Anaweza Kuchelewa Kujitaharisha Janaba?
Maswali: Twahara Najsi
SWALI:

Je, nikikutana na mume wangu kimwili na mara nyingi usiku sana. Je, nitalazimika kukoga usiku huo huo, au hakuna ubaya wowote hata nikilala mpaka nitakapotaka kusali alfajiri ndio nikoge?









JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allahu 'anhum jamiy'an) na watangu wema mpaka Siku ya Qiyaamah.

Hakuna ubaya wowote kisheria kuchelewesha kukoga janaba: na hali kadhalika hakuna lazima ya kisheria kuharakisha kukoga janaba, japo ni bora kiunadhifu kufanya hivyo.



Imepokewa riwaya kutoka kwa Abu Hurayrah (radhiya Allahu 'anhu) (Ya kwamba Abu Hurayrah (radhiya Allahu 'anhu) alikutana na Mtume (Swalla Allahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwenye mitaa ya Madiynah, huku akiwa na janaba, akarudi kinyumenyume (kwa kumkimbia Mtume (Swalla Allahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akaenda kukoga, na kuja tena mbele ya Mtume (Swalla Allahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) Mtume akamuuliza, "Ulikuwa wapi ewe Aba Hurayrah?) akasema nilikuwa na janaba, nikahisi kero kuketi nawe nikiwa si nadhifu, Mtume (Swalla Allahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema SubhaanaAllah, hakika Muislam hanajisiki"

(Al-Bukhaariy Hadiyth Namba 283 na Muslim Hadiyth Namba 309).

Ila ni bora zaidi kufanya wudhuu ikiwa Muislamu anataka kuchelewesha janaba kama ilivyokuja dalili katika Hadiyth zifuatazo:



YA KWANZA:

عن عائشةَ قالت: كان النبيُّ صلى الله عليه وسلم إِذا أرادَ أن [يأكل أو] يَنامَ وهوَ جُنُبٌ غَسلَ فَرجَهُ وتَوضَّأَ وضوءه للصلاة

Imetoka kwa ‘Aaishah (Radhiya Allaahu ‘anha) ambaye amesema: "Kila alipotaka (kula) au kulala akiwa katika hali ya janaba, (yaani baada ya kujimai na kabla ya kukoga) Mtume (Swalla Allahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiosha sehemu zake za siri na kufanya wudhuu kama wa Swalah “[Al-Bukhaariy na Muslim]

YA PILI:

عن أبن عمر رضي الله عنهما أن عُمرُ قال: يا رسول الله : أَيَنامُ أحدُنا وهوَ جُنبٌ؟ قال: ((نَعمْ، إِذا تَوضَّأَ)) وفي رواية ((توَضَّأْ واغْسِلْ ذَكَرَكَ ثمَّ نَمْ)) وفي رواية ((نَعَمْ. لِيَتَوَضَّأْ ثُمَّ لْيَنَمْ، حَتَّى يَغْتَسِلَ إِذَا شَاءَ)) وفي أخرى: ((نَعَمْ، وَيَتَوَضَّأُ إِنْ شاءَ))

Imetoka kwa Ibn 'Umar (Radhiya Allahu ‘anhuma) kwamba 'Umar alisema: "Ewe Mjumbe wa Allaah, je, tulale tukiwa katika hali ya janaba?" Mtume (Swalla Allahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akajibu: ((Ndio baada ya kuchukua wudhuu)) [Al-Bukhaariy Na Muslim]

Katika riwaya nyingine ((Fanya wudhuu na osha sehemu zako za siri kisha ndio ulale)) [Al-Bukhaariy Na Muslim]

Na katika riwaya nyingine ((Ndio, unaweza kufanya wudhuu, kulala na kuoga unapopenda)) [Al-Bukhaariy Na Muslim]

Na katika riwaya nyingine pia: ((Ndio na fanya wudhuu ukipenda)) [Ibn Khuzaymah na Ibn Hibbaan ni Swahiyh]

Riwaaya ya mwisho inaonyesha kuwa wudhuu huu sio fardh.

YA TATU:

عنْ عَمَّارِ بنِ يَاسِرٍ ، أنَّ رَسُولَ الله صلى الله عليه وسلم قالَ: ((ثَلاَثَةٌ لاَ تَقْرَبُهُمْ المَلاَئِكَةٌ: جِيْفَةُ الْكَافِرِ، وَالمُتَضَمِّخُ بِالخُلُوقِ، وَالْجُنُبُ إلاَّ أنْ يَتَوَضَّأَ))

Imetoka kwa 'Ammaar ibn Yaasir kwamba "Mtume Swalla Allahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Watu watatu Malaika hawawakaribii; maiti ya Kafiri, mwanamume anayejitia manukato ya kike, na mwenye janaba (aliyefanya jimai) hadi afanye wudhuu)) [Abu Daawuud, Ahmad na wengine ni Swahiyh]

Na Allah Anajua zaidi
 
Anaweza Kuswali Ikiwa Atatokwa Na Manii Bila Ya Kitendo Cha Ndoa?
Maswali: Twahara Najsi

Anaweza Kuswali Ikiwa Atatokwa Na Manii Bila Ya Kitendo Cha Ndoa?



Alhidaaya.com





SWALI



Je, mtu akishikana na mkewe mpaka akatoka manii bila ya kufanya tendo la ndoa anaweza kusali bila ya kuoga janaba?





JIBU:



AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.



Janaba inapatikana kwa hali ya kutokwa na manii sawa ikiwa manii yamekutoka kwa kuingiliana (yaani kwa kuzama kichwa cha dhakari ndani ya utupu wa mwanamke) au kuota, au kujichua n.k., na kwa hali hiyo huwezi ukaswali mpaka ujitwaharishe.



Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)



يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَقْرَبُوا الصَّلَاةَ وَأَنتُمْ سُكَارَىٰ حَتَّىٰ تَعْلَمُوا مَا تَقُولُونَ وَلَا جُنُبًا إِلَّا عَابِرِي سَبِيلٍ حَتَّىٰ تَغْتَسِلُوا ۚ

Enyi walioamini! Msikaribie Swalaah na hali mmelewa mpaka mjue mnayoyasema, na wala mkiwa mna janaba isipokuwa mmo safarini mpaka muoge josho. [An-Nisaa: 43]



Na katika Sunnah anasema Ummul-Muuminiyna ‘Aaishah (Radhwiya Allahu 'anhaa) kuna Mtu mmoja alimuuliza Nabiy (Swalla Allahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusu mtu anayemjamii mke wake kisha akakatisha ile jimai (katikati bila ya kushusha manii): Je, analazimika kuoga (janaba)? Na Bi ‘Aaishah wakati huo akiwa ameketi – Nabiy (Swalla Allahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: "Kwa hakika mimi na huyu bibie hufanya hivyo kisha tunakoga" [Muslim]



Bonyeza kiungo kifuatacho upate maelezo zaidi ya maudhui hiyo:



Ikiwa Mtachezeana Tu Na Kutokwa Manii Inapasa Kukoga Josho?







Na Allaah Anajua zaidi
 
Ikiwa Mtachezeana Tu Na Kutokwa Manii Inapasa Kukoga Josho?
Maswali: Twahara Wudhuu

Ikiwa Mtachezeana Tu Na Kutokwa Manii Inapasa Kukoga Josho?



Alhidaaya.com







SWALI



Assalamu aleikum,

Ninaelewa unaweza au mnaweza kugusana tupu baina ya mke na mume na ikawa hamtokuwa wenye kuhitajika kukoga Janaba.I sipokuwa kama ntatokwa na shahawa.

Swala langu lipo hapo najua vigumu kwa mwanamke kukumbana na umbile lauume au akawa mwenye kucheza nacho kiungo hicho bila kumtoka chochote. Kwa sisi inawezekana (wanaume) sasa tulijaalie suala hili kwa mwanamke ambae anajaribu kumridhisha mumewe, namzungumzia mwanamke hapa kwa sababu ana njia nyingi za kumridhisha mumewe kwa mfano: mkono, mguu kiuno au hata mdomo. Hivo wanaweza kuvitumia na khafla mume akajikuta tiari amekusha.Na mke akawa bado hajatokwa na chochote, Vipi hapa atahitajika kukonga na yeye. In Shaa Allaah liwe lenye kufahamika suala hili.





JIBU:



AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.





Tunavyoliona na kulisoma swali lako ni kwamba halipo wazi na kufuma pale panapotaka kuulizwa. Ni nasaha zetu kwa waulizaji wapendwa wawe ni wenye kuuliza swali moja kwa moja badala ya kuzunguka sana na hivyo hata kueleweka vibaya na wenye kujibu au kutoeleweka kabisa.



Ni muhimu ieleweke kuwa Wanazuoni wote wa Salaf (waliopita) na khalaf (wa sasa) wameafikiana kuwa ni wajibu kujitwaharisha kwa kuoga kwa yeyote yule (mwanamme na mwanamke) anayetokwa na manii akiwa usingizini au akiwa macho au kwa kujamiiana na pia pale mwanamke anapopata ada yake au damu anayotokwa baada ya uzazi. Hii ni kwa mujibu wa Hadiyth ya Umm Salamah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) kwamba Ummu Sulaym (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) aliuliza: “Ee Rasuli wa Allah! Allaah Haoni haya juu ya ukweli. Mwanamke anaona katika usingizi kama anavyoona mwanamme, je ni juu yake kuoga?” Akasema: “Ndio, anapoona maji” [Al-Bukhaariy na Muslim]



Wametofautiana Swahaba (Radhwiya Allaahu ‘anuhum) kuhusu kuwajibika kuoga kwa kujimai. Miongoni mwao ni wale wenye rai kuwa zinapokutana ngozi mbili zilizotahiriwa basi inakuwa wajibu kwa wote wawili kukoga ikiwa wametokwa na manii au la. Hii ni rai ya Faqihi wakubwa na hii ndiyo kauli ya Jamhuwr (‘Ulamaa wengi).





