Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com







36-Je, Tunatakiwa tutawassal kwa Allaah kwa vipi?



Tunapaswa kutawassal kujikurubisha Kwake kwa kutaja majina Yake Mazuri, na Sifa Zake, na ‘amali njema zetu.

وَلِلَّـهِ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ فَادْعُوهُ بِهَا ۖ



Na Allaah Ana Majina Mazuri kabisa, basi muombeni kwayo. [Al-A’raaf: 180]



((أَسْأَلُكَ بِكُلِّ اسْمٍ هُوَ لَكَ سَمَّيْتَ بِهِ نَفْسَكَ)) صحيح رواه أحمد - صححه الألباني في السلسلة الصحيحة (199)

((Nakuomba kwa kila Jina ambalo ni Lako Ulilojiita Mwenyewe)) [Hadiyth Swahiyh ameipokea Ahmad na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Silsilah Asw-Swahiyhah (199)]
 
Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com







37-Je, Unahitaji kumuomba Allaah kumtegemea kiumbe yeyote?



Hapana! Huhitaji kumtegemea kiumbe mwengine unapomuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)



وَإِذَا سَأَلَكَ عِبَادِي عَنِّي فَإِنِّي قَرِيبٌ ۖ أُجِيبُ دَعْوَةَ الدَّاعِ إِذَا دَعَانِ ۖ

Na watakapokuuliza waja Wangu (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu Mimi, basi Mimi ni Niko karibu (kwa ujuzi); Naitikia du’aa ya muombaji anaponiomba. [Al-Baqarah: 186]



((إِنَّكُمْ تَدْعُونَ سَمِيعًا قَرِيبًا وَهُوَ مَعَكُمْ)) رواه مسلم

((Hakika nyinyi mnamuomba Mwenye kusikia, Aliye karibu (nanyi) Naye Yuko na pamoja nanyi [kwa ujuzi Wake])) [Muslim]
 
Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com









38-Nini jukumu la Rasuli?



Jukumu la Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ni kubalighisha ujumbe.



يَا أَيُّهَا الرَّسُولُ بَلِّغْ مَا أُنزِلَ إِلَيْكَ مِن رَّبِّكَ ۖ

Ee Rasuli! Balighisha yale yaliyoteremshwa kwako kutoka kwa Rabb wako. [Al-Maaidah: 67]



((أللّهم هَلْ بلّغت؟ اللّهم اشهد)) مسلم

جواباً لقول الصحابة نشهد أنّك قد بلّغت

((Ee Allaah! Je nimebalighisha? Ee Allaah Shuhudia)) [Muslim]



Jibu la Maswahaba walosema kuwa: Tunashuhudia kuwa umebalighisha.
 
Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com







39-Nani tumuombe tukitaka kuombewa shafaa'ah na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)?



Tukitaka kuombewa shafaa’ah na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) inapasa tumuombe Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa).



قُل لِّلَّـهِ الشَّفَاعَةُ جَمِيعًا ۖ

Sema: “Uombezi wote ni wa Allaah Pekee. [Az-Zumar: 44]



((اللّهم شفّعه فيّ)) رواه الترمذي وقال حديث حسن.

((Ee Allaah! Ikubali shafaa’ah (maombezi) yake kwangu))
 
Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com







40-Vipi tumpende Allaah Na Rasuli Wake?



Mapenzi ya Allaah na Rasuli Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ni kutii na kufuata amri ya Allaah.



قُلْ إِن كُنتُمْ تُحِبُّونَ اللَّـهَ فَاتَّبِعُونِي يُحْبِبْكُمُ اللَّـهُ...

31. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Mkiwa mnampenda Allaah, basi nifuateni mimi, Atakupendeni Allaah [Aal-‘Imraan: 31]



((لا يُؤْمِنُ أَحَدُكُمْ حَتَّى أَكونَ أحَبَّ إِلَيْهِ مِنْ وَالِدِهِ وَوَلَدِه وَالنَّاسِ أَجْمَعينَ)) متفق عليه

((Hatoamini mmoja wenu mpaka niwe (mimi Muhammad) kipenzi chake kuliko mwanawe na wazazi wake na kuliko watu wote waliobakia)) [Al-Bukhaariy, Muslim]
 
021-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kusaidiana Katika Wema Na Taqwa


Riyaadhw Asw-Swaalihiyn





باب التعاون عَلَى البر والتقوى

021 – Mlango Wa Kusaidiana Katika Wema Na Taqwa



Alhidaaya.com



قَالَ الله تَعَالَى:



وَتَعَاوَنُوا عَلَى الْبِرِّ وَالتَّقْوَىٰ ۖ

Na shirikianeni katika wema na taqwa… (Al-Maaidah: 2)



وَالْعَصْرِ ﴿١﴾

Naapa kwa Al-‘Aswr (zama).



إِنَّ الْإِنسَانَ لَفِي خُسْرٍ ﴿٢﴾

Hakika mwana wa Aadam bila shaka yumo katika khasara.



إِلَّا الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ وَتَوَاصَوْا بِالْحَقِّ وَتَوَاصَوْا بِالصَّبْرِ ﴿٣﴾

Isipokuwa wale walioamini na wakatenda mema na wakausiana haki na wakausiana subira. [Al-‘Aswr: 1-3]







Hadiyth – 1

وعن أَبي عبد الرحمن زيد بن خالد الجهني رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم: ((مَنْ جَهَّزَ غَازِيًا في سَبيلِ اللهِ فَقَدْ غَزَا، وَمَنْ خَلَفَ غَازيًا في أهْلِهِ بِخَيرٍ فَقَدْ غَزَا)). مُتَّفَقٌ عَلَيهِ

Kutoka Kwa Abuu ‘Abdur-Rahmaan Zayd bin Khaalid Al-Juhaniy (Radhwiya Allaahu 'anhu) ya kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) amesema: “Yeyote atakayemtayarisha kwa kumpatia vifaa Mujahid katika njia ya Allaah ni kama yeye mwenyewe amehudhuria katika kupigana (hivyo kupata thawabu sawa). Na yeyote mwenye kuwatizama watu wanaomtegemea Mujahid (wakati ambao hayupo) ni kama pia amepigana katika vita.” [Al-Bukhaariy na Muslim]







Hadiyth – 2

وعن أَبي سعيد الخدري رضي الله عنه: أن رَسُول الله صلى الله عليه وسلم بعث بعثًا إِلَى بني لِحْيَان مِنْ هُذَيْلٍ، فَقَالَ: ((لِيَنْبَعِثْ مِنْ كُلِّ رَجُلَيْنِ أَحَدُهُمَا وَالأجْرُ بَيْنَهُمَا)). رواه مسلم

Kutoka kwa Abuu Sa’iyd Al-Khudriy (Radhwiya Allaahu 'anhu) ya kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) alituma kikosi kwa kabila la Lihyaan wa ukoo wa Hudhayl, akasema: “Atoke katika kila watu wawili mtu mmoja na ujira (thawabu) ni baina yao.” [Muslim]







Hadiyth – 3

وعن ابن عباس رضي الله عنهما: أنَّ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم لَقِيَ رَكْبًا بالرَّوْحَاءِ، فَقَالَ: ((مَنِ القَوْمُ؟)) قالوا: المسلمون، فقالوا: من أنتَ؟ قَالَ: ((رَسُول الله))، فرفعت إِلَيْه امرأةٌ صبيًا، فَقَالَتْ: ألِهَذَا حَجٌّ؟ قَالَ: ((نَعَمْ، وَلَكِ أجْرٌ)). رواه مسلم

Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhu) ya kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) alikutana na kikundi cha watu waliokuwa wamepanda vipandio katika sehemu ya Rawhaa na akawauliza: “Hawa ni watu gani?” Wakasema: “Waislamu.” Kisha wakasema: “Wewe ni nani?” Akasema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam).” Mwanamke mmoja aliyekwepo alimnyanyua mtoto mdogo na kuuliza: “Je,huyu ana hijja?” Akasema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam): “Ndio, nawe pia utapata ujira (kwa hilo).” [Muslim]







Hadiyth – 4

وعن أَبي موسى الأشعري رضي الله عنه عن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم أنَّه قَالَ: ((الخَازِنُ المُسْلِمُ الأمِينُ الَّذِي يُنفِذُ مَا أُمِرَ بِهِ فيُعْطيهِ كَامِلًا مُوَفَّرًا طَيِّبَةً بِهِ نَفْسُهُ فَيَدْفَعُهُ إِلَى الَّذِي أُمِرَ لَهُ بِهِ، أحَدُ المُتَصَدِّقين)). مُتَّفَقٌ عَلَيهِ

وفي رواية: ((الَّذِي يُعْطِي مَا أُمِرَ بِهِ))

Kutoka kwa Abuu Muwsaa Al-Ash’ariy (Radhwiya Allaahu 'anhu) ya kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) amesema “Muweka hazina Muislamu, ni yule aliye muaminifu mwenye kumpatia mtu anayestahiki haki yake kwa ukamilifu na kuwa na nafasi nzuri. Na kule kumpatia yule aliyeamriwa kwake inakuwa ni swadaqa.

Riwaya nyengine: “Yule ambaye anatoa katika yale aliyomrishwa.” [Al-Bukhaariy na Muslim]
 
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn



باب النصيحة

022 – Mlango Wa Nasaha



Alhidaaya.com







قَالَ تَعَالَى:

إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ إِخْوَةٌ

Hakika Waumini ni ndugu… [Al-Hujraat: 10]

وَأَنصَحُ لَكُمْ

Na nakunasihini… [Al-A’raaf: 62]



وَأَنَا لَكُمْ نَاصِحٌ أَمِينٌ ﴿٦٨﴾

Nami kwenu ni mtoaji nasiha mwaminifu. [Al-A’raaf:68]







Hadiyth – 1

عن أَبي رُقَيَّةَ تَمِيم بن أوس الداريِّ رضي الله عنه: أنَّ النَّبيّ صلى الله عليه وسلم، قَالَ: ((الدِّينُ النَّصِيحةُ)) قلنا: لِمَنْ؟ قَالَ: ((لِلهِ وَلِكِتَابِهِ وَلِرَسُولِهِ وَلأئِمَّةِ المُسْلِمِينَ وَعَامَّتِهِمْ)). رواه مسلم

Imepokelewa kutoka kwa Abu Ruqayyah Tamiym ibn Aws Ad-Daariyy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba; Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) amesema: “Dini ni nasiha” Tukasema, kwanini? Akasema: “Kwa Allaah, na kitabu Chake, na Rasuli Wake, na kwa viongozi wa Waislamu na watu wa kawaida.” [Muslim]





Hadiyth – 2

عن جرير بن عبد الله رضي الله عنه قَالَ: بَايَعْتُ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم عَلَى إقَامِ الصَّلاةِ، وَإِيتَاءِ الزَّكَاةِ، والنُّصْحِ لِكُلِّ مُسْلِمٍ. مُتَّفَقٌ عَلَيهِ

Imepokelewa kutoka kwa Jariyr bin ‘Abdillaah (Radhwiya Allaahu 'anhu) alisema kwamba: Nilimbay’ Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) juu ya kusimamisha Swalaah, kutoa Zakaah, na kumnasihi kila Muislamu. [Al-Bukhaariy na Muslim]







Hadiyth – 3

عن جرير بن عبد الله رضي الله عنه قَالَ: بَايَعْتُ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم عَلَى إقَامِ الصَّلاةِ، وَإِيتَاءِ الزَّكَاةِ، والنُّصْحِ لِكُلِّ مُسْلِمٍ. مُتَّفَقٌ عَلَيهِ

Imepokelewa kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) amesema: “Hatoamini mmoja wenu mpaka ampendelee nduguye kile anachopendelea nafsi yake.” [Al-Bukhariy na Muslim]
 
023 – Mlango Wa Kuamrisha Mema Na Kukataza Maovu



Alhidaaya.com





قَالَ اللهُ تَعَالَى:



خَيْرِ وَيَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ ۚ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفلِحُونَ ﴿١٠٤﴾

Na watokeze kutoka kwenu umati wa watu unaolingania kheri na unaoamrisha mema na unaokataza munkari. Na hao ndio waliofaulu. [Aal-‘Imraan: 104]





كُنتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ تَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَتَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ

Mmekuwa Ummah bora kabisa uliotolewa (mfano) kwa watu; mnaamrisha mema na mnakataza munkari… [Aal-‘Imraan: 110]





خُذِ الْعَفْوَ وَأْمُرْ بِالْعُرْفِ وَأَعْرِضْ عَنِ الْجَاهِلِينَ ﴿١٩٩﴾

Shikamana na usamehevu, na amrisha mema na jiepushe na majahili. [Al-A’raaf: 199]





وَالْمُؤْمِنُونَ وَالْمُؤْمِنَاتُ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ ۚ يَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ

Na Waumini wanaume na Waumini wanawake ni marafiki wandani wao kwa wao, wanaamrisha mema na wanakataza munkari… [At-Tawbah: 71]





لُعِنَ الَّذِينَ كَفَرُوا مِن بَنِي إِسْرَائِيلَ عَلَىٰ لِسَانِ دَاوُودَ وَعِيسَى ابْنِ مَرْيَمَ ۚ ذَٰلِكَ بِمَا عَصَوا وَّكَانُوا يَعْتَدُونَ ﴿٧٨﴾

Wamelaaniwa wale waliokufuru miongoni mwa wana wa Israaiyl kwa lisani ya Daawuwd na ‘Iysaa mwana wa Maryam. Hivyo ni kwa sababu ya kuasi kwao na walikuwa wakitaadi.





كَانُوا لَا يَتَنَاهَوْنَ عَن مُّنكَرٍ فَعَلُوهُ ۚ لَبِئْسَ مَا كَانُوا يَفْعَلُونَ ﴿٧٩﴾

Walikuwa hawakatazani munkari waliyofanya. Uovu ulioje waliyokuwa wakiyafanya. [Al- Maaidah: 78-79]





وَقُلِ الْحَقُّ مِن رَّبِّكُمْ ۖ فَمَن شَاءَ فَلْيُؤْمِن وَمَن شَاءَ فَلْيَكْفُرْ ۚ

Na sema: “Hii ni haki kutoka kwa Rabb wenu. Basi anayetaka aamini, na anayetaka akufuru.” [Al-Kahf: 29]





فَاصْدَعْ بِمَا تُؤْمَرُ وَأَعْرِضْ عَنِ الْمُشْرِكِينَ﴿٩٤﴾

Basi tangaza wazi yale uliyoamrishwa na jitenge na washirikina. [Al-Hijr: 94]





فَلَمَّا نَسُوا مَا ذُكِّرُوا بِهِ أَنجَيْنَا الَّذِينَ يَنْهَوْنَ عَنِ السُّوءِ وَأَخَذْنَا الَّذِينَ ظَلَمُوا بِعَذَابٍ بَئِيسٍ بِمَا كَانُوا يَفْسُقُونَ ﴿١٦٥﴾

Waliposahau yale waliyokumbushwa nayo; Tuliwaokoa wale wanaokataza uovu, na Tukawachukua wale waliodhulumu kwa adhabu mbaya kabisa kwa yale waliyokuwa wakifanya ufasiki. [Al-A’raaf: 165]







Hadiyth – 1

عن أبي سعيد الخدري رضي الله عنه قَالَ: سَمِعت رَسُول الله صلى الله عليه وسلم يقول: ((مَنْ رَأى مِنْكُمْ مُنْكَرًا فَلْيُغَيِّرْهُ بِيَدِهِ، فَإنْ لَمْ يَسْتَطِعْ فَبِلِسَانِهِ، فَإنْ لَمْ يَسْتَطِعْ فَبِقَلْبِهِ، وَذَلِكَ أضْعَفُ الإيمَانِ)). رواه مسلم

Imepokewa kutoka kwa Sa’iyd Al-Khudriy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba: Amemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) akisema: “Yoyote katika nyinyi atakayeona munkari na aubadilishe kwa mkono wake, na akiwa hawezi basi afanye hivyo kwa ulimi wake, na akiwa hawezi basi afanye hivyo kwa moyo wake, na huo ni udhaifu wa iymaan.” [Muslim]







Hadiyth – 2

عن ابن مسعود رضي الله عنه: أن رَسُول الله صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((مَا مِنْ نَبيٍّ بَعَثَهُ اللهُ في أمَّة قَبْلِي إلا كَانَ لَهُ مِنْ أُمَّتِهِ حَوَارِيُّونَ وَأصْحَابٌ يَأخُذُونَ بِسنَّتِهِ وَيَقْتَدُونَ بِأَمْرِهِ، ثُمَّ إِنَّهَا تَخْلُفُ مِنْ بَعْدِهِمْ خُلُوفٌ يَقُولُونَ مَا لا يَفْعَلُونَ وَيَفْعَلُونَ مَا لا يُؤْمَرونَ، فَمَنْ جَاهَدَهُمْ بِيَدِهِ فَهُوَ مُؤْمِنٌ، وَمَنْ جَاهَدَهُمْ بِقَلبِهِ فَهُوَ مُؤمِنٌ، وَمَنْ جَاهَدَهُمْ بِلسَانِهِ فَهُوَ مُؤمِنٌ، وَلَيسَ وَرَاءَ ذلِكَ مِنَ الإيمَانِ حَبَّةُ خَرْدَل)). رواه مسلم

Imepokewa kutoka kwa ibn Mas’uwd (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) amesema: “Hakuna Nabiy yoyote aliyetumwa kabla yangu isipokuwa alikuwa na wateule wake (Maswahaba na wanafunzi wake) katika Ummah wake. Hawa Maswahaba (wa Manabiy) walikuwa wakifuata mwendo wake (Sunnah za Nabiy wao) na kufuata maagizo yake. Baada yao wakaja wafuasi waliozua (mambo yao wenyewe) huku wakisema wasiyotenda na kutenda wasiyoamrishwa. Hivyo, yoyote atakayepigana nao kwa mkono wake ni Muumin, na anayepigana nao kwa moyo wake pia ni Muumin, na anayepigana nao kwa ulimi wake pia ni Muumin. Hapana nyuma ya haya chembe ya iymaan.” [Muslim]







Hadiyth – 3

عن أبي الوليدِ عبادة بن الصامِت رضي الله عنه قَالَ: بَايَعْنَا رَسُول الله صلى الله عليه وسلم عَلَى السَّمْعِ والطَّاعَةِ في العُسْرِ واليُسْرِ، والمَنْشَطِ وَالمَكْرَهِ، وَعَلَى أثَرَةٍ عَلَيْنَا، وَعَلَى أنْ لا نُنازِعَ الأمْرَ أهْلَهُ إلا أنْ تَرَوْا كُفْرًا بَوَاحًا عِنْدَكُمْ مِنَ اللهِ تَعَالَى فِيهِ بُرْهَانٌ، وَعَلَى أنْ نَقُولَ بالحَقِّ أيْنَمَا كُنَّا لا نَخَافُ في اللهِ لَوْمَةَ لاَئِمٍ. مُتَّفَقٌ عَلَيهِ

Imeokewa kutoka kwa Abul Waliyd ‘Ubadah bin As-Swaamit (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba: Tulimbay’ Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) juu ya kusikia na kutii wakati wa mazito na mepesi, na katika raha na shida na kuweza kuhimilia wakati unapobaguliwa (na kushinda). Na pia tusiwe ni wenye kuzozana na viongozi isipokuwa unapoona ukafiri wa wazi kabisa, hapo mtakuwa na dalili ya wazi na ruhusa kutoka kwa Allaah (Subhaanahu Wa Ta'aalaa). Na tuwe ni wenye kusema kweli popote tulipo wala tusiogope lawama ya anaye laumu.” [Al-Bukhaariy na Muslim]







