عن عمر رضي الله عنه ، قَالَ : كَانَ رسول الله صلى الله عليه وسلم يُعْطيني العَطَاءَ ، فَأقُولُ : أعطِهِ مَنْ هُوَ أفْقَرُ إِلَيْهِ مِنّي . فَقَالَ : (( خُذْهُ ، إِذَا جَاءكَ مِنْ هَذَا المَال شَيْءٌ وَأنْتَ غَيْرُ مُشْرِفٍ وَلاَ سَائِلٍ ، فَخُذْهُ فَتَمَوَّلْهُ ، فَإنْ شِئْتَ كُلْهُ ، وَإنْ شِئْتَ تَصَدَّقْ بِهِ ، وَمَا لا ، فَلاَ تُتبعهُ نَفْسَكَ )) قَالَ سَالِمٌ : فَكَانَ عَبدُ الله لاَ يَسألُ أحَداً شَيْئاً ، وَلاَ يَرُدُّ شَيْئاً أُعْطِيَه . متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Saalim bin 'Abdillaah bin 'Umar kutoka kwa babake 'Abdillaah bin 'Umar kutoka kwa 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba amesema: "Rasuli wa Alllaah (Swallla Alllahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akinipatia vitu (zawadi), nami nilikuwa nasema, 'Mpatie aliye fukara kuliko mimi.' Akasema: 'Chukua ikiwa utapewa katika mali hii kitu chochote bila ya wewe kutamani wala kuuliza (kuomba). Ichukue na uitie katika rasilimali au ukitaka itumie na ukitaka unaweza kuitoa swadaqah. Usitamani kupata kitu kwa njia nyengine.' Amesema Saalim: 'Alikuwa 'Abdillaah (yaani babake) hamuulizi (hamuombi) yeyeote kitu chochote wala harudishi kitu alichopatiwa'." [Al-Bukhaariy na Muslim]
 
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn



باب الحث عَلَى الأكل من عمل يده والتعفف به عن السؤال والتعرض للإعطاء

059-Mlango Wa Kuhimizwa Kula Kwa Kazi ya Mkono Wake na Kujizuilia Kuomba na Kupenda Kutoa



Alhidaaya.com





قَالَ الله تَعَالَى:

فَإِذَا قُضِيَتِ الصَّلَاةُ فَانتَشِرُوا فِي الْأَرْضِ وَابْتَغُوا مِن فَضْلِ اللَّـهِ ﴿١٠﴾

Na inapomalizika Swalaah, tawanyikeni katika ardhi, na tafuteni katika fadhila za Allaah, [Al-Jumua'ah: 10]







Hadiyth – 1

وعن أَبي عبد الله الزبير بن العَوَّام رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( لأَنْ يَأخُذَ أحَدُكُمْ أحبُلَهُ ثُمَّ يَأتِيَ الجَبَلَ ، فَيَأْتِيَ بحُزمَةٍ مِنْ حَطَب عَلَى ظَهْرِهِ فَيَبِيعَهَا ، فَيكُفّ اللهُ بِهَا وَجْهَهُ ، خَيْرٌ لَهُ مِنْ أنْ يَسْألَ النَّاسَ ، أعْطَوْهُ أَوْ مَنَعُوهُ )) رواه البخاري .

Imepokewa kutoka kwa Abuu 'Abdillaah Az-Zubaiyr bin Al-Awwaam (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mmoja wenu kuchukuwa kamba na kisha akaenda mlimani, akaja na mzigo wa kuni na kuziuza, Allaah akakinga uso wake, ni bora kwake kuliko kuomba watu, ima wampe au wamnyime." [Al-Bukhaariy]





Hadiyth – 2

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( لأَنْ يَحْتَطِبَ أحَدُكُمْ حُزْمَةً عَلَى ظَهْرِهِ ، خَيْرٌ لَهُ مِنْ أنْ يَسْألَ أحداً ، فَيُعْطِيَهُ أَوْ يَمْنَعَهُ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mmoja wenukubeba mzigo wa kuni mgongoni mwake ni bora kwake kuliko kuomba yoyote, ampe au amnyime." [Al-Bukhaariy, Muslim, At-Tirmidhiy, An-Nasaai na Maalik]





Hadiyth – 3

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، عن النبيِّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( كَانَ دَاوُدُ عَلَيْهِ السَّلام لا يَأكُلُ إِلاَّ مِنْ عَمَلِ يَدِهِ )) رواه البخاري.

Na imepokewa kutoka kwa Abuu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Alikuwa Daawuud ('Alayhis sallaam) hali isipokuwa kwa chumo la mkono wake." [Al-Bukhaariy]





Hadiyth – 4

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( كَانَ زَكرِيّا عَلَيْهِ السَّلام نَجَّاراً )) رواه مسلم .

Na imepokewa kutoka kwa Abuu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayni wa aalihi wa sallam) amesema: "Zakariyyaa ('Alayhi salaam) alikuwa ni seremala (akiendesha maisha yake kwa kufanya kazi hiyo)." [Muslim]





Hadiyth – 5

وعن المقدام بنِ مَعْدِ يكرِبَ رضي الله عنه ، عن النبي صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( مَا أكَلَ أَحَدٌ طَعَاماً قَطُّ خَيْراً مِنْ أنْ يَأكُلَ مِنْ عَمَلِ يَدِه ، وَإنَّ نَبيَّ الله دَاوُدَ عَلَيْهِ السَّلام كَانَ يَأكُلُ مِنْ عَمَلِ يَدِهِ )) رواه البخاري .