Rai ya pili ni ile inayosema si wajibu kukoga ikiwa hawakushusha, na hii ni kauli ya baadhi ya watu wa Dhwaahiriy.



Dalili zilizotolewa kwa wenye kuunga kauli ya kwanza ni kama zifuatazo:





1. Amepokea Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kutoka kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa amesema: “Anapokaa mmoja wenu baina ya viungo vinne vya mwili wake (yaani mkewe) na akafanya juhudi (jimai), basi inakuwa wajibu kuoga” [Ahmad na Muslim]





2. Amesema Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Anapokaa baina ya sehemu zake nne na zikakutana ngozi mbili zilizotahiriwa imekuwa wajibu kwao kuoga”.





3. Anahadithia Abu Muwsaa Al-Ash‘ariy (Radhwiya Allaahu ‘anhu): Kulizuka tofauti baina ya kikundi cha Muhajirina na kipote cha Answaariy, na tofauti yao ilikuwa Answaariy wakisema: “Josho la janaba linakuwa wajibu tu pale wanapotokwa na manii”. Lakini Muhajirina wakasema: “Pindi mtu anapostarehe na mwanamke kuoga inakuwa wajibu (ikiwa atashusha au la)”. Abu Muwsaa (Radhwiya Allaahu ‘anhu) akasema: “Sawa, mimi nitawatosheleza kwa hilo”. Abu Muwsaa (Radhwiya Allaahu ‘anhu) “Nilisimama na nikaelekea kwa ‘Aishah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) na kutaka ruhusa ambayo alinipatia”. Nikamwambia: “Ee Mama wa Waumini! Nataka kukuuliza kuhusu jambo fulani lakini naona haya kukuuliza”. Akasema: “Usione haya kuniuliza kuhusu jambo ambalo unaweza kumuuliza mamako aliyekuzaa, kwani mimi pia ni mama yako”. Kwa hili nikasema: “Ni kitu gani kinachofanya kuoga kunakuwa wajibu kwa mtu?” Akanijibu: “Umekuja kwa mtu mwenye ujuzi wa hilo. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ‘Yeyote mwenye kukaa kwenye sehemu nne (za mwanamke) na sehemu za siri zikagusana baina yao, josho la janaba itakuwa ni wajibu’” [Muslim, Ahmad na Maalik kwa maneno tofauti kidogo]





4. Dalili ya kauli ya pili ni Hadiyth hii: Aliulizwa ‘Uthmaan (Radhwiya Allaahu ‘anhu) akaambiwa: “Waonaje mtu anapostarehe na mkewe lakini hakushusha (hakutokwa na manii)?” Akajibu: “Atatawadha kama anavyotawadha mmoja wenu kwa ajili ya Swalaah, nimemsikia hayo Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) [Imenukuliwa na Muhammad bin Ahmad al-Qurtwubiy katika kitabu chake Bidaayatul Mujtahid, Mjalada wa kwanza]





Wenye kauli ya kwanza wanafuata Hadiyth ya kwanza na nyenginezo ambao tumezitaja na kusema kuwa hukumu ya Hadiyth inayotumiwa na wenye kauli ya pili imefutwa. Na kutilia mkazo Hadiyth hiyo ya kwanza ni ile Hadiyth aliyopokea Ubayy bin Ka‘ab (Radhwiya Allaahu ‘anhu) aliyesema: “Hakika Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alitoa ruhusa hiyo mwanzo wa Uislamu kisha akaamrisha kuoga (kwa wenye kujamiiana)” [Abu Dawuud].





Na pia maelezo ya ‘Aishah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) alipomjibu Abu Muwsaa (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kuhusu hilo.





Katika Hadiyth tulizozitaja hapo juu sehemu zilizotahiriwa ni utupu wa mwanamme na sehemu za siri za mwanamke. Hivyo, pindi utupu wa mwanaume unapoingia katika sehemu ya siri ya mwanamke, josho la janaba linakuwa wajibu kwa wote wawili. Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Anasema:



وَإِن كُنتُمْ جُنُبًا فَاطَّهَّرُوا ۚ

Na mkiwa na janaba basi jitwaharisheni. [Al-Maaidah: 6]





Kusherehesha kuhusu mas-ala haya, Ash-Shaafi‘iy amesema: “Katika lugha ya Kiarabu, janaba inamaanisha tendo aina yoyote ya kukutana kimwili baina ya mume na mke, bila kujali kama manii yametoka au la. Ikiwa mtu atasema: “fulani na fulani” wana janaba kwa sababu ya kadhaa na kadhaa’, hii inamaanisha janaba kwa njia yoyote ya kujamiiana baina yao (mume na mke) hata ikiwa hakutakuwa na kushusha. Hakuna anaye kataa kuwa zinaa ambayo ina adhabu maalumu ni kukutana kimwili baina ya wawili hata ikiwa hakuna kutokwa kwa manii”.



Na hakika Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Anatueleza kinaganaga pale Aliposema:



وَلَا جُنُبًا إِلَّا عَابِرِي سَبِيلٍ حَتَّىٰ تَغْتَسِلُوا ۚ وَإِن كُنتُم مَّرْضَىٰ أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ أَوْ جَاءَ أَحَدٌ مِّنكُم مِّنَ الْغَائِطِ أَوْ لَامَسْتُمُ النِّسَاءَ فَلَمْ تَجِدُوا مَاءً فَتَيَمَّمُوا صَعِيدًا طَيِّبًا

na wala mkiwa mna janaba isipokuwa mmo safarini mpaka muoge josho. Na mkiwa wagonjwa au safarini au mmoja wenu ametoka msalani au mmewagusa wanawake kisha hamkupata maji, basi mtayammam (ikusudieni) ardhi safi ya mchanga,[An-Nisaa: 43]





Na maana ya:



mmewagusa wanawake:



ni kukutana kimwili baina ya mume na mke kama anavyosema Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu ‘anhuma)



Kwa hivyo hapana shaka kuwa ni lazima kuwe na kuingiliana kwa sehemu za siri ili mtu iwe ni wajibu kuoga, lakini ikiwa ni kugusana kama alivyosema muulizaji kwa kucheza cheza au kupigana busu au kushikana shikana au jambo jengine lolote mbali na kuingiliana hakutakuwa na uwajibu kwa mke kukoga ikiwa hatotokwa chochote vilevile na mume kadhalika. Lakini ikiwa mwanaume kama ulivyosema atatokwa na maji ya uzazi basi itabidi akoge. ‘Ulamaa wote wamekubaliana (wameafikiana) katika hili.



Na Allah Anajua zaidi
 
Hukmu Ya Manyoa Ya Mbwa Anayefugwa Nyumbani
Maswali: Twahara Najsi
Hukmu Ya Manyoa Ya Mbwa Anayefugwa Nyumbani

www.alhidaaya.com





SWALI:



Asalamu aleykum. Nimeowa mwanamke waki Irish mwenye tabia ya kuniongelesha kwa ukali na inanifanya mimi kuelekea kumchukia mwaka wa 5 na hali ni the same. Haniamina ilihali mimi ni muaminifu ana wivu kiasi cha kuitilafia shughuri au kazi zangu zakupatia rizki. Pia amefuga mbwa mdogo mwenye manyoya mengi nimewajibika kumsafisha kumuosha kumfundisha tabia kuto kunya na kukojoa ndani kuto panda kwenye viti au kitandani na kuto rukiarukia watu nime fauru bali yeye hupenda kumbeba hatimaye manyoya hutapakaa nyumba nzima. Nifanye nini ili niedelee kuwa muisilamu? Maasalam.





JIBU:



AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.





Ni muhimu ufahamu kuwa Muislamu anafaa aoe Muislamu ambaye wana ada, tabia na khulqa moja kwa kuwa mambo yao wameyaegemeza katika kufuata Qur-aan na Sunnah.



Sijui huyu Muairish ni Muislamu au bado ni Mkristo au hana Dini au mshirikina. Ikiwa ni Muislamu basi huenda mwanzo ni wewe kumfundisha tabia za Kiislamu ili aweze kuishi nawe Kiislamu. Ikiwa ni Mkristo mbali na kuwa tumeruhusiwa ni lazima awe atatimiza masharti ya wewe kukubaliwa kumuoa na kulingana na maelezo yako ni kuwa bado kutekeleza hayo. Ama akiwa ni mshirikina au hana Dini basi umekatazwa na Uislamu kumuoa kabisa na hata ikiwa mmeoana basi hakuna ndoa nanyi mtakuwa mnazini tu.



Tukija katika mas-ala ya kufuga mbwa nyumbani kwetu Uislamu umetukataza isipokuwa tu ikiwa mmemfuga nje ya nyumba kwa ajili ya kuwinda au ulinzi wa nyumba. Ikiwa ni kwa ajili hiyo Shariy’ah imekubali kumfuga huko na kuhakikisha kuwa umemtekelezea haki zake zote kama kumpatia chakula, maji, kumsafisha na kumpeleka kwa daktari akiwa mgonjwa.