Hadiyth – 4

عن النعمان بن بشير رضي الله عنهما عن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((مَثَلُ القَائِمِ في حُدُودِ اللهِ وَالوَاقعِ فِيهَا، كَمَثَلِ قَومٍ اسْتَهَمُوا عَلَى سَفِينَةٍ فَصَارَ بَعْضُهُمْ أعْلاها وَبَعْضُهُمْ أَسْفَلَهَا، وَكَانَ الَّذِينَ في أَسْفَلِهَا إِذَا اسْتَقَوا مِنَ المَاءِ مَرُّوا عَلَى مَنْ فَوْقهُمْ، فَقَالُوا: لَوْ أنَّا خَرَقْنَا في نَصِيبِنَا خَرْقًا وَلَمْ نُؤذِ مَنْ فَوقَنَا، فَإِنْ تَرَكُوهُمْ وَمَا أرَادُوا هَلَكُوا جَميعًا، وَإنْ أخَذُوا عَلَى أيدِيهِمْ نَجَوا وَنَجَوْا جَميعًا)). رواه البخاري

Imepokewa kutoka kwa An-Nu’maan bin Bashiyr (Radhwiya Allaahu 'anhu) ya kwamba: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) amesema: “Mfano wa mwenye kusimama juu ya mipaka ya Allaah (kwa kumtii) ni wale walioingia ndani (wenye kupuuza mipaka Yake), ni mfano wa watu walioshindana (kuingia) katika Safina, baadhi yao wakawa juu ya wengine wakawa katika sehemu ya chini. Ama kwa wale waliokuwa chini walipokuwa wanataka maji ya kunywa iliwabidi wapande juu, hivyo wakasema: Lau sisi tukitoboa tundu katika sehemu yetu hii ya chini hatutokuwa ni wenye kuwaudhi wa juu. Ikiwa wataacha wafanye wanayoyataka basi wataangamia wote na wakiwashika mikono yao basi wataokoka wao na wote kwa pamoja.” [Al- Bukhaariy]







Hadiyth – 5

عن أُمِّ المؤمنين أم سلمة هند بنت أَبي أمية حذيفة رضي الله عنها، عن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم أنه قَالَ: ((إنَّهُ يُسْتَعْمَلُ عَلَيْكُمْ أُمَرَاءُ فَتَعرِفُونَ وتُنْكِرُونَ، فَمَنْ كَرِهَ فَقَدْ بَرِئَ، وَمَنْ أنْكَرَ فَقَدْ سَلِمَ، وَلَكِنْ مَنْ رَضِيَ وَتَابَعَ)) قَالوا: يَا رَسُول اللهِ، ألا نُقَاتِلهم؟ قَالَ: ((لا، مَا أَقَامُوا فيكُمُ الصَّلاةَ)). رواه مسلم

Imepokewa kutoka kwa Mama wa Waumini Ummu Salamah Hind bint Abu Umayyah Hudhayfah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) ya kwamba: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) amesema: “Hakika kutakuwa na watu watakaochaguliwa kama viongozi wenu, mtawajua na kuwachukia, yoyote atakayechukia atakuwa hana makosa, na yoyote atayechukia atakuwa hakika amesalimika, lakini (mwenye makosa) ni yule anayeridhika na akafuata.” Wakasema: Ee Rasuli wa Allaah! Je, tusipiganae nao? Akasema: “Msipigane nao, maadamu wataendelea kusimamisha Swalaah miongoni mwenu.” [Muslim]







Hadiyth – 6

عن أم المؤمنين أم الحكم زينب بنتِ جحش رَضِي الله عنها: أن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم دخل عَلَيْهَا فَزِعًا، يقول: ((لا إلهَ إلا الله، وَيلٌ للْعَرَبِ مِنْ شَرٍّ قَدِ اقْتَرَبَ، فُتِحَ اليَوْمَ مِنْ رَدْمِ يَأجُوجَ وَمَأجُوجَ مِثلَ هذِهِ))، وحلّق بأُصبُعيهِ الإبهامِ والتي تليها، فقلتُ: يَا رَسُول الله، أنَهْلِكُ وَفِينَا الصَّالِحُونَ؟ قَالَ: ((نَعَمْ، إِذَا كَثُرَ الخَبَثُ)). مُتَّفَقٌ عَلَيهِ

Imepokewa kutoka kwa Mama wa Waumini Ummul Hakam Zaynab bint Jahsh (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kwamba: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) aliingia kwake akiwa amefadhaika, akasema: “Hapana anayepaswa kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah. Ole wao Waarabu! kwa shari iliyokaribia. Imefunguliwa leo tundu katika ukuta unaowazuia Juwj na Ma-ajuwj mfano huo (na akachora duara kwa kutumia kidole gumba na kile kinachofuata).” Nikasema: Ee Rasuli wa Allaah! Tutaangamizwa na miongoni mwetu kuna watu wema? Akasema: “Ndio, pindi maovu yatakapokithiri.” [Al-Bukhaariy na Muslim]







Hadiyth – 7

عن أَبي سعيد الخُدري رضي الله عنه عن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((إيَّاكُمْ وَالجُلُوسَ في الطُّرُقَاتِ!)) فقالوا: يَا رَسُول الله، مَا لنا مِنْ مجالِسِنا بُدٌّ، نتحدث فِيهَا. فَقَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم: ((فَإذَا أبَيْتُمْ إلا المَجْلِسَ، فَأَعْطُوا الطَّريقَ حَقَّهُ)). قالوا: وما حَقُّ الطَّريقِ يَا رسولَ الله؟ قَالَ: ((غَضُّ البَصَرِ، وَكَفُّ الأَذَى، وَرَدُّ السَّلامِ، وَالأمْرُ بِالمَعْرُوفِ، والنَّهيُ عن المُنْكَرِ)). مُتَّفَقٌ عَلَيهِ

Imepokewa kutoka kwa Sa’iyd Al-Khudriy (Radhwiya Allaahu 'anhu) ya kwamba: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) amesema: “Nawatahadharisha nyinyi kwa kukaa kwenu njiani” Wakasema: Ee Rasuli wa Allaah! Hatuna budi isipokuwa kukaa (katika sehemu hizo) kwani tunazungumza na kujadiliana ndani yake. Akasema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) “Ikiwa ni hivyo basi ipatieni njia haki yake” Wakasema: Ni zipi haki za njia Ee Rasuli wa Allaah? Akasema: “Kuinamisha macho chini, na kuondoka uchafu (pingamizi), na kurudisha salamu, na kuamrisha mema na kukataza maovu.” [Al-Bukhaariy na Muslim]







Hadiyth – 8

عن ابن عباس رضي الله عنهما: أن رَسُول الله صلى الله عليه وسلم رأى خاتَمًا مِنْ ذهبٍ في يدِ رجلٍ فنَزعه فطرحه، وَقالَ: ((يَعْمدُ أحَدُكُمْ إِلَى جَمْرَةٍ مِنْ نَارٍ فَيَجْعَلُهَا في يَدِهِ!)) فقِيلَ لِلرَّجُلِ بَعْدَمَا ذهب رَسُول اللهِ صلى الله عليه وسلم: خُذْ خَاتَمَكَ انْتَفِعْ بِهِ. قَالَ: لا والله لا آخُذُهُ أبَدًا وَقَدْ طَرَحَهُ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم. رواه مسلم

Imepokewa na ibn ‘Abbas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) alimuona mtu amevaa pete ya dhahabu mkononi mwake. Alimtoa katika kidole chake na kuitupa. Kisha Akasema: “Mmoja wenu anakusudia kuliweka kaa la moto katika mkono wake!” Akaambiwa yule mtu baada ya kuondoka kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam). Ichukue pete yako na ufaidike nayo. Akasema: Hapana! Naapa kwa Allaah, siichukui milele baada ya kutupwa na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam). [Muslim]







Hadiyth – 9

عن أَبي سعيد الحسن البصري: أن عائِذَ بن عمرو رضي الله عنه دخل عَلَى عُبَيْدِ اللهِ بنِ زياد، فَقَالَ: أي بُنَيَّ، إني سمعت رَسُول الله صلى الله عليه وسلم، يقول: ((إنَّ شَرَّ الرِّعَاءِ الحُطَمَةُ)) فَإِيَّاكَ أنْ تَكُونَ مِنْهُمْ، فَقَالَ لَهُ: اجلِسْ فَإِنَّمَا أنْتَ مِنْ نُخَالَةِ أصْحَابِ مُحَمَّد صلى الله عليه وسلم، فَقَالَ: وهل كَانَتْ لَهُم نُخَالَةٌ إِنَّمَا كَانَتِ النُّخَالَةُ بَعْدَهُمْ وَفي غَيْرِهِمْ. رواه مسلم

Imepokewa kutoka kwa Abu Sa’iyd Al-Hasan Al-Baswariy ya kwamba: ‘Aa’idh bin ‘Amru (Radhwiya Allaahu 'anhu) alimtembelea ‘Ubaydullaah bin Ziyaad na kumwambia: Ewe mtoto wangu! hakika nimesikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) akisema: “Hakika viongozi wabaya kabisa ni wale wakali (kwa raia wao). Hivyo, kuwa na tahadhari usiwe miongoni mwao.” Kaa chini kwani wewe ni miongoni mwa kumvi wa Maswahaba wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam). Akasema: (‘Aa’idh) na je, yeye alikuwa na kapi, hakika kumvi walikuja baada yao na watu wengine wasiokuwa wao. [Muslim]







Hadiyth – 10

عن حذيفة رضي الله عنه عن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((وَالَّذِي نَفْسي بِيَدِهِ، لَتَأْمُرُنَّ بِالمَعْرُوفِ، وَلَتَنْهَوُنَّ عَنْ المُنْكَرِ أَوْ لَيُوشِكَنَّ اللهُ أنْ يَبْعَثَ عَلَيْكُمْ عِقَابًا مِنْهُ ثُمَّ تَدْعُوْنَهُ فَلا يُسْتَجَابُ لَكُمْ)). رواه الترمذي

Imepokewa kutoka kwa Hudhayfah (Radhwiya Allaahu 'anhu) ya kwamba: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) amesema: “Naapa kwa yule ambaye nafsi yangu ipo mikononi Mwake, mtaendelea kuamrisha mema na kukataza maovu au kama si hivyo basi Allaah Atawateremshia adhabu, kisha mtamuomba yeye kisha hatawojibu (du’aa zenu).” [At-Tirmidhiy]







Hadiyth – 11

عن أَبي سعيد الخدري رضي الله عنه عن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((أفْضَلُ الجِهَادِ كَلِمَةُ عَدْلٍ عِنْدَ سُلْطَانٍ جَائرٍ)). رواه أَبُو داود والترمذي

Imepokewa kutoka kwa Abu Sa’iyd Al-Khudriy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ya kwamba: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Jihadi iliyo bora kabisa ni kuzungumza maneno ya haki mbele ya kiongozi mjeuri.” [Abu Daawuwd na At-Tarmidhiy]







Hadiyth – 12

عن أَبي عبدِ الله طارِقِ بن شِهاب البَجَليِّ الأَحْمَسِيّ رضي الله عنه: أنَّ رجلًا سأل النَّبيّ صلى الله عليه وسلم وقد وضع رِجله في الغَرْزِ: أيُّ الجِهادِ أفضلُ؟ قَالَ: ((كَلِمَةُ حَقٍّ عِنْدَ سُلْطَانٍ جَائرٍ)). رواه النسائي

Imepokewa kutoka kwa Abu ‘Abdillaah Twaariq bin Shihaab Al-Bajaliy Al-Ahmasiy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ya kwamba, mtu mmoja alimuuliza Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ambaye alikuwa tayari ameweka mguu kwenye kipandio cha Ngozi (au kibao) cha ngamia akasema: Ni Jihadi gani iliyobora kabisa? Akasema: “Kuzungumza maneno ya haki mbele ya kiongozi mjeuri.” [An-Nasaaiy]







Hadiyth – 13

عن ابن مسعود رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: ((إنَّ أوَّلَ مَا دَخَلَ النَّقْصُ عَلَى بَنِي إسْرَائِيلَ أنَّهُ كَانَ الرَّجُلُ يَلْقَى الرَّجُلَ، فَيَقُولُ: يَا هَذَا، اتَّقِ الله ودَعْ مَا تَصْنَعُ، فَإِنَّهُ لاَ يَحِلُّ لَكَ، ثُمَّ يَلْقَاهُ مِنَ الغَدِ وَهُوَ عَلَى حَالِهِ، فَلا يَمْنَعُهُ ذلِكَ أنْ يَكُونَ أكِيلَهُ وَشَرِيبَهُ وَقَعِيدَهُ، فَلَمَّا فَعَلُوا ذلِكَ ضَرَبَ اللهُ قُلُوبَ بَعْضِهِمْ بِبَعْضٍ)) ثُمَّ قَالَ: {لُعِنَ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْ بَنِي إِسْرائيلَ عَلَى لِسَانِ دَاوُدَ وَعِيسَى ابْنِ مَرْيَمَ ذَلِكَ بِمَا عَصَوْا وَكَانُوا يَعْتَدُونَ * كَانُوا لا يَتَنَاهَوْنَ عَنْ مُنْكَرٍ فَعَلُوهُ لَبِئْسَ مَا كَانُوا يَفْعَلُونَ * تَرَى كَثِيرًا مِنْهُمْ يَتَوَلَّوْنَ الَّذِينَ كَفَرُوا لَبِئْسَ مَا قَدَّمَتْ لَهُمْ أَنْفُسُهُمْ} إِلَى قوله: {فاسِقُونَ} [المائدة: 78- 81].

ثُمَّ قَالَ: ((كَلا، وَاللهِ لَتَأمُرُنَّ بالمَعْرُوفِ، وَلَتَنْهَوُنَّ عَنِ المُنْكَرِ، وَلَتَأخُذُنَّ عَلَى يَدِ الظَّالِمِ، وَلَتَأطِرُنَّهُ عَلَى الحَقِّ أَطْرًا، وَلَتَقْصُرُنَّه عَلَى الحَقِّ قَصْرًا، أَوْ لَيَضْرِبَنَّ اللهُ بقُلُوبِ بَعْضِكُمْ عَلَى بَعْضٍ، ثُمَّ ليَلْعَنَنَّكُمْ كَمَا لَعَنَهُمْ)). رواه أَبُو داود والترمذي

هَذَا لفظ أَبي داود، ولفظ الترمذي، قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: ((لَمَّا وَقَعَتْ بَنُو إسْرَائِيلَ في المَعَاصي نَهَتْهُمْ عُلَمَاؤهُمْ فَلَمْ يَنْتَهُوا، فَجَالَسُوهُمْ في مَجَالِسِهمْ، وَوَاكَلُوهُمْ وَشَارَبُوهُمْ، فَضَربَ اللهُ قُلُوبَ بَعضِهِمْ بِبعْضٍ، وَلَعَنَهُمْ عَلَى لِسانِ دَاوُد وعِيسَى ابنِ مَرْيَمَ ذلِكَ بما عَصَوا وَكَانُوا يَعتَدُونَ)) فَجَلَسَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم وكان مُتَّكِئًا، فَقَالَ: ((لا، والَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ حَتَّى تَأطِرُوهُمْ عَلَى الحَقِّ أطْرًا)).

Imepokewa kutoka kwa ibn Mas’uwd (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ya kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Upungufu wa kwanza uliowafikia Banuu Israiyl ulikuwa mtu kukutana na mwenzake, akimwambia: Ewe fulani! mche Allaah na uache unayofanya kwani si halali kwako (kufanya hivyo). Kisha anakutana naye siku ya pili katika hali yake ya awali (bila ya mabadiliko), hilo halimkatazi yeye kutokula naye, kunywa na kukaa naye. Walipofanya hivyo, Allaah Alibadilisha mioyo yao baadhi yao kwa wengine.” Kisha akasema: “Wamelaaniwa wale waliokufuru miongoni mwa wana wa Israaiyl kwa lisani (lugha) ya Daawuwd na ‘Iysaa mwana wa Maryam. Hivyo ni kwa sababu ya kuasi kwao na walikuwa wakitaadi.” Walikuwa hawakatazani munkari waliyofanya. Uovu ulioje waliyokuwa wakiyafanya.” “Utawaona wengi miongoni mwao wanawafanya marafiki wandani wale waliokufuru. Ubaya ulioje yale yaliyowatangulizia nafsi zao, ndipo Allaah Amewaghadhibikia na katika adhabu wao watadumu.” “Na lau wangelikuwa wanamwamini Allaah na Nabiy (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) na yale yaliyoteremshwa kwake, wasingeliwafanya hao marafiki wandani, lakini wengi miongoni mwao ni mafasiki.” [Al-Maaidah: 78-81]

Kisha akasema: “Hasha! Naapa kwa Allaah ya kwamba mtaendelea kuamrisha mema na kukataza maovu na kuushika mkono wa dhalimu na kuwashawishi (kwa upole na ulaini) wafanye uadilifu, kuwafanya wawe imara juu ya haki na ukweli. Mkishindwa kufanya hivyo, basi jueni ya kwamba Allaah Atawaadhibu pamoja na wenzenu (madhalimu wa nafsi zao) na kisha Atawalaani kama Alivyowalaani wao (Mayahudi).” [Hii ni lafdhi ya Abu Daawuwd]



Riwaayah ya At-Tirmidhiy: Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): “Walipoingia Banuu Israiyl katika maasi, Wanachuoni wao waliwakataza lakini hawakuacha, hivyo wakaanza kukaa nao katika baraza zao na wakawa wanakula na kunywa pamoja nao. Hapo Allaah Aliwaadhibu wote pamoja na wakalaaniwa kwa ulimi wa Dawwuud na ‘Iysaa bin Maryam na hiyo ni kwa sababu waliasi na wakawa wanapindukia mipaka.”

Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akakaa baada ya kuwa ameegemea, kisha akasema: “Laa sivyo hivyo, naapa kwa Yule ambaye kwamba nafsi yangu ipo mikononi Mwake, mpaka muwashike mkono madhalimu ili waweze kusimama juu ya haki.” [At-Tirmidhiy]







Hadiyth – 14

عن أَبي بكر الصديق رضي الله عنه قَالَ: يَا أيّها النَّاس، إنّكم لتَقرؤُون هذِهِ الآية: {يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا عَلَيْكُمْ أَنْفُسَكُمْ لا يَضُرُّكُمْ مَنْ ضَلَّ إِذَا اهْتَدَيْتُمْ} [المائدة: 105].

وإني سمعت رَسُول الله صلى الله عليه وسلم يقول: ((إنَّ النَّاسَ إِذَا رَأَوُا الظَّالِمَ فَلَمْ يأخُذُوا عَلَى يَدَيْهِ أوشَكَ أنْ يَعُمَّهُمُ اللهُ بِعِقَابٍ مِنْهُ)). رواه أَبُو داود والترمذي والنسائي

Imepokewa kutoka kwa Abu Bakr As-Swidiyq (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ya kwamba alisema: Enyi watu! Hakika nyinyi mnaisoma Aayah hii: “Enyi walioamini! Jiangalieni nafsi zenu. Hawakudhuruni waliopotoka ikiwa mmeongoka.” Kwa hakika nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: “Hakika pindi watu wanapomuona dhalimu na wasimshike mikoni yake, huenda Allaah kwa ujumla akawateremshia adhabu kutoka Kwake.” [Abu Daawuwd, At-Tirmidhiy na
 
024-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Adhabu Kali Kwa Mwenye Kuamrisha Mema Au Kukataza Maovu Kisha Kauli Yake Ikawa Kinyume Na Matendo Yake


Riyaadhw Asw-Swaalihiyn



باب تغليظ عقوبة من أمر بمعروف أَوْ نهى عن منكر وخالف قوله فعله

024 - Mlango Wa Adhabu Kali Kwa Mwenye Kuamrisha Mema Au Kukataza Maovu Kisha Kauli Yake Ikawa Kinyume Na Matendo Yake



Alhidaaya.com





قَالَ الله تَعَالَى:

أَتَأْمُرُونَ النَّاسَ بِالْبِرِّ وَتَنسَوْنَ أَنفُسَكُمْ وَأَنتُمْ تَتْلُونَ الْكِتَابَ ۚ أَفَلَا تَعْقِلُونَ ﴿٤٤﴾

Je, mnaamrisha watu watende mema na mnajisahu nafsi zenu na hali ya kuwa nyinyi mnasoma Kitabu; je hamtii akilini? [Al-Baqarah: 44]



يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لِمَ تَقُولُونَ مَا لَا تَفْعَلُونَ﴿٢﴾

Enyi walioamini! Kwanini mnasema yale msiyoyafanya?