Imepokewa kutoka kwa Al-Miqdaam bin Ma'diykarib kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hajakula mmoja wenu chakula bora zaidi kuliko kile anachokula kwa kufanya juhudi kwa kutumia mikono yake. Na hakika Nabiy wa Allaah Daawuud alikuwa akila chakula anachopata kwa miono yake." [Al-Bukhaariy]
 
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn





باب الكرم والجود والإنفاق في وجوه الخير ثقةً بالله تعالى

060-Mlango Wa Ukarimu na Kutoa Katika Njia za Kheri na Kuwa na Imani Kwa Allaah Ta'aalaa



Alhidaaya.com





قَالَ الله تَعَالَى:

وَمَا أَنفَقْتُم مِّن شَيْءٍ فَهُوَ يُخْلِفُهُ ۖ ﴿٣٩﴾

Na kitu chochote mtoacho, basi Yeye Atakilipa,. [Sabaa: 39]





وَمَا تُنفِقُوا مِنْ خَيْرٍ فَلِأَنفُسِكُمْ ۚ وَمَا تُنفِقُونَ إِلَّا ابْتِغَاءَ وَجْهِ اللَّـهِ ۚ وَمَا تُنفِقُوا مِنْ خَيْرٍ يُوَفَّ إِلَيْكُمْ وَأَنتُمْ لَا تُظْلَمُونَ ﴿٢٧٢﴾

Na chochote cha khayr mtoacho basi ni kwa ajili ya nafsi zenu. Na hamtoi ila kutaka Wajhi wa Allaah. Na chochote mtoacho katika khayr mtalipwa kamilifu nanyi hamtodhulumiwa.



لِلْفُ ۗ وَمَا تُنفِقُوا مِنْ خَيْرٍ فَإِنَّ اللَّـهَ بِهِ عَلِيمٌ ﴿٢٧٣﴾

Na chochote mtoacho katika khayr basi Allaah kwacho ni Mjuzi. [Al-Baqarah: 272-273]









Hadiyth – 1

وعن ابن مسعود رضي الله عنه ، عن النبيِّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( لا حَسَدَ إِلاَّ في اثْنَتَيْنِ : رَجُلٌ آتَاهُ اللهُ مَالاً ، فَسَلَّطَهُ عَلَى هَلَكَتِهِ في الحَقّ ، وَرَجُلٌ آتَاهُ اللهُ حِكْمَةً ، فَهُوَ يَقْضِي بِهَا ويُعَلِّمُهَا )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Ibn Mas'uuwd (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa; Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hapana husuda ila katika mawili: Mtu Allaah amempa mali, akamsalitisha katika kuimaliza katika haki. Na Allaah amempa mtu hekima, anahukumu nayo na anawaelimisha wengine." [Al-Bukhaariy na Muslim]





Hadiyth – 2

وعن ابن مسعود رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( أيُّكُم مَالُ وَارِثِهِ أحبُّ إِلَيْهِ مِنْ مَالِهِ ؟ )) قالوا : يَا رسول اللهِ ، مَا مِنَّا أحَدٌ إِلاَّ مَالُهُ أحَبُّ إِلَيْهِ . قَالَ : (( فإنَّ مَالَهُ مَا قَدَّمَ وَمَالَ وَارِثِهِ مَا أخَّرَ )) رواه البخاري .

Imepokewa kutoka kwa Ibn Mas'uuwd (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Ni mtu gani miongoni mwenu ambaye anaipenda zaidi mali ya warithi wake kuliko mali yake mwenyewe?" Tukasema: "Ee Rasuli wa Allaah! Hakuna miongoni mwetu isipokuwa anaipenda mali yake zaidi." Akasema: "Hakika mali yake ni ile aliyoitanguliza na mali aliyoibakisha ni ya warithi wake." [Al-Bukhaariy]





Hadiyth – 3

وعن عَدِيِّ بن حَاتِمٍ رضي الله عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( اتَّقُوا النَّارَ وَلَوْ بِشِقِّ تَمْرَةٍ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa 'Adiyy bin Haatim (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba amesema: "Nimemsikia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ""Ogopeni Moto ijapo kwa kipande cha tende moja." [Al-Bukhaariy na Muslim]





Hadiyth – 4

وعن جابرٍ رضي الله عنه ، قَالَ : مَا سُئِلَ رسول الله صلى الله عليه وسلم شَيْئاً قَطُّ ، فقالَ : لاَ . متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Jaabir (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba amesema: "Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) hakuwahi kuombwa kitu chochote mara zote, akasema: hapana." [Al-Bukhaariy na Muslim]





Hadiyth – 5

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( مَا مِنْ يَوْمٍ يُصبحُ العِبَادُ فِيهِ إِلاَّ مَلَكَانِ يَنْزلانِ ، فَيَقُولُ أحَدُهُمَا : اللَّهُمَّ أعْطِ مُنْفِقاً خَلَفاً ، وَيَقُولُ الآخَرُ : اللَّهُمَّ أعْطِ مُمْسِكاً تَلَفاً )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakuna siku yoyote inayopambazuka kwa waja isipokuwa Malaika wawili huteremka, mmoja wao anasema: 'Ee Mola! Mrudishie mwenye kutoa (kila anachotoa kwa wingi)'. Na mwengine naye anasema: 'Ee Mola! Mharibie mwenye kuzuia (vitu vyake)'. [Al-Bukhaariy, Muslim na Ahmad]





Hadiyth – 6

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( قَالَ الله تَعَالَى : أنفِق يَا ابْنَ آدَمَ يُنْفَقْ عَلَيْكَ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Na imepokewa tena kutoka kwa Abuu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: Amesema Allaah Ta'aalaa: "Ee mwanadamu toa (katika njia ya Allaah) na Allaah atakupatia." [Al-Bukhaariy na Muslim]





Hadiyth – 7

وعن عبد اللهِ بن عمرو بن العاص رضي الله عنهما : أنَّ رَجُلاً سَألَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : أيُّ الإسلامِ خَيْرٌ ؟ قَالَ : (( تُطْعِمُ الطَّعَامَ ، وَتَقْرَأُ السَّلاَمَ عَلَى مَنْ عَرَفْتَ وَمَنْ لَمْ تَعْرِفْ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa 'Abdillaah bin 'Amruw bin Al-'Aas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba kuna mtu mmoja aliyemuuliza Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Ni Uislamu gani ulio bora?" Akasema: "Kulisha watu chakula na kuwatolea salamu unaowajua na usiowajua." [Al-Bukhaariy na Muslim]





Hadiyth – 8

وعن عبد اللهِ بن عمرو بن العاص رضي الله عنهما ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( أرْبَعُونَ خَصْلَةً : أعْلاهَا مَنِيحةُ العَنْزِ ، مَا مِنْ عَامِلٍ يَعْمَلُ بخَصْلَةٍ مِنْهَا ؛ رَجَاءَ ثَوَابهَا وَتَصْدِيقَ مَوْعُودِهَا ، إِلاَّ أدْخَلَهُ الله تَعَالَى بِهَا الجَنَّةَ )) رواه البخاري .