Ama kuhusu manyoa ya mbwa kwa mujibu wa ‘Ulamaa wengi wanaona kuwa yakiwa makavu si najisi bali yanapokuwa na maji au unyevunyevu ndio huwa ni najisi. Lakini kwa mujibu wa baadhi ya ‘Ulamaa wanaona hakuna dalili ya hilo na hivyo manyioa ya mbwa yawe makavu au yenye majimaji, basi hakuna unajisi. Unajisi uliotajwa ni mate yake. Hata hivyo, manyoa hayo yanaondoa unadhifu wa nyumba yakiwa yatatapakaa kote nyumbani. Unajisi wa mbwa ni zile sehemu ambazo zina unyevunyevu kama pua na mdomo. Na lau atanusa kitu au atalamba itabidi kukitwaharisha hiko kitu ukioshe mara saba; sita kwa maji na mara moja kwa mchanga. Na ikiwa mbwa huyo atakuwa huru anazunguka katika nyumba atakavyo, basi hapo kutakuwa na matatizo ya kupatikana hayo yasiyofaa kama kulambwa vitu, kunuswa na mengineyo.



Bonyeza viungo vifuatavyo upate faida zaidi:





Mbwa Wa Kufuga Je, Ni Najsi?



Jinsi Ya Kuondosha Najisi Ya Mbwa Kwenye Nguo





Na Allaah Anajua zaidi
 
Hukmu Ya Wadii Na Madhii
Maswali: Twahara Najsi




SWALI:





asalam alaikum,ndugu zangu waislamu.

Suali langu ni hili kuna vitu vingine vinavyomtokaga mwanamke kwenye sehemu ya siri,sijuwe kama ni wanawake wote,vile vitu ni vyeupe sio rangi ya maji,sijuwe nivifananishe na nini,ila vyeupe wakati mwengine vinarangi ya njano,naweza kidogo kuvifananisha na vitu ambavyovinavyomtokaga mtu kwenye meno kama anapitisha siku nyingi bila kupiga mswaki,naomba ndugu zangu munielekeze kama ile pia ni najisi na hukmu yake mtu akiswali navyo.naomba munijibu ili niondoe wasisi.asante








JIBU:




Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.






Shukran kwa swali lako hilo zuri. Hakika ni kuwa vipo vitu vyeupe aina mbili ambavyo vinamtoka mtu.



Kwanza: Wadii





Yanawatoka baadhi ya watu baada ya mkojo. Hii inafahamika kuwa ni najisi. ‘Aaishah (Radhiya Llahu ‘Anha) amesema: “Wadii inatoka baada ya kukojoa. Mtu anayetokwa anafaa aoshe sehemu zake za siri, kisha achukue wudhuu. Si lazima kuoga” (Ibn al-Mundhir).






Pili: Madhii





Ni maji meupe yanayonata yanayotoka katika sehemu za siri kwa sababu ya kuwaza tendo la ndoa au kutokana na matamanio yaliyozidi ya kimwili kwa kutazama, kushika, kushikwa n.k. Kawaida mtu hafahamu kwa uhakika kinachotoka. Inawatoka wanaume na wanawake, japokuwa kwa wanawake inakuwa ni nyingi zaidi. Wanazuoni wamekubaliana kuwa ni najisi. Ikiingia mwilini, ni wajibu kuiosha na inapoingia nguoni, inatosha kunyunyizia sehemu hiyo kwa maji. ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘Anhu) anasema: “Nilikuwa ninatokwa na madhii mengi, hivyo nikamuuliza mtu amuulize Mjumbe wa Allah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusu hilo kwani niliona haya kwa sababu ya nafasi yangu kwa binti yake. Alisema (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): “Fanya wudhuu na uoshe dhakari yako” (al-Bukhaariy).





Kwa mukhtasari ni kuwa ukitokwa na madhii inafaa uoshe sehemu yako ya siri, utawadhe na kama imeingia nguoni inatosha kunyunyiza maji katika hiyo sehemu.





Na ikiwa vinavyotoka sio katika hivyo viwili basi ni bora akaonane na daktari mahsusi wa wanawake ili ahakikishe zaidi isijekuwa ni maradhi fulani, Allaah Amuepushe nayo.





Na Allah Anajua zaidi
 
Inafaa Kuswali Na Nguo Ya Ndani Ambayo Haina Mkojo, Kinyesi Wala Damu Ila Ni Harufu tu?
Maswali: Twahara Najsi
SWALI:



ASALAM ALEHKUM



POLENI NA KAZI, NA MWENYEZI MUNGU ATA WAJAALIA NGUVU ZAIDI ILI MUWEZE KUTUSAIDIA SISI.



SWALI YANGU KAMA IFUATAVYO. JE KUSWALI NANGUO YA NDANI HAI FAI MWANAMKE KAWAIDA ANAKUA NA HARUFU KIASI SEHEM ZAKE JE KAMA NGUO YAKE IMEPATA JASHO IKATOA HARUFU JE ITA WEZEKANA KUSWALIA (NGUO HIYO INAKUA AINA MKOJO, WA KINYESI WALA DAMU NI HARUFU TU. NITASHUKURU KAMA MTANIJIBU HARAKA. NAWATAKIA KAZI NJEMA







JIBU:




Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.







Shukrani zetu kwa swali lako kuhusu kuswali na nguo ya ndani ambayo haina mkojo wala kinyesi lakini ina harufu.




Harufu ya jasho haitengui wudhuu wala haifanyi nguo ya ndani au ya nje kuwa najisi.







Linalohitajika ni kuwa kwa sababu ya unadhifu wa Muislamu, mwanamke au mwanamme, anapokuwa katika hali hiyo anawaudhi wengine. Kitu anachoweza kufanya ni kujisafisha ili kuondoa hiyo harufu tu.







Pia ni vyema Muislamu anaposwali awe na unadhifu kamili kwani anamkabili Mola Mtukufu Anayestahiki kukabiliwa kwa usafi wa kila aina: sehemu ya kuswalia, nguo za kuswalia na mwili wote uwe msafi na wenye manukato mazuri. Na ndio maana ikakatwza katika Hadiyth ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kutokuwa na harufu ya vitunguu mtu anapokwenda kuswali







Soma zaidi masuala ya Fiqh ndani ya kiungo hiki:




Swahiyh Fiqhus Sunnah







Na Allaah Anajua zaidi.
 
Jinsi Ya Kuondosha Najisi Ya Mbwa Kwenye Nguo
Maswali: Twahara Najsi


Jinsi Ya Kuondosha Najisi Ya Mbwa Kwenye Nguo





www.alhidaaya.com







SWALI:



Swali langu ni kwamba, Je hii najis inaondoshwa vipi ya mbwa? na je akininusa juu ya nguo sio kwenye ngozi inabidi nikoshe zile nguo tu au na mimi mwenyewe nijikoshe? na je inanuiwa vipi wakati wa kujikosha na kuiondosha hii najsi ya mbwa?

Natumai swali langu litawanufaisha waislamu wenzangu wengi hasa wanaoishi nchi za nje. Naomba tafadhalini munijibu haraka iwezekananyo kwani nategemea kuanza kazi pahala ambapo pana mbwa karibuni in shaa Allaah.



JIBU:







AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.





Kuhusu najisi inayopatikana kwa kunuswa na mbwa basi maelezo ni kama yafuatayo.

Pahali paliponajisiwa kwa kurambwa na mbwa au kunuswa kama chombo na kadhalika mfano huo. Ili kitu hicho kutwaharika na kusafishika na kurudi katika hali yake ya kawaida na usafi kinatakiwa kioshwe mara saba mojawapo kwa mchanga. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

"Anaporamba mbwa kwenye chombo cha mmoja wenu, basi akioshe mara saba, mojawapo kwa mchanga" [Muslim, Ahmad na Abu Daawuwd].



Ikiwa amenusa kwenye nguo utaiosha nguo tu kwa mchanga na maji ikiwa hakuna taklifa, la sivyo unaweza kutumia sabuni na maji hususan ikiwa utafua nguo hiyo kwa mashine ya kufulia nguo, na akiwa amenusa ngozi yako basi utaiosha hiyo sehemu ya ngozi kwa maji na mchanga mara saba. Pia unaweza kutumia sabuni pamoja na maji.



Niyyah ya kila kitu iko moyoni, hivyo ukishanuia moyoni mwako kuondosha najisi inatosheleza kabisa, huna haja kutamka wala kusema maelezo au kuyahifadhi.



Bonyeza viungo vifuatavyo kupata faida zaidi:





Mbwa Wa Kufuga Je, Ni Najsi?



Hukmu Ya Manyoa Ya Mbwa Anayefugwa Nyumbani



Jinsi Ya Kuondosha Najisi Ya Mbwa Kwenye Nguo



Na Allaah Anajua zaidi
 
Kiasi Cha Maji Kuondosha Najsi
Maswali: Twahara Najsi
SWALI:

nikiasi gani cha maji kinaweza ku twaharisha maali ambapo kuna najisi? Naona nikijibiwa mapema nitapata amani ya roho. asante ndungu zangu,Mola awajaanlie mwisho mwema.









JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Ikiwa najisi ipo kwenye ardhi basi inatosha kumwaga maji sehemu hiyo mara moja. Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliamrisha apatiwe maji ile sehemu ya Msikiti ambamo Bedui alikojoa (Al-Bukhaariy na Muslim).