كَبُرَ مَقْتًا عِندَ اللَّـهِ أَن تَقُولُوا مَا لَا تَفْعَلُونَ﴿٣﴾

Ni chukizo kubwa mno mbele ya Allaah kwamba mnasema yale msiyoyafanya. [Asw- Swaff: 2-3 ]



وَمَا أُرِيدُ أَنْ أُخَالِفَكُمْ إِلَىٰ مَا أَنْهَاكُمْ عَنْهُ ۚ

…Nami sitaki kukukhalifuni kufanya ninayokukatazeni… [Huwd: 88]







Hadiyth – 1

وعن أَبي زيد أسامة بن زيد بن حارثة رضي الله عنهما، قَالَ: سمعت رَسُول الله صلى الله عليه وسلم يقول: ((يُؤْتَى بالرَّجُلِ يَوْمَ القيَامَةِ فَيُلْقَى في النَّارِ، فَتَنْدَلِقُ أقْتَابُ بَطْنِهِ فَيدُورُ بِهَا كَمَا يَدُورُ الحِمَارُ في الرَّحَى، فَيَجْتَمِعُ إِلَيْه أهْلُ النَّارِ، فَيَقُولُونَ: يَا فُلانُ، مَا لَكَ؟ أَلَمْ تَكُ تَأمُرُ بالمعْرُوفِ وَتنهَى عَنِ المُنْكَرِ؟ فَيقُولُ: بَلَى، كُنْتُ آمُرُ بِالمَعْرُوفِ وَلا آتِيهِ، وأنْهَى عَنِ المُنْكَرِ وَآتِيهِ)). مُتَّفَقٌ عَلَيهِ

Kutoka kwa Abuu Zayd Usaamah bin Zayd bin Haarithah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa amesema: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) akisema: “Ataletwa mtu siku ya Qiyaamah na atiwe motoni. Matumbo yake yatatoka nje (huku ameyashika mkononi mwake) na atakuwa anazunguka nayo kama anavyozunguka punda anayesaga katika mtambo.” Watakusanyika mbele yake watu wa motoni na waseme: “Ee Fulani, una nini? Si wewe ndiye uliokuwa ukituamrisha mema na kutukataza maovu?” Atasema Fulani: “Ndio, nilikuwa nikiamrisha mema lakini mimi mwenyewe sifanyi na nilikuwa nikikataza maovu na nikiyaendea (nikifanya ninayokataza).” [Al-Bukhaariy, Muslim na Ahmad]





Share Email Telegram WhatsApp
‹ 023-Riyaadhw As-Swaalihiyn: Mlango Wa Kuamrisha Mema Na Kukataza Maovuup025-Riyaadhw As-Swaalihiyn: Mlango Wa Amri Ya kurudisha Amana ›
Chapisha
Bonyeza
Visitors

Sikiliza
Qur-aan
Hadiyth
Du'aa Skip to main content

Ukurasa Wa Kwanza
Search form
Tafuta
Submit
Ukurasa Wa Kwanza /Mukhtasari Wa 'Aqiydah Ya Muislamu: Maswali Na Majibu /39-Mukhtasari Aqiydah Ya Muislamu: Nani tumuombe tukitaka kuombewa shafaa'ah na Nabiy?
39-Mukhtasari Aqiydah Ya Muislamu: Nani tumuombe tukitaka kuombewa shafaa'ah na Nabiy?

Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com







39-Nani tumuombe tukitaka kuombewa shafaa'ah na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)?



Tukitaka kuombewa shafaa’ah na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) inapasa tumuombe Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa).



قُل لِّلَّـهِ الشَّفَاعَةُ جَمِيعًا ۖ

Sema: “Uombezi wote ni wa Allaah Pekee. [Az-Zumar: 44]



((اللّهم شفّعه فيّ)) رواه الترمذي وقال حديث حسن.

((Ee Allaah! Ikubali shafaa’ah (maombezi) yake kwangu))
 
025-Riyaadhw As-Swaalihiyn: Mlango Wa Amri Ya kurudisha Amana


Riyaadhw Asw-Swaalihiyn



025 – Mlango Wa Amri Ya kurudisha Amana

باب الأمر بأداء الأمانة



Alhidaaya.com



قَالَ الله تَعَالَى:



إِنَّ اللَّـهَ يَأْمُرُكُمْ أَن تُؤَدُّوا الْأَمَانَاتِ إِلَىٰ أَهْلِهَا

Hakika Allaah Anakuamrisheni kurudisha amana kwa wenyewe. [An-Nisaa: 58]



إِنَّا عَرَضْنَا الْأَمَانَةَ عَلَى السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَالْجِبَالِ فَأَبَيْنَ أَن يَحْمِلْنَهَا وَأَشْفَقْنَ مِنْهَا وَحَمَلَهَا الْإِنسَانُ ۖ إِنَّهُ كَانَ ظَلُومًا جَهُولًا ﴿٧٢﴾

Hakika Sisi Tulihudhurisha amana kwa mbingu na ardhi na majabali vikakataa kuibeba na vikaiogopa; lakini insani akaibeba. Hakika yeye amekuwa dhalimu mno, jahili mno. [Al-Ahzaab: 72]







Hadiyth – 1

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه: أن رَسُول الله صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((آيةُ المُنافقِ ثلاثٌ: إِذَا حَدَّثَ كَذَبَ، وَإِذَا وَعدَ أخْلَفَ، وَإِذَا اؤْتُمِنَ خَانَ)). مُتَّفَقٌ عَلَيهِ

وفي رواية: ((وَإِنْ صَامَ وَصَلَّى وَزَعَمَ أنَّهُ مُسْلِمٌ))

Imepokewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) ya kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) amesema: “Alama za mtu mnafiki ni tatu: Anaposema husema uongo, na napoahidi hatakelezi, na anapoaminiwa hufanya khiyana” [Al-Bukhaariy na Muslim]

Riwaayah nyingine: “Japokuwa atafunga na kuswali na akajichukulia kuwa yeye ni Muislamu.”









Hadiyth – 2

وعن حذيفة بن اليمان رضي الله عنه قَالَ: حدثنا رَسُول الله صلى الله عليه وسلم حدِيثَينِ قَدْ رأيْتُ أحَدَهُمَا وأنا أنتظرُ الآخر: حدثنا أن الأمانة نَزلت في جَذرِ قلوبِ الرجال، ثُمَّ نزل القرآن فعلموا مِنَ القرآن، وعلِموا من السنةِ.

ثُمَّ حدّثنا عن رفع الأمانة، فَقَالَ: ((يَنَامُ الرَّجُلُ النَّوْمَةَ فَتُقْبَضُ الأَمَانَةُ مِنْ قَلْبهِ، فَيَظَلُّ أثَرُهَا مِثلَ الوَكْتِ، ثُمَّ يَنَامُ النَّومَةَ فَتُقْبَضُ الأَمَانَةُ مِنْ قَلْبهِ، فَيَظَلُّ أثَرُهَا مِثلَ أَثَرِ المَجْلِ، كَجَمْرٍ دَحْرَجْتَهُ عَلَى رِجْلِكَ فَنَفِطَ، فَتَرَاهُ مُنْتَبرًا وَلَيسَ فِيهِ شَيءٌ)) ثُمَّ أخَذَ حَصَاةً فَدَحْرَجَهُ عَلَى رِجْلِهِ ((فَيُصْبحُ النَّاسُ يَتَبَايعُونَ، فَلا يَكَادُ أحدٌ يُؤَدّي الأَمَانَةَ حَتَّى يُقَالَ: إنَّ في بَني فُلانٍ رَجُلًا أمينًا، حَتَّى يُقَالَ لِلرَّجُلِ: مَا أجْلَدَهُ! مَا أَظْرَفَهُ! مَا أعْقَلَهُ! وَمَا في قَلْبِهِ مِثْقَالُ حَبَّة مِن خَرْدَل مِنْ إيمَان وَلَقدْ أتَى عَلَيَّ زَمَانٌ وَمَا أُبَالِي أيُّكُمْ بَايَعْتُ: لَئن كَانَ مُسْلِمًا لَيَرُدَّنَّهُ عليَّ دِينهُ، وَإنْ كَانَ نَصْرانِيًّا أَوْ يَهُودِيًا لَيَرُدَّنَّهُ عَلَيَّ سَاعِيهِ، وَأَمَّا اليَوْمَ فَمَا كُنْتُ أُبَايعُ مِنْكُمْ إلا فُلانًا وَفُلانًا)). مُتَّفَقٌ عَلَيهِ

Imepokewa kutoka kwake Hudhayfah bin Al-Yamaan (Radhwiya Allaahu 'anhu) ya kwamba: Ametuhadithia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) Hadiyth mbili, nami nimeiona Hadiyth moja kati ya hizo mbili na ninangoja kuiona hiyo ya pili. Alituhadithia ya kwamba, amana iliteremshwa na kukita katika mioyo ya watu. Wakati Qur-aan iliteremshwa waliweza kuelimishwa kwa Qur-aan na Sunnah. Kisha akatuhadithia kuhusu kunyanyuliwa amanah, akasema: “Analala mtu usiku na anapoamka na anajikuta kuwa amatolewa uaminifu katika moyo wake na kubakishwa kivuli chake tu. Kisha analala tena usiku na uaminifu unaondolewa katika moyo wake na kubakia alama ndogo mfano wa lenge lenge kama anapoguswa mmoja wenu na moto katika mguu wake na hivyo kupata lenge lenge ambalo linapasuka basi ndani huwa tupu kabisa.” Kisha akachukua vijiwe na kuanza kujipiga mguu wake: “Watu watakuwa wanapambazukia katika biashara (kuuza na kununua), lakini hakuna hata mmoja atayetekeleza uaminifu (kurudisha amanah), mpaka imesemwe, hakika katika ukoo fulani kuna mtu muaminifu, mpaka pia isemwe kwa mtu (ambaye ni hodari katika mambo ya dunia). Tazama jinsi gani alivyo hodari, jinsi gani alivyo mzuri, na jinsi gani alivyo na akili, lakini kwenye moyo wake hana hata chembe ya iymaan.” Hakika nimefikiwa na wakati ambapo sikujali mtu gani ninayefanya naye biashara. Akiwa ni Musilamu basi Dini yake ni dhamana tosha kwangu, na akiwa ni Naswara, au Myahudi basi (mzazi) au walii wake atatimiza amana hiyo (ni dhamana tosha). Lakini ama leo sifanyi biashara miongoni mwenu isipokuwa fulani na fulani. [Al-Bukhaariy na Muslim]







Hadiyth – 3

وعن حُذَيفَة وأبي هريرة رضي الله عنهما قالا: قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: ((يَجمَعُ اللهُ تبَارَكَ وَتَعَالَى النَّاسَ فَيَقُومُ المُؤمِنُونَ حَتَّى تُزْلَفَ لَهُمُ الجَنَّةُ، فَيَأتُونَ آدَمَ صَلَواتُ اللهِ عَلَيهِ، فَيقُولُونَ: يَا أَبَانَا اسْتَفْتِحْ لَنَا الجَنَّةَ، فَيقُولُ: وَهَلْ أخْرَجَكُمْ مِنَ الجَنَّةِ إلا خَطيئَةُ أبيكُمْ! لَسْتُ بِصَاحِبِ ذلِكَ، اذْهَبُوا إِلَى ابْنِي إِبْراهيمَ خَلِيل اللهِ.

قَالَ: فَيَأتُونَ إبرَاهِيمَ فَيَقُولُ إبراهيم: لَسْتُ بِصَاحِبِ ذلِكَ إِنَّمَا كُنْتُ خَليلًا مِنْ وَرَاءَ وَرَاءَ، اعْمَدُوا إِلَى مُوسَى الَّذِي كَلَّمَهُ الله تَكليمًا. فَيَأتُونَ مُوسَى، فَيَقُولُ: لستُ بِصَاحِبِ ذلِكَ، اذْهَبُوا إِلَى عِيسى كلمةِ اللهِ ورُوحه، فيقول عيسى: لستُ بصَاحبِ ذلِكَ.

فَيَأتُونَ مُحَمَّدًا صلى الله عليه وسلم فَيَقُومُ فَيُؤذَنُ لَهُ، وتُرْسَلُ الأَمَانَةُ وَالرَّحِمُ فَيَقُومانِ جَنْبَتَي الصِّرَاطِ يَمِينًا وَشِمَالًا فَيَمُرُّ أوَّلُكُمْ كَالبَرْقِ)) قُلْتُ: بأبي وَأمِّي، أيُّ شَيءٍ كَمَرِّ البَرقِ؟ قَالَ: ((ألَمْ تَرَوا كَيْفَ يمُرُّ وَيَرْجِعُ في طَرْفَةِ عَيْن، ثُمَّ كَمَرّ الرِّيحِ، ثُمَّ كَمَرِّ الطَّيْرِ، وَأَشَدِّ الرِّجَال تَجْري بهمْ أعْمَالُهُمْ، وَنَبيُّكُمْ قَائِمٌ عَلَى الصِّراطِ، يَقُولُ: رَبِّ سَلِّمْ سَلِّمْ، حَتَّى تَعْجِزَ أعْمَالُ العِبَادِ، حَتَّى يَجِيء الرَّجُلُ لا يَسْتَطِيعُ السَّيْرَ إلا زَحْفًا، وَفي حَافَتي الصِّراطِ كَلاَلِيبُ معَلَّقَةٌ مَأمُورَةٌ بِأخْذِ مَنْ أُمِرَتْ بِهِ، فَمَخْدُوشٌ نَاجٍ، وَمُكَرْدَسٌ في النَّارِ)) وَالَّذِي نَفْسُ أَبي هُرَيْرَةَ بِيَدِهِ، إنَّ قَعْرَ جَهَنَّمَ لَسَبْعُونَ خَرِيفًا. رواه مسلم

Imepokewa kutoka kwa Hudhayfah na Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) ya kwamba: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) amesema: “Allaah (Subhaanahu Wa Ta'aalaa) Atawakusanya watu. Watasimama waumini mpaka watakuja karibu na Jannah, na hapo watamuendea Aadam (‘Alayhis Salaam) na kumwambia: “Ee Aadam baba yetu, tufungulie Jannah. Atasema: Ni kosa la baba yenu ndio lililowatoa nyinyi katika Jannah. Mimi sina uwezo wa kuwasaidia, hivyo nendeni kwa mtoto wangu Ibraahiym (‘Alayhis Salaam), ni kipenzi cha Allaah (Subhaanahu Wa Ta'aalaa). Amasema: Watakwenda kwa Ibraahiym (‘Alayhis Salaam), na watamwambia. Atasema: Mimi sina uwezo, hakika mimi nilikuwa kipenzi tu na wala sina darja hiyo ya juu. Nendeni kwa Muwsaa ambaye Allaah (Subhaanahu Wa Ta'aalaa) Alizungumza naye kwa uwazi kabisa. Watakuja kwa Muwsaa (‘Alayhis Salaam), naye atasema: Mimi si mwenyewe wa jambo hilo. Hapo watakuja kwa Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa salaam). Atasimama mbele ya Allaah (Subhaanahu Wa Ta'aalaa) na atakubaliwa kuwatetea watu. Itatumwa amana na kuunganisha kizazi, nazo zitasimama pembezoni mwa Swiraatw (njia) kulia na kushoto. Wa mwanzo wenu watapita kama umeme. Nikasema: Baba yangu na mama yangu wawe fidia kwako unamaanisha nini? Akasema: “Huoni cheche za umeme zinazokwenda na kurudi katika kupepesa jicho? Kisha watapita kama upepo, kisha kama ndege, na wengine kwa kasi ya watu wanaokimbia, na tofauti hii (ya kasi) itakuwa kwa sababu ya ‘amali za kila mmoja wenu. Na Rasuli wenu (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) atakuwa amesimama juu ya Swiraatw, anasema: Mola wangu! Wasalimishe, wasalimishe. Mpaka matendo ya waja yashindwe, mpaka mtu aje hawezi kupita isipokuwa kwa kutambaa na katika pande zote mbili za Swiraatw kuna koleo zimening’ing’izwa, ambazo zimeamriwa (na Allaah Subhaanahu Wa Ta'aalaa). Yule atakayekwaruzwa atakuwa ni mwenye kufaulu na wasiokuwa wao wataingia motoni. Na yule ambaye kwamba nafsi ya Abuu Hurayrah ipo mikononi Mwake, hakika urefu wa Jahannam ni masafa miaka sabini. [Muslim]







Hadiyth – 4

وعن أَبي خُبيب- بضم الخاء المعجمة- عبد الله بن الزبير رضي الله عنهما، قَالَ: لَمَّا وَقفَ الزُّبَيْرُ يَوْمَ الجَمَل دَعَانِي فَقُمْتُ إِلَى جَنْبه، فَقَالَ: يَا بُنَيَّ، إنَّهُ لا يُقْتَلُ اليَومَ إلا ظَالِمٌ أَوْ مَظْلُومٌ، وَإنِّي لا أراني إلا سَأُقْتَلُ اليوم مظلومًا، وإنَّ مِنْ أكبرَ هَمِّي لَدَيْنِي، أفَتَرَى دَيْننا يُبقي من مالِنا شَيئًا؟ ثُمَّ قَالَ: يَا بُنَيَّ، بعْ مَا لَنَا وَاقْضِ دَيْنِي، وَأوْصَى بِالثُّلُثِ وَثُلُثِهِ لِبَنِيهِ، يعني لبني عبد الله بن الزبير ثُلُثُ الثُّلُث. قَالَ: فَإنْ فَضَلَ مِنْ مَالِنَا بَعْدَ قَضَاءِ الدَّينِ شَيء فَثُلُثُه لِبَنِيكَ. قَالَ هِشَام: وَكَانَ بَعْضُ وَلَدِ عَبْدِ اللهِ قَدْ وَازى بَعْضَ بَنِي الزُّبَيْرِ خُبيبٍ وَعَبَّادٍ، وَلهُ يَوْمَئذٍ تِسْعَةُ بَنينَ وَتِسْعُ بَنَات.

قَالَ عَبدُ الله: فَجَعلَ يُوصينِي بدَيْنِهِ وَيَقُولُ: يَا بُنَيَّ، إنْ عَجَزْتَ عَن شَيْءٍ مِنْهُ فَاسْتَعِنْ عَلَيهِ بِمَوْلاَيَ. قَالَ: فَوَاللهِ مَا دَرَيْتُ مَا أرَادَ حَتَّى قُلْتُ: يَا أبَتِ مَنْ مَوْلاَكَ؟ قَالَ: الله. قَالَ: فَوَاللهِ مَا وَقَعْتُ في كُرْبةٍ مِنْ دَيْنِهِ إلا قُلْتُ: يَا مَوْلَى الزُّبَيْرِ اقْضِ عَنْهُ دَيْنَهُ فَيَقْضِيَهُ. قَالَ: فَقُتِلَ الزُّبَيْرُ وَلَم يَدَعْ دِينَارًا وَلا دِرْهمًا إلا أرَضِينَ، مِنْهَا الغَابَةُ وإحْدَى عَشْرَةَ دَارًا بالمَدِينَةِ، وَدَارَيْنِ بالبَصْرَةِ، ودَارًا بالكُوفَةِ، ودَارًا بمِصْرَ.