Imepokewa kutoka kwa 'Abdillaah bin 'Amruu bin Al-'Aas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Sampuli arobaini za wema, ya juu kabisa ni kumwazima mtu ngamia (jike) wa maziwa ili apate maziwa (kisha amrudishie mwenyewe). Hakuna mfanyaji ambaye atafanya amali yeyote katika hizi akitarajia thawabu zake na kuswadikisha ile ahadi (aliyoahidiwa) isipokuwa Allaah humuingiza kwayo Peponi." [Al-Bukhaariy]





Hadiyth – 9

وعن أَبي أُمَامَة صُدّيِّ بن عَجْلانَ رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( يَا ابْنَ آدَمَ ، إنَّكَ أن تَبْذُلَ الفَضلَ خَيْرٌ لَكَ ، وَأن تُمْسِكَه شَرٌّ لَكَ ، وَلاَ تُلاَمُ عَلَى كَفَافٍ ، وَابْدَأْ بِمَنْ تَعُولُ ، وَاليَدُ الْعُلْيَا خَيْرٌ مِنَ الْيَدِ السُّفْلَى )) رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Abuu Umamah Sudayyi bin 'Ajlaan (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Ee mwanadamu! Hakika lau utatafutia fadhila (hela) za zaidi itakuwa bora kwako, na kuzuilia (kutotumia) ni shari kwako. Hutalaumiwa kuwa na hela kwa kadiri ya mahitaji yako. Na anza kuitumia kwa wale wenye haki kwako." [Muslim]





Hadiyth – 10

وعن أنسٍ رضي الله عنه ، قَالَ : مَا سُئِلَ رسول الله صلى الله عليه وسلم عَلَى الإسْلاَمِ شَيْئاً إِلاَّ أعْطَاهُ ، وَلَقَدْ جَاءهُ رَجُلٌ ، فَأعْطَاهُ غَنَماً بَيْنَ جَبَلَيْنِ ، فَرجَعَ إِلَى قَوْمِهِ ، فَقَالَ : يَا قَوْمِ ، أسْلِمُوا فإِنَّ مُحَمَّداً يُعطِي عَطَاءَ مَن لا يَخْشَى الفَقْر ، وَإنْ كَانَ الرَّجُلُ لَيُسْلِمُ مَا يُريدُ إِلاَّ الدُّنْيَا ، فَمَا يَلْبَثُ إِلاَّ يَسِيراً حَتَّى يَكُونَ الإسْلاَمُ أحَبَّ إِلَيْهِ مِنَ الدُّنْيَا وَمَا عَلَيْهَا . رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwake Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba amesema: Alikuwa katika Uislamu hakuombwa chochote Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) isipokuwa alimpatia. Na hakika alikuja mtu, naye akampatia mbuzi wengi sana waliojaa baina ya majabali mawili. Huyu mtu aliporudi kwa watu wake aliwaambia: "Enyi watu wangu kuweni Waislamu kwani Muhammad hutoa aina ya utoaji ambao haogopi ufakiri." Japokuwa mtu alikuwa akisilimu kwa sababu ya pato la kidunia, lakini baada ya muda mchache, Uislamu unakuwa ni mwenye kupendwa zaidi na yeye kuliko dunia na vilivyomo ndani yake." [Muslim]





Hadiyth – 11

وعن عمر رضي الله عنه ، قَالَ : قسم رسول الله صلى الله عليه وسلم قَسْماً ، فَقُلْتُ :يَا رسولَ الله ، لَغَيْرُ هؤلاَءِ كَانُوا أحَقَّ بِهِ مِنْهُمْ ؟ فَقَالَ : (( إنَّهُمْ خَيرُونِي أنْ يَسألُوني بالفُحْشِ ، أَوْ يُبَخِّلُونِي ، وَلَسْتُ بِبَاخِلٍ )) رواه مسلم

Imepokewa kutoka kwa 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aligawanya mali nami nikamwambia: "Ee Rasuli wa Allaah! Mbali na hawa kuna watu wenye haki zaidi ya kupatiwa kuliko hawa." Akasema: "Hakika wao wamenipatia uchaguzi (kutumia uamuzi wangu). Hivyo, wanatakiwa ima waniombe waziwazi, nami nitawapatia au waninasibishe na ubakhili, na mimi si bakhili." [Muslim]





Hadiyth – 12

وعن جبير بن مطعم رضي الله عنه ، قَالَ : بَيْنَمَا هُوَ يَسِيرُ مَعَ النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم مَقْفَلَهُ مِنْ حُنَيْن ، فَعَلِقَهُ الأعْرَابُ يَسْألُونَهُ ، حَتَّى اضْطَرُّوهُ إِلَى سَمُرَة ، فَخَطِفَت رِدَاءهُ ، فَوَقَفَ النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم ، فقال : (( أعْطُوني رِدَائي ، فَلَوْ كَانَ لِي عَدَدُ هذِهِ العِضَاهِ نَعَماً ، لَقَسَمْتُهُ بَينَكُمْ ، ثُمَّ لا تَجِدُونِي بَخِيلاً وَلاَ كَذّاباً وَلاَ جَبَاناً )) رواه البخاري

Imepokewa kutoka kwa Jubaiyr bin Mutw'im (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba amesema: Baada ya vita vya Hunaiyn tulikuwa tunarudi na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), baadhi ya Mabedui walimzunguka alipokuwa chini ya mti wakitaka kupatiwa fungu lao (katika ngawira) na mmoja wao akachukua shuka yake. Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasimama akasema: "Nipatieni shuka yangu; lau ningekuwa na neema nyingi sawa na idadi ya majani katika huu mchongoma ningewagawia baina yenu na hamungeniona mimi kuwa bakhili wala muongo wala mwoga?" [Al-Bukhaariy]





Hadiyth – 13

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( مَا نَقَصَتْ صَدَقَةٌ مِنْ مَال ، وَمَا زَادَ اللهُ عَبْداً بِعَفْوٍ إِلاَّ عِزّاً ، وَمَا تَواضَعَ أحَدٌ لله إِلاَّ رَفَعَهُ اللهُ عزوجل )) رواه مسلم .