Ikiwa najisi haipo kwenye ardhi, kwa mfano mbwa au nguruwe ameramba chombo panahitajika paoshwe mara saba mojawapo ikiwa ni kwa mchanga (Muslim).

Hukumu hii ni ya ya kijumla kwa vyombo na vyenginevyo kama nguo, godoro na kadhalika.

Ikiwa najisi ni ya mkojo, mavi, damu na mfano wake, unaiosha kwa maji mpaka sura yake, rangi, ladha na harufu yake iondoke. Hivyo, utumiaji wa maji hauna kiasi maalumu ila kila yakiwa kidogo ni bora zaidi. Utazame kuwa hutafanya israfu na ubadhirifu katika hilo. Ikiwa utatumia sabuni na madawa mengine ya kusafishia pia inajuzu.

Kwa maelezo zaidi bonyeza viungo vifuatavyo:

009 Najisi Zinazosamehewa
010 Namna Ya Kuzitwaharisha Aina Mbalimbali Za Najisi Ambazo Matini Imekuja Kuzibainisha
011 Je, Ni Lazima (kutumia) Maji Katika Kuondosha Najisi? Au Inajuzu Kuondosha Kwa Vimiminika Vinginevyo Au Mada Nyinginezo?
Na Allaah Anajua zaidi
 
Kiasi Gani Cha Alcohol Katika Vipodozi Kinahesibaki Kuwa Ni Najisi?
Maswali: Twahara Najsi
SWALI LA KWANZA:




a.a.m ndugu waislamu mimi nataka kujua kama ukitumia mafuta ya nywele yaliotiwa isoproyl alcohol na alcohol denat ni najis yafafaa kutumia au hayafai kutumia. Nafurahii sana kupata mahali kama hapa kuuliza maswali ya kiislamu inshl ALLAH awazidishie imaan zenu shukran







SWALI LA PILI:




Assalam alaykum.

Nimesoma jawabu kuhusu mafuta, lotion na dawa za nyele zenye alcohol. Tafadhali nifafanulieni asli mia ngapi ndio kiwango kidogo? Na je kama hatujui kiwango gani kimetumika tutajuwa vipi yafaa au haifai. Kuna tafauti baina ya alcohol na "alcohol denat" na "isopropyl alcohol". Zote ni najis au laa. Mungu awajazi kheir









JIBU :


Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.






Kwanza kabla hatujajibu swali lako, tunakukumbusha kuwa unapoandika Salaam hazifai kufupishwa kwa kuandikwa (A.A) au (A.A.W.W.) au kama ulivyoandika kwani haijafundishwa hivyo na pia ni kujikosesha fadhila za Salaam kama tulivyoelezwa na Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Hivyo nayo tujizoeshe kuandika (Assalaamu ‘alaykum) au (Assalaamu ‘alaykum wa rahmatullaah) au (Assalaamu ‘alaykum wa Rahmatullaah wa Barakaatuh) kwa ukamilifu na tutakuwa tumeiga mafunzo ya Mtume wetu (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na pia tutakuwa tumezoa thawabu zote za Salaam kama tulivyofundishwa. Na Mafunzo yote na fadhila zake zimo Alhidaaya katika kiungo kifuatacho: Maamkizi Ya Kiislamu.



Shukran zetu za dhati kwa swali lako kuhusu mafuta yenye alcohol. Mwanzo tungependa kufahamisha kuwa alcohol yenyewe (yaani methanol na ethanol) sio najisi kama tulivyotangulia kusema katika jibu letu kuhusu hilo. Ingia kwenye viungo hivi hapa chini:




Je, (pombe) Pombe Ni Katika Vitu Najisi?

Kutumia Lotion au Mafuta Ambayo Ingredient Yake Ina Alcholol




Isopropyl alcohol ina majina mengi mbali na hilo, baadhi yake yakiwa Isopropanol, 2-propanol, propan-2-ol, sec-propyl alcohol, dimethyl carbinol, isohol, petrohol, na kadhalika. Kulingana na jina inaonyesha kuwa alcohol aina hii ni tofauti na ethanol kwa kuwa hii ina C tatu na –OH yake iko katika C nambari 2, yaani ya katikati. Alcohol hii inawaka, haina rangi kama vile maji, ni maji yenye harufu inayofanana na ethanol. Na kulingana na utafiti uliofanywa kuihusu ni kuwa ina madhara mengi na makubwa kwa binadamu, hivyo kuifanya utumiaji wake kuwa haramu.




Kama tulivyoeleza hapo awali ni kuwa inaweza kutumiwa katika nywele lakini kuacha kutia ni bora zaidi kwani kule kunusa kunaweza kukuletea madhara na hata huenda kule kupaka kwenyewe. Kukiwa na utata katika jambo basi sheria inatuamuru kuliacha jambo hilo. Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

“Hakika halali iko wazi, na haramu iko wazi, na baina ya vitu viwili hivi kuna mambo yenye shaka, watu wengi hawayajui. Basi mwenye kuepuka mambo yenye shaka, hakika amehifadhi Dini yake na heshima yake. Na mwenye kuingia katika mambo ya shaka ameingia katika haramu…” (Al-Bukhaariy na Muslim).




Ingia katika viungo vifuatavyo upate maelezo zaidi:




Kutumia Lotion au Mafuta Ambayo Ingredient Yake Ina Alcholol




Ama jibu la Swali la pili ni kwamba kiwango ambacho kinaweza kutumika hakipo katika Uislamu. Hata hivyo, kiwango kinachotumika ni kule kuwepo kwake hata ikiwa ni asilimia ndogo na namba. Uislamu una kanuni: ‘Kiliweshacho kingi hata kidogo chake ni haramu.’ Hivyo ni bora kutotumia lotion na dawa za nywele zenye alcohol kama alivyosema Mwanachuoni Ibn ‘Uthaymin. Ama Isopropyl alcohol tafadhali tazama jawabu letu kuhusu hilo kwa swali lililo juu.




Kuhusu alcohol denat ni ethyl alcohol (au ethanol) ambayo imeongezwa kemikali zilizo sumu kama acetone au methanol kuifanya isiweze kutumika na watu kwa njia ya kunywa. Kwa ajili ya ile sumu inafanya matumizi yake yenye athari zaidi hata ikiwa ni kutiwa kwenye nguo. Tufahamu kuwa Allaah Aliyetukuka Anatuambia:

“Wala msijitie kwa mikono yenu katika maangamizi” (2: 195).




Hivyo, kama Waislamu inatakiwa tujiepushe na alcohol, isopropyl alcohol na alcohol denat mbali na kuwa zote si najisi lakini ni haramu kutumiwa.




Na Allaah Anajua zaidi
 
Kutambua Madhii Na Wapi Hasa Yapo Katika Nguo – Kiasi Gani Cha Madhii
Maswali: Twahara Najsi



SWALI:




Asalaam aleykum warahmatullah taala wabarakat. Ama baada ya salaam ningependa kwanza kutumia nafasi hii kuwapongeza na kuwashukuru kwa jitihada njema kabisa za kuuelimisha ummah juu ya mas-ala mbalimbali ya kidini, namuomba allah aikubali kazi yenu inshaallah.




Swali langu leo ni kuhusiana na "MADHII"

Swali hili lilishaulizwa kabla na mmoja wetu, alhamdullillah nilipata fursa ya kuyasoma majibu yako, lakini kutokana na ugumu wa hili jambo sikuweza kusuluhisha tatizo hili kwa kutumia ushauri ulioutoa. KAMA TUJUAVYO MADHII HUMTOKA MTU WAKATI WOWOTE, HUWA WAZI PALE MTU ANAPOPATWA NA MATAMANIO YA JUU SANA LAKINI VINGINEVYO SI WAZI NA NI VIGUMU KUJUA KAMA YAMEKUTOKA, JE NINI NI KIPIMO CHA KUKUJULISHA KUWA HUENDA MADHII YAMEKUTOKA? IKIWA UMETAMBUA KUWA MADHII YAMEKUTOKA NA HUENDA YAMEGUSA NGUO YAKO YA NDANI KWA MUJIBU WA MAJIBU YAKO YA AWALI ULISEMA NI TOSHA KUNYUNYUZIA MAJI KTK SEHEMU ILIYOADHIRIKA, JE UTAIJUA VIPI HIYO SEHEMU ILIYOINGIWA NA MADHII?







SWALI LA PILI:




mimi ni msichana ambae sijiolewa na nimesoma kwamba mtu akitoka manii ni lazima aoge ndipo afanye ibada ukweli siyajuwi isipokuwa nimesoma kuwa ni kama maji mazito na yana harufu swali je ni wingi gani yanapotoka na jee kuna tofauti wa wingi kwa mwenye kujimai na mwenye kutamani kwa kufikiri







JIBU:




Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.




Shukrani kwa swali lako kuhusu madhii.




Hakika ni kuwa madhii humtoka mtu akiwa na matamanio ya kutaka kufanya tendo la ndoa. Hakika hakuna kipimo cha kuweza kujua kuwa madhii yamekutoka isipokuwa ule utokaji wake hukujulisha hilo kwani madhii humtoka mtu akiwa macho tofauti na manii ambayo yanaweza mtu akiwa amelala au yuko macho. Ikiwa hali ni hiyo, yanapotoka utahisi na hivyo kujua sehemu yalipoingia.