قَالَ: وَإِنَّمَا كَانَ دَيْنُهُ الَّذِي كَانَ عَلَيهِ أنَّ الرَّجُلَ كَانَ يَأتِيهِ بالمال، فَيَسْتَودِعُهُ إيَّاهُ، فَيَقُولُ الزُّبَيْرُ: لا، وَلَكِنْ هُوَ سَلَفٌ إنِّي أخْشَى عَلَيهِ الضَّيْعَةَ. وَمَا وَليَ إمَارَةً قَطُّ وَلا جِبَايَةً، ولا خراجًا، وَلا شَيئًا إلا أنْ يَكُونَ في غَزْوٍ مَعَ رسولِ الله صلى الله عليه وسلم أَوْ مَعَ أَبي بَكْرٍ وَعُمَرَ وَعُثْمَانَ رضي الله عنهم، قَالَ عَبدُ الله: فَحَسَبْتُ مَا كَانَ عَلَيهِ مِن الدَّيْنِ فَوَجَدْتُهُ ألْفيْ ألْفٍ وَمئَتَي ألْف ‍! فَلَقِيَ حَكِيمُ بنُ حِزَام عَبْدَ الله بْنَ الزُّبَيْرِ، فَقَالَ: يَا ابْنَ أخِي، كَمْ عَلَى أخي مِنَ الدَّيْنِ؟ فَكَتَمْتُهُ وَقُلْتُ: مِائَةُ ألْف. فَقَالَ حَكيمٌ: واللهِ مَا أرَى أمْوَالَكُمْ تَسَعُ هذِهِ. فَقَالَ عَبْدُ اللهِ: أرَأيْتُكَ إنْ كَانَتْ ألْفَي ألف وَمائَتَيْ ألْف؟ قَالَ: مَا أرَاكُمْ تُطيقُونَ هَذَا، فَإنْ عَجَزْتُمْ عَنْ شَيءٍ مِنْهُ فَاسْتَعِينُوا بي.

قَالَ: وَكَانَ الزُّبَيرُ قَد اشْتَرَى الغَابَةَ بِسَبْعِينَ ومائة ألف، فَبَاعَهَا عَبدُ اللهِ بِألْفِ ألْف وَسِتّمِائَةِ ألْف، ثُمَّ قَامَ فَقَالَ: مَنْ كَانَ لَهُ عَلَى الزُّبَيرِ شَيْء فَلْيُوافِنَا بِالغَابَةِ، فَأتَاهُ عَبدُ اللهِ بنُ جَعفَر، وَكَانَ لَهُ عَلَى الزُّبَيرِ أرْبَعمائةِ ألْف، فَقَالَ لعَبدِ الله: إنْ شِئْتُمْ تَرَكْتُهَا لَكمْ؟ قَالَ عَبدُ الله: لا، قَالَ: فَإنْ شِئتُمْ جَعَلْتُمُوهَا فِيمَا تُؤَخِّرُونَ إنْ إخَّرْتُمْ، فَقَالَ عَبدُ الله: لا، قَالَ: فَاقْطَعُوا لِي قطْعَةً، قَالَ عَبدُ الله: لَكَ مِنْ هاهُنَا إِلَى هَاهُنَا. فَبَاعَ عَبدُ اللهِ مِنهَا فَقَضَى عَنْهُ دَينَه وَأوْفَاهُ، وَبَقِيَ مِنْهَا أرْبَعَةُ أسْهُم وَنِصْفٌ، فَقَدِمَ عَلَى مُعَاوِيَة وَعنْدَهُ عَمْرُو بْنُ عُثْمَانَ، وَالمُنْذِرُ بْنُ الزُّبَيْرِ، وَابْنُ زَمْعَةَ، فَقَالَ لَهُ مُعَاويَةُ: كَمْ قُوِّمَتِ الغَابَةُ؟ قَالَ: كُلُّ سَهْم بمائَة ألف، قَالَ: كَمْ بَقِيَ مِنْهَا؟ قَالَ: أرْبَعَةُ أسْهُم وَنصْفٌ، فَقَالَ المُنْذِرُ بْنُ الزُّبَيرِ: قَدْ أخَذْتُ مِنْهَا سَهمًا بِمائَةِ ألف، قَالَ عَمْرُو بْنُ عُثْمَانَ: قَدْ أخَذْتُ مِنْهَا سَهْمًا بمائَةِ ألْف. وَقالَ ابْنُ زَمْعَةَ: قَدْ أخَذْتُ سَهْمًا بِمائَةِ ألْف، فَقَالَ مُعَاويَةُ: كَمْ بَقِيَ مِنْهَا؟ قَالَ: سَهْمٌ ونصْفُ سَهْم، قَالَ: قَدْ أخَذْتُهُ بخَمْسِينَ وَمائَةِ ألْف. قَالَ: وَبَاعَ عَبدُ الله بْنُ جَعفَر نَصيبهُ مِنْ مَعَاوِيَةَ بستِّمِائَةِ ألْف.

فَلَمَّا فَرَغَ ابْنُ الزُّبَيرِ مِنْ قَضَاءِ دَيْنِهِ، قَالَ بَنُو الزُّبَيرِ: اقسمْ بَينَنَا ميراثَنا، قَالَ: وَاللهِ لا أقْسِمُ بَيْنَكُمْ حَتَّى أنَادِي بالمَوْسم أرْبَعَ سنينَ: ألا مَنْ كَانَ لَهُ عَلَى الزُّبَيرِ دَيْنٌ فَلْيَأتِنَا فَلْنَقْضِهِ. فَجَعَلَ كُلّ سَنَةٍ يُنَادِي في المَوْسِمِ، فَلَمَّا مَضَى أرْبَعُ سنينَ قَسَمَ بيْنَهُمْ وَدَفَعَ الثُّلُثَ. وَكَانَ للزُّبَيْرِ أرْبَعُ نِسْوَةٍ، فَأصَابَ كُلَّ امرَأةٍ ألْفُ ألف وَمِئَتَا ألْف، فَجَميعُ مَالِه خَمْسُونَ ألف ألْف وَمِئَتَا ألْف. رواه البخاري

Imepokwa kutoka kwa Abuu Khubayb, ‘Abdullaah bin Az-Zubayr (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) ya kwamba: Aliposimama Az-Zubayr katika vita vya Ngamia, aliniita nami nikasimama ubavuni mwake. Alinambia: Ee mtoto wangu! Hautauliwa leo isipokuwa dhalimu au aliyedhulumiwa. Nami nina hakika ya kuwa nitauliwa leo kwa dhulma. Na hakika hamu yangu kubwa ni deni langu. Je, unafikiria kutabakia chochote katika mali baada ya kulipa deni? Kisha akasema: Ee mtoto wangu! Uza rasimali yangu na ulipe deni langu. Na nausia ya kwamba thuluthi ya thuluthi (1/9) iwe ni ya watoto wako (yaani ‘Abdullaah bin Az-Zubayr), kwa kile kitakachobakia. Baada ya hii ikiwa kutabakia chochote basi thuluthi itakuwa ni ya watoto wako. Amasema Hishaam: Na walikuwa baadhi ya watoto wa ‘Abdullaah ni rika moja na watoto wa Az-Zubayr, kama Khubayb na ‘Abbaad, na wakati huo alikuwa na vijana tisa na mabinti tisa. Akasema: Ee mtoto wangu! Ukishindwa kulipa deni langu basi takamsaada kwa Bwana wangu. Akasema: Naapa kwa Allaah! Sikufahamu alilokusudia mpaka nilipouuliza: Ewe baba yangu! Nani bwana wako? Akasema: Allaah. Akasema tena (‘Abdullaah): Naapa kwa Allaah! Sijapatwa tena na shida ya deni lake isipokuwa nilikuwa nasema, Ee Bwana wa Az-Zubayr mwondoshee deni lake, Naye Allaah (Subhaanahu Wa Ta'aalaa) Alikuwa anamuondoshea. Az-Zubayr (Radhwiya Allaahu 'anhu) aliuliwa siku hiyo na hakuacha hata dinari moja wala dirhamu isipokuwa vipande viwili vya ardhi, moja katika hiyo ikiwa katika sehemu ya Ghaabah na nyumba kumi na moja Madiynah, na nyumba mbili Basrah, na nyumba moja Kufah, na nyumba moja Misri. Na kwa hakika deni lake lilitokana na watu waliokuwa wakimjia ili awahifadhie mali zao, lakini Az-Zubayr alikuwa anawaambia: Hapana! Siwezi jukumu hilo kwani huenda ikapotea lakini naweza kuichukua hiyo amana kama deni juu yangu. Yeye hakukubali nafasi ya uongozi wala wadhifa wa kukusanya kodi wala kitu chengine chochote isipokuwa ile ngawira aliyopatiwa katika vita alivyopigana wakati wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam), au Abu Bakr, au ‘Umar, au ‘Uthmaan (Radhwiya Allaahu 'anhum). Akasema (‘Abdullaah): Nikahesabu deni lake na jumla ikafika million mbili na laki mbili. Nilikutana na Hakiym bin Hizaam, naye akasema: Ee mtoto wa ndugu yangu! Ndugu yangu anadenia la kiasi gani? Nikaficha hilo kwa kusema: Laki moja. Akasema Hakiym: Kwa Allaah, sidhani ya kwamba mali yenu itafikia kiwango hicho. Nikasema: Unaonaje deni likiwa ni milioni mbili na laki mbili? Akasema: Sidhani ya kwamba mtaweza kuubeba mzigo huo, hivyo mkiwa na uzito wa aina yoyote njooni kwangu kwa msaada. Az-Zubayr alikuwa ameinunua ile ardhi ya Ghaabah kwa laki moja na elfu sabini, nami nikauza kwa milioni moja na laki sita. Kisha akasimama ‘Abdullaah na kunadi Az-Zubayr atukute katika ardhi ya Ghaabah. Akaja ‘Abdullaah bin Ja’far, ambaye alikuwa anamdai Az-Zubayr laki nne. Alimwambia ibn Zubayr: Mkipenda nitawaachia deni hilo? Nikasema: Hapana, Akasema: Ikiwa mnataka nitawapatia muda wa kunilipa. Akasema ibn Zubayr: Hapana. Akasema ibn Ja’far basi nikatie kipande cha ardhi. Akasema ‘Abdullaah: Kipande chako ni kuanzia hapa mpaka hapa. Kwa njia hii ‘Abdullaah alimlipia baba yake deni. Baada ya hapo ikabaki ardhi yenye kipimo cha siham nne na nusu. Akaja Mu’awiyyah pamoja naye ni ‘Amru bin ‘Uthmaan na Al-Mundhir bin Az-Zubayr na ibn Zam’ah. Akasema Mu’awiyyah: Hii Ghaabah ni bei gani? Akasema: Kila siham ni laki moja. Akasema: Imebakia kiasi gani? Akasema: Siham nne na nusu. Hapo akasema Mundhir bin Zubayr: Mimi nimechukua sihim moja kwa bei hiyo ya laki moja. Akasema ‘Amru bin ‘Uthmaan: Nami nachukua sihim moja kwa bei hiyo ya laki moja. Na akasema ibn Zam’ah: Nami nimechukua sihim moja kwa bei ya laki moja. Akasema Mu’awiyyah: Imebaki kiasi gani cha ardhi? Akasema (‘Abdullaah): Sihim moja na nusu. Akasema Mu’awiyyah: Nimeichukua kwa laki moja na nusu. Baadae ‘Abdullaah bin Ja’far alimuuzia Mu’awiyyah sehemu yake ya ardhi kwa laki sita. ‘Abdullaah bin Zubayr alipomaliza shughuli hii yote ya kulipa madeni ya baba yake, walimjia warithi wa Az-Zubayr na kumwambia: Tupatie fungu letu la mirathi. Akasema: Naapa kwa Allaah! Sitagawa mirathi mpaka mwanzo ninadi katika msimu wa Hijjah kwa miaka minne mfululizo. Mtu yoyote anayemdai Az-Zubayr basi atujie tumrudishie haki yake. Akajaalia kuwa ananadi kila mwaka katika msimu wa Hijjah. Ilipomalizika miaka minne aligawanya pesa zilizobakia baina yao akalipa thuluthi. Az-Zubayr alikuwa na wake wanne, hivyo kila mmke alipata milioni moja na laki mbili, kwani jumla ya mali yake yote ilikuwa milioni khamsini na laki mbili.
 
026-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Uharamu Wa Dhulma Na Amri Ya Karudisha Vilivyodhulumiwa


Riyaadhw Asw-Swaalihiyn



باب تحريم الظلم والأمر بردِّ المظالم

26 – Mlango Wa Uharamu Wa Dhulma Na Amri Ya Karudisha Vilivyodhulumiwa



Alhidaaya.com







قَالَ الله تَعَالَى:

مَا لِلظَّالِمِينَ مِنْ حَمِيمٍ وَلَا شَفِيعٍ يُطَاعُ﴿١٨﴾

Madhalimu hawatokuwa na rafiki wa dhati, na wala mwombezi anayetiiwa. [Ghaafir: 18]



وَمَا لِلظَّالِمِينَ مِن نَّصِيرٍ ﴿٧١﴾

Na madhalimu hawana yeyote mwenye kunusuru. [Al-Hajj: 71]







Hadiyth – 1

وعن جابر رضي الله عنه: أن رَسُول الله صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((اتَّقُوا الظُّلْمَ؛ فَإنَّ الظُّلْمَ ظُلُمَاتٌ يَوْمَ القِيَامَةِ. وَاتَّقُوا الشُّحَّ؛ فَإِنَّ الشُّحَّ أهْلَكَ مَنْ كَانَ قَبْلَكُمْ. حَمَلَهُمْ عَلَى أنْ سَفَكُوا دِمَاءهُمْ، وَاسْتَحَلُّوا مَحَارِمَهُمْ)). رواه مسلم

Imepokewa kutoka kwa Jaabir (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) amesema: “Ogopeni sana dhulma, kwani kudhulumu ni viza Siku ya Qiyaamah. Na ogopeni sana ubakhili kwani ubakhili uliwaangamiza waliokuwa kabla yenu, uliwafanya wamwage damu zao na wakahalalisha walioharamishiwa.” [Muslim]







Hadiyth – 2

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه: أن رَسُول الله صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((لَتُؤَدُّنَّ الحُقُوقَ إِلَى أهْلِهَا يَومَ القِيَامَةِ، حَتَّى يُقَادَ للشَّاةِ الجَلْحَاءِ مِنَ الشَّاةِ القَرْنَاءِ)). رواه مسلم

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) amesema: “Mtaendelea kutimiza haki za wenyewe Siku ya Qiyaamah mpaka kondoo asiyekuwa na pembe alipize kisasi juu ya mwenye pembe.” [Muslim]







Hadiyth – 3

وعن ابن عمر رضي الله عنهما، قال: كُنَّا نَتَحَدَّثُ عَنْ حَجَّةِ الوَدَاعِ، والنَّبيُّ صلى الله عليه وسلم بَيْنَ أَظْهُرِنَا، وَلا نَدْرِي مَا حَجَّةُ الوَدَاعِ حَتَّى حَمِدَ اللهَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم وَأثْنَى عَلَيهِ ثُمَّ ذَكَرَ المَسْيحَ الدَّجَّال فَأطْنَبَ في ذِكْرِهِ، وَقَالَ: ((مَا بَعَثَ اللهُ مِنْ نَبيٍّ إلا أنْذَرَهُ أُمَّتَهُ، أنْذَرَهُ نُوحٌ وَالنَّبِيُّونَ مِنْ بَعْدِهِ، وَإِنَّهُ إنْ يَخْرُجْ فِيكُمْ فَما خَفِيَ عَليْكُمْ مِنْ شَأنِه فَلَيْسَ يَخْفَى عَليْكُم، إنَّ رَبَّكُمْ لَيْسَ بأعْوَرَ وإنَّهُ أعْوَرُ عَيْنِ اليُمْنَى، كَأنَّ عَيْنَهُ عِنَبَةٌ طَافِيَةٌ. ألا إنَّ الله حَرَّمَ عَلَيْكُمْ دِمَاءكُمْ وَأمْوَالَكُمْ كحُرْمَةِ يَوْمِكُمْ هَذَا، في بلدكم هذا، في شَهْرِكُمْ هَذَا، ألا هَلْ بَلّغْتُ؟)) قالُوا: نَعَمْ، قَالَ: ((اللَّهُمَّ اشْهَدْ)) ثلاثًا ((وَيْلَكُمْ- أَوْ وَيْحَكُمْ، انْظُروا: لا تَرْجعُوا بَعْدِي كُفّارًا يَضْرِبُ بَعْضُكُمْ رِقَابَ بَعْضٍ)). رواه البخاري، وروى مسلم بعضه

Imepokewa kutoka kwa ibn ‘Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kuwa amesema: Tulikuwa tukizungumza Hijjah ya kuaga (Hijjatul Wadaa’) baina yetu wala hatujui nini Hijjah ya kuaga mpaka Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) alipomuhimidi Allaah (Subhaanahu Wa Ta'aalaa) na kumtukuza. Baada ya hapo akamtaja Masiyh Dajjaal na kuzungumza kwa kirefu. Kisha akasema: “Kila Rasuli aliyetumwa na Allaah (Subhaanahu Wa Ta'aalaa) amewaonya Ummah wake kuhusu (Masiyh Dajjaal). Nuwh na Rusul waliokuja baada yake walionya kumhusu. Na hakika yeye atatoka miongoni mwenu, hataweza kujificha (kwani tayari mmeshamjua), ukweli wake hautafichika nanyi. Hakika Mola wenu si chogo, bali yeye ni chogo jicho lake kulia kama kwamba jicho lake ni zabibu iliyovimba. Tahadharini! Hakika Allaah (Subhaanahu Wa Ta'aalaa) Ametahadharisha kwenu damu na mali yenu kama utukufu wa siku yenu hii (siku ya Hijjah), katika mji wenu huu (yaani Makkah), katika mwezi wenu huu (Dhul Hijjah). Je, nimefikisha ujumbe? Wakasema (Maswahaba): Ndio. Akasema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam): Ee Allaah! Shuhudia – mara tatu. Ole wenu tizameni sana! Msirudi baada yangu makafiri mnakata shingo (mnauana).” [Al-Bukhaariy na Muslim amepokea baadhi yake)







Hadiyth – 4

وعن عائشة رضي الله عنها: أن رَسُول الله صلى الله عليه وسلم، قَالَ: ((مَنْ ظَلَمَ قيدَ شِبْرٍ مِنَ الأرْضِ، طُوِّقَهُ مِنْ سبْعِ أرَضينَ)). مُتَّفَقٌ عَلَيهِ.