Na imepokewa kutoka kwa Abuu Huraiyrah (Radhwiya Allahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Swadaqah haipunguzi mali; na Allaah anamuongezea utukufu mwenye kusamehe. Na hakuna anayenyenyekea kwa ajili ya Allaah Ta'aalaa isipokuwa humnyanyua daraja yake." [Muslim]





Hadiyth – 14

وعن أَبي كبشة عمرو بن سعد الأنماري رضي الله عنه: أنّه سمع رسول الله صلى الله عليه وسلم ، يقول : (( ثَلاَثَةٌ أُقْسمُ عَلَيْهِنَّ ، وَأُحَدِّثُكُمْ حَدِيثاً فَاحْفَظُوهُ : مَا نَقَصَ مَالُ عَبْدٍ مِنْ صَدَقَةٍ ، وَلاَ ظُلِمَ عَبْدٌ مَظْلَمَةً صَبَرَ عَلَيْهَا إِلاَّ زَادَهُ اللهُ عِزّاً ، وَلاَ فَتَحَ عَبْدٌ بَابَ مَسألَةٍ إِلاَّ فَتَحَ اللهُ عَلَيْهِ بَابَ فَقرٍ - أَوْ كَلِمَةً نَحْوَهَا - وَأُحَدِّثُكُمْ حَديثاً فَاحْفَظُوهُ، قَالَ : (( إنَّمَا الدُّنْيَا لأرْبَعَةِ نَفَرٍ : عَبْدٍ رَزَقَهُ اللهُ مَالاً وَعِلماً ، فَهُوَ يَتَّقِي فِيهِ رَبَّهُ ، وَيَصِلُ فِيهِ رَحِمَهُ، وَيَعْلَمُ للهِ فِيهِ حَقَّاً ، فَهذا بأفضَلِ المَنَازِلِ . وَعَبْدٍ رَزَقهُ اللهُ عِلْماً، وَلَمْ يَرْزُقْهُ مَالاً ، فَهُوَ صَادِقُ النِّيَّةِ ، يَقُولُ : لَوْ أنَّ لِي مَالاً لَعَمِلتُ بِعَمَلِ فُلانٍ ، فَهُوَ بنيَّتِهِ ، فأجْرُهُمَا سَوَاءٌ . وَعَبْدٍ رَزَقَهُ الله مَالاً ، وَلَمَ يَرْزُقْهُ عِلْماً ، فَهُوَ يَخبطُ في مَالِهِ بغَيرِ عِلْمٍ ، لاَ يَتَّقِي فِيهِ رَبَّهُ ، وَلاَ يَصِلُ فِيهِ رَحِمَهُ ، وَلاَ يَعْلَمُ للهِ فِيهِ حَقّاً ، فَهذَا بأَخْبَثِ المَنَازِلِ . وَعَبْدٍ لَمْ يَرْزُقْهُ اللهُ مَالاً وَلاَ عِلْماً ، فَهُوَ يَقُولُ : لَوْ أنَّ لِي مَالاً لَعَمِلْتُ فِيهِ بعَمَلِ فُلاَنٍ ، فَهُوَ بنِيَّتِهِ ، فَوِزْرُهُمَا سَوَاءٌ )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن صحيح )) .

Kutoka kwa Abuu Kabshah 'Amar bin Sa'd Al-Anmaariy amemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Matatu naapa juu yake na nakuwahadithieni hadiyth ihifadhini: Mali ya mja haipapungui kwa swadaqah, wala mja hakudhulumiwa chochote akasubiri ila Allaah humzidisha utukufu, na hatafungua mja mlango wa kuomba isipokuwa Allaah humfungulia mlango wa ufukara, au neno mfano wake." na ninakuhadithieni hadiyth ihifadhini, akasema: "Hakika dunia ni kwa watu wanne: Mja Allaah amempa mali na elimu naye akamcha Mola ndani yake, akaunganisha ndani yake kizazi, na akajua ndani yake haki ya Allaah, huyu ni daraja bora, na cheo bora; na mja aliyepatiwa na Allaah elimu bila kupewa mali, naye akawa na nia ya kweli, akasema: 'Lau kama ningekuwa na mali ningefanya amali ya fulani', yeye atakuwa katika hiyo nia yake na ujira wa wote wawili ni sawa; na mja aliyepewa na Allaah mali lakini hakuruzukiwa elimu, nae anaifuja mali yake pasi na elimu. Yeye hamchi Rabb wake kwayo na wala haungi kizazi na wala hajui haki za Allaah juu yake, huyu atakuwa katika daraja ya chini kabisa; na mja ambaye hakuruzukiwa na Allaah mali wala elimu, naye akawa anasema: 'Kwa hakika lau kama ningekuwa na mali ningefanya amali ya fulani (amali ya mtu wa tatu).' Hiyo ianpokuwa ndio nia yake, wote watakuwa na madhambi sawa." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]





Hadiyth – 15

وعن عائشة رضي الله عنها : أنَّهُمْ ذَبَحُوا شَاةً ، فَقَالَ النبيُّ صلى الله عليه وسلم : (( مَا بَقِيَ مِنْهَا ؟ )) قالت : مَا بَقِيَ مِنْهَا إِلاَّ كَتِفُها . قَالَ : (( بَقِيَ كُلُّهَا غَيْرُ كَتِفِهَا )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديث صحيح )) .