Ikiwa hukuweza kutambua yameingia katika sehemu gani ya nguo, japokuwa jambo hilo ni muhali, ni wewe kuinyunyiza nguo yote kwa maji au kuiosha. Kwa kufanya hivyo utaondoa tatizo linalokukabili.




Manii yanapomtoka mtu akiwa amelala au yuko katika kitendo cha jimai basi hata yakiwa kidogo anapaswa kuoga ili awe safi kwa ajili ya ‘Ibaadah kadhaa. Kwa hiyo, ile hali ya kutokwa na manii tu inakubidi uoge.




Tafadhali bonyeza kiungo kifuatacho upate manufaa zaidi:




Tofauti Baina Ya Manii Na Madhii Na Hukumu Zake Za Ghuslu




Hukmu Ya Wadii Na Madhii




008 Nini Hukumu Ya Majimaji (utoko) Yanayotoka Kwenye Utupu Wa Mwanamke Na Kile Kiitwacho Unyevunyevu Wa Utupu Wa Mwanamke?







Mwanamke Akitokwa Na Majimaji, Je, Aoge Janaba?




Na Allaah najua zaidi
 
Tofauti Baina Ya Manii Na Madhii Na Hukumu Zake Za Ghuslu
Maswali: Twahara Najsi
SWALI

mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 25 na sijaolewa na pia ni mwislam safi na najiamini na pia nina imani katika dini yangu na namwomba MWENYEZI MUNGU anizidishie mimi na wewe INSHAALAAH NA WAISLAM WOTE AMINI. ninatatizo moja nalo ewe utakayesoma naomba nistiri. huwa nakuwa nikitokwa na manii mara kwa mara hata kama sijawaza au kutamani map












JIBU:

BismiLLaah wa AlhamduliLLaah was-Swalaatu wa Salaamu ‘alaa Muhammad wa ‘alaa aalihi wa Aswhaabihil Kiraam, wa ba’ad:

Inaonyesha kutokana na usemi wako kwamba yanayokutoka ni 'madhiy' na sio 'maniy'. Na kuna tofauti katika vitu hivi viwili kama ifuatavyo:

A-Tofauti zao kuhusu sifa zake:

Manii

Shahawa (manii) ya mwanamume ni maji meupe mazito. Kwa mwanamke ni ya rangi ya manjano na mepesi. Manii kwa kawaida huwa ni maji yanayotokwa kwa mwanamume au mwanamke wakati wa kilele cha raha wakati wa mapenzi.

Dalili ya sifa hiyo ya manii ni kutoka:

عن أم سليم رضي الله عنها أنها سألت نبي الله صلى الله عليه وسلم عن المرأة ترى في منامها ما يرى الرجل . فقال رسول الله صلى الله عليه وسلم : " إذا رأت ذلك المرأة فلتغتسل " فقالت أم سليم : - واستحيَيْتُ من ذلك - قالت : وهل يكون هذا ؟ . فقال النبي صلى الله عليه وسلم : " فمن أين يكون الشبه ؟ إن ماء الرجل غليظ أبيض وماء المرأة رقيق أصفر فمن أيهما علا أو سبق يكون الشبه " متفق عليه

Hadiyth ya Ummu Sulaym رضي الله عنها ambaye alimuuliza Mtume صلى الله عليه وآله وسلم kama mwanamke mwenye kuota ndoto ya kujimai inampasa afanye ghuslu. Mtume صلى الله عليه وآله وسلم alisema "Ndio ikiwa ataona maji".Ummu Sulaym akasema: "Niliona haya niliposikia hivyo nikauliza: "Inawezekana hivyo?" Mtume صلى الله عليه وآله وسلم akasema: "Vipi basi mtoto atamshabihi baba yake au mama yake? Maji ya mwanamume ni mazito na meupe na maji ya mwanamke ni mepesi na manjano. Yoyote kati ya hayo yatakayotoka mwanzo ndio yanayosababisha mzazi gani awe ni mwenye kumshabihi mtoto" [Al-Bukhaariy Na Muslim]



Sifa zifuatazo tatu ndizo zenye kujulisha manii ya mwanamume:

1. Kutoka kwake kunaambatana na kilele cha raha na kufuatilia uchovu.

2. Harufu yake ni kama chavuo (pollen) ya mtende ambayo huwa kama harufu ya unga uliokandwa.

3. Hutoka kwa kububujika kwa nguvu.



Mojawapo katika sifa hizo inatosha kutambulisha kuwa ni manii.

Ikiwa mtu ametokwa na maji na hazikupatikana sifa hizo basi hayatakuwa ni manii.



Sifa mbili za manii ya mwanamke:

1. Yana harufu kama harufu ya manii ya mwanamume.

2. Kutokwa kwake kunaambatana na hisia ya kilele cha raha na hufuatilia na uchovu.

Madhiy

Madhiy ni maji yenye kunata na yanamtoka mtu aidha anapokuwa anawaza au kutamani kujimai, au hata bila ya kuwaza kama ilivyo katika hali ya muulizaji. Na hazina sifa kama sifa za manii tulizozitaja hapo juu. Na pia huwatokea wanawake na wanaume ila aghlabu huwatokea sana wanawake. (Hii ni rai ya Imaam An-Nawawiy katika maelezo yake ya Sharh Muslim 3/213

B-Tofauti kuhusu ya hukumu yake baada ya kutokwa

Manii:

Yanapotoka manii, inampasa mtu afanye ghuslu kwa ajili ya kujitoharisha (janaabah) ikiwa yamemtoka mtu manii wakati wa kujimai au kwa hali yoyote nyingine ikiwa yu macho au ameota ndoto n.k.

Madhiy

Yanapomtoka mtu madhiy humpasa kufanya wudhuu tu. Na dalili ni:

((ما رواه علي بن أبي طالب رضي الله عنه قال : كنت رجلا مذّاء فأمرت المقداد أن يسأل رسول الله صلى الله عليه وسلم فسأله فقال : " فيه الوضوء ")) متفق عليه

((Kutoka kwa 'Aliy bin Abi Twaalib رضي الله عنه ambaye amesema: "Nilikuwa ni mtu niliyekuwa nikitokwa sana na maji ya urethra (madhii). Nikamuambia Miqdaad amuulize Mtume صلى الله عليه وآله وسلم kuhusu hilo. Akamuuliza na akasema: "Inahiitajika kufanya wudhuu")) [Al-Bukhaariy na Muslim]

C-Tofauti kama ni najisi au ni tohara

Manii

Manii ni tohara kutokana na rai za Maulamaa ambao wamechukua dalili kutokana na mapokezi yafuatayo:

((عن عائشة رضي الله عنها قالت : "كان رسول الله صلى الله عليه وسلم يغسل المني ثم يخرج إلى الصلاة في ذلك الثوب وأنا أنظر إلى أثر الغسل فيه")) . متفق عليه

((Kutoka kwa Bibi 'Aishah رضي الله عنها ambaye amesema: "Mtume صلى الله عليه وآله وسلم alikuwa akikosha manii (yaliyokuwa katika nguo yake) kisha akienda kuswali akiwa ameivaa nguo hiyo na nilikuwa naona sehemu aliyoiosha")) [Al-Bukhaariy na Muslim]

وفي رواية لمسلم " ولقد كنت أفركه من ثوب رسول الله صلى الله عليه وسلم فركا فيصلي فيه

Kutokana na mapokezi yaliyosimuliwa na Muslim "Nilikuwa nikiyafikicha vizuri (manii) kutoka nguo ya Mtume صلى الله عليه وآله وسلم kisha akiiswalia" (hiyo nguo).

وفي لفظ " لقد كنت أحكّه يابسا بظفري من ثوبه "

Na usemi mwingine: "Nilikuwa nikiikwaruza kutoka katika nguo kwa makucha yangu baada ya kukauka".

بل ثبت أن النبي صلى الله عليه وسلم كان يترك غسله وهو رطب ويكتفي بمسحه بعود ونحوه كما روى الإمام أحمد في مسنده عن عائشة رضي الله عنه قالت : "كان رسول الله صلى الله عليه وسلم يسلت " يزيل ويميط " المني من ثوبه بعرق الأذخر ثم يصلي فيه ويَحتّه من ثوبه يابسا ثم يصلي فيه " ورواه ابن خزيمة في صحيحه وحسنه الشيخ الألباني في الإرواء.

Imethibitika kwamba Mtume صلى الله عليه وآله وسلم alikuwa akiyaacha bila ya kuyaosha na yalikuwa bado maji maji, ilitosheleza kuyafuta kwa kijiti kama ilivyosimuliwana Imaam Ahmad katika Musnad yake kutoka kwa 'Aishah رضي الله عنها ambaye amesema: "Mtume صلى الله عليه وآله وسلم alikuwa akiyaondosha manii katika nguo yake kwa mche wa adhkhar (aina ya mti), kisha akiiswalia nguo, kisha akiyafikicha baada ya kukauka na akiiswalia nguo hiyo hiyo" [Ibn Khuzaymah na Shaiyk Al-Albaaniy ameipa daraja ya Hasan katika Al-Irwaa ]

Madhii

Madhii ni najisi kutokana na Hadiyth:

أن النبي صلى الله عليه وسلم أمر بغسل الذكر والأنثيين ( أي الخصيتين ) ويتوضأ كما)) أخرجه أبو عوانة في مستخرجه وقال ابن حجر في التلخيص : وهذا إسناد لا مطعن فيه

Kwamba Mtume صلى الله عليه وآله وسلم aliamrisha kuosha sehemu ya siri ya mwanamume kisha atawadhe)) [Imesimuliwa na Abu 'Awaanah katika Al-Mustakhraj – Ibn Hajar kasema katika Al-Talkhiys "Hakuna makosa katika isnaad hii']

Kwa hiyo madhii ni najisi na sehemu za siri zioshwe kwani yanatengua tohara.

