Napenda kuwakumbusha Ibada za makumi ya Mwezi wa Ramadhaan:
1. KUMI LA KWANZA
Hili ni kumi la
REHMA
Uradi uliopendekezwa kusoma katika kumi hili ni:
YAA ARHAMA R-RAAHIMIYN
IDADI ILIYOPENDEKEZWA NI 1,000 KILA SIKU
NIA YA URADI:
Ewe ALLAH uliyetukuka hakika nimetia nia ya kusoma uradi huu ili nipate radhi zako na unijaze rehma zilizopo katika kumi hili la mwanzo wa ramadhwaan. Nakuomba unikubalie ibada yangu hii kwako.
Ukijitahidi kufanya uradi huu mpaka ukamaluza kumi la mwanzo basi in shaa Allah utapata rehema zilizomo katika kumi hilo la mwanzo.
2. KUMI LA PILI
Hili ni kumi la
MSAMAHA yaani kusamehewa madhambi yote yaliyopita.
Uradi uliopendekezwa kusoma katika kumi hili ni:
ASTAGHFIRULLAAH LA'ADHWIM WA ATUUBU ILAYHI
IDADI ILIYOPENDEKEZWA NI 1,000 KILA SIKU
NIA YA URADI:
Ewe ALLAH uliyetukuka hakika nimetia nia ya kusoma uradi huu ili nipate radhi zako na unisamehe madhambi yangu yote niliyofanya kwa makusudi au kwa bahati mbaya naomba unipe radhi zako na msamaha wako uliopo katika kumi hili. Nakuomba unikubalie ibada yangu hii kwako.
3. KUMI LA TATU
Hili ni kumi la kuokolewa katika moto wa
JAHANNAM
Uradi uliopendekezwa kusoma katika kumi hili ni:
ALLAHUMMA AJIRNAA MINA NNAAR SAALIMIYN
IDADI ILIYOPENDEKEZWA NI 1,000 KILA SIKU
NIA YA URADI:
Ewe ALLAH uliyetukuka hakika nimetia nia ya kusoma uradi huu ili nipate radhi zako na uniepushe na adhabu za duniani na adhabu za jahannam nakuomba unikubalie ibada yangu hii kwako.
MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA KATIKA NYIRADI HIZO NI
1. Hakikisha unao UDHU.
2. Hakikisha unaelekea KIBLA.
3. Usikatishe uradi kwa ajili ya mazungumzo isipokua kwa dharura.
4. Chagua sehemu moja maalum ya kufanya nyiradi zako zote mpaka RAMADHAN itakapoisha. Labda itokee dharura kama KAZI,SAFARI, n.k.
5. Hakikisha baada kumaliza uradi kila siku kwa makumi yote omba dua ya shida zako na kisha mswalie Mtume (rehma na amani ziwe juu yake).
6. Muda mzuri wa kusomwa nyuradi hizi ni kabla ya kutoka adhana ya maghrib kwani muda huo ni muafaka kukubaliwa dua nyingi katika mwezi wa ramadhani. Ingawa inaruhusiwa kusoma nyuradi muda wowote.