Imepokewa kutoka kwa ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) amesema: “Atakaye dhulumu ardhi kiasi cha shubiri atabebeshwa ardhi saba (siku ya Qiyaamah) [A-Bukhaariy na Muslim]







Hadiyth – 5

وعن أَبي موسى رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: ((إنَّ الله لَيُمْلِي لِلظَّالِمِ، فَإِذَا أخَذَهُ لَمْ يُفْلِتْهُ))، ثُمَّ قَرَأَ: {وكَذَلِكَ أَخْذُ رَبِّكَ إِذَا أَخَذَ الْقُرَى وَهِيَ ظَالِمَةٌ إِنَّ أَخْذَهُ أَلِيمٌ شَدِيدٌ} [هود: 102] مُتَّفَقٌ عَلَيهِ

Imepokewa na Abuu Muwsaa (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) amesema: “Hakika Allaah Anampatia muda dhalimu (kwa kumcheleweshea adhabu), lakini anapomshika hatoki katika adhabu Yake. Kisha akasoma: Na hivyo ndivyo mkamato wa Rabb wako unavyokuwa Anapokamata miji na huku ikifanya dhulma. Hakika mkamato Wake unaumiza vikali. [Huwd: 102]” [Al-Bukhaariy na Muslim]







Hadiyth – 6

وعن معاذ رضي الله عنه قَالَ: بَعَثَنِي رَسُول الله صلى الله عليه وسلم فَقَالَ: ((إنَّكَ تَأتِي قَوْمًا مِنْ أهلِ الكِتَابِ فَادْعُهُمْ إِلَى شَهَادَةِ أنْ لا إلَهَ إلا الله، وَأنِّي رسولُ الله، فَإنْ هُمْ أَطَاعُوا لِذلِكَ، فَأعْلِمْهُمْ أنَّ اللهَ قَدِ افْتَرضَ عَلَيْهِمْ خَمْسَ صَلَواتٍ في كُلِّ يَوْمٍ وَلَيلَةٍ، فَإِنْ هُمْ أطَاعُوا لِذَلِكَ، فَأعْلِمْهُمْ أنَّ اللهَ قَدِ افْتَرَضَ عَلَيْهِمْ صَدَقَةً تُؤخَذُ مِنْ أغْنِيَائِهِمْ فَتُرَدُّ عَلَى فُقَرَائِهِمْ، فَإنْ هُمْ أطَاعُوا لِذَلِكَ، فَإِيَّاكَ وَكَرَائِمَ أمْوَالِهِمْ، وَاتَّقِ دَعْوَةَ المَظْلُومِ؛ فإِنَّهُ لَيْسَ بَيْنَها وَبَيْنَ اللهِ حِجَابٌ)). مُتَّفَقٌ عَلَيهِ

Mu’adh (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) alinituma kwa kuniambia: “Hakika utakwenda kwa (watu wa Ahlul Kitaab). Mwanzo waite katika kushuhudia na kukubali kuwa hapana Mola Apasaye kuabudiwa kwa haki ila Allaah na kuwa mimi ni Rasuli wa Allaah. Wanapokutii kwa hilo, wafahamishe kuwa Allaah Amewafaradhishia Swalaah tano kwa kila mchana na usiku. Wanapokutii kwa hilo, wafahamishe kuwa Allaah Amewafaradhishia Swadaqah (Zakaah) inayochukuliwa kutoka kwa matajiri wao na kurudishwa kwa mafakiri miongoni mwao. Wanapokutii kwa hilo, basi tahadhari sana na mali yao ya thamani. Na ogopa sana du’aa ya mwenye kudhulimiwa hiyo haina pazia na Allaah.” [Al-Bukhaariy na Muslim]







Hadiyth – 7

وعن أبي حُمَيدٍ عبد الرحمن بن سعد السَّاعِدِي رضي الله عنه قَالَ: اسْتَعْمَلَ النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم رَجُلًا مِنَ الأزْدِ يُقَالُ لَهُ: ابْنُ اللُّتْبِيَّةِ عَلَى الصَّدَقَةِ، فَلَمَّا قَدِمَ، قَالَ: هَذَا لَكُمْ، وَهَذَا أُهْدِيَ إِلَيَّ، فَقَامَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم عَلَى المِنْبَرِ فَحَمِدَ الله وَأثْنَى عَلَيهِ، ثُمَّ قَالَ: ((أمَّا بَعدُ، فَإِنِّي أسْتَعْمِلُ الرَّجُلَ منْكُمْ عَلَى العَمَلِ مِمَّا وَلانِي اللهُ، فَيَأتِي فَيَقُولُ: هَذَا لَكُمْ وَهَذا هَدِيَّةٌ أُهْدِيتْ إلَيَّ، أفَلا جَلَسَ في بيت أبِيهِ أَوْ أُمِّهِ حَتَّى تَأتِيَهُ هَدِيَّتُهُ إنْ كَانَ صَادِقًا، واللهِ لا يَأخُذُ أحَدٌ مِنْكُمْ شَيئًا بِغَيرِ حَقِّهِ إلا لَقِيَ الله تَعَالَى، يَحْمِلُهُ يَوْمَ القِيَامَةِ، فَلا أعْرِفَنَّ أحَدًا مِنْكُمْ لَقِيَ اللهَ يَحْمِلُ بَعيرًا لَهُ رُغَاءٌ، أَوْ بَقَرَةً لَهَا خُوَارٌ، أَوْ شَاةً تَيْعَرُ)). ثُمَّ رفع يديهِ حَتَّى رُؤِيَ عُفْرَةُ إبْطَيْهِ، فَقَالَ: ((اللَّهُمَّ هَلْ بَلَّغْتُ)) ثلاثًا مُتَّفَقٌ عَلَيهِ

Imepokewa na Abuu Humayd, ‘Abdur-Rahmaan bin Sa’d As- Saa’iydy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kuwa amesema: Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimtuma mtu kutoka katika ukoo wa Al-Azdiy aliyekuwa akiitwa inb Al-Lutbiyyah kukusanya Zakah. Aliporudi alisema: Hili ni fungo lenu na hivi nimepewa zawadi. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alisimama juu ya mimbar, akamuhidi Allaah na kumtukuza pamoja na kumsifu, kisha akasema: “Ama baada ya haya; hakika mimi nimempa kazi mtu miongoni mwenu juu ya kazi niliyopewa mamlaka na Allaah. Mtu huyo anakuja na anasema: Hiki ni chenu na hiki ni zawadi nimepewa. Basi angekaa mmoja wenu kwenye nyumba ya baba yake, au mama yake mpaka imfikie yeye zawadi hiyo yake ikiwa hakika yeye ni mkweli. Wa-Allaahi hatochukua mmoja wenu kitu chochote bila ya haki yake ila atakutana na Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) akiwa amekibeba siku ya Qiyaamah. Hivyo, nisije nikamjua yoyote kati yenu amekutana na Allaah akiwa amebeba ngamia anayeguna, au ng’ombe anayeroroma au mbuzi (kondoo) anayelia.” Kisha akanyanyua mikono yake mpaka uonekane weupe na makwapa yake, akasema: “Ee Allaah! Je, nimefikisha.” [Al-Bukhaariy, Muslim na Ahmad]







Hadiyth – 8

عن أَبي هريرة رضي الله عنه عن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((مَنْ كَانَتْ عِنْدَهُ مَظْلمَةٌ لأَخِيه، مِنْ عِرضِهِ أَوْ مِنْ شَيْءٍ، فَلْيَتَحَلَّلْهُ مِنْهُ اليَوْمَ قبْلَ أنْ لا يَكُونَ دِينَار وَلا دِرْهَمٌ؛ إنْ كَانَ لَهُ عَمَلٌ صَالِحٌ أُخِذَ مِنْهُ بِقَدْرِ مَظْلمَتِهِ، وَإنْ لَمْ يَكُنْ لَهُ حَسَنَاتٌ أُخِذَ مِنْ سَيِّئَاتِ صَاحِبِهِ فَحُمِلَ عَلَيهِ)). رواه البخاري

Imepokewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Mwenye kitu cha dhulma cha nduguye kutokana na kumvunjia heshima au kitu kingine chochote, basi amuombe amhalalishie leo kabla haijafika siku ambayo hakutakuwa na dinar wala dirham; akiwa ana ‘amali njema itachukuliwa kwa kadiri ya alichodhulumu, na ikiwa hana ‘amali njema zitachukuliwa dhambi za aliyemdhulumu na kubebeshwa (yeye).” [Al-Bukhaariy]







Hadiyth – 9

وعن عبد الله بن عمرو بن العاص رضي الله عنهما عن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((المُسْلِمُ مَنْ سَلِمَ المُسْلِمُونَ مِنْ لِسَانِهِ وَيَدِهِ، وَالمُهَاجِرُ مَنْ هَجَرَ مَا نَهَى اللهُ عَنْهُ)). مُتَّفَقٌ عَلَيهِ

Imepokewa na ‘AbduLLaah bin ‘Amru bin Al-‘Aasw (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Muislamu ni yule ambaye Waislaam wamesalimika kwa ulimi na mkono wake, na Muhajir ni yule anayehama yale aliyoyakataza Allaah.” [Al-Bukhaariy na Muslim]







Hadiyth – 10

وعنه رضي الله عنه قَالَ: كَانَ عَلَى ثَقَل النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم رَجُلٌ يُقَالُ لَهُ كِرْكِرَةُ، فَمَاتَ، فَقَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: ((هُوَ في النَّارِ)) فَذَهَبُوا يَنْظُرُونَ إِلَيْه، فَوَجَدُوا عَبَاءةً قَدْ غَلَّهَا. رواه البخاري

Kutoka kwake (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: Alikuwepo mtu mmoja akiitwa Kirkirah aliyekuwa mtunzaji wa mali ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) Akasema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): “Yeye yupo motoni”. Maswahaba wakaenda kumtazama wakapata juba alilochukua kwa khiyana.” [Al-Bukhaariy]







Hadiyth – 12

وعن أَبي بكْرة نُفَيْع بن الحارث رضي الله عنه عن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((إنَّ الزَّمَانَ قَدِ اسْتَدَارَ كَهَيْئَته يَوْمَ خَلَقَ اللهُ السَّمَاوَاتِ وَالأَرضَ: السَّنَةُ اثْنَا عَشَرَ شَهْرًا، مِنْهَا أرْبَعَةٌ حُرُمٌ: ثَلاثٌ مُتَوالِياتٌ: ذُو القَعْدَة، وذُو الحِجَّةِ، وَالمُحَرَّمُ، وَرَجَبُ مُضَرَ الَّذِي بَيْنَ جُمَادَى وَشعْبَانَ، أيُّ شَهْر هَذَا؟)) قُلْنَا: اللهُ وَرَسُولُهُ أعْلَمُ، فَسَكَتَ حَتَّى ظَننَّا أنَّهُ سَيُسَمِّيهِ بِغَيْرِ اسْمِهِ، قَالَ: ((ألَيْسَ ذَا الحِجَّةِ؟)) قُلْنَا: بَلَى. قَالَ: ((فَأيُّ بَلَد هَذَا؟)) قُلْنَا: اللهُ ورَسُولُهُ أعْلَمُ، فَسَكَتَ حَتَّى ظَنَنَّا أنَّهُ سَيُسَمِّيهِ بِغَيرِ اسْمِهِ. قَالَ: ((ألَيْسَ البَلْدَةَ؟)) قُلْنَا: بَلَى. قَالَ: ((فَأيُّ يَوْم هَذَا؟)) قُلْنَا: اللهُ ورَسُولُهُ أعْلَمُ، فَسَكَتَ حَتَّى ظَنَنَّا أنَّهُ سَيُسَمِّيهِ بغَيرِ اسْمِهِ. قَالَ: ((ألَيسَ يَوْمَ النَّحْرِ؟)) قُلْنَا: بَلَى. قَالَ: ((فَإنَّ دِمَاءكُمْ وَأمْوَالَكُمْ وَأَعْرَاضَكُمْ عليكم حَرَامٌ، كَحُرْمَةِ يَوْمِكُمْ هَذَا في بَلَدِكُمْ هَذَا في شَهْرِكُمْ هَذَا، وَسَتَلْقُونَ رَبَّكُمْ فَيَسْألُكُمْ عَنْ أعْمَالِكُمْ، ألا فَلا تَرْجعوا بعدي كُفّارًا يَضْرِبُ بَعْضُكُمْ رِقَابَ بَعْض، ألا لَيُبَلِّغ الشَّاهِدُ الغَائِبَ، فَلَعَلَّ بَعْضَ مَنْ يَبْلُغُهُ أنْ يَكُونَ أوْعَى لَهُ مِنْ بَعْض مَنْ سَمِعَهُ))، ثُمَّ قَالَ: ((ألا هَلْ بَلَّغْتُ، ألا هَلْ بَلَّغْتُ؟)) قُلْنَا: نَعَمْ. قَالَ: ((اللَّهُمَّ اشْهَدْ)). مُتَّفَقٌ عَلَيهِ

Imepokelewa kutoka kwa Abu Bakr Nufay’ kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa saalam) amesema: “Hakika zama (mwaka) unapita kama ilivyo siku ya Allaah Alivyoumba mbingu na ardhi: Mwaka una miezi kumi na mbili, miongoni mwayo ni miezi minne iliyo hurum (miezi ambayo vita ni haram hata wakati wa ujahiliyyah). Miezi mitatu ni ya kufuatana: Dhul Qa’dah, Dhul Hijjah na Muharram na Rajab Mundhwar, mwezi ambao upo baina ya Jumaadah na Sha’baan. Kisha akauliza: “Je, huu ni mwezi gani?” Wakasema (Maswahaba): Allaah na Rasuli Wake wanajua zaidi. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akanyamaza mpaka tukadhania atauita kwa jina lingine. Akasema: “Je, huu si mwezi wa Dhul Hijjah?” Tukasema: Ndio. Akauliza: “Je, huu ni mji gani?” Tukasema: Allaah na Rasuli Wake wanajua zaidi. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akanyamaza mpaka tukadhania atauita kwa jina lingine lisilikuwa jina lake. Akasema: “Je, huu si mji wa (Makkah)?” Tukasema: Ndio. Akasema: “Je, hii ni siku gani?” Tukasema: Allaah na Rasuli Wake wanajua zaidi. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akanyamaza mpaka tukadhania kuwa ataiita kwa jina lingine. Akasema: “Je, hii si ni siku ya kuchinja?” Tukasema: Ndio. Akasema: “Hakika damu zenu, mali zenu, na heshima zenu ni haramu kwenu kama uharamu (wa kufanya dhambi) siku yenu hii, katika mji wenu huu, katika mwezi wenu huu. Na bila shaka mtakutana na Mola wenu na kuwauliza juu ya ‘amali zenu. Fahamuni! Msirudi baada yangu katika ukafiri mkiuana ninyi kwa ninyi. Jueni! Aliyehudhuria amfikishie asiyekuwepo, huenda baadhi ya watakao fikishiwa wakawa wanafahamu nzuri zaidi kuliko waliosikia.” Kisha akauliza: “Je, nimefikisha?” Tukasema: Ndio. Akasema: “Ee Allaah shuhudia (hilo).” [Al-Bukhaariy na Muslim]







Hadiyth – 11

وعن أَبي أمامة إياس بن ثعلبة الحارثي رضي الله عنه: أنَّ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((مَن اقْتَطَعَ حَقَّ امْرئ مُسْلِم بيَمينه، فَقدْ أوْجَبَ اللهُ لَهُ النَّارَ، وَحَرَّمَ عَلَيهِ الجَنَّةَ)) فَقَالَ رَجُلٌ: وإنْ كَانَ شَيْئًا يَسيرًا يَا رَسُول الله؟ فَقَالَ: ((وإنْ كَانَ قَضيبًا مِنْ أرَاك)). رواه مسلم

Imepokewa kutoka kwa Abuu Umaamah Iyaas bin Tha’labah Al-Haarithiy (Radhiya Allaah ‘anhhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Mwenye kuchukua haki ya mtu Muislamu kwa kuapa yamini (ya uongo) imewajibika kwa Allaah kumuingiza motoni na kumharamishia Jannah.” Mtu mmoja akasema: “Hata kikiwa kitu kidogo ee Rasuli wa Allaah? Akasema: “Hata kikiwa ni kigaa cha mti Arak.” [Muslim]







Hadiyth – 12

وعن عَدِيّ بن عَميْرَةَ رضي الله عنه قَالَ: سمعت رَسُول الله صلى الله عليه وسلم يقول: ((مَنِ اسْتَعْمَلْنَاهُ مِنْكُمْ عَلَى عَمَل، فَكَتَمَنَا مِخْيَطًا فَمَا فَوْقَهُ، كَانَ غُلُولًا يَأتِي به يَومَ القِيَامَةِ)) فَقَامَ إليه رَجُلٌ أسْوَدُ مِنَ الأنْصَارِ، كَأنِّي أنْظُرُ إِلَيْهِ، فَقَالَ: يَا رَسُول الله، اقْبَلْ عَنِّي عَمَلَكَ، قَالَ: ((وَمَا لَكَ؟)) قَالَ: سَمِعْتكَ تَقُولُ كَذَا وكَذَا، قَالَ: ((وَأَنَا أقُولُه الآنَ: مَنِ اسْتَعْمَلْنَاهُ عَلَى عَمَلٍ فَلْيَجِئْ بقَليله وَكَثيره، فَمَا أُوتِيَ مِنْهُ أخَذَ، وَمَا نُهِيَ عَنْهُ انْتَهَى)). رواه مسلم

Imepokewa na ‘Adiy bin ‘Umayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba nimemsikia Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: “Yoyote tutakaye muajiri miongoni mwenu kwa kazi yoyote ile akawa ni mwenye kuficha sindano na zaidi yake, huo utakuwa ni wizi atakao kuja nao Siku ya Qiyaamah.” Akasema mtu mweusi mingoni mwa Answaar kana kwamba ninamtazama. Akasema: Ee Rasuli wa Allaah! Niruhusu nijiuzulu kazi yako (uliyonipa). Akamuuliza: “Kwanini?” Akajibu: Nimekusikia ukisema kadhaa na kadhaa. Akasema: “Yoyote atakayempa jukumu la kazi fulani basi alete kichache na kingi (alete chochote atakachopata). Atakachopewa atachukua, na atakachozuiliwa akiache.” [Muslim]







Hadiyth – 13

وعن عمر بن الخطاب رضي الله عنه قَالَ: لَمَّا كَانَ يَوْمُ خَيبَر أقْبَلَ نَفَرٌ مِنْ أصْحَابِ النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم، فقَالُوا: فُلاَنٌ شَهِيدٌ، وفُلانٌ شَهِيدٌ، حَتَّى مَرُّوا عَلَى رَجُلٍ، فقالوا: فُلانٌ شَهِيدٌ. فَقَالَ النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم: ((كَلا، إنِّي رَأيْتُهُ في النَّار في بُرْدَةٍ غَلَّهَا- أَوْ عَبَاءة-)). رواه مسلم

Imepokewa na ‘Umar bin Al-Khatwaab (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: Siku ya Vita vya Khaybar walikaribia kikundi cha Maswahaba wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuja kutazama waliokufa mashahidi. Wakasema: Fulani ni shahidi na fulani pia ni shahidi.” Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa salaam) akasema: “Sivyo hivyo. Hakika mimi nimemuona motoni kwa juba au gauni aliloliiba.” [Muslim]







Hadiyth – 14

وعن أَبي قتادة الحارث بن ربعي رضي الله عنه عن رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: أَنَّهُ قَامَ فيهم، فَذَكَرَ لَهُمْ أنَّ الجِهَادَ في سبيلِ الله، وَالإِيمَانَ بالله أَفْضَلُ الأعْمَالِ، فَقَامَ رَجُلٌ، فَقَالَ: يَا رَسُولَ الله، أرَأيْتَ إنْ قُتِلْتُ في سبيلِ الله، تُكَفَّرُ عَنّي خَطَايَايَ؟ فَقَالَ لَهُ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: ((نَعَمْ، إنْ قُتِلْتَ في سبيلِ اللهِ، وَأنْتَ صَابرٌ مُحْتَسِبٌ، مُقْبِلٌ غَيرُ مُدْبر)) ثُمَّ قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: ((كَيْفَ قُلْتَ؟)) قَالَ: أرَأيْتَ إنْ قُتِلْتُ في سبيلِ الله، أتُكَفَّرُ عَنّي خَطَايَايَ؟ فَقَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: ((نَعمْ، وَأنْتَ صَابرٌ مُحْتَسِبٌ، مُقْبِلٌ غَيرُ مُدْبِرٍ، إلا الدَّيْنَ؛ فإنَّ جِبريلَ قَالَ لي ذلِكَ)). رواه مسلم