D- Kuhusu nguo zilizoingia manii na madhii

Manii

Kwa vile manii ni tohara, basi yatakapoingia katika nguo hayafanyi nguo kuwa ni najisi, na anaweza mtu kuswalia nayo nguo hiyo. Lakini ni bora kuyafuta kama alivyosema Ibn Qudaamah katika Al-Mughni "Hata kama inasemekana kuwa manii ni tohara, lakini ni bora kuyafuta, lakini mtu akiswalia nayo Swalah itaswihi.

Madhii

Madhii yakiingia katika nguo inatosheleza kurashia maji juu yake kwa sababu kuepusha mashaka ya kuoga kila mara, kwani dini yetu ni nyepesi. Na dalili ni kutoka katika Hadiyth

عن سهل بن حنيف قال : كنت ألقى من المذي شدة وكنت اكثر من الاغتسال فسالت رسول الله صلى الله عليه وسلم عن ذلك فقال " إنما يجزئك من ذلك الوضوء . قلت : يا رسول الله فكيف بما يصيب ثوبي منه ؟ قال : يكفيك بأن تأخذ كفاً من ماء فتنضح بها ثوبك حيث تُرى أي تظنّ أنه أصابه " ورواه الترمذي وقال الألباني : هذا حديث حسن

Kutoka kwa Sahl ibn Haniyf ambaye amesema: "Nilikuwa nikitokwa na madhii na nilikuwa nikifanya ghuslu kila mara. Nikamuuliza Mtume صلى الله عليه وآله وسلم akasema: "Inakutosheleza kufanya wudhuu" Nikasema: "ewe Mjumbe wa Allaah, vipi yakiingia katika nguo yangu?" Akasema: "Inakutosheleza kuchukua maji mkononi na kurashia juu ya nguo zako popote unapodhani (kuna madhiy")) [At-Tirmidhiy na kasema Shaykh Al-Albaaniy : Hadiyth,Hasan]

Ili kutatua mushkila wako kuwa unatokwa na madhiy kila mara, ni bora kuvaa hifadhi nyepesi (panty-liners) au hata tissues ili ubakie safi katika nguo yako ya ndani na kila unapokwenda msalani kwa haja uwe unabadilisha. Kufanya hivi kutakuepusha na kurashia maji nguo yako ya ndani (underwear), na pia utakuwa unapata wepesi wa kutekeleza wudhuu wako.

Na Allah Anajua zaidi
 
Mwanamke Akitokwa Na Majimaji, Je, Aoge Janaba?
Maswali: Twahara Najsi
SWALI:




Assalam Alaikum ndugu zangu wa Alhidaya.




Je mwanamke akiwashwa katika uchi wake wa mbele ilhali hana hamu na mwanamume yeyote, akajikuna mpaka maji yakatoka na bado muwasho ule usiishe je anatakikana kuoga janaba, muwasho huu ni wa kawaida kama vile kuwashwa katika moja ya viungo vyengine vya mwili.




Inshallah Kheir.





JIBU:




Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.




Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu mwasho wa kawaida ambao mwanamke anapata. Mwasho kama huo kawaida unawapata si wanawake pekee bali hata wanaume. Kwa hiyo, awali ya yote tungetoa nasaha kwa dada yetu akaenda kwa daktari ili ajue ni kitu gani kwani unaweza au anaweza kukaa hivyo na huo ugonjwa alio nao ukawa unazidi.




Tukija sasa katika swali lako tunasema hivi: Mwanamke ni tofauti na mwanamme kwa kuwa katika sehemu za mbele za siri za mwanamke kunakuwa na majimaji ambayo hayadhuru nayo ni tofauti na manii. Kwa hiyo, mwanamke mwenyewe anaweza kuelewa wakati ametokwa na manii na wakati anapokuwa na majimaji ya kawaida.




Kuhusu manii Ummu Salamah (Radhiya Allaahu ‘anha) amesema:

Alikuja Ummu Sulaym (Radhiya Allaahu ‘anha) – mke wa Abu Twalhah (Radhiya Allaahu ‘anhu) – kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: “Ewe Mtume wa Allaah! Hakika Allaah Haoni haya juu ya ukweli. Je, mwanamke anahitajia kuoga anapoota?” Akaseme Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): “Ndio, anapoona maji?” (Al-Bukhaariy na Muslim).




Hivyo, mwanamke anapoona manii katika nguo yake inakuwa wajibu wake kuoga na ikiwa hakuona basi hakuna kuoga hata akikumbuka kuwa aliota. Hii ni kwa mujibu wa Hadiyth ya mama wa Waumini ‘Aaishah (Radhiya Allaahu ‘anha) aliyesema:

“Aliulizwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): kwa mtu anayeona unyevunyevu wala asikumbuke kuwa aliota?” Akasema: “Ataoga”. Na mtu aliyedhani kuwa ameota lakini asione unyevunyevu?” Akasema: “Hatooga” (Abu Daawuud na at-Tirmidhiy).




Tanbihi:




ü Mwanamke kwa yote ni kama mwanamme sawa kwa sawa, kumaanisha kuwa akitokwa na manii kwa kuota au kwa matamanio basi inabidi aoge josho la janaba.

ü Mwenye kutokwa na manii bila shahwa (matamanio) kwa sababu ya ugonjwa, baridi na mfano wake, hapaswi kuoga kwa kauli yenye nguvu na sahihi nayo ni madh-hab ya jamhuri kinyume na kauli ya Imaam Shaafi‘iy na Ibn Hazm.




Wamejumlisha wanazuoni uwajibu wa kuoga kwa kutokwa na manii kwa matamanio ukiwa macho na kwa kuota pamoja na kutokwa na manii.




Kwa muhtasari, mwanamke hutokwa na majimaji aina nyingi, mfano majimaji ya kawaida, manii, madhii na wadii. Ni akitokwa na manii tu ndio atapaswa kuoga. Hivyo, hayo majimaji yanayotoka ni manii nayo katika kujikuna anaingiwa na matamanio, itabidi aoge na bila shaka atakuwa anajua tofauti baina ya majimaji na maji ya manii.




Ingia katika viungo vifuatavyo upate maelezo zaidi:




Tofauti Baina Ya Manii Na Madhii Na Hukumu Zake Za Ghuslu




Hukmu Ya Wadii Na Madhii










Na Allaah Anajua zaidi
 
Kutumia Toilet Paper Kwa Kujisafisha Choo
Maswali: Twahara Najsi
Kutumia Toilet Paper Kwa Kujisafisha Choo









SWALI:



Inafaaa kujisafisha haja ndogo (mkojo) kutumia toilet paper?





JIBU:





AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho





Kutumia toilet paper au karatasi, Shariy’ah iko wazi ikiwa maji yamekosekana basi ni ya Istijmaar (kutumia mawe kujisafisha) na karatasi inachukua mahali pa mawe. Hata maji yakiwepo unaweza kujisafisha na karatasi kwanza kisha ukatumia maji ili usafi uwe mzuri zaidi, na hivyo ni bora zaidi.



Lakini tena kwenye suala hilo la kutumia makaratasi, tunavyojua vyoo vilivyopo nchi za kigeni ni kweli hawaweki vyombo vya maji kwa ajili ya kujisafishia, lakini tunavyofahamu kuwa hakatazwi mtu kuingia na chupa yake au kikombe chake cha kutumia na kutupa ‘disposable cups’ na kutumia kwa haja yake.



Kinachowazuia wengi kufanya hivyo, si makatazo, bali ni kuwaonea hayaa wazungu ndio kunawapelekea wengi kutafuta njia za mkato na hali hakuna dharura hiyo.



Ama ikiwa hakuna maji kabisa sehemu hiyo, basi hukatazwi kutumia toilet paper. Na kama kuna maji lakini umekosa kabisa chombo cha kutumia kutekea maji na kujisafishia, basi unaweza kuzitumia hizo toilet paper na kuzichovya kwenye maji kisha ukajisafishia ili kupatikane usafi zaidi na kutakatike na kuhakikishike kuwa hakujabaki aina yoyote ya uchafu.



Hata hivyo kwa zama za sasa imebainika kwamba vyoo vingi vya nchi za kigeni wanatumia maji.





Na Allaah Anajua zaidi
 
Mbwa Wa Kufuga Je, Ni Najsi?
Maswali: Twahara Najsi


Mbwa Wa Kufuga Je, Ni Najsi?



www.alhidaaya.com





SWALI:



Asalam alaykum

kwa uwezo wa Allah nimejaaliwa kuwepo nchini china kwa ajili ya masomo hata hivyo nimekutana na waislam wa nchi nyingine mbalimbali ambapo siku moja muislamu mwenzangu kutoka India nilimkuta kapakata mbwa nami nilimshangaa hata hivyo nilipomuuliza juu ya kunajisika kwa kufanya hivyo alinijibu mbwa wa mazoea (wa kufuga) hana najisi sikumpinga ila sikuridhika na jibu hilo hivyo naomba ufafanuzi naomba ikiwezekana nipate jibu kwa kupitia email yangu







JIBU:



AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.