Imepokewa kutoka kwa 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kuwa wao walichinja mbuzi, (wakaigawa) kisha Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimuuliza: "Imebaki nyama kiasi gani?" Alijibu: "Haikubaki isipokuwa mkono wake." Akasema: "Imebaki nyama yote ila mkono." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Swahiyh]





Hadiyth – 16

وعن أسماء بنت أَبي بكرٍ الصديق رضي الله عنهما ، قالت : قَالَ لي رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( لاَ تُوكِي فَيُوكى عَلَيْكِ )) .

وفي رواية : (( أنفقي أَوِ انْفَحِي ، أَوْ انْضَحِي ، وَلاَ تُحصي فَيُحْصِي اللهُ عَلَيْكِ ، وَلاَ تُوعي فَيُوعي اللهُ عَلَيْكِ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwake Asmaa bint Abuu Bakr As-Swiddiyq (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) Amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliniambia: "Usikusanye Allaah akakukatia riziki."

Na katika riwaayah nyingine: "Toa swadaqah kwa mali yako au anfahiy (toa) au andhahiy (kutoa) wala usizuie mali yako kwa kuhesabu (kwa kuhofia itapungua), Allaah asije akakunyima rehma zake na wala usiwanyime watu kwa ile fadhila uliyopatiwa na hivyo Allaah akakunyima." [Al-Bukhaariy na Muslim]





Hadiyth – 17

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه : أنَّه سمع رسول الله صلى الله عليه وسلم ، يَقولُ : (( مَثَل البَخيل وَالمُنْفِقِ ، كَمَثَلِ رَجُلَيْنِ عَلَيْهِمَا جُنَّتَانِ مِنْ حَديد مِنْ ثُدِيِّهِمَا إِلَى تَرَاقِيهِمَا ، فَأَمَّا المُنْفِقُ فَلاَ يُنْفِقُ إِلاَّ سَبَغَتْ - أَوْ وَفَرَتْ - عَلَى جِلْدِهِ حَتَّى تُخْفِيَ بَنَانَهُ ، وَتَعْفُو أثرَهُ ، وأمَّا البَخِيلُ ، فَلاَ يُريدُ أنْ يُنْفِقَ شَيْئاً إِلاَّ لَزِقَتْ كُلُّ حَلْقَةٍ مَكَانَهَا ، فَهُوَ يُوسِّعُهَا فَلاَ تَتَّسِعُ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba amamsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Mfano wa bakhili na yule anayetoa, ni kama mfano wa watu wawili waliovaa juba za chuma, mikono yao imelazimika kwenda kwenye maziwa na mitulinga yao. Ama yule mkarimu (mwenye kutoa swadaqah) akawa kila anapotoa swadaqah linatanuka mpaka linafunika vidole nyake, na linafunika alama zake zote. Na ama yule bakhili hataki kutoa kitu chochote ila zile kona hushikilia mahali pake na kuzidi kumbana, naye atakuwa anaitanua na wala haitanuki." [Al-Bukhaariy na Muslim]





Hadiyth – 18

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( مَنْ تَصَدَّقَ بعَدلِ تَمْرَةٍ مِنْ كَسْبٍ طَيِّبٍ ، وَلاَ يَقْبَلُ اللهُ إِلاَّ الطَّيبَ ، فَإنَّ اللهَ يَقْبَلُهَا بِيَمِينِهِ ، ثُمَّ يُرَبِّيهَا لِصَاحِبِهَا كَمَا يُرَبِّي أحَدُكُمْ فَلُوَّهُ حَتَّى تَكُونَ مِثْلَ الجَبَلِ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye kutoa swadaqah kama tende moja, kwenye chumo zuri, Allaah hakubali isipokuwa kizuri, hakika Allaah Ataipokea kwa Mkono Wake wa kuume, kisha Atamletea (swadaqah hiyo), kama mmoja wenu anavyolea mtoto wa farasi wake, mpaka iwe kama mlima." [Al-Bukhaariy na Muslim]





Hadiyth – 19

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، عن النبيِّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( بَيْنَمَا رَجُلٌ يَمْشِي بِفَلاَةٍ مِنَ الأَرْضِ ، فَسَمِعَ صَوْتاً في سَحَابَةٍ ، اسقِ حَدِيقَةَ فُلانٍ ، فَتَنَحَّى ذَلِكَ السَّحَابُ فَأفْرَغَ مَاءهُ في حَرَّةٍ ، فإِذَا شَرْجَةٌ مِنْ تِلْكَ الشِّرَاجِ قَدِ اسْتَوْعَبَت ذَلِكَ الماءَ كُلَّهُ ، فَتَتَبَّعَ المَاءَ ، فإذَا رَجُلٌ قَائمٌ في حَدِيقَتِهِ يُحَوِّلُ الماءَ بِمسحَاتِهِ، فَقَالَ لَهُ : يَا عَبْدَ اللهِ، ما اسمُكَ ؟ قال : فُلانٌ للاسم الذي سَمِعَ في السَّحابةِ ، فقال له : يا عبدَ الله ، لِمَ تَسْألُنِي عَنِ اسْمِي ؟ فَقَالَ : إنِّي سَمِعْتُ صَوتْاً في السَّحابِ الَّذِي هَذَا مَاؤُهُ ، يقولُ : اسْقِ حَدِيقَةَ فُلاَنٍ لاسمِكَ ، فَمَا تَصْنَعُ فِيهَا ، فَقَالَ : أمَا إذ قلتَ هَذَا ، فَإنِّي أنْظُرُ إِلَى مَا يَخْرُجُ مِنْهَا ، فَأتَصَدَّقُ بِثُلُثِهِ ، وَآكُلُ أنَا وَعِيَالِي ثُلُثاً ، وَأردُّ فِيهَا ثُلُثَهُ )) رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mtu alipokuwa anatembea jangwani, alisikia sauti katika wingu (ikisema): 'Nyweshea shamba la fulani.' Wingu hilo likakaribia na kumimina maji yake kwenye ardhi ya mawe. Maji hayo yakaenea katika kijito na kumiminika katika hodhi kubwa. Akafuata maji akamuona mtu amesimama ndani ya shamba lake anagawa maji kwa jembe lake. Akamwambia: 'Ee mja wa Allaah, jina lako nani?' Akasema: 'fulani.' Akataja jina ambalo amelisikia katika wingu. Akamwambia: 'Ee mja wa Allaah! kwa nini unaniuliza jina langu?' Akasema: 'Nilisikia sauti katika wingu ambalo haya ndio maji yake ikisema: Nyweshea shamba la fulani kwa jina lako. Unafanya nini katika hili?' Akasema: 'Kwa sababu umeniuliza hili, Mimi naangalia kinachotoka humo, na kutoa swadaqah thuluthi, na thuluthi nakula pamoja na ahli wangu, na narudisha humo (shambani) thuluthi yake." [Muslim]
 