Imepokewa na Abuu Qataadah bin Al-Haarith bin Rab’iyy (Radhwiya Allaahu ‘anahu) kwamba Rasuli wa Allaahu (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) alisimama mbele yao, akawatajia kuwa jihaad katika njia ya Allaah na kumuamini Allaah ndio ‘amali bora. Hapo alisimama mtu akasema: Ee Rasuli wa Allaah! Waonaje nikiuliwa katika njia ya Allaah nitasamehewa madhambi yangu? Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia: “Ndio, ukiuliwa katika njia ya Allaah nawe ukawa katika hali ya kusubiri na huku unatarajia malipo (kutoka kwa Allaah), ukiwa unasonga mbele katika vita wala sio kurudi nyuma (na kukimbia).” Kisha akasema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): “Umesema nini?” Akasema: Ee Rasuli wa Allaah! Waonaje nikiuliwa katika njia ya Allaah nitasamehewa makossa yangu? Akasema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): “Ndio, ukiuliwa katika njia ya Allaah nawe ukawa katika hali ya kusubiri na huku watarajia malipo (kutoka kwa Allaah), ukiwa unasonga mbele katika vita wala sio kurudi nyuma (na kukimbia) ila deni kwani Jibriyl ameniambia hilo.” [Muslim]







Hadiyth – 15

وعن أبي هُريرةَ رضي الله عنه: أنَّ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((أتدرونَ مَنِ المُفْلِسُ؟)) قالوا: المفْلسُ فِينَا مَنْ لا دِرهَمَ لَهُ ولا مَتَاع، فَقَالَ: ((إنَّ المُفْلسَ مِنْ أُمَّتي مَنْ يأتي يَومَ القيامَةِ بصلاةٍ وصيامٍ وزَكاةٍ، ويأتي قَدْ شَتَمَ هَذَا، وقَذَفَ هَذَا، وَأَكَلَ مالَ هَذَا، وسَفَكَ دَمَ هَذَا، وَضَرَبَ هَذَا، فيُعْطَى هَذَا مِنْ حَسَنَاتِهِ، وهَذَا مِنْ حَسناتهِ، فإنْ فَنِيَتْ حَسَناتُه قَبْل أنْ يُقضى مَا عَلَيهِ، أُخِذَ منْ خَطَاياهُم فَطُرِحَتْ عَلَيهِ، ثُمَّ طُرِحَ في النَّارِ)). رواه مسلم

Imepokewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu Alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Je, mnamjua Muflis?” Wakasema: Muflis kwetu sisi ni yule asiyekuwa na dirham wala mali. Akasema: “Hakika Muflis katika Ummah wangu ni yule atakayekuja Siku ya Qiyaamah akiwa ana Swalaah, Swawm na Zakaah. Na anakuja amemtusi huyu, amemsingizia huyu uzinifu, amekula mali ya huyu, amemwaga damu ya huyu na kumpiga huyu. Kila aliyedhulumiwa atapewa sehemu ya mema yake, na yule atapewa sehemu ya mema yake. Pindi mema yake yatakapomalizika kabla ya hukmu kuisha, zitachukuliwa sehemu ya dhambi zao (kulingana na alivyo dhulumu) na apewe yeye, kisha atupwe motoni.” [Muslim]







Hadiyth – 16

وعن أم سلمة رضي الله عنها: أنَّ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((إنَّمَا أنَا بَشَرٌ، وَإنَّكُمْ تَخْتَصِمُونَ إلَيَّ، وَلَعَلَّ بَعْضَكُمْ أنْ يَكُونَ أَلْحَنَ بِحُجّتِهِ مِنْ بَعْضٍ، فأَقْضِيَ لَهُ بِنَحْوِ مَا أسْمعُ، فَمَنْ قَضَيتُ لَهُ بِحَقِّ أخِيهِ فَإِنَّما أقطَعُ لَهُ قِطعةً مِنَ النَّارِ)). مُتَّفَقٌ عَلَيهِ

Imepokewa kutoka kwa ummu Salamah (Radhwiya Llaahu ‘anhaa) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Hakika mimi ni mwana Aadam, nanyi mnaniletea mashtaka yenu. Na huenda baadhi yenu mkawa mahodari kutoa hoja kuliko baadhi ya wengine wenu. Nami nikampatia haki (isiyokuwa yake) kwa niliyoyasikia. Yoyote atakaye mpatia haki ya nduguye, hakika nitakuwa nimemkatia kipande cha moto. [Al-Bukhaariy na Muslim]







Hadiyth – 17

وعن ابن عمر رضي الله عنهما قَالَ: قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: ((لَنْ يَزَالَ المُؤْمِنُ في فُسْحَةٍ مِنْ دِينهِ مَا لَمْ يُصِبْ دَمًا حَرَامًا)). رواه البخاري

Imepokewa na ibn ‘Umar (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Muumin atabakia katika duara la matumaini na Iymaan madamu hatamwaga damu iliyoharamishwa.” [Al-Bukhaariy]







Hadiyth – 18

وعن خولة بنتِ عامر الأنصارية وهي امرأة حمزة رضي الله عنه وعنها، قَالَتْ: سمعت رَسُول الله صلى الله عليه وسلم يقول: ((إنَّ رِجَالًا يَتَخَوَّضُونَ في مَالِ الله بغَيرِ حَقٍّ، فَلَهُمُ النَّارُ يَومَ القِيَامَةِ)). رواه البخاري

Imepokewa kutoka kwa Khawlah bint ‘Aamir Al-Answaariyyah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa), naye ni mke wa Hamzah bin ‘Abdul-Mutw-Twalib (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) kuwa amemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) Akisema: “Hakika watu wanaotumia mali ya Allaah (mali ya Ummah) pasi na haki, hao wana Moto Siku ya Qiyaamah.” [Al-Bukhaariy]
 
027-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Kuadhimisha Mambo Matukufu Ya Waislamu, Kubainisha Haki, Kuwasikitia Na Kuwahurumia


Riyaadhw Asw-Swaalihiyn



باب تعظيم حرمات المسلمين وبيان حقوقهم والشفقة عليهم ورحمتهم

27 – Mlango Kuadhimisha Mambo Matukufu Ya Waislamu, Kubainisha Haki, Kuwasikitia Na Kuwahurumia



Alhidaaya.com





قَالَ الله تَعَالَى:

وَمَن يُعَظِّمْ حُرُمَاتِ اللَّـهِ فَهُوَ خَيْرٌ لَّهُ عِندَ رَبِّهِ﴿٣٠﴾

Na yeyote anayeadhimisha vitukufu vya Allaah basi hivyo ni kheri kwake mbele ya Rabb wake. [Al-Hajj: 30]



وَمَن يُعَظِّمْ شَعَائِرَ اللَّـهِ فَإِنَّهَا مِن تَقْوَى الْقُلُوبِ ﴿٣٢﴾

Na yeyote anayeadhimisha Ishara za Allaah, basi hayo ni katika taqwa ya nyoyo. [Al-Hajj: 32]



وَاخْفِضْ جَنَاحَكَ لِلْمُؤْمِنِينَ﴿٨٨﴾

Na inamisha bawa lako kwa Waumini (kuwahurumia). [Al-Hijr: 88]



مَن قَتَلَ نَفْسًا بِغَيْرِ نَفْسٍ أَوْ فَسَادٍ فِي الْأَرْضِ فَكَأَنَّمَا قَتَلَ النَّاسَ جَمِيعًا وَمَنْ أَحْيَاهَا فَكَأَنَّمَا أَحْيَا النَّاسَ جَمِيعًا ﴿٣٢﴾

Atakayeiua nafsi bila ya nafsi (kuua), au kufanya ufisadi katika ardhi; basi ni kama ameua watu wote. [Al-Maaidah: 32]





Hadiyth – 1

وعن أَبي موسى رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: ((المُؤْمِنُ للْمُؤْمِنِ كَالبُنْيَانِ يَشُدُّ بَعْضُهُ بَعْضًا)) وشبَّكَ بَيْنَ أصَابِعِهِ. مُتَّفَقٌ عَلَيهِ.

Abuu Muwsaa (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) amesema: “Muumini kwa Muumini ni mfano wa jengo, sehemu moja inatilia nguvu sehemu nyingine.” Na akaviunganisha vidole vyake. [Al-Bukhaariy na Muslim]





Hadiyth – 2

وعنه قَالَ: قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: ((مَنْ مَرَّ في شَيْءٍ مِنْ مَسَاجِدِنا، أَوْ أَسْوَاقِنَا، وَمَعَهُ نَبْلٌ فَلْيُمْسِكْ، أَوْ لِيَقْبِضْ عَلَى نِصَالِهَا بكَفّه؛ أنْ يُصِيبَ أحَدًا مِنَ المُسْلِمِينَ مِنْهَا بِشَيْء)). مُتَّفَقٌ عَلَيهِ.

Kutoka kwake Abuu Muwsaa (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) amesema: “Anayepita Misikitini au masokoni mwetu na ilhali ana mshale, basi auzuwie au akishike chemba chake kwa mkono wake, asije akamdunga nao yeyote katika Waislamu.” [Al-Bukhaariy, Muslim na Ahmad]





Hadiyth – 3

وعن النعمان بن بشير رضي الله عنهما قَالَ: قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: ((مَثَلُ المُؤْمِنينَ في تَوَادِّهِمْ وتَرَاحُمهمْ وَتَعَاطُفِهمْ، مَثَلُ الجَسَدِ إِذَا اشْتَكَى مِنْهُ عُضْوٌ تَدَاعَى لَهُ سَائِرُ الجَسَدِ بِالسَّهَرِ والحُمَّى)). مُتَّفَقٌ عَلَيهِ.

Imepokewa na An-Nu’maan bin Bashiyr (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) amesema: “Mfano wa Waumini katika kupendana kwao, kuhurumiana kwao na kusaidiana kwao, ni mfano wa mwili, kiungo kimoja kikiumwa basi mwili mzima hukesha kwa homa.” [Al-Bukhaariy, Muslim na Ahmad]





Hadiyth – 4

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه قَالَ: قَبَّلَ النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم الحَسَنَ بْنَ عَليٍّ رضي الله عنهما، وَعِنْدَهُ الأَقْرَعُ بْنُ حَابِس، فَقَالَ الأقْرَعُ: إن لِي عَشرَةً مِنَ الوَلَدِ مَا قَبَّلْتُ مِنْهُمْ أحَدًا. فَنَظَرَ إِلَيْهِ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم فَقَالَ: ((مَنْ لا يَرْحَمْ لا يُرْحَمْ!)). مُتَّفَقٌ عَلَيهِ.

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuna wakati mmoja Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) alimbusu mjukuu wake Al-Hasan bin ‘Ally (Radhwiya Allaahu 'anhu) mbele ya Al-Aqra akasema: “Hakika mimi nina watoto kumi sijambusu yeyote miongoni mwao.” Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) alimtazama, akasema: “Yeyote asiye na huruma (kwa wenziwe) basi hahurumiwi.” [Al-Bukhaariy na Muslim]





Hadiyth – 5

وعن عائشة رضي الله عنها، قَالَتْ: قَدِمَ نَاسٌ مِنَ الأعْرَابِ عَلَى رسولِ الله صلى الله عليه وسلم، فقالوا: أتُقَبِّلُونَ صِبْيَانَكُمْ؟ فَقَالَ: ((نَعَمْ)) قالوا: لَكِنَّا والله مَا نُقَبِّلُ! فَقَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: ((أَوَ أَمْلِك إنْ كَانَ اللهُ نَزَعَ مِنْ قُلُوبِكُم الرَّحْمَةَ))!. مُتَّفَقٌ عَلَيهِ.

في هذا الحديث: الشفقة على الأولاد، وتقبيلهم ورحمتهم.

Imepokewa na ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) aliyesema: Mabedui walikuja kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam), wakasema: “Je, mnawabusu watoto wenu?” Akasema: “Ndio.” Wakasema: “Lakini sisi Wa-Allaahi hatuwabusu.” Hapo Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) akasema: “Je, naweza kuwamiliki ikiwa Allaah Ameondosha nyoyoni mwenu rehma (huruma).” [Al-Bukhaariy, Muslim na Ahmad]





Hadiyth – 6

وعن جرير بن عبد الله رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: ((مَنْ لا يَرْحَم النَّاسَ لا يَرْحَمْهُ الله)). مُتَّفَقٌ عَلَيهِ.

Imepokewa na Jariyr bin ‘Abdillaahi (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) amesema: “Asiye wahurumia watu, Allaah Hamrehemu.” [Al-Bukhaariy, Muslim na Ahmad]





Hadiyth – 7

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه: أنّ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((إِذَا صَلَّى أحَدُكُمْ للنَّاسِ فَلْيُخَفِّفْ، فَإن فيهِم الضَّعِيفَ وَالسَّقِيمَ وَالكَبيرَ، وَإِذَا صَلَّى أحَدُكُمْ لِنَفْسِهِ فَلْيُطَوِّل مَا شَاءَ)). مُتَّفَقٌ عَلَيهِ.

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) amesema: “Anaposwalisha watu mmoja wenu basi akhafifishe, kwani wapo miongoni mwao wanyonge, wagonjwa na wazee. Na anaposwali mmoja wenu peke yake, arefushe anavyotaka.” Na katika riwayah yengine: “Wenye haja.” [Al-Bukhaariy na Muslim]





Hadiyth – 8

وعن عائشة رضي الله عنها، قَالَتْ: إنْ كَانَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم لَيَدَعُ العَمَلَ، وَهُوَ يُحبُّ أنْ يَعْمَلَ بِهِ؛ خَشْيَةَ أنْ يَعمَلَ بِهِ النَّاسُ فَيُفْرَضَ علَيْهِمْ. مُتَّفَقٌ عَلَيهِ.

Kutoka kwake ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kuwa amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) mara nyengine alikuwa akiacha 'amali naye anapenda kuitekeleza kwa kuogopea wasije wakaifanya hivyo kufaradhishwa kwao. [Al-Bukhaariy, Muslim na Ahmad]





Hadiyth – 9

وَعَنْهَا رضي الله عنها قَالَتْ: نَهَاهُمُ النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم عنِ الوِصَال رَحمَةً لَهُمْ، فَقَالُوا: إنَّكَ تُوَاصِلُ؟ قَالَ: ((إنّي لَسْتُ كَهَيْئَتِكُمْ، إنِّي أبيتُ يُطْعمُني رَبِّي وَيَسقِيني)). مُتَّفَقٌ عَلَيهِ.

Amesema ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa): Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) aliwakataza Wiswaal kwa kuwahurumia wao. Wakasema: “Hakika wewe unaunganisha?” Akasema: “Hakika mimi si kama mmoja wenu. Hakika mimi ninalishwa na kunyweshwa na Mola wangu usiku.” [Al-Bukhaariy, Muslim na Ahmad]





Hadiyth – 10

وعن أَبي قَتادةَ الحارثِ بن رِبعِي رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: ((إنِّي لأَقُومُ إِلَى الصَّلاة، وَأُرِيدُ أنْ أُطَوِّلَ فِيهَا، فَأسْمَع بُكَاءَ الصَّبيِّ فَأَتَجَوَّزَ في صَلاتي كَرَاهية أنْ أشُقَّ عَلَى أُمِّهِ)). رواه البخاري.

Kutoka kwa Abuu Qataadah Al-Haarith Ar-Ri’biy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) amesema: “Kwa hakika mimi husimama katika Swalah na nikataka kuirefusha, basi huwa nikisikia kilio cha mtoto, hapo naifupisha Swalah yangu kwa kuchelea nisije nikampa uzito mama yake.” [Al-Bukhaariy]





Hadiyth – 11

وعن جندب بن عبد الله رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: ((مَنْ صَلَّى صَلاةَ الصُّبْحِ فَهُوَ في ذِمَّةِ الله فَلا يَطْلُبَنَّكُمُ الله مِنْ ذِمَّته بشَيءٍ، فَإنَّهُ مَنْ يَطْلُبْهُ منْ ذمَّته بشَيءٍ يُدْركْهُ، ثُمَّ يَكُبُّهُ عَلَى وَجْهِهِ في نَارِ جَهَنَّمَ)). رواه مسلم.

Kutoka kwa Jundub bin ‘Abdillaah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) amesema: “Mwenye kuswali Swalaah ya Al-Fajr yuko katika dhima ya Allaah (amani na ahadi Yake). Hivyo, usijiweke katika hali ambayo utakuja laumiwa na Allaah kwa kuvunja ahadi Yake. Hakika mwenye kufanyiwa hesabu kwa kufanya khiyana ulinzi wa Allaah, Allaah Atampatiliza, na kisha kumuingiza kwa uso wake moto wa Jahannam.” [Muslim]





Hadiyth – 12

وعن ابن عمر رضي الله عنهما أنَّ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((المُسْلِمُ أَخُو المُسْلِم، لا يَظْلِمهُ، وَلا يُسْلمُهُ. مَنْ كَانَ في حَاجَة أخيه، كَانَ اللهُ في حَاجَته، وَمَنْ فَرَّجَ عَنْ مُسْلِم كُرْبَةً، فَرَّجَ اللهُ عَنْهُ بها كُرْبَةً مِنْ كُرَبِ يَومِ القِيَامَةِ، وَمَنْ سَتَرَ مُسْلِمًا سَتَرَهُ اللهُ يَومَ القِيامَةِ)). مُتَّفَقٌ عَلَيهِ.

Kutoka kwa Ibn ‘Umar (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) amesema: “Muislamu ni ndugu yake Muislamu, hamdhulumu wala hamsalimishi (kwa adui). Mwenye kumtekelezea haja nduguye, Allaah Atamtekelezea haja yake. Mwenye kumondolea Muislamu dhiki, Allaah humondolea dhiki miongoni mwa dhiki Siku ya Qiyaamah. Na mwenye kumsitiri Muislamu, Allaah Atamsitiri Siku ya Qiyaamah.” [Al-Bukhaariy na Muslim]





Hadiyth – 13

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: ((المُسْلِمُ أخُو المُسْلِمُ، لا يَخُونُهُ، وَلا يَكْذِبُهُ، وَلا يَخْذُلُهُ، كُلُّ المُسْلِمِ عَلَى المُسْلِم حَرَامٌ عِرْضُهُ وَمَالهُ وَدَمُهُ، التَّقْوى هاهُنَا، بحَسْب امْرئٍ مِنَ الشَّرِّ أنْ يَحْقِرَ أخَاهُ المُسْلِم)). رواه الترمذي، وَقالَ: ((حديث حسن)).

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) amesema: “Muislamu mwengine, hamfanyii khiyana wala hamdanganyi wala haachi kumnusuru. Kila Muislamu mwenziwe ni haramu cheo (heshima) chake, mali yake na damu yake. Taqwah ipo hapa, inatosha kwa mtu kuwa katika shari kumchukia nduguye Muislamu.” [At-Tirmidhiy]





Hadiyth – 14

وعنه قَالَ: قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: ((لا تَحَاسَدُوا، وَلا تَنَاجَشُوا، وَلا تَبَاغَضُوا، وَلا تَدَابَرُوا، وَلا يَبعْ بَعْضُكُمْ عَلَى بَيْع بَعْض، وَكُونُوا عِبَادَ الله إخْوَانًا، المُسْلِمُ أخُو المُسْلم: لا يَظْلِمُهُ، وَلا يَحْقِرُهُ، وَلا يَخْذُلُهُ، التَّقْوَى هاهُنَا- ويشير إِلَى صدره ثلاث مرات-- بحَسْب امْرئٍ مِنَ الشَّرِّ أنْ يَحقِرَ أخَاهُ المُسْلِمَ، كُلُّ المُسْلم عَلَى المُسْلم حَرَامٌ، دَمُهُ ومَالُهُ وعرْضُهُ)). رواه مسلم.