Mbwa mwenyewe hawezi kusemwa ni najisi kwa kutokuwa na dalili ya hilo, isipokuwa mate yake na majimaji ya puani mwake yanachukuliwa ni najisi ki-Shariy’ah ikiwa ni wa kufuga au vinginevyo kwa dalili iliyopatikana kutoka katika Hadiyth. Na kwa hivyo chombo chochote ambacho kitarambwa na mbwa kinapaswa kutwaharishwa kwa kuoshwa mara saba bila kutofautisha ni mbwa gani aliyekiramba, mojawapo kwa mchanga. Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema, Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Kukitwahirisha chombo kilichorambwa na mbwa kunafanywa kwa kuosha mara saba, mojawapo kwa udongo” [Ahmad, Muslim, Abu Daawuwd na al-Bayhaqiy]



Na ikiwa ataramba chombo chenye chakula kikavu, kile chakula kilichoguswa na mdomo wa mbwa na kilicho pembezoni mwake kinatakiwa kitupwe, ama kilichobaki ni twahara kinaweza kubakishwa. Ama manyoya ya mbwa yakiwa makavu ni twahara. Sehemu iliyo najisi ya mbwa ni ule mdomo wake kwa ajili ya umandemande.



Hivyo, mtu kucheza na mbwa au kumpakata na kumfanya ni kichezeo, si jambo lenye kushauriwa kwa kupatikana uwezekano wa kunuswa au kurambwa nguo yake na maeneo ya kuswalia na sehemu mbalimbali za nyumba yake. Mbwa si kama paka, hivyo si jambo zuri watu kuiga tabia za wasio Waislamu na wao kuanza kufuga mbwa wa vichezeo na kuwafanya kama paka. Muislamu hata akibidi kuwa na mbwa wa ulinzi, anapaswa amweke nje ya nyumba; uani au sehemu ambayo si ndani ya nyumba ili kuepuka kutiliwa najisi vyombo, nguo na sehemu za kufanyia 'ibaadah.



Bonyeza viungo vifuatavyo upate faida zaidi:



Jinsi Ya Kuondosha Najisi Ya Mbwa Kwenye Nguo





Kwa Nini Nguruwe Na Mbwa Haraam?





Na Allaah Anajua zaidi
 
Kwa Nini Nguruwe Na Mbwa Haraam?
Maswali: Vyakula Vya Halali
Kwa Nini Nguruwe Na Mbwa Haraam?



www.alhidaaya.com







SWALI:



Na naomba unipe maelezo yanayofanya mbwa na nguruwe wawe haramu... just i need points that lead them to be haram to islam society



JIBU:



AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.





Mas-ala ya halaal na haraam ni haki ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Peke Yake. Hakuna mwengine yeyote ambaye ana jukumu kama hilo. Hii ni kuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Ambaye Ametuumba sisi wana Aadam Ndiye Mwenye kujua vilivyo vizuri kwetu na vile ambavyo ni madhara kwetu sisi. Sisi viumbe Vyake hatuna haki ya kumsaili wala kumuasi Yeye. Kwa kuwa Yeye ni Mwingi wa Rehma kwa waja Wake, Anahalalisha na kuharamisha kwa sababu na hekima, kwa kutilia maanani maslahi ya mwana Aadam. Hivyo, Alivyohalalisha ni safi na vizuri na Ameharamisha vile ambavyo ni vichafu na vibaya.



Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Enyi watu! Hakika Allaah ni Mzuri na Hapokei ila kilicho kizuri. Na Allaah Amewaamrisha Waumini kama Alivyowaamrisha Rasuli Anaposema: “Enyi Rusuli! Kuleni katika vizuri na tendeni mema, hakika Mimi kwa yale myatendayo ni Mjuzi.” [Al-Muuminuwn (23: 51)] Na Anasema: “Enyi walioamini! Kuleni vizuri Tulivyokuruzukuni.” Kisha akataja kisa cha mtu aliyekuwa safarini akiwa katika hali ya uchafu na mavumbi akiinua mikono yake mbinguni akiomba: Eee Rabb! Ee Rabb! Na hali chakula chake ni haramu, kinywaji chake ni haramu na kajengeka mwili wake kwa haramu vipi atakubaliwa du'aa yake?’ [Muslim]





Ni kweli kuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Aliharamisha baadhi ya vitu vizuri kwa Mayahudi kama adhabu ya ukaidi wao na kuvuka mipaka iliyowekwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa). Lakini Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Alipomtuma Rasuli Wake wa mwisho na Akaikamilisha Dini kwa wana Aadam Aliwarehemu watu kwa kuondosha vikwazo hivyo. Allaah (Subhaanahu wa Ta'alaa) Anasema:



يَأْمُرُهُم بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَاهُمْ عَنِ الْمُنكَرِ وَيُحِلُّ لَهُمُ الطَّيِّبَاتِ وَيُحَرِّمُ عَلَيْهِمُ الْخَبَائِثَ وَيَضَعُ عَنْهُمْ إِصْرَهُمْ وَالْأَغْلَالَ الَّتِي كَانَتْ عَلَيْهِمْ ۚ

Anawaamrisha mema na anawakataza munkari, na anawahalalishia vizuri na anawaharamishia maovu, na anawaondoshea mizigo yao na minyororo iliyokuwa juu yao. [Al-A’raaf: 7]





Kulingana na Uislamu vitu vinaharamishwa kwa sababu nyingi; ima kwa hekima, au bila hekima ikiwa ni sehemu ya mitihani na kupimwa viumbe utiifu wao, na kwa hekima mfano ni vichafu au vina madhara. Ikiwa kitu chochote kina madhara kinakuwa haraam; na kikiwa kina manufaa kinakuwa halaal; na kikiwa madhara yake ni makubwa kuliko manufaa kitakuwa ni haraam; ilhali madhara yake yakiwa ni kidogo kuliko manufaa kinakuwa ni halaal. Kanuni hii imeelezwa katika Qur-aan kuhusiana na pombe na kamari:



يَسْأَلُونَكَ عَنِ الْخَمْرِ وَالْمَيْسِرِ ۖ قُلْ فِيهِمَا إِثْمٌ كَبِيرٌ وَمَنَافِعُ لِلنَّاسِ وَإِثْمُهُمَا أَكْبَرُ مِن نَّفْعِهِمَا ۗ وَيَسْأَلُونَكَ مَاذَا يُنفِقُونَ قُلِ الْعَفْوَ ۗ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ اللَّـهُ لَكُمُ الْآيَاتِ لَعَلَّكُمْ تَتَفَكَّرُونَ ﴿٢١٩﴾

Wanakuuliza kuhusu pombe na kamari. Sema: “Katika viwili hivyo mna dhambi kubwa na (baadhi ya) manufaa kwa watu. Na dhambi yake viwili hivyo ni kubwa kuliko manufaa yake.” Na wanakuuliza nini watoe. Sema: “Yaliyokuzidieni.” Hivyo ndivyo Allaah Anavyokubainishieni Aayaat (na shariy’ah) ili mpate kutafakari. [Al-Baqarah: 219]





Kwa mantiki hiyo hiyo, ikiwa itaulizwa, ni kitu gani ambacho ni halaal katika Uislamu, jibu ni vitu vizuri. Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema:



يَسْأَلُونَكَ مَاذَا أُحِلَّ لَهُمْ ۖ قُلْ أُحِلَّ لَكُمُ الطَّيِّبَاتُ ۙ

Wanakuuliza wamehalalishiwa nini? Sema: Mmehalalishiwa vizuri [Al-Maaidah: 5]





Muislamu haitajiki kujua kwa uhakika uchafu au madhara ya Alivyoharamisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa); inaweza kuwa imefichikana naye au madhara yake hayajavumbuliwa. Kinachohitajika kwa Muislamu ni kusema: "Nimesikia na nimetii".





Lakini leo kwa hivi vitu ambavyo vimekatazwa upo uvumbuzi wa sayansi ambao unamyakinishia Muislamu hekima ya katazo hilo na kumuongezea yeye Iymaan.





Tukizama kwa makini tutaona ya kwamba Dini zote zimeharamisha nguruwe. Mfano tazama katika Biblia (Agano la Kale), Kitabu cha Walawi: "Na nguruwe msimle; ana kwato zilizogawanyika lakini hachuei; kwenu huyo ni najisi. Kwa sababu wanyama hao ni najisi msile nyama zao wala msiguse mizoga yao" (11: 7 - 8). Na katika Kitabu cha Isaya: "Allaah asema hivi: 'Wapo watu waaojitakasa na kutawadha wapate kuingia katika bustani za ibada za sanamu; wanafanya maandamano na kahini akiwa kati yao. Watu hao hula nguruwe, panya na vyakula vingine haramu'" (66: 17).



Na katika agano jipya, Yesu anasema: "Msidhani kuwa nimekuja kutangua sheria na mafundisho ya manabii. Sikuja kutangua bali kukamilisha" (Mathayo 5: 17).





Na Qur-aan ipo wazi kabisa kuwa nyama ya nguruwe haifai kuliwa. Allaah Anasema:



إِنَّمَا حَرَّمَ عَلَيْكُمُ الْمَيْتَةَ وَالدَّمَ وَلَحْمَ الْخِنزِيرِ وَمَا أُهِلَّ بِهِ لِغَيْرِ اللَّـهِ ۖ

Hakika Allaah Amekuharamishieni mzoga na damu na nyama ya nguruwe na kilichotajiwa katika kuchinjwa kwa ajili ya asiyekuwa Allaah [Al-Baqarah: 173]





Nguruwe pamoja na kuwa anakula vinyesi na vitu vichafu pia ina matatizo mengi ambayo watafiti wamegundua kuwa nguruwe hata akilishwa lishe safi, bado:



(i) Ni wanyama wachafu katika mambo mengine na nyama ya wanyama wachafu ikiliwa inamuathiri mlaji.