Baadhi ya post zangu za zamani...


WAISLAMU MNAFELI WAPI?


Kumekuwa na dhana kwamba waislamu wanafuga majini kitu ambacho si kweli kabisa na hata Dini hairuhusu hivyo.

Mwenyezi Mungu anasema hakuumba majini na watu Ila isipokuwa wamwabudu Mola wao,ebu tuangalie Maandiko;

((Nami sikuwaumba majini na watu ila waniabudu Mimi.))
51:56

Kwahiyo Majini na wanadamu waliumbwa Kwa lengo moja Tu la kumwabudu Mola wao na sio vinginevyo.

Lakini bahati mbaya Sana kuna baadhi ya waislamu ambao hushirikiana na majini katika mambo Yao,na hii sio waislamu Tu hata baadhi ya watu ambao sio waislamu hufanya hivyo pia,iwe Kwa kupiga ramli,kufanya miujiza huko kwenye nyumba za ibada na kadhalika.

Ila mazungumzo yangu Leo hapa nazungumza na waislamu, kuna baadhi ambao huwa na haya maruhani/majini ambayo wenyewe huyaita majini Waziri kwakuwa Tu yanawasaidia katika mambo Yao. Naomba niwaambie kuwa hakuna majini mazuri ambayo yanakaa mwilini mwa mtu hata kidogo,hayo ni mabaya na machafu,jini ambaye ameumbwa ili kumwabudu Mola wake hawezi kuja kufanya makazi katika mwili WA mtu kwakuwa hayo ni makosa na amekiuka sababu ya kuumbwa kwake kabisa.

Wanao mwabudu Mola wao wapo kwenye makazi Yao ya kijini na wanaendesha Maisha Yao huku wanamwabudu Mola wao,kwahiyo acheni kuwa watumwa WA hayo majini,kwani hakika mwisho wenu utakuwa sio mzuri.

Ebu tuangalie maongezi haya ya majini kama yalivyoelezwa katika Qur'an ;

((Na hakika walikuwako wanaume katika watu walio kuwa wakitafuta kujikinga kwa wanaume wa kijini; kwa hivyo wakawazidisha madhambi.))
72:6


Haya ni maongezi ya Majini baada ya kusikia Qur'an na kumwamini Mola wao,ndio wanahadithia kuwa kuna wanadamu wanaume ambao walikuwa wanatafuta hifadhi toka Kwa majini lakini matokeo yake wakazidishiwa madhambi. Na huo ndio ukweli kuna watu ambao wanaamini majini kuwa ndio watawalinda hapa duniani,na huwa hawafanyi Jambo lolote mpaka washaurieni na majini wao,hakika hiyo ni kufuru kubwa kumwamini kiumbe wa Mwenyezi Mungu kuwa ndio anakuwezesha kufanikiwa Kwa mambo hapa duniani.

Na mwisho wa siku shetani/ hayo majini machafu ambayo yameacha kusudio la kuumbwa kwao na kuja kushirikiana na wanadamu,mwisho wa siku yatawakana na kuwaambia ukweli, tuangalie Aya ifuatayo;

(Na Shet'ani atasema itapo katwa hukumu: Hakika Mwenyezi Mungu alikuahidini ahadi ya kweli. Nami nalikuahidini; lakini sikukutimizieni. Na sikuwa na mamlaka juu yenu, isipo kuwa nilikuiteni, nanyi mkaniitikia. Basi msinilaumu mimi, bali jilaumuni wenyewe. Mimi siwezi kuwa mtetezi wenu, wala nyinyi hamwezi kuwa watetezi wangu. Hakika mimi nilikataa tangu zamani kunishirikisha na Mwenyezi Mungu. Hakika madhaalimu watakuwa na adhabu chungu).
14:22


Hakika kuna Aya nyingi Sana juu ya majini kuwapotosha wanadamu na kuwaingiza Motoni,kubwa ni kujua kwamba hakuna majini ambao wanatakiwa kushirikiana na binadamu kwani wao Wana Maisha Yao na wanadamu tuna yetu,ushirikiano wowote baina yetu ni upotovu na mwisho wake ni jehenamu.

Mambo mengi na Mda ni mchache!
 
Baadhi ya post zangu za zamani...

JE WAISLAMU TUNAITENDEA HAKI QUR'AN?

Hakika Mtume Muhammad (rehma na Amani ziwe juu yake) ametuachia vitu viwili ambavyo ndio Muongozo wetu Sisi Waislamu ambavyo ni Qur'an na Sunna, ndio vituongoze siku zote katika Maisha yetu.

Lakini Kwa Masikitiko makubwa kabisa hakika tumeitupa Qur'an ambao ndio msingi mama WA kuwaongoza wanadamu katika njia iliyoonyoka,tunaisoma Qur'an katika swala Tu na baada ya hapo hatuna habari nayo kabisa,je Kwa staili hii umma huu utafaidikaje na Qur'an ?