Kutoka kwake Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) amesema: “Msihusudiane, wala msiongezeane bei (katika biashara), wala msitukanane, wala msipeane nyongo (msikatane), wala baadhi yenu wasiuze juu ya wageni; na kuweni nyote ni waja wa Allaah (Subhaanahu Wa Ta'aalaa), ndugu moja. Muislamu ni ndugu ya Muislamu; hamdhulumu wala hamdharau, wala haachi kumnusuru. Uchaji Allaah uko hapa – akaashiria mara tatu kifuani mwake – yatosha mtu kutenda sharia atakapomdharau nduguye Muislamu. Kila Muislamu juu ya Muislamu mwenziwe ni haramu: damu yake, mali yake na heshima yake.” [Muslim]





Hadiyth – 15

وعن أنس رضي الله عنه عن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((لا يُؤمِنُ أحَدُكُمْ حَتَّى يُحِبَّ لأخِيهِ مَا يُحِبُّ لنَفْسِهِ)). مُتَّفَقٌ عَلَيهِ.

Kutoka kwa Anas bin Maalik (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) amesema: “Haamini mmoja wenu mpaka ampende nduguye kwa analolipendelea nafsi yake.” [Al-Bukhaariy na Muslim]





Hadiyth – 16

وعنه قَالَ: قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: ((انْصُرْ أخَاكَ ظَالمًا أَوْ مَظْلُومًا)) فَقَالَ رجل: يَا رَسُول اللهِ، أنْصُرُهُ إِذَا كَانَ مَظْلُومًا، أرَأيْتَ إنْ كَانَ ظَالِمًا كَيْفَ أنْصُرُهُ؟ قَالَ: ((تحْجُزُهُ- أَوْ تمْنَعُهُ- مِنَ الظُلْمِ فَإِنَّ ذلِكَ نَصرُهُ)). رواه البخاري.

Kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) amesema: “Mnusuru nduguyo akiwa amedhulumu au amedhulumia.” Mtu mmoja akauliza: “Ee Rasuli wa Allaah! Nitamnusuru akiwa amedhulumiwa, nieleze nitamnusuru vipi akiwa amedhulumu?” Akasema: “Mzuilie asidhulumu, kufanya hivyo ndiko kumnusuru.” [Al-Bukhaariy]





Hadiyth – 17

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه: أنَّ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((حَقُّ المُسْلِم عَلَى المُسْلِم خَمْسٌ: رَدُّ السَّلامِ، وَعِيَادَةُ المَريض، وَاتِّبَاعُ الجَنَائِزِ، وَإجَابَةُ الدَّعْوَة، وتَشْميتُ العَاطِسِ)). مُتَّفَقٌ عَلَيهِ.

Imepokewa na Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) amesema: “Haki ya Muislamu kwa Muislamu mwenziwe ni tano: Kurudisha salamu, kumzuru mgonjwa, kumfuata jeneza, kuitikia mwaliko na kumwombea du’aa aliyepiga chafya (aliyechumua).” [Al-Bukhaariy na Muslim]

Riwaayah ya Muslim: “Haki za Muislamu ni sita: Unapokutana naye umsalimie, anapokualika umwitikie, akitaka nasaha mnasihi, anapochemua na akamuhimidi Allaah muombee du’aa, akiwa mgonjwa mzuru na anapokufa fuata (jeneza lake).”





Hadiyth – 18

وعن أَبي عُمَارة البراءِ بن عازب رضي الله عنهما، قَالَ: أمرنا رَسُول الله صلى الله عليه وسلم بسبع، ونهانا عن سبع: أمَرَنَا بعيَادَة المَرِيض، وَاتِّبَاعِ الجَنَازَةِ، وتَشْمِيتِ العَاطسِ، وَإبْرار المُقْسِم، ونَصْرِ المَظْلُوم، وَإجَابَةِ الدَّاعِي، وَإِفْشَاءِ السَّلامِ، ونَهَانَا عَنْ خَواتِيمٍ أَوْ تَخَتُّمٍ بالذَّهَبِ، وَعَنْ شُرْبٍ بالفِضَّةِ، وَعَن الميَاثِرِ الحُمْرِ، وَعَن القَسِّيِّ، وَعَنْ لُبْسِ الحَريرِ والإسْتبْرَقِ وَالدِّيبَاجِ. مُتَّفَقٌ عَلَيهِ.

وفي رواية: وَإنْشَادِ الضَّالَّةِ في السَّبْعِ الأُوَل.

Kutoka kwa Abuu ‘Umaarah Al-Baraa’ bin ’Aazib (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) ametuamuru kutekeleza mambo saba: Ametuamuru kuwazuru wagonjwa, kufuata jeneza, kumuombea aliyepiga chafya, kuamini kiapo, kumnusuru aliyedhulumiwa, kuitikia mwaliko na kutoa na kueneza salamu. Na ametukataza kuvaa pete ya dhahabu, kunywa kwenye chombo cha fedha, kupanda shogi la hariri nyekundu, Al-Qasiyy, kuvaa hariri, Istabraq na dibaji.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

Riwaayah nyingine: “Na kusaidia kupata kilichopotea mambo saba yaliyotajwa mwanzo.”
 
028-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kusitiri Aibu Za Waislamu Na Katazo La Kuzieneza Pasi Na Dharura


Riyaadhw Asw-Swaalihiyn



باب ستر عورات المسلمين والنهي عن إشاعتها لغير ضرورة

028-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kusitiri Aibu Za Waislamu Na Katazo La Kuzieneza Pasi Na Dharura



Alhidaaya.com





قَالَ الله تَعَالَى :

إِنَّ الَّذِينَ يُحِبُّونَ أَن تَشِيعَ الْفَاحِشَةُ فِي الَّذِينَ آمَنُوا لَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ ۚ وَاللَّـهُ يَعْلَمُ وَأَنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ ﴿١٩﴾

Hakika wale wanaopenda uenee uchafu wa kashfa kwa wale walioamini; watapata adhabu iumizayo duniani na Aakhirah. Na Allaah Anajua nanyi hamjui. [An-Nuur: 19]





Hadiyth – 1

وعن أبي هريرة رضي الله عنه عن النبي صلى الله عليه وسلم قال‏: ((لاَ يَسْتُرُ عَبْدٌ عَبْداً في الدُّنْيَا إلاَّ سَتَرَهُ اللهُ يَوْمَ القِيَامَةِ)) ‏‏ ‏رواه مسلم‏.‏‏

Na imepokewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Mja hatamstiri mja mwenziwe duniani ila Allaah Atamstiri yeye Siku ya Qiyaamah." [Muslim]





Hadiyth – 2

وعن أبي هريرة رضي الله عنه قال‏:‏ سمعت رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول‏:‏ ‏ ((‏كُلُّ أُمَّتِي مُعَافى :إلاَّ المُجَاهِرِينَ ، وَإنّ مِنَ المُجَاهَرَةِ أنْ يَعْمَلَ الرَّجُلُ باللَّيلِ عَمَلاً ، ثُمَّ يُصْبحُ وَقَدْ سَتَرَهُ اللهُ عَلَيهِ ، فَيقُولُ يَا فُلانُ ، عَمِلت البَارِحَةَ كَذَا وَكَذَا ، وَقَدْ بَاتَ يَسْتُرُهُ رَبُّهُ ، وَيُصبحُ يَكْشِفُ ستْرَ اللهِ عَنْه‏)).‏ ‏متفق عليه‏ ‏.‏

Na kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) alisema: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: “Ummah wangu wote umesalimika ila wanaodhihirisha (maovu) ni mtu kutenda amali (ya maasiya) usiku kisha apambazukiwa ilhali amesitiriwa na Allaah, asema: 'Ee fulani, usiku wa jana nilifanya kadha na kadha.' Na hakika alikuwa amepitiwa na usiku mzima akiwa amesitiriwa na Rabb wake, na anapambazukiwa akiifunua sitara aliyositiriwa na Allaah." [Al-Bukhaariy na Muslim]





Hadiyth – 3

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه، عن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: ‏((إِذَا زَنَتِ الأَمَةُ فَتَبيَّنَ زِنَاهَا فَلْيَجْلِدْهَا الحَدَّ ، وَلا يُثَرِّبْ عَلَيْهَا ، ثُمَّ إنْ زَنَتِ الثَّانِيَةَ فَلْيَجْلِدْهَا الحَدَّ ، وَلا يُثَرِّبْ عَلَيْهَا ، ثُمَّ إنْ زَنَتِ الثَّالِثَةَ فَلْيَبِعْهَا وَلَوْ بِحَبْل مِنْ شَعَر‏)).‏ ‏‏متفق عليه‏ ‏.‏

Na kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Pindi atakapozini kijakazi na ikabainika zinaa yake, basi apigwe mijeledi ya adhabu (iliyowekwa na Shariy’ah) wala asikaripiwe. Kisha akizini mara ya pili apigwe tena mijeledi ya adhabu wala asikaripiwe. Kisha akizini tena mara ya tatu, amuuze kwa japokuwa kwa kamba iliyotengenezwa kwa nywele." [Al Bukhaariy na Muslim]





Hadiyth – 4

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه قَالَ: أُتِيَ النَّبيّ صلى الله عليه وسلم برجل قَدْ شَرِبَ خَمْراً ، قَالَ ‏:‏‏((اضْربُوهُ)) قَالَ أَبُو هريرة : فَمِنَّا الضَّارِبُ بِيَدِهِ ، والضَّارِبُ بِنَعْلِهِ ، وَالضَّارِبُ بِثَوبِهِ . فَلَمَّا انْصَرَفَ ، قَالَ بَعضُ القَومِ : أخْزَاكَ الله ، قَالَ (( لا تَقُولُوا هكَذا ، لاَ تُعِينُوا عَلَيهِ الشَّيْطَانَ‏)).‏ ‏‏رواه البخاري‏‏‏.‏

Na kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiyah Allaah 'anhu) amesema: Aliletwa mtu mlevi kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), akasema: "Mpigeni." Akasema Abuu Hurayrah: Wapo miongoni mwetu waliompiga kwa mkono wake, wengine kwa viatu vyao na wengine kwa nguo zao. Alipoondoka (huyu mtu) walisema baadhi ya watu: "Allaah akupe hizaya (akudhililishe). "Akasema "Msiseme hivyo, msimsaidie shetani dhidi yake." [Al Bukhaariy]
 
029-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kuwakidhia Waislamu Haja Zao


Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

باب قضاء حوائج المسلمين

029-Mlango Wa Kuwakidhia Waislamu Haja Zao



Alhidaaya.com



قَالَ الله تَعَالَى



يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا ارْكَعُوا وَاسْجُدُوا وَاعْبُدُوا رَبَّكُمْ وَافْعَلُوا الْخَيْرَ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ ۩﴿٧٧﴾

Enyi walioamini! Rukuuni, na sujuduni na mwabuduni Rabb wenu, na fanyeni ya khayr ili mpata kufaulu. [Al-Hajj: 77]





Hadiyth – 1

وعن ابن عمر رضي الله عنهما أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال‏:‏ ‏ ((‏المُسْلِمُ أخُو المُسْلِمِ ، لاَ يَظْلِمُهُ وَلاَ يُسْلِمُهُ . مَنْ كَانَ في حَاجَة أخِيه ، كَانَ اللهُ في حَاجَتِهِ، وَمَنْ فَرَّجَ عَنْ مُسْلِمٍ كُرْبَةً، فَرَّجَ اللهُ عَنْهُ بِهَا كُرْبَةً مِنْ كرَبِ يَومِ القِيَامَةِ ، وَمَنْ سَتَرَ مُسْلِماً سَتَرَهُ اللهُ يَومَ القِيَامَةِ )).‏ ‏متفق عليه‏ ‏.‏

Na imepokewa kutoka kwa Ibn ‘Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Muislamu ni ndugu yake Muislamu, hamdhulumu wala hamsalimishi (kwa adui). Mwenye kumtekelezea haja nduguye Allaah Atamtekelezea haja yake. Na mwenye kumwondolea Muislamu dhiki, Allaah Atamwondolea dhiki miongoni mwa dhiki za Siku ya Qiyaamah. Na mwenye kumsitiri Muislamu, Allaah Atamsitiri Siku ya Qiyaamah." [Al-Bukhaariy na Muslim]





Hadiyth – 2



وعن أبي هريرة رضي الله عنه عن النبي صلى الله عليه وسلم قال‏:‏ (( مَنْ نَفَّسَ عَنْ مُؤْمِنٍ كُرْبَةً مِنْ كُرَبِ الدُّنيَا ، نَفَّسَ الله عَنْهُ كُربَةً مِنْ كُرَبِ يَوْمِ القِيَامَةِ ، وَمَنْ يَسَّر عَلَى مُعْسِرٍ يَسَّرَ الله عَلَيهِ في الدُّنْيَا وَالآخِرَةِ ، وَمَنْ سَتَرَ مُسْلِماً سَتَرَهُ الله في الدُّنْيَا وَالآخِرَةِ ، والله في عَونِ العَبْدِ مَا كَانَ العَبْدُ في عَونِ أخِيهِ ، وَمَنْ سَلَكَ طَريقاً يَلْتَمِسُ فِيهِ عِلْماً سَهَّلَ اللهُ لَهُ طَريقاً إِلَى الجَنَّةِ . وَمَا اجْتَمَعَ قَوْمٌ في بَيت مِنْ بُيُوتِ اللهِ تَعَالَى ، يَتْلُونَ كِتَابَ اللهِ ، وَيَتَدَارَسُونَهُ بَيْنَهُمْ إلاَّ نَزَلَتْ عَلَيْهِمُ السَّكِينَةُ ، وَغَشِيتْهُمُ الرَّحْمَةُ ، وَحَفَّتْهُمُ المَلاَئِكَةُ ، وَذَكَرَهُمُ الله فِيمَنْ عِندَهُ . وَمَنْ بَطَّأ بِهِ عَمَلُهُ لَمْ يُسْرِع بِهِ نَسَبُهُ)) رواه مسلم



Imepokewa na Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Mwenye kumfariji Muumini dhiki miongoni mwa dhiki za duniani, Allaah Atamfariji (na kumuondolea) dhiki miongoni mwa dhiki za Siku ya Qiyaamah. Na mwenye kumsahilishia mwenye uzito, Allaah Atamsahilishia duniani na Aakhirah. Na mwenye kumsitiri Muislamu, Allaah Atamsitiri duniani na Aakhirah. Na Allaah Anamsaidia mja huyu yu katika kumsaidia nduguye. Na mwenye kufuata njia akitafuta elimu katika njia hiyo, Allaah Atamsahilishia njia ya kwenda Jannah. Na watu hawatakusanyika katika nyumba miongoni mwa nyumba za Allaah (Ta’aalaa) wakisoma kitabu cha Allaah na wakifundishana isipokuwa huteremka utulivu, wakafunikwa na Malaika na Allaah Akawataja kwa walio Kwake. Na anayechelewesha na amali yake hatopelekwa mbele kwa nasaba yake.” [Muslim na
 
030-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Uombezi (shifaa)


Riyaadhw Asw-Swaalihiyn



باب الشفاعة

030-Mlango Wa Uombezi (shifaa)



Alhidaaya.com



:قَالَ الله تَعَالَى



مَّن يَشْفَعْ شَفَاعَةً حَسَنَةً يَكُن لَّهُ نَصِيبٌ مِّنْهَا ۖ وَمَن يَشْفَعْ شَفَاعَةً سَيِّئَةً يَكُن لَّهُ كِفْلٌ مِّنْهَا ۗ وَكَانَ اللَّـهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ مُّقِيتًا ﴿٨٥﴾

Atakayeombea uombezi mzuri atapata fungu lake katika hayo. Na atakayeombea uombezi mbaya atapata sehemu yake katika hayo. Na Allaah daima ni Mwenye kudhibiti na Mwangalizi wa kila kitu. [An-Nisaa: 85]





Hadiyth – 1

وعن أَبي موسى الأشعري رضي الله عنه، قَالَ: كَانَ النَّبيّ صلى الله عليه وسلم إِذَا أتاهُ طَالِبُ حَاجَةٍ أقبَلَ عَلَى جُلَسَائِهِ ، فَقَالَ : (( اشْفَعُوا تُؤْجَرُوا ، وَيَقْضِي الله عَلَى لِسَانِ نَبِيِّهِ مَاأحبَّ)) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

وفي رواية : (( مَا شَاءَ )) .



Na imepokewa kutoka kwake Abuu Muwsaa Al Ash'aariy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipokuwa anajiliwa na mwenye haja, huwaelekea walioketi naye akiwaambia: " Ombeni mtalipwa, na Allaah Hukidhi (haja) kwa ulimi wa Rasuli Wake Anavyopenda." [Al-Bukhaariy na Muslim]

Na katika riwaayah nyingine: " Anavyotaka".





Hadiyth – 2



وعن ابن عباس رضي الله عنهما في قِصَّةِ برِيرَةَ وَزَوْجِهَا ، قَالَ : قَالَ لَهَا النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم : (( لَوْ رَاجَعْتِهِ ؟ )) قَالَتْ : يَا رَسُولَ اللهِ تَأمُرُنِي ؟ قَالَ : (( إنَّمَا أَشْفَع )) قَالَتْ : لاَ حَاجَةَ لِي فِيهِ . رواه البخاري .

Na imepokewa kutoka kwa Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhummaa) Kuhusianana kisa cha Bariyrah na mumewe, Akasema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimwambia: "Waonaje lau ungerudi kwake?" Akasema (Bariyrah): " Ee Rasuli wa Allaah! Unaniamuru?" Akamjibu: "Hakika mimi naombea." Akasema (Bariyrah): "Sina haja naye." [Al-Bukhaariy]
 
UJUMBE WA SIKU:

Imepokewa na ‘Adiy bin ‘Umayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba nimemsikia Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: “Yoyote tutakaye muajiri miongoni mwenu kwa kazi yoyote ile akawa ni mwenye kuficha sindano na zaidi yake, huo utakuwa ni wizi atakao kuja nao Siku ya Qiyaamah.” Akasema mtu mweusi mingoni mwa Answaar kana kwamba ninamtazama. Akasema: Ee Rasuli wa Allaah! Niruhusu nijiuzulu kazi yako (uliyonipa). Akamuuliza: “Kwanini?” Akajibu: Nimekusikia ukisema kadhaa na kadhaa. Akasema: “Yoyote atakayempa jukumu la kazi fulani basi alete kichache na kingi (alete chochote atakachopata). Atakachopewa atachukua, na atakachozuiliwa akiache.” [Muslim]

Naam tumeona hapo hadith ya Nabii Swallallahu alaih wasallam kwamba yule atakaye ajiriwa kisha akaiba japokuwa sindano tu, hakika huyo atafufuliwa nayo siku ya kiama

Ebu tafakari sindano tu,je huwa tunawaaibia waajiri vitu vingapi?

Huwa tunawadhulumu mali zao mara ngapi?

Wengine huko serikalini ndio mna ufisadi wa kutisha,je hiyo siku ya kiama mtakuwa katika hali gani?