(ii) Nyama ya nguruwe ina mafuta mengi zaidi kuliko nyenzo za kujenga misuli.





(iii) Ina uwezakano wa kupata magonjwa kuliko aina nyengine yoyote ya nyama.





Athari ya madhara ya nyama hiyo sasa inajulikana vilivyo na kila mmoja. Asidi ya Uric, inapatikana kwa kila mnyama, na mwili wa mwana Aadam pia ina nasibu yake, ambayo inatolewa nje ya mwili na mafigo kwa 90% ya asidi ya uric inatolewa kwa njia hii, lakini chemia ya nguruwe ni kuwa inatowa nje ya mwili 2% ya asidi yake ya uric pekee. Iliyobaki inabakia ndani ya mwili wake. Hii ni sababu ya kupatikana kwa kiwango kikubwa ugonjwa wa baridi yabisi (rheumatism) wa nguruwe na wale wenye kula nyama yake [Maulana Wahiduddin Khan, God Arises, uk. 209 – 210].





Dkt. Simpson ana haya ya kusema kuhusu nyama hiyo: “Kwa sababu ya kuwa na mafuta mengi, nyama ya nguruwe ina tatizo kubwa kusagwa katika vyakula vyote. Mnyama huyo anaweza kuathiriwa kwa kiasi kikubwa na lava wa Taenia solium hivyo kufanya "tegu (surua ya nguruwe)" na hii tegu inaleta aina ya tegu, T. solium. Inaathiriwa zaidi na Trichinella spiralis ambayo inaleta maradhi ya "Trichinosis" [Imenukuliwa na Yousef Saleem, Pork, A Bad Diet Prohibited by Islam, al-Islam, March/April, 1980, p. 29].





Trichinosis ni ugonjwa ambao unaletwa na kiinitete cha Trichinella spiralis wakati vinapohama kutoka kwa utumbo wa mwana Aadam mpaka kwenye misuli. Katika wiki ya kwanza baada ya kuvamiwa mtu anaanza kutapika, kuhara na kusikia kichefuchefu. Ugonjwa unapoendelea inaleta matatizo ya kumeza, kuzungumza na kupumua.





Njia moja ya kuzuia ugonjwa ni kuipima nyama kwa tegu. Lakini Leavell na Clark wameandika: "Kwa vile cysts wa Trichinella ni wadogo sana kuonekana na macho, uchunguzi huo haufalii kitu. Wajerumani rasmi walikuwa wakifanya uchunguzi kwa hadubini kwa lengo hilo lakini ilikuwa ni ghali sana. Njia bora ya kuepukana na trichinosis ni kupika bidhaa za nguruwe barabara" [Imenukuliwa na Yousef Saleem, Pork, A Bad Diet Prohibited by Islam, al-Islam, March/April, 1980, p. 29].





Jambo jengine muhimu ni kuwa nguruwe ana shingo ndogo sana (kwa ndani, ingawa nje inaonekana pana), hivyo kuwa shida kuchinjwa. Hivyo, mwanzo anapigwa na chuma na baada ya kuzirai ndio anachinjwa. Hii ina matatizo kwa sababu Uislamu umeweka aina yake ya kuchinja ambayo inamfanya mnyama atoe kiwango kikubwa cha damu. Kama tunavyojua ni kuwa damu ni chombo cha kubeba viini vya ugonjwa na kemikali ambavyo vina madhara na hasa kwa mwana Aadam. Kubakia ndani ya mnyama damu huenda kukaleta madhara makubwa kwa mlaji. Na kwa kuwa nguruwe hachinjwi kama wanyama wengine, damu nyingi hubakia ndani ya mwili badala ya kutoka nje.





Mwisho, nyama ya nguruwe ni chakula duni. Charles Annondale ameandika, "Nyama freshi ya nguruwe, japokuwa kwa wengine inachukuliwa kuwa chakula kitamu, hasa anapouliwa akiwa mchanga, ni lishe duni ukilinganisha na nyama ya ng'ombe au mbuzi na inatumika kwa uchache" [Imenukuliwa na Yousef Saleem, Pork, A Bad Diet Prohibited by Islam, al-Islam, March/April, 1980, p. 29].





Tunayopata katika maagizo na Shariy’ah ya Kiislamu kuhusu mbwa ni kuwa yeye ni najisi na pia ni haramu kuliwa. Hivyo, Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ametuagizia kuwa ikiwa mbwa ataramba chombo chochote basi chombo hicho kioshwe mara saba moja wapo ikiwa ni kwa mchanga. Na utafiti wa sasa unaonyesha kuwa katika umaji maji wake vipo viini ambavyo ni hatari haviwezi kuuliwa wala kuondoshwa isipokuwa kwa mchanga, kwani mchanga una vitu ambavyo vinaua viini hivyo. Kwa kuwa maslahi ya mwana Aadam anayeyajua ni Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa). Na pia mbwa kama carnivorous (walaji nyama) wengine wanakula vitu vingi hivyo kuliwa na bin Aadam inamtoa katika ule ustaarabu na unaweza kumletea maradhi mengi kwa ajili ya hilo.





Na Allaah Anajua zaidi
 
Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com





31-Je, Waumini watamuona Rabb wao watakapoingia Jannah?



Naam. Waumini watamuona Rabb wao watakapoingia Jannah.



وُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ نَّاضِرَةٌ ﴿٢٢﴾



Nyuso siku hiyo zitanawiri.

إِلَىٰ رَبِّهَا نَاظِرَةٌ﴿٢٣﴾

Zikimtazama Rabb wake. [Al-Qiyaamah: 22-23]

(إنَّكُمْ سَتَرون رَبكُم) رواه البخاري ومسلم

((Hakika nyinyi mtamuona Rabb wemu)) [Al-Bukhaariy na Muslim]
 
Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com





32-Waislamu wanapaswa wawe wanahukumu mambo yao kwa kufuata nini?



Waislamu wanapaswa wahukumu kufuata Qur-aan na Sunnah ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).



وَأَنِ احْكُم بَيْنَهُم بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ

Na wahukumu baina yao kwa yale Aliyoyateremsha Allaah [Al-Maaidah: 49]



((الله هُوَ الْحكم وَإلَيْهِ المَصِير)) حسن رواه أبو داود

((Allaah ndiye mwenye kuhukumu na Kwake ndio marejeo)) [Hadiyth Hasan ameipokea Abuu Daawuwd]
 
Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com







33-Nini hukumu ya kufuata shariy’ah zisizo za Kiislam?



Kuzifuata shariy’ah zisizo za Kiislamu na kuzifanyia kazi na kuziacha shariy’ah za Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) ni kufuru kubwa.



وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْكَافِرُونَ﴿٤٤﴾

Na yeyote asiyehukumu kwa yale Aliyoyateremsha Allaah, basi hao ndio makafiri. [Al-Maaidah 44]



((وَمَا لَمْ تَحْكُمْ أَئِمَّتُهُمْ بِكِتَابِ اللَّهِ وَيَتَخَيَّرُوا مِمَّا أَنْزَلَ اللَّهُ إِلَّا جَعَلَ اللَّهُ بَأْسَهُمْ بَيْنَهُمْ)) حسن رواه ابن ماجه

((Na wasipohukumu viongozi wao kwa Kitabu cha Allaah na wakawa wanachagua katika Aliyoyateremsha Allaah, basi Allaah Atawajaalia kutoelewana (migongano) baina yao [Hadiyth Hasan ameipokea Ibn Maajah]
 
Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com







34-Je, Inajuzu kuapa kwa mwengine asiye Allaah?



Hapana! Haijuzuu kuapa kiapo kisicho cha Allaah.

قُلْ بَلَىٰ وَرَبِّي لَتُبْعَثُنَّ

Bali hapana! Naapa kwa Rabb wangu, bila shaka mtafufuliwa [At-Taghaabun: 7]



((مَنْ حَلَفَ بِغَيْرِ اللَّهِ فَقَدْ كَفَرَ أَوْ أَشْرَكَ)) رواه الترمذي وأبو داود وصححه الألباني في صحيح الترمذي .

((Atakayeapa pasi na Allaah, atakuwa amekufuru au amemshirikisha Allaah])) [At-Tirmidhiy, Abu Daawuwd na ameipa daraja ya Swahiyh Al-Albaaniy katika Swahiyh At-Tirmidhiy]
 
Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com







35-Je, Inajuzu kutundika au kuvaa hirizi?



Hapana! Haijuzu kutundika au kuvaa hirzi kwa sababu ni shirki.



وَإِن يَمْسَسْكَ اللَّـهُ بِضُرٍّ فَلَا كَاشِفَ لَهُ إِلَّا هُوَ ۖ

Na Allaah Akikugusisha kwa dhara, basi hakuna yeyote wa kukuondolea hiyo isipokuwa Yeye [Al-An’aam: 17]



((من علّق تميمةً فَقَدْ اشرك)) صحيح رواه أحمد

((Atakayetundika hirizi, atakuwa ameshirikisha Allaah)) [Hadiyth Swahiyh ameipokea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…