Na hata hao wachache wanaosoma pia hawayafikii malengo ya Qur'an kwasababu wanasoma pasina kujua maana yake pia. Ndugu zangu katika Imani kama ilivyokuwa makusudio ya kuletwa Mitume ili watuonye tuache mabaya na kufanya mema na kutubashiria yajayo mbele yetu ima mwisho mwema WA kuingia peponi Kwa watu wema wenye kufanya vitendo vizuri hapa duniani na mwisho mbaya Kwa watu wabaya wataingia Motoni.

Na ndo hivyo hivyo Qur'an nzima mafundisho yake kusudio lake ni kumfahamisha mwanadamu njia sahihi ya kufuata Kwa kutenda mambo mema na kumkanya kuepukana na njia mbaya ambayo itampelekea kuingia Motoni, Qur'an imeeleza ujumbe wake Kwa wanadamu kumtambua Mola wao na kumwabudu yeye Peke yake pasina kumshirikisha na chochote,pamoja na kufanya matendo yote mema anayoridhia Allah azza WA jallah na kujiepusha na makatazo yake,ni hiyo ndiyo njia sahihi itakayo mfanya mwanadamu awe salama dawamu.
Sasa wengi wetu tunaisoma Qur'an pasina mazingatio yaliyo kusudiwa,ebu tuangalie Aya moja ya Qur'an inasemaje juu ya hili;

((Na hakika tumekuteremshieni Kitabu ambacho ndani yake yamo makumbusho yenu. Je! Hamzingatii?))
21:10

Hapo tunaona kuwa Qur'an ni ukumbusho Kwa wanadamu ni ujumbe maalum ambao kusudio lake ni kumkumbusha mwanadamu juu ya dhumuni la uwepo wake duniani,je mwanadamu huyu atazingatiaje endapo hajui maana ya Hicho anachokisoma?

Tumekuwa tukihimizwa Sana kusoma Qur'an na Masheikh wetu lakini bahati mbaya Sana hatuhimizwi tusome Kwa kujua maana yake,je tutapataje ibrah au hiyo elimu ndani ya Qur'an itafahamika vipi? Matokeo yake unakuta watu wanasoma Qur'an lakini huoni Athari yoyote ambayo inapatikana katika nyoyo zao.

Ndio unakuta hao hao wasoma Qur'an ni wazinifu,wezi,wachawi,wapiga ramli na mambo kadha WA kadha ,yote hayo ni kwasababu hawasomi Qur'an Kwa mazingatio,Lau kwamba mtu akasoma Qur'an Kwa mazingatio na kujua maana yake wallah tusingekuwa na kizazi kibovu kama ambacho tunacho Leo hii.

Alhamdulillah Leo hii Misahafu ya tafsiri iko tele Mashallah je tunakwama Wapi? Na kuna kasumba ambayo naiona miongoni mwetu,tunaona Qur'an ni Ile iliyoandika Kwa lugha ya kiarabu Tu, laa tunakosea Sana. Qur'an ilishushwa Kwanza Kwa lugha ya kiarabu Kwa kuwa Mtume alikuwa muarabu na umma wake kipindi kile ulikuwa unazungumza lugha ya kiarabu,je ingekuwaje yeye ni mwarabu halafu Qur'an ije Kwa kizigua au kifaransa?

Vitabu vyote vya Mwenyezi Mungu vilishushwa Kwa Mitume kupitia ulimi WA lugha zao ili ujumbe upate kuwafikia,na baadae kutafsiriwa katika lugha mbali mbali ili uwafikie watu wote popote pale duniani,na kubwa zaidi na la kufurahisha Qur'an hata ikitafsiriwa katika lugha yoyote Ile lazima original yake iwepo pembeni ili kuzuia upotofu usitokee.

Kwahiyo ndugu zangu tunazinduana tuisome Qur'an Kwa kuielewa na kuizingatia,kwani Qur'an sio kusudio lake kukaririwa Tu na kusomwa Kwa sauti nzuri pasina kujua maana yake,na hakika asomaye Qur'an mara Kwa mara Kwa kuielewa hakika anapata mawaidha mazuri na hubadili hata mwenendo wake wa Maisha na kuwa Mcha Mungu,na hata kama atateleza kama mwanadamu lakini ni rahisi kukumbuka neno la Allah na akarejea katika mstari.

Bi Aisha (r.a) alipo ulizwa vipi kuhusu matendo/Maisha ya Mtume (s.a.w)
Alisema hakika Maisha yake ni Qur'an Kwa maana aliishi Kwa kufuata misingi ya Qur'an,je vipi Sisi umati wake? Tunaishi kama Qur'an inavyotutaka tuishi?


Leo hii nenda misikitini si rahisi kukuta Misahafu yenye tafsiri ya Qur'an, hata hao wanao nunua Misahafu na kuipeleka misikitini kama waqfu nao wanapeleka yenye lugha ya kiarabu Tu,je Kwa namna hii tutafikia kweli lengo la kusoma Qur'an ?

Tubadilike sasa tusisome Tu Qur'an Kwa kupata thawabu Bali tusome ili itutoe katika Giza na kutepeleka katika mwanga Kwa idhini yake Allah azza WA jallah
 
Ameanza Ujenzi Wa Swadaqatun-Jaariyah Kwa Ajili Ya Mzazi Aliyefariki Kisha Akamalizia Mtu Mwengine Atataqabaliwa?
Maswali: Taqwa - Tazkiyyah


SWALI:



NAULIZA SWALI LANGU KUHUSU SADAKATUL JAARIYA.



MFANO MIMI NIMEMTOLEA MZEE WANGU ALIYEKWISHA KUFARIKI DUNIA VIFAA VYA KUJENGEA MSIKITI AU CHUO KWA AJILI YA SADAKATUL JAARIYA. NA BAADA YA MUDA KAMA MIAKA MITATU (3) AKATOKEA MFADHILI MKUBWA KUJENGA MSIKITI HUO AU CHUO HICHO, NA IKABIDI KUVUNJWA WOTE, NA AKAANZA KUCHIMBA MSINGI MPYA NA KUTUMIA VIFAA VYENGINE KABISA BILA YA VILE VYA ZAMANI JE!!! HAPO ILE SADAKA YA MWANZO ILIYOTOLEWA PENGINE KWA KUCHANGIWA NA WENGI ITAENDELEA AU ITAKATIKA. NAOMBA KUFAHAMISHWA.







JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.



Shukrani zetu za dhati kwa swali lako zuri. Tufahamu kuwa hakuna amali inayofanywa kwa ajili ya Allaah Aliyetukuka ikapotea bure. Kila amali inazawidiwa na Allaah Aliyetukuka kwa nia njema na ikhlasi. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:



"Hakika vitendo huzingatiwa kwa nia, na kwa hakika kila mtu atalipwa kwa nia yake" (al-Jama'ah, yaani Ahmad, al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuud, an-Nasaa'iy, at-Tirmidhiy na Ibn Maajah).



Kwa ajili ya nia hiyo hata kama shughuli hiyo ya ujenzi haikumalizika bado thawabu utapata kwa juhudi na nia yako njema.



Kuhusu hili Hadiyth ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) iko wazi kabisa pale alipotuambia:



"Hakika Allaah Ameandika mambo mema na mabaya, kisha Ameyafafanua hayo kwa kusema kwamba mwenye kukusudia jambo jema na asilifanye Allaah Atamuandikia Kwake jema kamili" (al-Bukhaariy na Muslim).



Kwa hiyo, thawabu zako zipo kamili bila ya upungufu wala kasoro.



Bonyeza kiungo kifuatacho kwa faida zaidi:



‘Amali Za Kuwatendea Wazazi Waliofariki Waendelee Kupokea Thawabu





Na Allaah Anajua zaidi
 
Amekuwa Mbali Na Dini, Matatizo Yanamwandama Na Hajui La Kufanya
Maswali: Taqwa - Tazkiyyah
SWALI:



Assalamualeikum warahmatullahi wabarakatuh rehma za Allaah subhanahu wataala ziwe juu yenu.amin.



mimi ni mwanamke,nilikua nimeshika dini sana wakati nlipokua sijapata kazi,saivi nimepata kazi najitahidi nipate muda wa kusoma quran na kufanya ibada zangu nyingi lakini naposhika quran au kutaka kusoma tasbihi naingiwa na usingizi..wallah najitahidi kuongea na watu maneno mazuri anayopenda allah subhanahu wataala bado naambiwa mie mjeuri kwa kua watu wengi hawaapendi uwaendee kinyume na wanavotaka wao uende...nalia na naumia sana kuwa mbali na dini yangu na najiona nateseka sana sijui nifanyeje! nataka niwe nauliza maswali yangu humu kwa wingi lakini yanachelewa kujibiwa basi huwa sina mwengine wa kumwambia please nawaomba musichelewe kunijibu ndugu zanguni napata shida sana...



ahsante.





JIBU:



Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.



Tunashukuru kwa swali lako la kutafuta ufumbuzi wa kurejea kuwa karibu na dini.



Ndugu yetu, ni vyema tuelewe kuwa Qur-aan iko wazi kuwa mwenye kushikamana na mambo kama haya ya kuwaeleza watu kufanya mema na kuachana na mabaya kama hivi:



“Ewe mwanangu! Simamisha Swalah, na amrisha mema, na kataza maovu, na subiri kwa yanayokupata. Hayo ni katika mambo ya kuazimiwa” Luqmaan: 17.





Hivyo basi, kama kweli uko kama hivyo ulivyojieleza basi ushauri wa Qur-aan ndio kama huo hapo ‘subiri kwa yanayo kupata. Hayo ni katika mambo ya kuazimiwa’ na tarajia malipo kutoka kwa Allaah na usiwe na haja ya kutaka kuwaridhisha watu kwani huna uwezo huo hata kama utaona kuwa unaweza hiyo ni ndoto ya mchana.





Hivyo basi huna haja ya kulia wala kuumia, huna haja ya kujiweka mbali na dini wala huna haja ya kujiona kuwa unateseka; kwani hakuna baya litalokugusa, na hakikisha kuwa unafuata yanayomridhi Allaah; uliyonayo hayo yote ni mawazo anayoyapandikiza Shaytwaan katika nafsi yako ili ujione hivyo unavyojiona, hivyo basi unachotakiwa kushikamana nacho kila yakikujia mawazo kama hayo ni kurudi kwa Mola na kumtaka msaada Wake Akuepushe na Shaytwaan na kumuomba Akuwafikishe kushikamana na kauli Yake kama hii:



“…. Allaah Anatutosha, naye ni Mbora wa kutegemewa. Basi wakarudi na neema na fadhila za Allaah. Hapana baya liliowagusa, na wakafuata yanayomridhi Allaah. Na Allaah ni Mwenye fadhila kuu. Hakika huyo ni Shaytwaan anawatia khofu marafiki zake, basi msiwaogope, bali niogopeni Mimi mkiwa nyinyi ni Waumini.” Aal-‘Imraan: 173-175.





Pia soma Du'aa zifuatazo zikusaidie kuthibitisha iymaan yako Inshaa-Allaah.





اَللَّهُمَّ يَا مُقَلِّبَ الْقُلُوبِ ثَبِّتْ قَلْبِي عَلَى دِينِك

Allaahuuma Yaa Muqallibal-Quluub Thabbit Qalbiy 'Alaa Diynik

(Allaahuumma, Ewe Mgeuza nyoyo, thibitisha moyo wangu katika Dini Yako(

اّللَّهُمَّ ياَ مُصَرِّفَ الْقُلُوب صَرِّف قُلُوبَناَ عَلَى طَاعَتِك

Allaahuumma Ya Muswarrifal-quluub Swarrif Quluubana 'Alaa Twaa'atik

(Allaahumma, Ewe Muelekezaji wa nyoyo, Elekeza nyoyo zetu katika Twa'aa Yako)



Na Adhkhaar za asubuhi na jioni, na pamoja na Du'aa nyingi mbalimbali zilioko katika kitabu cha Hisnul Muslim kilochoko Alhidaaya. Bonyeza kiungo kifuatacho: Hiswnul Muslim







Na Allaah Anajua zaidi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…