Ndugu zangu Allah subhaanahu wa Taala,anapokea toba kabla roho ya mmoja wetu haijafika shingoni mwake na kuanza kukoroma kuelekea katika umauti wake

Allah anapokea toba kabla jua halijaanza kupambuzuka likichomozea upande wa magharibi

Tutubu ndugu zangu,hakika mauti yanakuja kwa ghafla mno,tutubu sasa na kujutia wizi wetu pamoja na kuadhimia kwamba hatutakuja kufanya dhuluma hiyo tena

Tumche Allah
 
Baadhi ya post zangu za zamani....

BINADAMU TUNA MIPANGO MINGI SANA LAKINI HATUJUI KESHO YETU

Ilisikika sauti toka ndani ya kaburi " Lete dongo, Lete reli, Lete ubao, lete majani". Nilikuwa miongoni mwa watu watano ambao wali bahatika kuchaguliwa kuingia ndani ya kaburi kumzika huyu shangazi yangu,na ndiyo ilikuwa mara ya Kwanza kufanya hivyo

Amekufa akiwa na Miaka 96 yaani bado minne Tu afikishe miaka 100. Shangazi huyu kama wiki mbili zilizo pita tulienda kumsalimia nikiwa na ndugu zangu,na kuna mdogo wangu anatarajia kuolewa October 2022, sasa Shangazi alisisitiza Sana kuwa lazima ndoa hii ya mdogo wangu ikafungwe kwake,alisisitiza kiasi ambacho akatuacha njia panda, je ndoa itaendaje kufungwa kwake wakati ilishapangwa kufungwa nyumbani Kwa Mzee,kutokana na utu uzima wake ikabidi Mimi niitikie Sawa ili siku ipite huku nikiwa najiuliza itakuwaje.

Kumbe alichokuwa hajui kuwa tayari visa yake ya kuishi hapa duniani ilikuwa imebakisha siku chache na hivyo kutakiwa kurudi Kwa Mola wake, September 20 ndiyo tuliyo mzika,nikiwa ndani ya kaburi naupokea mwili wake na kuuweka ndani ya mwanandani, nikawa najiuliza, Shangazi iko wapi ahadi yako ya kutaka ndoa ifungwe nyumbani kwako? Mbona umeondoka kabla ndoa haijafungwa?

Moral of the story:

Kwanza
, kama binadamu huwa tuna mipango mingi Sana lkn huwa hatujui kesho yetu ikoje? Kikubwa ni kumcha Mwenyezi Mungu, mda wowote tupo safarini.

Pili, kwa Jambo lolote lile usipende kusema nitalifanya kesho, au nitajenga mwakani au nitaoa mwishoni mwa mwaka huu,Ila useme Mungu akipenda nitafanya kadhaa wa kadhaa, ndio maana Tunatakiwa na Mwenyezi Mungu tuseme insha'Allah Kwa maana "Mungu akipenda" kwasababu hatuna tunachokimiliki au kukiweza isipokuwa akipenda yeye.
 
Aina Za Laana Na Wepi Waliolaaniwa na Allaah?
Maswali: Qur-aan


Aina Za Laana Na Wepi Waliolaaniwa na Allaah?



Alhidaaya.com







SWALI:



Kwanza kabisa namshukuru Allaah Subhaanahu wa Ta'aalaa. na kumtakia rehma Nabiy Muhammad kiongoza wa Umma (S.A.W) na Masheikh wote ambao usiku na mchana wako macho kujibu maswali yetu/ya waislaam.

Baada ya hapo ningependa kuuliza maswali yafuatayo. Ni Nani Haswa Anastahiki Kuambiwa Laana Za Allaah Ziwe Juu Yako. Je Ni Makafir Au Murtadina Au Wanaafiq? Je Kuna Laana Ya Mtu Mmoja Mmoja Ua Wengi Wengi?





JIBU:



AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho



Kwanza kabla hatujajibu swali lako, tunakukumbusha kuwa unapoandika jina la Allaah au Nabiy, usifupishe mbele yake kwa kuweka (S.W.) au (S.A.W.) kama ilivyozoelekea na wengi, bali andika kwa kirefu maneno hayo bila ya kuyafupisha. Andika (Subhaanahu wa Ta’aalaa) baada ya kumtaja Allaah, na andika Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) au (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) baada ya kumtaja Mtume. Hivyo ndivyo inavyopaswa, na ndio heshima zaidi na utukufu na ndivyo inavyotamkwa na si kama inavyofupishwa na wengi kimazoea na kivivu

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu mas-ala ya laana. Laana si kitu kumpata mtu yeyote yule na hasa akiwa ni Muislamu. Laana kutoka kwa Allaah au Nabiy Wake inampata mwenye kuacha amri na yule aliyekengeuka na maagizo yao. Allaah Aliyetukuka na Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'Alayhi wa aalihi wa sallam) wametutajia watu waliteremshiwa laana hizo.



Hebu tutazame baadhi ya mifano:



a) Allaah Aliyetukuka Anasema:

إِنَّ اللَّـهَ لَعَنَ الْكَافِرِينَ وَأَعَدَّ لَهُمْ سَعِيرًا ﴿٦٤﴾

Hakika Allaah Amewalaani makafiri, na Amewaandalia moto uliowashwa vikali mno. [Al-Ahzaab: 64].



b) Allaah Aliyetukuka Anasema:

لَّئِن لَّمْ يَنتَهِ الْمُنَافِقُونَ وَالَّذِينَ فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٌ وَالْمُرْجِفُونَ فِي الْمَدِينَةِ لَنُغْرِيَنَّكَ بِهِمْ ثُمَّ لَا يُجَاوِرُونَكَ فِيهَا إِلَّا قَلِيلًا ﴿٦٠﴾مَّلْعُونِينَ ۖ أَيْنَمَا ثُقِفُوا أُخِذُوا وَقُتِّلُوا تَقْتِيلًا ﴿٦١﴾

Ikiwa wanafiki, na wale ambao katika nyoyo zao mna maradhi, na waenezao fitnah katika Al-Madiynah hawatokoma, bila shaka Tutakusalitisha juu yao, kisha hawatokaa humo kuwa jirani zako isipokuwa kidogo tu. Maluuni hao! Popote wanapopatikana, wachukuliwe, na wauliwe mbali mauaji kamilifu. [Al-Ahzaab: 60 – 61].



c) Allaah Aliyetukuka Anasema:

إِنَّ الَّذِينَ يُؤْذُونَ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ لَعَنَهُمُ اللَّـهُ فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ وَأَعَدَّ لَهُمْ عَذَابًا مُّهِينًا ﴿٥٧﴾

Hakika wale wanaomuudhi Allaah na Rasuli Wake, Allaah Amewalaani duniani na Aakhirah, na Amewaandalia adhabu ya kudhalilisha. [Al-Ahzaab: 57].



d) Anasema tena Aliyetukuka:

فَبِمَا نَقْضِهِم مِّيثَاقَهُمْ لَعَنَّاهُمْ وَجَعَلْنَا قُلُوبَهُمْ قَاسِيَةً ۖ

Kwa sababu ya kuvunja kwao fungamano lao, Tuliwalaani na Tukazifanya nyoyo zao kuwa ngumu... [Al-Maaidah: 13].



e) Anasema tena:

..أَلَا لَعْنَةُ اللَّـهِ عَلَى الظَّالِمِينَ﴿١٨﴾

Tanabahi! Laana ya Allaah iko juu ya waliodhulumu. [Huwd: 18].



f) Anasema tena:

ثُمَّ نَبْتَهِلْ فَنَجْعَل لَّعْنَتَ اللَّـهِ عَلَى الْكَاذِبِينَ ﴿٦١﴾

Kisha tuombe mubaahalah, tuifanye laana ya Allaah iwe juu ya waongo. [Aal-'Imraan: 61].



g) Anasema tena Aliyetukuka:



لُعِنَ الَّذِينَ كَفَرُوا مِن بَنِي إِسْرَائِيلَ عَلَىٰ لِسَانِ دَاوُودَ وَعِيسَى ابْنِ مَرْيَمَ ۚ ذَٰلِكَ بِمَا عَصَوا وَّكَانُوا يَعْتَدُونَ ﴿٧٨﴾

Wamelaaniwa wale waliokufuru miongoni mwa wana wa Israaiyl kwa lisani ya Daawuwd na ‘Iysaa mwana wa Maryam. Hivyo ni kwa sababu ya kuasi kwao na walikuwa wakitaadi [Al-Maaidah: 78].



Tukizitazama Aayah hizi utapata ya kwamba waliolaaniwa na Allaah Aliyetukuka ni wengi miongoni mwao ni makafiri, madhalimu, walioasi, waliotupa mipaka, wanaomuudhi Allaah na Nabiy Wake, wanafiki, waongo, watangazao uovu, wenye kuficha Aliyoteremsha Allaah, na kadhalika.



Ama hawa watakaopata laana ya Allaah, basi Aliyetukuka Anatueleza:

أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ لَعَنَهُمُ اللَّـهُ ۖ وَمَن يَلْعَنِ اللَّـهُ فَلَن تَجِدَ لَهُ نَصِيرًا ﴿٥٢﴾

Hao ndio wale Allaah Aliowalaani. Na ambaye Allaah Amemlaani basi hatopata wa kumnusuru. [An-Nisaa: 52].





Na Allaah Anajua zaidi
 
Fisadi Gani Mbili Za Mayahudi Zilizotajwa Katika Suwrah Bani Israaiyl?
Maswali: Qur-aan



Fisadi Gani Mbili Za Mayahudi Zilizotajwa Katika Suwrat Bani Israaiyl?



Alhidaaya.com





SWALI:



Assalam alaykum
Natumai mnaendelea vizuri na afya njema na shughuli zenu za Dawa. Ningependa kuuliza: Katika kitabu kitukufu Qur'an, Allaah ameelezea katika Suwrah Al-Israa au Bani Israel katika aayah ya 4 - 5.
Napenda kujua hizo fisadi mbili zilizoandikwa kuwa Wana wa Israel watazifanya, haswa hiyo ya kwanza ilitokea wakati gani na wakati wa Nabiy gani. Na ni watu gani katika waja wake Allaah ambao aliwapeleka kuwatia adabu. Kisha napenda kujua hiyo fisadi ya pili ni ipi au lini itatokea. Na kama kuna mengine ya ziada tuchambulini kwa hawa watu ambao Allaah amewalaani kwa jeuri yao.
Shukran





JIBU:



AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.





Hakika hili ni swali nyeti ambalo inatakiwa kila Muislamu awe na ufahamu nalo. Swala la Mayahudi ambao Qur-aan, Hadiyth za Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na hata historia imetubainishia uovu wao usio kifani. Lakini hapa si mahali pake kuelezea hayo kwani swali mbele yetu ni jengine japokuwa linahusiana.



Hakika ufisadi wa Bani Israaiyl umetokea mara nyingi katika historia yao, idadi zake haziwezi kuhesabika. Na makusudio ya Aayah ni kuwa mara mbili hizi ufisadi ni dhahiri kabisa. Na kuwa Aayah inayofuata ni dalili kuwa kusalitishwa juu yao waja wa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kutaendelea mpaka Siku ya Qiyaamah kwa sababu ya ukafiri na uasi wao. Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema:



..وَإِنْ عُدتُّمْ عُدْنَا ۘ

Na mkirudia (ufisadi na dhulma), Nasi Tutarudia (kukuadhibuni).” [Al-Israa: 8]



Kabla hatujazifafanua Aayah hizo ni vyema tuandike tafsiri zake ili tuwe katika ufahamu kwa tunayoyaeleza. Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema:



وَقَضَيْنَا إِلَىٰ بَنِي إِسْرَائِيلَ فِي الْكِتَابِ لَتُفْسِدُنَّ فِي الْأَرْضِ مَرَّتَيْنِ وَلَتَعْلُنَّ عُلُوًّا كَبِيرًا ﴿٤﴾فَإِذَا جَاءَ وَعْدُ أُولَاهُمَا بَعَثْنَا عَلَيْكُمْ عِبَادًا لَّنَا أُولِي بَأْسٍ شَدِيدٍ فَجَاسُوا خِلَالَ الدِّيَارِ ۚ وَكَانَ وَعْدًا مَّفْعُولًا ﴿٥﴾

Na Tukawahukumia wana wa Israaiyl katika Kitabu kwamba: Bila shaka mtafanya ufisadi katika ardhi mara mbili, na bila shaka mtapanda kiburi kuasi kwa dhulma na kutakabari kukubwa. Basi ilipokuja ahadi ya kwanza kati ya fisadi mbili; Tulikutumieni waja Wetu wenye nguvu kali za kupigana vita, wakaingia kusaka (na kuwaua) ndani ya majumba na ikawa ahadi ni ya kutekelezwa. [Al-Israa: 4-5]



Wametofautiana Mufassiriyna kuhusu maana ya kufanya ufisadi mara mbili katika ardhi. Nasi tutaangalia baadhi ya tafsiri na kutaja mwishowe rai ambayo ina nguvu zaidi.



Ash-Shawkaaniy katika Fat-hul-Qadiyr amesema:

"Mara mbili inasemwa kuwa, mara ya kwanza ni baada ya kuuliwa Ash‘iyaa’ au kufungwa kwa Nehemia au kukhalifu amri za Tawraat. Na mara ya pili ni kuuliwa kwa Yahyaa bin Zakariyyaa (‘Alayhimas-Salaam) na azma ya kumuua ‘Iysaa ('Alayhis-Salaam). Na panasemwa kuwa ufisadi wa kwanza umetokea lakini wa pili bado. Nao walitumilizwa watu wetu wenye mapigano makali yaani wenye nguvu katika vita na ukali wanapopambana na adui. Panasemwa kuwa huyu alikuwa ni Nebukadneza na jeshi lake kutoka Babeli".



Hapa upo mgongano wa maelezo kwani mfalme Nebukadneza alikuja takriban miaka 580 kabla ya kuja kwa Yahyaa na ‘Iysaa (‘Alayhimas Salaam).



Na amesema Abul Fidaa’ Ismaa‘iyl bin Kathiyr katika tafsiri yake Tafsiyrul Qur-aanil ‘Adhwiym, mjalada wa 3, uk. 28 – 29:



"Hakika Mufassiriyna wa zamani na sasa wametofautiana ni kina nani hawa waliosalitishwa juu yao? Ibn ‘Abbaas na Qataadah wanasema kuwa ni Jaaluwt na jeshi lake ambao waliwasumbua lakini baadae wakawa ni wenye kupata nguvu na Daawuwd (‘Alayhis-Salaam) kumuua Jaaluwt". Na kwa hiyo Akasema (Ta’aalaa):



ثُمَّ رَدَدْنَا لَكُمُ الْكَرَّةَ عَلَيْهِمْ

Kisha Tukakurudishieni nguvu zenu dhidi yao... [Al-Israa: 6]



"Amesema Sa‘iyd bin Jubayr kuwa huyo alikuwa na mfalme wa Muswul, Senharib na jeshi lake. Na kutoka kwake na wengineo kuwa huyo alikuwa ni mfalme wa Babeli, Nebukadneza".



Wamesema baadhi ya Mufassiriyna kuwa maadui waliowatoa katika majumba yao walikuwa ni qaumu ya Jaaluwt ambao walikuwa wamewashinda Bani Israaiyl na kuwaua idadi kubwa. Hii ilikuwa ni kabla ya kurudishiwa nguvu zao chini ya uongozi wa Twaaluwt.



Na kauli ya Allaah Aliyetukuka:



ثُمَّ رَدَدْنَا لَكُمُ الْكَرَّةَ عَلَيْهِمْ

Kisha Tukakurudishieni nguvu zenu dhidi yao...[Al-Israa: 6]



Hii ni wazi kuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Aliwanusuru baada ya kujuta na kutubia, nao wakawa ni wenye kulishinda jeshi la Jaaluwt na Nabiy Daawuwd (‘Alayhis-Salaam) akamuua Jaaluwt.



Na kauli Yake:



وَأَمْدَدْنَاكُم بِأَمْوَالٍ وَبَنِينَ وَجَعَلْنَاكُمْ أَكْثَرَ نَفِيرًا ﴿٦﴾

...na Tukakuongezeeni mali na wana, na Tukakufanyeni wengi zaidi kwa idadi na nguvu. [Al-Israa: 6]



Hii ilipatikana katika kipindi cha dhahabu chini ya utawala wa Manabii Daawuwd na Sulaymaan (‘Alayhimas-Salaam) cha miaka 80. Ama baada ya kipindi hiki cha dhahabu dola hiyo iligawanywa sehemu mbili: Dola ya Yahudha na Dola ya Israaiyl. Ufisadi uliingia kati yao, mzozano na mapambano mpaka Dola ya Israaiyl ilipopigwa na kutawaliwa na Assyria mwaka wa 721 (kabla ya kuzaliwa kwa ‘Iysaa) na ufalme wa Yahudha kusambaratishwa katika mwaka 588 (kabla ya kuzaliwa 'Iysaa) na mfalme wa Babeli, Nebukadneza. Historia ya bani Israaiyl baada ya hapo haikuwa ila ni silsila ya maasi, adhabu, balaa na maafa ambayo yaliwapitia wakiwa na watu tofauti” [Banu Israaiyl Fiyl Qur-aan was Sunnah, Mj. 2, uk. 366].



Na wengine wamesema: "Ufisadi wao wa mara ya pili ulikuwa wakati wa utawala wa Warumi ambapo jemedari jeshi wake, Titus aliwaua wengi na wengine kushikwa mateka na wengine kukimbia. Tukio hili lilitokea baada ya kuuliwa Nabiy Yahyaa (‘Alayhis Salaam) kwa miaka kadhaa" [Al-Khatwarul Yahuwd, uk. 23-25].



Kwa ufupi tunaweza kusema kuwa ufisadi wa Wana wa Israaiyl ulikuwa mwingi kuanzia wakati wa Muwsaa (‘Alayhis-Salaam) na kila mara walisalitishwa watu wengine. Kwa mfano Fir-awn, Jaaluwt, Waasuri, Wababeli, Wayunani, Wamakdoni, Warumi, na mwisho kabisa watakuwa ni Waislamu. Waislamu ambao watasimama imara kwa kufuata maagizo ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na Rasuli Wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Wakati huo mpaka mawe na miti itazungumza kumuashiria Muislamu pale alipojificha Myahudi. Hapo watauliwa na kushindwa na ardhi tukufu hiyo kurudi mikononi mwa Waislamu.



Na Allaah Anajua zaidi
 
Hikmah Ya Kuteremshwa Qur-aan Kidogo Kidogo Na Kutokana Na Matukio
Maswali: Qur-aan





HikmahYa Kuteremshwa Qur-aan Kidogo Kidogo Na Kutokana Na Matukio



Alhidaaya.com







SWALI:



Kuna mantiki gani kwa Quran kushushwa kidogo kidogo, na tena mpaka kitokezee kisa ndio aya za Quraan zinashuka?





JIBU:





AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.





Hakika kuna hikma nyingi za kuteremshwa Qur-aan kidogo kidogo na pole pole tena kwa wakati mbali mbali, ima kwa tukio fulani au bila ya kutokea tukio lolote. Na mfano wa Aayaat au Suwrah ambao zimeteremshwa bila ya matukio ni khabari za kale kama visa vya Manabii, na pia mfano khabari na hali zitakavyokuwa za Aakhirah kama Siku ya Qiyaamah, hali za wakaazi wa Jannah na watakaotumbukizwa Motoni na kadhalika.



Maelezo na faida zaidi zinapatikana katika kiungo kifuatacho:



Hikmah Ya Kuteremshwa Qur-aan Kidogo Kidogo Wakati Mbali Mbali





Na Allaah Anajua zaidi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…